SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)

August 31, 2011

Majuzi tuliona jinsi Wenge kuanzia Mwanzo ilivyoaanza mpaka ilipofikia kumeguka kwa JB Mpiana na Werason (Kama uliikosa bofya hapa), Leo hii tunaanza kuiangalai Wenge BCBG ya JB Mpiana. Endelea…

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

image

Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Werrason, Didie Masela na Allain Makaba

walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris

Wenge BCBG ilizaliwa JB Mpiana akiwa kiongozi wa bendi,Blaize Bula akiwa Chef d’orchestre,Alain “Prince” Makaba akiwa artistic Director na SIMON SIPE akiwa producer. Waimbaji wakiwa JB mwenyewe, Alain Mpela, Aimelia Lyase Demingongo na Blaize Bula, wapiga guitar Alain Makaba,Burkinafaso Mbokalia na Japonais(solo & rhythm),Patient Kusangila(rhythm & Bass), Titina(Drums), Ali Mbonda, Seguin Mignon(Tumba), Theo Bidens (keyboard), na Powerful AtalakUs toka kwao Roberto Ekokota “Le Grand Chibuta na Tutu Caluggi.

image

Kundi la Wenge Musica BCBG 1987, Kwenye Mic ni Werrason na JB Mpiana, Picha na Wikipedia

Mwanzoni wanamuziki wengi wa kawaida kundini humo akiwemo Alain Mpela ambae amekiri walikua hawajui kinachoendelea walikua wakidhani bado ni wenge musica ileile moja kwa kuwa mpaka nyimbo za album ya TITANIC walizifanyia mazoezi pamoja (nadhani ndio maana hata tukisikiliza kwa makini TITANIC na FORCE INTERVENTION RAPIDE zinavyoanza ni kama zinafanana)na kwa wenge walivyokuwa wanafanya kazi,ilikua ni kawaida kwao wakati mwingine kupiga show hasa local wakiwa hawajakamilika wote,sometimes wanaweza kuwepo wote akamiss labda makaba na blaize bula au hao wakawepo akamiss werrason, au wote wakawepo akamiss JB,

Hivyo basi kitendo cha werra,adolphe na didier masela hakikuwashangaza na kuwafanya wahisi labda kuna mgawanyiko wa bendi tayari,wakajua ni utamaduni wa wenge wa kawaida si unajua mastaa wakiwa kundi moja tena,japo walikua wanajua mitafaruku imekuwa ikiendelea mara kwa mara katika maisha ya wenge lakini si yakufikia kuzigawa bendi.

Lakini walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris.,ndipo katika hali isiyo ya kawaida wakiwa na katika maandalizi ya ziara hiyo ambayo hupewa kipaumbele sana na wanamuziki wa congo wakawa wanashangaa mbona jamaa hawaonekani hata mazoezini wakati kuna safari nzito kama hiyo!na ilikua ni katika kipandi hicho hicho pia ambapo Ali Mbonda akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kuitosa bendi mpya ya WENGE BCBG kwenda kwa kina WERRASON baada ya jina lake kutokuwemo kwenye trip nyeti kama hiyo huku jina la msaidizi wake chipukizi wakati huo katika kupiga mbonda (tumba) Seguin Mignon likichukua nafasi yake(Seguin sasa hivi ndio mpiga drums namba moja wa BCBG).

Kwa hiyo hiyo ndio ikawa safari yao ya kwanza ulaya bila kina werrason,wakapiga show hiyo hapo chini kama wanavyoonekana huku wakihitajika kutoa maelezo ya kina kwa mashabiki kuwaeleza kilichotokea huko nyumbani Kinshasa na kupelekea kujiweka pembeni na wenzao(werra,adolphe na masela),Ekokota yupo kundini hapo anaonekana akifanya kazi na Tutu Caludji “no.1”.

na

Baada ya Ali Mbonda kujiondoa kundini baada ya kukerwa na kutojumuishwa kwenye safari ya ulaya jambo ambalo limekua la kawaida mno kwa Ali na wanamuziki wengi offcourse wa congo wanapokosa kuwemo kwenye tour za Ulaya,Mtu wa pili kujiondoa BCBG akawa ROBERTO EKOKOTA mara baada ya concert hiyo ya BATACLAN hapo juu aliamua kupumzika kutokana na matatizo ya kiafya hali iliyomfanya ashindwe hata kuweka Atalaku zake kwenye album ya TITANIC na kumuacha Tutu Caludji amalize kila kitu mwenyewe,ndio vile tunaisikia TITANIC mpaka leo,pale ni bila le Grand Chibuta Ekokota,angeshiriki sijui ingekuwaje,mi sijui tuwaachie wenyewe!.

Baada ya kumaliza recording ya TITANIC walirejea nyumbani congo wakimuacha Alain Makaba huko ulaya kwake ambako alishakua amehamia. Walipofika Congo wakawakuta kina werrason ndio wameshaitengeneza bendi yao wanajiandaa Force Intervention Rapide(Lakini walikua bado hawajaipa hilo jina, maana nalo lina hadithi yake halikuja tu kama mvua),Baada ya mapumziko mafupi ya safari ya ulaya kazi ikaanza kwa Chef d’Orchestre Blaize Bulla Kuanza kutafuta vijana wa kuwa recruit. Hapa walihitaji mpiga bass yani pure bassist atakaeziba pengo la Didier Masela badala ya kumtegemea Patien Kusangila ambae kiasili alikua ni mtu wa rhythm guitar,pia walihitaji atalaku ataeziba pengo la Ekokota,kwa upande wa bass Blaize Bulla akaanza kumchokonoa Koffi kwa kuvamia ngome yake na kufanikiwa kumshawishi Sunda Bass ambae hata hivyo hakua na nafasi huko Quartier latin, alikua ni under ground bassist nyuma ya Fally Tyson na mwingine pia.

image

Engineer Blaise Bula, Alishiriki kwa Kiasi kikubwa kuiunda Wenge BCBG ya sasa.

Hivyo Sunda Bass akawa mtu wa kwanza kuwa recruited,baada ya hapo chini wenge bcbg chini ya Blaize Bulla ambae alipania kuisuka bendi upya ikawaita ma-atalaku wa tatu kuwafanyia majaribio ili wampate mmoja atakaemsaidia Tutu Caludji,miongoni mwa walioitwa ni Bidjana ambae baadae alienda zaiko huyu Genta Lisimo “Anti biotique” ambae wakati huo alikua akitokea Anti Choc kwa mzee Bozi Boziana,Tutu Caludji akamkubali zaidi Genta ambae nafasi yake kule kwa Bozi ikazibwa na Theo Mbala toka Big Stars ya Defao.

Engeneer Blaize Bula hakuishia hapo katika harakati zake za kuijenga BCBG, akaona kuna haja pia ya kuimarisha safu ya uimbaji kwa kuongeza waimbaji wachache,ndipo akawasiliana na rafiki yake na muandishi wa nyimbo zake wa siku nyingi toka enzi za wenge musica original ambae pia alikua muandishi wa nyimbo wa CHOC STARS na si mwingine bali ni JULES KIBENGA MAKIESE a.k.a. Jules Kibens(najua wengi mtashangaa lakini ndio ukweli),pia akamtafuta RIO KAZADI “rIO de janeiro” ambae alikua Chef D’ Orchestre katika bendi iitwayo JOLINO akiwa na akina KABOSE, CHAI NGENGE na baadae BILL CLINTON Pia alikua chini yake hapo JOLINO.

image

Hata Rais Kabila pichani amejaribu kwa uwezo wake kuwapatanisha wanamuziki wa Congo, kama ilivyo kwa picha hii.

Rio nae akamwambia Blaize Bulla kwamba kama anamtaka yeye basi pia amchukue na rafiki yake Chai Ngenge,Blaize akakubali hivyo wote wakajiunga BCBG,Pia kutokana na kutomuamini Burkinafaso kutokana na tabia yake ya kuhamahama Bulla aliamua pia kumchukua ALBA ACCOMPA aje asaidiane nae na kwa kuwa wote kundini walimjua ALBA kutokana na kwamba alishajaribiwa kundini wenge oariginal na kuonekana anafaa lakini akawa amechelewa wakati anajiandaa kujiunga na bendi ndio ikawa inavunjika.Baada ya hapo ikawa ni mazoezi tu na show za ndani,then wakapata contract nyingine kubwa ya kupiga kusafiri kwenda ulaya kupiga ZENITH na OLYMPIA,Safari ambayo ilizua mtafaruku mkubwa ulioitingisha sana BCBG Katika historia ya maisha yake,mtafaruku uliosababisha JB awe kama alivyo hivi tunavyomuona sasa na BCBG yake.

Je nini kilitokea….twende pamoja siku ya Ijumaa tutakapo kuwa tunakamilisha makala hii ya Historia ya kuvunjika kwa Wenge Musica na miaka mitatu ya mwanzo ya JB Mpiana na Werrason.

Kama una maoni usisite kuniandikia kwa piusmicky@yahoo.co.uk au SMS ONLY 0713 666616.


Stoke yakwama kumsajili Lukaku wa Chelsea

August 31, 2011

Na BBC

Stoke imekwama katika mipango yake ya kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji mpya wa Chelsea Romelu Lukaku kwa sababu ya kanuni za Ligi Kuu ya England.

Romelu Lukaku

Romelu Lukaku

Romelu Lukaku, aliwasili Stamford Bridge akitokea klabu ya Anderlecht mapema mwezi wa Agosti na alicheza mechi yake ya kwanza na Chelsea siku ya Jumamosi.

Lakini kanuni ya Premier League namba M 7.1 inasema: “Usajili wa muda hautawezekana wakati wa dirisha la usajili ambapo mchezaji amekuwa ndio kwanza amekamilisha usajili na klabu nyingine.”

Wakati huo huo Stoke wamo mbioni kumsajili Wilson Palacios kutoka Tottenham kwa kitita cha paundi milioni 6 na kiungo huyo anajiandaa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Stoke katika siku za karibuni pia imehusishwa kutaka kumchukua mshambuliaji wa Spurs Peter Crouch.

Na vyombo vya habari vya Denmark vimesema mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner huenda yupo njiani kujiunga na Stoke.

Chelsea ilimsajili Lukaku kwa kitita cha paundi milioni 20 tarehe 6 mwezi wa Agosti. Ni mchezaji mashuhuri nchini Ubelgiji baada ya kuwa mfungaji bora katika ligi ya nchi hiyo msimu wa 2009-2010 alipokuwa na umri wa miaka 16.

Alifunga mabao 16 katika mechi 37 za ligi msimu uliopita na akafunga bao lake la kwanza katika mechi ya kimataifa Ubelgiji ilipoilaza Urusi mabao 2-0 mwezi wa Novemba.


Armand Traore wa Arsenal ajisajili QPR

August 31, 2011

Na BBC

Mlinzi wa kusoto wa Arsenal Armand Traore amejiunga na vijana wapya katika Ligi Kuu ya soka ya England QPR kwa kitita ambacho hakijasemwa.

Armand Traore

Armand Traore

Armand Traore mwenye umri wa miaka 21, anaondoka Arsenal baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka mitano akiwa ameshiriki mechi 23, amesaini mkataba wa miaka mitatu na QPR.

Traore anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na QPR chini ya mmiliki wake mpya Tony Fernandes, akifuatiwa na Joey Barton pamoja na Luke Young.

“Nilipozungumza na meneja Neil Warnock alionekana kuwa na matumaini makubwa nami katika klabu hiyo,” alisema Traore.

Traore aliichezea Juventus kwa mkopo msimu uliopita, lakini akawa anatafuta nafasi ya kuwa mchezaji atakayepangwa kila mechi.

Beki huyo atavaa fulana yenye nambari 13 katika klabu hiyo ya magharibi mwa London na Warnock amesema: “Armand amekuwa mchezaji nambari moja niliyekuwa namhitaji kwa muda mrefu.


Per Mertesacker kujiunga na Arsenal

August 31, 2011

Na BBC

Mlinzi wa Werder Bremen anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani Per Mertesacker anakaribia kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika klabu ya Arsenal.

Per Mertesacker

Per Mertesacker

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26- ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ya Werder Bremen inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga, pamoja ya kwamba yumo katika kikosi cha timu ya taifa hivi sasa, ameruhusiwa kusafiri hadi London.

Mipango ya Arsenal kumsajili Mertesacker, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6 aliyekwishacheza mechi 75 kwa timu ya taifa ya Ujerumani, inaweza ikawa ndio mwisho kwa klabu hiyo kutaka kumsajili mlinzi wa Bolton Gary Cahill.

Lakini Gunners pia wamo mbioni kumsajili beki wa kushoto Mbrazil Andre Santos.

Hatua ya wa meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuimarisha safu yake ya ulinzi, imetokana na timu hiyo kuadhiriwa kwa kuchapwa mabao 8-2 na Manchester United siku ya Jumapili katika Ligi Kuu ya England.

Hivi karibuni klabu hiyo ilimuuza mlinzi wake wa kushoto Gael Clichy kwa Manchester City, na mlinzi wa kuume Emmanuel Eboue kwa klabu ya Uturuki ya Galatasary, wakati siku ya Jumanne imemuuza Armand Traore kwa klabu ya Queens Park Rangers.

Mlinzi wa kati wa Arsenal Thomas Vermaelen aliumia akijiandaa kwa safari ya Old Trafford na msimu uliopita hakuweza karibu msimu mzima akiwa ameumia kifundo cha mguu.

Mertesacker alikuwemo katika kikosi cha Ujerumani kilichoilaza England mabao 4-1 katika Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Na ameitwa tena katika kikosi cha Ujerumani kitakachopambana na Austria katika mechi ya kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya siku ya Ijumaa baada ya kuumia kisigino mwishoni mwa msimu uliopita.


Pendejee Samuel Etoo Alipomwaga dola jukwaani

August 30, 2011

Ni kawaida kwa wanamuziki wa Congo kuwarusha Mapendejee na Meree safari hii ilikuwa zamu ya Kurushwa Samuel Etoo angalia jinsi alivyomwaga pesa na jinsi alivyomwaga mauno.

Pia utamuona Rogger Milla naye akichezeshwa jukwaani na wasanii hawa.


Wenger; Nimeaibishwa na Man U

August 30, 2011

Arsene Wenger aumizwa kwa mabao 8-2

Arsene Wenger amesema ameaibishwa kwa kuzabwa mabao 8-2 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

image

Arsene Wenger

Wayne Rooney alifunga mabao matatu katika mechi hiyo ikiwa ni mara yake ya sita kupachika mabao matatu katika mechi moja kwenye uwanja wa Old Trafford huku Manchester United kwa ushindi huo wakikamata usukani wa Ligi hiyo na kumuacha Wenger akiendelea kukabiliwa na mzozo unaokuwa katika klabu ya Arsenal.

“Bila shaka unajihisi kuabishwa unapofungwa mabao manane,” alisema meneja huyo wa Arsenal. “Ilikuwa siku mbaya sana.”

Wenger amesisitiza ni mapema mno kusema kama sera yake ya uhamisho imeingia dosari kufuatia kuondoka kwa Cesc Fabregas na Samir Nasri na kukosa kiungo wa kuchukua nafasi zao.

Lakini hivi sasa anakabiliwa na kibarua cha kusajili wachezaji kabla ya dirisha la usajili halijafungwa siku ya Jumatano saa tano usiku.

Wenger, ambaye amesisitiza hatang’atuka, anatarajiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Monaco, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini Park Chu-Young kabla muda wa usajili haujamalizika.

Pia anataka kusajili mlinzi wa kati na kiungo na Arsenal huenda ikarejea tena mbio za kumsajili mlinzi wa kati wa Bolton, Gary Cahill. Maombi yao mara ya kwanza yalitupwa.

Wenger, ambaye alianza kuwa meneja wa Arsenal mwezi wa Oktoba mwaka 1996, ameongeza kusema: “Hatuna budi kutafuta wachezaji wanaofaa na iwapo tutawapata tutawasajili. Pesa tunazo na iwapo tutawapata watakaoimarisha kikosi chetu tutafanya hivyo. Iwapo hatutafanya hivyo, basi itakuwa hatujawapata wachezaji hao wanaotufaa.

Baada ya Arsenal kufungwa vibaya mabao 8-0 mwaka 1896 ugenini na timu ya Loughborough Town katika ligi ya daraja la pili, Wenger ameongeza: “nahisi kufungwa huku kumetokana na hali maalum.

“Wachezaji wetu wengi hawachezi na tumecheza mechi tano tu. Tulichoka mwishoni lakini wachezaji wetu wanane muhimu hawakucheza.”

Meneja wa Manchester United Ferguson alitoa maneno ya kufariji akisema: “Tunaishi katika dunia iliyojaa kubeuana na vyombo vya habari vya habari vipo katika mashindano ya kutojali na kuwa tayari kumalizana.

“Ni vigumu kuelewa kwa wakati huu, lakini kazi iliyofanyika miaka 15 iliyopita sasa inaonekana ni ya ajabu sana.

“Alianzisha aina ya soka ya kipekee na mtindo wa usakataji soka wa aina yake na akachukua wachezaji wanaovutia kiuchezaji na pia amefanikiwa kuuza vizuri wachezaji. Hilo naliheshimu.”

Nahodha wa Arsenal Robin van Persie, ambaye alikosa kufunga mkwaju wa penalti uliookolewa na mlinda mlango wa United wakati Gunners walipokuwa nyuma kwa bao 1-0, amekiri timu yake haina budi kuimarika kabla ya mchezo ujao wa ligi utakaofanyika Emirates dhidi ya Swansea tarehe 10 mwezi wa Septemba.

“Hatuna budi kurudi katika mstari,” alisema mshambuliaji huyo. “Tutakabiliana na Swansea katika wiki mbili zijazo, ambao ni wapinzani wazuri na nausubiri kwa hamu mpambano huo.

“Sidhani kama tunaweza kujificha nyuma ya kivuli cha majeruhi ama kusimamishwa wachezaji. Hakuna kisingizio. Na wao wanao majeruhi pia, hii ni soka.”

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Lee Dixon amesema Gunners tayari hawakupewa nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini akasisitiza Wenger bado ni mtu anayefaa kwa kazi hiyo.


Eid Njema wadau

August 30, 2011

image


%d bloggers like this: