Ligi imenoga sasa!!

October 31, 2008

Mchezaji wa timu ya Manchester United’s Portugese midfielder Cristiano Ronaldo akishangilia goli baada ya kufunga goli la kwanza wakati wa mchezo wa Ligi ya Uingereza Premier league dhidi ya West Ham united huko Old Trafford, Manchester, Manchester ilishinda 2-0.

Matokeo mengine ya mechi za jana ni kama ifuatavyo:-

Wakati huo huo Idhaa ya Kiswahili ya BBC, pamoja na redio washirika, Jumamosi ya tarehe 01 Novemba 2008, itakuletea matangazo ya moja kwa moja, kati ya Chelsea na Sunderland.

Hii itakuwa ni mechi ya kwanza ya Chelsea itakayotangazwa na BBC msimu huu.

Jumla ya mechi nane zitachezwa siku ya Jumamosi.

Ratiba ya Jumamosi, 01 Novemba 2008, kwa kuzingatia saa za Afrika Mashariki
Chelsea v Sunderland, 18:00
Everton v Fulham, 15:45
Man Utd v Hull, 18:00
Middlesbrough v West Ham, 18:00
Portsmouth v Wigan, 18:00
Stoke v Arsenal, 18:00
Tottenham v Liverpool, 20:30
West Brom v Blackburn, 18:00

Jumapili, 02 Novemba 2008
Bolton v Man City, 19:00

Jumatatu, 03 Novemba 2008
Newcastle v Aston Villa, 23:00


Dini ya Maradona yashika kasi Argentina

October 31, 2008

Muumini wa knisa la Maradonian Church The hand of God, hehebu ambalo limeanzishwa kwa nia ya kumuenzi mwanasoka mkongwe wa Argentina  Diego Maradona, akifurahia na mwanaye sherehe za  Christmas, hii ilikuwa usiku wa kuamkia siku ya kuzaliwa kwa Maradona akiwa anatimiza miaka 48 huko  Buenos Aires juzi tarehe October 29, 2008. Mamia kwa makumi ya waumini wamekusanyika kwenye kanisa hilo usiku huo ikiwa ni kumtukuza na kufurahia sherehe yake ya kuzaliwa na kuchaguliwa kwake kuwa kocha mpya wa Timu ya Taifa


Majaliwa ya Michael Ballack timu ya taifa kujulikana leo

October 31, 2008

Prev 11 of 200

Picha hii iliyochukuliwa February 4, 2008 inamuonyesha Michael Ballack (2nd R), midfielder wa timu ya Taifa ya Ujerumani, Kocha mkuu wa timu ya Taifa Joachim Loew (2nd L), na mchezaji mwenza Gonzalo Castro (L) na kipa wa Timu hiyo Timo Hildebrand (R) wakiwa wamevalia kama wapanda milima wakati wa kuandaa tangazo la biashara huko  Gross-Gerau near Frankfurt/M., Magharibi mwa Ujerumani. Shirikisho la Soka la Ujerumani (The German Football Federation (DFB)) limesema jana kuwa wote hao watakutana uso kwa uso kuzungumzia kitendo cha Ballack kumshambulia kocha  Loew kwenye Magazeti ya Ujerumani, shirikisho hilo pia limesema majaliwa ya Ballack kwenye timu hiyo yatajulikana leo baada ya kocha huyo kutoa tamko lake leo.


Pambano la Yanga na Simba laingiza Sh239milioni

October 31, 2008

Picha ya Maktaba ya Uwanja wa Taifa

Picha ya Maktaba ya Uwanja wa Taifa

WAKATI pambano la mahasimu, Simba na Yanga likiingiza jumla ya Sh milioni 239,829,000 kila klabu zimeambulia Sh 44,191,000 huku fedha nyingine zikiwa ni gharama za mchezo.

Mapato hayo yalitangazwa jana Afisa Habari wa TFF, Florian Kaijage ikiwa ni siku nne baada ya kufanyika mpambano huo. Awali gazeti hili lilitoa makisio ya 242,435,000 kwa mapato hayo ikiwa ni pungufu ya Sh milioni 2,606,000. Kaijage alisema fedha hizo zimepungua kutokana na kuwepo kwa tiketi nyingi za mialiko.

Katika mgawo huo serikali imepata shilingi 43,358,000 sawa na asilimia 20 huku klabu za Simba na Yanga kijipatia 44,191,000 kila mmoja sawa na asilimia 19 .

Jumla ya shilingi Mil.239,829.000 zilipatikana na watu 52,890 waliingia katika pambano hilo lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita. Alisema asilimia 20 (43,358,948) zilikwenda kwenye gharama ya mchezo ambapo zilihusisha gharama mbalimbali zilizotumika wakati wa mchezo na kabla ya mchezo kufanyika, asilimia 10, (Sh21,679,474) zilikwenda kwa Shirikisho la soka Tanzania, TFF.

Fedha nyingine zilikwenda Baraza la Michezo la Taifa, BMT, waliopata asilimia moja sawa na Sh 2,167,947 wakati mfuko wa maendeleo ya soka ulipata asilimia tisa sawa na Sh19,511,526. Alisema watu 492 waliingia jukwaa la VIP A kwa kiingilio cha 20,000 na kupatikana Sh 9,840,000 wakati VIP B kiingilio kilikuwa 15,000 kwa watu 2301 na kupatikana sh34,515,000.

Jukwaa la VIP C, walioingia ni 3,101 kwa kiingilio cha Sh10,000 na zilipatikana Sh31,010,000. Viti vya Orange kilikuwa Sh 5,000 na watu 11,738 waliingia na kuingiza Sh58,690,000.

Katika viti vya blue na kijani mzunguko, kiingilio kilikuwa 3,000 watu kwa watu 35,258 na kiasi kilichopatikana ni Sh105,774,000.

Kaijage alisema kuwa tiketi zilizotolewa kwa wadau mbalimbali wa soka zilikuwa, VIP 246, VIP B 104, VIP C 125 na viti vya kijani 15 ikiwa ni tiketi 490 zenye thamani ya Sh7,775,000.

Alisema pia kulikuwa na kasoro baada ya wana usalama kushindwa kudhibiti mlangoni hivyo kuyna idadi ta watu waliingia bila kulipa na bado hawawezi kulizungumzia kwani bado halijafanyiwa uchunguzi na kuona ni kiasi gani cha fedha zilizopotea.


Houston na Vitongoji vya jirani kazi kwenu!

October 29, 2008
.

.


Uongozi Shirikisho la Ndondi watangaza kujiuzulu

October 29, 2008
Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Shaaban Mintanga, akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufikishwa akikabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama za kusafirisha dawa za kulevya kutoka Tanzania kwenda Mauritius na kushiriki katika tukio hilo.

Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Shaaban Mintanga, akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufikishwa akikabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama za kusafirisha dawa za kulevya kutoka Tanzania kwenda Mauritius na kushiriki katika tukio hilo.

UONGOZI mzima wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), umetangaza kujiuzulu kufuatia tuhuma za mabondia wa timu ya taifa ya ngumi kukamatwa na dawa za kulevya nchini Mauritius mwezi Juni mwaka huu.

 

Makamu Rais wa BFT, Chris Mutta alisema jijini jana kuwa hatua ya kujiuzulu inafuatia kikao cha kamati ya utendaji kilichokaa Oktoba 13 kwenye ofisi za chama hicho na kikao kilichofanyika Oktoba 14 kwenye Gereza la Keko ambako Rais wa BFT, Alhaji Shaaban Mintanga anashikiliwa kutokana na tuhuma hizo na kukubaliana kwa pamoja kujiuzulu kuanzia jana ili kulinda heshima ya nchi, chama, mchezo wa ngumi pamoja na viongozi waliojiuzulu.

 

“Kikao cha Oktoba 13 kilikuwa na mvutano, baadhi ya wajumbe wakiunga mkono kujiuzulu na wengine wakipinga, tutakafanya kikao kingine siku iliyofuata katika gereza la Keko na kumshirikisha rais (Mintanga) na tukakubaliana kwa pamoja kujiuzulu kuanzia leo,” alisema Mutta.

 

Read the rest of this entry »


“Wajanja” waingiza Album ya Bushoke sokoni kabla haijaachiwa!!

October 29, 2008

Bushoke ashangaa kukuta album yake SokoniMsanii wa kizazi Kipya Rutta Bushoke, ambaye bado anafanya vyema kiaina na pini lake ‘Dunia Njia’, amesema anashangazwa na kuuzwa kwa kile kinachosemwa ni Albamu yake mpya katika mikoa kanda ya ziwa,wakati bado hajaiingiza sokoni.

Akizungumza kwa mshangao na Dar411 msanii huyo alisema amedaka nyepesinyepesi hizo kwamba albam yake mpya inauzwa sana hasa mkoani Mwanza, wakati yeye ana uhakika wa asilimia 200 kuwa hakuna mtu hata mmoja mwenye copy ya albam au hata nyimbo zilizo katika project yake hiyo mpya.

“Ni kweli nina albamu mpya,lakini bado haijaingia sokoni wanaouza albam wanayosema ni yangu ni wezi na waongo wakubwa.” alisema kwa machungu Mkali huyo.

“Nimeachia wimbo mmoja tu ulio katika albam hiyo uitwao ‘Dunia Njia’ kama wana nyimbo zangu basi watakua wameweka nyimbo za zamani lakini si mpya,” alimalizia kwa kusema Bushoke.

Bushoke, mtoto wa mwanamuziki mkongwe Maxmillian Bushoke aliwataka mashabiki wake kutonunua albamu hiyo feki kwani ile ya ukweli itaingia sokoni mapema Desemba mwaka huu na itatangazwa muonekano wake.

“Mashabiki watusaidie wakinunua feki wanazidi kuwapa jeuri hao wezi waendelee kutuibia lakini wakikataa kwanza watanunua kitu chenye ubora na pia watatoa msaada kwa wasanii wao ili waendeshe maisha kwa umakini zaidi,” alisema msanii huyo.

Wizi wa kazi za wasanii kimekuwa na kilio sugu cha malalamiko yote yanayotolewa inaonekana kama vile Serikali haijali kwani hakuna hatua zozote za dhati zinazochukuliwa kuwasaidia vijana hao wanaofanya kazi halali.

Habari hii na Dar 411


%d bloggers like this: