Tafsiri ya Voyage ya Mboso yakwake Adolph Dominguez na Wenge Musica

August 30, 2013

Na Lubonji wa Lubonji

Ni wimbo ambao uliwahi kuleta ubishani nani hasa mtunzi wake, Kuna nyimbo ambazo kwa mashabiki wa Wenge Musica kwa ujumla wanazikumbuka sana wimbo huu wa Voyage Mboso, Wengi walijua huu Wimbo ni Wimbo wa JB Mpiana lakini ukweli ni kuwa huu ulikuwa ni Wimbo wa Adolph Dominguez na ndio maana walipoparanganyika Werasson alikuwa akiupiga sana wakati bado yuko na Dominguez na walipoanchana Werasson aliacha kuupiga na Dominguez aliendelea kuupiga.

Kwenye Original Version utamsikia vizuri Ekokota Machine Roberto Wunda,kwenye vyombo ni Patient Kusangira, Didie Masela Vando Mass, Mbonda na wengineo. Kwa kifupi katika wimbo Voyage (Safari ) Mwimbaji Adolphe Dominguez anaongela Safari na hatari zake kwa wapendanao!!!

Nini toweli ngai nayoo : kitugani kinacho leta ugonvi kati yetu?
Awa natikali Likombe yaya : Tizama ninavyo baki mpweke Kaka yangu!!!

Wapi O remplacer Ngai Voyage : Safari, Lini ukaja kuchukua nafasi yangu kwenye ndoa…

Mbala ya sima nako Refuser : mara nyingine sintokubali (usafiri)
Voyage!!! Ponini usalaka boye!!! : Safari!!! kwanini hufanya hivyo!!!

Okotika moto na Soucis!!! : wafanya mtu kabaki na majonzi
Désespoir na kati ya motema : Moyo wangu wakata tamaa!!!
Soki Likambo nani ako Consoler!!! ikitokea neno, nani yule atakae nifariji!!!
Soki Likambo nani akosalisa : nikipatwa na shida ni yupi atakae nisaidia!!!
Tuna Meje Kanuse ndenge azangaki Mc Mpanda kaka mpo na voyage : Muulizeni Meje Kanusi alivyo mkosa mpenzi wake Mc Mpanda kutokana na Safari.
Marie France Shungu azangaka Béa!!! kaka mpo na Voyage : Marie France Shungu nae kaachana na Béa kutokana na Safari!!!
Tuna Jeannot Canon ndenge azangaki Sabartino kaka mpo na voyage!! :
Muulizeni pia Jeannot Canon alivyo achana na Mpenzi wako Sabartino kisa ni Safari.
Pepo ekomataa!!! Ndege ndo hiyo ya Paa!!!
Masua ekochora ee!!! : Meli nayo yaondoa nanga!!!
Motema mauwaa!!! : moyo unauma na kusononeka!!!
Loboko ekopepa oyo akei!!! Mkono unampepea huyo anae safiri!!!
Voiture yo Complices : Gari nawe pia wanilia njama kwa kumpeleka Mpenzi wangu uwanja wa ndge!!!
Basusu bakokendeke Voyage ya makambo : Wamoja hua wanasafiri kutokana na mambo yao Flani!!!
Basusu bakokendeke Voyage ya Kelasi : wengine wana safiri kutokana na Shule!!!
Basusu bakokendeke Voyage ya Ba Affaires : Na wengine pia husafiri kwa mambo yao ya Biashara…


Happy Anniversary kwetu

August 26, 2013

387285_10150993246120154_773730153_22252945_2020409680_n

Tarehe 24 August 2001 nilifunga ndoa na mke wangu mpenzi Isabella Ghaty, mpaka leo tarehe 24 August 2013 ni takribani miaka 12 tumetimiza. Ni Miaka 12 ya ndoa iliyotanguliwa na miaka mingine sita ya kufahamiana hivyo kufanya maiaka 18 ya urafiki ambayo mi naijali sana.

Nasema naijali kwa kuwa urafiki ndio hudumisha upendo na kama hakuna urafiki ni sawa na kujenga nyumba kwenye mchanga bila misingi imara ni wazi msingi usipokuwa imara lazima ipo siku nyumba hii itaanguka au kama kunatokea dhoruba ni rahisi mjengo huu kuathirika.

Ni miaka 18 yenye historia, kwa vijana tuliooana kwenye umri mdogo chini ya miaka 25 ni wazi tunapitia majaribu mengi kama kwenye wimbo wa Voyage ya Mboso Dominguez amesema Safari isiyo na taa kwani hujui cha kesho ila mnakwenda tuu, mambo mengi yamepitia ikiwemo machungu na mazuri, katika safari ambayo tulishuhudia kumpoteza mtoto wetu Kipenzi Loreen ambaye aliugua na kufariki ghaflam ni machungu ambayo huwezi muadithia mtu lakini kwa kudra zake mola tumeyapita yote na bado tuko pamoja.

Namshukuru Mungu kwa kunipa mke mwema kama wewe Mamaa Ghaty kwani sijuti kukujua na wala sijuti kukuoa natumai Mungu aliye mwema atatuongoza mpaka kifo kitakapotutenganisha. Pia kwa namna ya pekee twamshukuru kwa wanetu Glory na Geebril, twamuomba waongoze na kuwapa hekima ili waweze kufuata nyayo za wazazi wafanikiwe katika maisha yao.

Nawaacha na Kibao Voyaje ya Mboso toka kwao Wenge Musica BCBG chini ya utunzi wa Adolph Dominguez.

Kwa kifupi katika wimbo Voyage (Safari ) Mwimbaji Adolphe Dominguez anaongela Safari na hatari zake kwa wapendanao!!!

Nini toweli ngai nayoo : kitugani kinacho leta ugonvi kati yetu?
Awa natikali Likombe yaya : Tizama ninavyo baki mpweke Kaka yangu!!!

Wapi O remplacer Ngai Voyage : Safari, Lini ukaja kuchukua nafasi yangu kwenye ndoa…

Mbala ya sima nako Refuser : mara nyingine sintokubali (usafiri)
Voyage!!! Ponini usalaka boye!!! : Safari!!! kwanini hufanya hivyo!!!

Okotika moto na Soucis!!! : wafanya mtu kabaki na majonzi
Désespoir na kati ya motema : Moyo wangu wakata tamaa!!!
Soki Likambo nani ako Consoler!!! ikitokea neno, nani yule atakae nifariji!!!

Soki Likambo nani akosalisa : nikipatwa na shida ni yupi atakae nisaidia!!!

Tuna Meje Kanuse ndenge azangaki Mc Mpanda kaka mpo na voyage : Muulizeni Meje Kanusi alivyo mkosa mpenzi wake Mc Mpanda kutokana na Safari.

Marie France Shungu azangaka Béa!!! kaka mpo na Voyage : Marie France Shungu nae kaachana na Béa kutokana na Safari!!!
Tuna Jeannot Canon ndenge azangaki Sabartino kaka mpo na voyage!! :
Muulizeni pia Jeannot Canon alivyo achana na Mpenzi wako Sabartino kisa ni Safari.

Usikose ijumaa nitaumalizia, Shukrani za Kipekee kwa kaka Lubonji wa Lubonji kwa Tafsiri hizi mwanana.


Tafsiri ya Wimbo Dis moi Amour

August 26, 2013

NA LUBONJI WA LUBONJI

Nawaleteeni Tafsiri ya Wimbo Dis Moi Amour ambao unapatikana kwenye albamu ya TH ya Wenge BCBG chini ya JB Mpiana, ni moja ya Rhumba ambazo kiukweli bado zinapendwa sana mpaka wa leo, Shukrani za kipekee kwa Le Suveree Lubonji wa Lubonji ulipotea sana kaka karibu tena natumai umekuja na mengi toka likizo yako.

Wimbo huu ni umeungwa na Kuimbwa na JB Mpiana Mukulumpa Le Maréchal Mukulu.

Seul Les Enfants savent aimer sans calcul. Dis moi Amour I love you:
Watoto pekee ndio wanao uwezo wakumpenda mtu bila hesabu yeyote.

Niambie mapendo I love you…
Comme une graine de diamant dans le deser ,amour je t’avais long temps cherché sans succès!!! sans succès!!! :
Kama vile kutafuta mchanga wa alimasi jangwani, pendo nakutafuta siku nyingi bila mafaanikio

oh ce soir mon coeur me souffle certaine melodie pour toi Amida ,moi ma claté ta beauté un Chef d’œuvres divin :
oh usiku wa leo,moyo wangu wapata pigo na msukumo wa kuimba wimbo huu kwa ajili yako Amida mtoto mwenye uzuri na urembo kutoka kwa Mungu.

Embrassé moi, serre moi dans te bras, mais dis moi pourquoi, tu m’envoûtes si tant,
mon jardin des roses, Amida tu exaltes le parfum du paradis!!! voilà que tu me rends si fou de toi!!! :

Nibusu,nikumbatie,niambie kwanini wanivutia sana namna hiyo, wewe ni bustani yangu ya pink flower, Amida wanukia marashi ya mbinguni,tizama wanifanya niwe kichaa kwa ajili yako.

Je t’aime, i love you,na kupenda sana oooh l’amour toujour, l’amour :
Nakupenda,oooh mapendo kila mara mapendo!!!

Tu fais le bonheur des uns, tu fais le bonheur des autres :
Mapendo !!! waleta furaha na raha kwa wamoja, wajaza majonzi na machozi kwa wengine.

Amour mystère dis moi ton identité eeee!!! qui es tu uuuuuu!!!
Mapendo wewe ni fumbo pia ni siri jitambulishe basi!!! wewe ni naniiiii!!!

Amour dis moi quel est ton Pays, pour que je vienne et que je construise un Paradis plein de toi!!! :
Mapendo niambie inchi yako ni ipi ili nije na nijenge paradise iliojaa wewe peke yako.

entourer d’une muraille de sécurité pour autre amour :
Bustani yenyewe nitaijengea ukingo mrefu wakuzuia pendo zingine zisije kupenya!!! .

Contre les charlatans de l’amour!!! contre les trafiquants de l’amour!!!:
ukingo utakao zuia walaghai wa pamenzi, pia waongo wa mapenzi!!

Amène moi ce soir!!! Amida!!! à la planète Venus!!! Amida, la planète des amoureux!!! Amida!!! conduis mois s’il te plait!!! Amida!!!:
twende wote usiku wa leo!!! Amida!!! kwenye sayari Venus!!! Amida!!! sayari ya wapendanao!!! tuongozane njia tafadhali!!! Amida!!!

Kataja majina kadhaa kwa kuwa dedication : MIMI KALUDJI,NÉNÉ MAKITAKANA,NELLY BOMEI, JACINTHE MWANANGANI, SHANY SHATUR, GRACE NJEKA, LILLY LA RÊVE MATITI…
Asanteni Bana Wenge Musica!!!


Sebene la Ngwasuma Balaa

August 26, 2013

Ni Moja ya bendi za Tanznaia ambayo imekaa kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu na kujipatia mashabiki wake ambao wengine wanaifata hata iende wapi, majina kama Madenge, J Single, Abdul Tall, Ndama aka Akayesu, Julie Weston Ilunga aka Babaa B na wengineo, ni majina utayasikia kila siku bendi hii ikipiga hata iwe tunduma au Mlimba. Hii ni kuonyesha ni jinsi gani wamejipatia nafasi yao kwenye soko la burudani bongo hii.

Nawakubali sana Ngwasuma ikija suala zima la Sebene, wanavyojituma bila kulewa sifa za mashabiki wao, hebu angalia video hii uone ma stage show walivyolishambulia jukwaa.


Christian Bella Mkali wa Bongo Rhumba

August 26, 2013

Kipimo kikubwa cha mwanamuziki hasa wanaoimbia kwenye bendi ni pale wanapotaka kutoka peke yako (Solo). Nasema ni kipimo kikubwa kwani hata waliona majina makubwa wamejikuta wakibwagwa na soko na mashabiki na wengine wameishia kubadili fani. Nani asiyejua Kilichompata Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Titina Alcapolne na wengineo wakubwa wanje kwa humu ndani kuna watu kama Ndanda Kosovo Kichaa, ambaye kwa wakati fulani jina lake lilikuwa juu akaamua kutoka kivyake lakini hakufanikiwa.

Nimeanza na kukukumbusha hilo kwani kwa mwanamziki kama Christian Bella angeweza kuwa Ferre Gola wa Tanzania na kama napata nafasi ya kuongea naye ningemwambia akomae kwenye nyimbo za taratibu tuu, Bella ni mmoja wa wanamuziki ambaye si tu anakipaji kikubwa cha utungaji bali hata cha kuimba bila kukinaisha. Sio kila mwanamuziki anaweza kuimba wimbo mrefu akakuvutia lakini nachelea kusema kuwa Bella ameonyesha kuwa anaweza.

Aina ya muziki anaopiga kiukweli huwezi kufananisha na wengine kwani anauwezo wa kujitengenezea mashabiki wake tuu, Tanzania hakuna bendi ya muziki wa dansi inayopiga Rhumba kiukweli, na ndio maana kwenye albamu ya Dunia Kigeugeu ya FM Academi nyimbo kama Acha Tamaa zilishika na bado watu wanazipenda mpaka wa leo kwani ni aina ya nyimbo ambazo ni nadra sana kuzisikia. Binafsi natamani sana niendelee kumsikia mtu kama Bella akiendelea na Marhumba haya ya ukweli atupe burudani mashabiki wa Rhumba.

Bella anaweza kabisa kuendelea aina hii ya muziki ambayo itakuwa ni style yake, kiukweli nimemiss kusikia hivi vitu toka kwenye bendi za densi za nyumbani Bongo Rhumba ni style ambayo Bella, au Rogert Hega au Ige Muyamba wanaipatia sana sijui ni kwanini tu hawatii mkazo humo.

Ukisikiliza wimbo huu ambao ameshirikiana na mtaalamu mwingine wa masauti Banana Zollo utakubaliana na mimi kuwa Bella ni kiboko. Nakutakia Jumatatu tulivu.


Harusi ya Zadio Kongolo gumzo Congo

August 25, 2013

Ni mtu wa karibu sana kwa Muziki wa Kongo na shabiki namba moja wa JB Mpiana akisifika kwa utunzaji wake ambapo kwa kuthamini hilo JB Mpiana ameshamtungia nyimbo kadhaa mbali na kumtaka kwenye karibu kila wimbo wake.

dedication

Ni mfanyabiashara wa madini na mtoto wa mjini mtafuta maisha ambaye anatumia kila njia kujipatia kipato chake. Harusi hii mbali kutumbuizwa na bendi kadhaa ilihudhuriwa na matajiri na watu maarufu wakiwemo wanamuziki mbalimbali wa Congo.

Kwa mujibu wa mtangazaji maarufu wa Luninga na mtengenezaji wa vipindi vya majadiliano almaarufu kama Zacharia Bababaswe anasema kwamba Harusi hii pia imetajwa kuingia kwenye historia ya moja ya harusi kubwa kupata kutokea kwa Mkongoman si tu ukubwa wa Harusi bali iliyogharimu pesa nyingi sana.

Zadio amemuoa mpenzi wake wa siku nyingi binti mrembo anayejulikana kwa jina la Carole katika sherehe zilizofanyika huko huko Ufaransa. Zadio au ZK kama alivyoitwa na mashabiki wake anajulikana kwa style yake ya utunzaji awapo jukwaani ambapo kuna wakati anatunza mpaka dola zaidi ya 20,000 katika show moja.

Nikuache na kibao ZK aka Zadio Kongolo toka kwake JB Mpiana, akiwa na Wenge BCBG kikiwa ni mahsusi kwa kijana huyo tajiri.


Bado “namlilia” Chai Ngenge

August 25, 2013

Kiukweli naipenda sana Wenge BCBG na huwa siwezi kuficha hisia zangu kwenye hilo, lakini kwa miaka ya karibuni karibu watu wote ambao binafsi nilikuwa nawapenda sana ndani ya bendi hii wameondoka.

Pengo kubwa la kwanza kwangu ilikuwa kuondoka kwa Aimelia ambaye nilimpenda sana alivyokuwa akichanganya sauti yake humo, ila huyu hakuniuma sana kwani JB Mpiana alikuwa na uwezo wa kuliziba pengo lake vilivyo na kwa wasio wajua kwa sauti zao huwezi kujua akiimba JB Mpiana au akiimba Aimelia Lyase Doming’ong’o. Pia kwa mtu kama Titina Alcapone ambaye aliwachezesha vilivyo kwa upigaji wake hatari wa drums, kidoogo naye amepokewa vizuri na Seguine Mignon ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa ndiye mpambe wa kribu kabisa wa JB Mpiana na muda mwingi anakuwa naye na ndiye mtunza siri wake huku wangine wakimtania kuwa Kaka yao akina Daida, waototo wa JB Mpiana.

Pendo jingine ambalo bado naliomboleza mpaka leo ni kuondoka kwa Allain Mpella Afande ambaye kwenye wimbo huo hapo anasikika kuanzia 4:06 na sauti yake mwanana, kiukweli Pengo la Afande halijazibika mpaka leo kwani alikuwa akiimba sauti ya Pili na ya Tatu vilivyo. mbali na wengine ambao waliondoka ondoka hapo katikati kwa sababu moja au nyingine.

Sio siri kuondoka kwa Tutu Kaludji pia kulikuwa tingisho jingine kwa JB Mpiana, lakini kwa wafuatiliaji wa mambo walilijua hili hata JB Mwenyewe alilijua pia na kumpa nafasi zaidi Genta Macine ambaye ndiye atalaku namba moja, nasema hivi kwa sababu habari za Tutu Kaludji kutaka kuondoka zilianza tangu 2010 na Kaludji anasemwa alijikita zaidi kwenye kuimba na ndipo wapambe wakamstua JB Mpiana kuwa jamaa anataka kuondoka na alikuwa na mpango wa awali wa kutoa nyimbo zake jambo ambalo JB hakulifurahia.

Wakati anatunga kibao cha Tchico Londonien inasemwa alitaka kiwemo ndani ya albamu yake na ndipo hapo walipoanza misuguano ya chini kwa chini na Boss wake JB Mpiana, inasemwa mgogoro wao haukuwahi kuripotiwa popote lakini watu wa karibu walijua na walikuwa wakichekeana na kukaa pamoja lakini kila mmoja rohoni alikuwa na yake. JB Mpiana sio mtu wa kisasi na hapendi kusemwa pembeni ili kusimamia hilo JB huwa anavijana wake ambao amewapandikiza kwenye bendi ili kumpa taarifa na mmoja wapo ni Seguine Mignon ambaye anatoka kabila moja na JB Mpiana.

Seguine Mignon (Segee) ndiye mpambe wa JB Mpiana anayeogopwa sana na wana bendi kwani anaushawishi mkubwa sana na amewatupa wapambe wengine mbali, Seguin anaaminiwa sana na JB Mpiana kiasi kwamba hata wakiwa kwenye show chupa ya maji ya kunywa ya Mukulu JB Mpiana anaishikilia na kukaa naye Seguin.

Ukaribu huo ndio uliomgharimu Chai Ngenge ambaye aliwahi kuwa rafiki na swaiba mkubwa sana wa JB Mpiana. Chai Ngenge alikuwa karibu sana kipindi JB Mpiana anapata matatizo na mkewe Amida Shatur na alimfariji mnoo na kumuuunganisha kwa Mchungaji ambaye alisaidia kumpa moyo na mafundisho JB Mpiana jinsi ya kukabiliana na hali hiyo kwanni alimpenda sana mkewe.

Chai alikuwa na mapenzi makubwa sana na Wenge kiasi alijitoa mno lakini ukaribu wa Seguin na JB Mpiana ulimfanya akarudisha moyo nyuma jambo lililomgharimu mwishoni.

Walipokuja nchini nilipata nafasi ya kukutana na Chai Ngenge kwenye Mgahawa wa Food World alipokwenda kununua simu akiwa na wapambe nikajitambulisha na kupiga naye stori sana kiasi alinipa hadi namba yake ya simu tukawa tunawasiliana, shukrani kwa Papaa Julie Weston Ilunga Presidaa na Bana Kongolee na Darisalama ambaye alinikutanisha na wadau hawa mara zote wakija nchini.

Chai ametunga nyimbo kadhaa kwenye kila albamu ya BCBG jambo lililomfanya awe ni mtu muhimu kwenye bendi, sidhani kama JB Mpiana halitambui hili ila hakuna jinsi tayari keshaondoka acha maisha mengine yasonge, nitamuomboleza Chai Ngenge daima.


%d bloggers like this: