May

Saturday, May 31, 2008

Taarabu yazidi kuchengua

Usiku wa kuamkia leo kundi la Jahazi Modern Taarabu kama kawaida yake lilipagawisha ile kinona na vibao vyake mbalimbali kikiwemo kile cha Msumali katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam na kufanya Mademu na Mabrazaneni waliofika kuwasarandia mademu hao kushindwa kukaa vitini mpaka majogoo.

VINARA AWARDS 2008: COPY YAIBUKA KIDEDEA, YANYAKUA JUMLA YA TUZO SABA!

Filamu ya COPY, usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa diamond jubilee jijini dar, imeibuka kidedea ya kuwa filamu bora ya mwaka na kuwa ndiyo filamu iliyonyakua tuzo nyingi kuliko filamu nyingine. Copy, ambayo imetengezwa kwa kutumia utaalamu wa kumfanya mtu mmoja kuwa na uhusika wa watu wawili tofauti kwa wakati mmoja, imeshinda kwenye vitengo vya filamu bora ya mwaka, mpiga picha bora, muigizaji bora wa kike na wa kiume, muongozaji bora, mhariri bora na mtunzi bora. Pichani, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akimkabidhi Ahmed Halfan ‘kelvin’ tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka ambaye pia ndiye muongozaji na muigizaji msaidizi wa filamu hiyo. Mkewe pia, Elizabeth, ndiye aliyeibuka mwigizaji Bora wa kike 2007 kutokana na filamu hiyo hiyo ya Copy!!!
Hassan Bumbuli kutoka upande wa majaji, akimkabidhi tuzo ya adui bora kwenye filamu, Sebastian Mwanangulo ‘seba'(kulia) kutokana na filamu ya Misukosuko 2.

Rashid Mrutu (kulia) akipokea moja kati ya tuzo mbili alizojinyakulia usiku wa kuamkia leo pale diamond jubilee baada ya filamu yake ya COPY kumpatia tuzo ya mpiga picha bora na mhariri bora wa filamu.

Imani Kajula, kutoka NMB, akimkabidhi Elizabeth Chijumba (kulia) tuzo ya mwigizaji bora wa kike wa mwaka 2007. Filamu iliyompatia tuzo hiyo ni COPY.
Steve Kanumba (kulia) akipokea tuzo yake ya Heshima kutokana na mchango wake mkubwa wa kuitangaza nchi za nje tasnia ya filamu tanzania.
Washindi wa tuzo za heshima Thea na Kanumba wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kukabidhiwa tuzo zao usiku wa kuamkia leo pale diamond jubilee hall.

PICHA ZOTE: CHRISTOPHER LISA/RICHARD BUKOS/GPL)

Nyumba ya 50 Cent yaungua MOTO!!

Jumba la kifahari la mwanamuziki 50 Cents limeungua moto jana ijumaa majira ya saa saa kumi na moja alfajiri, Watu wote sita waliokuwemo ndani ya nyumba hiyo walikimbizwa hospitali na kupatiwa matibabu na bado walikuwa chini ya uangalizi wa madaktari lakini hali zao zinasemwa kuendelea vizuri. Rafiki wa kike wa zamani wa mwanamuziki huyo alikuwepo pamoja na Marquise mtoto wa kiume wa 50 Cent mwenye miaka 10.

Nyumba hiyo yenye vyumba sita vya kulala, mabafu matano, pamoja na vikorombwezo kadha wa kadha imejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari moja, imeungua na kuteketea kabisa.

Habari zinasema moto huo wanahisi unahusiana na njama fulani lakini Mwanamuziki huyo bado hajasema kama anamhisi mtu yeyoye.

Gonga hapa kwa picha zaidi

Timu 40 za Africa zashuka dimbani leo, Taifa Stars yaikaribisha Mauritius

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mauritius wakiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tayari kwa mechi dhidi ya Timu ya Taifa Taifa Stars.

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars‘ leo inatarajia kushuka dimbani kuvaana na Mauritius katika mchezo kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2010 unaotarajia kufanyika Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo wa leo ni kwanza kwa timu hizo zilizopo Kundi la Kwanza pamoja na timu za Visiwa vya Cape Verde na Kameruni.

Taifa Stars itashuka dimbani ikiwa kamili kuikabili timu hiyo, ikiwa ni wiki moja baada ya kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Malawi na kufungana bao 1-1.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo amesema timu yake ipo vizuri na ana imani watashinda leo na kujiweka vizuri katika msimamo kwa ajili ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Afrika Kusini.

Kwa wikiend hii tu zaidi ya timu za soka 40 toka Africa zinashuka dimbani kwa ajili ya kuwania kucheza nafasi ya fainali ya Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Africa.

………………………………………………………………………………

Misri Vs Congo DRC
Pharaohs ya Misri
(pichani juu) itawakaribiosha Simba wa Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo ,Kocha wa Kongo Mbelgiji Patrice Neveu amewaita wachezaji muhimu wa kikosi chake kama Shabani Nonda na Tresor Lualua kujiunga pamoja kwa ajili ya ichuano hii. Mchezaji wa Misri na mfungaji bora wa Kombe la Mataifa ya Africa mwaka jana Mohamed Abu Traika atakosa mchezo huo wa ufunguzi kwa kuwa ni majeruhi.

………………………………………………………………………………


Cameroon Vs Cape Verde
Timu ya Taifa ya Cameroon Indomitable Lions itawakaribisha Cape Verde, kikosi cha Cameroon kinaundwa na wachezaji chipukizi ambapo wameongeza vijana sita watakao ongozwa na kijana mwenzao Samuel Eto’o, Rigobert Song na Geremi Njitap.

…………………………………………………………………………….
Ivory Coast Vs Msumbiji

Ivory Coast wakiwa ndio kwanza wamerejea toka Japan walipokwenda kucheza Kirin Cup wakiwa ni wawakilishi wa Africa kwenye michuano hiyo watakutana na Msumbiji. Mkongwe Didier Drogba anakazi kubwa ya kukiongoza kikosi hicho ambapo mchezo huu ndio mtihani mwingine kwa kocha mpya Vahid Halilhodzic wa Bosnia.

………………………………………………………………………………

Nigeria Vs Bafana Bafana
Nayo Nigeria Super Eagles ambao wameonyesha kutojali tena makocha wageni baada ya kocha Mjerumani Berti Vogts wa Germany kushindwa kuwaridhisha wapenzi wa soka kwa michuano iliyopita ya Ghana. Kwa sasa timu hiyo inafundishwa na makocha wazalendo Shaibu Amodu na mkongwe Daniel Amokachi, watakuwa na kibarua kigumu kukabiliana na waandaaji wa fainali hizo kwa mwaka 2010 timu ya Bafana bafana ya Africa Kusini.

…………………………………………………………………..

Morocco Vs Ethiopia
Baada ya mafanikio mabovu Atlas Lions ya Morocco itawakaribisha Ethiopia kwa kile ambacho kocha wao anasema ni mchezo wa kuanza kurudisha heshima ya Morocco kwa mchezo wa soka kimataifa.
……………………………………………………………………..

Senegal Vs Algeria
Simba wa Teranga wa Senegal nao walimtosa kocha wao wa kigenibaada ya kutofanya vizuri Ghana kocha mpya Lamine Ndiaye ana kibarua kwa kukutana na timu ya Algeria.

………………………………………………………………………………

Ghana Vs Libya
Ghana wanakutana na Libya huko Kumasi Ghana. nao pia ni mtihani hasa baada ya kuaachana na kocha wao Claude Leroy.

………………………………………………………………………………

Togo Vs Zambia
Timu ya taifa ya Togo inakutana na Zambia katika tukio ambalo si la kawaida kwani watachezea Ghana katika jiji la Accra. Hii ni baada ya FIFA kuwafungia Togo kwa kufanya fujo kwa timu ya Malian.

Kolabo ya Celeo Scam na Fally Ipupa Dicap

Celeo Scam alikuwa kijana wa Werason lakini akaamua kutoka kivyake na kwa sasa yuko Juu kioma, Celeo pamoja na Fally wanaitwa Kizazi cha Tano cha Muziki wa Congo. (Kizazi cha nne ni akina JB, werason nk). Katika Albamu mpya ya Celeo Nzoto na Nzoto 10+, kuna wimbo ambao ni kolabo ya Celeo Scam na Fally Ipupa, Single hii ni moto wa kuotea mbali. Prodyuza Maghambo upooo?

BCBG Ndani ya Rotterdam

Mdau akiwa amepozi na Genta, mmoja wa wanamuziki wa kundi la Wenge BCBG, Picha hii imepigwa na Ronald mnazi hasa wa Wenge. Kundi la Wenge BGBG waliwasili Rotterdam majuzi kwa ajili ya onyesho lao ambalo limefanyika usiku wa kuamkia leo. hapa ni kwenye duka maarufu la Muziki wa Kiafrika la Tshobo shop linalomilikiwa na “Mjasiriamali” Papaa Danny Kulia.
Mwanamuziki Tshai Ngenge akiwa mitaani Rotterdam

Nono Fuji, Ni mmoja wa vifaa vya JB Mpiana, kijana hatari huyu, Picha na habari za shoo hii zaja.

Kablba ya onyesho la jana BCBG waliwasha moto Sweden usiku wa tarehe 24 May 2008, pata kipande cha shoo ya Sweden hapo chini.

MISS UNIVERSE TZ 2008 NI AMANDA

Mrembo Amanda Sululu(pichani) jana aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Universe Tanzania 2008. Shindano hilo lilifanyikia jana usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jijini Dar-es-salaam.Kwa maana hiyo Amanda ndiye anarithi taji kutoka kwa Flaviana Matata mrembo ambaye mwaka jana alifanikiwa kuiletea sifa Tanzania baada ya kufanikiwa kuwemo katika tano bora ya mashindano hayo katika ngazi ya dunia yaliyofanyikia nchini Mexico.

Tatu bora-Katikati ni Amanda Sululu,kushoto ni Jamila Nyanga(mshindi wa pili) na kulia ni Eva Babuely(mshindi wa tatu)

Mashindano ya Miss Universe mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai katika ukumbi uitwao Crown Convention Center(Diamond Bay Resort) mjini Nha Trang nchini Vietnam.Zaidi ya washiriki 80 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki.

Habari na picha Bongo Celebrity

Ze Comedy waibukia TBC1

KUNDI la vichekesho la Ze Comedy jana lilitangaza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kituo cha televisheni la TBC 1.

Akizungumza kwa niaba ya kundi hilo, msanii Emanuel Mgaya ‘ Masanja’, alisema vituo vingi vya televisheni nchini waliomba kufanya nao kazi, lakini wao wamejali kituo kilichotoa mkataba mnono.
Alisema kwa sasa wameamua kuweka wazi mkataba huo, ili wapenzi wao wajue kuwa kundi lipo na sasa linaanza kazi rasmi kituo hicho walichokitangaza.
Pia alisema kundi hilo limepata mlezi mpya ambaye ni Yusuph Manji, hivyo wanaamini watafanya kazi vizuri.
Wasanii wanaounda kundi hilo ni Emanuel Mgaya ‘Masanja’, Vengu Shamba, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘Mark Leagan’, Issaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Sylvery ‘Mpoki’ na Sekion David.

Friday, May 30, 2008

Wazee wa Masauti kupamba Miss Tanga

Washiriki wa Miss Tanga mwaka jana, kabla ya mashindano, mwaka huu mashindano hayo yanafanyika uwanja wa Mkwakwani na yatasindikizwa na Wanapekechapekecha Akudo Impact wazee wa Masauti.

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Akudo Impact ya Jijini Dar es Salaam, inatarajia kutumbuiza katika mashindano ya Urembo ya Miss Tanga yanayotarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu Mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertainment Nassor Makau alisema kuwa shindano hilo litafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani.

Akizungumzia mashindano hayo Makau aliwataja warembo watakaoshiriki kinyang’anyiro hicho kuwa ni Doris Steven, Judith Assey, Mariam Mhando, Amina Sadick, Halima Khalfani, Aisha Abdalah, Nuru Salim na Beatrice Lwimba.

Aliwataja wengine kuwa ni Oliver Mango Mwajuma Msangi, Agnes Mwakipesile, Hadija Ramadhani, Hawa Njama, Mariamu Hajibu, Marie Frederick, Mwanamina Bausi, Silvia Urio, Samia Mohamed, Shamim Said, na Evelyine Thomas.

Makau alisema kuwa warembo hao wamepatikana kutokana katika vitongoji vya Miss Usagara, Miss Korogwe, Miss Vyuo na Miss Lushoto.

Warembo watatui watakaopatikana katika shindano ya Miss Tanga, watapata tiketi ya kushiriki Miss Tanzania mwaka huu. Mrembo anayeshikilia taji hilo ni Victoria Martin ambaye alifanya vyema katika mashindano ya Taifa mwaka jana na kuingia tano Bora.

Blanchard Deplaizir anataka “Kolabo” na Alikiba

Msanii DePlaizer ameweka wazi kuhusiana na hisia zake za kutaka kufaya kazi na wanamuziki wa barani afrika ikiwa ni moja katika malengo yake katika kuunyanyua muziki wa kifrika duniani.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 anayeendeleza makamuzi huko nchini Uingereza katika jiji la Manchester ameweka wazi sana kuwa anavutiwa saaaaaana na msanii Alikiba na yuko mbioni kuangalia uwezekano wa kurekodi nae wimbo wa pamoja “nadhani nitafurahi sana iwapo nitapata nafasi ya kupiga nae mkono” alisema msanii huyo alipokuwa akifanya mahojiano na Bongo5.

Alitaja sababu zilizopelekea yeye kuvutiwa na msanii Alikiba, ni wimbo wake wa ‘cinderela’ kuanzia sauti na melody hata mpangili wa Beat vinamfanya jamaa azidi kupagawa na msanii huyu.
Wimbo wa Cinderela inasemekana uko juu sana nchini Uingereza kuliko ngoma kibao za watanzania ambazo husikika.

Msanii Alikiba ambaye yupo nchini Uingereza kwa sasa, kwa ziara maalum ya kimuziki ambapo ameshafanya maonesho kadhaa na hivi karibuni anatarajia kurejea nchini.

De Plaizir nusra achanganyikiwe baada ya kusikia msanii Alikiba amekuja nchini Uingereza kwa ajili ya maoenesho “nilipata taarifa ya ujio wa Alikiba Uk kutoka kwa meneja wangu wa Tanzania Sophia Kessy ambaye alikutana na Alikiba kabla ya kuja huku na kumtaka akutane na mimi na kupanga lolote kuhusiana na kazi za kisanii na yeye hakuwa na pingamizi, sasa nachokifanya nadhani nitahakikisha namtafuta kabla hajaondoka”

Unaweza kuona ni jinsi gani msanii De Plaizir anavyoweza kujitanga za pande hizi za bongo na afrika kwa ujumla, jitihada za kumtafuta alikiba bado zinaendelea na akipitakana tutasikia nae upande wake una lipi kuhusiana na show yake na kolabo yake na mtu mzima De Plaizir.

Bongo5

Thursday, May 29, 2008

Ali Kiba ndani ya Club Afrique – London

CLUB AFRIQUE LONDONPROUDLY PRESENTSALI KIBA
TANZANIA’S CHART BURSTING ARTISTEWHEN : FRIDAY 30TH MAY 2008WHERE:CLUB AFRIQUECANNING TOWN, LONDON


FEE: £10ALL EAST AFRICANS ARE WELCOME

Mtanange wa Taifa Stars na Mauritius

Mwenyekiti wa baraza la michezo nchini (BMT )Idd Kipingu,katikati,akifafanua jambo kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha watanzania kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye pambano la kimataifa na Mauritius litakalofanyika jumamosi wiki hii kwenye uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika kwenye ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana,kushoto ni Afisa habari wa Kampuni ya Serengeti Bia(SBL) Tedy Mapunda na kocha mkuu wa Stars Macio maximo.
Na Haki Ngowi

WENGE BCBG yawakati huo

Enzi hizo bado wakiitwa Wenge BCBG wakiwa wamekamili JB Mpiana, Werason Makanda, Adolph Dominguez, Engineer Blaise Bulla, Allain Makaba, Alan Mpella na Roberto Wunda Ikokota Machine, Typewriter,Honet F15 vyovyote utakavyomuita, Big Prodyusa Magambo upoo? Bonyeza hapa upate Sebene.

CHELSEA yatenga Paund M80 kwa ajili ya usajili

Didier Drogba akiwa na kombe la FA pamoja na tajiri Roman Abramovich, Abramovinch anatarajia kocha ajaye wa Chelsea atarudisha hadhi ya Chelsea kwa kurudisha Vikombe vya ushindi.

Kocha mpya wa Chelsea atapokelewa na kitita cha Paund milioni 80 kwa ajili ya kununua wachezaji wakuongeza nguvu kwenye timu hiyo. Hayo yalisemwa na mmiliki wa timu hiyo Bilionea Roman Abramovich alipokuwa akiongelea juu ya mstakabali ya kocha wa klabu hiyo alipokuwa anahojiwa na Television ya Chelsea.
“Kocha mpya lazima aelewe tunataka nini, pesa imetengwa kwa ajili ya usjili, tutasajili kutokana na mapendekezo ake pia, ila mwisho wa siku ni vikombe ndio tunataka” alisema Abramovinch
Chelsea imewataja Straika wa Valencia David Villa, Mchezaji kijana wa Barcelona Giovan Dos Santos pia wamemtaja mpachika mabao wa Inter Millan Zlatan Ibrahimovic

Celtel imejitosa kudhamini Gofu

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Celtel imejitosa kudhamini kwa miaka mitatu mashindano ya kimataifa ya gofu yanayotarajia kuanza Dar es Salaam kesho kwa sh.milioni 120.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Beatrice Singano, alisema Celtel inaona fahari kudhamini mashindano hayo kwa vile ni mwendelezo wa sera yake ya kuboresha maisha.

Alisema Celtel ilisaini mkataba huo na klabu ya gofu ya Lugalo ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Februari mwaka huu, ambapo jana Celtel ilikabidhi sh. milioni 7 ikiwa ni sehemu ya mkataba huo, ambao ni sh.milioni 40 kwa mwaka.

Naye nahodha wa klabu ya gofu ya Lugalo, Brigrdia Jenerali, Julius Mbilinyi, aliishukuru Celtel kwa kuokoa mashindano hayo na kuyapa nguvu ya uhakika wa kufanyika kwa miaka mitatu mfululizo.

Alisema mashindano hayo ya siku tatu yatakayokuwa wazi kwa washiriki wa ndani na nje ya nchi yanatarajiwa kuanza kesho na yanatambuliwa na Shirikisho la Gofu Tanzania (TGU) na yanatarajia kushirikisha wachezaji 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Alisema kwa udhamini huo wa Celtel, klabu hiyo ya Lugalo imeweza kumwagilia maji kwenye uwanja utakaotumika na kuupa hadhi ya kimataifa na kutoa zawadi bora kwa washindi, ambazo zitahusisha vikombe na fedha taslimu na pia kuboresha miundombinu mingine uwanjani hapo.

Serikali ya China yasimamisha burudani kwa siku 3 kuomboleza

Yao Ming

AFP/Shanghai
Television nchini China zilisimamisha kwa muda kutangaza aina yeyote ya michezo na burudani kwa siku tatu mfululizo ikiwa ni ishara ya kuomboleza walikufa kwa tetemeko ambalo limegharimu maisha ya maelfu ya watu nchini humu siku za karibuni.

Tangazo la serikali lilisambazwa kwenye vituo vyote vya Redio na Televisheni nchini humo, China imekuwa na idadi kubwa ya waangalia hasa mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu ya NBA baada ya Mchezaji mwenye asili ya Uchina Yao Ming anayechezea timu ya Houston Rockets kujiunga na ligi hiyo. Ming kwa sasa ndio mchezaji mrefu kuliko wote kwenye ligi ya NBA akiwa na urefu wa 7 feet 6 inches (2.29 m). Katika mchezo wake wa kwanza kwenye ligi hiyo inakisiwa wachina wapatao milioni 200 duniani waliuangalia mchezo huo kati ya Houston Rockets and Milwaukee.
Pamoja na machungu ya kupotelewa na ndugu jamaa na marafiki bado wachina walilalamika kwa idara husika na kuomba walao mechi za NBA pekee ziruhusiwe. Kwa kuonyesha mchezo huu ni maarufu kwa sasa NBA wamefungua ofisi China ambayo pamoja na mambo mengine inaratibu shughuli zote za kibiashara ikiwa ni mauzo ya Jezi, usimamizi wa Matangazo ya biashara na mikataba kwani kwa sasa kampuni za huko zinatangaza zaidi kwenye ligi hiyo.

Wimbo wa Taifa

Kelly Rowland toka kundi la Destiny’s Child akiimba wimbo wa taifa wa USA kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu kati ya USA na England iliyofanyika Wembley Stadium hapo jana, England ilishinda kwa magoli 2-0.

BASATA wachimba mkwara kuzifungia FM Academia, TOT Respect na Akudo Impact

Mmoja wa wanenguaji wa Akudo Impact akipekecha jukwaani, Uvaaji kama huu ndio uliopigiwa mkwara na Baraza la Sanaa la Taifa.
Na Majira
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limetishia kuzifungia bendi za FM Academia, TOT Respect na Akudo Impact kwa maelezo kuwa wanenguaji wake kuvaa vichupi wawapo jukwaani.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na BASATA kwenda kwa Wakurugenzi wa bendi hizo yenye tarehe ya juzi na kusainiwa na F.Magoti kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, ilieleza kuwa katika siku za karibuni bendi hizo zimekuwa zikifanya maonesho ya muziki yanayoambatana na wanenguaji wa kike waliovaa ‘vichupi’.
Barua hiyo ilieleza kuwa kitendo hichoo ni ukiukwaji wa maadili ya Watanzania na ni kuwdhalilisha wanenguaji na watazamaji wanaohudhuria maonesho ya bendi hizo.
“Kwa barua hii Baraza la Sanaa la Taifa linawapa onyo kali kuacha kabisa vitendo hivyo na kuhakikisha kuwa wanenguaji wenu wanavaa nguo za heshima zisizoonesha kwa namna yeyote ‘vichupi’ hadharani.

” Baraza halitasita kuchukua hatua ikiwemo ya kufungia bendi zenu, ikithibitika kuwa mnaendelea na ukiukwaji huo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Alizitaka bendi hizo kukumbuka kuwa maonesho yao hayaishii katika kumbi za burudani pekee, bali yamekuwa yakiharibu kwa kuwaonesha watoto wadogo kupitia vyombo vya habari kama vile magazeti na televisheni.
“Tukiamini kuwa lengo letu ni kuonesha umahiri na ustadi wa muziki wa bendi zetu, basi suala la kuonesha ‘vichupi’ halitajitokeza katika bendi zenu, “ilisema barua hiyo.

Nakala ya barua hiyo imepelekwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni na Maofisa Utamaduni wa Wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala.

Bekham na kofia ya dhahabu

Mchezaji wa England David Beckham akiwa na Kofia yake ya Dhahabu aliyopewa na Mkongwe Boby Charlton, ikiwa ni kuthamini mchango wake wa 100 kwa timu ya Taifa ya England kabla ya kuanza kwa mchezo wa jana dhidi ya USA.

ENGLAND yaichapa USA 2-0

Mchezaji wa England John Terry (R) akishangilia goli lake dhidi ya USA wakati wa mechi baina ya England na USA wembley jana.

Wachezajiwa England David Bekham (l) John Terry namba 6 mgongoni wakishangilia baada ya kuwabwaga USA kwa goli 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki jana.

Mchezaji Stephen Gerald akishangilia baada ya kupachika bao la pili dhidi ya timu ya USA kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Wembley Stadium jana.

Wafungaji wa magoli ya England ya jana John Terry na Stephen Gerald wakipongezana.

LONDON (AFP) –
John Terry aliweka pembeni machungu ya Champions League na kuisaidia timu yake ya taifa ya England kushinda dhidi ya timu ya taifa ya USA katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana.

Krosi ya David Bekham ndio iliyozaa goli la Terry mwishonbi mwa kipindi cha kwanza ambapo England hawakuonyesha machchari ki viiile.

Gareth Barry Stephen aliingizwa na kocha Cappelo ili kuongeza nguvu na kusaidiana na Steven Gerrard aliyepachika bao la pili.

Nafasi pekee ambayo USA waliipata ya wazi ni pale Eddie Johnson mpira wake ulipogonga besela kwani walikuwa na wakati mgumu wakishambuliwa sana hasa kipindi cha pili.

Mechi ya jana ilikuwa muhimu kwa Terry kupachika bao kwanza kama Kepteni kwa wakati mwingine chini ya kocha Capello na pili ni kufuta machungu ya kukosa penati siku saba zilizopita kwenye mechi ya Champions Ligi dhidi ya Manchester United.

Kocha Fabio Capello alisema ni “nafasi pekee ya kumsaidia kisaikolojia vinginevyo angeona hatuna imani naye, penati ni 50 kwa 50, lakini tabia ya waingereza hawaoni ni kwa nini ukose penati, kipa anasamehewa kwa kufungwa penati lakini sio mpigaji” alisema Capello.

Kwangu mimi kama kocha naelewa ni nusu nusu lakini wapenzi wa huku hata kwa maoni yao hawaoni ni kwa nini ukose penati aliongeza Capello huku akicheka.

Hapakuwa na idadi kubw ya watu kama ilivyotarajiwa kwani baadhi ya viti vilikuwa wazi hasa upande mwekundu kwa kile kilichooelezwa ni “Low profile match” na mashabiki.

Wednesday, May 28, 2008

John Terry kuongoza kikosi cha England dhidi ya USA

Kocha wa timu ya England Fabio Capello amemtaja John Terry (pichani) kuwa ndiye captain katika mchezo wa kirafiki dhidi ya USA utakao fanyika leo.

Terry amepewa heshma hiyo ikiwa ni utaratibu wa sasa wa kubadilishana kabla ya kuteuliwa mchezaji mmoja kuongoza hilo jahazi kwa kipindi chote.

Capello amesema kuwa anatumai kumpa Terry ukepten ni kuonyesha imani yake kwake na kumfanya aone kuwa bado tunaimani naye hasa baada ya kukosa penalti dhidi ya manchester jambo ambalo Terry linamuuma sana na hataki kamwe kukumbushwa hilo, “nafikiri ataichukulia ile kama changamoto aweze kuonyesha umma kuwa kosa ni kurudia kosa” alisema Capello. Mchezo wa leo n wa kirafiki baina ya England na USA lakini kila mtu katika mataifa hayo mawili amekuwa akiuzungumzia.

Barcelona yamchukua Gerald Pique wa Manchester

Timu ya soka ya Barcelona imemsajili mchezaji wa Manchester United Gerard Pique katika mkataba wa miaka minne kwa gharama ya paund milion 5.

Mchezaji huyo mwenye miaka 21 alijiunga na klabu ya Manchester mwaka 2004 lakini alikuwwa hapangwei mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester kwani tangu aingie amecheza mechi 23 tuu na kufunga magoli mawili pekee dhidi ya Dynamo Kiev na Roma. Kocha wa Barcelona amesema anamjua Pique na combination ya mpira anayocheza ndio maana hakuweza kupata mafanikio Manchester na kusema ana hakika atafanya vizuri kwa combination aliyonayo Barcelona.

ESPN May 2008.

Liverpool yaichimbia mkwara Chelsea kuhusu Torres

Timu ya mpira ya Liverpool imechimba mkwara kwa klabu ya Chelsea na kuwaambia mchezaji wao mwenye uraia wa Spain Fernando Torres hauzwi hata kwa gharama yeyote!.

Chelsea inasemekana kuweka nguvu nyingi sana katika kumuwania kumchukua Torres hasa baada ya mchezaji huyo kumaliza msimu huu kwa mafanikio makubwa.

Chelsea walikuwa wameahidi kutoa kitika cha paund milioni 50 kwa klabu ya Liverpool kwa ajili ya kumuchukua nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid lakini Liverpool imekataa ofa hiyo kwa kusema kuwa bado wanamuhitaji ila kama Chelsea wana mchezaji mwenye kiwango cha Toress wao Liverpool wangemtaka pia.alisema Rafa Benitez.

Ufaransa mbabe kwa Ecuado

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Bafetimbi Gomis akishangilia mara baada ya kupachika kimiani goli la pili kwenye mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ecuado.

Mchezaji wa Ufaransa Hatem Ben Arfa, shoto, akisakata goma kumtoka mchezaji wa Ecuado Isaac Mina, wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya timu hizo mchezo uliofanyika huko Alps stadium, Grenoble Ufaransa, jana jumanne, May 27, 2008. Ufaransa ilishinda 2 – 0. Ufaransa ilitumia mechi hii ya mwisho ya majaribio ili kuchagua kikosi chake cha watu 23 kwa ajili ya michuano ya EURO 2008, kwa sasa kikosi kina wachezaji 30.

Austria 1-1 na Nigeria mechi ya kirafiki

Mchezaji wa Austria Emanuel Pogatetz (L) akiwania mpira na Ikechukwo Uche wa Nigeria wakati wa mchezo wa kirafiki wa soka huko Graz, Austria wanajiandaa na mtanange wa kombe la EURO, mechi hii ilimalizika droo ya 1-1.

Tuesday, May 27, 2008

Fally kuwasha moto Ufaransa

Kila mtu na nyota yake, Tiketi za kumuona mwanamuziki toka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FALLY IPUPA “DICAP LA MERVEILLE” zimekwisha na zilikuwa zinauzwa Euro 100 kila moja, Waandaaji wa onyesho hilo wametenga kuuza Tiketi 200 tuu na hakutakuwa na tiketi ambayo itauzwa mlangini siku ya onyesho, ilisema taarifa hiyo toka kwa Yemima Ipupanaise. Onyesho hili litafanyika june 6. katika ukumbi wa Claude Makelele’s posh club, Paris.

Ferre Gora atimuliwa ulaya kwa kudanganya VISA!

Mwanamuziki wa Congo Ferre Gola (pichani) hivi karibuni alipata dhahma baada ya kitiwa nguvuni yeye pamoja na wanamuziki wa bendi yaki akiwa kwenye mpaka wa Belgium kuingia Ufaransa, akielekea kwenye shoo yake ambayo ilipangwa kufanyika Strasbourg ,inadaiwa kuwa Ferre alipata dhahma hiyo baada ya kutumia pasi za kusafiria ambazo zilikuwa zimekwisha muda wake, Akiongea nami mdau Mumuu Chizange alisema Kabla ya dhahma hiyo Ferre alifanya onyesho Belgium, onyesho ambalo linadaiwa kuwa na wahudhuriaji wachache sana hata baada ya kiingilio kushushwa toka Euro 30 hadi 10 bado hakupata watu, akizungumzia dhahma hiyo promota wa mwanamuziki huyo Lumba Bawu ambaye alikuwa akiratibu safari ya ke amesema kuwa kitendo alichofanya Ferre si cha kiungwana kwani alithubutu hata kudanganya pale alipoulizwa kuhusu Visa za Ufaransa akasema kuwa anazo ziko Valid hadi mwezi July, naye producer Fridolin Bokomo ambaye alikuwa akiratibu ziara ya mwanamuziki huyo Holland alisema kuwa Ferre amewatia hasara kwa ajili ya maandalizi ya maonyesho yake, Ina wezekana Ferre akapata adhabu kali kutokana na kitendo hicho kwani mwanamuziki Papa Wemba aliwahi kupata matatizo kama hayo pia.

Pichani ni baadhi ya matangazo ya maonyesho ya Ferre

Pichani ni baadhi ya matangazo ya maonyesho ya Ferre

Nani kumrith Grant Chelsea?

BAADA ya aliyekuwa Mocha Mkuu wa timu ya Chelsea Avram Grant (pichani) kufungashiwa virago mwishoni mwa wiki, tetesi zimeanza kusambaa juu ya makocha ambao watarithi mikoba yake.

Grant alitimuliwa Jumamosi baada ya Chelsea kufungwa na Manchester katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika Jumatano iliyopita na baada ya timu hiyo kumaliza Ligi Kuu ya England ikishika nafasi ya pili, hali ambayo imeacha milango wazi kwa kocha atakayechukua mikoba hiyo.

Kutokana na hali hiyo magezeti ya Uingereza tangu Jumapili yalikuwa yamejaa tetesi mbalimbali juu ya atakayekabidhiwa funguo na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich kitendawili ambacho bado kinasumbua vichwa mashabiki wa Ligi Kuu hadi utakapokuwa umefikiwa uamuzi.

Kocha anayepewa nafasi kubwa kuchukua mikoba hiyo ni Frank Rijkaard, ambaye naye alifungashiwa vilago na timu ya Barcelona mara tu baada ya Grant kutimuliwa.

Rijkaard alitimuliwa katika nafasi yake baada ya klabu hiyo ya Catalan kukosa ubingwa msimu huu ikiwa ni mara ya pili mfululizo, lakini hata hivyo kocha huyo bado anaaminika ndiye kocha bora katika klabu kubwa duniani, hali ambayo inamfanya apewe nafasi kubwa kuinoa Chelsea.

Kocha mwingine ambaye ametajwa na vyombo vya habari vya Uingereza ni Guus Hiddink, ambaye anapewa nafasi hiyo kutokana na kuonesha ni kocha mzuri kufuatia mafanikio aliyoyaonesha katika kazi yake ya sasa ya kuinoa timu ya taifa ya Urusi, ambayo mshahara wake analipwa na mmiliki wa Chelsea, Abramovich.

Mbali na hayo pia kocha huyo ni rafiki wa karibu wa Abramovich na hivi sasa Hiddink tayari amekubali kwa masharti kuinoa timu ya taifa ya Urusi.

Makocha wengine ambao wanapewa nafasi hiyo ni Roberto Mancini, ingawa kocha huyo anapewa nafasi kama Rijkaard na Hiddink wataikataa nafasi hiyo wao wenyewe.

Pia kyumo Sven-Goran Eriksson ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akimvutia Abramovich na mara mbili kocha huyo amewahi kukutaa kuifundisha Chelsea .

Kocha huyo aliwahi kunaswa na kamera akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Chelsea, Peter Kenyon wakati alipokuwa bado Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England na hivi sasa anakaribia kuwa huru baada ya mmiliki wa Manchester City, Thaksin Shinawatra kumtema.

Mark Hughes naye pia ni miongoni mwa kundi hilo, ambapo Hughes anapewa nafasi hiyo, baada ya kuifanya Blackburn Rovers kuwa moja ya timu ngumu msimu huu, hali iliyoifanya kumaliza msimu huu ikiwa nyuma ya timu nne za mwanzo.

Hughes vilevile ana uzoefu na timu za taifa baada ya kuiongoza Wales kutinga katika michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2004 na pia amewahi kuichezea Chelsea hadi alipotundika daruga.

Mwingine ni aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo ya Stamford Bridge na baada ya kuondoka mwezi Septemba mwaka jana uhusiano na Abramovich unaonekana kuwa mzuri.

Uhusiano huo ulidhihirika baada ya Mrusi huyo kumnunulia Mourinho gari aina ya Ferrari yenye thamani ya dola milioni 4 mwaka huu kama zawadi.
Na Majira

Picha zaidi za shoo ya BCBG

Mdau wa BCBG Twaha Makau pamoja na wadau wengine wameomba kuona picha zaidi za Papa Cherry na kundi zima la BCBG walipokuwa Bruxells Belgium hivi karibuni nami sina hiana ipo stock ya kutosha tuu hata kutumiwa watumiwa.

Anaitwa Virginie, Kifaa hiki kinasemekana kuwindwa sana na hasimu mkuu wa JB Werason na Koffi, angalia live za JB uone mambo yake.
Papa Cherry

Zadio Congolo akimtunza JB Mpiana, Jamaa huyu ni mpenzi mkubwa wa JB Mpiana husafiri kila mara JB anapokuwa na Onyesho nchi yeyote ya Ulaya.
Elodie Lipassa

[image]
Genta

[image]
Rio

[image]
JDL


Jules Kibens

Genta – Kibens – Chai Ngenge – Rio

Watu wakitawanyika hasubuhi saa moja kasoro baada ya shoo kuisha
Wadau wakitawanyika majira ya saa moja asubuhi baada ya shoo ya usiku kucha.

Monday, May 26, 2008

Marina Bay: Mahali pa maraha Singapore

Pamoja na njia mbali mbali za kufika Marina Bay ukitumia njia ya Boat maalum unapata mandhali nzuri zaidi na picha mwanana kama hii.
Uwanja wa Mpira ambao umo kwenye sehemu ya Bahari ambao uko mbioni kukamilika sehemu chache za nje ila uwanja waweza kutumika, picha hii niliipiga nikiwa ndani ya Singapore Flyer (picha ya chini).
Singapore Flyer ina urefu wa mita 165, ndio flyer kubwa zaidi duniani na ya kwanza kwa Asia imejengwa kwenye muinuko katika eneo maarufu la Marina Bay, Ndani ya hii flyer unaweza kuona mandhari ya mji mzima wa Singapore na nchi jirani kama Malaysia na Indonesia. ilizinduliwa tarehe 15 April na tiketi kwa ajili ya uzinduzi zilikwisha kwa siku tatu mfululizo zikiwa zinauzwa USD 8000, Booking ya Flyer inabidi ifanywe mapema kwani huwa imejaa kwa miezi miwili hadi mitatu kabla ila nafasi maalumu huwekwa kwa ajili ya wageni (watalii). soma hapa zaidi

Reuters – Pictures of the Year 2007

Kalbfleisch (anayechungulia) akijiandaa kumkabili mshindani wake katika michezo ya wazi ya Sumo huko Los Angeles, April 7, 2007. REUTERS/Lucy Nicholson.
Wakati huo akiichezea timu yake ya Arsenal, Thierry Henry akionyesha kuumiliki mpira kwa style ya aina yake huku David Bentley wa Blackburn Rovers akimuangalia wakati wa mchezo baina yao uliofanyika uwanja wa Emirates London February 17, 2007. Picha na Eddie Keogh.
Mchezaji wa Manchester United Nani (aliyeruka juu) akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya timu ya Tottenham Hotspur huko Manchester, Kaskazini mwa England, August 26, 2007. REUTERS/Phil Noble, Picha hizi ni baadhi ya picha zilizomo kwenye mkusanyiko wa Picha bora za mwaka jana za shirika la habari la REUTERS, kwa picha zaidi za Mwaka 2007 bofya hapa

Miss Tanzania Europe 2008

The mission of the Miss Tanzania Europe Pageant is to promote Tanzania and its people in the rest of the World: Tourism, culture, the beauty of this East African Nation.
We aim to further raise awareness on issues pertinent to Tanzania and most of all empower the Tanzania Queen to educate and enlighten communities as a goodwill ambassador for Tanzania.
The winner of Miss Tanzania Europe 2008,chosen on June 28th in Essen, Germany,and first runner up will represent Tanzania Europe*at the Miss Tanzania pageant to be held in Dar es Salaam in August 2008.
If you want to apply,
please go on the Application-
Page If you wish to apply for running in the Miss Tanzania Europe Pageant,you must be at least 18 years of age,of Tanzanian origin and residing in any State of the European Union which is a Member of the so called
“Schengen-Agreement”.
Na Haki Ngowi

Taifa Stars yatoka Sare ya 1-1 na Malawi

Jioni hii Taifa Stars ya Tanzania ilikuwa ikipimana ubavu na timu kutoka Malawi, The Flames, ambapo timu zilitoka sare ya bao moja kwa moja. Pichani ni mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa(kulia) akijaribu kumtoka beki wa Malawi, Wisdom Ndlovu.

TIMU ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ na ile ya Malawi jana zilifungana bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja Mkuu mpya wa Taifa, Dar es Salaam.

Maelfu ya mashabiki wa Taifa Stars iliwabidi wasubiri hadi dakika ya 79 kushangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Salum Sued baada ya kutokea kizaazaa katika lango la Wamalawi.

Kabla ya bao hilo Stars ilifanya mashambulizi mengi langoni kwa Malawi, lakini umaliziaji haukuwa mzuri, huku washambuliaji Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda, Emmanuel Gabriel kwa nyakati tofauti wakikosa nafasi nyingi za ushindi.

Iliwachukua dakika tano Stars tangu kuanza mchezo kwa kubisha hodi langoni mwa Malawi, baada ya Gabriel kukosa bao akiwa amebaki na kipa wa Malawi, kabla mpira haujaokolewa.

Stars ilizidisha mashambulizi, ambapo dakika ya 14 Mrisho Ngassa kidogo afunge, wakati shuti lake lilipookolewa na kipa Valence Kamzere.

Malawi nayo ilijipanga na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini nayo pia umaliziaji ulikuwa dhaifu, huku ngome ya Stars ikiondoa baadhi ya hatari.

Bao la Malawi lilifungwa dakika 54 na Essau Kanyenda aliyeunganisha vyema mpira kutoka wingi ya kushoto, huku mabeki wa Stars wakiwa wamezubaa.

Nafasi ambayo Stars itaijutia zaidi ni ile ya dakika ya 86 wakati shuti la Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lilipogonga mwamba na mpira kurudi uwanjani, lakini mchezaji huyo alipigwa na butwaa huku akinyoosha mikono kushangilia, akijua tayari mpira ulitinga wavuni.

Wachezaji Nizar Khalfan na Godfry Bonny nao kwa nyakati tofauti walipiga mashuti langoni kwa Malawi na kutia matumaini.
Habari na Majira, picha na Global Publishers

Sunday, May 25, 2008

Photo Baraza na utani kwa picha.
Aaaah!! Bwana wee, kila mmoja ana jicho lake anavyouangalia mpira huo huo tulio uangalia mimi na wewe, tembelea Photo Baraza uone hizi na nyinginezo!!

Bwana wee, furaha haina mwisho atii


Bwana wee furaha haina mwisho mtu waweza sherehekea hata mwaka mzima Rukhsa!!!!

BOB Wine-From Zero to Hero

Bob Wine akiongea na mdau kwenye mahojiano maalum ambayo utayapata ndani ya jarida la Eastafrica Uk
Mhh wapo wengi waliwabeza wanamuziki wa kizazi kipya si Tanzania tuu hata Mwanamuziki kutoka Uganda Bob Wine hakutarajia kufika na kufanikiwa kama alivyosasa, pichani ni “mjengo” wa mwanamuziki huyo. Kwa mahojiano kamoli tembelea gazeti tando la Miss East Africa.

Mr & Miss East Africa, ha ha haa Habari ndiyo hiyooo!

Mashindano ya Mr & Miss East Africa Uk yanatazamiwa kufanyika tarehe 26 July 2008 na kushirikisha walimwende na vijana watanashati toka pembe hiyo ya Africa. Mshindi wa mashindano haya pamoja na mambo mengine husaidia kwenye shughuli za kujitolea kwa ajili ya watoto waliona shida huko nyumbani Africa ya Mashariki kwa ujumla. Kwa mwaka huu pamoja na burudani kadha wa kadha zilizoandaliwa usiku huo utapambwa na Mwanamuziki Ali Kiba
Kwa mengi zaidi Bofya hapa. Pia waweza tembelea gazeti lao linalopatikana online, pichani chini ni moja ya picha zilizomo kwenye Issue Mpya ya Gazeti hilo

Beauty in the Jungle
washiriki wakiwa kwenye pozi katikati ya Jungle
Blanchard De Plaizir Nyota mpya katika Muziki wa Congo

Wimbo huu umeandikwwa na Muimbaji kijana anayekuja kwa kasi kwenye fani ya Muziki wa Congo kwa jina ni Blanchard de Plaizir, Homme Plus inaongelea hadithi ya mdada mmoja mdogo mrembo ambaye aliangukia kwenye penzi la kijana mtanashati na maarufu ambaye binafsi alimuona kwenye Tv na magazeti ya watu maarudu (celebrity magazines) na kuamini kuwa hatoweza kukutana na kijana huyu kamwe katika maisha yake ya kawaida mdada analalamika na kuona kuwa dunia haimtendei haki katika ulimwengu wa mapenzi, kijana anajitahidi na muziki wake ni mzuri kwa kweli.
Cover ya CD ya Deplaizir

Blanchard anaishi Manchester Uingereza, alizaliwa Congo lakini alihamia Uingereza akiwa na umri mdogo ila anasema nia yake ni kuuendelez utamaduni wake hata kama yuko nje ya nchi yake. Katika albamu yake hii Blanchard amemshirikisha aliyekuwa mpiga Gitaa mahiri wa BCBG Burkina Faso Mboka lia. (utamsikia vizuri kwenye Albamu ya Pentagone)


Kwa sasa shughuli za kimuziki za Blanchard kwa East Africa zinaratibiwa na Meneja wake Mtanzania akiwa ni mtangazaji wa Radio ya Clouds FM Sophia Kessy ndiye anayeratibu shughuli za Blanchard na kwa sasa anamuandalia safari ya kuitambulisha Albamu yake ya kwanza nchini Tanzania.

Vichapo vya Man U vyaotesha nyasi “chibarua” cha Grant Chelsea.

Pamoja na kumaliza wakiwa nafasi ya pili kwa mashindano yote mawili la ligi na na la UEFA, bado sio kigezo kwa uongozi wa klabu ya Chelsea kumpa mkataba kocha Avram Grant.

Hayo yalitanabaishwa katika waraka uliotolewa na Klabu hiyo kwa media na kwenye mtandao wa Chelsea http://www.chelseafc.com.

“Chelsea inathibitisha kwamba mkataba wa kocha Avram Grant umevunjwa rasmi toka leo, hii inafuatia majadiliano ya siku mbili ndani ya klabu. Kila mmoja katika klabu ya Chelsea FC anampongeza na kumshukuru Grant kwa kuwa Manager wa timu hii tangu mwezi Septermber mwaka jana.”
Kwa sasa tunaegemeza nguvu zetu katika kusaka kocha mpya, hakuna lolote litasemwa mpaka uamuzi ufanyike,

Grant aliichukua timu hiyo toka kwa Jose Mourinho mwezi September mwaka jana, Grant hakuwahi kuiongoza timu yeyote katika Uingereza alitakiwa kuchukua mikoba na baadaye angepewa mkataba wa miaka minne kama timu ingefanya vizuri.

Hebu fikiria kama wamefika Fainali na mambo ndio hayo, je sie tunatolewa hatua za awali wa kwetu si ndio wasingekaa kabisa!!!.

Lyon mabingwa wa Ufaransa

Kepteni wa timu ya soka ya Lyon’s , Antonio Ribeiro Reis, shoto, Gregory Coupet, kati, na Sidney Govou wakiwa wameshikilia Kombea na kushangilia baada ya timu yao kuwachapa Paris Saint Germain 1-0 katika mtanange wa fainali ya soka Kombe la Ufaransa. Mchezo huu ulifanyija jana tarehe 24 May katika uwanja wa Stade de France stadium nje ya jiji la Paris.

Stars, Malawi leo, Mtihani mwingine kwa Maximo

TIMU ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ leo inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuumana na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Taifa Stars ambayo Jumamosi wiki iliyopita ilifungana bao 1-1 na Uganda ‘The Cranes’ na kusonga mbele katika michuano ya Afrika inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani itatumia mchezo wa leo kujianda na mchezo wake dhidi ya Mauritius wiki ijayo kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2010.

Ni wazi kuwa yeyote atakayepangwa kati ya wachezaji hawa Fredy Mbuna, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Stephano Mwasika, Juma Jabu, Salum Swed, Nadir Haroub na Kelvin Yondani atakuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Pia katika safu ya kiugo yeyote kati ya hawa watawaunganisha vyema wenzao, ambao ni Geofrey Bonny, Athuman Iddy, Adam Kingwande, Kigi Makassy, Shaaban Nditi na Nizar Khalfan.

Tumaini la ushambuliaji litakuwa kwa Ulimboka Mwakingwe, Jerson Tegete, Uhuru Seleman, Mrisho Ngasa na Emmnauel Gabriel.

Hadi sasa Taifa Stars imecheza michezo nane ya kimataifa ya kirafiki chini ya Marcio Maximo tangu aanze kibarua hicho karibu miezi 19 iliyopita.

Katika michezo hiyo Taifa Stars imeshinda mitatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uganda na Zambia na kutoka sare mara nne dhidi ya Kenya, Angola, Zambia na Uganda na kufungwa na Yemen.
Source: Majira

Ilala bingwa Taifa Cup

TIMU ya Mkoa wa Ilala jana ilitwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Taifa 2008 baada ya kuifunga Kinondoni mabao 5-0 katika mchezo wa fainali uliopooza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo Ilala licha ya kutwaa kombe pia ilizawadiwa sh. milioni 30 na medali kwa wachezaji wote, wakati Kinondoni ilizawadiwa medali na sh.milioni 15.

Dalili kwamba Ilala ingetwaa ubingwa zilianza kujionesha dakika ya 8 mfungaji akiwa Mussa Hassan ‘Mgosi’ akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Matangalu Anthony.

Bao la pili lilifungwa dakika ya 43 na Mohammed Kijuso akitumia vyema pasi ya Athumani Machupa aliyeingia badala ya Mgosi aliyeumia.

Kijuso alifunga bao la tatu dakika ya 50 akiunganisha krosi ya Mohammed Banka na kuongeza la nne dakika dakika kumi baadaye kwa pasi ya Salum Kanoni, kabla ya Ramadhani Chombo kufunga bao la tano dakika ya 85.

Kinondoni iliyoingia fainali kwa kuitoa Mbeya kwa mabao 2-0 katika nusu fainali, haikuonesha cheche zozote kiasi cha muda mwingi mpira kuchezwa langoni mwao na hivyo kumpa nafasi kipa Juma Kaseja kupumzika.

Katika michuano hiyo iliyoshirikisha mikoa 23 ya kimpira, Juma Kaseja alitangazwa kipa bora, wakati kocha bora ni Madaraka Bendera wa Arusha na timu yenye nidhamu pia ikiwa Arusha, huku Mussa Mgosi akiibuka mfungaji bora baada ya kupachika mabao 8 wavuni. Wote walizawadiwa sh. milioni 2 kila mmoja.

Katika mchezo wa mapema jana, timu ya Mbeya iliifunga Arusha mabao 4-3 katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu, hivyo Mbeya kuikwaa nafasi hiyo na kuzawadiwa sh. milioni 7.5 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Source:Majira

Tyson anakuja “Bongo”

BINGWA wa zamani wa ndondi katika uzito wa juu duniani, Iron Mike Tyson, anatarajiwa kutua nchini Septemba mwaka huu akiambatana na bondia Laila Ali, ambaye ni binti wa nguli wa masumbwi duniani, Muhammed Ali.

Wakati Tyson akiwa amestaafu ndondi, Laila ni miongoni mwa mabondia mahiri wa kike wanaotamba kwa sasa duniani.

Akizungumza katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa ujio huo, Zuwena Kibene, alisema mabondia hao wanakuja kwa mwaliko rasmi wa kutoa semina kwa mabondia wa Tanzania.

Alisema, kutokana na ujio huo, anatarajia kuanza ziara ya kuzunguka nchi nzima ili kuhamasisha mabondia kufika katika mikoa ya jirani ambako wageni hao wataifikia.

Kibene aliitaja mikoa ambayo mabondia hao wataifikia, ni Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, hivyo amewataka mabondia wa jirani na mikoa hiyo, kufika katika mikoa hiyo kwa gharama zao.

Alisema, mabondia watakaokuwa wakitoka nje ya mikoa hiyo, watajigharamia usafiri, huku yeye (Kibena), akigharamia malazi, chakula na nauli za kurejea makwao.

bondia Laila Ali

Alipoulizwa kama mabondia hao watacheza pambano lolote, alisema hawatacheza pambano lolote kwani hakuna anayeweza kupambana nao.

Alisema, kitakachofanyika ni mabondia hao kutoa mafunzo kabla ya kushuhudia mapambano ya mabondia mbalimbali wa hapa nchini.

Tyson, mbabe aliyetamba vilivyo katika ulimwengu wa masumbwi duniani, ni miongoni mwa mabondia walio na mashabiki wengi kutokana na umahiri na vituko vyake.

Miongoni mwa kituko kinachokumbukwa, ni pale alipomng’ata sikio bondia mwenzake, Evander Hollyfield katika kuwania ubingwa wa dunia.

Source: Tanzania Daima

Saturday, May 24, 2008

Miss Tabata

Miss Tabata 2008 Anet John akiwa katika picha na mshindi wa pili Christin Sigala (kushoto) na Christine John baada ya kutangazwa washindi katika shindano la Miss Tabata lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dar West Park jijini Dar es Salaam.
soma zaidi kwa Haki

Lionel Messi

Lionel Messi alizaliwa 24 June 1987 huko Rosario – Argentina. kwa sasa anachezea timu ya FC Barcelona. alionyesha uwezo mkubwa akiwa na umri mdogo sana na medi zilimpachika kuw ndiye “Diego Maradona Mpya”. Messi alikaraishwa sana na timu yake kutochukua Kombe lolote kwa mwaka wa pili mfululizo na alitajwa kuwaniwa na vilabu vya Uingereza lakini timu yake ya Barcelona inasema itafanya kila linalowezekana kuendelea kuwa naye Messi. na huyu ndiye mchezaji wetu wa wiki hii na hii chini ni moja ya Video zake.

Sweta la 50 Cent lilipoleta kizaazaa.

Ni kawaida kwa wanamuziki au wanamichezo kuvua mavazi yao na kuwazawadia watazamaji, hivi karibuni mwanamuziki 50 Cent alitua Bongo baada ya kupokelewa uwanja wa ndege wa Dar akiwa njiani aliwarushia mamia ya mashabiki wake Fulana yake, Kimbembe kilichotokea hapo si cha kitoto ilibidi askari wa usalam kuingilia ili kuamua mashabiki hao waliotaka kutoana macho.
Kwa video zaidi za Msanii huyo ndani ya bongo Bongo5.com hapa

England Vs USA, Mtihani mwingine kwa Capello

Baada ya kukosa fainali za michuano ya Euro 2008, timu ya soka ya England kwa sasa inajiandaa na mechi za kirafiki ikiwa imeegemeza nguvu kwenye michuano ya kombe la Dunia mwaka 2010. Tarehe 28 mwezi huu England wanawakaribisha USA katika mechi ya kirafiki ambayo itafanyika katika uwanja wa Wembley.

Kocha mpya Fabio Capello (pichani) anakibarua kigumu kuwahakikishia na kuwarudishia waingereza matumaini na timu yao hassa baada ya kuchapwa kwenye mchezo wao wa kirafiki na Ufaransa jambo ambalo lilileta kelele toka kwa mashabiki wa soka wa Uingereza na kuamsha hisia kuwa wachezaji wa kigeni wanachangia kuharibu soka la Uingereza kwa timu zinakuwa zinawategemea wao zaidi kuliko kukuza vijana kwa ajili ya Taifa lao. Hii ni nafasi nzuri kwa Capello kama watashinda itampa milege na kumjengea heshima kwa waingereza ambao wanaona timu yao ikifanya vibaya mfululizo. Mara ya mwisho mwaka 1994 walipokutana England waliichapa USA mabao 2-0 yaliyofungwa na Alan Shearer.

Pool hadi Mlimba!

Mchezo wa Pool umekuwa maarufu sana Tanzania kila kona si jambo la ajabu kukuta meza na watu wamerundikana, Hii ilikuwa Mlimba Ifakara Morogo nilikuwa na kijana wangu Robert Mwafrica akaomba game moja duh dogo alimtoa nishai katika michezo minne alishinda mmoja tuu, Batty ndiye mwalimu wangu wa Pool na vijana wake wengi kwa sasa wanatisha. Ama kweli jogoo wa mjini hawiki shamba pia.

Laiti kamaaa……!


Hebu pata picha ndio Tanzania ingefanikiwa kufika Fainali tuu za Ghana ingekuwaje, Pichani ni watanzania wakiongozwa na Rais Kikwete (picha katikati) kipindi tunajongea kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa. Watanzania wanapenda sana Mpira basi tuu.

Serikali/TFF yaunda Kamati kusimamia Uwanja wa Taifa

Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeunda kamati itakayosimamia Uwanja mkuu wa Taifa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Kamati hiyo itafanya kazi kwa kusimamia uwanja huo pamoja na timu kwa michezo mitatu itakayofanyika nchini ukiwa kati ya Stars na Malawi unaotarajia kufanyika kesho pamoja na michezo kati ya Mauritius na Kameruni.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wake Kijazi Mtengwa ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, chini ya Katibu Mkuu wake Lawrance Mkwaji ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa wizara hiyo.

Mwakalebela alisema kamati hiyo pia itakuwa na wajumbe ambao watakuwa wenyeviti katika kamati ndogo ndogo zitakazosimamia shughuli hiyo.

Aliwataja kuwa ni Tido Mhando (Habari, itifaki na uelimishaji), Leodger Tenga (Ufundi na matumizi ya uwanja), Aloyce Mushi (mtaalamu wa uwanja), Alfred Tibaigana (Ulinzi na usalama) na Laison Mwanjisi (fedha).
Na Majira

Tibaigana achimba mkwara Polisi kuingiza “Dezo” Taifa mechi za Stars

JESHI la Polisi limesema limeimarisha ulinzi na kuwataka askari wa majeshi yote nchini kuingia uwanjani kwa kulipa kiingilio katika mechi mbili za kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Malawi na ile ya Maritius zitakazochezwa Uwanja mpya wa Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana alisema jana kuwa askari walioteuliwa kulinda usalama katika mechi ya kesho kati ya Taifa Stars na Malawi watakuwa na beji maalum zitakazowatofautisha na askari wengine wanaovaa sare za jeshi kwa lengo la kuingia mpirani bure.

Tibaigana ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Taifa ya kusimamia uwanja wa Taifa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alisema wanajeshi si masikini wa kutaka kila mara kuingia mpirani dezo, hivyo amewataka kuchangia timu yao ya Taifa kwa kulipa kiingilio.

Alisema mechi ya pili ambayo Stars itacheza na Maritius, Jumamosi ijayo pia kutakuwa na ulinzi wa kutosha na kuagiza kuwa magari yatakaoruhusiwa kuingia ni yale yaliyokatiwa tiketi za kuingia uwanjani.
Na Majira

Friday, May 23, 2008

Kung Fu Panda, Filamu ya Vikatuni iliyoshirikisha Magwiji wa Filamu

Kung Fu Panda ni picha ya Vikatuni inayomhusu mnyama Panda ambaye aliamua kujifunza Sanaa ya Kung Fu na baadaye kutumia ujuzi huu kupigana na kujihami na maadui zake. ni Filamu ya vichekesho sana na inafurahia sana. Picha hii imeongozwa na John Stevenson na Mark Osborne na producer ni Melissa Cobb. Wazo la picha hii lilibuniwa na Michael Lachance, Boss wa kampuni ya DreamWorks Animation . Filamu hii itakuwa sokoni June na itaonyeshwa rasmi June 6, 2008. na kusambazwa na Paramount Pictures.

Katika picha hii sauti za vinara wa Sinema zimetumika kama Jack Black, Seth Rogen, David Cross, Jackie Chan, Dustin Hoffman, Angelina Jolie na Lucy Liu. kama wanavyoonekana hapo chini. kwa habari zaidi Bofya hapa.

Angelina Jolie voices Master Tigress in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008
David Cross voices Master Crane in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008
Dustin Hoffman voices Shifu in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008


Jackie Chan voices Master Monkey in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008


Lucy Liu voices Master Viper in DreamWorks Animation’s Kung Fu Panda – 2008

Wakutanapo Celebrities wa Sinema

Angelina Jolie & Brad Pitt
Aishwarya Rai Kulia toka Bollywood
Jean-Claude Van Damme
Madonna
Star Jones

Marcio Maximo!

Marcio Maximo, Kocha mwenye uraia wa Brazili, aliteuliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama kocha mkuu wa Taifa Stars .

Kuchaguliwa kwake kumefuatia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Kikwete kuhakikisha anaboresha sekta ya michezo kwa kuanzia na mpira wa miguu.

Amewahi kuifundindisha Livingston Football Club huko Scotland mwaka 2003/2004. Pia ni mwanachama wa Chama cha makocha cha Brazil’s .

Kwa mujibu wa wikipedia.

Yanga kuwakosa Chuji, Cannavaro

Hivi karibuni Chuji aliweka wazi kwamba hategemei kuwepo ndani ya kikosi cha Yanga msimu ujao kutokana na kuitwa na mjomba wake nchini Hispania kwa lengo la kutafutiwa timu ya kufanya majaribio na baadaye kucheza soka huko.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es Salaam, Cannavaro (pichani jezi kijani) alisema kuna mtu ambaye anashughulikia mipango yake ya kwenda kufanya majaribio nchini humo na kama mambo yatakamilika ataondoka hivi karibuni.

Alisema amefikia hatua hiyo kutokana na kuliangalia zaidi soka la kulipwa baada ya kwenda mara ya kwanza na Timu ya Taifa ya Zanzibar na kufanya majaribio na baadhi ya timu lakini kipindi hicho hakubahatika kupata soko kwa sababu hakuwa katika kiwango cha juu kama ilivyo sasa.

“Nategemea kwenda tena Ujerumani kufanya majaribio na nikifanikiwa nitacheza huko, kuna mtu anasimamia kila kitu na amefikia hatua nzuri kwa sasa, awali nilifanya lakini sikufikia kiwango kilichokuwa kinahitajika,” alisema Cannavaro.

Mlinzi huyo wa kati aliyeitumikia Yanga kwa misimu miwili sasa, amesema ana uhakika mkubwa wa kupata timu nchini Ujerumani kwani kiwango chake kimeimarika kuliko ilivyokuwa awali.

Aidha Cannavaro aliweka bayana kuwa, kwa sasa hana mkataba na Yanga baada ya ule wa awali kumalizika pindi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilipofikia ukingoni mwezi uliopita.

“Kama Yanga wakinihitaji kwa msimu ujao, nitasaini kuichezea, lakini mambo yangu yatakapokamilika muda wowote nitaondoka kwenda kusaka maisha mapya nchini Ujerumani,” alisema mlinzi huyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo ndani ya uongozi wa Yanga, kilitueleza kwamba, piga ua lazima beki wa Simba Kelvin Yondan arithi mikoba ya Cannavaro endapo ataondoka.

“Ni kweli kuna uwezekano wa kumkosa Cannavaro endapo mipango yake itakamilika mapema, lakini hilo hatuna wasiwasi nalo kwani Yondan anatua Yanga kwa milioni 18, kwa ajili ya kuziba pengo hilo.

“Hata kama Cannavaro hataondoka, lazima tumnase Yondan ili aweze kusaidiana naye, kwani huyo ndiye chaguo la kwanza la kocha, kwa sasa mipango inaendelea vizuri,” kilieleza chanzo chetu huku kikitahadharisha kutotajwa jina gazetini.

Kiliongeza kuwa, uwezekano wa kumnasa kiungo ambaye ametupiwa virago na Timu yake ya Al Tadhamon ya Kuwait, Nizar Khalfan bado ni tata kutokana na mchezaji huyo kudai dau kubwa ambalo ni milioni 20 huku Meshack Abel anayeichezea Mujis ya Oman akitaka milioni 12.

Kadhalika Yanga imedaiwa pia kuwa mbioni kumnasa mlinzi machachari wa pembeni wa Klabu ya Tanzania Prisons ya Mbeya, Stephano Mwasika ambaye kwa sasa anakichezea kikosi cha Taifa Stars.

“Ukweli ni kwamba Klabu ya Yanga imenipa ofa ya nyumba pamoja na milioni kadhaa endapo nitakubali kuichezea msimu ujao, sitaweza kuikataa ofa hiyo,” Mwasika aliliambia Championi jana.

Wakati huo huo, Kondic anatarajia kurudi nchini kesho sambamba na wachezaji wawili kutoka Afrika Kusini alikoenda mapema wiki hii kufanya mazungumzo nao.

Kondic alimwambia mwandishi wetu kabla ya kuondoka kuelekea Afrika Kusini kuwa, tangu kumalizika kwa ziara yao alikuwa na mawasiliano ya karibu na wachezaji hao ambao walicheza mchezo wa kirafriki na Yanga ilipokuwa imeweka kambi nchini humo.

Alisema wachezaji hao ambao walikuwa wasumbufu katika mchezo wao wa majaribio nchini humo wanatokea katika Klabu ya Might Blues na kwamba wote ni washambuliaji.

“Wachezaji ambao naenda kukutana nao ni wazuri na kikubwa ambacho walinivutia ni kasi yao wawapo katika eneo la hatari, naamini wanaweza kuisaidia Yanga ambayo inakabiliwa na michuano migumu ya kitaifa na kimataifa,” alisema Kondic.
Habari na Global Publishers, Picha na BBC

Wanja la Liverpool likikamilika


Wanja la Liverpool likikamilika, Katika picha hizo zilizotolewa na The Daily Mail zinaonyesha jinsi wanja likikamilika litavyokuwa, Wanja hili litakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wamekaa “Konfotabo” na uwezo wa kuegesha magari mengi kwa wakati mmoja, utakamilika mwaka 2010. Gharama yake inakadiriwa kufikia Paund Milioni 300.
Soma habari za uhamisho wa Klabu hii hapa chini:-

Liverpool

Liverpool
Latest News:

Udinese left-back Andrea Dossena is said to be close to a £9 million deal to join Liverpool, although Tottenham and Juventus have reportedly entered the fray. Liverpool are close to sealing a £9 million deal for Udinese left-back Andrea Dossena. Liverpool appear to be in pole position for the 26-year old after opening negotiations recently with Udinese sporting director Pietro Leonardi.

Rafa Benitez is lining up former France ‘keeper, and current Bordeaux number one Ulrich Rame to deputy for Pepe Reina. 20-year-old Napoli midfielder Marek Hamsik and Espanyol’s £6m-rated winger Albert Riera are other names being linked with the club. Riera could be a likely option as he has informed his club that he would like to leave this summer.

Liverpool have reportedly turned down a £25 million bid from Inter Milan for Steven Gerrard. The Italian giants want to make the 27-year-old their main signing as they begin their centenary celebrations.

Xabi Alonso is being linked with a £12 million move to Juventus.

Peter Crouch is up for sale and though a £15 million price tag has been hung around the striker’s neck there is still plenty of interest. Martin O’Neill and Roy Keane would be interested in buying Crouch and have the funds to pay the asking fee, as do Villareal, who, unlike Aston Villa and Sunderland, would be able to offer him Champions League football next season. At the same time the club have checked on Barcelona’s French left-back Frank Abidal, and are allegedly considering an £8 million offer.

Liverpool are preparing alternatives in case their bid to sign Gareth Barry falls through. Stewart Downingis one option that is currently being considered at Anfield, with Rafael Benitez ready to pay £12 million for the Middlesbrough winger.

Kwa habari zaidi za uhamisho wa klabs mbali mbali Gonga The Daily Mail Hapa

Miss Tanzania EU 08

Nyote mnakaribishwa

Ali Kiba kuanza makamuzi leo UK

Pichani Alikiba akiwasili UK
Ali Kiba akiwa na Wadau ndani ya Uk tayari kuanza makamuzi Leo

Kwa mara nyingine tena mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali Kiba yuko ziarani UK kwa Mualiko wa Bongo Family UK, Ali Kiba anaye tamba na nyimbo zake kam Cinderela, Nakshi Nakshi, yuko kwenye Tour iliyopewa jina la “SPRING BREAK TOUR ’08 (A BIG BANK HOLIDAY WEEKEND)”


Ratiba za Ziara hiyo iko kama ifuatavyo


Ijumaa ya leo 23rd May atakuwa :
SCOTLAND 23RD @ TIGER TIGER CLUB, GLASGOWJumamosi 24th May:

MANCHESTER @ AQUA BAR


Jumapili 25th May:

BIRMINGHAMNa Onyesho la mwisho ni Ijumaa 30th May:


IN LONDON @ CLUB AFRIQUEKwa habari zaidi watembelee
http://www.bongouk.com

Thursday, May 22, 2008

David Cook ndiye American Idol Mpya!!

David Cook – American Idol Mpya!!

David Cook alisherehekea jana usiku baada ya kuibuka mshindi wa American Idol 2008 kwa kumshinda mpinzani wake David Archuleta , David mwenye miaka 25-alimshinda David (17) kwa kura Milioni 12 zaidi.

Na katika jambo la kushangaza jaji Simon Cowell aliomba msamaha kwa Cook kwa kile alichosema kumkosoa wakati akiimba wimbo wake wa mwisho.

Cowell alisema kuwa, maoni aliyotoa kwa Cook usiku mmoja kabla ya fainali hiyo hayakuwa ya busara na hayakumstahili David.

Alisema, nilipokwenda nyumbani na kuiangalia tena nilijiona nimemkosea kwa maoni ambayo niliyatoa. Hatimaye Cowell aliwapongeza wote wawili kwa ushujaa waliounyosha mpaka kufikia fainali hiyo, “kwa mara ya kwanza tangu nianze sitojali nani atashinda, kwangu wote mko sawa”

Kinyume na matarajio ya wengi ambao kwa kiasi kikubwa walimpa nafasi Archuleta ya ushindi wa mashindano haya, David Cook na David Archuleta kwa kiasi kikubwa waliwagawa mashabiki kiasi wasijue nani wa kumchagua kwani kila mmoja alikuwa na hisia na mvuto wa kipekee.

Rafiki yangu Tanzania Dream naona una kila sababu ya kufurahi.

Pamoja na kupata mkataba wa kurekodi na promotion ya Albam na pesa Taslimu mshindi wa kwanza na wa pili wa American Idol wameibuka na gari hii aina ya Ford Escape Hybrid SUV.

RONALDO MFUNGAJI BORA UEFA CHAMPS LIGI

Christian Ronaldo (pichani) ndiye mfungaji bora wa mashindano yaliyoisha jana ya UEFA Champions Ligi kwa kupachika jumla ua magoli 8.
Msimamo wa wafungaji na timu zao ni kama ifuatavyo:-
2007/08 UEFA Champions League top scorers
Player Club Goals
Cristiano Ronaldo Manchester United FC 8
Lionel Messi FC Barcelona 6
Didier Drogba Chelsea FC 6
Steven Gerrard Liverpool FC 6
Fernando Torres Liverpool FC 6
Ryan Babel Liverpool FC 5
Dirk Kuyt Liverpool FC 5
Raúl González Real Madrid CF 5

Ni Manchester Kombe la UEFA Champions Ligi!

Wachezaji wa Man U (juu na chini) wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe

Cristiano Ronaldo akiwa na Kombe la Ubingwa

Mchezaji wa Chelsea Didie Drogba akisononeka mara baada ya timu yake kutolewa kwa penalti

Kocha wa Chelsea akimfariji kijana wake, Tunaomba radhi kwa kutokuwa hewani tangu jana kwa sababu za kiufundi hasa kwa siku na mechi kali kama ya jana.
Ila pata yaliyojiri hasa kipindi cha Penalti kwa kubofya hapa.

video

Wednesday, May 21, 2008

Serge Mavili aka Celeo Scram kijana wa Wera anayekuja juu kwa kasi

Celeo kwenye Cover ya CD/DVD yake

Pichani Celeo kulia akiwasili kwenye msiba wa Madilu na kwa mbaali anaonekana Boss wake wa Zamani Werason akiwa na Miwani Nyeusi.

Kwa wale wapenzi wa Wenge Musica Maison Merre Watakuwa wana Mjua “Serge Mavili aka Celeo Scram” ni mmoja wa wanzilishi wa Maison Merre alikuwa anasaidiana na Bill Clinton kwenye Atalaku (kughani), Walipoondoka akina Bill yeye alibaki, kwa sasa hivi naye ametoka kwenye Maison Merre, kama ujuavyo wanamuziki Kitendo chake cha kuondoka hakikumfurahisha bosi wake Werason, na tangu hapo Celeo amekuwa anajizolea umaarufu na sifa kila uchao, maana alikutana na Bosi wake wa zamani kwenye Msiba wa Madilu,ameshindwa hata Kumuangalia usoni, Seleo ametoa Album inaitwa ” Nzoto na Nzoto”,inatamba sana kwa sasa na hata kwenye Soko la Ulaya, Seleo na shabiki mkubwa wa “Shabani Nonda” kwenye kila nyimbo lazima amtaje “Shabani Nonda”,Shabani Nonda aliwahi kumnunulia Celeo gari lenye thamani ya Usd 20,000. Wapenzi wa mpira Shaban Nonda aliwahi kuichezea timu ya soka ya Yanga kabla ya kwenda kucheza mpira wa kulipwa nje, Celeo anaishi Ufaransa ameoa mwanamke wa kizungu na ana watoto wawili wa kiume.


Tuesday, May 20, 2008

Rooney amkandia Drogba

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney amemwambiamshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba kwamba hana lolote.

Nyota huyo wa Manchester United amempiga madongo mfungaji wa Blues muda mfupi kabla ya kufanyika kwa pambano la fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya litalozikutanisha timu zao.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England alisema: ” Wakati (Drogba) yuko katika kiwango cha juu, ni mchezaji asiyeaminika. ni mkubwa, imara, anafunga magoli kwa mguu wa kushoto, mguu wa kulia, kichwa na wakati wote si wa kumchezea,” alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa Drogba kushutumiwa katika mashindano haya ambayo yanakutanisha timu za Uingereza tupu.

Kocha wa Liverpool, Rafa Benitez aliponda mchezaji huyo kutoka Kodivaa kwamba amekuwa akijiangusha kabla ya mechi ya pili ya nusu fainali mwezi uliopita.

Rooney na mchezaji mwenzie Nemanja Vidic pia wamemshutumu kuwa amekuwa akidanganya.

Rooney alisema kuwa alijisikia uchungu kuona Liverpool ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya miaka mitatu iliyopita itamfanya yeye kujiamini zaidi mjini Moscow.

Alisema: Ni vigumu kuona mmoja wa wapinzani wako anafanikiwa vitu. Wakati Liverpool ilipotwaa ubingwa, ilitia uchungu sana. Ilitufanya sisi tutake kutwaa na hata zaidi,” alisema.

Mdau akiwa “Vakesheni”

Mdau wangu Abuu “Mr Bean” wakongwe wa Mjini akiwa mbele ya Twin Tower ndani ya Kuala Lumpur Malaysia. Kazi na dawa.

Ni David Archulete ama David Cook American Idol

Kindumbwendumbwe cha mashindano ya American Idol ndio kinafikia ukingoni wiki hii huku mashabiki wakishuhudia mpambano mkali kati ya wawili hao pichani David Archulete (shoto) na David Cook ambao kwa kiasi kikubwa wamewagawa mashabiki hasa baada ya kutoka msichana pekee Syesha wiki iliyopita. Kila mmoja anapewa nafasi ya kushinda na kila mmoja ana mashabiki wake, wakati wa mwanzo wa mpambano wawili hawa walikuwa wakishabikiwa na watu wote lakini imefika mahala ni lazima kuchagua mmoja hilo ni jukumu gumu sana hata siwezi kusema nani ni zaidi ya mwingine, binafsi nawaona wote wana vipaji, kwangu huu ni mtihani kila mmoja na mvuto wa kipekee na wote wana kipaji alisema Simon, Jaji maarufu wa shindano hilo alipokuwa akiongea na Television ya FOX.

Bekham awatakia ushindi Manchester.

Fainali zilizopita Bekham aliisaidia Manchester kuchukua Kombe.

“Nimevunja ratiba yangu yote kwa ajili ya mechi ya jumatano” ndivyo alivyoaanza Bekham akiongea na Yahoo Sports, sitabahatika kwenda lakini nitaangaliazia nyumbani mechi pamoja na familia yangu na marafiki zangu, ni tukio kubwa, linanikumbusha enzi za maisha yangu ya mpira Manchester” alisema Bekham.
Manchester wanakutana na Chelsea kwenye fainali ya Mtanange wa Kombe la UEFA hapo kesho.
Mapenzi ya Bekham kwa Manchester yalianza tangu akiwa mdogo alipokuwa na miaka 12 na baba yake Ted alikuwa akimchukua umbali wa Maili 400 hadi Old Trafford kwenda kuwaona Manchester bila kukosa mechi zote muhimu, hapo ndipo Bekham alipoanza kuipenda timu hiii na kutimiza ndoto ya kuichezea.
“Nitaangali mpambano huu kwa na wasiwasi mkubwa, tuna mapumziko ya mazoezi kwenye klabu yetu, najua ni mpambano mkali maana timu zote zinajuana na zina wachezaji wazuri, ila nina imani kubwa na Manchester kushinda ila wasiidharau Chelsea ni wazuri”

Monday, May 19, 2008

Bono amshawishi Bekham kupanda Mlima Kilimanjaro

Katika kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kampeni za Unicef, Mwanamuziki wa kundi la Muziki la U2 na muanzilishi wa The ONE Campaign and (PRODUCT) RED, Bono ameamua kumshawishi na kumshirikisha Bekham (Pichani-si halisi) katika mpango huo kwa kupanda Mlima Kilimanjaro. Bado tarehe rasmi haijajulikana lakini itakuwa ni nafasi nzuri kwa Bodi yetu ya utalii na wadau wa Utaliii kwa ujumla kutumia nafasi hii kuutangaza utalii wetu na nchi yetu kwa ujumla.

Katika mashindano ya Kombe la Dunia Korea/Japan chumba alicholala nyotan huyo hadi leo bado kinauzwa aghali mnoo na muda sasa umepita. Tanzania tunaweza kuitumia nafasi hii kutangaza package za utalii na kupata watalii wengi zaidi kwani wapo wengi ambao wangependa kupanda Mlima Kilimanjaro na nyota huyu.
Bono akiwa na Mama Eusebia nchini Tanzania

ziara hiyo inaweza kumjumuisha pia golikipa wa West Ham Robert Green.
Bono amekuwa mstari wa mbele na kwa kipindi amekuwa nchini Tanzania kishiriki kwenye shughuli mbali mbali akisaidiana na Kampuni ya FOX/American Idol na Spoti na Starehe tuliwahi kumtoa habari zake bofya hapa humu.
Kujua zaidi ya Bekham angalia gazeti la The Sun hapa.

Portmouth alipochukua Ubingwa wa Kikombe cha FA

Goli moja lililofungwa na Kanu lilifanya timu ya Portmouth kunyakua ubingwa wa Kikombe cha FA. Kulikuwa na kila sababu kwa klabu ya Portmouth kusherehekea ubingwa huu baada ya kuichapa Cardiff kwa goli moja bola (1-0) katika mchezo wa Fainali wa kombe la FA uliochezwa hivi karibuni. kwani Portmouth wameshinda kikombe hicho baada ya miaka 69 kwani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1939 walipowachapa Wolves. baada ya hapo wamekuwa wakijitahidi bila mafanikio, Hata hivo Portmouth walikuwa na nafasi nzuri ya kushinda kwa magoli zaidi mchezo wa jana, baada washambuliajia wake akiwembo Kanu kukosa magoli ya wazi tangu dakika za awali za mchezo.

Mashabiki wa Portmount na Cardiff wakiingia uwanja wa Wembley kushuduhia mpambano kati ya Portmouth na Cardiff

Kanu akishangilia na mwenzie kwa Style ya chamukwale baada ya kuwatandika Cardiff bao 1-0.
Jikumbushe yaliyojiri hapa.

Ujasiriamali wa Kitamaduni

Ukipita mitaa ya Kuala Lumpur-Malaysia muda wa Usiku Eneo la Burkit Bintang utakutana na hawa jamaa ni wajasiriamali huwa wanajaza watu kwa aina ya Ngoma wanayopiga hizo ala zinatoa mlio mzuri na wamerekodi kwenye CD na hutumia nafasi hiyo kuuza CD zao ambazo hununuliwa kama njugu na bei yao ni 12 Ringit (3500) kwa kila CD.

Emillian na Irene
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Bwana na Bi Emillian Samwel Kiwehle baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mtakatifu Joseph na baadaye kwenye Sherehe ya Harusi iliyofanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View Hotel hivi karibuni. “…My Loving Shem Irene (Irene Maugo) all the best katika maisha yako mapya, Inshallah Mungu atawabariki na kuwaongoza”.

Ziara ya BCBG Ulaya


Pichani ni Papa Chery akilishambulia jukwaa katika onyesho la kwanza Bruxells Belgium
Mwanamuziki JB Mpiana na kundi zima la Wenge Muzika BCBG bado wanaendelea kukonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa Muziki wa lingala katika ziara ambayo inampitisha nchi za mbali mbali za Ulaya, katika onyesho lililofanyika wiki mbili zilizopita inasemekana palitokea fujo ambazo ziliwazidi nguvu walinzi, katika siku za karibuni kumekuwa na hati hati ya onyesho ambalo limepangwa kufanyika nchini Uingereza kutokana na masuala ya kiusalama kutokana na mashabiki kusababisha fujo kwenye onyesho la mwisho la mwanamuziki Koffi Olomide.
Ratiba ya kundi hilo iko kama ifuatavyo:-

 • 24 May – Stockholm
 • 30 May – Rotterdam
 • 31 May – Paris
 • 06 June – Lyon
 • 07 June – Switzerland
 • 13 June – Dublin
 • 14 June – Liège — farewell concert Belgium
 • 20 June – Portugal
 • 21 June – Bruxelles — Onyesho limefutwa mpaka itakapotangazwa vinginevyo
 • BCBG watarejea Kinshasa tarehe 26 June.

  Jikumbushe live hii ya Zenith (Audio Studio Version)

  JB Mpiana :: 14 June 08 :: Liège Belgium

  Kaunazi kwa mbaaaaaali!!

  sio “Unazi” ila sometimes ukikutana na kajibango ka namna hii na we unakaupenzi si mbaya kuchukua kumbukumbu atii. hii ni ndani ya Twin Tower KLCC-Kuala Lumpur Malaysia

  MIRIAM CHEMMOSS: muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model)

  Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).

  Miriam ni muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho.Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza.Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.

  Bofya hapa upate mahojiano kamili na Bongo Celebrity

  Inter Milan wachukua Ubingwa tena!!!

  MILAN, May 18 (Reuters) – Zlatan Ibrahimovic akiwa ameifungia timu yake mabao mawili na kuihakikishia ushindi na kuchukua kikombe tena, katika mchezo uliochezwa leo dhidi ya Palma na kushinda magoli 2-0 na kuwafanya kuchukua kombe kwa miaka mitatu mfululizo.

  Mechi ya leo ilikuwa ngumu na kila timu ilikuwa inataka ushindi, mashabiki waliipania na wachezaji walipania, jambo lililofanya mashabiki kadhaa kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na polisi mmoja kwenye fujo zilizotokea nje ya uwanja mara baada ya mpira kumalizika.

  Mc wa Uzinduzi wa Akudo wamuona atiii?

  Maimatha Jesse, mtangazaji wa Channel 5 ndiye alikuwa MC katika uzinduzi wa Akudo Impact Diamond Jubilee.

  Uzinduzi wa Akudo wawachengua mashabiki

  Sehemu ya kundi la Akudo Impact likishambulia jukwaa wakati wakitambulisha nyimbo za albamu yao mpya ya Impact, katika ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia jana katika onesho ambalo lilisindikizwa na Jahazi Modern Taarab na Bozi Boziana kutoka DRC. Mtindo wa Pekechapekecha uliacha mashabiki wakipagawa!

  Wazee wa masauti wakikabidhiwa ‘mikoba’ na Bozi Boziana wakati wa uzinduzi wa albamu yao alfajiri ya jana Diamond Jubilee.

  Mwanamuziki kutoka DRC, Bozi Boziana, ‘Benz’ akiwa katika jukwaa la Akudo Impact alfajiri ya jana wakati akiwasindiza ‘wazee wa masuati’ katika uzinduzi wao. Bozi alikonga nyoyo za mashabiki wa vibao vyake vya zamani ambavyo wabongo wanavikumbuka.
  Huyu ni miongoni mwa safu ya wanenguaji machachari wa Akudo Impact akipagawisha mashabiki katika uzinduzi wa albamu yao uliofanyika jana pale Diamond Jubilee na kuacha gumzo jijini Dar.

  Picha zote na habari na Global Publishers

  Defao na Wazee wa Mujini!

  Mwanamuziki kutoka Kongo Jenerali Defao akionyesha umahiri wake wa kunengua katika onyesho la sherehe za kutimiza miaka kumi ya bendi ya FM Academia zilizofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Msasani Club.

  Mc wa onyesho la bendi ya FM Academia kutimiza miaka kumi Beni Kinyaia akimtambulisha mwanamuziki kutoka Kongo Jenerali Defao mara baada ya kupanda jukwaani usiku wa kuamkia jana.
  Habari na picha na Global Publishers

  Mbwembwe za wanasoka!!

  Mchezaji wa Sevilla Dragutinovic akishangilia baada ya timu yake ya Sevilla kushinda 4-1 dhidi ya Athletic wakati wa mchezo wa ligi ya Spain taree 18 May 2008.

  Furaha ya ushindi!!

  MADRID, SPAIN – MAY 18: Marcelo (kati) wa Real Madrid akiwa amelishikilia kombe la ubingwa wa Ligi ya La Loga akiwa na wenzake Sergio Ramos (L) na Ruud van Nistelrooy (R) mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Levante huko Santiago uwanja wa Bernabeu.

  Raha ya Ubingwa Real Madrid

  Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wamelishikilia kombe lao la Ubingwa baada ya kushinda ligi ys Spain kwa msimu huu huko Santiago kwenye uwanja wa Bernabeu, Madrid mnamo May 18,2008

  Saturday, May 17, 2008

  Ronaldo: “Napenda kucheza La Liga Spain”

  Cristiano Ronaldo amedokeza kuwa ataifikiri zaidi klabu yake ya Manchester United zaidi mara baada ya Fainali ya dhidi ya Chelse ingawa anashawishika na ligi ya Spain La Liga kupitia klabu ya Real Madrid.

  Ronaldo (23) amekuwa gumzo katika soko la wachezaji soka ulimwenguni kwa sasa hasa baada ya kuifungia timu yake jumla ya magoli 41 msimu huu,

  Madrid wameonyesha nia ya kumtaka Ronaldo na kwa siku za karibuni harakati zinasemekana zimepamba moto na wamesema wako tayari kutoa kitita cha Pound £100million. Sijaamua lolote kwa sasa najisikia raha kucheza hapa, mawazo yapo kwenye mchezo na Chelsea kwa sasa ngoja tuangalie baada ya mchezo huo, alisema Ronaldo akihojiwa na Spanish TV network Antena 3.

  ‘Najua Real Madrid wanavutiwa na uchezaji wangu, najua pia kuna Timu Spain zinavutiwa na mimi pia, ni vizuri kujua kuwa kuna timu zinavutiwa na wewe, nimesema mara milioni kuwa ninapenda sana kucheza Spain, alimalizia Ronaldo.

  Viera: Arsenal watampoteza Gallas wasipokuwa makini

  Kapteni wa zamani wa timu ya Arsenal Patrick Vieira anasema anahofia matokea kama kocha Arsene Wenger ataamua “kumvua” nafasi ya kepten mchezaji William Gallas.

  Uongozi wa Gallas’s umeleta kelele sana kwa siku za karibuni kutokana na timu yake ya Arsenal kutofanya vizuri na hata kutochukua kikombe kwa mara nyingine tena, matokeo ambayo inasemekana yatamfanya Wenger kubadili na kumtoa Gallas kama Kepten wa timu hiyo.
  “Arsenal wanahitaji ubembeleza wachezaji wao, kwa mujibu wa malipo ya Arsenal kwa sasa ni rahisi kwa mchezaji kuondoka, tayari wamepata pigo kwa kuondokewa na Flamini aliyekwenda AC Milan alisema Viera, ni lazima watoe mikataba minono ili kuwafanya wachezaji wazuri wakae, vinginevyo timu haitakuwa wachezaji”.

  Bayern Bango kuuuuuuubwa!!

  Mafundi wakimalizia kuweka bango kubwa likiwa na wachezaji wa timu ya Bayern Munich katika eneola “Alte Boerse” (Soko la zamani la Hisa) katikati ya jiji la Munich. Bango hilo lina ujumbe usemao “Sisi ni FC Bayern ! Tuna rekodi ya ubingwa!, Tunarekodi ya Vikombe vya ushindi!, Tuna rekodi ya bango kubwa!, Twashukuru wapenzi wetu!, Bango hilo lina ukubwa wa Mita za mraba 180.

  Oliver Kahn Kucheza mechi yake ya mwisho leo

  Golikipa wa Bayern Munich Oliver Kahn, Jumamosi ya leo anacheza mechi yake ya mwisho kabla ya kustaafu mchezo wa soka rasmi baada ya kutumikia mchezo huo kwa miaka 21, Mchezo wa leo ni mgumu kwani timu inayocheza na Bayern ni nzuri pia na Oliver Kahn atataka kustaafu vizuri kwa ushindi kwa timu yake na bila yeye kufungwa, Bayern Munich wanawakaribisha Hertha Berlin leo kwenye ligi ya Bundesliga.

  Miss Chang’ombe Mazoezini

  Pilika pilika za kumsaka Miss Tanzania zimeanza hivo pichani baadhi ya wanyange wanaowania Taji la Miss Chang’ombe 2008 wakijifua katika Ukumbi wa Sigara (TTC), Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.

  Na Global Publishers

  Philipp kuichezea Bayan Munich mpaka 2012.

  Beki wa Ujerumani Philipp Lahm, ameamua kuongeza mkataba na timu yake ya Bayan Munich baada ya kuwa na maongezi na kocha wake Jugen Klinsmann, katika mkataba mpya Philipp atakaa na timu hiyo mpaka mwaka 2012.

  Thursday, May 15, 2008

  Ngoma Inogile American Idol

  Wanafainali wa shindano la American Idol David Cook na David Archuleta, hii ni baada ya Syesha Mercado mwanadada pekee aliyekuwa amebakia “kupata kura chache” katika onyesho la jana.

  Syesha Mercado, Kura hazikutosha na hivyo kupigiwa kura ya kutoka na kubaki kindumwendumbwe kwa vijana wawili.
  Majaji wa American Idol toka shoto Randy Jackson, Paula Abdul na Simon Cowell
  Mshiriki wa American Idol David Archuleta pamoja na mama yake, Lupe Archuleta, shoto, wakiwapungia mashabiki kwenye shule anayosoma May 9, 2008, huko Murray, Utah. Mashabiki wanampa David nafasi kubwa ya kushinda.
  David Cook akiimba wimbo wa ‘Take Me Out to the Ball Game’ kwenye mchezo wa ligi ya Baseball kati ya Baltimore Orioles na the Kansas City Royals uliofanyika Kansas City, Mo.

  Video na Mchezaji wa Wiki: Didier Drogba

  Tarehe ya kuzaliwa 11-Mar-1978

  Mahali alipozaliwa Abidjan, Ivory Coast
  Urefu 6’2
  Uzito 13st 3lbs
  Club Chelsea
  Nafasi Forward

  Didier Drogba
  Kwa mujibu wa gazete la Sports Gazzette la Italy, Dgrogba ni mmoja wa washambuliaji hatari sana katika bara la ulaya, linizungumzia sifa binafsi za Drogba gazeti hilo lilisema, “Drogba haogopi, ana mbio, ana nguvu na uwezo wa kumiliki mpira, misuli yake imeshika vyema, ni aina ya washambuliaji ambao mabeki wengi wanawaogopa”.

  Akiongea na Televishen ya Chelsea kuhusu kucheza kwake mpira Uingereza Drogba alisema anafurahia sana kwani ligi ya uingereza inakutanisha wachezaji toka nchi mbali mbali duniani wenye vipaji lakini kitu pekee anacholalamikia ni ubaguzi, Drogba aliongelea hili alipoongea na Televisheni ya CFI (Chanal Franc Internationa) wakati wa kombe la mataifa ya Africa juu ya kitendo chake cha kumshika korodani mchezaji mwenziwe Van Bommel’s wakati timu yake alipocheza na Netherlands, Drogba alisema

  “natamani ningekuwa na tape recorder ili niweze kuyarudia maneno ambayo wanasemaga hawa watu yenye ubaguzi, huwezi kuvumilia, wakati mwingine huoni adhabu anayofaa kupewa hivyo unaamua lolote lililoko kichwani kwa muda huo.

  Bozi Boziana ndani ya Africa Bambataa

  Toka kushoto mfanyakazi wa Clouds Fm Nasoro, Mwanamuziki wa Bozi, Prodyuza wa Africa Bambataa Joyce Kiria, Dj Too Short, Bozi Boziana, Malkia Sofia Kessy na Agape Msumari wakipiga picha ya pamoja baada ya mahojiano ya moja kwa moja na Bozi Boziana kwenye kipindi cha Africa Bambataa jana jioni.
  Muzee Bozi Boziana akiwa na muimbaji wake walipokuwa Live kwenye kipindi cha African Bambataa Jana jioni.
  Mtangazaji wa Clouds FM African Bambataa Malkia Sofia Kessy akirusha kipindi cha mahojiano na Bozi Boziana Jana. Sofia leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, Happy Birthday Dadaa.

  Toka kushoto Muimbaji wa Bozi, Prodyuza wa Africa Bambataa joyce kiria , Agape Msumari na Bozi Boziana.
  Muimbaji wa Bozi Boziana, Prodyuza Joyce Kiria, Malkia Sofia Kessy, Bozi Boziana na Baunsa wa Akudo jana kwenye studio za Clouds Fm.

  Akiongea kwenye kipindi hicho jana, pamoja na mambo mengine yahusuyo muziki Bozi aliongelea mabadiliko ya muziki kama haya walioyafanya akudo impact kuufanya muziki wa dance kuwa tofauti na wazamani yani kuuweka katika sura ya kizazi kipya cha muziki wa dance. Bozi alisema “Ni vizuri nakubali na nafurahia sana kuona mabadiliko na ndio maana leo nipo hapa Tanzania kuwarithisha mikoba yangu vijana wa masauti kwakuwa na mimi ni baba wa masauti Pia Bozi alizungumzia suala la kijitoa kwa wanamuziki na kuanzisha bendi zao wenyewe au wanakuwa Solo na kusema “Unajua watu wamekuwa na mitazamo tofauti tofauti tofauti wakidhani kuwa akiondoka katika bendi fulai ndio kupata mafanikio lakini sivyo na wakati mwingine ndivyo so sikatai kuhama kwao ila wajiangalie kabla ya kufanya maamuzi maana unaweza kutoka ukafanikiwa na unaweza ukatoka na usifanikiwe pia, lakini mara nyingi nyota ya mtu hung’aa akiwa na bendi husika na unaweza usifanye vizuri, kwani katika muziki watu hutegemeana pia.
  Mwanamuziki Bozi Boziana atawasindikiza Akudo sound kwenye uzinduzi wa albamu yao kesho.

  Jikumbushe na wimbo huu wa Bozi Boziana

  Wednesday, May 14, 2008

  Bozi ndani ya Zizou Fashion  Mwanamuziki Bozi Boziana akifanya shopping kwenye dula la Zizzou Fashion Sinza leo asubuhi, akiwa ameongozana na stage shoo wake, pichani Bozi Boziana akichagua kiatu kutokea huku mnenguaji wake Blaisesse Ayembe akimsistiza kutokiacha kibuti hicho ambacho mabrazameni wamekipa jina la Ngwasuma.
  Na Global Publishers

  Uzinduzi wa Akudo Bozi atua Dar

  Baadhi ya warembo waliojitokeza kumlaki Muzee Benzi, aliyeipa mgongo camera na kaptula ya khaki ni Aunt Lulu aliyekuwa Bingwa wa shindano la Kimwana Manywele wa Twanga Pepeta mwaka juzi.

  Mkongwe wa DRC – Congo Bozi Boziana (kushoto) akisalimina na King Kikii na Kassim Mapili (katikati) alipowasili jana jijini Dar es Salaam.


  Mwanamuziki mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbezu Bokili maarufu kama Bozi Boziana akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuwasili nchini jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal Nyerere Dar es Salaam. Atasindikiza uzinduzi wa albam ya Akudo.
  Leo Bozi Boziana atakuwa na mahojiano na Kipindi cha Africa Bambataa kinachorushwa na Clouds Fm. Clouds ni mmoja wa wadhamini wa uzinduzi wa wanapekechapekecha Akudo Impact.
  HAbari na picha na Father Kidevu

  Concert ya JB Mpiana Rotterdam

  Kagera Yapeta kombe la TAIFA

  TIMU ya soka ya Mkoa wa Kagera ‘Lweru Eagles’ jana ilitinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa baada ya kuifunga Ruvuma kwa penalti 4-2.
  Hatua hiyo ya kupigiana matuta ilikuja baada ya timu hizo kufungana mabao 2-2 katika dakika 90 za mchezo huo. Katika utaratibu huo Kagera ilipata penalti 4, huku Ruvuma ikipoteza penalti 2 na hivyo Kagera kutinga hatua hiyo, ambapo sasa itacheza na Arusha.
  Penalti za Kagera zilikwamishwa kimiani na David Charles, Martin Muganyizi, Juma Seif na Yahya Khan, wakati za Ruvuma n Ramadhani Kudunda na Paston Chawinga, huku Idd Ajira na Abdallah Ausi wakipoteza. Katika dakika 90 za mchezo huo, Kagera ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya pili na Mussa Ngunda akiunganisha krosi ya Shamte Ally Ruvuma ilisawazisha bao hilo dakika ya 31 mfungaji akiwa Abdallah Ausi aliyetumia vyema makosa ya kipa Odo Nombo wa Kagera aliyetoka langoni. Kagera ilipachika bao la pili dakika ya 45 mfungaji akiwa Paul Ngwai kwa shuti lililomshinda kipa Faraja Luanda, ambapo Ruvuma ilisawazisha dakika ya 69 mfungaji akiwa Omari Kapilima.Paul Kabange wa Kagera alioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi kwa mchezo mbaya.

  Scolari: Nategemea Ronaldo kuwa kwenye kiwango hichohicho

  Ronaldo ameifungia klabu yake ya Manchester magoli 41 kwa msimu huu.
  kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno (Portugal) Luiz Felipe Scolari amemtaka Ronaldo kuonyesha umahiri wake kama anapokuwa na kikosi chake atakapojiunga na timu ya Taifa mara baada ya Mechi yao n Chelsea tarehe 22 mwezi huu kwenye kinyang’anyiro cha Euro 2008.
  Ronaldo na Nani wote wakiichezea Manchester United wametajwa kuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya michezo hiyo inayotazamiwa kuanza tarehe 7 June.
  “Hakuna wasiwasi Ronaldo yuko fit na kwenye kiwango, ila siwezi kuahidi kuwa atacheza kwa kiwango mnachomuona nacho leo hii akiwa na klabu yake ya Manchester, alisema Scolari.
  difenda wa Chelsea Ricardo Carvalho na Paulo Ferreira ni miongoni mwa wachezaji waliomo kwenye kikosi cha Scolari.
  Hivi majuzi Chelsea wametangaza kumnyakuwa mchezaji mweingine machachari toka Urno mzaliwa wa Kongo Jose Bosingwa kwa kitita cha £16.2milioni.

  Drogba, Terry kucheza na Man U.

  Boss wa Chelsea Avram Grant anategemea wachezaji wake John Terry (shoto) na Didier Drogba (kulia) wanatarajia kupona na kuwemo kwenye kikosi cha Chelsea kitakachocheza kwenye fainali Moscow.
  Terry na Drogba wote kwa pamoja waliumia wakati wa mchezo na Bolton jumapili iliyopita.

  akiongea kuhusu wachezaji hao Grant alisema: “Tunahitaji kusubiri mazoezi ili siku ya Jumatano ili tuone hali zao, lakini Terry nafikiri atakuwa ok mpaka siku ya Mechi, Drogba alipata maumivu makali kwenye kisigino ila daktari anasema ataweza kucheza, nafikiri atafanya linalowezekana tuwe naye uwanjani tunamhitaji”.
  Drogba aliliambia gazeti la Ufaransa L’Equipe kuwa kuumia kwake si saaaana na aliongeza kuwa hakuna anayetaka kuikosa hii mechi, nitakuwepo.”
  Drogba alisema kuwa mguu alioumia ni ule ule alioumia na kufanyiwa upasuaji mdogo mwezi December mwaka jana, ila si kitu nitakuwepo mazoezini wiki hii.
  Chelsea wanatarajiwa kukutana na Manchester United kwenye Kinyang’anyiro cha Fainali za Kombe la UEFA kitakachofanyika Moscow Urusi tarehe 22 May 2008.

  Thiery Hanry ndani ya Champion for Africa.

  ‘Kanoute’s friends’ team player Thierry Henry (R) shakes hands with International Team’s goalkeeper Casillas before thier friendly football match “Champions for Africa” at the Sanchez Pizjuan stadium in Sevilla, southern Spain, on May 13, 2008.

  Champions for Africa

  Kanoute’s friends team and International Team players are pictured before their friendly football match “Champions for Africa” at the Sanchez Pizjuan stadium in Sevilla, southern Spain, on May 13, 2008

  Atlas na Boca leo

  Kocha wa timu ya Atlas ya Mexico Miguel Brindisi, wa tatu toka kulia, akiongea na wachezaji wake wakati wa mazoezi kwenye uwanja wa Amalfitani Stadium huko Buenos Aires, jana, Timu hii itacheza na Boca Junior ya Argentina leo tarehe 14, katika mtanange wa kinyang’anyiro cha Copa Libertadores.

  Mashabiki wa Bekham

  Mashabiki waliofika kwenye uwanja wa Commonwealth Stadium, Edmonton huko Alberta kuangalia mpambano wa soka wa kirafiki kati ya Los Angeles Galaxy na Vancouver Whitecaps, jana May 13, 2008.Timu ya Los Angels Galaxy ndiyo timu anayochezea David Bekham kwa sasa.

  Tuesday, May 13, 2008

  Mwana wa Rais Bush, Jenna Bush Afunga ndoa.

  Rais Bush akila Pose la Picha muda mfupi kabla ya kufungwa ndoa kati ya Mwanaye Jenna na Henry Hager Jumamosi tarehe 10 May, 2008

  Familia ya Rais Bush toka shoto Barbara ambaye ni pacha mwenzie Jenna, Laura na George
  siku ya harusi ya Jenna.

  Jenna na Henry wakishikana mikono mbele ya Kiongozi wa Kanisa wakati wakifungishwa ndoa Jumamosi ya tarehe 10 May, 2007.

  Rais Bush alitumia mwezi mzima kwa maandalizi ya harusi ya kipenzi binti yake Jenna. hatimaye Jumamosi yakatimia katika harusi iliyofanyika katika Ranchi ya Rais huyo.

  “Mwanetu kipenzi Jenna amefunga ndoa na kijana mzuri kwa kweli, ni rafiki yake wa siku nyingi Henry Hagga, alisema Bush akiwa sambamba na na mkewe Laura wakati wakipanda ndege kurejea Ikulu kwa shughuli za ujenzi wa Taifa.

  Ndoa hiyo ilifungwa huku kukiwa na ilinzi mkali eneo lote ikiwa ni tangu siku kadhaa kabla ya harusi eneo hilo lilikuwa kwenye ulinzi mkali, ndugu jamaa na marafiki wa familia zote mbili walijumuika kula na kunywa.

  Tukio hili la kifamilia halikuonyeshwa moja kwa moja na Televisheni za Marekani kwani familia ya Bush haikupenda hilo.

  Na southernledger.com

  Mkongwe Suge Knight alambwa kichapo

  Mkongwe Suge Knight alilambwa kichapo katika ugomvi ambao ulihusisha kundi la watu wakiwa Club.

  Kwa habari na picha zaidi mtembelee Haki Ngowi

  Kapt. Komba Awakoromea Misambano,Hegga


  Mkurugenzi wa T-RESPECT (T.O.T), Kapteni John Komba (pichani) ,mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka mbogo na kutaka kuwalamba vibao wanamuziki wake,Rogart Hegga na Abdul Missambano ambao walishindwa kusimamia vizuri mazoezi ya bendi yao, yaliyokuwa yakifanyika ndani ya Ukumbi wa Dar West Park, Tabata, Dar es Salaam.
  “Nononooo, hebu njoooni hapa, bado sijaridhika na safu ya unenguaji, kuna sehemu wanakosea, nataka warudie kucheza na makosa kama hayo nisiyaone tena,” alisikika akifoka Kapteni Komba.Pamoja na makosa hayo madogo madogo, bendi hiyo kwa sasa inakuja juu katika sanaa ya dansi na tayari imeshaonesha kuwakuna mashabiki kibao wanajitokeza mazoezini.Habari hii kwa hisani kubwa ya Haki Ngowi

  Bekham aitwa Kikosi cha Uingereza

  NYOTA wa zamani wa Manchester United, David Beckham ametajwa katika kikosi cha England kitakachocheza mechi za kirafiki na Marekani, Trinidad na Tobago. Kocha Mkuu wa England, Fabio Capello amemtaja kiungo huyo ambaye hivi sasa anakipiga katika klabu ya Los Angeles Galaxy kuwa ni miongoni mwa wachezaji 3, ambao wataivaa Marekani kwenye Uwanja wa Wembley Mei 28 na katika mechi nyingine dhidi ya Trinidad itakayofanyika Juni mosi.
  Terry aliyepata majeraha wakati wa mechi ambayo Chelsea ilitoka sare ya bao 1-1 na Bolton anatarajiwa atakuwa amepona na ni miongoni mwa wachezaji watano kutoka kikosi chaBlues. Mbali na wachezaji hao, pia kocha Capello ameita wachezaji wanne kutoka timu ya Manchester United, ambayo juzi ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya 10 katika kipindi cha miaka 16 na mara ya pili mfululizo baada ya kuichapa Wigan mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya ligi hiyo. Katika kikosi hicho Capello amewaita mabeki watatu wapya akiwemo wa Everton, Phil Jagielka wa Middlesbrough, David Wheater na wa Blackburn, Stephen Warnock na pia amemuingiza mshambuliaji wa West Ham, Dean Ashton ambaye alitajwa katika kikosi ambacho kiiikabili Ugiriki mwaka 2006, lakini akakabiliwa na matatizo ya enka akiwa mazoezini.
  Kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone mshambuliaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor na mlinda mlango wa Manchester City, Joe Hart pia kwa mara kwanza wataonekana kwenye kikosi hicho. Kikosi kamili kilichotajwa na kocha huyo ni walinda mlango, David James (Portsmouth), Joe Hart (Manchester City) na Chris Kirkland anayedakia Wigan.
  Mabeki ni Wayne Bridge (Chelsea), Wes Brown (Manchester United), Ashley Cole (Chelsea), Rio Ferdinand (Manchester United), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Portsmouth), John Terry (Chelsea), Stephen Warnock (Blackburn), David Wheater (Middlesbrough) na Jonathan Woodgate (Middlesbrough). Viungo ni Gareth Barry (Aston Villa), David Beckham (Los Angeles Galaxy), David Bentley (Blackburn), Joe Cole (Chelsea), Stewart Downing (Middlesbrough), Owen Hargreaves (Manchester United), Tom Huddlestone (Tottenham), Steven Gerrard (Liverpool), Jermaine Jenas (Tottenham), Frank Lampard (Chelsea), Theo Walcott (Arsenal) na Ashley Young (Aston Villa). Washambuliaji ni Gabriel Agbonlahor (Aston Villa), Dean Ashton (West Ham), Peter Crouch (Liverpool), Jermain Defoe (Portsmouth), Michael Owen (Newcastle) na Wayne Rooney (Manchester United).

  Maradona uwanjani tena


  Mchezaji wa Argentinean Mkongwe Diego Armando Maradona akionyesha mbwembwe katika mchezo wa Hisani jana.

  Maradona na Zico

  Wakongwe wa soka Diego Armando Maradona, kushoto, na Mchezaji wa zamani wa Brazili ace Zico wakati wa mchezo wa Maalum wa hisani wa Soka kwenye uwanja wa Rome Olympic stadium, jana jumatatu May 12, 2008.

  Bekham wa makeke…

  Mchezaji wa Los Angeles Galaxy’s David Beckham akipita kwenye uwanja wa ndege wa Edmonton International Airport akiwa na timu yake Jumatatu May 12, 2008 huko Edmonton, Alberta. The Galaxy wako Edmonton kucheza na timu ya Vancouver Whitecaps leo jumanne, May 13. Tangu mchezaji huyo ahamie Ligi ya Amerika kumekuwa na ongezeko kubwa la wapenzi wa mchezo huo ikilinganishwa na awali na amekuwa kivutio kila anapopita.

  Ferguson ahaidiwa Mshiko kuimarisha Kikosi

  Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester David Gill

  Mkurugenzi mtendaji wa Manchester United David Gill amemuahidi Sir Alex Ferguson kitika kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake cha ushindi kwa msimu ujao.
  Gill alisema: “Tuko kwenye nafasi ambayo tunahitaji kuiimarisha ili tuweze kubaki juu”.
  “Mi ligi bora katika dunia, kama tunahitaji kuwa bora zaidi ni lazima kuangalia katika kikosi chetu, tuanzie hapa tulipo kuhakikisha kila udhaifu unafanyiwa kazi”
  Mkurugenzi huyio aliyasema hayo katika shamrashamra za kusherehekea ubingwa wa timu yake iliyoupata jumapili hii.

  Tunafurahia kuwa pamoja na Owen Hargreaves, Anderson, Carlos Tevez pamoja na Nani ambao kwa pamoja waliongezwa kwenye kikosi na matunda tunayaona.

  CHELSEA yamnyakuwa Mcongo toka Porto

  Timu ya soka ya Chelsea imekamilisha kutia saini mkataba na mchezaji wa Porto Jose Bosingwa mkataba wa miaka mitatu kwa thamani ya Pound £16.2milioni.
  Mchezaji huyo mwenye miaka 25 raia wa Ureno na mzaliwa wa Congo ataungana na timu yake mpya ya Chelesea mara baada ya michezo ya Euro 2008.
  Bosingwa, ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Manchester United, alizaliwa katika Jamhuri ya watu wa Kongo lakini alihamia Ureno akiwa bado mdogo.
  Ndoto zangu ni kucheza timu kubwa, nilikuwa nachezea timu kubwa lakini kwa sasa nakwenda wenye timu kubwa zaidi, nina marafiki kule Chelsea, nia na ndoto yangu ni kuona tunabeba Kombe, na natumai tutafanikiwa nikiwemo pia. alisema Bosigwa alipokuwa akiongea na Chelsea Televisheni.

  FM V/s Akudo Ngoma inogile

  Vita ya Akudo ya Akudo na FM inaendelea na FM kusisitiza uwepo wa onyesho lao, likiwa na kila kitu kimeshabihiana na maandalizi ya Uzinduzi wa Akudo “wazee wa masauti”, Katika Onyesho la FM ambalo linatazamamiwa kuwa katika ukumbi wao wa nyumbani wa Msasani Fm wapepanga kumleta General Def Defao akiwa na Montana ambaye alijitoa kipindi fulani na kuwa na Koffi pia wameweka kikundi cha Taarabu cha zanzibara star ambapo katika uzinduzi wa Akudo wao wanamleta Nguli Bozi Boziana na watasindikizwa na Mzee Yusuph na Jahazi Morden Taarab.
  Pamoja na wadhamini wengine Akudo wanadhaminiwa na mabingwa wa Burudani Redio ya watu Clouds FM kupitia kipindi chao cha Africa Bambataa.
  Wakiongea baadhi ya wapenzi wa burudani wametoa maoni yao wengi wakikilaumu kitendo cha FM kwa kusema kuwa FM wangewaachia Akudo wamalize Uzinduzi wao, “sio kweli kila mmoja ana wapenzi wake” alisema mmoja wa wadau hao. Ukienda FM mashabiki ndio hao hao unaowkuta kwenye shoo za Akudo, sikiliza hata ma PDG wanaoimbwa ni wale wale tuu, hiii inaonyesha kuwa wanategemea kwa upande wa wapenzi”.
  Binafsi nafikiri FM wanatumia nafasi ya kuwa kwenye soko siku nyingi na ni kweli FM wana waenzi wakudumu ambao pia huenda kwa Akudo, lakini wao kwa vile wako kwenye game siku nyingi wangewaacha Akudo wamalize tu haiwapunguzii chochote, alisema shabiki mwingine ambaye ni maarufu kwa bendi zote mbili.

  Monday, May 12, 2008

  Yaliyojiri Viwanjani Jana

  Baada ya miezi tisa ya Mchakamchaka wa Mtanange wa Premier League hatimaye Manchester wanatawazwa mabingwa kwa kushinda pointi mbili zaidi ya Chelsea ambao waligawana point na Bolton katika michezo yote ilochezwa jana.


  Ferguson akifurahia ushindi wake wa 10 tangu ashike usukani na timu hiyo ya Old Trafford, Manchester wanakibarua kingine wanapokutana na Chelsea kwenye mtanange wa fainali za Champions League.

  Chelsea wakishangilia goli lao katika uwanja wao wa nyumbani, hata hivyo Bolton walikaza na kumalizika 1-1.

  Birmingham 4-1 Blackburn: Mcameron Jerome akishangilia baada ya kupachika bao katika mchezo wa Birmingham na Blackburn ulikwisha kwa mabao 4-1.

  Derby 0-4 Reading: Reading walipata goli la kwanza dakika ya 15 ya mchezo kwa shuti maridhawa lililoacha mlinda mlango wa Derby akigaagaa asijue la kufanya.

  Everton 3-1 Newcastle: Yakubu aliumalizia vizuri mpira wa adhabu uliopigwa Manuel Fernandes na kuwapa goli la kuongoza mnamo dakika ya 28 ya mchezo, mpaka mwisho Everton 3-1Newcastle.

  Middlesbrough 8-1 Man City: Ilikuwa ni karamu ya Magoli, Stewart Downing ndiye aliyefungua karamu hii kwa kupachika bao kwa mkwaju wa Penati baada ya Richard Dunnes kumchezea madhambi Tuncay ndani ya Boksi.

  Sven-Goran Eriksson akiangalia timu yake ikikabiliwa na mtihani mgumu jana, hii itakuwa mechi yake ya mwisho kama Meneja wa Klabu kwani kichapo cha magoli 8-1 kimepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Bosi huyo.

  Portsmouth 0-1 Fulham: Danny Murphy ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo baada ya kuwasaidia Fulham wasishuke daraja baada ya kupachika bao mwanana dakika ya 76 ya mchezo wao na Portmouth uliochezwa Fratton Park.

  Sunderland 0-1 Arsenal: Theo Walcott alisukuma mpira kiulaini na kumuacha golikipa wa Sunderland Marton Fulop asiwe na la kufanya na kuipa Arsenal ushindi wa 1-0.

  West Ham 2-2 Aston Villa: Mpira wa adhabu uliopigwa na Nobby Solano dakika ya 8 ya mchezo, uliwapa wagonga nyundo “The Hummers” bao la kuongoza lakini mpaka mwisho wa mchezo mabao yalikuwa 2-2.

  Ashley Young alipachika bao la kusawazisha kwa Villa kabla ya Gareth Barry hajafunga na kufanya Villa waongoze mechi hiyo ilofanyika Upton Park.

  Baada ya Filimbi ya mwisho kupulizwa, wachezaji na mashabiki wa Manchester walilipuka kwa furaha na kuanza kushangilia ushindi wao wa 10 chini ya Bosi Alex Furguson, Man U walikuwa na kila sababu ya kushangilia kwani Vinara wenzao Chelsea walikuw wamewakalia kooni na wao kutoka droo ya 1-1 dhidi ya Bolton.

  Sunday, May 11, 2008

  Ni Manchester United

  Cristiano akipiga penati kufunga goli la kwanza

  Giggs Chini akipongezwa baada ya kupachika bao la pili.

  Timu ya Manchester United imefanikiwa kuchukua kombe la Ubingwa wa Premier League kwa pointi mbili zaidi ya Chelsea ambao walikuwa kwenye kinyang’anyiro kwa kuwa na pointi sawa mchezo ulikuwa mkali kwa upande wa Manchester na Wigan huku Wigan wakionyesha kuwabana na kutowapa nafasi Manchester kipindi cha kwanza ingawa kulikuwa na kosa kosa nyingi kwa kila upande, mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-o Manchester wakiongoza kwa bao moja lililofungwa na Cristian Ronaldo kwa njia ya Penati baada ya Rooney kuchezewa madhambi ndani ya boksi. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Manchester wakilishambulia lango la Wigan na Wigan kurudisha mashambulizi ingawa hayakuwatisha sana ManU kwani baada ya kubadilishwa Scholles na kuingia Gigs alileta changamoto kwa upande wa Manchester na alifanyikiwa kupachika bao la pili baada ya kupewa pasi akiwa karibu kabisa na kipa na ku press mpira ule na kuandika bao la pili, hadi mwisho ManU 2-0 Wigan.
  Matokeo ya michezo ya leo yalikuwa kama ifuatavyo.


  Mabingwa ni :
  Manchester United
  Klabu zitakazo cheza Champions League ni:
  Manchester United, Chelsea, Arsenal, Liverpool
  Uefa Cup ni: Everton
  Intertoto Cup ni: Aston Villa
  Walioshuka ni: Reading, Birmingham, Derby
  PREMIER LEAGUE
  FT Birmingham 4-1 Blackburn
  FT Chelsea 1-1 Bolton
  FT Derby 0-4 Reading
  FT Everton 3-1 Newcastle
  FT Middlesbrough 8-1 Man City
  FT Portsmouth 0-1 Fulham
  FT Sunderland 0-1 Arsenal
  FT Tottenham 0-2 Liverpool
  FT West Ham 2-2 Aston Villa
  FT Wigan 0-2 Man Utd

  Mashabiki matumbo moto

  Huku zikiwa yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya mitanange ya fainali mechi za mwisho kuamua mshindi, mashabiki wako roho juu kila mmoja akijaribu kutetea upande wake kuwa utashinda kikombe hicho. Hakuna mechi inayotabirika leo kwani kwa droo yeyote Man anabeba “chikombe” kwani Man U wanatofauti kubwa ya magoli, kwa Upande wa Chelsea wanatarajiwa kubebwa na mashabiki 62,000 walioshakata tiketi kwa ajili ya kuuona mtanange huu, ambapo inakadiriwa 90% ni mashabiki wa Chelsea, kwani Chelsea wanacheza nyumbani leo na Man U wanacheza ugenini.

  Mechi za leo ni kama ifuatavyo:-

  15:00 Birmingham C. ? – ? Blackburn R.
  15:00 Chelsea ? – ? Bolton W.
  15:00 Derby County ? – ? Reading
  15:00 Everton ? – ? Newcastle U.
  15:00 Middlesbrough ? – ? Manchester C.
  15:00 Portsmouth ? – ? Fulham
  15:00 Sunderland ? – ? Arsenal
  15:00 Tottenham H. ? – ? Liverpool
  15:00 West Ham U. ? – ? Aston Villa
  15:00 Wigan Athletic ? – ? Manchester U.

  Saturday, May 10, 2008

  Mchizi wangu Remix

  Wimbo wa wasanii Nako 2 Nako ‘We ndo mchizi wangu’ hivi karibuni umerudiwa na kufanyiwa remix ambayo imewakutanisha wasanii kibao na wakali akiwemo, Jay Moe, Fid Q, Mansu-Li, Geez Mabovu, Dr K wa Mapacha, Adili Chapakazi, Chidi Benz, Mwanafalsafah, Mheshimiwa Temba, Babuu wa King’oko na wenye ngoma yao ambao ni Nako 2 Nako Souldierz. Bofya hapa ukausikilize

  Taboo Fatoo Top Model

  Mwanamuziki Faustin Ipupa Nsimba aka Fally Ipupa Di Caprio, Album yake ya “Droit Chemin” ndiyo Album bora ya Mwaka 2007/2008, kwa sasa Albamu hiyo ndio inauza na kufanya vizuri kwenye soko, katika Album hiyo kuna wimbo unaitwa “Liputa” kwenye huo wimbo amededicate kwa Taboo Fatou ” Mama na Compressor”(pichani), huyu ni Mfanyabiashara Mrembo anaishi Belgium, ana miliki maduka kadhaa ya Nguo huko Paris(France) na Beligium,na inasemekana zile Pamba zote za Fally, Taboo Fatou ndiyo anamvalisha, kwa wale wapenzi wa JB Mpiana watumbuka katika Album yake ya Kwanza(Solo) Feux D’Lamour,kuna wimbo unaitwa “Top Model” utampata humo Tabu Fatou.

  Gonga hapo umsikie Jb Mpiana na Taboo Fatoo Top Modele”.

  Ze Comedy wajitoa East Africa TV

  KUNDI maarufu la sanaa za maigizo The Comedy (pichani) limemaliza mkataba wake na kituo cha televisheni cha East Afrika (EATV) kinachorushwa kila siku ya Alhamis.

  Kutokana na kumalizika mkataba huo kipindi hicho maarufu hakitarushwa kuanzia Alhamis ijayo. Kundi hilo liliingia mkataba wa mwaka mmoja na miezi nane kufanya kazi na EATV uliofikia ukingoni juzi.

  Ukiondoa Ze Comedy, naye Mratibu wa kundi hilo Sekioni David amesitisha mkataba na kituo hicho na sasa anaelekeza nguvu zake ndani ya kundi hilo.
  “Baada ya kuufahamisha uongozi nia yetu, nilipatwa na mtihani mgumu sana, maana niliambiwa nichague kuendelea kutangaza au kupumzika na Ze Comedy. Nimechagua kupumzika na kundi hili na sitajutia uamuzi huu hakika, mimi ni msanii msanii wa siku nyingi na nina uzoefu wa muda mrefu. Kama nilivyoweza mwazo kuiinua Ze Comedy, ndivyo nitakavyoweza kuiendeleza zaidi,’’ alisema Seki.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi hilo, Isaya Mwakilasa (Wakuvanga) alisema wameamua uamuzi huo ili kupata mapumziko kwa muda kabla ya kuendelea na sanaa hiyo.

  Mwakilasa alisema wanasikitika kumaliza mkataba na EATV na hivyo wameamua kurudi nyumbani kujipanga upya lakini pia wanaweza kuingia mkataba mpya endapo watakubaliana.

  “Mkataba wetu na EATV umeisha nasi tumeamua kurudi nyumbani kupumzika kwa nia njema, hasa kwa maslahi ya wengi zaidi na tulikuwa tukifanya kazi nao vizuri na huu si mwisho wetu,” alisema Mwakilasa.

  Mwakilasa alikanusha taarifa kuwa Ze Comedy lina mpango wa kuingia mkataba mpya na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC 1) na kuongeza kuwa sanaa ni ajira yao hivyo kama watahitajika hawasita kuingia mkataba na kituo hicho.

  Kamali ya Mpira yawanufaisha mashabiki

  Kilomita 50 toka mji wa Kuala Lumpur Malaysia, Genting (pichani) ni maarufu kwa starehe za aina zote kuna kasino kubwa ambayo hukutanisha mataikun wa kila sehemu ikiwa ni pamoja na Singapore, Malaysia, Thailand na hata Indonesia, ukifika usiku ni milio ya Helcopter kila mmoja akiingia na kutoka kwenye jumba la Casino la sehemu hii changamfu.

  Kuanzia wiki iliyopita mahoteli yamejaa kwa ajili ya weekend hii ambapo wacheza kamali wanamiminika kwa ajili ya kubashiri ushindi wa mchezo wa Mwisho unaowajumuisha Manchester na Chelsea kila mmoja akiwa na kibarua chake.

  Asia mpira ni biashara, toka kuuza jezi, sticker hadi matokeo kwani kunawaopoteza nyumba, magari na pesa taslimu kila siku, imekuwa ni sehemu ya utamaduni na ndio maana hizi timu kubwa haziishi kuja alisema Raj, Tax driver anayefanya shughuli zake Genting.

  Kuna wanaotegemea mechi hizi kula na kulisha familia, nimekuwa nikicheza kamali ya mpira kwa mika nenda rudi, ni rahisi kupoteza na kupata pia kwani kwa mechi ndogo dau ni dogo kwa mechi kubwa ambayo matokeo hayatabiriki hapo ndio wengi hucheza na wengi hupoteza alisema Raj.

  Binafsi nimenunua ticket za Ringit 800 (dola 250) nategemea ikishinda napata mara mara nne ya hapo, nasali Man washinde, siku ya Chelsea na Man nilipata Ringit 5000 (sawa na dola 1600). Nilifurahi mke wangu alikuwa na wasiwasi lakini Inshallah tukapata.

  Ronaldo na Drogba, nani ataibeba timu yake?

  Ni wazi kuwa mtanange huu wa kesho unawategeme hawa watu wawili kufanya maajabu, thamani ya magoli kwa ushindi wowote utaibeba timu husika, na nani atabaki na Kombe muamuzi ni dakika 90, kwani Machester anacheza ugenini na Chelsea anacheza nyumbani, Chelsea ana historia nzuri ya kuutumia uwanja wa Nyumbani lakini pia Manchester bado ana rekodi ya kushinda mechi nyingi hata za ugenini, hii inawapa matumbo joto mashabiki kwani kuna uwezekano mkubwa mtanange huu ukaamuliwa kwa idadi ya magoli ambayo mpaka sasa Man wako mbele kwa tofauti ya magoli 17.

  Swali langu bado lipo pale pale kombe litawekwa wapi kusubiria mwenyewe apewe kwani timu zote zinacheza kwenye viwana tofauti na kipigo cha timu moja ni furaha ya ushindo kwa mwingine iwe atatoka sare au atashinda kwa idadi yeyote ya magoli.

  Porto wapigwa faini kwa tuhuma za kupanga matokeo

  Raisi wa FC Porto Jorge Nuno Pinto da Costa, katikati na maofisa wa klabu hiyo Adelino Caldeira, right, naFernando Gomes wakiinuka kumaliza mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye uwanja wa Dragao Porto, Portugal, ijumaa May 9, 2008. Kamati ya nidhamu ya chama cha mpira wa miguu nchini humo kimewanyang’anya point Porto na Uniao Leiria kwa madai ya kupanga matokeo katika kashfa kubwa ya mchezo wa soka ambayo haijawahi kutokea. Kamati hiyo iliamua kwamba Porto walimhonga Refarii kwenye mechi mbili katika msimu wa 2003-04 na kuamua kuwanyang’anya pointi 6 na kuwapiga faini ya Euro150,000 (US$230,000) na kumzuia Mwenyekiti Jorge Pinto da Costa kwenye kuonekana kwenye benchi la akiba kwa miaka miwili.

  Figo ana imani na Pep Guardiola

  Midfielder wa Inter Milan Luis Figo, ambaye amechezea klabu ya Barcelona kwa misimu mitano mfululizo amesema, Kocha mpya wa klabu hiyo ambaye alikuwa Kepteni ya timu hiyo zamani Pep Guardiola anauwezo mkubwa na anaweza kuleta matumaini mapya kwenye klabu hiyo. Barcelona ambayo haijafanya vizuri kwenye ligi ya na hasa mechi zake za kribuni pia imeongeza nguvu kwa kumpa timu mchezaji huyu wa zamani nafasi ya kuifunza timu hiyo.
  Na BBC sports

  Wenger asema Adebayo na Hleb bado ni wa kwao

  Mchezaji mahiri wa klabu ya Arsenal Emmanuel Adebayor amekanusha uvumi kuwa anataka kuondoka klabu yake ya Arsenal na kukimbilia Italy.

  “Nina furaha na amani sana kwenye klabu yangu ya Arsenal,” alisema mshambuliaji Adebayor. “habari zinazosema nataka kuondoka ni uzushi mtupu.”

  Hleb ana husishwa na kutaka kujiunga na klabu ya Inter Milan na agent wake amekuwa akiliongelea suala hilo la mchezaji huyo mwenye miaka 27 kuwa anataka kutoka Arsenal.

  LAkini akiongea na BBC Radio 5 Live: Wenger alisema “bado hatujawa na maongezi na klabu yeyote juu ya Adebayo wala Alexander Hleb.” Hivyo mpaka sasa hawa bado ni wachezaji wetu.
  Habari za kuondoka wachezaji hawa ziliwatia matumbo joto mashabiki wa Arsenal hasa baada ya kuondoka mchezaji Flamini.
  Na BBC Sports

  Jose Mara: Akudo waache maneno tufanye kazi.

  Pichani ni Baadhi ya wanamuziki wa FM wakimpongeza Jose Mara siku ya harusi yake, Nyoshi, Pablo masai, Patchou mwamba, roger muzungu,King blaise na kushoto kabisa ni Collins (mzee wa USA), mshabiki wa FM

  Mwanamuziki Jose Mara amemsihi mwenzake Christian Bella wa Akudo Impact kuacha maneno maneno na kufanya kazi, “mashabiki hawataki maneno, mashabiki wanataka kufurahishwa” alisema Jose Mara.

  “Nilisikitishwa na kitendo cha Bella kuongea na vyombo vya habari na kusema hawezi kufananishwa na mimi, kuwa eti mi ni mchafu mchafu, na bado mtoto kisanaa ya Muziki, Bella hapaswi kusema maneno hayo, alisisitiza Jose.
  Hii yote ilitokana na suhindanishwaji wa wanamuziki hawa wawili kwenye kipindi cha kinachorushwa kwenye TV cha (Nyumbani ni Nyumbani) cha C2C na (Afro Beat) cha East Africa TV, Huwa wanashindanisha wanamuziki wawili au vikundi vinavyofanana, Kumetokea kushindanishwa zaidi ya mara mbili kati ya mwanamuziki Jose na Bella, na Jose amekuwa akishinda.

  Inasemekana hili lilimuuma sana Bella, na alipoongea na gazeti moja akasema mimi nashang’aa kushindanishwa na Jose, Kwanza Jose si wa rank yangu,Kwanza Mchafu Mchafu, yeye yupo sawa na kila Fally, Jose anasema yeye awezi kumjibu sababu majibu anayo yeye Bella, wakati wanatoka Congo, Jose alimlea Bella kwa kila kitu kula hadi Mavazi ni kama mdogo wake, anasikitishwa na kauli za Bella.

  Ushindani wa bendi hizi umekuwa kwa kasi na hasa habari za hivi karibuni ambapo Akudo wanazindua albam yao na kumleta Mzee Bozi Boziana na FM wameandaa shoo usiku huo huo wa tarehe 16 ambapo walikuwa kwenye mipango ya kumleta Bozi Boziana, jambo linalotafsiriwa kuwa wanataka kuvuruga uzinduzi wa Akudo.

  Friday, May 9, 2008

  Ronaldo aomba msamaha.

  SAO PAULO, Brazil – Kufuatia kesi ya kugombana na “mashoga” siku kadhaa zilizopita, Mchezaji nyota MBrazilia Ronaldo ameomba msamaha na jamii imusamee kwa kilichotokea kwani anajua amewakasirisha baadhi ya watu, haikuwa nia yake ila ni mapungufu ya kibinadamu. Ronaldo ameita hiyop ni aibu kubwa ya mwaka na ni kosa ambalo atajutia maisha yake yote. Huku akitoa sauti ya huruma na kuonyesha majuto Ronaldo aliiambia Televisheni maarufu ya Brasil Globo TV kuwa anajuta kwa kilichotokea, “Kwa kipindi kifupi nimeshtukia nimepungua kilo kwani hii kitu inanitesa, kama binadamu wa kawaida inauma, najuta, natamani ningeweza kurudisha wakati nyuma ili kufuta yaliyotokea, tatizo ni kuwa kumbukumbu zinahifadhika na kudumu milele, Najua kumbukumbu yangu ya mpira itadumu milele nilijivunia hilo, ila sasa nikifikiria hili nalo litadumu naombea hata niitoe vichwani mwa watu, alisema Ronaldo kwa sauti ya huruma.
  Ronaldo alituhumiwa kuchukua wanawake watatu ili akafanye nao mapenzi katika chumba chake cha hoteli lakini baada ya kufika aligundua kuw wale walikuwa si wanawake bali ni mashoga na kuwataka waondoke lakini wao walitaka mchezaji huyo awalipe jambo ambalo lilianzisha ugomvi mpaka polisi kuitwa.

  Kesi ya R. Kelly yaanza kuunguruma

  Mwanamuziki R. Kelly, lakiwasili mahakamani ya Cook County Criminal Courthouse, Chicago leo hii (ijumaa) akiwa ameongozana na mlinzi wake katika siku ya kwanza ya kusikilizwa kesi inayomkabili, Mwanamuziki huyu anashtakiwa kwa kujihusisha na udhalilishaji watoto kijinsia kutokana na makanda wa Video ambao unadaiwa kuwa unaonyesha akifanya mapenzi na mtoto wa miaka 13.

  Video na Mchezaji wa Wiki: Samuel Etoo’

  Video yetu ya wiki hii tunammulikia mchezaji wa Barcelona, Raia wa Cameroun Samuel Etoo’, mpira una matamu na mchungu, hasa kadamnasi ikionyesha kukuamini na unapoangaliwa na watu wapatao 60,000 na wote wanategemea uwafurahishe na kuwatia machungu inaumiza sana, Etoo anasema katika vitu vinavyomnyima raha kuliko vyote ni hicho. Angalia Video hii ili ujue machungu na uwezo binafsi wa mchezaji huyu.

  Jina:
  Samuel Eto’o Fils
  Uraia: Cameroon
  Tarehe na Pakuzaliwa: March 10, 1981 Nkon, Cameroon
  Nafasi anayochezea: Mshambuliaji wa kati / winger
  Klabu anayochezea: FC Barcelona (Spanish La Liga)
  Historia ya Vilabu: 1997-1998 Leganes – Mechi 28, magoli 3

  1998-1999 Real Madrid – Mechi 3 , bila goli

  1999-2004 Real Mallorca – Mechi 133, magoli 54.

  2004-mpaka sasa FC Barcelona

  Uchezaji wa kulipwa: 1996-Mpaka sasa

  Samuel Eto’o anaheshimika kama mchezaji mwenye uwezo na mmoja wa washambuliaji bora duniani kwa sasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuumiliki mpira na akili ya maamuzi ya haraka sana hasa awapo karibu na goli. Katika muda alocheza kilabu ya Real Mallorca Eto’o ndiye aliyekuwa mfungaji bora katika historia ya Klabu hiyo akimaliza na jumla ya magoli 54. uwezo huu ndio ulivutia vilabu vingi vya ulaya na kutaka kumsajili Mhcezaji huyu matata.

  Eto’o baadaye alihamia FC Barcelona 2004 kwa donge nono la ada ya uhamisho jumla ya Pound Milioni £24.
  2006 Eto’o alizawadiwa taji la “pichichi” (Mfungaji bora kwenye ligi ya La Liga) baada ya kuifungia Barcelona goli kwenye mechi ya mwisho ya msimu wa ligi dhidi ya Athletic de Bilbao.

  Etoo alipata maswahibu kwani aliumia mwaka 2006 na tangu hapo imekuwa ikimletea matatizo mara kwa mara na kumfanya kuwa nje ya dimba, ingawa timu yake haikufanya vizuri kwa msimu huu lakini bado kijana huyu amerudi kwa kasi kwenye uwezo wake wa kawaida, ingawa kuna tetesi kuwa anawaniwa na timu za Uingereza, iwe ni Spain au Uingereza bado nyota ya Etoo inaashiria kuendelea kuwaka kwa muongo mwingine kwani bado umri unamruhusu.

  Nani kuwa American Idol wa 7?

  Baada ya matokeo ya wiki hatimaye walibari watatu David Cook, David Archuleta & Syesha Mercado, mchuano bado ni mkali hasa katika ya David wawili ingawa Syesha anatoa upinzani kwa wa aina yake, ila mvuto wa akina David unamfanya awe kwenye wakati mgumu. Nani ataibuka mshindi? swali juu yako msomaji.

  Burudani ya Mpira na Muziki Giraffe Hotel

  Kwa wapenzi wa mpira, Giraffe Ocean View Hotel wanaonyesha mechi zote kwenye mandhari mwanana ya Makuti Bar ikitazama Bahari ya Hindi, Bila kusahau ijumaa ya Leo Deo Mwanambilimbi kama kawaida anatumbuiza na bendi yake ya Kalunde Band, hii ni kila ijumaa na Jumamosi, nyote mnakaribishwa.

  Allex Miller abwaga manyanga Liverpool

  Pihani ni Miller na Benitez enzi wakifanya kazi pamoja Liverpool

  Kocha namba moja wa LIVERPOOL Alex Miller amemwaga manyanga na kujiunga na timu ya JEF United Chiba ya Japan. Vyombo vya habari vya Japan vimeripoti kuwa timu hiyo ya JEF imemchukua Miller baada ya kumtimua kocha wao M-Croatian Josip Kuze wiki hii.

  Katika mkataba mpya na timu hiyo kocha Miller atalipwa mshahara wa £500,000.

  Miller, ambaye amekaa kwa kipindi cha takribani muongo mmoja Anfield, alikuja kuwa kocha wa kwanza wa Liverpool mwaka 2004 wakati Rafael Benitez alipochaguliwa Meneja.
  Ni habari njema kwa Alex, alisema Benitez jana, hii ni nafasi nzuri kwake kufanya kazi Japan, napenda kuchukua nafasi hii kumtakia mafanikio mema katika kibarua chake kipya, alimalizia Benitez.

  Kombe litakuwa wapi?

  Kwa kuwa timu zote mbili Manchester United na Chelsea wananafasi ya Kuchukua Kombe na wote wanacheza kwa siku moja, Je Kombe hili litaa wapi kwani hawa wanacheza kwa miji tofauti. Kwani inajulikana Kombe hukabidhiwa kwa Timu husika mara baada ya Mchezo kumalizika, Je kwa mpango huu Kombe litakaa mji gani?

  Manchester United: Tutajitahidi yasijirudie ya 1968

  Alex Stepney (Pichani) aliyekuwa golikipa wa Manchester United Mwaka 1968 anakumbuka sikuiku ya fainali huku wakipewa shinikizo na mashabiki kutokana na habari za mchezo uliokuwa unaendelea uwanja mwingine huku timu zote mbili zikigombea ushindi ili kuchukua kombe.

  ManU walikuwa na pointi 56 sawa na pointi 56 za mahasimu wao Manchester City, ManU walikuwa wakicheza dhidi ya Sunderland. Mashabiki walikuwa walikuwa akimpa Stepney maendeleo juu ya mchezo wa ManCity ambao kwa wakati huo huo walikuwa wakikipiga dhidi ya timu ya Newcastle. Mashabiki walikuwa wakiufatilia mchezo ule kwa njia ya redio na kutupa matokeo ili kutuhamasisha kwa ushindi, lakini mhhhh alisema Alex.

  Kiukweli sikupenda nilichokuwa nakisikia wakati ule kwani kiukweli mpaka mwisho wa mchezo tulifungwa 2-1, City wakashinda 4-3 na kuchukua ubingwa, upinzani ule haujajirudia tena mpaka sasa ndio tunaona kwenye mtanange wa jumapili hii.

  “Mashabiki walikuwa karibu kabisa na uwanja na walikuwa akipiga kelele kutwambia matokea ya City ambayo yalitutia tumbo joto na kutufanya kupanic na kushindwa mchezo ule” alisema Stepney, mwenye miaka 65 sasa.

  Mtanange wa Premier League ndio unafikia ukingoni wiki end hii huku tukishuhudia timu mbili zikikabana makoo kwa point sawa mpaka sasa Manchester United na Chelsea, wote wana point 84. ManU wanamagoli mengi zaidi ya Chelsea kwani mpaka sasa wana magili 17 zaidi ya Chelsea , kwa hivo basi matokeo ya sare yeyote kati ya timu hizo nne zitakazo cheza yanawafanya Man kuchukua ubingwa la hasha ni kuwa Chelsea ashinde na Man ashindwe, au Chelsea atoe droo na Man ashindwe, Safari ya Man U wigan na huku Chelsea ikicheza uwanja wa nyumbani inaweza kuwapa faida Chelsea kwani hizi timu ndogo zikiwa kwao huwa zinadinda sana kwa timu kubwa.

  Kimbembe hakitaishia hapo kwani kwa matokeo yeyote bado wawili hao wanakwenda kuumana tena kwenye mtanange wa fainali ya kufa mtu itakayofanyika Mei 21 jijini Moscow kwenye mtanange wa kwanza wa fainali kuzikutanisha timu zote toka Uingereza.

  O’Neill: Ofa ya Liverpool inamshusha thamani Barry

  Martin O’Neill amesisistiza kuwa kitendo cha Liverpool cha kusema kumtolea mchezaji wao Gereth Barry kiasi cha Pound 10milion ni kumshusha thamani.

  O’Neill na Barry watakauwa na maongezi katika kikao kitakachofanyika baada ya kumalizika kwa mchezo wa jumapili wa fainali ya Barclays Premier League dhidi ya West Ham kuhusu majaliwa ya baadaye ya mchezaji huyo ambaye Liverpool wanamtaka kwa nguvu zote.

  Ofa ya Liverpool ni kutoa mchezaji mmoja pamoja na donge hilo la Pound milioni 10 ambapo walitoa dau hilo hivi karibuni lakini O’Neill bado anaona kama dau ni dogo. Pia O’Neil alisema Liverpool hawajasema watatoa mchezaji gani kwani wanaweza wakakupatia mtu ambaye humuhitaji kwenye timu yako ndio maana tunakazia kwenye pesa zaidi au wangeweka wazi.

  Mazungumzo yetu si kwamba hatumtaki Barry, kwani dhamira yetu si kuuza wachezaji, dhamira yetu ni kuwa na kikosi imara na kizuri ili na sisi tufike hapo juu na ndio nafasi tunayoitaka, sasa kama mtu kampenda mchezaji wetu basi ajichinje mwenyewe, tutafanya kila linalowekana Barry abaki kwetu la haiwezekani basi tukipata dau nono litatuwezesha kutafuta mbadala wake alisema O’Neil.

  Marcio amfagilia Ivo Mapunda


  • Asema kwa Tanzania Hakuna kipa kama yeye.

  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, Marcio Maximo amesema atamtumia katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mauritius kipa Ivo Mapunda (pichani) badala ya Farouk Ramadhani.

  Mapunda aliitwa katika kikosi hicho hivi karibuni ikiwa ni miezi sita tangu awe benchi kutokana na kufungiwa na klabu yake ya Yanga kwa madai ya utovu wa nidhamu.

  Kufungiwa kwa Mapunda aliyekuwa chaguo la kwanza la Maximo kulimfanya amuite kipa Farouk Ramadhani katika mchezo wa awali wa michuano mipya ya Afrika inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani tu, ambapo katika mchezo wa kwanza Stars iliitoa Kenya ‘Harambee Stars’ kwa jumla ya mabao 2-1. Mchezo wa kwanza uliofanyika Kenya, Harambee ilishinda bao 1-0, lakini ziliporudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Taifa Stars ilishinda mabao 2-0, kipa akiwa Farouk.

  Pia katika mchezo wa kwanza hatua ya pili ya michuano hiyo dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Taifa Stars ilishinda mabao 2-0, kipa pia akiwa Farouk.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Maximo alisema analazimika kuanza kumtumia Mapunda kwa kuwa ni kipa mzuri zaidi ya Farouk na ana uwezo mkubwa kuliko kipa yeyote nchini, hivyo ana umuhimu kumtumia kwa mashindano makubwa.

  Alisema tofauti na Farouk, Mapunda amecheza michezo mingi ya kimataifa ana uwezo mkubwa kumudu mashindano yeyote makubwa na kwamba tangu kipa huyo arudi kwenye kikosi chakr amesharudi kwenye chati.

  Hata hivyo alisema katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda wiki ijayo huenda akaanza Farouk, lakini mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2010 dhidi ya Mauritius mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam atacheza Mapunda, ambapo Farouk atakuwa benchi.

  Kuhusiana na mchezo dhidi ya Uganda, Maximo alisema kikosi chake kipo katika hali nzuri isipokuwa kuna majeruhi wachache, ambao ni Uhuru na Abdi Kassim aliosema huenda wasiwepo katika mchezo huo wa marudiano kwani watakuwa nje kwa muda mrefu.

  Majeruhi wengine ni Ulimboka Mwakingwe na Henry Joseph, ambao hata hivyo watarejea uwanjani wakati wowote.

  Mheshimiwa Pinda kuupamba Uzinduzi wa Akudo

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact utakaofanyika Mei 16, mwaka huu.

  Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa tamasha hilo, Bahati Singh alisema katika uzinduzi huo, bendi hiyo itasindikizwa na mwanamuziki kutoka Kongo, Bozi Boziana na Jahazi Morden Taarabu na utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee.

  Alisema Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi huo imeahidi kutoa sh. milioni moja kwa ajili ya kusaidia kununua vitanda na magoro katika wodi ya wazazi ya hospitali ya mwananyamala.

  “Wanamuziki wametamba kutoa burudani ya kukata na shoka, ambapo wapenzi wataulizwa kama ni funika bovu au la, kama burudani haitakonga nyoyo za mashabiki, hiyo ndio itakuwa mwisho wa bendi ya Akudo,” alisema Singh.

  Singh alisema uzinduzi huo umedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake Ndovu, Vodacom, QSSP Group LTD, Clouds FM Dotnata Decoration, C2C televisheni na CM LTD.

  Tchasho Mbala

  Kwa wale wapenzi wa Muziki wa Kikongo watakuwa wanamjua au kumsikia Richard Tshasho Mbala aka Kashogi (Pichani na mkewe),ukisikiliza nyimbo nyingi za Congo utasikia jina hili, yeye ndiyo mdhamini mkuu wa Album ya Fall Ipupa (Droit chemin’) amemuoa Elvira Mujinga Mukuna,katika harusi ya kifahari ilifanyika huko Orléans (France), Inasemekana watu maarufu katika Congo na wanamuziki wakubwa wa Congo walialikwa ikiwa ni pamoja na wengine kupatiwa Ticket za Ndege kushuhudia harusi hiyo.
  Na Big Producer Maghambo

  Celtel Idols

  Hatimaye lile shindano la kumsaka kijana mwenye kipaji cha kuimba, maarufu kama Celtel Pop Idols limefanikiwa kuwapata wakali 24 (Top 24), Julius Kihampa anaanguka nayo.Washiriki hao ambao walichaguliwa na majaji Angela Angwenyi, TK Siyandi na Scar, walipatikana juzi kupitia mchujo mkali uliofanyika nchini Kenya ambapo kati yao 19 ni wasichana na wavulana 5.
  Waliotajwa kuingia Top 24 na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na Adiona Maboreke (Zimbabwe), Alice Chinyimbe (Zambia),Alice Kalufyanya (Zambia),Ammara Brown (Zimbabwe), Chibwe Chapenuka (Zambia),Christine Apondiadda (Kenya),Cynthia Kuto (Kenya),Deborah Chansa (Zambia),Doris Onyango (Kenya),Eric Moyo(Zimbabwe),Faycal Birikunzira(Uganda) na Irenne Njunguna (Kenya).Habari hii na Abdallah Mrisho.
  Na Haki Ngowi

  Thursday, May 8, 2008

  Real Madrid walipomuua Barca 4-1

  Real Madrid wamesherehekea ubingwa wa Ligi ya Spain kwa kuwachapa watani wao Barcelona mabao 4-1 kwenye kinyang’anyiro cha El Clasico derby.
  Bonyeza Player upate uhondo

  KIJIWE MAARIFA

  Karibuni kwa mara nyingine tena, husika na WAPI …tukio la kila mwezi. Kama kawaida”WAPI” inaendelea. safari hii tunajumuika na watu wa mataifa mbali mbali kwenye mada yetu BILA KUJALI TOFAUTI… kwenye KIJIWE MAARIFA tutakuwa na Kemi KALIKAWE, FATMA AMOUR WANAMITINDO/WABUNIFU mahiri. WASAMBAZIE huu waraka watu wengine kwenye orodha yako ya anuani


  Yawaletea

  Mboli -MC mahiri chipukizi, Rage- mwakilishi wa MC Afrika TZ, Enika

  Mitindo na Kemi Kalikawe, Fatma Amour.

  Wasanii wa sauti ya handaki(undeground), Katika harakati.

  Madijei, ma emsii, machata, mabreka ,michoro mbali mbali, ushairi,ngoma, maigizo na usanifu mitindo.

  Mahali: British Council, Dar Es Salaam
  (maelekezo: Samora na Ohio, mkabala na Steers kati kati ya jiji)


  Mbali na kukutwa na Kichwa cha binadamu Rama ni msanii pia…

  Mchoro huu (Uliopigwa picha na Global Publishers) unaweza kutoa majibu ya akili ya mtoto Rama na fikra zake, Rama ni mtoto ambaye alitawala vichwa vya habari vya magazeti siku za karibuni kuhusu kukutwa na kichwa cha Mtoto Salome na kukinyonya damu mbele ya kadamnasi.

  Sanaa ya uchoraji huwa inamuwezesha Mchoraji kutoa kilichomo mawazoni mwake na kukiweka katika muonekano, mara nyingi unaweza kuona picha tuu lakini akatokea mtu na kuitolea maana na maelezo lukuki picha hiyo hiyo moja, ama kuweza kutafsiriwa na watu tofauti pia.

  Sijui huyu mtoto alikuwa akiwaza nini alipochora picha hii, lakini nafikiri wataalamu wa Saikolojia (Noel Kilonzo) wanaweza kuoanisha picha hii na tabia ya mtoto husika. Je wewe unafikiria nini?

  FM wadaiwa kupanga kuvuruga uzinduzi wa AKUDO

  Kundi la Muziki la FM Academia linatarajia kumleta mwanamuziki General Defao kuja kutumbuiza nao siku ya May 16 katika onyesho lililoitwa “Uchwara” ambalo dhamira yake ni kuvuruga uzinduzi wa Akudo Wazee wa Masauti, ambapo siku hiyo pia watakuwa na Uzinduzi wa Albamu yao mpya, Ikumbukwe pia Akudo walishatangaza kumleta Mwananamuziki Bozi Boziana ili kuwasindikiza kwenye uzinduzi huo ambao unasemekana kuwa wa aina yake. Lakini habari zinasema endapo Defao akitia timu hapa Tanzania, huenda akalakiwa na pingu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
  Defao anatarajia kuja nchini hivi karibuni kwa mwaliko wa bendi ya FM Academia ambapo inadaiwa atatumbuiza na bendi hiyo katika onesho ‘uchwara’ linalodaiwa kuandaliwa mahususi kwa ajili ya kuvuruga uzinduzi wa bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ Mei 16 mwaka huu.

  Madai ya Defao kutiwa mbaroni yamekuja kutokana na kile kinachodaiwa kuwa alipofanya ziara ya mwisho hapa nchini alitoroka akiwa anadaiwa mamilioni ya hela za pango katika Hotel ya Sea Cliff pamoja na fedha ya matibabu katika Hospitali ya TMJ.
  Kumekuwa na mashindano kati ya Bendi hizi nchini siku za karibuni na kwa sasa ushindani unatarajia kuwa mkubwa kwani ujio wa TOT Respect utanogesha burudani ukizingatia bado kuna Twanga Original na Twanga Chipolopolo, Patamu hapo mwanangu.

  Source: Global Publishers

  Taifa Stars wapongezwa

  Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries iliandaa chakula cha jioni katika kuwapongeza wachezaji na makocha wa Timu yetu ya Taifa Stars, hii inasaidia kuwatia moyo na morali wachezaji na kuona kuwa watu wanatambua mchango wao. Mgeni Rasmi alikuwa waziri wa Habari na Michezo Mh. George Mkuchika.
  Pia inanikumbusha jinsi watanzania walipojitoa wakati timu yetu ikishiriki hatua za awali za kombe la Africa, natuma Taifa Stars itawapa raha watanzania na kuleta kombe nyumbani, inshallah kila kiti chawezekana.

  Pichani Kocha wa Taifa Stars na msaidizi wake akikokokotwa na watoto wa kikundi cha sanaa ya Ngoma na Sarakasi kwenda kucheza Sindimba.

  Golikipa wa Taifa Stars, Ivo Mapunda akitoa mkono baada ya kukamata kilicho chake
  Deo Mwanambilimbi pia alikuwapo kutoa Burudani na Bendi yake ya Kalunde.
  (picha zote na Sir Michuzi.)

  Wednesday, May 7, 2008

  Mbwembwe za Wanamuziki mazishi ya Madilu System

  Wazaire wanaongoza kwa mbwembwe iwe kwenye shughuli yeyote hata msiba!! ilibidi Polisi na wanajeshi kuingilia kati kutuliza umati hasa walipokuwa wakiwasili wanamuziki wakubwa wenye uhasimu kwenye msiba wa Nguli wa Muziki wa Kilingala Madilu System. angalia video hii jinsi JB Mpiana na Werason walipoweza kushikana mikono na mbwembwe zao hata mazikoni.

  Wenger asikitishwa kuondoka Flamini

  Kocha Arsene Wenger ameonyesha kusikitishwa kwake na mpango wa mchezaji wake Mathieu Flamini ambaye anaondoka kwenda AC Milan msimu ujao.

  Mfaransa huyo mwenye miaka 24 amekamilisha uhamisho wake wa kwenye kucheza ligi ya Seria A na klabu yake mpya ya AC Milan. Arsenal walijitahidi kwa hali na mali kuendelea kwa na mchezaji huyu ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa anaelewa sana kiuchezaji na Cesc Fabregas kwa uhai wa timu na aina yao ya uchezaji. Pamoja na ahadi ya donge nono kwenye mkataba mpya ambapo waliahidi kumpatia kitita cha Pound £55,000 kwa wiki lakini mchezaji huyo hakubadili nia.

  Kwa sababu alikuwa ni mchezaji huru tayari basi Flamini alionelea kuwa anaweza kupata “Handsome Package” mahala pengine zaidi ya hiyo. na habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Inter Milan wamepania kumchukua mchezaji mwingine Alexander Hleb au hata Fabregas kabisa bado haijajulikana kama atakuwa bado kwa washika bunduki hao kwa msimu ujao ama la!!.

  “I Am Because We Are” Makala ya Filamu ya Madona juu ya umasikini

  BLANTYRE, Malawi – Ni umbali wa maili 100 toka mji mkuu wa Malawi, ndipo kilipo kijiji cha Lipunga, huko hakuna huko hakuna TV wala jumba la sinema kwani hakuna hata umeme,, lakini mwanakijiji Yohane Banda (Mzazi wa mtoto David Band) amesikia kuwa Makala ya Filamu mpya ya sasa ambayo mwanamuziki Madonna inakusudia kuamsha uelewa wa jamii kuhusu suala la umasikini mkubwa unaolikabili eneo hili lililopo kusini mwa jangwa la sahara.

  Pichani Yohana Banda Mzazi wa David Banda akiwa nyumbani kwake

  “I Am Because We Are,” ndio jina la makal ya filamu hiyo ambayo Madona ameitengeneza. Nia ni kuamsha uelewa wa watu kuhusu umasikini wa sehemu ya pili ya dunia, hatufanyi hivi kubeza, la hasha nia yetu ni kuwaonyesha watu kujua maisha halisi ya jamii nyingine na taabu wanazo pata ili kuamsha hari ya kujitolea kusaidia, alisema Madona.

  Kati ya watu waliohudhuria uzinduzi huo walitaka kujua uguu uliopo katika kuchukua mtoto nchini malawi,

  Madona alisema, “si kazi ndogo, inabidi ujitolee, inataka muda kwani ni suala geni kwenye utamaduni wao, halipo ama halijazoeleka”.

  Filamu hii inaonyesha umasikini na maradhi yanavyochangia kugharimu maisha ya watu wa eneo husika. Madona ametaka watu kujitolea kusaidia, yeye alikutana na Banda alipokuwa katika harakati zake za kutoa misaada nchini Malawi.

  Siku JB walipokutana na Koffi kwenye harusi ya Titina Alcapone.

  Ni muda umepita tangu hii itokee lakini Je unamkumbuka Titina Alcapone? huyu aliwahi kuwagombanisha wanamuziki magwiji JB Mpiana wa Wenge BCBG na Koffi Olomide kwa kile Jb alicholalamikiwa Koffi kumchukulia wanamuziki wake akiwamo huyu Titina, kwa kipindi hicho Titina alipokuwa anaoa alimfanya Koffi kuwa Best Man wake lakini alimualika JB Mpiana pia. Kwa sasa Titina anasema ameamua kufanya muziki kivyake zaidi.
  Koffi Olomide akisalimiana na Wageni wengine waalikwa
  Mwanamuziki kiongozi wa Wenge Musica BCBG JB Mpiana akiserebuka na Bi harusi Nene, mke wa Titina Alcapone siku ya harusi yao.
  Meza ya wageni waalikwa anaonekana JB Mpiana, Alain Mpela (aliyevaa kiarabu), Dadé Mpoko, Papito Mbala, Thitsho Lembe
  JB Mpiana na tajiri mtoto PDG Patrick Bolognia, aliyesimama nyuma yao suti nyeusi ni Titina Alcapone. Majina haya wengi wa wapenzi wa Lingala watakuwa wamezoea kuyasikia kwenye kila wimbo na leo kubahatika kuwaona katika picha hizi.

  Lugha kuwabana wahamiaji ila si wachezaji waliopo.

  Mchezaji wa Manchester United mwenye uraia wa Argentina Carlos Tevez akishangilia ushindi baada ya kuwachapa Barcelona katika mechi ya kombe la UEFA Champions League mzunguko wa pili, April 2008. Idara ya uhamiaji ya Uingereza imesema hakuna raia mchezaji ambaye si raia wa European ambaye hawezi kuzungumza “kidhungu” atafukuzwa chini ya sheria mpya ngumu za uhamiaji ambazo zitaanza kutumika mwaka huu ambapo lugha ni suala muhimu.

  Chelsea wamuwania Sergio Ramos

  Mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos akishangilia ushindi baada ya kushinda mechi ya fainali ya ligi ya Spain dhidi ya Osasuna katika uwanja wa Reyno de Navarra stadium, Pamplona, tarehe 4 May. Imesemekana kwamba Chelsea wametoa ofa ya dau nono kwa Real Madrid jumla ya 70 million euros (108 million dollars) kwa ajili ya mchezaji huyu na kama mambo yakienda kama ilivyopangwa basi atahamia kucheza ligi ya UK, kwani Real Madrid wameonyesha kuridhia ofa hiyo. imeripotiwa na gazeti la michezo la El Mundo.

  Tottenham wamtaka Etoo

  Mchezaji machachari wa Barcelona’s Samuel Eto akishangilia wakati wa mchezo wa ligi wao ya Spanish dhidi ya Valencia huko Camp Nou stadium Barcelona, May 4.
  Inasemekana kuwa klabu ya Premier League ya Tottenham iko kwenye maongezi na klabu ya Barcelona kuhusu mchezaji huyu Mcamerun Samuel Etom limeripoti gazeti la michezo la Spain la sports daily Marca. Habari hazijafafanua kwambu ni wapi wamefikia kwenye maongezi hayo ila wanasema maongezi yanakwenda vizuri.

  Schorali kumrith Ericson Manchester City?

  Timu ya Manchester City wamefanya uamuzi wao na kuamua kumpendekeza Luiz Felipe Scolari kuwa kocha wao ajaye.

  Kwa sasa mkataba unafanyiwa kazi kati ya Manchester City na Mwakilishi wa Kocha huyo Mreno Scolari ili aweze kuja Eastlands, Imefahamika kuwa Manchester City watavunja mkataba na kocha wa sasa Sven-Goran Eriksson baada ya msimu huu.

  Thaksin kwa sasa anangojea jibu tu toka kwa Scolari, kama mkataba huo utakwenda kama ilivyopangwa basi kocha huyo ataondoka na donge nono la Paundi £3.2milioni kwa mwaka na mkataba unangoja jibu la mwisho ili upigwe muhuri. kwani kwa sasa kocha huyo yuko busy na kazi ya kuinoa timu Portugal kwa ajili ya Euro 2008.

  Suala la kuondoshwa Ericson lilikuwa gumzo na hata katika mechi ya Manchester City na Chelsea majuzi mashabiki walionyesha kumuunga mkono kocha Ericson lakini ni suala la mmiliki na uongozi.

  Mashabiki wameonyesha kukerwa sana na uamuzi wa klabu yao lakini uongozi umechukua jukumu la kumtangaza Scholari haraka ili kupunguza ghadhabu za mashabiki wao.

  Kombe la Taifa na mfufuko wa soka letu

  Michuano ya Kombe la Taifa imeanza kwa kasi na msisimko wa ajabu huku mikoa yote 23 ikishiriki kwenye kinyang’anyiro hicho, pichani Wachezaji wa Timu ya Manyara kushoto Zawadiel Stephen na Marwa Gabriel wakiwania mpira mshambuliaji wa timu ya Iringa Bunda Oden. Iringa ilishinda 4-1 katika mashindano ya Taifa Cup yanayodhaminia na Safari Lager.

  Kwa kiasi kikubwa watanzania ni watu wanaopenda michezo sana hasa mchezo wa kandanda, itakumbukwa jinsi watanzania walivyojitolea kwa uzalendo mkubwa wakati Timu yetu ya Taifa ilipokuwa ikishiriki katika michuano ya Awali ya African Cup of Nations, kila mtu alionyesha uzalendo na watu wote walikuwa ama wanapeperusha bendeka iwe kwenye magari binafsi, daladala, Teksi, hata magari ya Serikali au ya Umma, iwe vibanda vya Chipsi au mabanda ya Mitumba, watu walinunua Jezi za timu ya Taifa lakini kama kamaida bahati haikiwa yetu.

  Wengi walisema soka letu lingefanya vizuri kama michuano mbali mbali ingefufuliwa mbayo inachangia kupata wachezaji chipukizi kuchangia katika timu kubwa na Timu ya Taifa pia ili kuondoa utegemezi wa wachezaji wengi toka klabu kubwa za Simba na Yanga. Wengi wa wachezaji chipukizi jicho la TFF haliwafikii huko waliko, lakini kwa mpango kama huu wa Kombe la Taifa (TAIFA CUP) ni rahisi kuwaona wachezaji wenye moyo na chama cha makocha wakishirikiana na timu ya Ufundi ya TFF na Kocha mkuu pamoja na Msaidizi wanaweza kupata vijana wazuri kwa ajili ya timu yetu ya Taifa. Hongera Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na makampuni mengine pamoja na wadau bila kuwaacha TFF kwa kufanikisha hili.

  Tunaimani kuwa kama michuano hiyo ikitumiwa vizuli inaweza kulisha timu kongwe na kuwa chachu ya kupata wachezaji wa Timu ya Taifa.

  Tuesday, May 6, 2008

  JB Mpiana: Tatizo lilo wapi?

  Wapenzi wa muziki wa Kizaire haya tena Video ya JB mpiana iko sokoni, ile video ya albam mpya ya Quel Est Ton Probleme?” Tatizo ni nini au shida iko wapi? na mtindo mpya wa uchezaji unaojulikana kwa jina la Kizubanata.
  Bonyeza Playa upate vitu:-

  Msimamo wa Ligi Primier mpaka sasa.

  Msimamo wa Ligi ni kama ifuatavyo:-

  2007/2008 English Premiership

  Kwa Ujumla
  Nyumbani Ugenini

  GP W D L GS GA W D L GS GA W D L GS GA GD P
  1 Man Utd 37 26 6 5 78 22 17 1 1 47 7 9 5 4 31 15 56 84
  2 Chelsea 37 25 9 3 64 25 12 6 0 35 12 13 3 3 29 13 39 84
  3 Arsenal 37 23 11 3 73 31 14 5 0 37 11 9 6 3 36 20 42 80
  4 Liverpool 37 20 13 4 65 28 12 6 1 43 13 8 7 3 22 15 37 73
  5 Everton 37 18 8 11 52 32 10 4 4 31 16 8 4 7 21 16 20 62
  6 Aston Villa 37 16 11 10 69 49 10 3 6 34 22 6 8 4 35 27 20 59
  7 Blackburn 37 15 13 9 49 44 8 7 4 26 19 7 6 5 23 25 5 58
  8 Portsmouth 37 16 9 12 48 39 7 8 3 24 13 9 1 9 24 26 9 57
  9 Man City 37 15 10 12 44 45 11 4 4 28 20 4 6 8 16 25 -1 55
  10 West Ham 37 13 9 15 40 48 7 6 5 22 22 6 3 10 18 26 -8 48
  11 Tottenham 37 11 13 13 66 59 8 5 5 46 32 3 8 8 20 27 7 46
  12 Newcastle 37 11 10 16 44 62 8 5 6 25 26 3 5 10 19 36 -18 43
  13 Wigan 37 10 10 17 34 49 8 5 5 21 15 2 5 12 13 34 -15 40
  14 Middlesbrough 37 9 12 16 35 52 6 5 7 19 22 3 7 9 16 30 -17 39
  15 Sunderland 37 11 6 20 36 58 9 3 6 23 20 2 3 14 13 38 -22 39
  16 Bolton 37 9 9 19 35 53 7 5 7 23 18 2 4 12 12 35 -18 36
  17 Fulham 37 7 12 18 37 60 5 5 9 22 31 2 7 9 15 29 -23 33
  18 Reading 37 9 6 22 37 66 8 2 9 19 25 1 4 13 18 41 -29 33
  19 Birmingham 37 7 11 19 42 61 5 8 5 26 22 2 3 14 16 39 -19 32
  20 Derby 37 1 8 28 20 85 1 5 12 12 39 0 3 16 8 46 -65 11

  Msimamo wa wafungaji hadi tarehe 5May na idadi ya magoli yao kwa ligi ya FA Primier

  Rank Mchezaji Timu Idadi ya magoli
  1 Cristiano Ronaldo Man Utd 30
  2 Emmanuel Adebayor Arsenal 24
  3 Fernando Torres Liverpool 23
  4 Roque Santa Cruz Blackburn 19
  5 Robbie Keane Tottenham 15
  Dimitar Berbatov Tottenham 15
  Benjani Mwaruwari Man City 15
  8 Carlos Tevez Man Utd 14
  9 John Carew Aston Villa 13
  Ayegbeni Yakubu Everton 13
  11 Jermain Defoe Portsmouth 12
  Wayne Rooney Man Utd 12
  13 Steven Gerrard Liverpool 11
  Nicolas Anelka Chelsea 11
  Gabriel Agbonlahor Aston Villa 11
  16 Michael Owen Newcastle 10
  Frank Lampard Chelsea 10
  18 Dean Ashton West Ham 9
  Dave Kitson Reading 9
  Mikael Forssell Birmingham 9
  Obafemi Martins Newcastle 9
  22 Gareth Barry Aston Villa 8
  Benedict McCarthy Blackburn 8
  Didier Drogba Chelsea 8
  Tuncay Sanli Middlesbrough 8

  Kudwalika….

  Watu wakidwalika kwenye Usiku wa Black and White, unataka kujua kulikoni na Black and White mtembelee dada Shamim kwa kubofya hapa.

  TBL yamwaga 140milioni kwa Kusaka mwanamuziki bora.

  KAMPUNI ya Bia Tanzania, TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro imetangaza kutumia zaidi ya Sh140milioni kuandaa Tuzo za Kilimanjaro zitakazotolewa kwa wasanii mbalimbali baadaye mwezi ujao.

  Meneja Masoko wa Bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo alisema jana kuwa tayari TBL imetenga fedha hizo, zaidi ni kuenzi wasanii pamoja na kuibua vipaji vipya katika fani ya muziki.

  ” Nia yetu ya kudhamini mashindano hayo na kwa miaka saba sasa tumeibua na kukuza vipaji vya wasanii na kuwafanya watunge nyimbo ambazo zitaleta ushindani katika soko letu na kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa,” alisema Shelukindo.

  Alisema zoezi la kupendekeza wasanii ambao watashiriki katika tuzo hizo litaanza Mei 9 na Mei 28 utakuwa mwisho wa zoezi hilo na majaji wataangalia orodha ya asanii waliochaguliwa na kuakikisha kila aliyechaguliwa a akakaa kundi analostaili.

  Shelukindo alisema Juni 2 watataja wasanii walioteuliwa na kila kundi litakuwa na wasanii watano Juni 4 watatangaza majina kwenye magazeti ili wananchi waweze kupiga kura kumchagua mshindi.

  Alisema njia ya kutuma kupiga kura ni kwa ujumbe mfupi, kwa njia ya kuponi kwenye Magazeti na barua pepe.

  Naye Mwenyekiti wa Tuzo hizo John Mhina alitaja vipengele vinavyoshindaniwa katika tuzo hizo kuwa ni Mwimbaji bora wa kike, Kiume, Albamu bora ya Taarab, Wimbo bora wa Taarab, Wimbo bora wa Mwaka.

  Nyingine ni Wimbo bora wa Kiswahili, Albamu bora ya Kiswahili,, Albamu bora ya R’ n B’, Wimbo bora R’ n B, Wimbo bora wa Asili ya Kitanzania, Albamu Bora ya Asili ya Kitanzania.

  Alisema Wimbo bora wa Hip Hop, Albamu Bora ya Hip Hop, Albamu bora ya Afrika mashariki, Mtunzi bora wa Muziki, Mtayarishaji bora, Mwandikaji nyimbo bora, Mtayarishaji bora wa Video, Mwanamziki aliyechangia mafanikio makubwa ya Muda, Wimbo bora wa Zouk na Mwanamziki au kikundi bora kinachochipukia.

  Mwaka huu TBL haitaendesha mashindano ya Kanda kutokana na kukosa fungu la kuendesha mashindano kama ilivyokuwa mwaka jana.

  Na Mwananchi

  Kila Mtu alitaka kupiga picha na 50 Cent!

  Mara nyingi ikitokea super star fulani akatokea mahali,mashabiki au wapenzi wa chochote anachokifanya(iwe sinema,muziki nk) hupenda kujipatia japo nafasi ya kupiga naye picha kwa minajili ya kuweka kumbukumbu na mambo kama hayo.Kama inavyoonekana pichani,mashabiki na wapenzi wa 50 Cent waliopata nafasi ya kuwa karibu naye hivi majuzi jijini Dar,walikuwa na shauku ya kupiga naye picha!Go 50!

  Kaseja Kutua Jangwani, Nsajigwa kwenda Simba!

  Golikipa wa Simba Juma Kaseja Juma, ambaye anasemekana anataka kuhamia Yanga.

  Na Gobal Publishers

  Kuna mipango ya chini kwa chini inafanywa ili timu hizo zibadilishane wachezaji. Habari ambazo zimelifikia gazeti Championi kutoka chanzo kilichopo ndani ya Klabu ya Yanga na Simba, zimeeleza. Chanzo hicho kilieleza kwamba, Yanga ipo tayari kuipa Simba beki wao wa kulia ambaye walimfungia kwa miezi sita kwa utovu wa nidhamu, Shadrack Nsajigwa ili kumnasa golikipa, Juma Kaseja.Kiliendelea kueleza kuwa, hatua hiyo imefikiwa kutokana na mvutano mkubwa uliopo klabuni hapo kutoka kwa viongozi wakitaka kumnasa Kaseja kutokana na kudaiwa kuwa mnazi wa klabu hiyo.“Kaseja ni golikipa mzuri, na ni mnazi wa Yanga ingawa awapo langoni huweka mapenzi yake pembeni na kutanguliza maslahi ya klabu anayoichezea, tunaamini akitua Jangwani atafanya kazi kwa raha zaidi,” Kilieleza chanzo hicho na kuomba hifadhi ya jina lake.Kiliongeza kuwa, pia kuna mvutano mkubwa kwa baadhi ya viongozi wakitaka Nsajigwa na Ivo Mapunda warejeshwe kundini huku baadhi wakidai watupiwe virago.Mweka Hazina Msaidizi wa Simba, Chano Almasi alipoulizwa kuhusu baadhi ya nyota wao kudaiwa kuihama klabu hiyo alisema timu yao haiwezi kutishika kwa hilo hata kama wachezaji wote wataondoka.
  “Simba ni kama chuo kikuu cha soka, kwani tunatengeneza wachezaji na tunapokamilisha zoezi hilo, ndipo timu zingine huanza kuwamendea.“Sisi kama viongozi hatuna wasi-wasi hata kama wachezaji wote wataamua kuondoka upo uwezekano wa kupatikana wachezaji wengine ndani ya siku moja tu,” alisema mweka hazina huyo.Kwa upande wa Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema, suala zima la nani asajiliwe litajulikana pindi Kamati Kuu itakapokaa.
  Alisema Kamati Kuu inategemea kukutana wiki hii ili kupitia mapendekezo ya Kocha Mkuu, Mserbia Dusan Kondic na baada ya hapo watajua wachezaji watakaotemwa na watakaosajiliwa.Akizungumzia suala la Ivo na Nsajigwa alisema wachezaji hao kuwepo ama kutokuwepo ndani ya kikosi chao msimu ujao itajulikana siku hiyo.
  “Katika kikao hicho kutakuwa na mada mbalimbali lakini suala la kurudi kwao litajadiliwa na kuachwa kwa mwalimu ambaye atakuwa na kauli ya mwisho endapo atawahitaji au la,” alisema Lucas.Championi lilipobisha hodi kwa Kaseja, ili kupata uhakika wa habari hizo, alisema hata kama suala hilo lipo bado hajapewa taarifa kutoka kwa kiongozi yeyote.“Sina habari hizo na pia Simba hawawezi kukubali kuniachia kirahisi namna hiyo, wewe unafikiri hilo linawezekana?” Kaseja alihoji. Chove na Haule wanadaiwa kutaka kutemwa kwa sababu Aprili 27, mwaka huu wakati wa mechi ya Simba na Yanga inadaiwa kuwa, waligoma kucheza hadi uongozi ulipoingilia kati na kuwabembeleza.

  Happiness Magese aendelea kuchengua A.Kusini


  Happiness Magesa ambaye alishanyakua Taji la Miss Temeke na baadaye Miss Tanzania 2001 anaendelea kutesa vyema nchini South Africa kwenye Fashion Show Mbalimbali nchini humo kama muonavyo Pichani, Happiness kwa sasa anaishi Africa ya Kunisi akijishughulisha na shughuli za U model huko.

  Na Haki.N.

  Chelsea waunusa Ubingwa, waichapa Newcastle 2-0

  Kushoto kabisa anaonekana Ballack na mpira ndio huo ukimpita kipa wa Newcastle

  Magoli mawili yaliyopachikwa na Michael Ballack pamoja na Florent Malouda yalifanya mchezo wa jana jioni kuisha kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya New CastleUnited na kuwafanya kuwa na point sawa na vinara wa Ligi hiyo Man U huku wakiwa na tofauti ya magoli.

  Michael Owen kwa upande wa Newcastle alikuwa na nafasi mbili za wazi kipindi cha kwanza kuipa timu yake ushindi lakini nafasi hizo hazikuzaa matunda kwa kosa kosa ya kwanza dakika ya 18 baada ya kipa kutoka mpira uliokolewa na Mchezaji wa Chelsea akiwa yeye na goli pekee. na dakika ya 27 Ballack naye alikosa golo la wazi baada ya kupata pasi saaafi toka kwa Essien kwani Ballack hakuwa na haja ya kuwa na papara na mpira ule kwani tayari kulikuwa na watu wawili kwenye eneo la goli la Newcastle ambao Ballack angewachezea ule mpira walikuwa wanapata goli.

  Mpaka mapumziko 0-0, baada ya mapumziko Chelsea waliumiliki mpira zaidi na kulishambulia lango la Newcastle na dakika ya 61 ya mchezo Ballack akatia kimiani gili mwanana kabla ya Malouda hajaongeza la pili.

  Ushindi wa jana unaipa Chelsea nafasi nzuri kwani kwa sasa wamelingana point na Manchester wakiwa wote na Point 81 huku Manchester akiongoza kwa idadi ya magoli.

  emp_load.getEmpEmbeddedParams(“emp_7384584”);

  Manchester United, wanasafiri kwenda nyumbani kwa Wigan jumapili hii, wakiwa wanajua ushindi dhidi ya timu hii ndio utawahakikishia Kuchukua ubingwa tena msimu huu, na kuwaacha Chelsea ambao wanacheza na Bolton nyumbani kwao,

  Timu hizi ndogo ndio huwa na upinzani mkubwa sana wanapocheza na timu kubwa kama Man U au Chelsea, Chelsea wananafasi kubwa ya kushinda kwani wanachezea nyumbani ilihali Man u wako ugenini.

  Monday, May 5, 2008

  Real Madrid Bingwa Primera La Liga

  Kwa mara nyingine tena Real Madrid walifanikiwa kukalia kiti cha Ubingwa wa ligi ya Spain ya La Liga jumapili hii baada ya kushinda magoli 2-1 huko Osasuna ikiwaacha Real Madrid wakiwa na pointi 10 zaidi ya wenzao Villarreal kwenye msimamo wa Ligi hiyo ya Primera Liga, huku wakiwa na mechi tatu mkononi ambazo wanatakiwa kucheza kukamilisha ratiba. Real Madrid walicheza wakiwa 10 uwanjani ilibidi wafanye kazi ya ziada kwani Osasuna walikuwa wakiongoza kwa goli lililofungwa na Patxi Punal kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Real Madrid Gabriel Heinze kuunawa mpira katika eneo la hatari. Na Fabio Canavaro kutolewa nje kwa kadi nyekundu na hivyo kuwafanya Real Madril kucheza wakiwa kumi uwanjani.
  lakini winga machachari M-Dutch Arjen Robben ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Chelsea aliipatia bado timu yake dakika tatu kabla mpira kuisha na kufanya magoli kuwa 1-1, mpira ulizidi kuwa mkali kadri dakika za lala salama zikiyoyoma huku Real Madrid wakilishambulia goli la wapinzani wao ambao kwa wakati huo walirudi kulinda goli, na ndipo Gonzalo Higuain alipiga kiufundi free kick na kufanya Real kuongoza kwa mabao 2-1.
  Kwa ushindi huo basi Real Madrid wamefanikiwa kuongoza ligi hiyo na kuchukua ubingwa kwa msimu huu huku wakiwaacha wapinzani wao timu kubwa ya Barcelona ikiwa ya tatu na nyuma kwa point 35 dhidi ya 42 za Real Madrid.

  Msimamo wa Ligi hiyo mpaka jana ulikuwa kama ifuatavyo:-

  CLUB GP W L D PTS GD
  Real Madrid 35 25 7 3 78 42
  Villarreal 35 21 9 5 68 17
  Barcelona 35 18 7 10 64 35
  Atlético Madrid 35 17 11 7 58 18
  Racing Santander 35 16 11 8 56 3
  Sevilla FC 35 17 14 4 55 18
  Mallorca 35 12 9 14 50 12
  Deportivo La Coruña 35 14 14 7 49 1
  Almeria 35 13 12 10 49 -1
  Espanyol 35 13 13 9 48 -4
  Athletic Bilbao 35 12 13 10 46 -1
  Real Betis 35 12 14 9 45 -4
  Getafe 35 11 15 9 42 -6
  Valladolid 35 11 15 9 42 -15
  Valencia 35 12 17 6 42 -21
  Real Zaragoza 35 10 14 11 41 -9
  Osasuna 35 11 17 7 40 -6
  Recreativo Huelva 35 10 15 10 40 -20
  Murcia 35 7 19 9 30 -25
  Levante 35 7 23 5 26 -34

  Chelsea mtihani mzito leo

  CHELSEA iko katika mbio za kuwania ubingwa na Manchester United leo itakuwa ugenini Uwanja wa St. James Park kupambana na Newcastle.

  Mechi hiyo ina umuhimu mkubwa kwa Chelsea ambayo ilifufua matumaini ya kuwania ubingwa baada ya wiki iliyopita kuwafunga vinara wa ligi hiyo Manchester United mabao 2-1 katika uwanja wa Stamforde Bridge na kulingana nayo pointi kuwa 81-81.

  Lakini juzi United ilishinda mechi yake nyingine dhidi ya West Ham United mabao 4-1 katika uwanja wa Old Trafford na kufikisha pointi 84 ikiwa imesaliwa na mechi moja dhidi ya Wigan.

  Chelsea inayonolewa na Avram Grant leo italazimika kushinda ili kulingana pointi na Manchester na kisha kuiombea mabaya itoke sare au kufungwa na Wigan na yenyewe kushinda mechi yao ya mwisho dhidi Bolton na kutawazwa ubingwa.

  Lakini United itatwaa ubingwa kama itashinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Wigan hata kama Chelsea nayo itashinda mechi zake zote kutokana na kuwa na uwiano mkubwa wa mabao ya kufunga.

  Liverpool yamchapa Manchester City Kimoja (1-0)

  Huku akifikisha goli lake la 32 msimu huu Fernando Torres aliiwezesha Liverpool kushinda bao 1-0 dhidi ya Manchester City.

  Torres alimzunguka na kumuacha Richard Dunne na kuachia shuti kwenye angle na kuwafanya Liverpool kuongoza kwa goli 1-0, goli ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

  Liverpool walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa magoli mengi mchezo wa jana kwani kichwa cha Dirk Kuyt kiligonga mwamba na shuti la Ryan Babel kupaa juu.

  Kijana Benjani kidogo awatoe nishai kwa mpira wa adhabu dakika za mwisho bahati ukaokolewa na Pepe Reina.

  Pamoja na kufungwa mashabiki wa Man City walionyesha kum supoti kocha wao

  Manchester City walikwenda kwenye mechi hiyo huku bosi wao Sven-Goran Eriksson akitegemea kutimuliwa baada ya msimu huu, lakini wapashaji wanasema kelele za mashabiki zinaweza kumuokoa akawepo.

  Kelele za mashabiki wakionyesha kumshangilia ni ishara kuwa bado wanaimani naye aendelee kuwepo katika timu yao.

  Kapteni wa Liverpool Steve Gerald na Torres jana walicheza vizuri lakini umaliziaji haukuwa mzuri kwani kama nilivyosema Liverpool walitengeneza nafasi nyingi nzuri na za wazi lakini wao wenyewe walishindwa kuzitumia na kumalizia mipira kimiani. Mchezo ulikuwa mzuri na wa kasi huku kila timu ikijaribu kuonyesha uwezo wake huku Liverpool wakionyesha kubebwa na mashabiki wao wa nyumbani.

  Hadi mwisho wa mchezo Liverpool 1-0 Man City, najua Michuzi unacheka tuu.

  50 Cent achengua mashabiki Dar


  Mwanamuziki 50 Cent amechengua mashabiki wa muziki katika ukumbu wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo, habari zinasema mashabiki walifurahi kwani walipata walichotegemea na shoo ilikuwa ya kufa mtu.
  Awali akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika Dar, 50 alisema ana hamu sana kutembelea sehemu mbalimbali kila anakokwenda lakini ratiba ya waandaaji inamzuia kuona vitu vingine zaidi ya uwanja wa ndege, chumba cha hoteli na jukwaa la muziki.

  ameeleza mipango ya kurejea bongo kama mtalii na kusema ana hamu sana kuona kwa macho yake mbuga ya serengeti na mlima kilimanjaro ambao amesema anatambua hauko kwa watani wa jadi.

  amesema kwamba atalitilia maanani ombi la mwenyeji wake joseph kusaga kusaidia kunyanyua vipaji vya wasanii chipukizi wa bongo kwa kuomba propoza za afanye nini.

  amesema kwa sasa anaelekea london, kisha los angeles ambako ana mradi wa filamu kubwa anayoshuti na mzee mzima al pacino. hakutaja jina lake ila itamalizika mwishoni mwa mwaka huu.
  Kwa habari zaidi na picha zaidi Mtembelee Sir Issa Michuzi

  Nani kuwa mshindi wa American Idol?

  Katika picha hii iliyotolewa na FOX, washiriki wa American Idol waliobaki kwenye kinyang’anyiro toka shoto David Archuleta, Syesha Mercado, David Cook na Jason Castro. Ushindani ni mkali na kila mtu ni mzuri kwa waliobaki, kwa vile inabidi apatikane mmoja basi tungoje tuone.

  Uchunguzi waonyesha American Idol yapungua Umaarufu

  Majaji wa American Idol toka shoto Randy Jackson, Paula Abdul na Simon Cowell

  Ingawaje American Idol bado ni show kubwa na ianyotazamwa na watu wengi zaidi, matokeo ya uchunguzi yanaonyesha umaarufu wa kipindi hiki unashuka kwa watazamani vijana wa umri wa kati hasa miaka kati ya 20 na 34. Mpaka kufikia mwisho wa msimu huu, Fox ndio watakuwa wanaongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi kuliko kipindi kingine chochote.

  Shoo hii imetazamwa na watazamaji takribani milioni 28.7 kwa mwaka huu, kwa mujibu wa kampuni ya Nielsen Media Research. hii ni chini kwa asilimia 7% ukilinganisha na jumla ya watazamaji milion 31 wa mwaka jana.

  “Hatupingi kuwa idadi imepungua,” alisema ofisa wa juu wa Fox waandaaji wa American Idol Preston Beckman. “Kuna vitu unaweza kuvi control na vingine huwezi, hili liko nje ya uwezo wetu kwani kama ni ubora basi kipindi chetu kila mwaka kinazidi kuongezwa ubora ukilinganisha na kilichopita” alisema ofisa huyo.

  Ripoti inaonyesha kuwa Kati ya wanawake wa umri wa kati ya miaka 18 na 34, idadi imepungua kwa asilimia 18 kwa msimu huu ambapi kwa idadi ya vijana kati ya miaka 12 na 17 wameshuka kwa 12%.

  Kuna vitu ambavyo viongezeka kwani waangaliaji walikuwa ni vijana hadi miaka ya mwanzoni ya 30 lakini kwa sasa hadi umri wa miaka 42 idadi ni kubwa.alisema Nielsen.

  Kali kuliko yote ni wazee wa miaka hadi ya 50 ambao wengi waliohojiwa wameonyesha kuangalia zaidi vipindi vinavyoandaliwa na Fox Amerikan Idol ikiwa ni mojawapo.

  Uchunguzi pia unaonyesha mashabiki kuchukia kitendo cha juma lililopita cha Paula Abdul, mmoja wa majaji wa AmeriCan Idol kuchemka kwa kutoa maoni ya wimbo wa pili wa mmoja wa washiriki ilihali wimbo huo ukiwa haujachezwa bado, hii iliwapa watu maswali mengi na kusema kuwa majaji wanakuwa na mtu wao kwani hata siku hiyo akiimba vipi uamuzi wanakuwa nao wao. Post ya kipindi hicho tuliitoa wiki iliyopita angalia chini au kwenye lebels gonga American Idol utaiona.

  Sunday, May 4, 2008

  Arsenal Yaichapa Everton 1-0

  Bendtner akiruka kupachika mpira na kufanya Arsenal kuongoza kwa goli moja.
  Gael Clichy, ambaye hivi karibuni alitajwa kwenye timu ya Bora ya mwaka ambayo inajumuisha wachezaji mahiri walioshiriki kwenye ligi hii ya Barkley’s Premier Ligi

  Goli moja lililofungwa na Striker Nicklas Bendtner dakika ya 76 ya mchezo, limeihakikishia Arsenal nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi msimu huu.

  Bendtner alifunga mpira huo kutoka krosi ya Armand Traore na kupachika kichwa maridhawa na kuupachika langoni mwa Everton.

  Ingawaje mchezo wa leo Arsenal hawakuwa kwenye kiwango chao kwani kabla ya goli la Bendtner, Emmanuel Adebayor na Gilberto walikosa nafasi za wazi kufunga.

  Andy Johnson na Joleon Lescott walicheza vizuri kwa upande wa Everton, ambao kwa kiasi fulani mechi hii ilikuwa muhimu kwao kwani wangeweza kujihakikishia nafasi ya tano ambayo ni muhimu kushiriki kombe la Uefa.

  Kwa kichapo hicho cha kagolikamoja, Everton wamejipa mtihani mkubwa kwani katika mechi inayokuja wanakutana na Newcastle, wanahitajika kushinda ilikujihakikishia nafasi hiyo.

  Kwa ushindi wa ManU jumamosi ya jana, Arsenal hawanan nafasi ya kuchukua ubingwa ila wanaweza kushindana na Chelsea kugombea nafasi ya pili.

  Wenger akubali uamuzi wa kutonunua wachezaji unawagharimu

  Uwanja wa Arsenal (Emirates Stadium, uliigharimu Paund 430milioni.
  Kocha/Manager wa Arsenal, Arsene Wenger amekubali kuwa timu yake inagharimika sana na uamuzi wa kutotengeneza kikosi kidogo cha Yoso kwa ajili ya kulisha kikosi kikubwa, pia amesema uamuzi wa kutotumia pesa kununua wachezaji pia unawagharimu.

  Wenger aliyasema hayo alipokuwa akiongelea ushindi wa Man U ambao kwa kiasi Arsena msimu huu ataondoka mikono mitupu, “ni wazi uamuzi wetu wa kutumia pesa kwa ajili ya uwanja mwaka 2004 ndio unaotutesa mpaka sasa, nina kikosi imara lakini ningekuwa na uwanja mpana zaidi wa mapendekezo ya kuimarisha timu kama tungekuwa na fungu la kutosha” alisema Wenger.
  Ila bado matumaini yangu ni kwa kikosi cha vijana nilionao, naimani ni bora kutengeneza vijana nitakaa nao kwa muda mwingi kuliko kutumia pesa kumnunua mtu.
  Arsenal waliamua kujenga uwanja mwaka 2004 uamuzi ambao ulisababisha Club kuingiza pesa nyingi, ni mkopo (Mortgage) wa muda mrefu wa Pound £300milioni ambao utailipwa kwa muda mrefu kwa hivyo pesa nyingi inatumika kulipa deni hilo.
  “Kwa kipindi kile ndio ulikuwa uamuzi wetu sasa tulikubaliana kwenda na Policy mpya ambayo ni kutonunua wachezaji kwa gharama kubwa, najua kwenye mchezo huu hilo suala ni gumu kwani kila msimu ukiisha mashabiki wanataka kuona usajili mpya walao hata mmoja wa maana” alisema. Msimu huu tumepambana ingawa kombe si letu lakini tunajitahidi tusiwe mbali na washindi, tutajitahidi tufikie hizo point 83, zitatukea rekodi nzuri.
  Emirates waliubadilisha jina uwanja huo wenye uwezo wa kukalisha watu 60,000, katika deal ya udhamini wa kiasi cha Pound 100m baada ya Klabu kukubali donge hilo, mkataba ambao utadumu kwa miaka 15 ikiwa ni pamoja miaka nane ya kuvaa jezi za shirika hilo la Ndege la Emirates.

  Saturday, May 3, 2008

  Taifa Stars yafanya kweli, yawanyuka waganda 2-0

  TANZANIA Taifa Stars Jumamosi iliwapa watanzania raha tena baada ya kufanikiwa kuichapa timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes” mabao 2-0 kwenye mchezo mkali wakutafuta tiketi ya kucheza michuano ya mabingwa wa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

  Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Stars baada ya wiki chache zilizopita kufanikiwa kuitupa nje timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 2-1 huku Uganda ikifanikiwa kuitoa Elitrea kwa jumla ya mabao 3-0.

  Stars ikiwa na kikosi kile kile kilichoitoa Kenya isipokuwa kiungo Geofrey Bonny alichukua nafasi ya Athumani Idd aliyekuwa na kadi mbili za njano, ilianza mchezo wa jana kwa makeke makali na katika dakika ya 3 walikuwa wameshapiga hodi langoni mwa Uganda baada ya Uhuru Suleimani kupiga krosi lakini shuti la Amir Maftah likaokolewa na mabeki wa Uganda.

  Bao la kwanza la Stars liliwekwa kimiani na Emanuel Gabriel katika dakika ya 12 baada ya kupata krosi safi toka kwa mshambuliaji machachari Mrisho Ngassa na kuunganisha mpira kimiani.

  Shaabani Ndity aliyeingia kuchukua nafasi ya Henry Joseph mwanzoni mwa kipindi cha pili aliipatia Stars bao la pili katika dakika ya 60 baada ya kona safi iliyopigwa na Amir Maftah na kumkuta Nadil Haroub ‘Cannavaro’ ambaye alipiga kichwa kilichopanguliwa na kipa wa Uganda na kumkuta Nditi aliyepiga shuti kali na kutinga wavuni.

  Katika dakika ya 15 Laurence Segawa alipewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Mrisho Ngassa ambaye alikuwa akiisumbua ngome ya Uganda kila mara.

  Kipindi cha kwanza Stars walionyesha kiwango cha hali ya juu na kulisakama lango la Uganda muda mwingi wa mchezo.

  Kipindi cha pili Stars walifanya mabadiliko baada ya Henry Joseph kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Shaaban Nditi, Uhuru Suleiman alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Ulimboka Mwakingwe Uganda alitoka Jeremiah Sebuyira na nafasi yake kuchukuliwa na Jonhson Bangole.

  Dakika za mwanzo katika kipindi cha pili Uganda walitawala mchezo lakini Stars walitumia mwanya huo kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

  Katika dakika ya 63 Uganda walikosa bao baada ya kipa wa Stars Farouk Ramadhan kuupangua mpira ambao uliwahiwa na Nadil Haroub aliyeonyesha uwezo wa hali ya juu jana.

  Na Mwananchi

  Manchester YAUA, Yamtwanga mtu 4-1

  Pichani Cristiano Ronaldo akishangilia moja ya magoli yake
  Magoli mawili ya Cristian Ronaldo dakika ya 3 na ya dakika ya 24 ya mchezo na goli moja la Carlos Teves ambaye hakuonyesha huruma kwa timu yake ya zamani alilofunga dakika ya 26 yalifanya matokeo kuwa 3-1 kwenye nusu ya kwanza ya mchezo kati ya Manchester na Westham. Bao pekee mpaka mapumziko la West ham lilifungwa na D. Ashton dakika ya 28.
  Ronaldo ambaye amefikisha magoli 40 sasa katika msimu huu wa ligi huku akisherehekea Tuzo ya Mwanamichezo bora aliyopewa na Chama cha waandishi wa habari wa Soka.

  Goli la West Ham lilifungwa a Dean Ashton kupachika goli murua dakika ya 28 ya mchezo. Kabla ya M.Carick kupachika goli la nne na kuhitimisha karamu ya magoli kwa Manchester. Mchezo wa leo ulitawaliwa na rafu za hapa na pale kwani jumla ya kadi moja nyekundu aliyopewa Nani wa Manchester, na kadi nne za Njano moja ikiwa ya C.Ronaldo, na kwa upande wa West HAm walipewa kadi za njano ni L.Neil, G.McCatney, na B. Zamora.

  Matokeo ya Mechi nyingine ni kama ifuatavyo
  Bonyeza kwenye magoli upate Yaliyojiri pamoja na wafungaji wa magili hayo

  FT Aston Villa 0 – 2 Wigan Athletic
  FT Blackburn R. 3 – 1 Derby County
  FT Fulham 2 – 0 Birmingham C.
  FT Middlesbrough 2 – 0 Portsmouth
  FT Reading 0 – 1 Tottenham H

  Kalunde Band ndani ya Giraffe Ocean View Hotel

  Wanaitwa Kalunde Band, chini ya Uongozi wa Gwiji Deo Mwanambilimbi, wamekuwa gumzo katika wapenzi wa muziki wa dansi kwa jinsi wanavyoshambulia jukwaa na ustadi wa upigaji wa Vyombo. Kalunde Band wanapatikana kila siku za ijumaa na Jumamosi ndani ya Giraffe Ocean View Hotel

  Halle Berry bado wamo.  Mhceza sinema maarufu Halle Berry alionekana kwa mara ya kwanza kwenye kadamnasi tangu ajifungue mtoto wake wa kike Nahla katikati ya mwezi Machi. Halle Berry amekuwa adimu na kuwindwa na Camera za vyombo vya habari kila kona. Hata baada ya Kujifungua magazeti yanasema Berry bado wamo na bado anamvuto kama kawa.

  Kiingilio cha Taifa Stars na Uganda, Wananchi walia

  Taifa Stars
  V/s

  The Cranes

  KIINGILIO cha mechi ya timu ya Tanzania,Taifa Stars na Uganda, The Cranes, itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kimelalamikiwa na mashabiki wa soka hapa kuwa ni kikubwa.

  Shirikisho la soka Tanzania, TFF limetangaza kuwa watakaotaka kuuona mchezo huo watalazimika kulipa sh,5,000 kwa mzunguko na sh,20,000 kwa jukwaa kuu.

  Baadhi ya mashabiki wameanza kugwaya na kupanga kuusikiliza mchezo huo kupitia redio na kwa kile walichodai kuwa kiingilio ni kikubwa.

  Taarifa mbalimbali zilizokuwa zikipatikana jijini humo kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa soka tangu kutangazwa kwa kiingilio hicho zilikuwa zinasema kwamba kiingilio hicho ni kikubwa mno kiasi kwamba mashabiki wengi hawataweza kumudu hali ambayo inaweza kupunguza mapato kwa timu hizo.

  Na Mwananchi

  Leo ni Leo Taifa Stars Vs The Cranes

  WINGA machacha wa timu ya Yanga na Taifa Stars, Fred Mbuna amewataka Watanzania kuwa na imani nao kwani wataweza kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Uganda utaochezwa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Tunataka kuwaonyesha Watanzania kuwa hatukubahatisha kuifunga Kenya tulipocheza nayo Dar es Salaam, leo tuna kila sababu ya ushindi pamoja na kuwa tunacheza na mmoja ya timu ngumu Afrika Mashariki.

  Ushindi ni wetu tu tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunashinda leo na kurudisha heshima ya Tanzania katika ramani ya soka Afrika.

  Naye Jerry Tegete aliongezea kuwa wanatambua kuwa mechi ya marudiano itakuwa ngumu kwao watapokuwa nchini Uganda kwahiyo watacheza kwa moyo na kujituma wasiwaangushe mashabiki.

  Kwenye mchezo lolote linaweza kutokea lakini sisi lengo letu ni kuhakikisha tunashinda na kujitegenezea mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua nyingine ya michuano hii.

  Na Mwananchi

  Shoo ya mavazi na vito vya madini yafana

  Mgeni rasmi waziri wa nishati na madini mh. william ngeleja (mwenye tai juu kati) akipozi na waandaji na mamodo walioshiriki katika shoo ya mavazi na vito vya madini mbalimbali usiku huu kwenye hoteli ya movenpik, dar. shoo hiyo iliyofana sana iliandaliwa na chama cha wachimba madini wanawake
  Na Michuzi

  Gattuso: Natamani kucheza Premier ligi UK

  Tetesi kuwa mchezaji matata wa AC Milan stalwart Gattuso anatarajia kuhama, zimeenea kila mahala hasa kwa mashabiki wa klabu hiyo ya Italy lakini yeye mwenyewe amekaa kimya bila kusema chochote juu ya hatma yake kwa msimu ujao.

  ‘Bado sijaamua mpaka sasa ila ningependa kupata nafasi ya kucheza ligi ya uingereza the Premier League,’ aliiambai Televisheni ya Italy’s Sky TV ijumaa hii, ni ndoto ambayo ninayo kila siku na sio siri tena naweka wazi, ningependa sana kucheza kule nahisi aina ya mpira wanaocheza ningeifurahia zaidi, watu wengi wakiwemo wa karibu yangu wamekuwa wakiniuliza kuhusu wapi nitaenda,siko tayari kuongelea kwa sasa lakini nitafanya hivyo muda ukifika kwani sitaki kuleta kutokuelewana katika klabu yangu alisema GAttuso.

  Timu za Uingereza zimekuwa katika heka heka za kutafuta wachezaji kwa msimu ujao wa ligi, wajuzi wa mambo wanasema Gattuso anaweza kuwa tumaini kwa vilabu vikubwa vya Uingereza na habari zinasema kumeonekana maajenti wa wachezaji toka Uingereza kwenye mechi za AC Milan bila kufafanua zaidi.

  Video ya Wiki: Cristiano Ronaldo

  Kuna maisha nje ya uwanja na wengi wanamjua Ronaldo akiwa uwanjani, kijana huyu kwa wiki mbili hizi amefanikiwa kuchukua tuzo mbili za uchezaji bora angalia posti za chini.
  Bonyeza Player ujue Ronaldo anakula nini, anaendesha nini, anapenda muziki gani, analala wapi anaendesha gari gani n.k, na hii ndio Video yetu ya wiki hii.

  Ronaldo alamba Tuzo nyingine

  Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo (23) kwa mara nyingine tena amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwaka na Chama za Waandishi wa habari za Kandanda FWA (Football Writers’ Association) kwa mwaka wa pili mfululizo.

  Winga huyo wa Ureno ndiye aliyechukua tuzo hiyo kwa mara ya pili baada ya Thiery Henry kuchukua tuzo hiyo mwaka 2004.

  Zawadi hii inakuja baada ya wiki moja tuu kupata Tuzo nyingine kutoka kwenye chama kingine wakimtaja kama mchezaji bora wa mwaka.

  Mshambuliaji wa Liverpool Fernando Torres na goilikipa wa Portsmouth David James waliambulia nafasi ya pili na tatu.

  Kutokana na Tuzo hizi Ronaldo kwa sasa ndiye mchezaji pekee mwenye tuzo nyingi katika Ligi ya Uingereza.

  “Kufunga magoli 38 katika msimu mpaka sasa si kitu cha mchezo, inaonyesha kipaji na kujituma kwa mchezaji husika, alisema mwenyekiti wa Chama hicho (FWA) Paul Hetherington.

  “Hakupata asilimia 100% ya kura zote lakini tangu kura zianze kupigwa alikaa namba moja mpaka tunamaliza upiganji wa kura hizo alikuwa kileleni, hii inaonyesha ni jinsi gani watu pia wamemkubali”

  “Kutokana na umri wake na namna ya uchezaji wake anayo nafasi ya kushikilia Tuzo hii kwa miaka, hiyo inategemeana na juhudi zake yeye mwenyewe kama ataendelea kujituma namna hii”

  Furguson: “Hakuna wa kutuzuia Ubingwa”

  Maneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini kuwa timu yake iko kwenye nafasi kubwa ya kuchukua Ubingwa wa Premier League, achilia mbali kipigo walichokipata toka kwa Wazee wa darajani Chelsea jumamosi iliyopita.

  Matokeo ya 2-1 na Chelsea yaliwafanya kuwa na pointi sawa kwenye msimamo wa ligi.

  Lakini kocha Ferguson anasema ni lazima tukalie uongozi wa ligi, hata kama tuko na point sawa ila tumewazidi kwa magoli ya kufunga.

  “Natarajia tutashinda mechi yetu na Westham jumamosi (leo) ambayo nauhakika itatuhakikishia kushinda ligi” alisema Furguson.

  Wakati ManU wanakutana na Westham, Chelsea wao wanasafiri kwenda Newcastle jumatatu .

  Defender Nemanja Vidic inawezekana asicheze kwenye mechi hiyo huku kukiwa na habari za matumaini kuwa Wayne Rooney hali yake imekuwa imeimarika hivyo anaweza akacheza pia, kwani aliukosa mtanange na Barcelona Manchester waliposhinda.

  American Idol: Paula Hakulewa!

  Paula Abdul ambaye alionekana akinywa na baadhi ya watu walimuona na kumshutumu kwa mchemsho ambao kiufundi ilikuwa nje ya uwezo wake, kwani ilitokea pale alipotoa maoni baada ya Jason Castro kuimba, Ikumbukwe kuwa kwa sasa washiriki wanaimba nyimbo mbili katoka show moja, sasa Paula alitoa maoni kwa wimbo wa pili ambao ulikuwa haujaonyeshwa bado, kwani wao wanakuwa wamepata nafasi ya kuwaangalia na kuwasikiliza washiriki wote kabla ya show kwenda hewani (Live), kwa upande wao American Idol wanasema haya ni makosa ya kiufundi kwa maonyesho ya moja kwa moja ni rahisi kwa mtu kujichanganya. Bonyeza player upate kipande hicho.

  Kumekuwa na malalamiko toka kila upande wakishutumu kuwa Paula alikuwa na agenda ya siri na Jason kwamba anampenda na kutaka ashinde ndio maana alishindwa kuficha hisia zake.

  Mariah Carey afunga ndoa na Cannon

  Mariah Carey, 38, ameoana na rafiki yake mpenzi (boyfriend) ambaye urafiki wao unasemwa ulidumu kwa mwezi mmoja tu kabla ya kuamua kufanya kweli jumatano hii.

  Cannon ambaye ni muigizaji sinema ambaye yuko juu kwa chati, inasemwa alianza uhusiano wa kimapenzi na sugar mummy wake Carey yapata mwezi mmoja sasa.

  Carey na Cannon waliamua kwenda kufungia ndoa hiyo katika kisiwa moja ya visiwa vya Caribbean cha Eleuthera Jumatano hii, Henrietta White, ambaye anamiliki duka la maua kwenye kisiwa hicho cha Eleuthera, aliwaambia shirika la habari la E! News kuwa mwanaye ndiye aliyetengeneza maua kwa ajili ya harusi hiyo.

  wawili hao wamefunga ndoa kwenye sherehe ndogo ambayo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu na ndugu wachache sana.

  Carey alimpenda sana Cannon, na hata katika video yake inayotarajiwa kutoka hivi karibuni , Carey amemtumia ameigiza kama mpenzi wa Cannon.


  Mariah Carey amekuwa kwenye sekta ya muziki siku nyingi na kwa sasa Albam yake mpya ya E=MC2 ambayo aliitumbukiza sokoni tarehe 15 April inafanya vizuri sana na iko kwenye chati za juu ikiongoza, hivyo mafanikio bado anayo.


  Carey amemuoa Cannon kwenye nyumba yake ambayo amenunua hivi karibuni kisiwani Eleuthera, habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo maarufu ambaye alipata tuzo ya Grammy zilithibitisha.

  “Wamekuwa pamoja kwa masiku sasa, mara nyingi wako pamoja, lakini mara nyingi wamekuwa na mikwaruzo ya hapa na pale, ni uhusiano ambao umedumu kwa mwezi mmoja kama mtu na rafiki wake wa kiume, sasa wameamua kuoana” alisema rafiki wa Carey.

  PAmoja na suala la miaka kupishana sana lakini bado mapenzi ndio yaliyopelekea wawili hawa kufikia hapo, kwani Carey amemzidi mume wake kwa miaka 11.

  Habari hii kwa msaada wa Ihano Kilonzo na FoxNews.

  Friday, May 2, 2008

  Je Unajua Ze Comedy ilipoanzia?

  “Ze Comedy ilipoanzia ilikuwa baada ya kualikwa katika show ya live iliyokuwa inaendeshwa na kituo cha televisheni cha EATV maarufu kama Chanel 5 ambapo tuliitwa wachekeshaji wote nchini akiwemo Zembwela,Mtanga, Senga,Joti ,Bambo,Mpoki nk


  Wakati show inaendelea tuliulizwa kama swali la uzushi kuwa je tuna uwezo wakuchekesha? tukakubali na tukaona kama chalenge na baada ya show Seki na Seko walituuliza je tunauwezo wa kuchekesha watu mfano tukipewa live show…sie tuliichukulia kama chalenge na tukaanza kujifua na ndipo tulipoibuka na zile Live show ambapo tulikubaliana tuwe tunafanya show na kisha inarushwa kwenye tv na tukaanza na ile ya Slip Way na kisha Star Light

  Baada ya vipindi vile kurushwa kuna wengine walishindwa wenyewe na mwendo kasi wetu kutokana na ule moto tuliokuwa tumeanza nao kuna wenzetu ambao waliona wao wako na majina makubwa kushindwa Ze Comedy hivyo ikawa kuna tatizo na wakaamua kujiengua na wengine kutokana na kushindwa kurandana na sisi pia waliondoka hadi mwisho tukajikuta tumebaki mimi, Mpoki na Joti na baadae wakajiunga Masanja, Vengu na Mc Regan na tukatimia watu 6 ambao tupo had leo hii mwaka wapili huu unakuja.

  Soma mahojiano zaid DarHotWire

  Nafasi imejaa Taifa Stars, walioikosa walie tuu.

  Pichani ni Taifa Stars walipokuwa Denmark kwa ziara ya mafunzo.

  KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa Stars, Ally Bushir amesema mfumo wa kubadilisha wachezaji timu ya Taifa sasa umekwisha na kama mchezaji hakupa nafasi hiyo huku nyuma sasa atafanya kazi ya ziada kuipata.

  Stars ipo Mwanza ikijiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano mipya ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda mchezo utakaopigwa kesho jijini humo.

  Bushir aliiambia Mwananchi juzi kuwa kocha mkuu wa Stars, Marcio Maximo amewaita wachezaji wale wale kwenye kikosi chake kwa kuwa ule muda wa kujaribu wachezaji kwenye kikosi hicho sasa haupo tena.

  ”Sisemi ya kwamba hawataitwa kwenye kikosi kama wakionyesha uwezo hapana, lakini watatakiwa kufanya kazi kubwa sana kwa kuwa wachezaji wengi kule wameiva na kuwatoa itawabidi waonyeshe uwezo sana,” alisema Bushir.

  Mwananchi

  Mkurugenzi wa Arsenal aachia ngazi.

  Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Arsenal Keith Edelman pichani, ametangaza kuacha kazi na klabu yake ya Arsenal imethibitisha habari hiyo.

  Edelman amekaa katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka minane (8), na ameona hatua zote za mafanikio ya Arsenal. Sababu hasa hazikuwekwa wazi ila habari za ndani zinasema Mkurugenzi huyo hajaondoka kwa mabaya, ni katika hali ya kawaida mtu anaamua kubadili hali ya  hewa.
  Amejiuzulu kama Mkurugenzi wa Arsenal Holdings PLC lakini atabaki kuwa mashauri wa karibu kwa kipindi cha miezi 12 kuhakikisha mambo hayaharibiki mpaka Mkurugenzi mpya atakapozoea usukani wa jahazi hili, ilisema taarifa ya Arsenal. Arsenal tayari imeshaanza kumtafuta mtu wa kuziba pengo la Edelman, chini ya Mkurugenzi mwingine Ken Friar ambaye aliiongoza kampuni hiyo kwa miaka 18 hadi mwaka 2000. na kwa sasa atashikilia kiti hicho wakati tunasubiri kama tutapata mtu mwingine zaidi, ilisema taarifa hiyo.

  Thursday, May 1, 2008

  JB Mpiana alipompigia kampeni Kabila

  Wakati mwingine wanamuziki wanachangia kwa kiasi kikubwa sana katika mambo ya kijamii, JB Mpiana alishiriki katika kumpigia kampeni Joseph Kabilla katika uchaguzi ulipita ambapo wanamuziki waligawanyika na kuna wale ambao walimuunga mkono Jean Piere Bemba na wengine kwa Kabila, Wanamuziki kwa Congo-Kinshansa wanamvuto wa namna ya pekee kwa jamii kwani ndio sekta ya burudani inayopendwa na wengi ukilinganisha na burudani nyingine.
  Bonyeza player upate uhondo.

  Siku 98 Zimebaki kwa Michezo ya Olympic ianze

  Picani ni wakimbiaji wa mbio ndefu wakikimbia kuadhimisha siku 100 hadi kuanza kwa michezo ya Olympic wakiwa nje ya Uwanja wa Bird Nest, uwanja ambao utatumika katoka ufunguzi na ufungaji wa michuano hiyo.

  Bird Nest: Uwanja wa Taifa wa Beijin China

  Mwaka 2002, serikali ya China ilitangaza shindano rasi dunia nzima kushindana kubuni michoro kwa ajili ya uwanja wa Taifa utakao tumika kwa ajili mashindano ya Olympic. Ai Weiwei, ni mshauri wa mambo ya Sanaa ndiye aliyeshinda shindano hilo na kuja na mchoro ambao aliuita Bird Nest (Kiota cha Ndege), Eneo la ujenzi lilivunjwa rasmi siku ya mkesha wa Christmas Eve December 2003, na ujenzi kuanza rasmi mwezi Marchi 2004, ila ujenzi ulisimama baada ya kusema kuwa gharama za ujenzi ni kubwa sana August 2004, na baadaye ujenzi uliendelea mwezi January 2008. suala la usalama kipindi cha ujenzi liliamsha hisia za watu pale idadi ya watu walikufa kwenye ujenzi huo ilipofikia 10 kwani kasi ya ujenzi ilikuwa kali ili kukamilika kwenye tarehe iliyopangwa.
  Hatimaye uwanja umekamilika na unaweza kuchukua idadi ya watu 91,000 kipindi cha michezo ya Olympic ila idadi hiyo itapungua baada ya michezo hiyo na kufikia 80,000. Uwanja huu ndio utakao kuwa mbadala wa uwanja mwingine wa Guangdong Olympic Stadium.
  Uwanja huu una ukubwa wa Mita 330 kwa urefu, mita 220 upana, na una urefu wa mita 69.2, Uwanja umetumia jumla ya Mita za mraba 258,000. Umetumia jumla ya Kilomita 36 za chuma.
  ambazo zina jumla ya Tani 45,000. kuna kilomita za mraba 11,000 za vyumba vya chini kwa chini (Underground rooms with waterproof walls.) Mpaka kukamilika uwanja unakadiriwa kutumia jumla ya USD 423 million USD.

  Chelsea 3 – 2 Liverpool (4-3)

  Didier Drogba ndiye aliyekuwa mwiba jana usiku kwenye mtanange wa kukata na mundu wa nusus fainali dhidi ya Liverpool

  Mu Ivory Coast huyo ndiye aliyefungua kitabu cha magoli kwa shuti kali toka yadi 12 golini mwa Liverpool baada ya kipa kuutema mpira na kumfikia Drogba aliumalizia vizuri, lakini alikuwa Fernando Torres aliyeisawazishia Liverpool baada ya fowadi za Liverpool kuichambua ngome ya Chelsea na Tores kuutumbukiza mpira kwa shuti la chinichini, kwa vile mchezo wa jana ni lazima mshindi apatikane ikizingatiwa katika raund ya kwanza walitoka droo ya 1-1 ilibidi muda uongezwe baada ya kuwa sare ya 1-1 hadi daki 90 za mwanzo.

  Magoli ya Lampard na Drogba dakika za nyongeza ndio yaliyoipeleka Chelsea fainali itakayo fanyika Moscoe mwezi ujao ambapo watakutana na Manchester.

  Ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu afiwe na mama yake mzazi wiki iliyopita Lampard hakufanya ajizi kwani Kocha wa Chelsea alisema Lampard atamuenzi mama yake kwa kupachika goli huku akiwa bado kwenye majonzi, Baada ya kufunga goli hilo lililomchambua kipa kulia mpira kushoto Lampard alishangilia huku akishika kitambaa chake cheusi na alikwenda na kuinamisha kichwa chini mikono usoni akionyesha kumkumbuka mama yake mzazi.

  Mchezo wa jana ulikuwa mkali sana na kosa kosa nyingi kwa kila upande, mpira ulikuwa mzuri Liverpool walicheza vizuri lakini bahati haikuwa yao.
  Hali ya uwanja ilikuwa ya utelezi lakini Chelsea walionyesha kuimudu vilivyo labda ni kwa kuwa walikuwa wakichezea nyumbani na uwanja wao wameuzoea.

  Hata hivyo goli moja la Essien lilikataliwa na msaidizi wa refa (L.man).
  Chelsea wanakwenda kukutana na Manchester United katika Fainali zitakazofanyika mwezi ujao Moscow Urusi, mchezo ambao unatazamiwa kuwa mgumu, Pole Michuzi, Pole Balua, poleni Liverpool ndio ukubwa huo.

  4 Responses to May

  1. Katt says:

   I love this, any its kool.

  2. Grace Muhamiriza says:

   nina shagaha sana kwa kua watu wanamuwa mtu bila kosa

  3. Grace Muhamiriza says:

   nina shagaha sana kwa kuwa Acteur wangu amefariki “STEVEN KANUMBA”

  4. I love the efforts you have put in this, appreciate it for all the great blog posts.

  Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google photo

  You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: