Adebayor ajiunga Real lMadrid kwa mkopo

January 27, 2011

Mshambuliaji wa Manchester City Emmanuel Adebayor amejiunga kwa mkopo na klabu ya Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu. Emmanuel Adebayor Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa yaTogo, anatazamiwa kuelekea Hispania siku ya Jumatano kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika klabu hiyo. Madrid watakuwa na uchaguzi kama watahitaji kumnunua moja kwa moja Adebayor mwenye umri wa miaka 26 mwishoni mwa msimu, wakati mkataba wake wa mkopo utakapomalizika. Adebayor alijiunga na Manchester City akitokea Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 25 mwaka 2009 na ameshafunga mabao 19 katika michezo 36 ya ligi na mashindano mengine katika Manchester City. Anakuwa mshambuliaji wa pili mwandamizi wa Manchester City kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi cha miezi sita, baada ya Robinho kwenda AC Milan na anaonekana atamsaidia meneja wa Real, Jose Mourinho kuziba pengo la mshambuliaji Gonzalo Higuain, anayesumbuliwa na matatizo ya mgongo. Kabla ya kumtupia jicho Adebayor, Real ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa Hamburg, Ruud van Nistelrooy, huku dau lao la paundi milioni 39 likikataliwa kwa kutaka kumchukua mpachika mabao wa Atletico Madrid, anayechezea pia timu ya taifa ya Argentina, Sergio Aguero. Adebayor ataweza kucheza mashindano ya Ligi ya Ubingwa wa Ulaya na pia ligi ya Hispania, maarufu La Liga, Reala Madrid wakiwa wanashikilia nafasi ya pili, na iwapo mambo yake yatakwenda vizuri huko Bernabeu, anaweza kusaini mkataba wa kudumu kwa dau la uvumi la paundi karibu milioni 15.


Kitenge dress with 3 Zips Now available

January 19, 2011

image


Vitu ungependa kujua kuhusu Yvone Cherry “Monalisa”

January 18, 2011

Wengi wanamjua kama Monalisa lakini jina kamili anaitwa yvone Cherry, ni mmoja wa waigizaji wa mwanzo kwenye michezo ya TV na Ulimwengu wa Bongo Movie ambaye alijizolea umaarufu sana. Mwanadada huyu alipita safari ndefu mpaka alipo leo hii akiwa ameshaonekana kwenye movie kadhaa, matangazo ya biashara na hata michezo ya kwenye majukwaa kama data zinavyoonyesha hapo chini.

 • FILMS
  BLACK SUNDAY ZIFF AWARD BEST ACTRESS FROM TANZANIA
  PAYBACK
  NIMEOKOKA
  CELLULAR
  WRONG NUMBER
  KABURI 1 Directed by YVONNE CHERRYL
  BINTI NUSA Directed by YVONNE CHERRYL
  WHERE IS GOD DIrected by YVONNE CHERRYL
  CHANZO NI MAMA Directed by YVONNE CHERRYL
  WEDDING PRESSURE
  KWA HESHIMA YA PENZI
  JERAHA LA NDOA
  BEHIND THE SCENE
  WHO IS SMATTER
  SHE IS MY SISTER
  DILEMMA
  SABRINA
  GIRLFRIEND
 • Hapa Monalisa (Pili shoto) akiwa na waigizaji wengine maarufu, nyuma yake ni Mzee Chilo. 
 •  
 • STAGE PLAYSA MAN OF THE PEOLE-KENYA NATIONAL THEATRE(NAIROBI KENYA)
  KIU-KENYA NATIONAL THEATRE (NAIROBI KENYA)
  DONT DRESS FOR DINNER-RUSSIAN CULTURAL CENTRE(TZ)
  THE SONG OF LAWINO-LITTLE THEATRE(TZ)
  ZAWADI YA USHINDI-ZIFF(ZANZIBAR)
  THE GOVERNMENT INSPECTOR-BAGAMOYO ART FESTIVAL

  COMMERCIALS

  HEINEKEN-2001
  ASSAS DIARY MILK-2002
  COMFY-2010

  AWARDS
  ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL-BEST TANZANIA ACTRESS 2010 for BLACK SUNDAY
  KIU NEWSPAPER-QUEEN OF BONGO FILMS-2008


“Wapenzi wangu naweni mikono, chakula tayari” Solo Thang

January 17, 2011

Travellah Kazini

Mwanamuziki Msafiri kondo aka Solo Thang aka Travellah aka Msafiri amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani albamu yake itakuwa tayari hivi kkaribuni.

Solo Thang aliyasema hayo alipooongea nami leo hii kuhusiana na albamu yake ya Traveller ambayo iko kwenye hatua za mwisho za umaliziaji.

Aidha Solo amesema kuwa Albam hiyo yenye nyimbo 14 itakuwa sokoni kuanzia February.

Travellah Mwenyewe

Solothang alisema kuwa ameshirikisha wanamuziki kadhaa kwenye Albamu yake hiyo ikiwa ni mchanganyiko wa vichwa vya zamani kama Chidy, Jay Moe na Mfalme wa Wasukuma Fid Q, ” Kuna kazi nimefanya na CHIDY inaitwa VIINIMACHO..kuna nyingine na FID..Inaitwa AIRBUSS na moja nimefanya na JAYMOE inaitwa Family” alisema Solo Thang.

Nyimbo zote hizi  zitakua kwenye album…Video moja nimefanya ..nyimbo inaitwa ALL I NEED,ndio nipo kwenye mipango ya kufanya nyingi zaidi..nadhani baada ya mwezi nitakua na Video mpya hewani na album itakua inapatikana Online” Aliongeza Solo Thang.

Msafiri Kondo aka Traveller aka Msafiri aka Solo Thang ni mmoja wa wanamuziki ambao walijizolea umaarufu sana enzi za mwanzo za muziki wa Bongo Flava na pia ni kati ya wanamuziki wachache wa kizazi kipya mwenye elimu ya kutosha akiwa na Diploma ya Diplomasia toka Chuo cha Diplomasia na Kisha kuendelea na Degree nchini Uingereza na pia ameshasoma kozi mbalimbali.


Arts Journalism Training opportunities at Sauti za Busara 2011

January 17, 2011
If you are a print, radio, internet, TV or photo-journalist from East Africa, please note there is a limited number of vacancies for arts journalism training at Sauti za Busara 2011 next month in Zanzibar

All applications must be sent by Friday 21 January 2011. Send applications to brickhill.paul.zim@gmail.com

“The workshop training and arts journalism collaboration,” organisers say “will be conducted with experienced media professionals. The goal is to upgrade standards of African arts reporting in all media, with depth and analysis through critical feature writing and production. The activities will be geared to creative media production in a real working environment against the backdrop of an exciting arts festival – it will be intensive, packed, and demanding.”

More info at:

www.compassnewspaper.com/NG/index.php?option=com_content&view=article&id=73367:intl-bodies-fund-african-art-groups-train-journalists&catid=54:arts&Itemid=694

Yusuf Mahmoud, Director
+255 777 428 478 (mobile)

Busara Promotions, PO Box 3635, Zanzibar, Tanzania

Tel: +255 24 223 2423 or +255 773 822 294

director@busara.or.tz, www.busaramusic.org

Looking forwards >>> 8th Sauti za Busara music festival, 9 – 13 February 2011

Powered by Norwegian Embassy, Zantel, HIVOS, Goethe Institut, US Embassy, ACP Music Festivals Network, Culturesfrance, Memories of Zanzibar, Gallery Tours, Zanzibar Grand Palace Hotel, Grand Malt, British Council, ZG Films, Zanlink, SMOLE II


Dalglish hajapanga kusajili wachezaji

January 17, 2011

Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish bado hajazungumza na wamiliki wa klabu juu ya usajili wa wachezaji wapya wakati huu wa msimu wa dirisha dogo la usajili mwezi wa Januari.

Kenny DalglishKenny Dalglish

 

Liverpool ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, walitoka sare ya mabao 2-2 na watani wao wa jadi Everton siku ya Jumapili.

Lakini zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa, Dalglish amesema: “Hakuna kilichojadiliwa kuhusiana na wachezaji wapya au jambo jingine.

Dalglish ambaye tangu achukue hatamu za uongozi wa klabu ya Liverpool, hajashinda mchezo hata mmoja- alianza kuchambua kikosi chake alichorithi kutoka kwa mtangulizi wake, Roy Hodgson, na anahisi baadhi ya wachezaji wanapaswa kupewa nafasi ya pili kuonesha uwezo wao.

Hodgson alishindwa kuifikisha Liverpool panapotakiwa na aliwasajili Paul Konchesky na Christian Poulsen, ambao wameshindwa kujiimarisha na kuonekana ni wa kutumainiwa katika kikosi cha kwanza.


Manchester United kileleni tena

January 17, 2011

Manchester United iliendelea na rekodi yake nzuri ya kutoshindwa katika mechi yoyote msimu huu, baada ya kucheza jumla ya mechi 21, na vile vile kufanikiwa kurudi kileleni katika ligi kuu ya Premier ya England.

Hii ni baada ya kutofungana na Tottenham.

David Beckham alikuwa katika uwanja wa White Hart Lane, akitizama timu ya Tottenham, anayotazamia kuichezea, lakini licha ya yote yale aliyoyaona uwanjani, timu hiyo haikuweza kufunga bao.

Man U ililazimika kucheza dakika 16 za mwisho pasipo mchezaji wao maarufu kutoka Brazil, Rafael, ambaye mwamuzi alimtolea kadi ya pili ya manjano, kwa kumchezea vibaya Benoit Assou-Ekotto.

Hata hivyo Spurs (Tottenham) walishindwa kuitisha Manchester United, licha ya kucheza wakiwa uwanja wa nyumbani.

Mshambulizi Wayne Rooney bado hajafikia hali yake ya ubora kikamilifu, lakini mara mbili aliweza kuitisha Spurs, na kumfanyisha kazi ngumu mlinda lango Heurelho Gomes mapema katika kipindi cha pili.

Spurs pia walipata nafasi za kufunga mabao kupitia Peter Crouch na Rafael van der Vaart lakini hawakufua dafu.

Hata hivyo meneja wa Man U Sir Alex Ferguson ataridhika kwamba walitoka katika uwanja wa kati ya maadui wao wakubwa zaidi pasipo madhara.

Manchester United inawatangulia wapinzani wao wakubwa zaidi, majirani Manchester City, kutokana na wingi wa magoli, na muhimu zaidi, wakiwa na mechi mbili za akiba, na ambazo wanatumaini kuzitumia vyema na hatimaye kuandikisha ubingwa wao wa ligi ya Premier wa 19.


%d bloggers like this: