Simba 1-3 ES Satif …. Simba yasonga mbeleeeeeeeeee

April 6, 2012

image

Mpira umekwisha na simba inasonga mbele, Bao pelee la Simba limefungwa na Emanuel Okwi Dakika ya 91.


Taarifa ya Afande Sele kwa Jamii baada ya kuwekwa ndani Juzi kati huko Moro

April 6, 2012

image

Afande na 20% huko Moro

Ndugu zangu ambao ni mashabiki wangu!! Juzi wakati nimerejea kutoka Tanga, majira ya jioni ndugu zangu Ballet Wallet(mtupori) , Adam Lumbe na Twenty Percent (20%) walitoka na gari yangu, kwa bahati nzuri au mbaya wakapita maeneo ya NMB hapa Morogoro, wakapaki gari kwa haraka kwa kuwa Adam Lumbe alimuona kijana ambae alimtapeli katika mauziano ya pikipiki, likatokea zogo!! Polisi waliokuwa Lindo pale Bank wakaja kuizuia gari na pia wakawaweka chini ya Ulinzi Ballet Wallet na Adam Lumbe, licha ya maelezo waliyowapa hawakuwaelewa, 20% akataka kuchukua gari wakamkatalia, ikabidi akodi pikipiki aje nyumbani kunifuata nikafuate gari, nimefika pale Bank polisi wakakataa kunipa gari ili niende kituo kikubwa cha polisi kuwawekea dhamana ndugu zangu kwa kuwa muda huo Ballet na Adam walikua washapelekwa kituoni.

Kilichotokea baada ya hapo nilielezwa nisubiri gari ya doria nipewe Eskoti mpaka polisi lakini baada ya kufika gari ya doria wakiwa na wanamgambo wa manispaa walituvamia na kuanza kutupiga marungu na kutujerehi, wananchi ambao ni kama ndugu zangu wanamorogoro wakasogea eneo la tukio, Polisi wakafyatua risasi hewani kuwasambaratisha tukapelekwa Polisi kituoni, pale hatukuchukuliwa maelezo haraka, baadae tukatoa maelezo baada ya wale mabwana wadogo askari kupata amri toka kwa wakubwa wao!!

Jana tukafikishwa mahakamani tukakosa dhamana, tukapelekwa ngome (jail) tukiwa kama mahabusu, leo kwa bahati nzuri tumepata dhamana, na tumeweka wanasheria makini kusimamia HAKI yetu. si kweli hata kidogo kuwa kwenye gari yangu kulikua na silaha za kijadi kwa lengo la kumdhuru mtu, walikuta fimbo yangu ile ya Mfalme wa rhyemes na kisu au kama panga ambao ni kitu cha kawaida kuwa nacho kwenye gari, na si kweli hata kidogo kuwa Ballet alikua kavaa kic..p* tu.

Ndugu zangu wapendwa watanzania wenzangu,na mashabiki wetu kiukweli hali za jela na selo zetu ni mbaya mazingira mabovu ndugu zetu wanateseka. Nilitumia muda mchache niliokua kuwa kule kuwafariji na kuwapa moyo ingawa nilienda kwa Matatizo, na muda huu nipo hapa Nyumbani Misufini na Twenty Percent na Ballet pamoja na ndugu wengine! Tumechinja Mbuzi kama Sadaka au dhabihu kwa Mungu na kuchoma, kuelekeza moshi kwake kama ishara ya kumpenda na kushukuru kwa yote!! mwisho tunaomba radhi kwa mashabiki wetu wote kwa usumbufu mulioupata. ASANTENI KWA FARAJA ZENU KWANGU WAKATI WOTE ,Ni mimi SELEMANI ABDALLAH JUMA MUTABHAZI MSINDI .. KING OF RHYEMEZ. (AFANDE SELE)”” + MWISHO WA KUMNUKUU.


Mortel Combat toka kwa Mpela Brothers

April 6, 2012

Wanaitwa Mpela Brothers wakiwa ni makaka wawili Allain Mpela na Geco Bouro Mpela, Hawa vijana wote ni matunda ya makundi mawili makubwa ambapo Allain Mpela alikuwa na kundi la Wenge Musica BCBG chini ya nguli JB Mpiana huku Geco Bouro Mpela ye akiwa anatokea kundi cha Koffi Charls Olomide.

Alain Mpela aling’aa sana alipokuwa na Wenge Musica BCBG hasa kwenye albamu yao ya Titanic ambapo aliimba sana na beti zake kuvutia wengi nyimbo kama Liberation, Serge Palmi na nyinginezo. wakati Geco Mpela yeye aling’ara zaidi kwenye Ultimatum ya Koffi Olomide.

Allain Mpela aliamua kutoka solo na mpaka sasa ana Album moja sokoni inaitwa INTIFADA huku Geco Mpela naye alitoka kivyake na album yake inaitwa ICE DE PROCEDURE, lakini wawili hao huwa wanafanya show ya pamoja na walitoa album moja wote wawili ikiitwa Mortel Combat ambayo ilitengenezwa na Professionally Solorist Allain Prince Makaba huko Bruxells Belgium.

Kwa kumbukumbu tu Mpela na Mpiana hawakukutana barabarani na kuwa pamoja BCBG,Wametoka mbali toka wenge musica 4*4 the best of the world,mpela aliletwa hapo wenge na JB MPIANA,naweza sema alikua ni kijana mwenye bahati ya kupata nafasi ya kufanya kazi na watu wa kazi yeye akiwa bado mdogo,nakumbuka ni yeye na LE GRAND CHIBUTA ROBERTO OKOKOTA ndio walikua wadogo zaidi,ndio maana Alain Mpela licha ya kuondoka BCBG lakini bado amekuwa royal kwa mwalimu wake tofauti na watu kama FERRE GOLA na DE CAPRIO DE KINSHASA FALLY wanavyowatoa jasho walimu wao wakiweweseka usiku kucha namna ya kuwazima vijana wao kimuziki.

Iliwahi kutamkwa kuwa Allain Mpella alikuwa tayari kurejea kundini juhudi ambazo zilifanywa na ZK Zadio Congolo akishirikiana na tajiri mwingine lakini mpela alisema kuwa kwa sasa hawezi kwa kuwa anamipango yake ambayo bado hajaikamilisha pindi ikikamilika basi ataufikiria huo mpango.

Alain Mpela ni moja ya mapigo makubwa sana kwa JB Mpiana kwani alikuwa ana wapenzi wengi sana lichaya ukweli kuwa ana sauti nzuri na tamu.

Weekend njema waungwana.


%d bloggers like this: