Watoto wa Werra

September 30, 2011

Hawa hapo chini ni “watoto” wa Ngiama Makanda Le Roi De La Forret Werrason,ni watoto watundu na watukutu sana ukiwakuta stejini,Hapa Flamme Kapaya aliwashirikisha Bill Clinton na Celeo Scram ili kuwapa angalau kidogo burudani wanayoikosa watoto wa Congo Kwenye matamasha ya WMMM Siku hizi.Pata sebene na mautundu ya ku dance toka kwa Bill Clinton


KILICHOMTOA FLAM KAPAYA WMMM

September 30, 2011

Tumtazame Fundi Flamme Kapaya hapa ,anaimba na kupiga guiter kwa pamoja vyote anavifanya kwa ustadi wa hali ya juu.Hapa walipiga na Bill Pamoja na Celeo ndani ya Gombe na kati ya KIN

Na The Romantic
Mnamo mwaka 2005 Werrason na Wenge makao makuu kwa kiswahili au wenge head office (kiingereza) au wenge maison mere waliachana rasmi na udhamini wa kampuni kubwa ya BRACONGO inayotengeneza Bia maarufu ya SKOL badala yake wakaingia mkataba na kampuni nyingine kubwa ya BRALIMA ambayo inatengeneza na kusambaza bia aina ya PRIMUS. Na katika kusherehekea ndoa hiyo mpya kati ya WMMM na BRALIMA – PRIMUS ambao pia ndio wadhamini wakuu wa Wengee Bcbg ya JB Mpiana, BRALIMA wakaandaa tamasha la bure kubwa sana huko Kikwit ambao ni mji aliozaliwa Werrason uliopo kaskazini mwa jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa congo. Inakadiriwa onesho hilo la bure lilihudhuriwa na watu kati ya 300,000 hadi 700,000! watu wengi sana, lilikua ni moja kati ya maonyesho makubwa kupata kutokea katika historia ya muziki wa congo. Sasa tatizo kati ya FLAM na Werra lilianzia hapa.

 

image

“Flam Kapaya mtaalamu akiwa kazini, Ikumbukwe Flam anaimba, anapiga gitaa, anapiga kinanda, ana rap na pia ni muandaaji wa muziki, kwa kifupi jamaa ni mwanamuziki full na pengo lake halizibiki”

Werra hakuwagawia pesa yeyote wanamuziki wake kutokana na concert hiyo licha ya kulipwa pesa nyingi sana na BRALIMA. Werrason akapata utajiri mkubwa sana kutokana na deal la BRALIMA lakini wanamuziki wake hawakuambulia lolote licha ya kazi kubwa, Ndipo Flam Akawa analalamika kwamba ametunga nyimbo nyingi na kuzi arrange yeye mwenyewe lakini bosi werra akazisajili (Sacem)France kwa jina lake akiziandika “arrangeur-compositer werrason kwenye C.D. nadhani wengi tumeziona hizo C.D za kipindi hicho, Flam akawa anatajwa kama mpiga guitar tu, licha ya ukweli kwamba kila mtu hata mawerasonique die hard wanajua kwamba FLAM was the musical Brain behind kibuisa mpipa.

Huyo ndio Neol Ngiama makanda mtu wa watu kama wazee wa head office wenyewe wanavyopenda ajulikane. Lakini Thanx God Kwa wapenda muziki wa congo wote kwamba baada ya kuhangaika kuziba pengo la Flam werra sasa amempata mpiga solo mahiri mwenyewe amempachika jina anamuita new makaba (nadhani bado werra bado anamuota prince) maana amemshawishi mara kadhaa Alain Prince makaba ajiunge nae bila mafanikio. Je makaba huyu mpya ataweza kurudisha enzi za mafanikio ndani ya wmmm, enzi za kibuisa mpipa na FLAM KAPAYA? Je radha ile itarudi tena kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki (sio wa werrason pekee) tena? ni suala la kusubiri na kuona maana werrason  anae mpiga guiter kijana mahiri ambae amepachikwa jina kama New Makaba,tumpe muda yeye na wenzake hapo.


Fally LIVE

September 30, 2011

image


Tottenham hotspurs yaepuka aibu.

September 30, 2011

Katika michuano ya Ligi ya Europa zilizochezwa alhamisi usiku, timu ya Tottenham Hotspurs ya uingereza iliponea kuadhibiwa na Shamrock Rover ya Ireland kabla ya kujikusanya na kufunga magoli matatu ya haraka haraka.

Ingawa Hotspurs ilishinda mechi hiyo kwa mabao 3 – 1 lakini Shamrock ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga.

Katika dakika ya 50 Stephen Rice aliifungia Shamrock goli.

Bao hilo liliwafanya Tothenham kushambulia lango la Klabu ya Shamrock na kufaulu kufunga mabao matatu katika muda wa dakika tano tu.

Waliofunga walikuwa Roman Pavlyuchenko katika dakika ya 60, dakika moja baadae Jermain Defoe akafanya mabao kuwa mawili na katika dakika ya 60 Giovani dos Santos alikamilisha kibarua kwa kufunga bao la tatu.

Naye Mchezaji wa kimataifa wa kenya ,Victor Mugabe Wanyama , ambaye ni nduguye mdogo MacDonal Mariga wa Real Sociedad ya Uhispania alipokea kadi ya njano katika hali ya kuisaidia klabu chake cha Celtic ya Ireland kutofungwa na Udinese ya Italy.

Celtic waliokuwa wakiongoza kwa 1-0 waliwakasirisha mashabiki wao wapatao 37,000 pale bao hilo lilipokombolewa kwa njia ya penalti kukiwa kumesalia dakika saba mechi kumalizika.

Sare hiyo imeiwacha Celtic ikivuta mkia katika kundi I.

Katika michuano hiyo ya Ligi ya Europa ,Stoke City ya Uingereza iliizoa alama tatu katika mechi za kundi E baada ya kuifunga timu ya Besiktas ya Uturuki.

Mabao ya Stoke yalifungwa na Peter Crouch na Jon Walters.

Timu nyegine ya uingereza Fulhama ilipata ushindi wa 2-0 kwa kuwa aibisha wenyeji wao Odense BK ya Denmark .

Mabao yote ya Fulham yalifungwa na Andy Johnson.

Kwengineko timu ya Sporting Lisbon ya Ureno wakiwa wamesalia na wachezaji 10 waliweza kuwafungua Lazio ya Italy 2-1.

Kwa ushindi huo wa Sporting Lisbon inaongoza kundi D kwa alama sita baada ya kucheza mechi mbili.

Mabao yaliofungwa na Igor Gabilondo na Markel Susaeta iliipatia Athletic Bilbao ushindi wa 2-0 win dhidi ya Paris St Germain.

Ilikuwa ni siku ya mkosi kwa Paris St Germain kwani mchezaji wao Mohamed Sissoko alitolewa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 53 ya mechi hiyo.


Akumbukwe Defao

September 29, 2011

image

Leo tunakwenda angle tofauti kidogo,tunamzungumzia Genaral Defao Matumona na bendi yake ya Big Stars ambayo ilitesa sana katika ulimwengu wa muziki wa congo kwenye miaka ya tisini.Defao alianza kuimba mwanzoni mwa mwaka 1976 katika bendi za mitaani ndani ya kinshasa kama orchestre soka movema,fogo stars,korotoro n.k.Inasemekana alishawishika kupenda kuimba kutokana na uimbaji wa wakali wa zaiko langa langa wakati huo Papa wemba na Nyoka Longo,lakini mwenyewe amekuwa akikiri kwamba TABU LEY amekuwa main inspiration kwake.Defao alianza kujulikana zaidi nje congo mwaka 1991alipoanzisha bendi yake ya BIG STARS Iliyokuja kuitijisa miji mikubwa ya africa kama Abidjan,Dar es salaam,Kinshasa,Oagadougou n.k.Hapa chini kwa mfano mtaweza kuiona video ya live concert Abidjan enzi hizo likiwa jiji la maraha kwelikweli kabla ya kukumbwa na machafuko ya kisiasa.

Hapo mwanzo ni THEO MBALA enzi hizo akiwa ndio yuko kwenye kiwango cha juu kabisa anamchezesha Chocholi chocholaa mcheza show mahiri wa big stars.Pia anawachezesha Defao na Kina Kabose anaeimba na kushikwa kichwa na defao,ilikua safi sana.


George Weah Miley Kunde wa Koffi Olomide

September 29, 2011

Mdau wangu Yasmiza uliyeniuliza huyu mdada anaitwa nani, Angalia video hii huyo mrembo anaemshika mkono na pochi ndio George Weah Miley Kunde,msikie suzukii hapo anavyoingia,uzuri wa japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wake toka enzi hizo yuko flexible,akipiga rhumba anapatia akipiga sebene pia anaweza.

Sijawahi kumchukia Koffi hata siku moja kama mdau alivyosema kwenye Comment na kwa taarifa tu nina collection ya Koffi ya kusikiliza ambayo mdau nikuonyesha huwezi amini labda nikuonjeshe screen shot ya Real Player uone … Nimelazimika kuweka maneno ya mdau yalikuwa mazito na kilichonisikitisha aliambatanisha na matusi bwana, sio fresh naomba tuvumiliane na ushabiki wa muziki si wa uhamasama namna hiyo.

image

Msikie tena suzukii na Bouro Mpela hapa,hiki mi nasema ndio kilio kikosi bora kabisa cha koffi na QL kiujumla.


Ferre Golla Zazou

September 29, 2011

Ferre Gola ni mmoja wa vijana zao la Wenge Musica ambaye amefanikiwa tofauti na wengine ambao hawakufanikiwa kwenye muziki tangu wajiengue ama kwa JB Mpiana au kwa Werrason.

Namkubali sana Ferre kwani utaona hata alipokuwa kwa Werrason alikuwa ni kiongozi mzuri japo hakudumu naye sana lakini naweza sema amefanikiwa kwenye suala zima la management.


Wenge BCBG- Eve Sukali

September 29, 2011

Wakati ule tunaongelea walipoanzia akina Mpiana mpaka kuunda BCBG tuliona yaliyotokea. Ukitaka kujikumbusha basi angalia sehemu ya pili na ya tatu ya ile stori yetu utajua zaidi.


Huyu ndie Willy Bula kaka wa Blaize Bula

September 29, 2011

image

Alikuwa wapi na kwa sasa yuko wapi? Tega sikio inakuja hapa hapa…


Fifa tayari kuchukua hatua

September 29, 2011

Na BBC

Makamu mwenyeki wa shirikisho la soka duniani,FIFA Bw.Jim Boyce amesema kua ikiwa itathibitishwa kua mchezaji Carlos Tevez alikataa kushiriki mechi dhidi ya Bayern Munich kama alivyotakiwa na kocha wake, basi anaweza kuwekewa kikwazo asishiriki mchezo huo kote duniani.

Carlos Tevez

Tevez na bintiye

Boyce ambaye hapo zamani alikua Rais wa chama cha mpira cha Ireland, amesema kua tukio hilo halipendezi.
Aliongezea kusema kua, ‘nadhani Fifa iwe na uwezo wa kumuadhibu mchezaji asishiriki kwa njia yoyote ile mchezo wa soka.

Wakati huo huo, klabu ya Manchester city imemsimamisha mchezaji huyo kwa kipindi cha wiki mbili.

Kocha Roberto Mancini

Kocha Roberto Mancini

Katika kipindi hicho cha majuma mawili, mawakili wa klabu hiyo wanachunguza vipengele vya kumfungulia mashtaka endapo mkataba wake utasimamishwa.

Lililo bayana hata hivyo ni kwamba endapo itathibitishwa kwamba mchezaji huyo alikataa kucheza licha ya mwenyewe kukana madai hayo, atakua amekiuka mkataba na hivyo klabu ya Manchester City inaweza kuchana mapatano ya mshahara mkubwa wa pauni lakini mbili kwa kila wiki.

Adhabu ya chini ambayo inaweza kumfika Tevez ni kutozwa faini ya mshahara wa wiki mbili, kama ilivyokubaliwa chini ya makubaliano ya chama cha wacheza mpira wa kulipwa.

Tatizo jingine linalojitokeza ni kwamba kuurarua mkataba wa Tevez ili kupunguza gharama za mshahara mkubwa, miongoni mwa mishahara mikubwa inayolipwa wacheza soka, wakiwepo watatu duniani wanaolipwa mishahara mikubwa’ huenda kukamaanisha kupoteza hadi pauni milioni 40 kwa kumfuta kazi mchezaji huyo.

Kuhusu uwezekano wa Fifa kumchukulia hatua, Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Jim Boyce amesema ikiwa mchezaji huyo amefanya kama ilivyodaiwa, na kama klabu yake itamuachisha kazi na ifahamishe Fifa, basi hatua zitachukuliwa kuona kwamba anawekewa kikwazo asishiriki wala kujihusisha na masuala ya soka kote duniani.


Sunderland yamsimamisha Bramble

September 29, 2011

Na BBC

Klabu ya mpira inayocheza katika Ligi kuu ya England, Sunderland, imemsimamisha beki wake Titus Bramble baada ya mchezaji huyo kukamatwa akishukiwa kuwa na dawa ya kuongezea nguvu pamoja na kosa la ubakaji.

Bramble

Titus Bramble

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye hapo zamani alichezea klabu ya Newcastle na Wigan alihojiwa kabla ya kuachiliwa kwa dhamana hapo jana.

Taarifa ya klabu imesema kuwa: “Titus Bramble amesimamishwa wakati majibu ya upelelezi yakisubiriwa.

Taarifa hiyo imeongezea kusema kuwa “mchezaji huyo hatoshiriki mazowezi ya timu au kuwa tayari kuchaguliwa kwa ajili ya kushiriki mechi yoyote kwa wakati huu.”

Titus Bramble alianza kucheza soka katika klabu ya mji alikozaliwa wa Ipswich, kabla ya kuhamia Newcastle United kwa kitita cha pauni milioni sita.

Baada ya hapo akajiunga na klabu ya Wigan Athletic kabla ya kurejea kaskazini mashariki alipojiunga na Sunderland mwaka uliopita.

Beki huyo aliyechaguliwa mara kumi kuichezea Timu ya vijana wa England wenye umri ulio chini ya miaka 21, alishiriuki mchuano wa klabu yake ilipofungwa na Norwich 2-1 mnamo siku ya jumatatu.


Ligi ya Uingereza mpaka leo

September 29, 2011

image


Ya 5; Best of Lady Jay Dee iko tayari

September 26, 2011

image

Mwanamuziki Lady Jay Dee ametangaza kutoka kwa Albamu yake ambay ni Compilation ya nyimbo zake bora zilizotamba tangu aingie kwenye ulimwengu huu wa Muziki.

Jay Dee ambaye alikuwa akiwajulisha wapenzi wake kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema kuwa Albamu hiyo itajumuisha nyimbo toka albamu zote Asubuhi ya 2000, Machozi, Binti, Moto na Shukrani. “…Album inaitwa YA 5 & THE BEST OF LADY JAYDEE Inaunganisha na nyimbo za zamani kuanzia Asubuhi ya 2000, Machozi, Binti, Moto na Shukrani…” ilisema sehemu ya status ya mwanamuziki huyo.

Jay Dee ni mmoja wa wanamuziki wenye mafanikio makubwa kimuziki huku mafanikio na graph yake ikizidi kupanda kila uchao, Mbali na hivyo ni mwanamuziki ambaye ni kioo cha vijana wengi kwani tofauti na wanamuziki wengine si rahisi kusikia kashfa au kusoma kwenye “tabloids” habari yeyote ya ajabu inayomhusu yeye, nachelea kusema kwa heshima anaongoza huyu mdada.

Hongera Jay Dee mashabiki wako tunakungoja, tuko pamoja wakukufuta machozi binti machozi.


Sean Kingston in Uganda

September 25, 2011

300221_10150303857288359_592028358_8215729_1914590669_n307897_10150303859008359_592028358_8215756_147254221_n309624_10150303857343359_592028358_8215730_221434397_n309741_10150303857423359_592028358_8215731_332413131_n

Huu ni umati wa Live Concert ya Mwanamuziki Sean Kingston toka Jamaica iliyofanyika jana huko Uganda, Picha zaidi na habari zinakuja.


Vipaji adimu toka kwa Werrason.

September 23, 2011

Leo nimeamka na Werrason tuu, mi huwa nasikiliza vitu vingi sana kwenye wimbo naomba usikilize jinsi vijana walivyopangilia sauti kwelye wimbo huu kisha sikiliza solo ilivyopigwa humu. Werrason analeta mambo si mchezo na ndani yake kuna style ya Mapouka fulani basi raha tuu.


Werrason kwa Sebene bana namkubali

September 23, 2011

Huwa nikiongea na ma werasonike nasemaga kabisa bila kuficha katika vitu ambavyo Werasson amefanikiwa ni Sebene lake, huwa napenda sana nyimbo za Werrason zinazoanza na moto tangu mwanzo tofauti na JB ambaye nyimbo zenye sehemu mbili huwa anazipatia sana yaani zinaanza na kupokezana kwa Verse kisha zinachanganya, anyway huuu ni mtazamo wangu na jinsi nilivyojipanga ili kuwatendea haki wote wawili na niwe na sababu ya kununua albamu za wote wawili, Werrason anaenda akibadilika na katika wimbo huu bado nahisi Animateur alikuwa na kazi ya ziada ya kutuletea ladha ile yaki Maison Merre. Nawatakia Weekend njema msikose uwanjani kwani wiki ijayo tutaendelea na makala zetu za Wenge na habari nyingine kemu kemu hapa hapa jamvini.

Kama kawaidauwanja uko wazi kama vitu tuma message kwa 0713 666616 sio usiku wa manane au tuma email kwa piusmicky@yahoo.co.uk

Weekend njema.


Msechu jukwaa moja na Cabo Snoop, Shaggy & Eve kwenye Tusker All Stars Performance.

September 21, 2011

Hatimaye imethibitishwa kuwa Eve, Shaggy and Cabo Snoop watatumbuiza jukwaa moja pamoja na wa Star watattu wa Tusker Project Fame All Stars Davis, Msechu na Alfa hapo  1st October 2011.

Wakenya wengi walikuwa na wasiwasi juu ya ushiriki wa wanamuziki hawa kutokana na Promoter wao kutokuwa na majibu ya moja kwa moja hapo awali.

Milango itafunguliwa saa sita mchana huku performances zikianza saa nane mchana . VIP tickets za Golden Circle zinauzwa kwa 3,500 Kshs na 1,500 Kshs kwa maeneo mengine ya mzunguko,

Angalia hizo Video zao walizo confirm ushiriki wao hapo chini ili kufuta mashaka, kwa wale wanaotaka kwenyda kamata mchuma kuna Flights za kutosha Dar Nairobi, Nairobi – Arusha au kamata basi utawahi kwani kitu gani banaaaaa.

Eve Confirms Tusker All Stars Concert Attendance

Cabo Snoop Confirms Tusker All Stars Concert Attendance


Koffi na Cindy walivyomuomboleza Mamaa Editha Bongo au Editha Sasou Nguesso

September 21, 2011

Nimewachagulia wimbo huu hapo  ambao koffi olomide na cindy wake walimuimbia Mamaa EDITA OMARI BONGO au EDITA SASOU NGUESSO ambae alikua mke wa presidaa OMARI BONGO wa Gabon na pia alikua ni binti wa kumzaa wa Rais DENNIS SASOU NGUESSO wa CONGO BRAZAVILLE, huu ni wimbo wa majonzi baada ya kifo cha maman EDITA. Natumai kwa Post hii nitakuwa nimekujibu mdau wangu  Mkemimi, wa Kigoma ujiji. Shukrani sana kwa kuwa pamoja.


TP Mazembe yanunua ndege mpya kwa ajili ya safari za timu yake

September 21, 2011

image

Ndege mpya wa TP Mazembe aina ya MD-83 yenye uwezo wa kubeba watu 140 ilitua jijini Lubumbashi juzi Jumapili.

image

Iki0pokelewa kwa heshima ya wanaanga jijini Lubumbashi

image

Kama inavyoonekana kwa ndani, ni jitihada binafsi za Moize Katumbi Chapwe, Rais na Mwenyekiti wa TP Mazembe

KINSHASA, DR Congo (Picha zote na TP Mazembe)

Na Mwananchi
WAKATI ikiwa ni ndoto kwa klabu za Yanga na Simba kuwa na viwanja vyao, wakongwe wenzao mabingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe wamenunua ndege ya pili mpya kwa ajili ya kusafirisha timu itapokuwa ikicheza mashindano mbalimbali msimu huu.

Yanga na Simba zilizoanzishwa zaidi ya miaka 70 iliyopita zikiwa na wapenzi wengi zaidi zimeshindwa kuwa na viwanja kwa ajili ya kutumia kwa michezo yao ya Ligi Kuu na kulazimika kuomba kutumia uwanja wa klabu ya Azam wa Chamazi iliyoanzishwa miaka mitano tu iliyopita.
Wakati wakongwe hao wa Tanzania wakiendeleza ubabaishaji, vigogo wa DR Congo waliosimamishwa kutetea taji lao la Ligi ya Mabingwa mwaka huu kwa kumchezesha mchezaji kimakosa, wamenunua ndege nyingine kwa ajili ya kusafirisha wachezaji wao katika michezo ya ndani na kimataifa.
Ndege hiyo mpya aina ya MD-83 yenye uwezo wa kubeba watu 140 ilitua jijini Lubumbashi juzi Jumapili.

Mazembe tayari ilishanunua ndege nyingine mwaka jana.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Moise Katumbi aliviambia vyombo vya habari kwamba amenunua ndege hiyo kwa lengo la kuwa moja ya klabu kubwa zaidi barani Afrika.”Tunataka kuwa Tembo wa Afrika katika soka na kulifikia hilo unahitaji kuwa na vitu vyote muhimu,”alisema.
Mwaka jana Mazembe ilitangaza bajeti yake ya dola 10m kwa ajili ya matumizi yao ya msimu huu. Hata hivyo, klabu hiyo mwaka huu haitakuwa na mechi yoyote ya kimataifa baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika, Caf.
Mazembe ilizuiwa kucheza mechi za kimataifa baada ya Simba ya Tanzania kuwashtaki mabingwa hao kumtumia mchezaji kimakosa hivyo Mazembe kutolewa katika raundi ya pili.
Caf ilibaini kwamba mchezaji Janvier Bokungu alikuwa na mkataba na klabu ya Esperance ya Tunisia, lakini akaichezea Mazembe.
Katika ligi ya DR Congo, Mazembe walipoteza nafasi ya kuwa vinara wa Ligi Kuu ya DR Congo Jumapili walipolazimishwa suluhu na mabingwa wa sasa Vita Club ya Kinshasa.
Vita Club inaongoza ligi ya DR Congo ikiwa na  pointi 23 ikifuatiwa na Mazembe yenye pointi 22.


DAN FLEVOR, Mganda anayetaka Kolabo na Wabongo!!

September 20, 2011

image

 

msanii kutoka Uganda anaitwa DAN FLEVOR ambae kwa sasa ameamua kuja Tanzania kwa lengo la kutengeneza fan base ya hapa TZ, pia anahitaji kujifunza kiswahili zaidi na kufanya kazi na wasanii wa TZ. Kati ya wasanii ambao Dan Flevor ana mipango ya kufanya nao kazi ni pamoja na Lady Jaydee na Linex. Wimbo huu ni hatua za mwanzo za kutimiza ndoto zake. wimbo umefanywa katika studio ya Tetemesha Recordz ya Mwanza chini ya producer Kid bwoy. Dan Flevor kwa upande wa Tz anasimamiwa kazi zake na Ujazo Entertainment.

 


%d bloggers like this: