Ronaldo mwanasoka Bora wa Dunia 2008

January 13, 2009

.

.

Mchezaji Wa Manchester United toka Ureno Cristiano Ronaldo akiwa amekula pozi baada ya kunyakuwa zawadi yake ya mwanasoka bora wa FIFA kwa mwaka 2008. (FIFA world Footballer of the Year 2008 award) hapo jana January 12, 2009 huko  Zurich. Ronaldo, ambaye pia anashikilia taji la the prestigious Ballon d’Or for the European Footballer of the Year, aliwagalagaza washindani wake akiwemo bingwa wa mwaka juzi 2007 Kaka (Brazil), Lionel Messi (Argentina), Fernando Torres (Spain) na Xavi (Spain).

Pichani chini akiwa na zawadi zake tofauti tofauti

.

.


Marta anyakua tena zawadi ya Mwanasoka bora wa kike wa Dunia.

January 13, 2009

.

.

Mchezaji bora wa mpira wa miguu wa kike toka Brazili wanawake Marta akiwa ameshikilia zawadi yake toka kwa  mwanasoka nguli wa Ujerumani Franz Beckembauer. Marta ameweza kutetea taji lake kwa miaka mitatu mfululizo.


Floating Stadium, Uwanja ulioko kwenye maji huko Marina Bay Singapore

January 13, 2009

Ukiwa umejengwa kwenye eneo jipya la jiji la maraha la MArina Bay, ambapo awali palikuwa ni sehemu ya Bahari na kilichofanyika ni kujaza kifusi (re claim land) na hatimaye kuweka mijengo/vikwangua anga vya maana na kuufanya kuwa mji wa pekee uliobuniwa na kunakshiwa barabara, moja kati ya vivutio katika eneo hili ni uwanja wa mpira wa Floating Stadium Huu ndio uwanja wa mpira wa miguu unaoelea juu ya bahari,uwanja huu upo nchini singapore unaitwa Marina Bay Floating Stadium kuna hatari ya kufungwa kama timu inakuwa haijaandaliwa kisaikolojia kwenda kucheza kwenye uwanja huu, kwani ichezapo timu ngeni boat ziendazo kwa kafi hupita na mashabiki kufurahia kwa kupiga kelele na kuamka vitini jambo linalofanya hata wachezaji kushangaa hehehe.

Side elevation photo( picha ya upande ) ya uwanja huo ikionyesha uwanja na jukwaa ambalo linauwezo wakuchua watizamaji  30 000 kwa wakati mmoja.
.

.

Uwanja huu si tu kwa matumizi ya mpira la hasha bali unaweza kutumika kutokana na mahitaji ya wakati huo kwani unaweza kuchezewa Tenesi, Badminton, Rugby na michezo mingine kadha wa kadha, Pichani Sherehe za mwakampya zilifanyika katika uwanja wa floatingm Stadium na kufanya anga ibadilike kwa miale ya fataki, mamia kwa maelfu ya raia wa Singapore walihudhuria sherehe hizi


Kanoute apigwa fine kwa Tshirt ya Palestina

January 11, 2009
.

.

Shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu la Spanish la Spanish Football Federation (RFEF) limemhukumu mchezaji Frederic Kanoute kulipa fine kwa kitendo chake cha kuvua jezi na kuonyesha fulana yenye maneno ya kulaani mauaji PAlestine katika mchezo wao na Deportivo La Coruna baada ya kushinda goli la pili.

Ingawa taarifa ya Shirikisho hilo haikusema kiwango cha Fine lakini habari zinasema kuwa Faini hiyo ni dola 4,000 za kimarekani. Wakiongelea adhabu hiyo mashabiki wamesema kuwa fulana ile haikuandikwa kingine bali ni neno Palestina kwa lugha mbalimbali na hilo halistahili adhabu hiyo, Ikumbukwe Kanoute ni Muislam aliyezaliwa Ufaransa mwenye uraia wa Mali.


Waziri mkuu awazawadia Stars

January 10, 2009

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametimiza ahadi yake kwa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ya kuwapa Sh milioni tatu kama zawadi kutokana na kufika hatua ya fainali ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).

Pinda alitoa ahadi hiyo, Desemba 15 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kukipokea kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kikirejea kutoka Sudan. Stars imekata tiketi ya fainali hizo za kwanza baada ya kuiondoa Sudan kwa jumla ya mabao 5-2 ikiwa ni baada ya kushinda kwa mabao 3-1 katika mechi ya Dar es Salaam na ule wa marudiano wa mabao 2-1 uliofanyika Khartoum.

Akikabidhi hundi hiyo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alisema kuwa fedha hizo ni ahadi ya Waziri Mkuu na kuwa uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), utajua jinsi ya kugawa fedha hizo kwa wachezaji. Pia Bendera alimpongeza Waziri Mkuu kwa kutimiza ahadi aliyoitoa na kuthamini kazi iliyofanywa na wachezaji hao.

“Nampongeza Waziri Mkuu kwa kutimiza ahadi yake, pia ninawaomba wadau na kampuni kumuunga mkono Waziri Mkuu katika kuwasaidia vijana wetu. “Ushindi walioupata ni hatua ya awali na sasa wako katika hatua ya fainali ambayo mahitaji yake ni makubwa, kwani vijana watahitaji, vifaa, motisha ili wachezaji watambue kuwa Watanzania wanawajali,” alisema.


%d bloggers like this: