TOP 5 YA KILLY MUSIC AWARDS 2011 HII HAPA…

February 28, 2011

image

image

image

image

image

image


Geco Bouro Mpela, Mdogo wa Allain Mpela aliyetesa kwa Koffi

February 28, 2011

Anaitwa Geco Bouro Mpela ni mdogo wake na Alain Mpela kijana machachari sana aliyekuwa akiimbia kundi la Wenge Musica. Geco Mpela ni matunda ya Koffi Charls Olomide na baada ya kuiva aliamua kutoka kivyake na wakati fulani akishirikiana na kaka yake Alain Mpela walitoa Albam yao iliyoitwa Mortal Combat, ambayo kwa kiasi fulani ilifanya vizuri. I*nasemekana kuwa Koffi alikuwa akimtumia Geco kumshawishi kaka yake Allain Mpela ajiunge na Quartier Latin ya Koffi bila mafanikio, Kwani kwa Koffi uhodari wa Wenge BCBG ulikuwa ni tishio kwa ngome yake kwani ulisababisha kugawana mashabiki jambo ambalo yeye binafsi hakulipendelea.

Geco Mpela na Allain Mpela, Wawili hawa wanatoka kwenye familia ambayo kiasi fulani inajiweza huku kaka mtu Allain Mpela kiwa ni mwanajeshi aliyeihasi kambi na ndio maana kila alipofikia kuimba JB Mpiana alikuwa akimuita “Afande” kama jina lake la utani.

 

Geco Mpela kwa sasa anafanya kazi kibyake huku akiwa na albamu hiyo yenye wimbo ulioshika wa

Vice de Procedure Nakutakieni jumatatu njema na wiki njema.

Kili Marathon & Vodacom’s 5km FUN RUN 2011 kwa Camera ya Michuzi

February 28, 2011

Pikipiki

 

Wanaume… eeeeh!

Maji maji….

Jamani eeehh… si nimekwambia ntakulipa nikimaliza hii marasoni???

 

Mbio mbio mbio…

Tanzania oye!


Bongo Movie yalala 2-0 kwa Bongo Flava

February 28, 2011

Sehemu ya umati wa mashabiki wakishuhudia mchezo baina ya Wapaka Poda (Bongo Movie) na Wabana Pua (Bongo Flava). Mchezo uliomalizika kwa Bongo Flava kushinda bao 2-0 Magoli yaliyofungwa na mchezaji mahiri H Baba.

Posted with WordPress for BlackBerry.


Man U, Marseille nguvu sawa

February 24, 2011

Olympic Marseille ya Ufaransa imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare tasa na Manchester United ya England.

Marseille

Marseille watoka sare na United

United ambao walisafiri kwenda Ufaransa bila ya wachezaji wao watano wa kikosi cha kwanza walihimili vishindo vya Marseille.

Hata hivyo haukuwa mchezo wa kusisimua sana kama michezo mingi katika ngazi ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya.

Gomez

Mario Gomez

Katika mchezo mwingine, mabingwa watetezi Inter Milan ya Italia nayo imeshindwa kutamba mbele ya Bayern Munich ya Ujerumani baada ya kufungwa 1-0.

Goli ya Bayern Munich limefungwa na Mario Gomes katika dakika ya 90.


Arsenal yainyatia United kileleni

February 24, 2011

 

Arsenal imeisogelea Manchester United kileleni katika ligi kuu ya England, baada ya kuichapa Stoke City kwa bao 1-0.

Bao hilo pekee na la ushindi limefungwa na mlinzi Sebastien Squillaci katika dakika ya 8.

Arsenal

Squillaci

Hata hivyo ushindi huo umetiwa doa, kutokana na wasiwasi baada ya nahodha Cesc Fabregas na Theo Walcott wakitoka uwanjani kutokana na majeraha.

Walcott awali aligonga mwamba na shuti lake, kabla la Squillaci kupiga kichwa mpira wa krosi ya Niklas Bendtner.

Stoke walijaribu kujibu mashambulizi, lakini kipa Wijciech Szczesny alizuia mkwaju wa John Carew, kalba ya mkwaju mwingine wa Robert Huth kupita juu kidogo ya mwamba wa Gunners.

Kwa matokeo haya, Arsenal wako pointi moja tu nyuma ya United walio kileleni.


Mamito Sofia wa Kessy

February 23, 2011

kessy

Anaitwa Mamaa Sofia wa Kessy si mpiga Tumba la hasha bali ni katika misele yake ya kukusanya matukio kwenye kipindi chake mwanana cha Mama Land kinachorushwa na Clouds TV kila siku ya Jumamosi, Alipoongea nami muda si mrefu Mamaa Sofia wa Kessy anakwambia Mama Land ya jumamosi hii si ya kukosa.


wamkumbuka Tutu Caludji wa Wenge BCBG?

February 23, 2011

image

Wakati Wenge Musica BCBG wakianza walikuwa na rapper (atalaku) mmoja alikuwa akiitwa Roberto Wunda ikokota ambaye anasemwa kuwa ndiye baba wa ghani za muziki wa Lingala leo hii. Huyu bwana inasemekana alipata tatizo la Cancer ya koo, wakati kabla hajazidiwa siku moja wakiwa katika onyesho lao la kawaida alishindwa kuimba kabisa na hivyo wakati huo akiwa hajulikani Tutu Caludji alisema anawza kuchukua nafasi yake na aliimudu na hivyo ndio ukawa ujio wake kwenye ulimwengu wa Muziki wa Congo.

Caludji ambaye amezindua Albamu yake tarehe 14 February mwaka jana kwenye siku ya wapendanao huko Ufaransa, albamu ambayo inakwenda kwa jina la Paris Match. albamu hiyo ina nyimbo 12 ambapo 8 kati yake ni Rhumba ambapo binafsi amesema kuwa anawazimia sana papa Wemba na Bingwa mwingine Lokua Kanza.

Caludji ameshirikisha watu tofauti kuleta ladha ambapo yumo King David aliyewika na Wenge Musica Maison Merre na jamaa mwingine mkali toka Ivory Coast ambaye alikataa kumtaja kwa sasa.

Caludji alifanya vyema sana kwenye albamu karibu zote za Wenge hasa baada ya kutengana na Werasson anasikika vyema kwenye Titanic, Internet, TH na nyingine huku akiwa na wimbo wake wa Tshico Londonien ambao alitokea kupendwa sana aliutunga akiwa na Wenge BCBG. dulla muzee wa Tigo anasema kuwa jamaa hapa aliimba si mchezo, na huu ndio ulikuwa mwanzo wa kuonyesha uhodari wake kwenye kuimba badala ya kughani zaidi.

Caludji aliamua kutoka solo ikiwa ni muendelezo wa mmomonyoko wa Wenge na kuendeleza Clan Wenge.

Kuna wakati JB Mpiana alimhusisha Didie Kinuani na maadili mabaya ya wanamuziki wake kwa kupenyeza faranga ili aweze kuisambaratisha Wenge ya JB Mpiana. Ikumbukwe kuwa huyu Didie Kinuani ndiye aliyefanya mipango ya kumuachisha Mpiana na Mkewe, na yeye kumuoa. alipokuwa anafanya mipango hiyo alimuomba Werrason na Bendi yake ya WMMM kutumbuiza lakini Werrason alikataa akisema kuwa hawezii kufanya hivyo kwa kuwa yeye alikuwa mmoja wa washenga wakati JB Mpiana alienda kumchumbia mkewe huyo. Bahati kwa sasa JB Mpiana Alirudiana na mkewe.

Kinuani pia alihusishwa na kutoka watu kama Titina Alcapone ambaye ye alitoka kipindi JB Mpiana na Koffi walikuwa hawapatani na wakati Titina alipooa Koffi ndio alikuwa Best Man wake, jambo ambalo JB Mpiana hakulifurahia na hivyo mahusiano yake na Titina yalitetereka na baadaye aliamua kutoka Wenge.

Kwa sasa Caludji anamiliki Bendi yake mwenyewe huku akiwa na Albamu tayari, kuna wakati inasemekana Zadio Congole ambaye ni shabiki mkubwa sana wa JB Mpianana alitaka kuwarudisha Allain Mpela, Titina na Tutu Caludji ili kurejesha ladha ya zamani, lakini walionyesha kuukwaza mpango mzima na alihojiwa JB Mpiana alisema kuwa Wenge ni kama timu ya Taifa kila siku vipaji vinazinduliwa.

Kundi la Wenge Musica lina kikosi chake kinaitwa PPU ambacho kinatumika kulisha kikosi kikubwa, unapoiva kwa PPU basi uhodari wako utakuingiza Wenge BCBG.

Basi leo Naomba nikusikilizishe wimbo huu Tchico Londonien utunzi wake Tutu Caludji alipokuwa na wana BCBG baada ya kupanguka kisha amua mwenyewe.

Mdau wangu Papaa Likolo uliyeniuliza Caludji yuko wapi nadhani marudio ya post hii yamejibu swali lako, Heshima kwenu mashabiki wangu usisite kuniambia unataka kusikia nini au niandike nini na kama una chochote unataka kushare na wadau basi niandikie kwa piusmicky@yahoo.co.uk


Nafasi ya kazi: Muandishi anahitajika haraka

February 23, 2011

 Blogging-Writer-Therapy

Anahitajika muandishi wa habari za Michezo na Burudani kwa ajili ya Blog hii ya Spoti na Starehe.

Sifa za muandishi ninayemtaka “:

  • Uwezo wa kuandika habari kiufasaha na zenye uhakika
  • Uwezo wa kutafuta habari zenye mvuto hasa kwa vijana
  • Kuleta habari kwa wakati
  • uwezo wa kutuma walao habari tano kwa siku
  • Kama una uwezo wa kuandika makala za burudani utafikiriwa zaidi

Muandishi awe na vifaa vyake na jinsi ya kuleta habari unatuma kwa njia ya mtandao (utawezeshwa modern kwa ajili ya internet kutuma habari)

Maombi yatumwe kwa piusmicky@yahoo.co.uk uonyesha na mapendekezo ya malipo yako.

Mwisho wa kutuma maombi ni wiki mbili tangu tarehe ya tangazo hili. Kwa habari zaidi unaweza piga simu 0713 666616 au Email: piusmicky@yahoo.co.uk


Mambo ya Nathan Kijasti

February 23, 2011

mkorogo 1


Msimamo ulivyo sasa

February 23, 2011

Jumatano, 23 Februari 2011 00:00 UK

Position Timu M TG PNT
1 Man Utd 26 32 57
2 Arsenal 26 29 53
3 Man City 27 19 49
4 Tottenham 27 7 47
5 Chelsea 26 24 45
6 Liverpool 27 3 39
7 Sunderland 27 0 37
8 Bolton 27 1 36
9 Newcastle 27 4 35
10 Stoke 26 -2 33
11 Blackburn 27 -8 32
12 Blackpool 27 -9 32
13 Fulham 27 0 31
14 Everton 26 -3 30
15 Birmingham 26 -10 30
16 Aston Villa 27 -15 30
17 West Brom 27 -17 28
18 Wigan 27 -18 27
19 West Ham 27 -18 25
20 Wolves 27 -19 25

Evra, Giggs wamwaga wino tena Man U.

February 22, 2011

Evra

Defender Patrice Evra wa Man United amemwaga wino kwenye klabu yake na hivyo kuwajibika kuichezea hadi hapo 2014. Hii inakomesha uvumi kuwa Evra alikuwa kwenye harakati za kuhamia klabu ya Hispania ya Real Madrid.

Evra mwenye miaka 29 tayari ameshaisaidia klabu yake ya Man U kuchukua vikombe vitatu vya Ligi ya Uingereza kama wakichukua na hiki kitakuwa cha nne.

Wakati huo huo mchezaji mkongwe wa klabu hiyo Ryan Giggs amesaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja kuongeza kuichezea timu yake ya Man United.

Huyu ni mchezaji mwenye muda mrefu klabuni hapo na inasemekana anaweza kuja kuchukua ukocha wa klabu hiyo kongwe ambayo ameifungia bao kwenye kila msimu wa maisha yake klabuni hapo.


Djojo Ngonda ya Fi Carre Mwamba na Wenge BCBG

February 22, 2011

Kwenye Wenge BCBG ya wakati huo kulikuwa na mtu anapiga gitaa la Rhythim anaitwa Fi Carre Mwamba, huyu jamaa alikuwa ana uwezo mkubwa sana kwenye zana na ndiye alikuwa akiwapanga wapiga magitaa wengine akiwemo Patient kusangira, Allain Prince Makaba na wengineo.

Mbali na uwezo wake mkubwa mkubwa wa kupiga gitaa pia alikuwa mtunzi, kibao hiki kiliimbwa kwa kiasi kikubwa na Werasson pamoja na Adolph Dominguez akishirikiana na machampion wengine ni utunzi mahiri wa kijana Fi Carre Mwamba. Wakati huo list ilikuwa imekamilika kila idara.

Albamu hii ni moja ya albamu zenye mafanikio makubwa kwa kundi la Wenge kama Wenge ambapo kila mmoja alipata nafasi ya kumamua na vijana walikamu vilivyo, hebu sikiliza kisha uniambie wewe unakumbuka nini ukisikia nyimbo hizi, Mi namkumbuka Jema Mandari huyu jamaa alikuwa akiupenda sana huu wimbo, pamoja na wana BCBG woote bila kuwasahau Werassonique.


Chelsea yaizaba Copenhagen 2-0

February 22, 2011

Chelsea imezinduka baada ya kutolewa katika kombe la FA na kuizaba FC Copenhagen kwa mabao 2-0 katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.

AnelkaAnelka na Drogba, ambaye alianzia benchi

Mabao yote mawili ya Chelsea yamefungwa na Nicolas Anelka katika dakika za 17 na 54.

FC Copenhagen wakicheza nyumbani hawakuonesha cheche zozote, na kuifanya Chelsea kucheza kwa uhuru katika mchezo wa kwanza wa timu 16 bora.

Mshambuliaji mpya wa Chelsea Fernando Torres licha ya kuanza, bado hajaweza kupata bao lake la kwanza kwa timu hiyo. Drogba alianzia benchi.

Katika mchezo mwingine Real Madrid ililazimishwa sare na FC Lyon ya Ufaransa kwa kutoka sare ya 1-1.

KarimKarim Benzema

Karim Benzema, alifunga bao hilo la Real, muda mfupi baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba baada ya Emmanuel Adebayor kutoka katika dakika ya 65.

Bafetimbi Gomis wa Lyon alisawazisha bao hilo katika dakika ya 85.


Waoooooo baba!!

February 17, 2011

Kila Kinyozi ana Kinyozi wake; Arsenal yainyoa Barca

February 17, 2011

Nakupa Dozi ya “Aspirine” yakwake Koffi Olomide

February 17, 2011

Kuna wanamuziki wachache sana wenye uwezo wa kuimba wimbo mmoja mwanzo hadi mwisho na bado wakakuacha unatamani kuendelea kuusikiliza. Kama unakubaliana na mimi basi Koffi ni mmoja wapo, Wataalamu wa muziki wanasema Koffi anazaidi ya sauti saba ambazo anaweza kucheza nazo akiaanzia kuimba sauti ya chini sana ama ya bass sana.

Hii ni strength kubwa ya Koffi na ndio maana amekuwa akifanikiwa sana kwenye nyimbo zake kwani pale ambapo anataka uimbe kama ye anavyotaka ukishindwa basi anapanda mwenyewe.

Huu ni mmoja ya nyimbo zake za Rhumba ambazo zilitokea kupendwa na kila unapopigwa mwili wangu husisimuka sana. Vijana wengi ambao walitoka kwa mwamba huyu walifanikiwa kimuziki na wamekuwa moto wa kuotea mbali kwenye game nzima ya Muziki.


Nahodha wa AC Milan Gattuso aomba radhi

February 17, 2011

Nahodha wa AC Milan Gennaro Gattuso ameomba radhi kwa kumpiga kichwa kocha wa Tottenham Joe Jordan, baada ya timu yake kulazwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa timu 16 kuwania ubingwa wa Ulaya.

Gattuso akimkaba koo Joe JordanGattuso akimkaba koo Joe Jordan

Gattuso anayechezea pia timu ya taifa ya Italia, alizozana na Jordan mwenye umri wa miaka 59 na baadae akamsukuma kichwani.

Nahodha huyo wa AC Milaa mwenye umri wa miaka 33 ambaye siku za nyuma aliwahi kuichezea klabu ya Rangers ya Scotland, anasubiri kuadhibiwa kutokana na vitendo vyake vya utovu wa alivyoonesha uwanjani.

“Nilishindwa kujizuia,” alisema Gattuso, ambaye awali alimsukuma Jordan usoni. “Hakuna kisingizo kwa niliyoyafanya. Nabeba lawama zote kwa yote hayo.” Read the rest of this entry »


Feux De L’Amour (Moto wa Mapenzi) Wimbo wenye ujumbe murua wa Mapenzi kwa kizazi cha sasa.

February 13, 2011

JB Mpiana ni mwanamuziki ambaye anasifika sana kwa Rhumba za uhakika na zenye mguso hasa,

Leo nitakuchezea kibao chake kinaitwa Feux De L’Amour akimaanisha mioto ya mapenzi.

Kwa wasiojua lugha iliyotumika humu JB Mpiana alikuwa akiongelea mapenzi ya sasa akiwalalamikia akinadada akisema kuwa yapo wapi mapenzi ya ukweli ya enzi za mababu zetu ambapo watu walikuwa wakipendana kiukweli tofauti na siku hizi ambapo akinadada wamekuwa wakichagua wanaume kila mtu anataka mwanaume aliyesoma, mwanaume alina kazi nzuri, mwenye pesa, inakuwaje kwa wale ambao hawajasoma? Inakuwaje kwa wale ambao hawana kazi nzuri na hawana pesa?

kiujumla ameongelea mtaguso wa mapenzi wa sasa ambapo nadharia nzima ya mapenzi ni unanini? wewe ni nani? na dhana hii ndio inayojenga mapenzi kwenye ulimwengu wa sasa.

Hii si tafsiri sahihi ni majumuisho ili kukupa nini hasa kimeongelewa kwenye wimbo huu, naungana na Bw. Shaibu Thabit ambaye amenitumia tafsiri ya Wimbo huu kama ifuatavyo:-

L’amour est-ce aimer ou etre aimer? Bien que L’amour soit Le symbole d’un sentiment partage, etre aimer n’est jamais le signe d’un bonheur parfait = Je mapenzi ni kupenda au kupendwa? ingawa mapenzi ni ishara ya kubadilishana hisia, kupendwa kamwe si maana ya faraja iliyokamilika.

Bolingo eza maladie mabe dokotolo nango motema symptoma nango souci, kasi kisi nayango se presence ya motooyo ozali kolula, Lokola nalula masiya ye nde kisi nangai= Mapenzi ni ugonjwa mbaya, Dalili yake ni mawazo lakini dawa yake ni kuwepo kwa umpendaye,kama navyompenda Masiya(Yesu) ndio dawa yangu.

Bolingo lokola maladie contagieux tuna na bamoureux decus tuna na B’aveugles d’amour surtout na badivorces, Bakopesa yo temoignage na bango okoyoka mawa, okoyoka ngolo, okotikala stupefart, se kokamwa kamwa mama, se koimbaimba mama, se kotuna tina nzambe akela L’amour = Mapenzi kama ugonjwa wa kuambukiza lazima uwaulize waliokosa kupendwa, waulize vipofu wa mapenzi, waulize walioachika watakupa ushuhuda wao, utawaonea huruma,utakarahishwa, utastaajabika, Utakuwa unashangaashangaa mama, na kuimbaimba na kujiuliza kwa nini Mungu aliumba mapenzi.

Yango na po na nga Amida, hata na pasi tokovanda, hata bikebi tokoliya hata thomson tokotonda. Yesu kutu mwana ya nzambe babota ye na nandako ya mpata, Kasi mokili oyo ya tata naye, Likolo nase ya bango, kamweve o makamwisi mama = Kwa hiyo nimemchagua Amida katika mashaka tutaishi, hata samaki(thomson) tutakula tutashiba, Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alizaliwa katika zizi la wanyama. Lakini dunia hii ni ya Babaye, mbingu na ardhi ni vya kwao Usishangae maajabu.

Na Kin Liboso ya kolinga moto bakoma kotuna ofandaka wapi, A biso tovandina mwalekwa nani akolinga biso mingi baboya bango na bango, Mosika eleki, bangungi baleki Taxi kutu eboya bango = Kinshasa kabla ya kumpenda mtu wamekuwa akiuliza unakoishi, Ah sisi tunaoshi Malekwa (Manzese,Uswahilini) nani atakaetupenda. Wengi wamekataliwa eti ni mbali mno mbu wamezidi huko hata Taxi haziendi huko.

Basusu liboso ya koloba Oui” bakoma kotuna otangaka wapi, Ah biso tubuka Bic mwa kala nani akolinga biso, Tika tokosa hata kokosa, Nga nazali graduet, Nga nazali licencie, Nga nazali enginieur, mpo balinga nga mama = Wengine kabla ya kusema ndio” huuliza ulikosoma wapi Ha sisi tuliovunja kalamu (Bic)yaani (kuacha shule) toka siku nyingi nani atatupenda, Wacha tudanganye mimi nina degree, mimi nina shahada ya juu, mimi mkandarasi ili tupendwe.

Basusu liboso ya kolinga moto bakoma kotuna de quele famille es-tu? Ah biso famille ezanga riche nani akolinga biso nzambe ya mpungu bandela mokili oyo otunaka mokomoko soki nani akolinga kobotama lisusu na famille ya pauvre. = Wengine kabla ya kumpenda mtu huuliza umetokea katika familia ya namna gani? Ha sisi familia fukara nani atakayetupenda,Baba Mungu rdia maumbile halafu muulize kila mtu kama yupo atayekubali kuzaliwa tena katika familia ya kimaskini.

Passe na nga eleki mabe yango naeffacer basouvernir nyoso ya mabe na bango nanga, memoir nanga eyebi kaka kombo ya Amida Chaty naye nde pelerinage edainayo petola nga mama sukolangamama, salisa nga nabika. = Maisha yangu yaliyopita ni mabaya ndio maana napenda kufufa zote mbaya kwenye ubongo wangu. Kumbukumbu yangu yajua tu jina la Amida Chaty Nimekuja kwako kama mpitaji,nitakase,nisugue nisaidie nipone.

Nalinga mindele,Bayindo,mikuse, milayi nalinga mike mpe minene, kasi chancelier wapi alatisanga palata ata bronzo hatanatolo, soit disant nga se amoureux,ancien de saio asala kala, roi de guere O mosala mpunda mama = nimependa weupe na weusi warefu na wafupi wembamba na wanene yupo wapi afisa zawadi hata medali ya chuma kifuani ieleweke kuwa mimi ni mpenzi mkongwe wa Saio( aliyepigana vita vya Saio mfalme wa vita Kazi isiyo na Mshahara……

Mtohoo huo ni mchango wa msomaji wangu maarufu Shaibu Thabit Mwambungu ambaye alikuwa nao kwenye maktaba yake.

Respect kwa wasomaji wangu wote, Mamaa Sophia Kessy, Pendejee Maghambo Philipo popote ulipo tuko pamoja, Julie ellyston Suvereign, Batty My Brother pamoja, Mukubwa Edgar Kiiza muzee ya Malaysia, Ally Tandika diwani muzee ya Azam, Mukubwa Six Mzee wa Matombo, Tom Baba Maya aka Chiluba, Mukubwa Gerald Kitima Baba Kara, Dulla Asumani muzee ya Tigo, Hadj le Jbnique, Patrol de Patrol Shaibu Thabit, Farid, bila kumsahau Swahiba Alhaj Tameem Mngoya Juma Ahmed Lukuta wa Kibanda Kicheba kwa Semkopi pamoja na Werasonique wooote, . Pamoja sana.

Nakutakieni Weekend njema.

Alamsiki.


JackzCosmetics

February 10, 2011


%d bloggers like this: