MPYA HIYO !!! VIDEO YA WERRASON WIMBO ” BLOCK CADENAS “

October 15, 2014

http://www.youtube.com/watch?v=m0ZEx1dTeQ4

 

BONYEZA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO

KAMA KAWAIDA TUNAWALETEA VITU VIPYA,

BAADA YAKUSIKILIZA AUDIO YA BLOCK CADENAS, SASA TIZAMENI VIDEO YAKE ILIO SAFI KABISA.

BURUDIKENI.

 

L.W.L

 


USIKU MWEMA NA VIDEO YA LINO VERSACE FEAT FERRE GOLA

October 14, 2014

 

TUCHEZE KWA MIONDOKO YA COUPER DECALER!!!! WIMBO ” KO KO KO ”

LINO VERSACE  AMBAE SIKU HIZI HUPENDWA KUITWA ” Soundjata Soumangourou ” Ni Mwimbaji kutoka Inchi ya COTE D’IVOIRE .

NI MMOJA KATI YA WAASISI WA MIONDOKO YA ” COUPER DECALER ”  WAKIWA PAMOJA NA MAREHEMU  ” DOUK SAGA ”

 

L.W.L

 

 


TUMKUMBUKE GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI / NYIMBO ZAKE ZILIZO PIGWA MARUFUKU

October 14, 2014

 

Miaka 25 Sasa tokea Afariki Dunia Guiji wa Muziki wa Rumba FRANCO LUAMBO MAKIADI.

Ingawa Mengi yamesha andikwa kwa kumhenzi GRAND MAITRE FRANCO, Leo hii nachukua fursa ya kuchambua Baadhi ya Nyimbo zake zilizo pigwa Marufuku.

Wala sio Siri tunapo tamka ya kwamba ” GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI FRANCO ” katokea kua Tajiri sana katika kipindi cha Utawala wa Rais MOBUTU SESESEKO.

Mbali na Urafiki ambao FRANCO LUAMBO alikuanao na RAIS MOBUTU, ilifikia wakati fulani Serekali ikazipiga marufuku Baadhi ya Nyimbo zake zilizo kua na Ujumbe uliokeuka Maadili ya Umma.

Kutokana pia na Sababu mbali mbali, SEREKALI YA RAIS MOBUTU, ilikua makini sana na Wanamuziki, hasa palikua na Watu hodari ambao kazi yao kuu ilikua kufanya uchunguzi wakina kwa Ujumbe unao patikana kwenye NYIMBO. Ikiwa kwa Namna moja au Nyingine kwenye Wimbo wewe Msanii ukithubutu Kutamka Jina la Mpinzani, Basi Wimbo huo kamwe hauta ruhusiwa na Wewe mwenyewe utajikuta ukiwa matatani.

1. Mkasa kama huo umemkuta  TABU LEY ROCHEREAU, wakati katunga Wimbo ” KASHAMA NKOYI ” kwenye Wimbo huo, ROCHEREAU kayatamka Maneno haya : ” Boni Oweleli, Okende liboso ya Baninga, Soki okutani na LUMUMBA okoloba nini PAPA ?  Tokengelaki yoo te  KASHAMA  NKOYI / INAKUAJE UKASAFIRI, WATUTANGULIA SISI WENZIO, HUKO UENDAKO, UTAKAPO KUTANA NA LUMUMBA UTAMWAMBIAJE BABA ? WALA HATUJAWAHI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KWA YALE YALIYO KUKUTA ” KASHAMA NKOYI “.

Wimbo umepigwa Marufuku, sio kwasababu  Katajwa LUMUMBA hapana, Bali Jina ” KASHAMA NKOYI “, Serekali ya MOBUTU yamushutumu ROCHEREAU TABU LEY kutumia Jina hilo Bandia kwakumhenzi ” PIERRE MULELE ” ambae alikua Mmoja kati ya MAWAZIRI wa EMERY PATRICE LUMUMBA,SHUJAA WA UHURU WA CONGO. Baada ya kuuwawa LUMUMBA, PIERRE MULELE kasimama kidete kupambana na SEREKALI ya MOBUTU. Vikosi vya Waasi vilio tawala mashariki mwa Congo hasa kwenye Mikoa ya KIVU. VIlikua vikimchukulia yeye kama Kiongozi wao Mkuu. Ndiko katokea LAURENT DESIRE KABILA. PIERRE MULELE kauwawa Mwaka 1968.

2. FRANCO LUAMBO NA WIMBO WAKE ” LUVUMBU NDOKI “, Kwenye Wimbo huo, FRANCO kaimba kwa KIKONGO, Lugha yake ya Asili. Ujumbe kwenye Wimbo huo ni kwamba ” WEWE LUVUMBU MTU AMBAE KIJIJI KIZIMA KINAKUTEGEMEA, WANAKIJIJI WOTE WAKO CHINI YA USIMAMIZI WAKO, KUTOKANA NA UCHAWI WAKO, UMEWAMALIZA NDUGU ZAKO WOTE WAKIKE KAMAVILE WAKIUME, SASA WAKATI UTAKAPO FARIKI, NANI YULE ATAKAE KUZIKA ? MIMI FRANÇOIS NASHINDWA KABISA KULIA, KWAKWELI HUA NAJIULIZA, KWANI UCHAWI WAKO UPO MGONGONI AU TUMBONI MWAKO.

Wimbo huo Ulipigwa marufuku paletuu ulipo tolewa, SEREKALI ya RAIS MOBUTU, yasema kwamba, Kupitia Wimbo huo, FRANCO LUAMBO MAKIADI kawatukuza Wanasiasa Wanne Walio Uwawa kwa Kunyongwa kwa Madai kwamba walikua na nia ya kuipindua Serekali Mwaka 1966.  Wanasiasa hao walio nyongwa ni hawa :

1. JÉRÔME ANANY ( WAZIRI WA ZAMANI WA ULINZI WA TAIFA )

2. EMMANUEL BAMBA ( SENETA )

3. ÉVARISTE KIMBA ( WAZIRI MKUU WA ZAMANI )

4. ALEXANDRE MAHAMBA ( WAZIRI WA ARDHI )

Baada ya Wimbo huo kutolewa, FRANCO LUAMBO  Tetesi zilimjia kana kwamba SEREKALI ipo kwenye harakati ya kumfungulia Mashitaka na Kumuweka Jela. LUAMBO kavuka yeye pamoja na Group lake nakwenda kujihifadhi kwa Mda JIJINI BRAZZAVILLE.

Akiwa JIJINI BRAZZAVILLE, RAIS MOBUTU kamtumia Wajumbe na kumshawishi arudi KINSHASA, maisha yake haitakua hatarini. FRANCO LUAMBO kaupokea wito huo ila kawa katika hali ya Mtu mwenye Kusita. Mwishowe kaamua kurudi KINSHASA.

Akiwa JIJINI KINSHASA, FRANCO LUAMBO kajikuta yuko matatani, Kakaribishwa na kikosi cha Wanajeshi. Wakamuamuru yeye na Group lake wapande ndani ya Gari lao, nakupelekwa moja kwa moja  Jela ya NDOLO. Huko walikaa kwa Mda wa Siku Mbili, yasemekana Walicharazwa bakora sawasawa,

Baada yakutolewa kwenye Jela ya NDOLO,  FRANCO LUAMBO na Group lake, wakahamishwa kwenye Kambi ya Jeshi ” TSHATSHI “. Huko pia wakashikiliwa kwa siku kadhaa wakiwa kambini humo.

Ndipo Ikatokea Siku amabayo RAIS MOBUTU akaja mwenyewe kujadiliana na LUAMBO MAKIADI. kamtamkia Maneno haya : ( KUANZIA LEO HII HADI ITAKAPO FIKIA WAKATI WA MIMI KUONDOKA MADARAKANI, UTAKUA UKINIIMBIA MIMI, WATAKIWA KUNIFANYIA KAZI ZANGU ZOTE, NA TENA KWA WAKATI WOWOTE NTAKAO KUHITAJI ) .

Nakwakeli Tokea siku hiyo, FRANCO LUAMBO kawa kiungo kikuu sana kwa Kampeni ya RAIS MOBUTU. na kutokana na ushirikiano huo, kanufaika sana kuwazidi Wanamuziki wengine wote wa Inchi hiyo katika kipindi hicho cha utawala wa Serekali ya MOBUTU SESESEKO KUKU NGBWENDU WAZABANGA JOSEPH DESIRE.

Mwaka 1978,  FRANCO LUAMBO MAKIADI kawekwa tena JELA kutokana na Utunzi wa Nyimbo ( HELEINI na JACKIE ),

Nyimbo mbili hizo zilikua na Maneno machafu sana tena yaku yaharibu maadili ya Umma. Sheria ikachukuliwa kuzipiga Marufuku zisipitishwe kwenye Radio na TV ya taifa. FRANCO mwenyewe kajitetea, kasema wala NYIMBO hizo hajizauzwa Sokoni zilikua bado hazijawekwa kwenye CD. bali Watu walikua wakizisikiliza Wakati wa SHOO kwenye Ukumbi wake wa 1.2.3 KINSHASA.

Aliekua MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI kipindi hicho  ” Mr  LEON KENGO WA DONDO “,kalisimamia swala hilo, nakuamuru FRANCO LUAMBO awekwe Jela, kapelekwa kwenye JELA ya ” LUZUBU ” inayo patikana kwenye MKOA WA BAS CONGO aliko zaliwa FRANCO.

Huko JELA, FRANCO kawa mwenye masikitiko, Kwanini RAIS MOBUTU kashindwa kumsaidia ? yeye ambae alikua akimchukulia kama Rafiki. FRANCO kapigwa na Ugonjwa wa HEMORRHOID. katabaanika kabisa. Kabaki na chuki na kinyongo dhidi ya MWANASHERIA ” LEON KENGO WA DONDO ” aliempeleka JELA. Haelewi kwanini kawekwa kizuizini wakati Hajawahi kuzidumbwiza Nyimbo hizo hadharani.

Miaka michache baadae, palitokea na mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, LEON KENGO WA DONDO  Kanenguliwa Cheo cha MWANA SHERIA MKUU WA SEREKALI na kutomwa JIJINI BRUSSELS kama BALOZI WA CONGO.

Furaha ilikuaje kwa FRANCO LUAMBO MAKIADI ?, bila kukawia kamtungia Wimbo ” TAILLEUR ” kwenye Wimbo huo FRANCO kanena haya : ( LIKAMBO NALOBAKI LOBI, MONOKO NA NGAI NGANGA / UTABIRI WANGU WATOKEA KUA KWELI, MDOMO WANGU KAMA WA MGANGA WA JADI ).

MOKOLO TONGA ABOTOLI TONGA OKOTONGA NANI ? / MWENYE SINDANO YAKE KESHA ICHUKUA, SASA UTATUMIA NINI ILIUENDELEE KUWACHOMA WENGINE?

OLOBAKI TROP NA ESIKA YANGOO BATIE YO PEMBENI LOBA LISUSU MAMA / ULIKUA UKIKIJIVUNIA SANA CHEO HICHO, SIUMEONA WAMEKUONDOA, UNANINI CHAKUONGEA? Wimbo huo pia ukapigwa Marufuku kwa Mda.

Mwaka 1982, RAIS MOBUTU Kamwitisha LEON KENGO WA DONDO , na kamteua kama WAZIRI MKUU WA INCHI.

FRANCO LUAMBO hajaridhishwa ni kitendo cha RAIS MOBUTU kumpa KENGO WA DONDO cheo cha WAZIRI MKUU, bila kusita Katunga Wimbo ” TRES FACHE “. Mtamsikia akiiimba : ( OKOSI NGAI MAMA YONAYE BOBOYANA, LOBI LISUSU BAKUTI YO NA VOITURE NA YEE, ELOKO NASALA NAYEBI TEEOO MOKILI / WANIDANGANYA KAMA NYIE WAWILI SIO TENA MARAFIKI, KESHO YAKE WATU WAMEWAONA MKIWA PAMOJA NDANI YA GARI, JAMANI KOSA GANI NILILOLIFANYA MIE!!! ). Kadhalika Wimbo huo Ulipigwa pia Marufuku.

GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI KAFARIKI DUNIA  INCHINI BELGIUM TAREHE  12-10-1989.

SIKU YA MAZISHI YAKE, LEON KENGO WA DONDO AMBAE NDIE ALIEKUA WAZIRI MKUU, KAJA KUTOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA NIABA YA SEREKALI.

WAKATI WA MISA  YA MAZISHI YAKE, PADRE KASEMA : ” LUAMBO ALIKUA MTUME WA MUZIKI, HAKUNA ALICHOKISAHAU KATIKA UTUNZI WAKE, KAVICHAMBUA VITU KADHALIKA NA WATU WAKILA RIKA, HATA RAIS MOBUTU HAJAACHWA NYUMA.

NYIMBO ZAKE KADHAA ZILIPIGWA MARUFUKU, HATA HIVYO ZILIENDELEA KUPENDWA SANA NA UMMA. HUKU NYIMBO ZAKE  NYINGINE HADI LEO HUCHUKULIWA KAMA NEMBO YA TAIFA.

L.W.L

 

 

 

 

 

 

 


MA DANCERS WA WERRASON WAFURAHIA TUZO ZA BOSI WAO KWAKUNENGUA!!!

October 13, 2014

 

HAYA TIZAMENI WENYEWE, KWA NAMNA GANI WANENGUAJI WA WERRASON WANAVYO SHEHEREKEA KURUDI KWA BOSI WAO NA TUZO MBILI KUTOKA AMERICA!!!

 

L.W.L


WERRASON KALITEKA JIJI LA KINSHASA, WATU WENGI WAMEJITOKEZA KUMPOKEA KWA SHANGWE UWANJA WA NDJILI

October 13, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO YA MAPOKEZI MAKUBWA YA WERRASON.

PALIKUA NA PATASHIKA JANA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA NDJILI JIJINI KINSHASA,

WENGI WALIJITOKEZA KUMPOKEA WERRASON LE ROI DE LA FORET .

WERRASON KARUDI NYUMBANI AKITOKEA AMERICA AMBAKO KAPEWA TUZO MBILI KWENYE SHINDANO LA NAFCA, LIKIWEMO TUZO LA MSANII BORA WA AFRICA.

 

L.W.L


MKE WA MAREHEMU BABIA NDONGA CHOKORO KAJIELEZA KUHUSU KIFO CHA MWANAMUZIKI HUYO ( SIO MIMI NILIE MUUWA BABIA )C

October 12, 2014

 

Katika mahojiano yake na Waandishi wa Habari, Mama ” HALIMA “, ambae ndie Mke Halali wa BABIA NDONGA kajieleza kwa kirefu kutokana na Kifo cha Mmewe.

HALIMA : Ilitokea Siku Moja BABIA kaniambia, ” Sikiliza HALIMA, Sikutaki tena, Tokea leo hii jisikie kuwa huru, jitegemee mwenyewe. Nimeshampata Kimwana mwengine ” ( yasemekana Kimwana huyo ni  Binti wa Waziri Mmoja kwenye Serekali ya Congo ).

Nikamwambia, hebu Mme wangu, kweli waweza kuniacha Baada ya takriban miaka Minane ya Ndoa, nakwenda kuishi na Mwanamke mwengine? Maneno hayo yaliniuzi sana, Nikafungasha vitu vyangu na kuondoka Nyumbani pale ambapo tulikua tukiishi pamoja. nikahamia sehemu nyingine. Ila tukawa tunaendelea kuwasiliana kupitia njia ya Simu.

Mimi HALIMA ndie Mama mlezi wa Watoto wa BABIA alio wazaa Inje na Wanawake wengine. Hadi leo Wako Nyumbani kwetu KINSHASA kwenye Barabara ya FUNA. Watoto wake PRINCE na ANNA wanaishi kwetu.

SIKU ALIO FARIKI BABIA, KWAKWELI ALIKUA NYUMBANI KWANGU, Mimi ndo nimemuitisha aje tuzungumze. Ila kabla yakuja Nyumbani kwangu, katokea Uwanja wa Ndege akimsubiria Kimada wake aliekua akitokea Ulaya, kwa Bahati mbaya, Mwanamke huyo hajatokea, yaani kahairisha Safari yake bila kumpa BABIA taarifa yeyote.

BABIA kaja Nyumbani kwangu, Kabisha hodi mlangoni, Nilikua niko kwenye Msala nikipiga Rakaa, Mkononi mwangu nilikua nikishikilia Tasbihi, kwakua Mimi ni Muislamu.

Nikaenda kumfungulia BABIA Mlango, pindi tuu alipo ingia ndani nakukaa kwenye Kiti, BABIA akesema HALIMA nahitaji Mazungumzo yakina na!!! kabla hata hajamalizia maneno, Akawa anashindwa kabisa kuendelea kuongea, huku nikamuona Mtu akiwa mwenye kupooza Mikono hadi kwenye Miguu.

Nikashtushwa na hali hiyo, Mwenyewe nikaanza kupiga kelele,  BABIA NIKITU GANI, UNAUMWA NINI, NIKAOMBA MSAADA KWA MAJIRANI, WAKAJA, TUKAMUWAHISHA KWA HARAKA KWENYE HOSPITALI NDOGO KWA DOKTA JUDE.

MTANGAZAJI : Kwani ilichukua Mda gani tokea pale mlivyo achana? yeye akiwa anaishi Nyumbani kwake na wewe Ukawa unapanga Sehemu yako ?

HALIMA : Ilichukua kama Wiki Moja na Siku Tano vile tokea tuachane. Mwenyewe ndo kaniacha, Kaniambia fungasha vitu vyako, anza Maisha yako jinsi uonavyo. Bado ninayo MSG yake nyingi tuu aliokua akinitumia kupitia mtandao wa VIBER. kasema HALIMA JITEGEMEE MWENYEWE, ACHANA NAMIMI, NINAYO MIPANGO MINGI SANA AKILINI MWANGU. MWAKA HUU NILAZIMA NIENDE ZANGU ULAYA, NIMESHA KAA SIKU ZA KUTOSHA JIJINI ” LUANDA “, WAKATI WAWADIA SASA KWAMIMI KUMALIZIA ALBUM YANGU.

Haya narudilia ongezi la hapo awali, TULIPO MFIKISHA BABIA KWENYE HOSPITALI YA DOKTA JUDE, YEYE KAMPOKEA, kamchunguza na kumchoma sindano, Ndipo katushauri tumpeleke kwenye Hospitali kubwa, hali yake yahitaji Tiba nzito zaidi. Ilibidi tumkimbizie kwenye Hospitali KUU, Wakampokea na kumpeleka Moja kwa Moja kwenye Chumba cha dharura, wakamuweka Chupa za maji kwa haraka sana. Ila hali ya BABIA ilikua si nzuri kabisa, alikua hana tena Kauli, kawa Mtu mwenye kutizama tuu.

Nikachukua Simu yake, Nikaanza kuwapigia Marafiki zake nakuwajulisha hali halisi alionayo BABIA, Hakuna yeyote alie jitokeza na kuja kumjulia hali mwenzao. Kutokana na hali yangu ya uchovu, Ma Dokta wakanishauri niende Inje maramoja wao wanaendelea na kazi ya kumuhudumia.

BAADA YA MDA, NIKAAMUA KURUDI CHUMBANI KUCHUNGUZA HALI YA BABIA INAENDELEAJE ?, NDIPO MA DOKTA WAKANIAMBIA KWAMBA BABIA KAFARIKI DUNIA. (ANALIA …)

MTANGAZAJI : Kwani Wewe na huyo Mwanamke mwengine Mmshawahi kuonana ? Mmegombana kiukewenza? au kubadirishana maneno kwenye Simu?

HALIMA : Kuna Siku kanitumia Ujumbe kupitia MSG ya Facebook, kanitukana, kasema BABIA ni wakwake, anajiandaa kuja kumchukua na kuondoka naye, Mimi simuwezi , Baba yake ni KIGOGO kwenye Serekali ya CONGO. Hakuna kitakacho mzuia asifunge Ndoa na BABIA. kasema Mimi ni mjinga. Wala sijawahi kumuona , hata BABIA mwenyewe alikua bado hajamuona. Leo hii ndo nimepata taarifa kwamba kawasili JIJINI LUANDA.

MTANGAZAJI : HEBU TUAMBIE UKWELI Kuhusu Safari yako ya kwenda kwenye MJI WA WAMBO, Ulienda huko kufanya nini  ?

HALIMA : Kwenye MJI WA WAMBO nilienda kufanya BIASHARA ZANGU, hua nauza CD, BABIA alivyosikia niko WAMBO, kanifwata kwa haraka sana, kajakunitishia Nirudi haraka LUANDA, vinginevyo atanifanyia mpango nipelekwe moja kwa moja CONGO KINSHASA.

Nikamuambia kamwe haitowezekana kwangu mimi nirudi CONGO, Mwanaume gani wewe usie nijali? sipati hata Dola 10 kutoka kwako. Ukwali ni kwamba BABIA kaambiwa na Watu kanakwamba Mimi nimeolewa WANDO ndo kwamaana hiyo kaja akiwa mwenye hasira sana. kanigombeza hadi tukaishia Polisi.

Bado tukiwa kwenye MJI WA WAMBO, BABIA kamleta nakunionyesha Mwanamke mwengine Mbele ya macho yangu,  Dada huyo anajulikana kwa Jina la ” LOTTY “, BABIA kanifahamisha ya kwamba huyo ndo Mkewe tokea sasa. Nikamwambia BABIA naomba unipe talaka, nimesha choshwa na vituko vyako. Kwani amenisikia ?

Nikaamua kumuacha pale kwenye MJI WA WAMBO nikarudi zangu LUANDA, Bado akiwa WAMBO, BABIA kapata tenda ya kufanya SHOO mbili. Alipopewa taarifa kwamba nimeshakimbilia LUANDA, Huyo kafunga Safari nakunifwata hadi LUANDA, kaja kuniomba Msamaha, kanitaka radhi, kasema Mimi ndie MAMA WATOTO WAKE, kapagawishwa na Mambo ya Ulimwengu. Kanigea Zawadi ya Dola Elfu Tatu, na Mkufu wa Dhahabu. BABIA kaangua kilio … Moyo wa Umama,Moyo wa Huruma ukanijia, nikamsamehe… Tukaendelea kuishi tena pamoja.

MTANGAZAJI : Tumesikia kwamba Zawadi hiyo ya Mkufu wa DHAHABU ilileta kasheshe iliompelekea BABIA kuwekwa Mbaroni Polisi, ilikuaje?

HALIMA : Kumbe Mkufu huo wa Dhahabu, BABIA kapewa na Kimada wake LOTTY, walipo pezana zawadi zao kutokana na Mapenzi yao mimi wala sikuwepo. Yasemekana  BABIA alikua kampa LOTTY ahadi za uongo kama ndie Mchumba wake, wataishia kufunga Ndoa. Hali hiyo ya Wachumba, ikamfanya LOTTY aanze kumgharamia BABIA kwakumnunulia vitu kadha, ikiwemo Mkufu huo.

Ikatokea Siku moja, BABIA kapokea simu, alie mpigia ni LOTTY, wakaanza kujibishana kwa ukali, nikamsikia LOTTY akisema UMENISALITI, UMEMRUDILIA HALIMA, HAKUNA SHIDA, MWENYEWE UTAONA YATAKAYO KUKUTA.

Wala haijapita Siku, LOTTY huyo katua kwenye MJI WA LUANDA, akiongozana na MABAUNSA wawili waliojaa sawasawa. Jamaa hao walimshikilia BABIA, WAKMTWANGA MBAYA SANA, hadi kaumia Usoni, Mdomo ukamjaa kwelikweli.

Polisi wakaja kuingili kati, wakawachukua wote nakuwapeleka Kituoni kuwasikiliza. Wamewekwa huko kwa siku mbili mfululizo. Mimi nikaambiwa nirudi zangu Nyumbani wala sina hatia yeyote. Kesi yawahusu Wapenzi, Huko waliko kabidhiana Zawadi zao wala mimi sikuwepo.

Huko Kituoni cha Polisi, Muafaka ulipatikana, BABIA KAKUBALI DENI, KASAINI KARATASI NA KATOA AHADI YA KUMRUDISHIA LOTTY VITU VYAKE.

JAMANI ACHENI KUNIPAKAZIA, WALA SIO MIMI NILIE MUUWA BABIA, ALIKUA TAYARI KESHA NIKATAA, KASEMA HALIMA BASI SIKUTAKI TENA, KWENYE MAISHA YANGU, NIMESHA MPATA ” HELENA MWANZA “. YEYE KANIPA AHADI YAKUNISAIDIA NA KUNIPELEKA ULAYA NIKAMALIZIE ALBUM YANGU. JAMANI ,NTAMUUAJE BABA WATOTO WANGU? SIWEZI KUMTAKIA BABIA UBAYA WOWOTE. ACHENI KUNICHAFUA!!!

NDIO BABIA ALIKUA MME WANGU, NDIE PIA KANILEA KWAHIYO KWA UPANDE MWENGINE NILIKUA NIKIMCHUKULIA KAMA BABA YANGU. WALA SIJAMUUWA BABIA, KAFA KIFO CHA KAWAIDA KUTOKANA NA MAPENZI YAKE MUNGU. NILIVYO HAPA MWENYEWE NASHINDWA KABISA KUAMINI …

 

L.W.L


PICHA YA JB MPIANA AKIWA INCHINI AMERICA

October 11, 2014

10348390_673161909447886_2761523108126892526_npia3

 

PAPA CHERI MOTO PAMBA TOKEA MAJUZI YUKO INCHINI AMERICA,

KAENDA KUUNGANA NA FAMILIA YAKE WALIO MTANGULIA HUKO, KWA AJILI YAKUFWATILIA MIPANGILIO YA CHUO KIKUU ALICHO UNGANA NACHO BINTIE DAIDA MPIANA.

JB MPIANA KIMUONEKANO KWENYE PICHA ANAPUNGUA, YASEMEKANA ANAJIWEKA SAFI KWA MAZOEZI ILI AWE FITI KABISA WAKATI WAKUTOLEWA KWA ALBUM “BALLE DE MATCH” MWISHONI MWA MWAKA HUU.

L.W.L


SIKILIZENI UMAHIRI WA UIMBAJI WA VIJANA WA WENGE BCBG ( JB MPIANA ) SAFI SANA

October 11, 2014

 

VIDEO SAFI, SAUTI NZURI  ISIOKUA NASHAKA, KWA KWELI ALBUM ” BALLE DE MATCH ” NATABIRI ITAKUA JUU NA ITAPENDWA NA WENGI

VIJANA WA WENGE BCBG WAKIONGOZWA NA YAYA ZULEMA,  ATSHUDA  (DIEGO MILITO), HUGO BOSS, KWENYE GITA  YUKO FRENCHIE KEMBE.

SIKILIZENI WENYEWE UIMBAJI WA ” YAYA ZULEMA STRANGALEY “, ANZIA KWENYE DAKIKA 2:37 : MTAMSIKIA AKIPAA ( YE YE YE YEEEE, MA BOUCHE NE CESSE DE RÉPÉTER CE MOT JE T’AIME SOUVE / KAMWE MDOMO WANGU HAUTOCHOKA KUNENA NENO NAKUPENDA SOUVE ( JB MPIANA ).

MES YEUX RÉCLAMENT TA BEAUTÉ JAMAIS IRRESISTIBLE / MACHO YANGU YAHITAJI KUONA UZURI WAKO USINAKIFANI

SOLO NAYO YA NZOTO EKOMA ATA PARFUM PRÉFÉRÉ NANGAI : HARUFU YAKO YA MWILINI ITOKEE KUA MARASHI YANGU NIIPENDAYO …

JAMANI KAZI KWENU

 

L.W.L

 

 


KOFFI OLOMIDE KAMPOKEA KISI NDJORA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUTOLEWA JELA LEO

October 10, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO YA KISI NDJORA AKIWA NYUMBANI KWA KOFFI OLOMIDE.

HATIMAE KISI NDJORA YUU HURU BAADA YAKUPEWA MSAADA KUTOKA KWA MAWAKILI WA KOFFI OLOMIDE.

JB MPIANA NDIE ALIEKUA WAKWANZA KUMFUNGULIA MASHITAKA KISI NDJORA KWAKOSA LA KUMPAKAZIA MAMBO YASIOKUA NA UKWELI WOWOTE, BAADA YA KUTAFAKARI, JB MPIANA KUPITIA MAWAKILI WAKE, KAIOMBA MAHAKAMA JIJINI KINSHASA IMFUTIE KISI NDJORA KESI.

WAKATI AKIACHIWA HURU KUTOKANA NA KESI YA JB MPIANA, FALLY IPUPA KWAUPANDE WAKE, KAJA PIA KUMFUNGULIA MASHITAKA KISI NDJORA,KASHUTUMIWA KOSA LA KUMTUKANA , KUMTISHIA MAISHA FALLY IPUPA…

IZINGATIWE YAKWAMBA KATIKA MZOZO ULIOKO KATI YA JB MPIANA NA KOFFI OLOMIDE, KISI NDJORA YEYE NI MPAMBE NAMBA MOJA WA KOFFI OLOMIDE, KWAKUTAKA KUMUUMIZA ZAIDI JB MPIANA, KAMTUPIA KHASHFA MBAYA KWAKUSEMA, ALIMUHARIBU MMOJA KATI YA WANENGUAJI WAKE NA KUMPA MIMBA , BINTI ANAEJULIKANA KWA JINA LA ” MWANATSUKA ” AMBAE KIUMRI BADO MDOGO CHINI YA MIAKA 16.

INGAWA KISI NDJORA ANAO MUONEKANO WAKIUME, BALI NI MWANAMKE NA ANAISHI NA MWANAUME, ANA WATOTO HADI WAJUKUU!!!

KISI NDJORA ( CHRISTINE ) NI DADA WA MAREHEMU BABIA NDONGA CHOKORO ALIE FARIKI JUZI JIJINI LUANDA ( ANGOLA ).

 

L.W.L

 


KOFFI OLOMIDE ( MUTSHIRIBARA ) / CLAUDIA BAKISA NA AWILO LONGOMBA ( MUTSHIRIBARA )

October 10, 2014

HAPO JUU VIDEO YA WIMBO MUTIRIBARA ( UTUNZI WA CLAUDIA BAKISA AKISAIDIWA NA AWILO LONGOMBA )

 

  MUTSHIRIBARA KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO

 

Takriban Wiki Mbili zilizopita KOFFI OLOMIDE QUADRA-KORAMAN katoa Wimbo ” MUTSHIRIBARA ” ambao unatamba vibaya sana Kwenye Hit Parade Mbalimbali, hata kwenye YOUTUBE Umetizamwa na zaidi ya Watu Laki Mbili.

Jana Mwana Dada ” CLAUDIA BAKISA ” akisaidiwa na Mkongwe ” AWILO LONGOMBA ” Wanatoa kibao ” MUTSHIRIBARA “.

Huku Kwenye Nyimbo zote hizo Mbili, wanarudilia Refrain ( Mutshiribara laisse moi danser mutshiribara ) Mutshiribara yes yes Mutshiribara .

Nategea Mtaburudika na NYimbo zote Mbili, Ila Mimi kaupendeleo kangu kwa MOPAO, kanirudisha Nyuma kidogo na RAPA za zamani zilizo pendwa ( PUSA MAMA PUSA, OYO BABELELAKA SAMBELA, SITUTALA SITUTALA MAMA…) .

 

L.W.L


MPYA HIYO YA WERRASON NGIAMA MAKANDA WIMBO ” BLOCK CADENAS ” AUDIO

October 9, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UPATE KUSIKILIZA  GENERIC MPYA YA WERRASON

 

KAMA KAWAIDA YETU TUNAWALETEA GENERIC MPYA HIYO YA WERRASON, ” BLOCK CADENA ”

UNAWEZA UKAUNUNUA KWENYE ITUNE KWA BEI ISIOZIDI DOLA 1

KACHANGANYA VYOMBO KIAINA !!!

BURUDIKENI.

 

L.W.L

 

 


TUMKUMBUKE ” BABIA NDONGA CHOKORO ” TAFSIRI YA WIMBO ” AMEN “

October 9, 2014

 

MSANII MWANAMUZIKI BABIA NDONGA KAFARIKI JANA TAREHE 08-10-2014 JIJINI LUANDA ( ANGOLA )

TUNAWALETEA TAFSIRI YA WIMBO WAKE ” AMEN ” UNAO PATIKANA KWENYE ALBUM ” MAGIE ”

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA !!! AMINA


Ameeeeeeeeeeeen
Notre Père qui est aux cieux, yo moko oza mona, mapamboli tozwa / BABA YETU ALIE MBINGUNI,MWENYEWE WAONA BARAKA ZAKO ZIMETUFIKIA
Quartier Latin anti dopage / QUARTIER LATIN NI KIKOSI KINACHO PAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA!!!

Nzambe ozomona, Le Chokoro babia Ndonga azwa mapamboli!! MUNGU MWENYEWE KAYAONA, BABIA NDONGA KABARIKIWA

Papa na ngai motu ya pasi, mama aboti ngai nde mobola,/ BABA YANGU NI KABWELA ASIE NAKITU, MAMA YANGU MZAZI PIA NI MASKINI

Motema etonda posa ya kokabela mozangi, okokaba nini eee,/ MOYO WANGU WAJAWA NA NIA YAKUWASAIDIA MASKINI, SASA NTAWASAIDIAJE ILHALI MWENYEWE SINA UWEZO!!!

Nzambe na sengi se na yo ooo, bomengo oo bwanya mayele eeee, ooo bwanya aaaa. / NTAKACHO KUOMBA MUNGU WANGU UNIJAALIE  KIPATO, BUSARA NA HEKIMA

Ngai papa na ngai motu ya pasi, mama aboti ngai nde mobola,/ BABA YANGU NI KABWELA ASIE NAKITU, MAMA YANGU MZAZI KADHALIKA NI MASKINI

Motema etonda posa ya kokabela mozangi, okokaba nini eee,/ MOYO WANGU WAJAWA NA NIA YAKUWASAIDIA MASKINI,NTAWASAIDIAJE ILHALI MWENYEWE SINA UWEZO!!!

Nzambe na sengi se na yo ooo, bomengo oo bwanya mayele eeee, bwanya aaaa. / NTAKACHO KUOMBA MUNGU WANGU JAALIA NIPATE KIPATO, BUSARA NA HEKIMA

Bomengo po nini eee nalelaka na Nzambe ee/ UTAJIRI KWANI KITU GANIII, HUA NAMLILIA BABA MUNGU WANGU

Eli Eli lama saba tani, lokola Yesu na ngomba ya golgota eee Nzambe po nini yo otiki nga eee / ELIA ELIA LAMA SABACHTHAMI, KAMA KILIO CHA YESU AKIWA KWENYE MLIMA WA GOLGOTHA!!!

Bomengo po nini eee nalelaka na Nzambe ee /UTAJIRI KWANI KITU GANI, HUA NAPELEKA KILIO CHANGU KWA BABA MUNGU.

Eli Eli lama saba tani, lokola Yesu na ngomba ya golgota eee Nzambe po nini yo otiki nga eee /ELIA ELIA LAMA SABACHTHAMI, KAMA KILIO CHA YESU AKIWA KWENYE MLIMA WA GOLGOTHA!!! MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA!!!

Bomengo po nini ee na tunaka aa na maman, / UTAJIRI KITU GANI !!! LIPO SWALI HUA NAPENDELEA MAMA YANGU ANIJIBU.

Est ce que babota nga po na niokamaka, aaa ngai nalembi bo pauvreté eee / KWANI MMENILETA HAPA DUNIANI ILINIJE KUTESEKA ? NACHOSHWA  SANA NAUMASKINI

Bomengo po nini ee na tunaka aa na maman,/ UTAJIRI KITU GANI !!! LIPO SWALI HUA NAPENDELEA MAMA YANGU ANIJIBU.

Est ce que babota nga po na niokamaka, aaa ngai nalembi bo pauvreté eee / KWANI MMENILETA HAPA DUNIANI ILINIJE KUTESEKA ? NACHOSHWA  SANA NAUMASKINI

Bomego po nini ee okoma koleka ngai na mosika,/ UTAJIRI KWANI KUNANINI, PESA NAZIONA KWAUMBALI

Na sala yo na nini ee nzoka nayebi que mobola pe azwaka, po nini ngai te eeee / MBONA SIJUI KIPI KIBAYA NILICHO KUTENDEA, INGAWA BADO NAKAA NIKIWA NA IMANI KWAMBA, IPO SIKU YULE AMBAE NI MASKINI HUTOKEA KUA TAJIRI, MBONA KWANGU MIMI BADO !!!
Bomego po nini ee okoma koleka ngai na mosika, / UTAJIRI KWANI KUNANINI, PESA NAZIONA KWAUMBALI

Na sala yo nini ee nzoka nayebi que mobola pe azwaka, po na nini ngai te eeeaaaaah / MBONA SIJUI KIPI KIBAYA NILICHO KUTENDEA, INGAWA BADO NINAYO IMANI KWAMBA, IPO SIKU YULE AMBAE NI MASKINI HUTOKEA KUA TAJIRI, MBONA KWANGU MIMI BADO !!!
Bomengo na sala yo nini aaa , naluka yo na ba boulot, na mo mbongo pe na losambo,/ UTAJIRI KWANI KOSA LANGU NINI ?,KAZI NAIFANYA KWA BIDII,  KAMA NI MAOMBI KILA SIKU NATOA MAHITAJI YANGU.

Yeba ba kati ngai maboko te eee mongongo pe ezali ya Nzambe eeee / JUA YAKWAMBA BADO NINAYO MIKONO YANGU ,NA SAUTI YANGU NI ZAWADI KUTOKA KWA BABA MUNGU!!!

Bomengo ozala ata benja, na yemba yo na loyembo,/ UTAJIRI UNGELUKUA BASI WEWE NI BENJA ILI NIPATE FURSA YAKUKUTUNGIA WIMBO

Lokola Wendo ayembaka Marie Louisa, Kiabukuta ayembaka Babi ii, mbambula ya Koffi Acraaaaame eee. / KAMA VILE WENDO KAMTUNGIA WIMBO MARIE LOUISA, KIAMBUKUTA KAIMBA WIMBO BABII, MBAMBULA IKAIMBWA NA KOFFI OLOMIDE ACRAMEEE

Bomengo ozala ata benja, na yemba yo na loyembo,/ UTAJIRI UNGEKUA BASI WEWE NI BENJA NIPATE FURSA YAKUKUTUNGIA WIMBO

lokola Wendo ayemba Marie Louisa, Kiabukuta ayemba Babi ii, mbambula ya Koffi papa toooop eee. / KAMA VILE WENDO KAMTUNGIA WIMBO MARIE LOUISA, KIAMBUKUTA KAIMBA WIMBO BABII, MBAMBULA IKAIMBWA NA KOFFI PAPA TOOOPE

Nsango ya babia bakobelela na monde entier ahaha / HABARI ZA BABIA ITAZAGAA ULIMWENGUNI KOTE!!!
Nzambe yoka kolela oyo ya bana na yo ooo aaah mama aaa / BABA MUNGU SIKIA KILIO CHA WANAO
kotika te Alise baba amona se pasi iii aaah mama aaa / WALA USIMUACHE ALISI BABA KATIKA SHIDA
Yo moko osala biso Nzambe yaka kotala biso aa ah aa / ALIETUUMBA NI WEWE, BASI BABA MUNGU TUTIZAME
Oooo kotika te le vieux Manzekou amona ba pasiii aah mama aa / USIMUACHE MZEE MANZEKOU KWENYE MATATIZO
Ehh Nzambe yoka kolela oyo ya François Baniota aah mama ee / MUNGU BABA SIKILIZA KILIO CHA FRANCOIS BANIOTA
Nzambe yoka ata kolela oyo ya Lebou Kabuya aa mama eee / BABA MUNGU SIKIA BASI KILIO CHA LEBOU KABUYA
Losambo na ngai bakobele na monde entier aa mama aaeee / MAOMBI YANGU YASIKIKE POPOTE PALE DUNIANI
Bomengo atandele, aa maman aaeee (2x) / UTAJIRI IPO SIKU
Tutu Roba mwana londre papa na … Tokotika Izé bola amona se pasi / TUTO ROBA WEWE AMBAE NI MTOTO WA LONDON, BABA YAKE YA …USIMTUPILIE IZE BOLA NAKUMUACHA ATESEKE
Yo moko osala biso Nzambe yaka kotala biso aa ah aa / ALIETUUMBA NI WEWE, BASI BABA MUNGU TUTIZAME
Kotika te quartier latin bazanga.. / USIIACHE QUARTIER LATIN WAWE KATIKA HALI YA UKOSEFU
Eeee Nzambe yoka kolela oyo ya papa na Rocky iii /  EH MOLA SIKILIZA KILIO CHA  BABA ROCKY !!!
Nzambe yoka kolela oyo ya bana babola eeeehh / BABA MUNGU SIKIA KILIO CHA WANAO WALIO MASKINI
Losambo na ngai nakobelela na monde entier eee /  MAOMBI YANGU YASIKIKE POPOTE PALE DUNIANI
Bomengo atandele, aa maman aaeee (2x) / UTAJIRI IPO SIKU !!! MAMA AAEE !!!

 

L.W.L


HABARI YA MASIKITIKO KWA WAPENZI WA MUZIKI WA RUMBA, MSANII ” BABIA NDONGA CHOKORO ” KAFARIKI DUNIA

October 8, 2014

 

 

Nimeambatanisha na Post hii WIMBO WAKE ” AMEN ” ambao ndio utunzi wake wa Kwanza akiwa na KOFFI OLOMIDE kwenye ALBUM MAGIE.

Taarifa tulizo zipokea tokea Usiku wa kuamkia leo Tarehe 08-10-2014, Bado tulikua tukiifanyia kazi kabla yakuiweka kiwanjani, zaashiria kwamba Msanii Mwanamuziki wa Zamani wa Group Quartier Latin International BABIA NDONGA CHOKORO  kafariki Dunia JIJINI LUANDA ( ANGOLA ),kutokana na MUSHTUKO WA MOYO.

Wengi Wanaambatanisha Kifo chake na kitendo cha JB MPIANA , FALLY IPUPA, FELIX WAZEKWA, kumfungulia mashitaka DADA YAKE CHRISTINE maarufu kwa jina la ” VIEUX KISI NDJORA ” ambae tokea Jana yuko kizimbani kwenye Jela kuu JIJINI KINSHASA ya MAKALA.

Kwa utafiti wetu, yaonyeshakua, BABIA NDONGA, Tayari kawa na Matatizo ya Kifamilia, maelewano yalikua simazuri katiyake na Mkewe.

Usiku wa Kifo chake, Walitokea kua namabishano makali sana yakindoa, yalio sababisha BABIA NDONGA kudondoka  chini na kupoteza ufahamu,.

Wakampeleka kwa Haraka kwenye Hospitali Kuu ya PREDA JIJINI LUANDA ambako umauti ukamkuta.

BABIA NDONGA CHOKORO kajiunga na Group Quartier Latin ya KOFFI OLOMIDE tokea Mwaka 1993, Album yake ya kwanza aliochangia ni ” MAGIE ” Iliotolewa Mwaka 1994.

BABIA NDONGA Kajiondoa kwenye Group hilo Mwaka 2001, Kisha baadae akaja tena kujiunga kwa Mara Nyingine tena na Quartier Latin Mwaka 2003 .

Mwaka 2011, kaamua kujiondoa  Moja kwa Moja kwenye Orchestra Quartier Latin ya KOFFI OLOMIDE na kaanza kujitegemea Mwenyewe Kimuziki.

Baada yakujiengua kwenye Group Quartier Latin, BABIA NDONGA CHOKORO kahamia INCHINI ANGOLA JIJINI LUANDA ambako kaweka Maskani yake.

BABIA NDONGA alikua kwenye Matayarisho ya Album yake ” VRAI MOMENT ” Kutokana na Ukosefu wa Producer wa Uhakika, Ilimjia vigumu kabisa kwa  Album hiyo kutolewa.

Salamu zetu za Rambi rambi ziwaendee Familia yake, Tulimpenda sana ila Mwenyezi Mungu kampenda zaidi.

 

 

L.W.L


VIDEO YA WERRASON KAWASILI JIJINI PARIS LEO

October 7, 2014

 

TIZAMA VIDEO YA WERRASON AKIPOKELEWA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA CHARLES DE GAULE JIJINI PARIS,AKITOKEA MAREKANI.

KAMA TULIVYO WATAARIFU SIKU ZILIZO PITA, WERRASON ANATARAJIA KUONDOKA JIJINI PARIS JUMAMOSI IJAYO AKIELEKEA KINSHASA AMBAKO ANASUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA WAPENZI WAKE.

KWAUKUMBUSHO, WERRASON LE ROI DE LA FORET KAPEWA TUZO MBILI KWENYE SHINDANO LA NAFCA Mjini ((Beverly Hills California). Tarehe 13-09-2014. ( MSANII BORA WA AFRICA,  GENERIC MALEWA IKAPEWA TUZO LA GENERIC  BORA ).

 

L.W.L


FERRE GOLA / MTU SI MANENO BALI VITENDO ( NYUMBA YAKE YAONYESHWA KWENYE VIDEO )

October 7, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO YA FERRE GOLA AKIWA NYUMBANI KWAKE

 

Kwenye Video hii FERRE GOLA kafanya mahojiano na Mtangazaji International LUMBU BAWU akiwa Nyumbani kwake JIJINI KINSHASA,

FERRE GOLA kajibu maswali Mengi yakiwemo :

1. Unalionaje hilo Swala la Mtu kukuchukulia Wanamuziki wako ?  / FERRE GOLA : Unacho takiwa kuelewa ni kwamba Baadhi ya Wanamuziki wingi ambao walichangia kwenye Album ” BOITE NOIRE ” bado wapo kwenye Group. Wale walioondoka Mchango wao kwenye ” BOITE NOIRE ” ulikua Mdogo sana.Kwenye Group langu kwanza ni Mimi, hakuna atakae niyumbisha, Nyimbo nyingi hua nazitayarisha nikiwa Ulaya, nakuja nazo KINSHASA, nawagea ” Vocal “. Sehemu nyingi nachangia mwenyewe. Mimi ndo nawasikitikia hao, naona hawaja tafakari vizuri vipi yatakavyo kua Maisha yao ya Baadae, wala siwatakie Ubaya wowote, Nawaombea Kwa Mungu awafariji Mambo yao yawe mazuri..

2. Tuambie FERRE GOLA ni hasa kilicho wapelekea Vijana hao kuondoka kwenye Group ? nawataja hasa  CHIKITO na NICODEM.  / FERRE GOLA : Mbona kabla yao wapo wengi walio jiondoa?  akina VIBRATION, SESELE,na wengine wengi, kwa taarifa yako Wapo Wengi wanaoondoka na Wanarudi, Wanajua kwamba hapa ni Nyumbani kwao, Mlango upo Wazi kwa wakati wowote ule . kilichokua cha muhimu nikuona Group inaendelea vizuri, Namimi Mwenye niko vizuri kiafya, Hapa si unaona nimewakaribisha Nyumbani kwangu ? Mnaona wenyewe nilivyo .

3. Tufafanulie kuhusu Kijana RICE MATADIEN ambae kajiondoa kwa WERRASON na kaja kujiunga na Group lako . FERRE GOLA / RICE nikijana Mzuri kwamuonekano wake, na pia ni Mwimbaji mzuri, Ni Kijana mwenye heshima kabisa. Kama kawaida, Sisi wenjeji wa Mji wa MATADI hua watulivu na hatuna tabia ya Utovu wa nidhamu.

4. Yasemekana kwamba siku hizi FERRE GOLA kawa Mtu wa Malumbano sana, hunatena heshima kwa Kaka zako kwenye Muziki,kwakua umeshakua mwenye mafaanikio. / FERRE GOLA : Mbona ninao Uhusiano mzuri na Kakazangu wote? FELIX WAZEKWA tunaelewana vizuri, KOFFI OLOMIDE, tupo sawa kabisa naye, Hata Kaka zangu wa WENGE maelewano yako mazuri. Kilicho cha Muhimu hapa ni kwamba kila mmoja anajitegemea kivyake,kila Mtu na Mambo yake, Kila mmoja wetu anakabiliana na Maisha kwa namna yake . Huo Mda wa Malumbano sinao tena. Tusiwachukulie Mashabiki wetu kama Mambumbumbu, hapana , ni Watu na akili zao timamu. kwahiyo Msinitegemee tena kuniona napita kwenye TV na Radio nikiongea Ujinga. Mtu si Maneno bali nivitendo. Muziki nikuelemisha pia Umma!!! Tunaiwakilisha vilivyo Inchi yetu Inje ya Mipaka na Tunakubalika . Tunazunguuka Dunia nzima, JOHANNESBOURG, COTE D’IVOIRE, Unavyo niona hapa nimerudi safarini nikitokea CUBA. KAKA ZANGU  KAMWE WATABAKI KUA KAKA ZANGU, KADHALIKA WADOGO ZANGU PIA. SINA TABIA YA MALUMBANO, MIMI NI MCHAPA KAZI, NA MATUNDA KUTOKANA NA KAZI YANGU YANAONEKANA!!!.

 

L.W.L

 


MALUMBANO KATI YA KOFFI OLOMIDE NA JB MPIANA YAZIDI KUPAMBA MOTO ( WASEMAJI WA KOFFI NA JB MPIANA KIZIMBANI )

October 6, 2014

images

 

PICHANI anaitwa VIEUX KISI NDJORA ( CHRISTINE )

 

 

 

Ingawa Serekali ya Congo yatoa Onyo bilamafaanikio ili Mzozo kati ya JB MPIANA na KOFFI OLOMIDE utafutiwe suluhisho, Pande zote Mbili bado wanaendelea kutupiana Maneno Makali!!!

Siku Mbili zilizo pita, Msemaji  Mkuu wa JB MPIANA ( MOSAKA ) kafikishwa polisi kwa madai kwamba Kamchafua Matusi ya Nguoni KOFFI OLOMIDE,

MOSAKA kasema namnukuu : Kama kawaida tulikua kwenye kipindi cha BCBG NEWS, Baada ya kipindi hicho, Tukiwa tunarudi Nyumbani pamoja na akina ” ROGER NGANDU “, Ulikua tayari Usiku wa Giza, Ndipo Likatolewa pendekeza kwamba Bora tupitie kwenye CLUB  tupate Bia moja Baridi…

Ilipofikia Mida ya Saa tisa unusu za Usiku, Wakaja kujitokeza Mapolisi wawili,na silaha zao mikononi, Wakaniuliza kama Mimi ndie MOSAKA nikakubali Ndio, Wakanionyesha hati ya kukamatwa, Nikawaambia Mbona usiku huu, hakuna Ofisi yeyote ambayo bado iko wazi, Wakanijibu kwamba Walipewa mamlaka yakuniweka chini ya Ulinzi kwa Mda wowote ule, Nikawaambia kwani Mmetumwa na nani? papo hapo Wakapiga simu wakanigea iliniongee, nikajikuta naongea na yuleyule mnae mfahamu ( KOFFI OLOMIDE ). Kaniambia Kijana unatakiwa utulie, Unaona yanayo kukuta ? Sasa jamani, Mimi ni Mpambe tuu wa JB MPIANA PAPA CHERI na kamwe siwezi msaliti, Umeshapewa majina kibao ila hilo nililo kupachika mimi la ” EBOLA ” linazidi mengine yote !!! Nikapelekwa kwanye Kituo cha Polisi, na baada ya Mda Mchache nikaachiwa huru !!!

Habari zilizo tufikia Mda si mrefu, zaashiria kwamba, Mpambe wa KOFFI OLOMIDE ” KISI NDJORA ” kawekwa ndani Jana siku ya Jumapili kwenye mida ya Saa Kumi na moja Jioni, Wamemkuta akiwa kwenye maongezi na Producer wake, Polisi wakaja kumchukua na kwendanae kituoni, ambako kakaa huko hadi kwenye Saa Saba za Usiku, Mawakili wa KOFFI OLOMIDE , Walimsimamia nakumtetea hadi pale alipo achiwa huru.

Leo hii Asbuhi KISI NDJORA ambae ni Mwanamke ingawa anao muonekano wa Mwanaume, Kafikishwa Mahakamani ambako kafunguliwa Mashitaka kwakosa lakutumia Lugha ya MATUSI dhidi ya JB MPIANA,

SWALI LINAKUJA : MZOZO HUU UTAISHIA WAPI ? TUNAENDELEA KUFWATILIA NAKUWALETEA HABARI KADRI INAVYO JITOKEZA…

Pichani hapo Juu Ndie Msemaji wa JB MPIANA MOSAKA

 

L.W.L

 

 


ANZIA JUMATATU YAKO NA SHOO NZURI YA ” FALLY IPUPA NA FLAVOUR NABANIA “

October 6, 2014

 

Tizama video Nzuri ya SHOO ya FALLY IPUPA wakichangia Jukwaa na FLAVOUR NABANIA,

SHOO Hiyo  imefanyika kwenye Shindano la AFRIMAMA INCHINI MAREKANI, ambako wote Wawili wamepewa Tuzo : FALLY IPUPA Best Male Central Africa 2014 , FLAVOUR  Kapewa Tuzo Mbili ( Best Video of the Year 2014, Best Traditional Artist 2014 ) .

BURUDIKENI

 

L.W.L


TUMKUMBUKE DOKTA NICO KASSANDA ” BABA WAWAPIGA SOLO GITA “

October 5, 2014

 

NICO KASANDA WA MIKALAYI Aka DOKTA NICO, kazaliwa Tarehe 07-07-1939 Mjini LULUABOURG leo hii hujulikana kwa jina la KANANGA.

Kafariki Dunia JIJINI BRUSSELS Tarehe 22-09-1985 kwenye Hospitali ya SAINT LUC. Baada ya kuugua kwa Mda mrefu.

DOCKTA NICO KASANDA katokea kwenye Familia ya Wasanii, Baba yake Mzazi akiwa ” accordionist “, Huku Kaka yake Mkubwa anaefahamika kwa jina la ” CHARLES MWAMBA DECHAUD ” akiwa Mpiga GITA mashuhuri.

DOKTA NICO KASANDA kajifunza GITA kutoka kwa Binamu yake ” EMMANUEL TSHILUMBA WA BALOJI Aka TINO BAROZA ” Mmoja wawapiga GITA Mahiri sana kwenye Historia INCHINI  CONGO.

DOKTA NICO KASANDA,Msanii ambae ni Mkali kwa GITA kawa kishawishi kikubwa kwakizazi kizima cha Wapiga GITA Inchini CONGO,Tutawataja : GUVANO, ATHEL, DIZZY MANDJEKU, MAVATIKU, PEPE FELLY MANUAKU, ROXY TSHIMPAKA…

Tukiachia Mbali Inchi ya CONGO, Ushawishiwake kwenye GITA Umevuka mipaka hadi kwenye Baadhi za Inchi za Africa wanamkubali, kama alivyodai Mpiga GITA kutoka Inchi ya GUINEA ” SEKOU BEMBEYA ” kasema yeye ni mfwasi kamili wa DOKTA NICO KASANDA.

DR NICO KASANDA kakumbatia Fani ya Muziki akiwa bado Mdogo wa Umri wa miaka 14, Kaka yake DECHAUD ndo kamleta kwenye Group ” AFRICAN JAZZ ” nakumuunganisha na NYOTA wa Muziki wa Congo ambae si Mwengine bali ni ” JOSEPH KABASELE GRAND KALLE “.

Kabla yakuchagua kazi ya  Muziki, DOKTA NICO KASANDA alikua Fundi mekanica JIJINI KINSHASA kwenye Kiwanda kinachotengeneza Mafuta yakupikia. na wakati alipoamua kujiunga rasmi na Muziki, kaanza kwenye sekta ya Uimbaji, Basi ikaja kutokea siku Moja Binamu yake ambae ndie Fundi wake Mkuu wa Gita ” TINO BAROZA ” hajatokea mazoezini, Kwakua DOKTA NICO KASANDA tayari  kesha jifunza Gita, Kapewa fursa yakushirikiana na Kaka yake ” DECHAUD “wakati wakiwa kwenye STUDIO ” OPIKA ” Kwenye matayarisho ya Wimbo Maarufu   ” PARAFIFI ” Utunzi wake  ” JOSEPH KABASELE GRAND KALLE .  ” Studio ” OPIKA ” ilikua ikimilikiwa na ” MOUSSA BENATHAR “,

Ndipo kazaliwa Lengend NICO KASANDA. Wapenzi wake humpachika Jina la “mungu wa Gita ” . Kalisakata Gita pasipokua na Mpinzani…

Mwaka 1961, Tofauti ilijitokeza kati ya DOKTA NICO KASANDA na JOSEPH KABASELE LE GRAND KALLE , Kutokuwepo kwa maelewano katiyao, kukapelekea DOKTA NICO KASANDA kuchukua uamuzi wakujiondoa kwenye Group ” AFRICAN JAZZ ”  na kaunda Group lake kalipa jina ” AFRICAN JAZZ aile NICO KASANDA “,

Akiwa Kwenye Group lake, Ndipo kamleta ROCHEREAU TABU LEY ambae alikua Mkalimani kwenye Shule ya ” ATHÉNÉE DE KALINA ” kwaleo hii hujulikana kama ” ATHÉNÉE DE LA GOMBE ” . Wakawa wanafanya  mazoezi kwenye  MTAA WA KIGOMA Manispaa ya KINSHASA .

Baadhi ya Nyimbo nzuri Mfano  ” CHERIE STAROFINA ” , ” AFRICAN JAZZ MOKILI MOBIMBA ” walikua tayari wakizicheza mazoezini. Kwaupande wake JOSEPH KABASELE LE GRAND KALLE bado kaendelea kuwatumia kwenye GITA ” TINO BAROZA na EDO CLARY LUTULA ” .

Mwaka 1962, Baada yakuuwawa Waziri Mkuu na Shujaa wa Uhuru wa CONGO ” PATRICE LUMUMBA “, Baadhi ya Wabunge kutoka Mkoa wa ” STANLAYVILLE ” kwaleo ” KISANGANI “, Tutawataja akina : ( Waheshimiwa KIDISHIO, MBARIKO, BADJOKO ), waliingilia kati ilimzozo kati ya KABASELE JOSEPH GRAND KALLE na DR NICO KASANDA upate kupatiwa suluhisho. Kwa bahati nzuri muafaka ukapatikana , na wakaja kujiunga pamoja kwa mara nyingine tena. Wakafaanikiwa kusafiri JIJINI BRUSSELS kumalizia baadhi ya Nyimbo  kwenye Studio za huko.

Mwaka 1963, Tofauti ya mapato ya Pesa ikajakujitokeza, Kwasafari hii DR NICO KASANDA kajiondoa kabisa nakwenda kuunda ” ORCHESTRA FIESTA ”  akiwa pamoja na ROCHEREAU TABU LEY, ROGER IZEIDI, DECHAUD na MUJOS, Huku JOSEPH KABASELE LE GRAND KALLE akiendelea kusapotiwa na Mpiga Gita Hodari TSHILUMBA WA BALOJI Aka ” TINO BAROZA ”

Tarehe 16-11-1965, GROUP AFRICAN FIESTA ikasambaratika, ROCHEREAU TABU LEY akaunda Group lake  ” AFRICAN FIESTA NATIONAL, huku DR NICO KASANDA akawa Mmiliki wa ” AFRICAN FIESTA SUKISA

Mwaka 1966, DR NICO KASANDA kafaanikiwa kumiliki ” Musical Editions SUKISA ” pia kajitahidi kuliunda kwa upya Group lake ” AFRICAN FIESTA INTERNATIONAL “. Group hili lilikua Juu na kupeta sifa nyingi kwenye Muziki hadi pale ulipofikia Mwaka 1974.

Kwahapa yahitajika vizingatiwe vitu 4 Muhimu :

1. Timu ya waimbaji ilikua ikiongozwa na : APOTRE, VIGNY, MICKY, na MIZELE ,

2. Wanamuziki CHANTAL KAZADI ,na KUTU KABENGELE SANGANA wakaja kujiunga na Group Mwaka 1967. Kujiunga kwao kukapelekea watupwe benchi hao walio tangulia. kwakweli walileta Moto mkali wa aina yake kwenye Group, hasapale walipo onyesha umahiri wao wakuimba kwenye Nyimbo : ” Mbandaka “, ” Yaka Toyambana “, ” La Jolie Bébé “, ” Chantal “, ” Bougie ya motema “, ” Limbisa ngai “, ” Tu m’as déçu “, ” Marie Nella “, ” Je m’en fous “,” Saouda “…

3. Mwaka 1969, CHANTAL KAZADI na SANGANA wakajiondoa nakwenda kuunda  Group lao ” AFRICA SOUL ”

Ndipo pale walipoletwa kwenye Group AFRICAN FIESTA SUKISA Waimbaji ” LESSA LASSAN ” na ” KIAMBUKUTA JOSKY “, ambae kaja kuonyesha Umahiri wake wauimbaji kwenye Wimbo ” BOLINGO EZALI MPE NA KISI ” , na ulipo fikia Mwaka 1970 kaimba ” BOLINGO YA SENS UNIQUE ” kachaguliwa kama Mwimbaji Kinara wa Group hilo.

Mwaka 1972, KIAMBUKUTA JOSKY kajiondoa kwenye Group AFRICAN FIESTA INTERNATIONAL nakwenda kujiunga na Group ” CONTINENTAL “. kamuacha Dr NICO KASANDA katika Shida sana yakimpangilio kadhalika pia  kipesa.

4. NICO KASANDA kajikuta yuko hoi, akiwa kwenye hali ngumu sana kimaisha, Ingawa kaja kusapotiwa na Mama Mwimbaji LUCIE EYENGA alie jiunga na  Group AFRICAN FIESTA SUKISA , Mchango huo  wala haujasaidia chochote.

Afya ya Dokta NICO KASANDA ikaendelea kuzorota, Serekali ya Rais MOBUTU akitoa Msaada iliapelekwe JIJINI BRUSSELS kwamatibabu zaidi, Ndipo Kifo kikamkuta DOKTA NICO KASANDA akiwa na Umri wa Miaka 49.

DOKTA NICO KASANDA KAWEKA ALAMA KUU KWA ZAMA ZAKE KUHUSU UPIGAJI WA GITA,

KAMWE ATABAKIKUA MMOJA WA NEMBO WA MUZIKI WA CONGO…

 

L.W.L

 

 


INAKUJA HIYO YA WERRASON ( BLOCK CADENA )

October 5, 2014

 

BONYEZA KICHWA CHA HABARI UTIZAME SPOTI YA MATANGAZO

HUKU SHAMRASHAMRA YA MAPOKEZI MAKUBWA YAKIENDELEA KUUANDILIWA JIJINI KINSHASA KWA AJILI YA WERRASON NGIAMA MAKANDA, KAMA INAVYO TARAJIWA ATAWASILI JIJINI HUMO SIKU YA ALHAMISI TAREHE 09-10-2014, AKITOKEA INCHINI MAREKANI AMBAKO KAFAANIKIWA KUPEWA TUZO MBLILI ZA NAFCA. ( MSANII BORA WA AFRICA na GENERIC MALEWA KUTEULIWA KUA BORA ).

HIVI KARIBUNI, KABLA YAKUTOLEWA RASMI ALBUM ” FLECHE INGETA “, WERRASON NGIAMA ATATUPIA SOKONI WIMBO ( BLOCK CADENA ). AKIMAANISHA KAJA KUWAFUMBA WA NIGERIA MIDOMO, KUONYESHA KWAMBA MUZIKI WA CONGO BADO UPO JUU!!!

 

L.W.L


MFAHAMU SERGE CAPPUCCINO KIJANA ALIEJIONDOA WENGE MUSICA MM ( WERRASON )

October 4, 2014

 

Bofya kichwa cha habari upate kutizama Video safi ya mazoezi ya CAPPUCCINO

SERGE MUKANDILA MULONGODI  MAYI, Aka CAPPUCCINO LE BEAUGARS  , Ni kijana Mwimbaji pia Mtunzi wa Nyimbo.
Kajiunga na WENGE MUSICA MAISON MÈRE tokea Mwaka 2004, wakati ilipotolewa Album ” ALERTE GÉNÉRALE “.
Mwaka 2008, kapewa fursa yakuweka Wimbo wake ” POINT CARRE ” Kwenye Album ” TEMPS PRÉSENT “. Ndipo kipaji chake cha Uimbaji hasa cha Utunzi kilidhihirika zaidi.
Mwaka 2011, SERGE CAPPUCCINO, Katoa kibao ” MUKUTA ” kinachopatikana kwenye Album ” TECHNO MALEWA SUITE ET FIN ” . Wimbo huo ulikua kati ya Nyimbo 10 bora zilizo pendwa kwenye Hit Parade Inchini Congo, Ingawa palikua na Upungufu wa Matangazo.
Mwaka 2013, SERGE CAPPUCCINO Ambae ni mwenyeji wa MJI WA GOMA ulioko Mashariki mwa CONGO, kaamua kujitegemea mwenyewe, paletuu alivyo jiondoa  kwenye Group WENGE MUSICA WENGE MERE.
Baada ya Takriban Miaka 3 akiwa Jijini PARIS, ambako kafaanikiwa kuingia STUDIO na kutengeneza Album yake  ” DOUBLE FACE ” Nyimbo zake  ” SYLLA na CILIA FANTASTIC” zimepokelewa vizuri sana na wachambuzi wa Muziki Inchini CONGO.
SERGE CAPPUCCINO kateremka JIJINI KINSHASA akitokea PARIS, Kwenye Video mtamuona akijifua vilivyo na Vijana wake… Tunamtakia kila lakheri na mafaanikio katika kazi yake .

L.W.L

 

 

 

 


%d bloggers like this: