WERRASON NA JB MPIANA WAMPONGEZA PAPA WEMBA KUTOKANA NA NDOA YAKE YA KANISANI

 

PAPA WEMBA : Shukrani zangu za dhati zimwendee MAMA huyu ambae si mwengine bali ni MKEWANGU,Yeye kanivumilia katika kipindi cha Miaka 44. Yeye ni Shahidi kabisa wa Uhuni wangu wote niliokua nao katika kipindi chote hicho. Kutokana na hayo yote, Ndipo nikachukua Uamuzi wa kumleta Kanisani,Kanisa lililo nikuza katika Imani yangu ya Ukristo,Nimemleta Mke wangu Ilitupate kuungana wote kwa pamoja katika IMANI. ASANTE SANA MKE WANGU

MAMA AMAZONE : NI KWANGU MIMI KUKUSHUKURU KWA HESHIMA ULIONILETEA!!!

JB MPIANA : PAPA WEMBA MZEE EKUMANYI LE KURU YAKA, ambae kwa siku hizi kajulikana zaidi kwa jina la ” MAÎTRE D’ÉCOLE “, WEWE NI MKUZAJI WA VIPAJI, KAMA LEO HII BAADHI YA WATU HUJITOKEZA NA KUA MA STAR, NIKUTOKANA NA MCHANGO WAKO ULIO MKUBWA.

Kwakweli sisi Wadogo zako, Sisi Wanao,tunayo furaha sana kuona Umetuletea Heshima. Waheshimisha kabisa Kazi ya Muziki Inchini Congo.Waondoa Doa kubwa machoni mwa watu ambao wengi kati yao hufikiria kwamba kazi ya Muziki niya WAHUNI. Kwakweli kwangu mimi Kitendo cha Wewe kufunga Ndoa,kimeniletea raha sana moyoni mwangu.Wamuheshimisha MAMA mbele ya MWENYEZI MUNGU,Wahitimisha hitaji kubwa ambalo Wanawake wengi hua wakilisubiria maishani mwao. ” KUVAA USHUNGI WA NDOA ” .

Katika Imani yetu ya Kikristo,Mwanmke hufunga Ndoa Mara moja,wala si mara mbili, KITENDO CHENU CHA KUFUNGA NDOA BAADA YA MIAKA 44 YA KUISHI KWA PAMOJA, BASI NI JAMBO MUHIMU KABISA NA SOMO TOSHA KWAKWELI. Ni mangapi ya Shari kama vile ya Raha mlioyapitia? Ila uamuzi wa mwisho ni kufunga Ndoa tena Kanisani. Kunakipindi fulani Mlifanya dhiara kwenda ROMA, na huko Mkakutana na PAPA ambae kawabariki,kwa wakatiule,mlikua bado si Wanandoa, Kwasasa Nyinyi ni Bwana na Bibi Harusi. TUNAWASHUKURU SANA KWA HILO. NAWATAKIA KILA LA KHERI,NAHISI NA SISI PIA TUPO MBIONI KUZIFWATA NYAYO ZENU. ASANTE SANA PAPA WEMBA, HONGERA SANA KWAKO MAMA AMAZONE MUKARAME.

WERRASON : Nashukuru sana kwakunipa kauli, Kwakweli Tukio la PAPA WEMBA kufunga Ndoa,limefwatwa na Wengi Uliwenguni kote. Kilicho kizuri zaidi nikuona twaheshimika sisi WANAMUZIKI.

KWETU SISI, YEYE NI BABA,KAKA,TAYARI YUKO NA WAJUKUU,PIA ANAO WADOGO WENGI,NA MAMILIONI YA WATU WAPO NYUMA YAKE NA HUA WANAMPENDA.

Kwa siku hizi,Watu walipuuzia sana Tendo hilo muhimu la kufunga Ndoa, wakati hata katika Biblia yapo maandishi yanao tushurutisha tufunge Ndoa. NDOA NIKUMUHESHIMISHA MKEO MBELENI MWA MWENYEZI MUNGU, NA MACHONI MWA BINADAMU.WAONYESHA KWAMBA WEWE NA MKEO NI KITU KIMOJA,MWILI MMOJA.

Nafikiri katika Kipindi kirefu cha Miaka 44,Wamejenga Maisha yao kwa pamoja,Wamezaa watoto, kadhalika wametokea kuwapata Wajukuu wengi. KWAKWELI FURAHA ILIOJE KUONA WAMEHITIMISHA AGANO LA NDOA.

Kitendo hicho ni Heshima kubwa kwa sisi Wasanii hasa wanamuziki. MAMA AMAZONE, KATIKA KIPINDI CHOTE HICHO CHA MAISHA YENU NA PAPA WEMBA, YAPO MAMBO MENGI YALIYO JITOKEZA,YA HUZUNI KAMA VILE YA FURAHA, NTAKUOMBA UYASAHAU KABISA YALE MABAYA,NA UYAPEKIPAUMBELE KAULI MBILI MUHIMU ZAIDI NAZO NI : ( SAMAHANI NA ASANTE ).

Binafsi niliudhuria Sherehe ya Ndoa yenu nikiongozana na MAMA PASTEUR (SYLVIE MAMPATA ) NILIPATWA NA FURAHA TELE MOYONI MWANGU. Watu wengi walijitokeza kuwa mashahidi wa tukio hilo,Maandalizi yalikua mazuri sana, NIKASEMA MOYONI KWAMBA : KITENDO HICHI NDO SALIO LA MWISHO LA PAPA WEMBA ,HATIMAE KAFUNGA NDOA.

KWAKWELI PAPA WEMBA, SISI WADOGO ZAKO HATUNA BUDI KUZIFWATA NYAYO ZAKO,KWETU SISI WEWE NI MFANO, NI KWAMAANA HIYO HUA NAKUITA ” KOCHA “.

Kitendo chenu cha Kufunga Ndoa, ni somo kubwa kwa wengi, yaani Watu Mnakaa kimapenzi kwa miaka kadhaa,Mnazoeana,Ni jambo la kawaida Kwa matatizo kujitokeza wakati Watu mnaishi kwa pamoja, ila mnakabiliana nayo,mwisho wa mwisho mkaja kuchukua uamuzi wa kufunga ndoa, RAHA ILIOJE ? na Baada ya Ndoa nikipi kingine cha muhimu zaidi kilicho salia maishani mwa Mwanadamu? hakuna!!!

MZEE BOKOUL ( PAPA WEMBA ) Ni Mtu mwenye Ushahuri mwema. KWAKO WEWE MAMA AMAZONE, NAJIONA MTU MWENYE RAHA SANA, WEWE NI DADA YANGU. ASANTE SANA

LUBONJI WA LUBONJI

One Response to WERRASON NA JB MPIANA WAMPONGEZA PAPA WEMBA KUTOKANA NA NDOA YAKE YA KANISANI

  1. Odessa Knori says:

    Extremely good weblog and fantastic and articles or blog posts.precious style, as share great stuff with good tips and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: