Werason azidi kukimbiwa na wanamuziki wake.

January 25, 2009


Hii ni siku WMMM walipokuwa jijini Dar na mwanadada Bibiciya Mfwengi alipoawaacha midogo mwaa mashabiki kwa mauno yake

Yule mwanadada aliyewapagawisha wengi kwa uchezaji wake Bibiciya Mfwengi wa Wenge Musica Maison Merre amesemekana kuikacha bendi ya werason na kukimbilia kwa Koffi Olomide alikokuwa mwanzoni.

Akizungumza na 2Mukwata DMTV Bibiciya amesema kuwa bado hajaamua kuliongelea kiuwazi sana hasa sababu za yeye kuhama lakini kwenye Clip hiyo Bibiciya anaonekana akifanya mazoezi na wanamuziki wa Koffi.

Habari zinasema Werason amekuwa akikimbiwa na wanamuziki wake kwani hata bingwa wa Atalaku/kughani wa bendi hiyo Prince amesemakana kuondoka, si yeye tu bali hata mwanamuziki mwingine mahiri na mtunzi Eboa pia wamesemwa kuondoka kwenye bendi hiyo na Eboa Lotin amesemekana akionekana mara kwa mara na Watu wa Koffi Olomide.

Hivi karibuni kundi la WMMM (Wenge Musica Maison Mere) lilifanya ziara huko Ulaya na mwanamuziki wake mmoja Olivier alisemekana kubakia nchini Ufaransa ambako alisema kuwa anataka kurudi shule kidogo. Angalia video hii na mahojiano kwa wale wanaofahamu Kifaransa.Werasson awakana wanamuziki wa Congo nchini

June 30, 2008
[image]

MWANAMUZIKI mkongwe wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo, Werasson amesema hamjui mwanamuziki hata mmoja kutoka Kongo anafanya muziki hapa Tanzania.

Hivi karibuni wanamuziki wengi kutoka Kongo waliokuja hapa nchini walijitangaza kuwa wengine ni ndugu wa Werrason huku wengine wakisema kuwa wenyewe ni watoto wa mkongwe wa Muziki nchini humo Pepe Kalle, na katika tukio la karibuni ni pale mwanamuziki ally Choki alipoonekana amepiga picha na Werason alipokwenda kutafuta wanamuziki huko na kusema kuwa Werasson alimsaidia kutafuta vijana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juzi Werasson alisema ’simfahamu mwanamuziki hata mmoja wa Tanzania wala mkongo ambaye anaimba muziki hapa huyo anayejiita mtoto wa Pepe Kalle pia hamfahamu.

“Mimi nipo na mtoto mmoja wa Pepe Kalle ambaye namfundisha muziki pale Kongo, lakini huyu wa Tanzania mimi simfahamu kwakuwa watoto wake wote nawajua na hivyo labda awe mwingine zaidi,” alisema Werassons.

Werrason alisema kwa kuwa hawajui wanamuziki wa Kongo walipo hapa nchini lakini yuko tayari kukutanao na kufanya mazungumzo ya kuendelea muziki Tanzania.
(Picha na Mpoki Bukuku)


Werason awasha moto Dar

June 29, 2008Mwanamuziki Werasson Ngiama Makanda usiku wa leo amefanya balaa katika ukumbi wa Ubungo Plaza na kuwapagawisha vilivyo mamia kwa maelfu ya mashabiki walifika katika onyesho hilo.
Werasson ambaye ameingia nchini majuzi aliingia jukwaani kama kawaida lilitangulia sebene na kisha yeye kuingia huku akiimba wimbo maarufu wa Kala Yi Boing Remix huku mashabiki lukuki nao wakimfatiisha kwa kuimba naye, kisha alifululizwa kwa vibao kama Sourire ambacho kinapatikana kwenye Albamu ya Zamani ya Volume I, Solo la bien,Kibuisa Mpipa, Kuna nyimbo inaitwa Simeone inapatikana kwenye single Album Soul Soul.
Mashabiki walipagawishwa na mauno ya mwandada mrembo aliyeumbika si kitoto Bibiciya Mfwengi kila mara alikuwa akijivuta mbele na kijana wa atalaku kama kawa anampa mapande mashaki wote wana lipuka kwa mayowe.Kwa ujumla shoo ilikuwa nzuri na kila mtu aliyeingia aliridhika na burudani ya haja aliyoipa.
Awali akizungumza na waandishi wa habari Werasson alisema kuwa amekaidi wito wa Rais wa Kongo Brazaville Denis Sasou Nguesso aliyemtaka kwenda kufanya shoo kadhaa kwa wiki nzima lakini alisema kuwa hawezi kuwaangusha mashabiki wake wa Dar Es Salaam ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wakimngojea hasa baada ya onyesho la awali kutofanyika huku watu wakiwa wameshakata tiketi.
Werasson na kundi lake la wanamuziki 24 watapiga Arusha kesho.
Kama nakuona Big Producer Maghambo Philipo – Baba Martha, Collins na Fikire wazee wa USA, Mukubwa Ling’ande, Mwanangu Dulla nakati ya IFM, Abuu na Boss Chizenga!! Tuko pamoja.
Picha na Big Producer Magambo/Mpoki Bukuku

Werasson kuanzia Ubungo Plaza Leo

June 27, 2008
Mkurugenzi wa Clouds fm/Prime Time Promotions Joseph Kusaga akiteta jambo na Werrason mara baada ya kuwasili Dar. Werrason anatafanya onesho lake la kwanza leo Ijumaa usiku Ubungo Plaza ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni sh 20,000/= pamoja na msosi wa nguvu, Pia leo atafanya mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Radio cha Clouds FM kupitia kipindi cha African Bambataa kinachoongozwa na Bibi Sophia KEssy, Big Producer Maghambo, Boss Chizenga, Mukubwa Collins, Dulla Boy na kati ya IFM, Mama Irene Maggi, Fikiri Le Boss, Abuu na wapenzi wote wa Werasson kila la heri najua hamtakosa. Picha na Issa Michuzi.

Werasson: Niko tayari kupiga na JB Mpiana Tanzania

June 26, 2008
Pichani ni Rais wa Kongo RDC Joseph Kabila akiwa na timu ya Wanamuziki akiwemo Marehemu Madilu System alipokutana nao na kuwapatanisha baadhi yao akiwemo JB Mpiana na Werasson mwaka juzi.
MWANAMUZIKI hodari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ngiama Makanda ‘Werrason’ amewasili Dar es Salaam na kusema yupo tayari kupiga pamoja na Jean Bedel Mpiana ‘JB Mpiana’ endapo atapatikana promota wa kuwaleta Tanzania kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania.Msanii huyo aliwasili juzi jioni akitokea Jamhuri ya Kongo ambapo na kundi la wanamuziki 24, anatarajiwa kutoa burudani kesho kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza kabla ya kupiga Arusha Jumapili kwenye Hoteli ya Naura Springs.

Endapo ‘Werrason’ atapiga pamoja na ‘JB’ Mpiana itakuwa ni historia baada ya nyota hao kuingia katika mzozo mkubwa ulioibua vita kati yao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makanda alisema atafurahi kupiga pamoja na Mpiana ambaye inadaiwa ni wapinzani na chanzo cha kuvunjika kwa kundi maarufu la Wenge BCBG lililowahi kutamba Afrika.

“Sina matatizo na Mpiana ni rafiki yangu napenda siku moja nije naye hapa tufanye onesho la pamoja nipo tayari hata sasa cha msingi apatikane promota mwenye uwezo nitamwambia lakini naomba nipate uhakika kama mnatuhitaji kabla ya mwaka huu kumalizika,” alisema Makanda.

Makanda alisema anapenda kuona muziki wa Tanzania unapiga hatua kama ilivyo Jamhuri ya Kongo na kuongeza kuwa endapo atapata fursa ya kuzungumza nao atawashawishi watengeneze albamu ya pamoja.

Msanii huyo alisema alishindwa kutoa burudani mwaka jana kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake na alitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi Watanzania kutokana na tukio hilo.

Alisema amejiandaa kuacha historia kwa kupiga nyimbo zake mfululizo ili kukata kiu ya mashabiki wa burudani ambao walikuwa na shauku kubwa ya kumuona nyota huyo akiwa jukwaani katika ardhi ya Tanzania.

Ziara ya mwanamuziki huyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya Embassy kwa kushirikiana na Club E.


%d bloggers like this: