Ni Single mpya ya mwanamuziki Werasson Ngiama Makanda ambayo anongelea Uhuru wa Congo huku akiwalilia akina mama na akina dada wa Mashariki mwa Congo ambao wamekuwa ndio waathirika wakubwa wa Vita hii. Ikumbukwe kuwa Congo imekuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kitambo sasa na Werasson ni balozi wa amani wa Unicef. Muziki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo una nguvu sana. akiongea na mtandao wa digit congo Werasson amesema ni wakati sasa wanamuziki kufikisha ujumbe kwenye dunia kupitia vipaji vyao vya muziki kugeukia matatizo yanayoikabili jamii na kuacha kuimba kuhusu burudani na mapenzi pekee.
Humu ndani utasikia maneno ya Kiswahili yakisema muache kuwatesa wanastahili maisha, akisisitiza kuwa akina mama tunastahili kuwaenzi badala ya kuwatesa na kuwabaka na hata kuwaua, kwani wao ndio waathirika wakubwa, Pia sikiliza kuanzia 3:58 kuna mtu anaitwa Capuccino anaimba verse ya kiswahili kizuri sana analalamika jinsi Congo watu wanavyouana, ni wimbo wa taratibu (Rhumba) Mzuri sana. Kwa sasa wimbo huu unapigwa sana kwenye stesheni za redio na Televisheni huku ukikumbusha umuhimu wa Amani.
Wimbo wake JB Mpiana- Sultan De Bruneil Kaskinto ilikuwa kwenye albamu ya Tojou Humble au TH, ikiwa ni majibu kwa mwanamuziki Werason alipotoa Albamu ya Solola Bien akimwambia JB Mpiana sema tena na JB akamjibu mi ni mnyenyekevu daima.
Katika Wimbo huu ambapo JB alitaka kujifananisha na Mfalme wa Brunei na kuwapa shavu baadhi ya washabiki wake huko Nchini Brunei hali haikuwa hivyo kwani ni mwaka jana tuu wananchi waliandamana na kutumia picha za wimbo huo kwa kile walichotafsiri wao ni muonekano wa familia ya kifalme kwani familia ya Kifalme inalaumiwa kwa kuponda starehe na kutumia mamilion ya dola za walipa kodi kwa ajili ya maisha yao binafsi, hasa mtoto wa kiume wa mfalme huyo ambaye anajulikana kwa kuponda maraha na mkali wa wanawake jambo ambalo ni kinyume kwa wananchi wa nchi hiyo ambao wengi wao ni wadini.
Awali akiongea nami kwa njia ya email mmoliki wa blog ya Papar Demokrasi (asubuhi ya Demokrasia) Saifudin Alhadawi alitaka nimwambie maana ya wimbo huu. “Ni mfalme wetu, hatujui mnasema nini juu yake, mbona kuna wanawake wanacheza nusu uchi? ilihoji sehemu ya email hiyo ndefu iliyoandikwa kwa Kiingereza na Bahasa Malayu ambayo ni lugha inatumika huko.
Baada ya kupitia Blog ile nikaona picha za maandamano ambazo nilizichapisha kwenye Blog yangu ya kwanza ambayo ilifungwa na Google pamoja na akaunti yangu ya Youtube.
Baada ya kutafuta maana ya wimbo ule na kuwasiliana na Saifudin akaniambia Blog yake haiko hewani ila tafsiri ile waliitumia kwenye gazeti la Borneo Bulletin.
Akijibu kupitia kwa webmaster wake Guy Guy Mpeye, JB alinijibu kuwa hakuwa na leo hilo kabisa kwani yeye alifananisha maisha ambayo mfalme wa Brunei anaishi na huku ikifahamika kuwa Brunei wananchi wake wanaishi kwa raha kwa sababu ya hazina ya mafuta iliyo nayo.
Leo nakuletea tafsiri ya Wimbo huo kama ilivyokokotolewa na Wenge BCBG die hard member Mwambungu nakati ya Tunduma.
Majuzi nilipokea Copy ya DVD ya Live ya Werasson huko Bukavu DRC show ambayo ilipigwa tarehe 15/10/2010. Ilikuwa shoiw ya kufa mtu ikizingatiwa Werasson alikuwa hajafanya show maeneo haya kwa muda mrefu.
Eneo la Bukavu linawazungumzaji wengi wa kiswahili na ili kuwabamba basi Werason alitumbukizia ghani ndani yake ana sema “Ngiama analeta mambo…” huku mashabiki kwa mamia wakiitiakia.
Bofya upate mambo, Asante sana Julie Ellystone we ni kiboko na tutapanda Punda tu hata kama mtaleta mambo. Hakuna malewa wala nini hata mkilewa tutawapandisha Punda mtakwenda tuu. Salaamu kwa Werasonique wote.