Wera Magic at Zenith

April 1, 2012

Mbwembwe za show za Live ni swali huwa ataingiaje? atavaa nini ? na ataanza na wimbo gani… Kiukweli huwa namkubali sana Werason kwenye LIVE perfomance anaiweza sana ni mzuri kwa Sebene. na mpangilio wa jukwaa zima kwani huwa jamaa anajipanga sana kiukweli na kuchangamsha jukwaa.


Papito Live ya Olympia

April 1, 2012

Mdau wangu Mamaa Flower Titanic ananiuliza yule mtoto kwenye hii concert ya Olyimpia alikuwa anacheza ni mtoto wa nani? Dada yangu yule ni mtoto wa D.Dimonukeni (I hope sijakosea jina kuandika) mtoto alicheza sana na hii ilikuwa ni moja ya show zenye mafanikio sana za Wenge BCBG. angalia kisha unaweza na wewe sema.

Kiukweli nikiangaliaga show hii kwenye liblary yangu huwa najikuta namchukia Mpela kwa kutoka Wenge na namlaani sana mshauri wake kwa kweli, atabaki kuwa ni mmoja wa vijana niliowapenda sana ndani ya BCBG.


Wenge el Paris live!

April 1, 2012

Na Hadji Le JBneeque

Unamkumbuka Marie Paul “Le Roi Soleil”???? Huyu hapa anaendeleza libeneke na Wenge El Paris yake….kwa wanaoijua vizuri historia ya wenge musica jina Marie Paul halitakuwa geni kwao,huyu ni mmoja kati ya waanzilishi wa wenge musica original kabla hata Jb Mpiana hajajiunga na wenge,walikuwa yeye werrason,didier masela….na wengine,Jb alikuja baadae japo ujio wake ndio ulioitoa wenge mafichoni na kuipatia utambulisho rasmi congo nzima na africa kwa ujumla kufuatia nyimbo zake mbili Mulolo na Kin e bouge ambao uliipatia wenge tuzo ya kwanza ya muziki ndani ya congo na kuwapatia changamoto kubwa zaiko langalanga ambao kabla yaujio huu wa wenge na nyimbo hizo walionekana kama hawana mpinzani ndani ya Kinshasa,wenge ikaja kivingine na kufuta utawala huo wa zaiko wa muda mrefu kwenye muziki wa congo.

Marie Paul na wenzake kina Aime Buanga ndio walikua watu wa mwanzo kujiondoa wenge na kuasisi hii wenge el paris ambapo baadae kina Aime Buanga wakajitoa tena ndani ya wenge el paris na kumuachia jahazi Marie Paul ambae anaendeleza libeneke kama nilivyosema hapo juu kama kawa japo amekua hasikiki sana na wenge yake kama wenge mbili maarufu,ya mpiana na werrason ambazo ndio zinafanya vizuri na ziko juu,lakini El Paris hawavumi tu ila wamo!


Watoto wa London

April 1, 2012

Zawadi ya watoto wa London toka kwa Adolphe Dominguez na Wenge Tonya tonya yake!


%d bloggers like this: