We ndio mchizi wangu-Remix yake Fid Q

February 7, 2009

“Bwana we mi hupenda hizi nyimbo maneno yake kusikiliza sijui hawa watu huwa wanawaza nini…” Maneno ya Balozi wangu Cisco Mtoro tulipokuwa tumekaa tunajadili mstakabali wa Muziki wa nyumbani na kundi la wanamuziki wa Kilimanjaro Connection kwenye kiambaza cha nyumbani kwa Balozi Mh. Cisco alipowaalika wanamuziki hawa nyumbani kwake kwa chakula cha mchana huko Kuala Lumpur Malaysia.

Kimsingi nataka kuongelea mashairi ya Bongo Flava, mbali na kuburudisha hizi nyimbo kwa kiasi ikubwa huwa na ujumbe na huweza kufikisha ujumbe kwa jamii moja kwa moja kwani mengi ya yanayoimbwa ni matukio ya kila siku yanayoigusa jamii na nyingi ni visa halisi vya maisha ya kila siku ya Mtanzania.

Sikiliza vichwa makini vilivyokutana na kutengeneza huu wimbo wa We ndio mchizi wangu ndani yake wamo Fid Q, Chid Benz, Mansu Li, Mh Temba, MWana FA, Geez Mabovu, Babuu, Ibra De Hustler, Jay Moe Mchopanga, K wamapacha.

Gonga player upate mambo


Fid Q

July 18, 2008
.

.

Anaitwa Fid Q Jabali la muziki wa Hip Hop nchini, Muziki wa kizazi kipya, hapa anadhihirisha kuwa ni mfalme hasa wa Hip Hop, mambo mazuri toka kwa Fid Q yako jikoni.


%d bloggers like this: