Werrason alivyo warusha Brussels.

June 30, 2010

Hii ilikuwa mwezi May mwaka huu pale Werrasson na Wenge Musica Maison Merre walipofanya onyesho huko Brussels Belgium na kuwachengua sana, Shukrani kwa mdau wangu Bielefelder mwenyewe anajiita The Most Dedicated and Passionate Wenge-ist, Heshima kwako na tuko pamoja.

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]

[image]


Sugu na Ruge malizeni tofauti zenu kimya kimya.

June 30, 2010

Ni muda sasa kwa wapenda burudani tumesikia bifu lililopo kati ya Joseph Mbilinyi aka Mr II / Sugu na Ruge Mutahaba bila kuwa na suluhisho lenye jitihada za makusudi.

Kwa wafuatiliaji wa burudani n stori za burudani bifu hii haijaanza leo na si ya juzi wakati wa Project ya Malaria kama inavyosemwa la hasha kwani ikumbukwe ni tangu Sugu hajaondoka nchini na aliwahi pia kudisi kimtindo kwenye moja ya nyimbo na video yake.

Inawezekana ukajiuliza mbona nimeandika hivi, ni kwa makusudi mazima nikiangalia mustakabali wa sekta ya burudani na hili lililopo ni wazi kuwa ugomvi unapanuka na kuingia kwenye matawi yao huku Sugu kwa upannde mmoja akitetea kile anachoita Muziki wa ukweli (hip hop) ambapo kwa sasa hamlengi Ruge tuu bali kama umesikiza ule wimbo (gonga hapa) utaona ni kwa umbali gani ugomvi huu umetanuka kwa kwena hata kwa watangazaji na wana THT ambao kwa upande wao watakuwa na chuki binafsi na msaanii husika au hata waliokaribu naye.

Hii ni hatari hasa kwa sekta ya burudani na wasanii kwani kuna kuwa na mgawanyiko na kuwatia uwoga wasanii wale ambao wanahisi wangetaka kumshirikisha Sugu kwenye nyimbo zao ama kwa kuogopa kuingia kwenye malumbano au kwa nyimbo zao kutopigwa redioni kabisa.

Ukisikiliza wimbo unaolalamikiwa (huo hapo juu)  utaona kuwa ni hasira za Mr. II kwenye kwa wahusika, na hii ni muendelezo ya bifu ninayoiongelea mimi.

Si vyema kuuongelea sana ugomvi uliopo sasa kwa kuwa jambo hilo liko kwenye vyombo vya dola lakini kama ilivyo soka ugomvi wa Sanaa na wasanii umalizwe na baraza la Sanaa ambalo hawa wasanii wote wako chini yake.

Hatupendi kufikia mahali kugawa hadi vyombo vya habari na waandishi kutokana na matatizo kati yenu ambayo kiukweli tatizo lililopo linaweza kusuluhishwa na vyombo husika kwa kuhusisha pande zote. Binafsi naimani Baraza la Sanaa ambalo hawa ni wadau wao wanauwezo na migogoro kama hii, hata sio kwa mwamvuli wa BASATA basi mlioko tumieni busara zenu kumaliza mpasuko kama huu.

Ni mtazamo tuu.


“Gerezani” ya huko China wakitengeneza VUVUZELA

June 29, 2010

image

Ndio ujue wenzetu wako makini sana kutumia opportunity kila zinapojitokeza, Majuzi makampuni kibao yameagiza Vuvuzela tokanje ilihaki kuna viwanda kibao vya plastic hapa lakini wameshindwa kuchangamkia na kujua soko linataka kitu gani kwa sasa.

Ripoti zinasema kuwa asilimia zaidi ya 90 ya Vuvuzela zilizouzwa huko Afrika ya Kusini zimetengenezwa China na kusafirishwa kilomita zipatazo 11,756.19 toka China hadi Afrika ya Kusini.

Angalia mshkaji alivyokomaa pekeyake na mzigo pembeni ama kweli penye miti hakuna wajenzi.

image

Gonga hapa usome zaidi.


“Hakuna Mwanajeshi abebay sifa ya kikosi kizima” Werasson

June 29, 2010

Kuna watu waliwahi kuondoka WMMM lakini pigo aliloacha Ferre Gola ama kwa hakika Werrason hatoweza kulisahau.

Ferre Gora aliondoka na wapenzi wake, kiukweli Ferre aliweza sana kuibeba WMMM lakini wenyewe kwa nyakati tofauti werasson aliwahi kusema WMMM ni sawa na jeshi ambalo hufanya kazi zake kwa kushirikiana hatuna sifa zinaweza kumuendea mpiganaji mmoja na kusema yeye anabeba jeshi zima. Sina uhakika na ukweli wa hayo lakini sikiliza wimbo huu wa 100 Kilos kisha uniambie nafasi ya Ferre kwenye jeshi la WMMM ilikuwa ipi?


Teknolojia ya goli yazua mjadala

June 29, 2010

Frank Lampard wa England

Frank Lampard akiwa ametaharuki baada ya kukataliwa goli lake wakati wa mechi ya timu yake ya England dhidi ya Ujerumani

Na BBC

Shirikisho la soka dunia FIFA limekataa kuzungumzia uwezekano wa kukubali kutumia teknolojia inayowezesha marefa kubaini ikiwa mpira umevuka mstari wa golini au la.

Mjadala kuhusu haja ya kutumika kwa teknolojia hiyo ulichacha siku ya Jumapili wakati wa mechi ya Kombe la Dunia kati ya Ujerumani na England, ambapo kiungo wa England Frank Lampard alikataliwa bao , licha ya mpira kuonekana wazi ukiwa umevuka mstari wa golini.

Baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 na kufuzu kwa robo fainali, Ujerumani sasa inasubiri kukutana na Argentina ambayo iliifunga Mexico mabao 2-1 na kujiandikishia nafasi miongoni mwa nane bora.

Mchuano kati ya Argentina na Mexico pia ulichochea mjadala kuhusu teknolojia ya kubaini goli, baada ya Carloz Tevez kuifungia Argentina bao la kwanza , akionekana ameotea.

Lakini katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kwenye Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, msemaji wa FIFA Nicolas Maingot alisema pahali pa kujadiliwa swala hilo sio kwenye Kombe la Dunia.

Alisema uamuzi wa kutotumiwa kwa teknolojia hiyo uliafikiwa na bodi ya kimataifa ya vyama vya soka ambayo pia inashirikisha FIFA na Uingereza, na kwa hivyo hakuna uwezekano wa kubadilisha uamuzi huo.

Sepp Blatter

Sepp Blatter, FIFA

Maingot pia aliongeza kusema FIFA haitaruhusu matukio ya uwanjani yenye utata kurudiwa kwenye skrini kubwa zinazowekwa ndani ya viwanja kama ilivyofanyika kufuatia bao la Carlos Tevez, hatua ambayo ilisababisha mabishano uwanjani.

Rais wa FIFA Sepp Blatter ambaye alipinga kutumika kwa teknolojia ya mstari wa golini alikuwepo katika uwanja wa Free State mjini Bloemfontein wakati England iliposhindwa 4-1 na Ujerumani, na kushuhudia refa kutoka Uruguay Jorge Larrionda na msaidizi wake Mauricio Espinosa wakishindwa kutambua kwamba mpira uliopigwa na Frank Lampard ulivuka mstari wa lango la Ujerumani.

Baada ya mechi hiyo kiungo huyo wa klabu ya Chelsea alitoa wito wa teknolojia ya mstari wa golini kuanza kutumika ili kuwasaidia marefa.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron pia ni miongoni mwa wale waliosisitiza teknolojia hiyo ianze kutumika.

Tetesi za rais wa FIFA Sepp Blatter za kukataa teknolojia hiyo ni kwamba hatua ya kusimamisha mechi ili kuthibitisha ikiwa mpira umevuka mstari au la itavuruga mtiririko wa mchezo na engine hata kuinyima timu fursa ya kufunga bao.


Soyon Serieux ya JB Mpiana kutoka rasmi kesho!!!

June 29, 2010

Video ya Onyesho la JB Mpiana Live FIKIN wimbo wa Soyons serieux

Albamu inayosubiriwa kwa hamu huko Congo na kwingineko ya Soyon Serieux ya kwake JB Mpiana inatarajiwa kutoka rasmi kesho.

Kwa mujibu wa msemaji wa kundi Roger Ngandu amesema kuwa, matarisho yoote yako tayari na albamu itakwenda sokoni kesho Mungu akipenda.

Akiongelea Video ya Albamu hiyo Ngandu amesema kuwa bado hazijakamilika ila kwa ushirikiano na Manuruvaka mambo yatakuwa tayari karibuni.

Ili kujua kionjo kwenye hiyo albamu mpya gonga player usikie ni nyimbo mpya.


Tiketi za onyesho la Werrason CANADA mwezi wa Tisa zaanza kuuzwa leo!!

June 29, 2010

image

Mwanamuziki Werrason Ngiama na kundi lake la Wenge Musica Maison Merre (WMMM) watatumbuiza kwenye uwanja wa Olympique huko Montreal Canada mwezi Septemba mwaka huu. Ajabu ni kuwa ticket kwa ajili ya onyesho hilo zimeanza kuuzwa sasa na inasemwa kutakuwa na idadi kamili ya Ticket ambazo zikifikiwa basi hakutauzwa tiketi tena. Kwa kawaida maonyesho yanayofanyika hapa hujuisha waafrica toka Canada, Marekani na nchi jirani na mara nyingi huwa yanakuwa na watu wengi sana.!! Habari ndio hiyo!!


%d bloggers like this: