Hasheem kaenda hewa si kitoto.

August 31, 2012

Photo: Njemba imepanda juu kuliko.

Mtangazaji wa BBC Swahili Eric David Nampesya akifanya mahojiano na Hasheem Thabeet ambaye alikuwa nchini hivi karibuni na kuendesha Clinic ya mpira wa kikapu akishirikiana na mwenzake wa Chicago Bulls katika viwanja vya Don Bosco. Tanzania ingependa kuwaona akina Hasheem wengine waking’ara kwenye ulimwengu huku wakipeperusha bendera ya nchi yetu.


Maisha Plus Mama Shujaa wa Chakula yaendelea kuchanja mbuga.

August 31, 2012

MaishaPlus/MamaShujaaWaChakula2012:
Hifadhi ya Ngorongoro, njiani kuelekea kijiji cha Engaresero kufanya usaili na kumuona Mwakilishi wa Mama Shujaa wa chakula mkoa wa Arusha.
Powered by NMB and Oxfam.


Uchokozi mwingine bana: Aliyemliza RAGE huyu hapa.

August 31, 2012

Dah huyu ndio mchezaji ambaye Simba wanamuota na alifanya Rage akatoa mchozi mpaka kutangaza kujiuzulu ujumbe kwenye kamati ya TFF, ni Mnyarwanda Mbuyi Twite ambaye alisemekana kusaini na Simba kabla Yanga mahasimu wao wakuu hawajawazidi ujanja na kumchukua, Hapa alikuwa akizongwa na mashabiki na wanahabari baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa hapo jana.

Mashabiki wa Yanga walimpatia jezi hiyo aliyovaa ya Yanga ambayo nyuma ina jina la Rage.


Allain Mpella Kurejea kwenye Muziki baada ya kushindwa ubunge.

August 31, 2012

Baada ya kuanguka kwenye uchaguzi wa mwaka jana wa 2011 wa Wabunge, Mwanamuziki wa Zamani wa Wenge Musica BCBG Allain Mpela Afande amesema kuwa atarejea kwenye muziki kwa kasi. Mpela ambaye kwa sasa hana Albamu wala single yeyote inayo heat sokoni amesema kuwa anajikusanya ili atoe kitu kitakachotikisa anga la muziki.

Mpela amesema kuwa kwa sasa anaandaa Albamu yake ambayo itaitwa Flèche empoisonnée (Mshale wa Sumu) jina lainalofanya mashabiki kuwa na hamu ya kuisikia hiyo Albamu, Mpela ambaye ni kaka wa damu wa Mwanamuziki Geco Bouro Mpela ambaye aliwahi kuwa na Koffi Olomide aliyasema hayo kwenye Anniversary ya miaka mitano ya kifo cha Madilu System.  Wote wawili waliondoka kwenye bendi zao na kujiunga kwa pamoja na kutoa albamu ya Mortal Combat ambayo haikufanya vizuri, wakiitolea maoni mtangazaji wa siku nyingi wa burudani Zakarie Bababaswe alisema kuwa kwa maoni yake Allain Mpella na Geco Mpella wote kwa pamoja waliwahi kuondoka kwenye bendi zao, bado walitakiwa kupata uzoefu zaidi jambo ambalo hata Spoti na Starehe inakubaliana nalo.

Ngoja tusubiri tuone huo mshale wa moto utakuwaje.


Wenge Musica Maison Mere – Prince Au Congo

August 31, 2012

Kiukweli kila ninapoulizwa mapenzi yangu kwa Werasson Ngiama Makanda huwa moja kwa moja narudi kwenye albamu hii ambayo kwangu mimi huwa ni Albamu ambayo naikubali sana.

Niilikubali sana hii albamu kabla sijaujua mgogoro wa Wenge vizuri, lakini baada ya kuusoma kwa ndani utagundua hapa Werrason alikuwa na kikosi kilichokuwa kimetimia sana.

Watu wengi walitaka kuonyesha vipaji vyao, Ferre, Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya ni baadhi ya majina ambayo yaliibeba sana ngao ya WMMM, Posti hii ni kwa heshima yako Pius Mikongoti Jr aka Mlala ambaye najua unampenda sana huyu bwana, anyway nilimpenda JB ili kujitofautisha na bwana huyu kwa vile tumefafa hadi majina hahahahaaa . Ukitaka kujikumbusha wote walivyokuwa recruited bofya hapo chini.

Read the rest of this entry »


Seguin Mignon Wa Wenge BCBG

August 31, 2012

Alain Prince Makaba 188 Memoir et Mignon Garcon Seguin

Seguin Mignon(kulia) mpiga drums wa bcbg wa sasa enzi hizo akiwa na Alain Prince Makaba”internet”, Ukisikiliza Omba Remix ile Live kuna mahala JB Mpiana alilalamika sana na kuanza kuwaita wanamuziki wake akiwataja sana Afande, Caludji na kisha kuwataja wengine alianza na Seguen kwa wanaosikiliza vizuri Seguen aliliza sana Drumz JB alipomuita huyu ndiye aliyechukua mikoba ya Titina Alcapolne na kwa kweli kazi yake inasikika.

Msikilize JB hapo chini


Kalala kuanza kazi rasmi Ijumaa hii.

August 31, 2012

Akiwa na warembo wa Twanga Pepeta wanaounda safu ya mbele ya wanenguaji.

Kalala ataanzia rasmi kufanya kazi katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo katika Jengo la Millenium Tower lililopo maeneo ya Makumbusho Jijini Dar es salaam. Jumamosi itakuwa zamu ya ukumbi wa nyumbani wa Mango Garden na Jumapili atamalizia Leaders Club Kinondoni mchana kuanzia saa nane. Habari ambazo Twanga wametoa zinasema kuwa Kalala amejiandaa kuwapa uhondo mashabiki na wamewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishuhudia bendi yao ambao kwa kiasi kikubwa inaongoza kwenye burudani ya muziki wa dansi jijini.


%d bloggers like this: