Chelsea yaibuka kidedea kwa Man City kwenye “Mchezo wa Kitajiri”

September 14, 2008
Wachezaji wa Man City wakimpongeza Robinho baada ya kupachika bao la kwanza dhidi ya mchezo wao na Chelsea leo

Wachezaji wa Man City wakimpongeza Robinho baada ya kupachika bao la kwanza dhidi ya mchezo wao na Chelsea leo

Klabu ya Chelsea usiku huu imeibuka mbabe wa mchezo kati yake na Man City kwa kuitungua mabao matatu kwa moja (3-1) katika mchezo “wa kitajiri” uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa.

Huku akilipa limbikizo la ada ya uhamisho ilovunja rekodi ya Paund £32.5million, Robinho aliweza kuwafanya Man City waongoze dakika ya 13 ya mchezo kwa kupachika bao safi la free kick na kufanya Man City iongoze, bao lao lilidumu kwa dakika tatu tu kwani Chelsea kupitia kwa Ricardo Carvalho iliweza kuasawazisha bao lile na kufanya ngoma kuwa droo mpaka mapumziko, Dakika ya Frank Lampard alipachika ao safi la pili kwa Chelsea na kufanya mayowe ya Man City kuanza kuzizima, Chelsea walizidi kulisakama langoo la Man City na kufanikiwa kuongeza kimoja kupitia kwa mchezaji mkongwe Nicolas Anelka na kufanya mabao kuwa 3-1. Hata hivyo nahodha John Terry alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza madhambi.


Man City wamnyakua Robinho

September 2, 2008
Roginho

Robinho

Manchester City wamefanikiwa kuwazidi kete Chelsea kwa kumchukua Mbrazili forward Robinho toka klabu ya Real Madrid kwa rekodi ya uhamisho ya kwa UK ya £32.5m.

Chelsea wamekuwa wakimfukuzia mchezaji huyo mwenye iaka 24 lakini Man City wamefanikiwa kumnyakuwa kwa mkataba wa miaka minne.

“Binafsi nafurahi kufanya kazi na kijana mdogo mwenye uwezo na akli ya mpira awapo uwanjani, tunafarijika kuwa ataleta changamoto ya ushindi kwenye timu yetu alisema Boss wa Man City  Mark Hughes  kwa mujibu wa Mtandao wa BBC.

Baada ya kusikia habari za Man City klabu ya Chelsea imekiri kumkosa Robinho ni pigo kwenye mikakati yao lakini pia imehakikisha kikosi ilichonacho kinatosha kufanya mambo kwa vikombe.


Ronaldinho: Bye bye Barcelona

July 15, 2008

Mchezaji wa Barcelona Ronaldinho akiingia kwenye gari yake mara baada ya kikao na viongozi wa Klabu yake ya Barcelona hapo jana 14 July, 2008, Rais wa klaby ya Barcelona Joan Laporta amesema wamepokea ofa ya Euro 32 million (sawa na Dola 51 million) toka klabu ya Manchester City kwa ajili ya kumuachia mchezaji huyu ambaye alipata kuwa mchezaji bora wa Dunia kwa miaka miwili said. AFP PHOTO / JOSEP LAGO (Photo credit should read JOSEP LAGO/AFP/Getty Images)


%d bloggers like this: