Ballack na Mkewe baada ya ndoa kanisani jana.

July 16, 2008
.

.

Mchezaji Michael Ballack, wa timu ya Taifa ya Ujerumani na Klabu ya Chelsea akiwa na mkewe Simone Lambe huko Berg, Kusini mwa Ujerumani jana jumanne, July 15, 2008. Ballack na Simone wanasemwa kuwa kwenye urafiki wa siku nyingi na ulidumu kwa muda mrefu kabla ya kuoana juzi jumatatu kwa msajili wa ndoa na kumalizika kikanisa jana jumanne. (AP Photo)


Kaijage unawaonaaaa??????

July 15, 2008
Wachezaji wakibadilishana jezi

Michael Ballack na Clarence Seedorf

Mchezaji wa Ujerumani Michael Ballack (L) na Clarence Seedorf Msuriname mwenye uraia wa Holland wakibadilishana  jezi baada ya mchezo wa hisani hapo majuzi tarehe 12 July, Mchezo huu ulishirikisha Nyota wa dunia katika kuchangia Taasisi ya  “Goal4Africa” ambayo inatoa misaada mbali mbali kwa nchi za Africa, mchezo uliochezwa huko Allianz Arena stadium, Jijini Munich, kusini mwa Germany, Picha hii inanikumbusha sakata la mchezaji wa Taifa Stars aliyedaiwa Jezi baada ya kubadilishana na mwenzie Samuel E”too baada ya mchezo kuisha, Ingawa Rais wa TFF alitoa ufafanuzi lakini kitendo hicho kililaaniwa vikali na wapenzi wa soka. (AFP PHOTO DDP/PHILIPP)


Michael Ballack aoa jana

July 15, 2008
Balack na Mkewe baada ya ndoa yao jana.

Balack na Mkewe baada ya ndoa yao jana.

Mwasoka wa Ujerumani na klabu ya Chelsea Michael Ballack, na mkewe Simone wakiwaaga ndugu, jamaa na marafiki baada ya kufunga Ndoa jana huko Kempfenhausen, kusini mwa Ujerumani, (AP Photo/Christof Stache).


%d bloggers like this: