Kauthar Toka Dar, Alex toka Mbeya na Neema wa Shinyanga waingia kikaangoni Maisha Plus

February 2, 2010

IMG_0079

Kipindi cha Maisha Plus bado kinaendelea na wiki hii majina matatu yametajwa kuingia kikaangoni ila kwa taarifa yako wiki hii hakuna mtu atakayetoka kwani unachotakiwa kufanya katika ya majina hayo matatu yaani Kauthar Toka Dar, Alex toka Mbeya na Neema wa Shinyanga, wawili kati yao wanatakiwa kwenda kwenye hoteli moja ya kula kuku.

Kauthar yeye anaingia kikaaongoni kwa mara ya tatu huku Neema akiingia kwa mara ya pili na Alex kwa mara ya kwanza. Siji kama ingekuwa kutoka nani ambaye angetoka kwani hatima huwa iko kwa watazamaji ambao humpigia kura mtu ya kubaki ambapo kwa wiki iliyopita Neema wa Shinyanga alipata kura zaidi ya elfu moja ili abaki huku mshiriki Kelvin kutoka Morogoro akiambulia kura mia tatu na ushehe tuu.

Angalia maoni ya wanakijiji juu ya nani atoke na kwa nini, Haya ni baadhi tu ya maoni yao.

Alex Mbeya ataka watu wajiamini na kusema kuwa kutokujiamini kunapelekea watu kuwa na hofu na kujenga makundi ndani ya kijiji.

 Neema Tabora

Neneema yeye kwa upande wake alilalamikia ushirikiano mdogo na kusema unapelekea watu kutengana akiwataka watu waishi kama wanavyoishi kwenye uhalisia wao huko nyumbani.

 

William Iringa

Alimlalamikia Kaushak akisema kuwa Kauthar hafai kuwa kiongozi kwa kuwa ni mdhaifu na hajiamini kwa kutolea mfano kuwa kuwa yeye ndie kiongozi wa makundi ndani kijijini.

 

Jeremiah Dar

Yeye kwa upande wake alimpendekeza Alex wa Mbeya atoke kwa kuwa anasema kuwa wakati wake umefika na yeye ndiye anawakoroga pale kijijini kwani amekuwa akiwachanganya na kuwatenganisha. Anasema pale kijijini kila mt anahaki ya kuamua nani anampigia kura

Taiba Zanzibar

naye alimppigia kura Alex kwa sababu zinazofanana na Jeriamia akisema kuwa Alex amekuwa akipita huku na huku kuwataka watu wampigie fulani atoke jambo ambalo kwake anaona ni kinyume cha maadili ya kijijini.

Mwishehe wa Dodoma

Anasema Kauthar anatakiwa atoke kwa kuwa hawezi maisha ya kijijini kwani hata yeye mwenyewe Kauthar wakati mwingine anasema kuwa maisha yale hayawezi. amekuwa akilalamika sana na kuonyesha kuwa ni mdhaifu kwa maisha yale ya kijijini. Aliongeza kusema kuwa Kauthar amezoea maisha ya uzunguni zaidi.

Jaquiline wa Moro

Yeye alimtaja Luthende, yeye alisema mshkaji ana bore sana na anatabia ya uchoyo na umimi sana. Hapendi ushirikiano na saa nyingine kitu kidogo kinaweza kuwa kikubwa huku akitolea mfano mshkaji anaweza kukunyima kisu tuu. Kwa mujibu wa Jaq yeye anapenda kukuza mambo.

 

Leonard toka Dar

alimpendekeza Neema Tabora kuwa atoke ni mvivu hawezi kuamka asubuhi anapenda sana kujipodoa hawezi hata kuchota maji kwa kuwa make up kibao sio. Anasema mshkaji anaushirikiano mdogo kwa sababu ya uvivu wake.

 

Luthende Tabora

Anamshukuru Mungu kwa kumpa uzima na anasema kuwa matatizo yaliyopo ni madogo madogo tuu, kwa upande wa mtu anampendekeza Kauthar, anasema yeye kama yeye anadhani kuwa mchizi anamchukia, ye anasema kuwa hamchukii kuhitilafiana ni jambo la kawaida tuu.

Kingine anasema kuwa yule dada anakosea lakini hataki kuomba msamaha hivyo inamfanya kuwa mbinafsi sana. Kingine aliwahi kulalamika kuwa anabaguliwa alipoambiwa ataje alishindwa ana kusema kuwa ata afanywe nini hataji. Huo ni udhaifu na ameonyesha kutoaminiana. Ila kwa mtazamo wangu nikiangalia naona hapa kuna issue kati ya wawili hawa. ni mtazamo tuu.

Kauthar Dar

Kama nilivyosema kwa Kauthar sijui kati yao ni nini kinaendelea maana kwa washiriki wengine pamoja na kuwa wanatajana majina lakini inawachukua muda mfupi kuelezea sababu za kum nominate mtu jambo ambalo ni tofauti kati ya Luthende na Kauthar, wao wamechukua muda mwingi kila mmoja kuelezea ubaya wa mwenzake.

Kwa upande wa Kauthar ambaye ni mmoja wa washiriki toka mkoa wa Dar Es Salaam, Yeye anasema Luthende hamfagiliii hata kidogo, na pia alilalamikia kuwa watu wanambeza na kusema kuwa msomali akishinda watanzania wataandamana. anasema Luthende hajawahi kumtreat kibinadamu lakini anamuona yeye hastahili kukaa kijijini pale. Anadai kuwa katika kuhakikisha matkwa yake yanatimia hadi Babu aliitwa ili eti yeye aweze kutoa ufafanuzi wa malalamiko yake na aliye engineer ni Luthende jambo ambalo yeye binafsi hakulifurahia hata kidogo.

Julius Arusha (Mmasai)

Anasema kuwa Alex atoke ana kelele na hawezi kuwapa watu wengine nafasi ya kuonyesha kipawa chake na anatumia mwamvuli wa Uchungaji kujifanya mtakatifu wakati mambo anayoyafanya hayana manufaa kwa jamii.

Julius anadai kuwa mtu anatakiwa atajwe kutokana na tabia yake na kusisitiza kuwa Tabia za Alex si za kiungwana, alisema kuwa kutofautiana ni jambo la kawaida na kutoa mfano kuwa hata unapofungia mbuzi kwenye uzio lazima hata mmoja ataruka.

Kwa mujibu wa uongozi, wiki hii unatakiwa kupiga kura ili washiriki wawili wakale misosi kwenye moja ya hoteli za kitalii kwani anayepigiwa kura hatotoka.

Hii inamaana gani hii itawafanya washiriki wapunguze chuku kwa kutajana majina kwa ajili ya visasi zaidi kwani inawafanya kujiona kuwa hakuna nafasi ya kusameheana au kulippiziana kisasi isipokuwa kum nominate mtu jambo ambalo si msingi hasa wa Maisha Plus.

Tuonane kesho tena kwenye muendelezo wa Maisha Plus….


Maisha Plus; Washiriki waanza kuonyesha Uhalisia wao!!

January 15, 2010

Wengi wapinga Pendo kulaumiwa!!

IMG_0080

Huku wakiwa na siku 12 katika kijiji cha Maisha Plus. Washiriki wa Reality Show ya Maisha Plus wameanza kuonyesha uhalisia wao na tabia zao. Katika siku za mwanzoni ilikuwa kazi kutambua tabia za watu kwani wengi  walionyesha kuigiza zaidi kuliko kuishi uhalisia wao lakini kwa sasa kila mmoja anaanza kutoa makucha yake” alisema mmoja wa mashabiki waliokuwa wakifatilia kipindi cha jana.

Mada hii ilikuja baada ya mshiriki mmoja kuamua kwa nia ya kufurahisha au kuchangamsha kuwatisha wenzie kwa kuvaa shuka jeupe na kujipaka poda usoni, wengi wa mashabiki walifurahishwa na kitendo kile na walisema kuwa kimeonyesha ubunifu na kuchangamsha kijiji.  Jambo ambalo lilipingwa na washiriki ambapo asilimia kubwa waliangukia kulaumu.

IMG_0102

Washabiki wengi walionyesha kukerwa na kauli ya mshiriki toka Zanzibar ambaye alisema kuwa hatomsamehe Pendo mwanzo wa dunia na hata mwisho wa dunia na haikanushi kauli yake, jambo ambalo lilitafsiriwa vibaya na mashabiki waliokuwa wakifuatilia show hiyo.

Kitendo cha Pendo si kibaya kuwatisha wenzio ndio mambo yanayotokea vijijini na katika maisha ya kila siku kwa umri wake na jinsi alivyo ule ni uhalisia wake, amefanya mchezo umechangamka sioni mbaya kwa kweli alisema shabiki mmoja kwa jina la mwafrika.

Binafsi nilifurahishwa na washiriki wawili tuu katika kijiji ambao walilichukualia suala hili kama kosa la kwanza na kutaka mwenzao apewe nafasi zaidi jambo ambalo lilipingwa zaidi na washiriki wengine na siku ikaisha.

IMG_0088

Likifika sualala kazi ndio utamjua mchapa kazi na mvivu, kwa upande huu jamaa wanajituma


Ni Grand Finale ya Maisha Plus

April 22, 2009
Washindaniao Million 10

Washindaniao Million 10

Shindano la Maisha Plus linafikia tamati Jumapili, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 papo hapo baada kudumu kwa siku 56.

Shindano hilo lililoanza Machi 1,2009 linafikia tamati ikiwa ni sehemu ya kwanza na ya pekee katika historia ya mashindano ya uhalisia( Reality Shows) nchini Tanzania.

Mratibu wa shindano hilo, David Sevuri anasema shindano hilo linamalizika huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Tulilenga kuwawezesha vijana kujitambua,Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali, Kuendeleza vipaji vyao,kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki,kubadilishana utamaduni na kuburudisha watazamaji, tunajivunia kusema kuwa tumeweza kufanikisha yote haya” alisema.

‘Eviction’ ya aina yake kufanyika Jumapili

Shindano limebakiwa na washiriki 10 ambao mmoja kati yao ndiye atakayechukua zawadi hiyo kubwa hapo kesho.

Mtoano utaanza kuonyeshwa kupitia TBC1 Jumapili saa tatu asubuhi ambapo kwa kuanza saa nne kamili asubuhi washiriki wawili wataaga na baadae washiriki wengine wataaga saa saba kamili mchana.

Mtoano wa mwisho utafanyika saa mbili na nusu usiku ambapo shindano litakuwa limebakiwa na washiriki watatu tu.

Mpigie kura mshiriki umtakaye ashinde

Miloni kumi imetengengwa kwa mshindi lakini uamuzi wa kumpa mshindi upo kwa mashabiki ambao ndio waamuzi katika shindano hili.

Maulid 33, Hamis 15, Moshy 19, Abdul 32, Charles 11, Steve 14, Upendo 18, Boniface 20, Teddy 36 na Modesta 37.

Unaweza kupiga kura kwenye mtandao ambao ni maishaplus.g5click.com au kwa njia ya simu kwenda 15522.

Maisha Plus kurudi tena

Ni miezi miwili imepita tangu shindano hilo lianze, kutokana na uhalisia wa shindano hilo kureflect maisha ya Watanzania wengi wameomba liendelee kuwepo,kwa mujibu wa waandaaji shindano hilo litarejea baada ya mapumziko ya muda mfupi.

Mraribu wa shindano hilo David Sevuri ameliambia Starehe kuwa kutokana na maoni ya watu wengi shindano hilo litakuwa tena TBC1 baada ya timu ya shindano hilo kijipanga upya.

“Tutarudi tena tukiwa tumeliboresha zaidi shindano hili, lakini watazamaji bado watakuwa na vitu vingi vya kutazama kwa wakati wote ambao hatutakuwepo kijijini kwa kuwa tuna vitu vingi havijaonyeshwa” alisema.

Sevuri alisema kipindi cha Maisha Plus cha Jumapili kitaendelea kama kawaida kwa muda wote wakati ‘season’ II ikisubiriwa.

Thank you all
Regards
Julieth Kulangwa


Maisha Plus: Nani kuibuka na M 10,000,000????????

April 18, 2009

maisha plus

Washiriki 10 tayari wamebakia kwenye mtanange wa Fainali ambapo hapo mmoja ndio ataibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha Reality Show ya Maisha Plus.

Pamoja na vigezo vingine kura yako ndio itatoa mshindi hivyo shime piga kura sasa.

Namba za kupiga kura ni hizo hapo chini ikiambatana jina na namba ya mshiriki.

Abdul …………32
Maulid ……….33
Upendo …….18
MOdesta …..37
MOshy ….…..19
Charles ….…11
Steve ……….14
Boniface …..20
Hamis ………23
Teddy ………36

Je Nani anafaa kunyakua zawadi?


Umepitwa na chochote kwenye Maisha Plus…?

April 16, 2009

kijiji

Usikose kuangalia hapa kujua nini kitatokea na kusoma maoni toka kwa wadau wetu ambao wanachangia sana Bonyeza hapa!! kusoma habari na story zote za Maisha Plus humu.

Baada ya kutegeshewa kinasa sauti ambacho kwa kiasi kikubwa kimewezesha kujua uhalisia wa watu wakiwa mbali na Camera nini kitafuata?

Usikose kuangalia Maisha Plus TBC 1 na kusoma Spoti starehe kila uchao kwa habari motomto.


Maisha Plus: Kumi bora kujivinjari Mikumi

April 15, 2009

Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwanguna ameahidi kuwapeleka washindi 10 wa shindano hili kwenda Mbuga za Wanyama za Mikumi mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo wiki ijayo.

Mwangunga alitoa ahadi hiyo alipokutana na washiriki hao Jumapili ya wiki iliyopita ambako alialikwa kama mgeni rasmi wakati wa mtoano ( Eviction)  wa mwisho wa sehemu ya kwanza ya shindano hilo.

"Mmeonyesha ujasiri wa hali ya juu kwa kuweza kufanya kazi ngumu kwa kipindi kirefu, mimi kama mama ninawapa zawadi ya kwend akupumzika katika mbuga za wanyama Mikumi zilizopo mkoani Morogoro" alisema.

Asha na Nassib nje

Asha kushoto na Nasib kulia

Baada ya ‘Fake eviction’ wiki hii washiriki wawili kutoka Zanzibar na Mbeya wameliaga shindano hili ambalo limebakiza wiki mbili lifikie tamati.
Nassib alikuwa mshiriki pekee aliyekuwa amebaki ndani yashindano hilo akiwakilisha mkoa wa Mbeya baada ya Kissa kuondoka wiki tatu zilizopita.
Kuondoka kwa Asha kunamfanya Abdul awe mshiriki pekee anayeiwakilisha Tanzania visiwani katika shindano hili.

Mwanza Juu

Mkoa wa Mwanza ndio mkoa pekee unaowakilishwa na washiriki wote watatu mpaka katika hatua ya fainali huku mikoa mingine kama Tanga ikiwa imepoteza washiriki wake mapema.
Mwanza inawakilishwa na Moshy Mahona, Boniface Michael na Upendo Peneza ambaye ndiye pekee aliyewahi kuingia kiaangoni huku wengine wakiendelea ‘kutesa’.
Mikoa ambayo imepoteza washiriki wake wote ni Tanga, Dodoma na Mbeya.

Nani kunyakua milioni kumi?

xxxx
Nani kata ya hawa 10 atanyakua kitita cha shilingi milioni kumi, Jumapili ya tarehe 26 mmoja kati ya washiriki atakwenda nyumbani na kitita cha shilingi milioni 10.
Je ni Boniface, Maulid, Upendo, Steve, Teddy, Charles, Moshy, Hamis (Kingunge), Modesta au Abdul? endelea kufuatilia habari zao katika mtandao wa maishaplus.g5click.com na Tazama TBC1 kila siku.

Usikose kutembelea Spoti na Starehe kujua nini kitafuata ndani ya Maisha Plus!!


Maisha Plus wiki hii

April 10, 2009

Charles na Steve Kikaangoni tena


Washiriki wawili kutoka Arusha ambao mwishoni mwa wiki hii waitolewa na kwenda kula bata katika hotel ya Grand Villa wamepigiwa kura tena na kurudi kikaangoni na sasa watapigiwa kura tena Jumapili hii.

Jumanne ya wiki hii washiriki hao walirudi kijijini baada kupigiwa kura za kwenda kula bata lakini wiki hii wawili watakaotolewa watarudi makwao moja kwa moja.
Wiki hii washiriki hao wamewekwa kikaangoni na washiriki wengine wawili kutoka Zanzibar na Mbeya, Asha na Nassib.
Wiki hii washiriki wawili watafunga pazia la kuondoka na shindano hilo litabakiwa na washiriki 10 wa mwisho.

Nani kuaga wiki hii, unaweza kumuokoa mshiriki wako kwa kumpigia kura kwenda namba Chaz 11, Steve 14, Asha 31 na Nassib 23.

Kukesha Masaa 48, Steve awa wa kwanza kulala

Baada ya washiriki wawili kurejea kijijini washiriki wakapewa task ya kushindania shilingi milioni moja kwa kutolala kwa masaa 48 kuanzia saa sita usiku Jumanne wiki hii.
Mshiriki kutoka Arusha pamoja na kulala kwa siku mbili mfululizo alijikuta akiwa wa kwanza kuanza kulala masaa matano tu tangu kuanza kwa shindano hilo.
Steve alilala saa 12.30 asubuhi ya siku ya kwanza na kufuatiwa na  Abdul na Maulid ambao kwa pamoja walilala saa tano asubuhi siku ya kwanza ya shindano hilo.


Kwenye Maisha Plus wiki hii!!

March 31, 2009

Kissa out!!

Mwanamke pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Mbeya, Kissa Kiposa ameaga mashindano haya Jumapili ya wiki hii.
Kisa ambaye alikuwa kikaangoni na washiriki kutoka Mwanza na Dar es Salaam, Maulidi Wadi na Upendo Peneza aliaaga baada ya kukosa kura nyingi za kumwezesha kuendelea kubaki ndani ya shindano hilo.
Kissa alilazimika kurejea nyumbani akiwa peke yake tofauti na ilivyozoeleka baada ya mshiriki mmoja kuondoka wiki iliyopita, Juma Madaraka.

Machalii wa Arusha kikaangoni

Machalii wawili wanaowakilisha pande za A Town, Charles Ngaja na Steve Sandhu wamewekwa kikaangoni lakini kama watapa kura nyingi hawatarudi makwao na badala yake watapelekwa kula bata katika hoteli ya Grand Villa iliyopo maeneo ya Kijitonyama.
Kama kawaida washiriki hao hawajui kama wamependekezwa na pia siku ya Jumapili kama wakitolewa hawata aambiwa kama kutolewa kwao ni FAKE.
Wasichana wawili kutoka Dar na Zanzibar, Asha na Modesta nao wanaiwania nafasi hiyo ya kwenda kula bata kwa siku mbili.
Washiriki watakao tolewa watakaa kwa siku mbili katika hoteli hiyo bila kuambiwa kinachoendelea na usiku wa siku ya Jumanne watarudishwa kijijini ambako pia wanakijiji wenzao watakuwa hawaufahamu mpango mzima.

King Kong atimba kijijini

Chidi Benzino akiwa na chama zima la Familia aliibukia kijijini usiku wa ‘Live’ ya mtoano na kufanya shoo ya ‘Surprise’ kwa washiriki wa shindano hilo.
Pamoja na kuburudisha Chid pia alizungumza na washiriki huku akipigwa maswali ya hapa na pale ambayo yalimlazimu pia kukanusha tuhuma za kuwa na Bif na Profesa Jay.
Washiriki walimuuliza kama kweli ana ugomvi na msanii huyo  naye kwa kifupi alikanusha kwa kusema kuwa hana bifu na msanii yeyote Bongo.

Namba za kupigiwa kura za washirki walioko kikaangoni

Charles 11,  Steve 14, Asha 31 na Modesta 36

Unaandika MP then namba ya mshiriki na unatuma kwenda 155222


Maisha Plus Updates: Grace na Levina out!!

March 24, 2009

Mshiriki pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Tanga, Levina Abdon ameyaaga mashindano haya baada ya kutopigiwa kura nyingi ambazo zingemuwezesha kubakia katika shindano hilo .
Levina ambaye ameweka rekodi ya kuwa mshriki pekee aliyekuwa na ujasiri alikuwa akiwaukilisha mkoa wa Tnaga baada ya washiriki wawili kuodnolewa katika hatua za awali za shindano hili mapema mwezi huu.
Washriki waliokuwa wakiuwakilisha mkoa wa Tanga ni Ramadhani Runza na Athanas Milanzi ambao waliodnolewa katika  hatua za mwisho za shindano hilo lililofanyika Machi 1 mwaka huu.
Naye Grace Samuel amekuwa mshiriki wa kwanza kuondoka anayeuwakilisha mkoa wa Mwanza.
Zanzibar na Mwanza ndiyo mikoa pekee iliyokuwa ikiwakilishwa na washiriki wote watatu.mkoa huo sasa unawakilishwa na Asha Alfan na Abdulkhalim Hafidhi.

Grace, Modesta na Teddy wazimia

Toka Kushoto; Modesta, Teddy na Grace


‘Eviction’ ya wiki hii ilitawaliwa na vilio baada ya washiriki watatu kuzimia baada ya kupokea matokeo.
Washriki hao walizimia kila mtu akiwa na ‘emotion’ yake, Teddy alizimia baada ya kuambiwa anabaki kijijini wakati Grace alizimia baada ya kuambiwa kuwa anarejea nyumbani.
Katika hali ya kushangaza mshiriki mwingine ambaye hakuwepo hata kwenye ‘nomination’ alizimia kizimbani wakati akimwondoa Teddy aliyeanguka na kuzimia kizimbani.

Maulid Kikaangoni tena

Baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuwatoa washiriki wawili Jumapili hii, washiriki wengine watatu walipendekezwa kuingia katika kikaango cha kupigiwa kura.
Washiriki waliopendekezwa wiki hii ni Maulid kutoka Dar es Salaam , Kissa kutoka Mbeya na Upendo kutoka mwanza.
Hii ni mara ya pili kwa Maulid kupendekezwa, wiki ya kwanza alipenya baada ya kuwa amependekezwa sambamba na Efrancia

Mangii na Putir Peter.

Mshiriki wa Dodoma atolewa kwa ugonjwa
Mshiriki  pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Dodoma , Juma Madaraka amelazimika kuyaaga mashindano haya baada ya kuugua Typhoid na Malaria kali kwa muda wa siku tatu.
Mshiriki huyo alilazwa hospitalini kwa siku tatu katika hospitali hospitali moja iliyo karibu na kijiji cha Maisha Plus.

TID aka Prison Voice atua kijijni

Khalid Mohamed, maarufu kama TID a.k.a Prison Voice alitumbuiza katika shoo ya Surprise iliyoandaliwa kwaajili ya washiriki hao dakika chache kabla ya kufanyika kwa ‘eviction’.
Washiriki walilipuka kwa shangwe ya aina yake kwa kuwa ilikuwa ni mara yao ya kwanza kumuona msanii huyo tangu alipomaliza kutumikia kifungo chake mwishoni mwa mwaka jana.
TID ambaye alimbatana na Inspector Felly aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project Fame mwaka jana.


Efrancia na Putir out ndani ya Maisha Plus!

March 16, 2009

Kama tulivyoahidi awali kuwaleteeni updates za shindano la Maisha Plus,

Washiriki wawili waliokuwa wakiwakilisha kanda ya kati, Efrancia Mangii (kulia) na Peter Putir (Shoto) wameliaga shindano la Maisha Plus hilo huku Maulid Wadi akirejea baada ya kupata kura nyingi.

Washiriki hao wamefungua dimba la kuaga katika shindano hilo lililoanza wiki mbili zilizopita. Shindano hilo linabakiwa na mshiriki mmoja anayewakilisha kanda hiyo, Juma Madaraka.

Wakati huohuo Putir ameapta shavu la kutangaza katika kituo cha redio cha TBC Fm mara baada ya utolewa katia shindano hilo.

Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando aliitangaza ofa hiyo wa Putir baada ya uvutiwa na sauti nzuri ya mshiriki huyo.

Watatu kikaangoni tena

Washiriki watatu kati ya 16 waliobakia wametupwa tena kwenye ukanda wa hatari ya utolewa huu mchakato huo ukiendeshwa kwa namna ya pekee.

Mara baada ya kumalizika kwa shoo ya moja kwa moja ya kuwatoa washiriki wawili washiriki 16 waliobakia walitiwa kupendekeza majina ya watu wanaowakwamisha katika kazi zao wanazopewa kila siku.

Washiriki wawili kutoka Zanzibar, Abdulhalim Hafidhi na Grace Samuel walipendekezwa katika mchakato huku mshiriki pekee kutoka Tanga, Levina Abdon naye akianguka katika kikaango hicho.

Katika mchakato wa wiki hii majina ya washiriki yaliyo Katika kikaango hayakutajwa mbele ya washiriki na badala yake yatadhihirishwa jumapili wakati watakapotakiwa kutoka na kila kitu chao tayari kwa safari.

Hakuna jina la mshiriki litakalotajwa mpaka siku ya jumapili ambapo wote watakuwa na mizigo yao tayari kwa safari kwa watakaotajwa.

Imetayarishwa na Julieth Kulangwa


%d bloggers like this: