Mwanamziki mkongwe HAMISI KITAMBI amefariki dunia

February 26, 2010

cid:BC52857B-A7FC-4972-80CA-945541E1BD19/GetAttachment.jpg
Mwanamziki mkongwe wa dansi Bw.Hamisi Kitambi,amefariki dunia siku Ijumaa alfajiri ya tarehe 26/02/2010
katika Hospatali ya Muhimbili.
Marehemu aliwahi kupigia bendi za Msondo Ngoma ,kabla ya kupata maumivu ya mguu yaliotokana katika hajali alipokuwa safarini na bendi ya msondo ngoma .

marehemu pia alikuwa mwanamziki nyota enzi za Tabora jazz,ambako alipigia bendi ya Tabora kabla ya kuhamia
Juwata Jazz sasa Msondo Music band.
Kwa taarifa zaidi tafadhali mnaweza kuwasiliana kwa simu na familia ya marehemu kwa simu namba 0713 802370 Almasi Kassanga.
au Bi.Mwamini Kitambi simu namba 0712 217740

Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi
Amin


Zaiko Langa Langa, Kundi la Muziki tangu mwaka 1970

February 26, 2010

image

Huwezi kuzungumzia Congo pia bila kuwataja Zaiko Langa Langa chini yake Nyoka Longo.

Zaiko wamekuwa maarufu na kuendeleza umaarufu wao tangu kuanzishwa kwake miaka ya sabini huko wakati huo Congo ikiitwa Zaire. Kwa mtu asiyejua na kwa we msomaji kwa taarifa yako watu kama Papa Wemba, Bozi Boziana, Dindo Yogo, Evolocko Jocker na Nyoka Longo wote ni kizazi cha Zaiko Langalanga.

Kama ilivyo Wenge Musica na makundi yake, Zaiko nayo imefanikiwa kuzaa bendi nyingi kama Isifi Lokole, Viva La Musica, Langa Langa Stars, Zaiko Familia Dei, Anti Choc, Choc stars, and Zaiko Nkolo Mboka.

Ilianzishwa rasmi mwaka 1970 wakati huo ikijulikana kama Orchester Zaiko, baadaye kidogo washabiki wakaanza kuwaita Langa Langa wakimaanisha “Kulewa” kwa kuwa nyimbo zao zilikuwa zikipigwa sana kwenye vilabu vya pombe kila kona. Waanzilishi wakiwa ni Papa Wemba, Evolocko Lay Lay, Zamungana na  Nyoka Longo.

Zaiko ndio waanzilishi wa sebene la leo ambapo wao walichukua mtindo wa kiasili na kuingiza ala kama magitaa, Chants, na rap kwa mbali jambo lililonogesha muziki wao na kuufanya kupendwa na rika lote.

Mwaka 1973 Zaiko walikuwa maarufu sana si tu kwa Zaire bali hata kwa nchi za jirani huku mwanamuziki wake Evolocko Jocker akiwa ni maarufu sana kwenye bendi hiyo ambapo aliweza kuingiza mtindo maarufu wa cavacha wa uchezaji ambao ulikuwa maarufu sana na kupendwa kote.

Miaka ya kati kati mwa sabini bendi hii ilianza kumong’onyoka ambapo waliondoka walikuwa wanamuziki wake maarufu kama Papa Wemba ambaye aliondoka na Bozi Boziana, Evolocko na  Mavuela ambao kwa pamoja walianzisha Bendi iliyoitwa Isifi Lokole, ambayo hata hivyo haikukaa sana kwani nayo ilimeguka na kutoa bendi mbili Yoka Lokole, na  Viva La Musica ya Papa Wemba.

Mwishoni mwa miaka ya sabini Bendi ilikuwa iko juu si mchezo huku wanamuziki wake wakiwa wanasifika kwa kila kitu, inakumbukwa wanamuziki kama Nyoka Longo, Lengi Lenga, Bimi Ombale, Dindo Yogo, Evolocko walileta laha sana kwenye bendi hii.

Ilienda mpaka miaka ya mwanzoni mwa 80 ambapo bendi ilimeguka tena. Hii ilitokana na wakongwe kama Meridjo, Nyoka Longo na  Dindo Yogo kutokubaliana na mambo waliyoyaita mageuzi ambayo yaliletwa na vijana wapya kama Lengi Lenga, Ilo Pablo na Bimi Ombale. Hii ilipelekea kusambaratika na kundi la akina Nyoka Longo likajiita Zaiko Langa Langa Nkolo Mboka, na lile la Bimi likajiita   Zaiko Langa Langa Familia Dei. Makundi yote kwa pamoja yanamafanikio na mchango mkubwa kwenye ulimwengu wa Muziki wa Congo.

Hizi hapa ni baadhi ya kazi zao toka mwaka 1970

  • 1970 : Pauline
  • 1972 : L’amoureux decu
  • 1973 : Mete la vérité, chouchouna
  • 1974 : Liwa ya somo
  • 1981 : Sarah Djenni
  • 1983 : La Tout Neige

Read the rest of this entry »


Fally Ipupa ndani ya Bicarbonate

February 26, 2010

Utaongeleaje muziki wa Congo bila kumtaja Fally Ipupa?

Utaongeleaje mafanikio ya muziko huo bila kumtaja Fally, Inawezekana Fally akawa ni mtoto mdogo sana unapoongelea muziki wa Congo lakini kwa sasa Fally yuko juu utake usitake, hiyo inadhihirishwa na mtiririko za Ziara zake kwa mwaka huu ambapo ratiba inaonyesho kuwa atakuwa na shoo karibu mara tatu kwa mwezi kwa mwaka mzima.

Usikose kusoma hapa kumjua zaidi Fally Ipupa na hata lile swali toka kwa mdau wangu kuwa Fally na Ferre Gola nani zaidi nitalijibu humo kwa mtazamo wangu.

Mamaa Flower nakati ya Canada tuko pamoja nadhani.

Bofya player umuone kijana


Eti gari ya Miss Tanzania iliibiwa taa/kioo kituoni

February 26, 2010

Kuna habari kuwa Gari ya Miss Tanzania Miriam Gerald iliibiwa Kioo na Taa wakati yeye akiwa ndani, Kwa mujibu wa Mpashaji Habari wetu gari hiyo ambayo ilihifadhiwa katika kituo cha Oysterbay kwa takribani siku nne lilipatikana na mapungufu yaliyopelekea ufumbuzi wa haraka kutafutwa ili kuondokana na aibu na kashfa hiyo.

Inasemwa kuwa juhudi za maksudi ilibidi zifanyike kabla Miss hajatoka na watu walihaha kuziba makosa hayo hasa iliposmwa miss huyo anatoka kwa dhamana.

Tunalifanyia kazi suala hilo na likikamilika tutalileta, kama ni kweli inasikitisha sana.

Habari ndio hiyo.


Anderson kutocheza msimu mzima

February 26, 2010

image

Kiungo wa Manchester United Anderson hatocheza hadi msimu huu utakapomalizika baada ya kuumia goti wakati akicheza dhidi ya West Ham.

Mbrazil huyo aliumia katika dakika ya 19 siku ya Jumanne wakati Manchester United ilipoizaba West Ham mabao 3-0 na huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza baada ya kuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja.

Anderson akiwa na umri wa miaka 21 inaelekea hatokuwemo pia katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya Kombe la dunia na Sir Alex Ferguson amesema hilo ni pigo kubwa.

Nae winga Ryan Giggs, huenda akacheza mchezo dhidi ya AC Milan mwezi ujao katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kuvunjika mkono tarehe 10 mwezi huu wa Februari baada ya kugongana na Steve Sidwell wa Aston Villa, katika mchezo ambao timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Villa Park.

Na BBC


Bridge ajiondoa timu ya taifa England

February 26, 2010

image

Mlinzi wa Manchester City Wayne Bridge amejiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na hatoichezea timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Dunia.

Katika taarifa iliyotolewa na mawakili wake, Bridge mwenye umri wa miaka 29, amesema nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ameona haitakuwa na "ufanisi na anaepusha mgawanyiko".

Mlinzi huyo wa upande wa kushoto amekuwa akitajwa kuhusiana na tuhuma za mpenzi wake wa zamani kuwa na uhusiano na John Terry.

Kocha wa England Fabio Capello mwezi huu alimvua unahodha Terry.

Katika taarifa hiyo ya Bridge iliyotolewa siku ya Alhamisi, ameongeza kusema amefikiria kwa muda mrefu nafasi yake katika kikosi cha England na hasa akihusisha matukio yaliyokuwa yakiarifiwa kwa wiki kadha.

Ameendelea kusema ni jambo la heshima kila wakati kuichezea England. Hata hivyo baada ya kufikiria kwa makini anaamini nafasi yake katika kikosi hicho kwa sasa haitakuwa na ufanisi na huenda kungesababisha mgawanyiko.


Mr & Miss East Africa 2010 (UK)

February 26, 2010

image

ONE NIGHT TWO PRESTIGIOUS PAGEANTS MR & MISS EAST AFRICA UK 2010 AUDITIONS & LAUNCH PARTY THE BEAUTY PAGEANTS THAT SET THE STANDARD, THE BENCH MARK, THE PINNACLE OF ALL BEAUTY PAGEANTS. WITH A JUDGING PANEL OF SUCCESSFUL ENTREPRENEURS. PROMOTING BEAUTY, PHILANTHROPY & …ENTREPRENEURSHIP. IT’S BIGGER & BETTER. ENDORSED AND SUPPORTED BY FORMER CONTESTANTS, QUEENS AND KINGS. CREATED ENTREPRENEURS, MODELS, ROLE MODELS, BEAUTY QUEENS, DESIGNERS, ALL IN THE NAME OF OUR COMMUNITY
☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆ AUDITIONS FOR 2010 LOOKING FOR MALE AND FEMALE CONTESTANTS TO BE MR AND MISS EAST AFRICA UK. FROM BURUNDI, KENYA, TANZANIA, SUDAN, ETHIOPIA, UGANDA, ERITREA, DJIBOUTI, SOMALIA, SOMALILAND, RWANDA MR EAST AFRICA UK 2010 CASH PRIZE MISS EAST AFRICA UK 2010 CASH PRIZE DONATING TO HAITI DONATING TO AFRICAN CHILDREN’S CHARITIES LOOKING FOR PERFORMERS, DANCERS, VOLUNTEERS, DESIGNERS, CHOREOGRAPHERS, MAKE UP ARTISTS, STYLISTS, DJS, MCS, HOSTS, PROMOTERS, PR & MARKETING, ENTREPRENEURS,PHOTOGRAPHERS, PRESENTERS.SINGERS, MUSICIANS, TRADITIONAL DANCERS. SPONSORS, CAMERA MEN, FILM MAKERS.

☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★

AND THE OFFICIAL LAUNCH PARTY FORMER & CURRENT QUEENS AND KINGS, CELEBRITIES, COMEDIANS PUBLIC FIGURES WILL BE IN ATTENDANCE. MUSIC BY BEST RESIDENT & GUEST DJS, MCS. PERFORMANCE BY ALI KIBA, MYCO CHRIS, MC MOSEH AND MANY MORE DATE:27TH FEBRUARY 2010 VENUE:CLUB VALENTINO ADDRESS:750 TOTTENHAM HIGH ROAD, LONDON, N17 0AL NEXT TO TOTTENHAM HOTSPURS STADIUM

☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆

AUDITIONS FROM 12 NOON TILL 7PM (SEND YOUR NAME CONTACT, NUMBER) LAUNCH PARTY STARTS 9PM TILL 5AM HOST: SPORAH OF THE SPORAH SHOW & ED K EDRIS SUPPORTED BY JUNGLE DREAM, BEFFTA AWARDS & FAMOUS FIGURES

☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★•☆•★★

FOR MORE INFO TEL: 07511385337 / 07944456643 / 07771122531 / 07956671176 registration@misseastafrica.co.uk ed@misseastafrica.co.uk yenabi@misseastafrica.co.uk info@misseastafrica.co.uk http://www.misseastafrica.co.uk AN AWB EXECUTIVE LTD EVENT SUPPORTED BY JUNGLE DREAM


Robin van Parsie huenda akarejea Aprili

February 26, 2010

image

Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie huenda akarejea kucheza mapema mwezi wa Aprili kwa mujibu wa kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk.

The Gunners wanakadiria Robin atarejea uwanjani mwishoni mwa mwezi wa Aprili baada ya kufanyiwa upasuaji wa kiwiko cha mguu.

Lakini baada ya kuzungumza na Van Persie kwa njia ya simu, Van Marwijk sasa ana matumaini makubwa atapona haraka baada ya kujeruhiwa mwezi wa Novemba.

Van Persie alikuwa katika kiwango cha juu cha usakataji soka kwa klabu na nchi yake kabla hajaumia kiwiko cha mguu dakika ya 10 ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya Uholanzi na Italia tarehe 14 Novemba.


Reggae Night @ Sweet Eazy

February 26, 2010

Saturday Night Live presents: Jhikoman & Afrikabisa Band. Tanzania’s leading Reggae Orchestra live at Sweet Eazy Oysterbay.

Saturdays, from 9pm – 2am. Reservations: 0755 75 40 74.

See below flyer for details.

image


WHITE SHADOWS’ PROJECT – ALBINOS IN TANZANIA

February 25, 2010

albino

Hello Pius,

I’m Liron Shimoni an Israeli photojournalist, we were in touch about three months ago. Two weeks ago I returned from Tanzania where I witnessed the difficult lives of the Albinos there. I documented the life of the albino society and distributed more than one thousands pairs of sunglasses to people with albinism in Shinyanga, Tabora, Mwanza and Dar es Salam. These sunglasses were collected by me in Israel during the past three months and I am in touch with companies that will donate thousands of sunglasses and sunscreen lotion more to the albinos.

My photographs that were taken in Tanzania will be on display at the exhibition ‘White Shadows’ at the Tel Aviv Cinemateque-
Israel and I hope to let people in my country know about the albinos problem.
Attached is a  short film on the project.

Best regards,

Liron Shimoni


Zawose kupamba tena tamasha la Rainforest Music Festival – Malaysia

February 25, 2010

image

Mwanamuziki wa asili Dr. Hukwe Zawose atakuwa mmoja wa wanamuziki ambao watatumbuiza katika Tamasha la Rainforest ambalo linakusanya wasanii toka kila pembe ya dunia na kufanyika huko Malaysia. Kwa mujibu wa waandaaji Bodi ya Utalii Malaysia Zawose ametajwa kuwa mmoja wa washiriki wa mwaka huku.

Zawose ambaye mwaka jana alijizolea sifa kem kem anatarajiwa kuwa mmoja wa wanamuziki toka barani africa watakao pamba shughuli hiyo. Tamasha la mwaka jana  lilikuwa na vikundi vingi lakini kwa mujibu wa magazeti ya Malaysia Zawose alifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki na washiriki wenzake hasa kwa mavazi yao pampja na jinsi wanavyoimba na kupiga ala zao za asili.

Tamasha hili la Rainforest Music World Festival linafanyika kila mwaka katika jimbo wa Sarawak na linafanyika katika misitu ya Santubong na kujuisha vikundi mbalimbali toka duniani kote likiwa na sura ya utamaduni zaidi likiambatana na workshop mbalimbali.

image

kwa habari zaidi gonga hapa na hapa

Gonga Player umuone Zawese Tamasha la mwaka jama. Mamaa Grace inakuhusu hii ya Idodomya


TRACK MPYA – HUSSEIN MACHOZI (ZA MWIZI 40)

February 24, 2010

FRONT COVER (PIC)

Wimbo huu mpya wa Hussein Machozi unaoitwa ZA MWIZI 40, ambao umetoka rasmi kwenye vitui vya redio,   wimbo huu unapatikana katika album yake ya KWA AJILI YAKO. Hii ni single yake ya 3 kutoka katika album hiyo, single mbili zilizotangulia ni pamoja na KWA AJILI YAKO na UTAIPENDA.

Kwa sasa yuko katika hatua za mwisho za kushot video ya wimbo huo, ambayo inategemewa kufanyika jijini Dar es Salaam na Adam Juma wa Visual Lab wiki ya kwanza ya March, na video itatoka mara tu tukikabidhiwa na Adam.

SONG’S DETAILS

Track Name: ZA MWIZI 40

Singer: HUSSEIN MACHOZI

Produced by: AMBA & KID BWOY

Written by: HUSSEIN MACHOZI

song arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY

Mixed by: KID BWOY

Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS

Bofya player hapo chini kuusikiliza


Mali yangu na Alikiba

February 24, 2010

Kama mafanikio ya Muziki yanaweza kupimwa kutokana na ziara za nje basi Ali Kiba anaweza akawa ni mmoja wa wanamuziki wa Bongo Flava mwenye mafanikio sana kutokana na Ziara nyingi za Nje ya nchi ambazo amezifanya.

Kutoka Africa, Europe na hata America, alikiba amekuwa akipata mialiko ya kufanya show huko, bila kuangalia ni ukubwa kiasi gani wa show ambazo amekuwa akifanya lakini Kiba kiukweli amekamua kiwanja vya kutosha.


WALEMAVU WA VIUNGO WALAANI VYOMBO VYA HABARI KWA UZUSHI KUWA OMBAOMBA AMEMGEUZA MTU!!

February 24, 2010

Bi.Neema Robert mkazi wa Chang’ombe Temeke akihojiwa na waandishi wa habari.

Baadhi ya walemavu wa viungo jijini Dar-es-Salaam wamelalamikia habari zilizovumishwa katika vyombo vya habari zikidai ombaomba wa Salender Bridge amemfanya mtu kugeuka mkono wake na kuwa na manyoya mithiri ya paka.

Wamesema kitendo hicho kimewafanya kunyanyapaliwa kila mahali katika sehemu mbali mbali za huduma za kijamii,wakielezea zaidi mbele ya waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, walemavu hao wamesema hivi karibuni vyombo kadhaa vya habari(Radio) na magazeti vilitoa taarifa kuwa katika maeneo ya salender bridge kuna mwanamke ambaye mkono wake uliota manyoya baada ya kutoa msaada kwa omba omba waliokuwa mahali pale.

Taarifa hizi kwa mujibu wa watu mbali mbali na vyombo mbali mbali zimeonekana kuvuta hisia za watu wengi,tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo inadaiwa mwanamke mmoja alilazimika kumbusu omba omba ili arudi katika hali yake ya kawaida,kitendo ambacho kilipelekea omba omba huyo kupotea na mwanamke huyo kimazingara.

walemavu hao wamesema walifika eneo la tukio na kukitaka chombo hicho kudhibitisha taarifa hizo lakini bado haikuthibitishwa kama kuna ukweli wowote,baada ya hapo waliamua kwenda katika Idara ya habari maelezo na kutoa tamko la kuwa taarifa si sahihi na kwamba zimewafanya walemavu wa viungo na omba omba kuitwa MIZIMU na jamii nzima,pamoja na kunyanyapaliwa hata kwenye vyombo vya usafiri,migahawani na sehemu mbali mbali za huduma ya jamii.

Akihitimisha Bi.Rehema ambaye ni mmoja wa walemavu hao amesema,mpaka sasa tayari kuna walemavu 3 anaowafahamu ambao wamepewa NOTICE za kuondoka kwenye nyumba walizopanga.Hivyo wameiomba Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ijaribu kuliangalia swala hilo kwani maisha yao hivi sasa yamekuwa ni yenye huzuni na masikitiko na wakati mwingine kujiona hawafai kuishi.

Habari hii na Mdau Bukuku wa Full Shangwe


Werrason na WMMM kuwasha moto Zenith March 13

February 24, 2010

 

image

Mwanamuziki Werason Ngiama Makanda wa Wenge Musica Maison Merre (WMMM) ameendelea kutamba kwa ziara za nje na kwa mara hii Concert yake ya Zenith inaongelewa sana na kusubiriwa kwa hamu.

Werrason ambaye wiki iliyopita alitangazwa kuwa balozi wa Amana wa Vijana na waziri anayeshughulikia masuala ya Usalama huko Congo DRC, anatarajiwa kufanya show hiyo mnamo March 13.

“Zenith ni mahali ambapo ni kipimo cha mwanamuziki kukubalika, kama mwanamuziki ukapita mwaka hujafanya show Zenith basi inaonyesha we umeshuka kidogo umaarufu au uwezo wako” alisema Dim Makanda mmoja wa waandazi wa show hiyo.

Makundi kama Wenge BCBG, Koffi, Papa Wemba, Fally Ipupa, Ferre Gora, kwa nyakati tofauti wamekuwa wakifanya maonyesho yao huko Shengeni na Ufaransa ikiwa ni matokeo ya kuwa na waafrika wengi wanaozungumza lugha ya Kifaransa na hasa wa Congoman.


HUMMER HT7 MADE IN UKARA

February 22, 2010

Zipo njia nyingi sana za kukuza utalii wetu na kuwafanya Watalii wakumbuke Tanzania, angalia ngoma hii huko Angola mweee…!!

image001

image003

image004

image005

image006

image002


Malcom X on Fotobaraza

February 22, 2010

image

Malcom X alizaliwa katika familia yenye maisha duni na akiwa na umri wa miaka 13, baba yake ambaye alikuwa mpigania haki za watu weusi pia aliuawa na wazungu wabaguzi waliojulikana kama Ku Klux Klan (KKK), na mama yake alikuwa amefungiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili. Hivyo Malcom akaanza maisha ya kujitegemea akitumia wizi wa mifukoni kama njia ya kujipatia kipato.

Mwaka 1946 Malcom alifungwa jela kutokana na wizi. Akiwa Jela, Malcom ambaye hakuwahi kusoma vitabu akajikuta akiwa msomaji mkubwa wa vitabu ambavyo vilimwongezea maarifa aliyokuja kuyatumia baadae katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa watu weupe kwa watu weusi.

Malcom X aliwahi kusema, "Ukitaka kumshinda adui yako, jifunze lugha yake". Hivyo akiwa jela Malcom X mbali ya kusoma vitabu vingi changamoto aliyojiwekea ilikuwa ni kukariri Kamusi ya Kiingereza ya Oksfodi, changamoto ambayo aliweza kuivuka. Malcom aliweza kujieleza vyema katika mahakama na vyombo vya habari juu ya mapambano yake, kitu ambacho kiliwaudhi sana wazungu waliokuwa wakitaka kupindisha ujumbe wake.

Ukisoma kitabu chake cha "The Autobiography of Malcolm X" kuna wakati Maclom alikutana na dada wa kizungu aliyetamani kufanya kazi ya ukombozi na Malcom lakini Malcom akamwambia, "Mzungu ni mzungu tu hata kama roho yako ni nzuri lakini bado wewe ni mzungu, hatukuamini!" Dada yule akaondoka amefadhaika.

Lakini mwaka 1964 akapata bahati ya kwenda kuhiji Mecca, huko akakutana na Wazungu, Weusi, na Waasia ambao waliketi pamoja, wakila pamoja na kulala pamoja. Kufikia hatua hii Malcom X akagundua jambo moja na akasema katika barua yake iliyopewa jina la ‘A Letter from Mecca’, "Nimegundua kwamba tatizo sio wazungu (watu weupe) bali ni mfumo wa Kibepari wa Kimarekani". Baadae aliwahi kusema, alipokuwa akimzungumzia yule dada wa Kizungu, "Siku zote nimekuwa nikiomba Mungu anisaidie nikutane tena na dada yule ili nimwombe msamaha lakini sijafanikiwa, natumaini dada huyu asomapo kitabu changu (The Autobiography of Malcolm X) atanisamehe kwa ujinga wangu".

Ni mabadiliko ya falsafa ya Malcom X toka kwenye falsafa ya ‘Jino kwa Jino’ au Militant Philosophy kwenda falsafa ya ‘Ukipigwa Shavu la Kulia Geuza na lile Lingine’ ndio iliyomjengea uadui mkubwa zaidi na shirika la kijasusi la CIA na lile la kikachero la FBI ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakituhumiwa kuwa ndio waliopanga mauji ya Mtume huyu. Mashirika haya yaliogopa kwa sababu yaliona Malcom yuko njiani kuunganisha watu wa rangi zote kufikia lengo lake.

Kaisome zaidi hapa http://fotobaraza.ning.com


Ferguson ataka Scholes kuendelea kucheza

February 22, 2010

image

Meneja wa Manchester Alex Ferguson amemtaka Paul Scholes kuweka kando mawazo ya kustaafu na atie saini mkataba mpya na klabu hiyo.

Mwaka jana mwezi wa Mei Scholes ambaye mkataba wake na Manchester Uinited unamalizka mwezi wa Juni, alisema msimu huu "huenda ukawa wa mwisho kucheza soka".

Lakini kufuatia bao lake katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya, walipoilaza AC Milan na kushinda mabao 3-2 siku ya Jumanne, Ferguson amemtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35 kuendelea kucheza soka.

Mwezi wa Decemba Scholes ambaye wakati huo alikuwa ameanza kucheza michezo sabu tu kati ya 14 ya Ligi Kuu , alionesha kutokuwa makini na mipango yake ya baadae ya usakataji soka na Manchester United.


Arsenal, Chelsea, West Ham washinda

February 22, 2010

image

Timu ya Chelsea imeyatumia vyema makosa ya Manchester United kupoteza mchezo na Everton na kuzidi kujikita kileleni kwa kuzoa pointi tatu dhidi ya Wolves.

Mabao hayo mawili ya Chelsea yaliwekwa wavuni na mshambuliaji hatari wao hatari Didier Drogba. Kwa matokeo hayo Chelsea inazidi kupaa kileleni kwa kuzoa pointi 61.

Kwa upande mwengine Arsenal waliutimia vyema uwanja wa nyumbani wa Emirates kwa kuwafunga Sunderland mabao 2-0. Bao la kwanza likiwekwa kimiani na Niclas Bendtner na la pili likafungwa na nahodha Cesc Fabregas kwa njia ya mkwaju wa penalti dakika moja kabla mchezo kumalizika.

Arsenal sasa wamefikisha pointi 55.

West Ham nao hawakufanya ajizi katika uwanja wake wa nyumbani wa Upton Park walipowalaza bila huruma Hull kwa mabao 3-0.

West Ham wamezidi kujiondoa katika lindi la kushuka daraja na sasa wapo katika nafasi ya 13 kwa kuzoa pointi 27.


Nassib anadi sera zake TFF

February 22, 2010

Nassib

Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), anayetetea nafasi yake, Ramadhan Nassib (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Hadees, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mjuembe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Makamu Mwenyekiti wa mashindano, Wallace Karia.

MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ramadhan Nassib, amewataka wajumbe kuchagua kiongozi kwa manufaa ya maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mgahawa wa Hadee’s, Nassib, alisema wakati umefika kwa wajumbe kuchagua viongozi wenye upeo wa kuongoza.

“Ni vizuri wajumbe wakachagua viongozi wenye nia thabiti ya kuendeleza soka na siyo kwa manufaa ya wengine,” alisema.
Alisema katika mwaka wake mmoja wa uongozi, alifanya mambo mengi likiwemo la kudhibiti mapato ya viingilio vya milango na kuendesha ligi za vijana.

Mgombea huyo alisema wakati akiingia madarakani, aliahidi kuboresha ligi ya vijana wenye umri tofauti kwa kushirikiana na viongozi na wenzake, jambo ambalo alilitekeleza.
“Mahakama ya michezo nchini, hilo lilikuwa suala mojawapo na tunaendelea nalo, likikamilika litamaliza mambo mengi ya michezo,” alisema.

Nassib alisema kuwa, kwa upande wa soka la vijana, kwa kushirikiana na viongozi wenzake, walifanikiwa kuendesha ligi ya vijana wenye miaka chini ya 17 ya Copa Coca Cola kwa udhamini wa kampuni ya Coca Cola na ligi ya vijana wenye miaka chini ya 20.
Alisema hivi sasa wako katika mchakato wa kuendesha ligi ya U20 kwa kushirikisha timu mbalimbali nchini na siyo za ligi kuu pekee kama ilivyo hivi sasa.

Mgombea huyo alisema wajumbe watakaopiga kura za kujaza nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais, wasitumike kwa ajili ya maslahi ya wengine na badala yake wazingatie zaidi masuala ya kitaifa.
Akizungumzia kumzidi mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, John Nchimbi  kwa kura moja, Nassib alisema ushindi huo unaonesha jinsi klabu za Ligi Kuu zinavyomuunga mkono.
“Kwanza, ni changamoto kubwa kwangu, ushindani utakuwa mkubwa sana, lakini nina imani na wajumbe watakaopiga kura,” alisema.

Katika upigaji kura wa klabu kumteu mgombea wao, Nassib alipata kura tano dhidi ya nne za alizopata Nchimbi na kuwafanya wadau wa soka washangae na kuamiani kuwa uchaguzi utakuwa mgumu.

Habari na Picha na Mdau Frank Balile.


%d bloggers like this: