Sasa waweza jipatia kipato kwa njia rahisi Mtandaoni.

January 31, 2009

hisapepe.com

Sasa wapenzi wasomaji hata wewe waweza kujitegenezea pesa kwenye mtandao kwa kusoma mail au kusoma matangazo. KAmpuni ya kizalendo ya hisapepe ndio inayokuletea mambo hayo,

Gonga hapa kwa ajili ya kufahamu zaidi na kujiunga upate Pesa kwa kusoma email pekee na mengineyo.


Saturday Night Live & Sweet Eazy are bringing

January 31, 2009
Dear All,

Saturday Night Live & Sweet Eazy are bringing you another top Tanzanian artist live on stage:

T.I.D. & Top Band.

Saturday, 31 January, from 9:00. Gate: 5’000/=

Advance bookings: 0755 75 40 74.

Please see the below flyer for more information/upcoming events.


Wamkumbaka “Baunsa” huyu?

January 29, 2009

Dullah baada ya kupasha mwili.

Dullah baada ya kupasha mwili.

Kwa wapenzi waburudani wanamkumbuka Dulla au Abdallah Herry kama anavojulikana. Kwa sasa Abdallah anafanya kazi zake huko Abu Dhabi akiwa ameajiri wa kama Gym and Aerobic Instructor katika kampuni kubwa ya mazoezi ya Wadosiaila lakini Abdallah anasema kuwa amepata kazi nyingine ya Etihadairways akiwa na jukumu la kuwatrain wafanyakazi wa ndege ili wawe fit.

Kabla ya kuondoka Dullah aliwahi kufanya kazi na kampuni ya Clouds Entertainment enzi za disko la Tazara na kwenye matamasha tofauti katika jiji la Kandoro. By the way Dullah ni classmate wangu High School, Spoti na Starehe inakupa shavu mkuu.

n1123060874_30176111_6303Dulla akiwa na wanafunzi wake kabla ya kuanza mazoezi ya Aerobics

Maisha baada ya kazi

Maisha baada ya kazi


Cheka kispoti unenepe…!!!

January 29, 2009

Aboutrika aliposhinda tuzo ya BBC

January 29, 2009
Wanasoka wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa BBC Afrika

Habari na BBC
Mohamed Aboutrika, mchezaji wa kiungo wa Al Ahly ya Misri, ametangazwa Ijumaa, tarehe 16 Januari 2009, kama mshindi wa tuzo ya BBC ya mchezaji bora zaidi mwaka 2008.

Aboutrika alipata zaidi ya asilimia nusu ya kura zote za mashabiki walioshiriki katika kumchagua mshindi, ikiwa ni juma ya kura 155,000.

Idadi ya walioshiriki katika kura hiyo imeongezeka maradufu, ikilinganishwa na tuzo lililotangulia.

Hili ndilo tuzo la pekee ulimwenguni la kuamua mchezaji bora wa soka ambalo hutoa fursa kwa mashabiki kuamua mshindi.

Aboutrika ameweza kuwabwaga wachezaji mahiri kama vile Emmanuel Adebayor, mshindi wa tuzo hilo mwaka 2007.

Aliwashinda pia wachezaji kama Didier Drogba, Samuel Eto’o na Amr Zaki.

Tuzo hilo limemletea fahari kubwa, kwani linamtambua kama mchezaji aliyefanikiwa kuiwezesha nchi yake kuchukua ubingwa kwa mara ya sita, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kuishinda Cameroun katika fainali za Ghana, mwaka 2008.

Akizungumza na waandishi wa kipindi cha michezo wa BBC, kipindi kinachotangazwa kwa lugha ya Kiingereza cha Fast Track, Aboutrika alisema “mwaka 2008 ulikuwa mzuri sana”.

Alielezea kwamba ni mwaka uliompa nafasi yeye na wenzake kuonyesha uwezo mkubwa wa timu ya Misri.

Aboutrika aliweza kufunga bao la pekee katika fainali dhidi ya Cameroun, na kuiwezesha timu yake ya Pharaohs kuiangamiza Indomitable Lions.

“…Kumradhi wadau kwa kuchelewa kuirusha habari hii wakati muafaka, asante wasomaji wangu mlioiulizia, Pius


Robinho akanusha kubaka!!

January 29, 2009

.

.

Mchezaji anayeongoza kwa kusajiliwa kwa gharama kubwa Mbrazir Robinho amekanusha shutuma ambazo zime failiwa police dhidi yake kwamba amemnyanyasa kijinsia binti wa miaka 18 ambaye kisheria inasomeka kama ubakaji.

Ingawa haijasemwa wazi alichokifanya hasa Robinho hanbari zinasema alimshika maungo kwa kumdhalilisha binti huyo bila idhini yake.

Habari kutoka kwa msemaji wa mchezaji huyo Chris Nathaniel zinasema kwamba Robinho alihojiwa na police na si kwenli kwamba alikamatwa bali alikutana na Polisi kwa utaratibu ambao pande zote mbili zilikubaliana. Pia aliongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa shutuma hizo na Robinho mwenyewe amesema yuko tayari kushirikiana na Polisi.


Kobe Bryant alipwa mabilioni kwa ajili ya Ku Blog…!!

January 29, 2009

.

Mchezaji Kobe Bryant akipiga makofi akiwa ndani ya vazi rasmi la Kichina mara baada ya kuzindua Blog yake.

Mchezaji kikapu maarufu wa MArekani Kobe Bryant ameingia mkataba wa mamilioni na kampuni ya mtandao ya sina.com kwa ajili ya kublog kwa kichina kwenye mtandao huo, Blog hii imeandikwa kwa kichina http://kobe.sina.com.cn/

Hii ni katika hali ya makampuni ya kimataifa kukabiliana na mkengeuko wa kiuchumi ambapo makampuni yanaangalia zaidi maslahi, kwa miaka ya karibuni Uchina imekuwa ni soko zuri la mchezo wa Basket Ball tangu mchina Yao Ming aingie kucheza kwenye ligi ya kikapu ya NBA kwani inasemekana siku ya kwanza Yao Ming kucheza NBA wachina Millioni 200 duniani waliangalia TV hivyo kufanya Uchina kuwa soko zuri kutokana na Population yake.

Katika Blog Hiyo Kobe atakuwa akiongelea mambo kadha wa kadha ya kimichezo na kimaisha na hasa Burudani ya kikapu, kwa ujumla ni Spoti na Starehe, sehemu ya ujumbe kwenye blog hiyo inasema

“Hey everyone in China, this is Kobe! I am really excited to have my own Chinese blog with SINA. I feel this blog really gives me the chance to connect directly with all of you - my Chinese fans. It’s kinda like staying close to you while I can not be in China right now in person because of the NBA Season. Through my blog, I look forward to getting to know all of you better, and for you to learn more about me.”


%d bloggers like this: