Nawapa shavu wana wa Pakaya IFA Sound Band

June 13, 2009
Fundi Hussein akisafisha viatu huku akipata Burudani ya vijana wa IFA SOUND BAND mchana huu katika mtaa wa Samora Evenue jijini Dar vijana hawa wanatokea kule Ifakara mkoani Morogoro na hutoa burudani maeneo mbalimbali jijini.

Vijana wa kundi la IFA SOUND BAND wakifanya vitu vyao mtaa wa Samora Evenue jijini Dar huku watu wakiwa wamewazunguka ili kupata burudani yao kutoka kulia ni Selemani Makwati, Oswald Damka, Jafari Ligomba, Adam Komba, Chande Kilowile na Majuto Mdodo.

Vijana hawa ambao kwa hakika wana vipaji wanahitaji kuendelezwa na hii inakuwa changamoto kwa watu wa Mkukuta. Kwani kupitia burudani vijana wanaweza kujikwamua na hali mbaya ya maisha jambo ambalo Rais alilitilia mkazo alipotangaza kufungua milango kwa ajira milioni moja na hii inaweza ikawa moja ya milango hiyo.

Picha na mzee wa Full Shangwe

Gonga hapa uwaone The Big Tone Sound Band ya Ifakara ambao sina hakika kama ni hawa hawa ama lah.

Morogoro ni mkoa ambao una historia ndefu ya Muziki ukiwa na Bendi kama Moro Jazz, watu kama akian Mbaraka Mwishehe na wanamuziki wengine wengi.


Tell me why… Mjumbe hauwawi

January 21, 2009

Kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe hasa kwa dunia ya sasa ambayo watu wapo busy kusaka noti, weka mkutano wa hadhara hawaji, lakini kuna njia nyingi za kuwafikia wahusika hata kama hamji kwenye majukwaa ya siasa basi tutawafikia kwa njia ya Nyimbo, pata burudani na ujumbe kwenye nyimbo ifuatayo then umpe bwana mdogo jibu


Tamasha la Fest Afrika Finland

July 17, 2008
.

.

Start Time: Friday, July 18, 2008 at 9:00pm

End Time: Saturday, July 19, 2008 at 4:00am

Location: Klubi Tampere

Street: Tullikamarin aukio 2, Tampere

City/Town: Tampere, Finland

Phone: 358449571438

Email: www.festafrika.net


%d bloggers like this: