Muungano wa Africa Mashariki na Magharibi Kimuziki

February 28, 2009

NI RAY C NA RF CHORD

Original ya wimbo huu uliimbwa na Ray C Peke yake ikiwa ni Remix ya wimbo wa Sikuhitaji wenye mahadhi ya Taarabu enzi hizo alipopachikwa jina la Kiuno bila mfupa, Wanamuziki wa Bongo Flava wameamua kwenda kimataifa kwani Ray C aliamua kuukarabati huu wimbo na kuuimba tena akishirikiana na mwanamuziki RF Chord toka Siera Leone ambaye makazi yao ni MAshariki ya MBali, Wimbo huu kwa RF Chord unaitwa YAWO, RF Chord ni wanachama wa UMPA [Union Movement of Performing Artists of Sierra Leone] ,

Wakiwa ni moja ya vikundi vya muziki vyenye chart ya juu kabisa nchini mwake Siera Leone.
RF Chord ambaye anatumia zaidi mtindo wa “Dance Hall” huku akichanganya na midundo ya asili kwa nyimbo zake nyingi amejipatia umaarufu sana na Wimbo huu aliopiga na Ray C.

Hii inasaidia kuufanya muziki wa Kizazi kipya kutambulika zaidi ingawaje kwenye wimbo huu Ray C aliuimba kwenye mahadhi ya Kipwani zaidi, ukiwa ni Remix ya wimbo wake wa Sikuhitaji ambayo ilipigwa kitambo kidogo,

Hivi karibuni tumesikia Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi Uingereza Blanchard Deplaizir akifanya kolabo na baadhi ya wanamuziki wa TAnzania akiwemo Lady Jay Dee, BAnana na wengineo, Pia Kolabo ya AY na P Square.

Shime kumekucha muziki huu umekubalika nchini ni wakati wa kuuza kimataifa na kwa jinsi hii mtatoka tuu.
Pata burudani kwa kubofya Player…


David na Victoria Bekham wazindua Mishumaa maalum kuchangia mfuko maalum.

February 28, 2009

bkm Mwanasoka mahiri David Bekham na mkewe Victoria Bekham wametoa toleo maalum la mishimaa yenye manukato kwa ajili ya kuchangia watoto wenye mahitaji maalum.

David na Victoria walizindua mishumaa hiyo majuzi tarehe 25 Feb ambapo MShumaa mmoja utauzwa kwa Pound 20 (Tsh 60,000) na Pound 2 zitaingia kwenye mfuko maalum.

Mishumaa hiyo ambayo imetngenezwa kwa nta inayotokana na mimea hasa ya Palm (jamii ya minazi) na manukato ya ua Rose (vegetable wax blended with the fresh aroma of tuberose).

Kwa wanaotaka kununua moja wa moja bofya hapa


Msimamo wa mtanange wa CHAN uko kama ifuat

February 26, 2009
GROUP A
02-22-2009 Cote d’Ivoire 0 – 3 Zambia
02-22-2009 Senegal 1 – 0 Tanzania 
02-25-2009 Zambia 00 Senegal
02-25-2009 Tanzania 1 – 0 Cote d’Ivoire 
02-28-2009 Cote d’Ivoire 16:00 Senegal 
02-28-2009 Zambia 16:00 Tanzania 
Group A
Team MP W D L GF GA GD Pts
Zambia 2 1 1 0 3 0 3 4
Senegal 2 1 1 0 1 0 1 4
Tanzania 2 1 0 1 1 1 0 3
Cote d’Ivoire 2 0 0 2 0 4 -4 0

Taifa Stars yaichapa Ivory Coast 1-0

February 26, 2009

Goli la Mrisho Ngasa limewapa matumaini watanzania kwa timu yao kusonga mbele ingawa bado ina mechi moja mkononi.

TAifa stars huku ikicheza kwa kujiamini imewatoa nishai wenyeji wa michuano hiyo Ivory coast kwa kuwachama bao moja bila majibu kwenye mchezo uliochezwa hapo jana.

Wachezaji mahiri wa Ivory Coast kama Karamoko Alassane, Guehi Kouko na N’gossan Antoine waliisumbua sana ngome ya Stars na walishangiliwa kwa nguvu kila waliposhika mpira.

Kwa mujibu wa matangazo ya Television iliyokuwa inaonyesha live kwenye mtandao Taifa Stars walionyesha kuumudu na mara kwa mara mtangazaji alikuwa akisema Taifa Stars walionyesha kiwango cha hali ya juu tofauti na alivyoifahamu.

KWa sasa TAifa Stars inahitaji kushinda na msemo wa adui muombee njaa ndio pahala pale kwani Taifa Starz ikishinda itakuwa na Point 6 au ikitoa Droo itakuwa na point 4 na hivyo kuipiku Zambia na Senegal.

kikosi cha mauaji

Mechi ya ufunguzi TAifa Stars ilipoteza mchezo kwa Senegal ikafungwa kwa taabu 1-0.

Kocha Maximo amesema kuwa anaauhakika vijana wake watafika mbali kwani wamezoea mashindano kwa sasa.

Go stars gooooo!!!


Stigo Mwamba, toka mwana bongo flava hadi Prodyuza.

February 25, 2009
  • Ndoto yake ni kufanya Albam na kundi lake la awali la Deplomatz
  • Studio yake imeuza beat kwa Foxbrown
  • Anamkubali sana AY

stigo1 Katika pitapita za Spoti na Starehe nilikutana na mmoja wa waanzilishi wa Kundi la Diplomatz, kundi ambalo lilikuwa moja ya chachu za muziki wa Bongo Flava wakati huo ukiyataja makundi kama GWM, Deplomatz, Kwanza Unity, Hard Blasters etc, Hapa nauongelea Stigo Mwamba. ambaye anatupa machache kuhusu maisha yake y sasa, Stigo anaishi huko Sayville, New York, USA akiwa anajishughulisha na muziki bado na anaongoza lebo yake inaitwa S & S Recording Studios.

Nilianza kwa kumuuliza maendeleo yake kimuziki kwa sasa na kama bado anajishughulisha na Muziki.

Stigo: Maendeleo yangu ya music yanaendelea vizuri and i took another level baada ya kuamua kuwa producer,when i got here in New york city (The city of dreams).

Vipi ulipoondoka nakumbuka tuliagana kuwa unakwenda kupiga shule ufanye kazi za kiofisi kulikoni?

Stigo: mawazo yangu yote yalikuwa kuhusu shule nilikuwa nataka kusomea Computer Engineering but at the same time the otherside of me wanted to do music so i changed my mind and i did sound productions.

stigo123Sehemu ya vyombo vya S & S, mwenyewe anasema hii ni set ya mazoezi tuu kazi kwenu. 

Je umewezaje kufikia kuwa na Studio yako kama unavyosema ulienda shule na ulifanya mambo ya muziki, ninavyojua vyombo vinagharimu kidogo

Stigo: baada ya kumaliza shule nikawa nafanya kazi at the same time nilikuwa nasave fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya studio,Then nikaanza kuhang out na watu waliomo kwenye business ya music ( big names kama vile Dj Rob E Rob wa Club Therapy ya New York City,90’s R& B singer from Roc a fella records RELL, etc) but all that time i never hit any studio till 5 yrs ago when i went to studio with Cashmere (NYC’s Hottest Underground Rapper) i saw some producers there n i was a big surprise that day after i came up with best ideas n thats when i knew it was about time for me to open my own studio,so i kept saving money till last year when i opened my 1st studio called it S & S Records and 2 month later i opened another one n change the name from S & S Records to S & S Recording Studios.

Je Studio hizi ziko wapi?

Stigo: One is located in Long Island,NY and another one Brooklyn,NY.

Je wewe binafsi bado unaimba kama zamani ama?

Stigo: mhhh well im still writing but im into producing more n sometimes i make some freestyles for myself so i can listen in my car while im driving.

Je kazi zako zimeshapata kusikika, nikiwa na maana kuna mtu ambaye anang’aa kwa sasa akiwa ni matunda ya studio yako?

Stigo: Well,actually wat i do is im making beats n sale them so the ppl who buy beats can do anything they want most of ppl who buy beats they buy ideas n take the sounds they like,The big name i sold beat to till now r Foxbrown she used one of my beats for her underground freestyle, The hottest Spanish Rapper which i did the all song for him,His name is De la Ghetto the song called Tato – Remix you can find that song on http://www.youtube.com by writting Tato remix by De la Ghetto. n a lot of underground hits which u can find them in youtube.com.

Kwenye mwezi wa nane kuna upcoming artist name Shanice Stevens is the R&B artist,she is comin with an album from Sony, i got one song on that album.

Je tukirudi nyuma enzi za Deplomatz kuna chochote ambacho unajutia na kuhisi ungefanya ukiwa na kundi hilo?

Stigo: kwa kweli hakuna chochote nachojutia katika kundi langu la Deplomatz unajua miaka ile ya 90 was all bout having fun we werent into business that much its not like the way it is right now. But still we gotta do 1 more album for our funs just for fun n everything will be on me thats my Dream.

stigo

Toka kushoko Shaka, Jamaa wawili ndio wa kundi la Ta To De La Ghetto na kulia ni Stigo mwenyewe

……………………………………………………….

huoni umuhimu wa kuchangia ujuzi wako na wanamuziki wa nyumbani kwa kuweka studio yake pale na kusaidia kukuza muziki wa nyumbani?

Stigo: I was thinking of Opening a high quality (American level) studio ( high def sound) in Dar since i have a good connections with guitar center( one of American big music equipments store), possibly a Company ya kurekodi video/ movie even a club.

Kuna mengi yamefanyika kwa muziki wa nyumbani wa Bongo Flava enzi za miaka ya tisini na kizazi cha sasa cha 2000, JE binafsi yako unaona tofauti yeyote?

Stigo: Tofauti ipo kubwa kupindi chetu na hiki wakati wetu was all bout messages but this time its all bout club bangers means nice danceble beats which is good too.Siku hizi sipati muda wa kusikiliza sana bongo flava but i know few of them i wish ningekuwa nawajua wote ningekupa jibu zuri but for wat i know i really feel AY the kid is doing it,he is good,Mwana Fa is good too na mwanangu mwenyewe Fred Malik wa wagosi wa kaya ( i dont really like the style they use but i think they do good to their fans which is really matters ).

stigo12

Kuna channel mbili ambazo vijana wanaimba nyumbani ikiwa ni Hip Hop na Bongoo flava, wengi wanalalamika Hip Hop haibambi je una lolote juu ya hili?

Stigo: kwa soko la hip hop bongo i cant lie i really dont know i havent been there for like forever!!!,lol.

Je unadhani nini kifanyike muziki wetu utoke nje ya Africa Mashariki?

Stigo: Quality is the most important thing,if we have high quality productions n videos def tutauza music wetu kimataifa sababu music wetu sio mbaya na wanamusic bongo wanajitahidi ile mbaya ila quality ndiyo inawaangusha.

Nashukuru mkuu kwa muda wako karibu sana Spoti na Starehe.

Stigo: Big up nashukuru saamu kwa wote


Tifa Stars yapoteza mchezo wa kwanza 1-0

February 22, 2009

Mpira umekwisha kati ya Taifa Stars na Senegal huko Abdijan na matokeo ni kwamba tumepewa kimoja bila majibu.

No sweat bado nafasi tunayo kwani tutacheza na wenyeji ambao washakula mabao matatu toka kwa Zambia kwenye mechi ya ufunguzi.


Tiketi kombe la Dunia 2010 zaanza kuuzwa leo hii!!

February 20, 2009

Ticket za kuona mashindano ya Kombe la Dunia mwakani huko Afrika ya Kusini zinaanza kuuzwa leo huko nchini Afrika ya Kusini kwa mbwembwe za aina yake ambapo tiketi ya bei ya chini ni Tsh 27,000/=

Leo hii waganga wa jadi na wananchi wapenda michezo walikutana huko Port Elizabeth kwa ajili ya kutambika kwenye moja ya kiwanja ambacho kitatumika kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa ya soka.

Maafisa wanasema wananchi walioko nje ya Africa ya Kusini watatumia mtandao kukata Ticket hizo na wale walioko ndani watanunua tiketi kwa kutumia fomu maalum ambazo zinapatikana kwenye Benki ya FNB National Bank ambayo imezagaa nchini kote.

Maofisa wanasema kuwa mipango yote imekamilika na sasa hii itawapa mtazamo wa mapokeo toka kwa mashabiki.

Michuano ya Kombe la Dunia inatazamiwa kuanza mwakani huko nchini Africa ya Kusini.

Bei ya Ticket iko kama ifuatavyo:-
Siku ya Fungua dimba: $200-$450.
Mechi ya raundi ya kwanza: $80-$160.
Round of 16: $100-$200.
Robo fainali: $150-$300.
Nusu fainali: $250-$600.
Fainali: $400-$900.


%d bloggers like this: