Mwana FA kutoka na “Naona Nazeeka”

June 2, 2009

2646_148119030149_783400149_6321465_7392924_n Mwanamuziki Hamis Mwinyijuma au Mwana FA ambaye yuko masomoni “kwa bibi” ameachia single mpya inayokwenda kwa jina la Naona Nazeeka ambayo amemshirikisha Mr II aka sugu na Heavy Weight Mc Profesa Jeezah. hayo aliyasema kwenye ukurasa wake wa facebook na kuwataka mashabiki wake kutega sikio ndani ya masaa 24 kitu kitakuwa kimepakuliwa. Habari ndio hiyoooo!


Mnyalu kuendeleza mpambano wa Inspector na Mwana FA

March 30, 2009

 

Mnyalu kuendeleza mpambano wa Inspector na Mwana FA
Msanii Mike Mwakatundu a.k.a Mike T au Mnyalu ambaye hivi karibuni aliachana na ukapera kwa kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ameibuka na kuendeleza malumbano yaliyoanzishwa na Inspector Haroun aliyejibu wimbo wa Mwana FA, ‘Bado nipo nipo’.
Mike T alisema kwamba, wimbo wake mpya wenye jina la ‘Wala wasielewe’ aliomshirikisha Mwana FA aliyeimba wimbo wa ‘Bado nipo nipo’ unawazungumzia wana ndoa ambao huzisaliti ndoa zao na kutafuta wapenzi wengine wa pembeni.
“Kwa kifupi nataka kuleta changamoto kwa wasanii wengine waliowahi kufanya nyimbo za aina hiyo wakiwemo Mwana FA na Inspector Haroun, sipendi watu wanifikirie vibaya kwa kuwa yote ni sanaa tu na si vinginevyo,” alisema Mnyalu.

Habari hii na Abdallah Mrisho (Gonga hapo umtembelee kujua mengi zaidi)


We ndio mchizi wangu-Remix yake Fid Q

February 7, 2009

“Bwana we mi hupenda hizi nyimbo maneno yake kusikiliza sijui hawa watu huwa wanawaza nini…” Maneno ya Balozi wangu Cisco Mtoro tulipokuwa tumekaa tunajadili mstakabali wa Muziki wa nyumbani na kundi la wanamuziki wa Kilimanjaro Connection kwenye kiambaza cha nyumbani kwa Balozi Mh. Cisco alipowaalika wanamuziki hawa nyumbani kwake kwa chakula cha mchana huko Kuala Lumpur Malaysia.

Kimsingi nataka kuongelea mashairi ya Bongo Flava, mbali na kuburudisha hizi nyimbo kwa kiasi ikubwa huwa na ujumbe na huweza kufikisha ujumbe kwa jamii moja kwa moja kwani mengi ya yanayoimbwa ni matukio ya kila siku yanayoigusa jamii na nyingi ni visa halisi vya maisha ya kila siku ya Mtanzania.

Sikiliza vichwa makini vilivyokutana na kutengeneza huu wimbo wa We ndio mchizi wangu ndani yake wamo Fid Q, Chid Benz, Mansu Li, Mh Temba, MWana FA, Geez Mabovu, Babuu, Ibra De Hustler, Jay Moe Mchopanga, K wamapacha.

Gonga player upate mambo


%d bloggers like this: