Onesho la Mavazi kwaajili ya kuchangia Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar lafana sana

July 31, 2010

Wanamitindo tofauti tofauti kutoka jijini Dar es Salaam wakipita jukwaani na mavazi ya mbunifu maarufu Tanzania na duniani Mustafa Hassanali wakati wa Onesho maalum la mavazi kuchangia Hospitali ya wagonjwa wa akili Zanzibar iliyofanyika Serena Hotel.
(picha zote na Father Kidevu Blog)


Albam ya Mapacha watatu iko mbioni

July 30, 2010

Na Sophia Kessy

image

Albamu ya swanza ya kundi la muziki linaloundwa na Mapacha wa 3 vijana kutoka bendi mbili kubwa hapa nchini imekamilika Khalid Chokoraa, ambaye ni mmoja wa wanamuziki wanaounda kundi hilo, ndio alietoa kauli hiyo kwamba wameshamaliza kazi yote na sasa wapo katika mipango ya kuizindua.

Album yao na hii ni baada ya ule uzinduzi waliowahi kuufanya wa utambulisho wa bendi ambapo mmoja wao aliingia mitini muda wowote kutoka sasa yadaiwa wataweka wazi ni wapi na lini watazindua hio album yao wakati huo huo katika kundi la mapacha wa tatu mmpja wa pacha hao nae anajiandaa kuipua album yake binafsi ambayo iko njiani na huyo si mwingine bali ni jose mara ambae kwa sasa anatamba na shani.


Ellen DeGeneres kuachana na American Idol

July 30, 2010

image

Mmoja wa majudge wa American Idol Ellen DeGeneres ametangaza kuachana na nafasi ya ujaji kwenye shindano maarufu duniani la American Idol.

Kwa mujibu wa habari zilizotangazwa na shirika la habari la News Corp. Ellen amesema kuwa anaona uamuzi wake wa kujiunga na shindano hilo lililo maarufu zaidi huko USA si wa busara kwani hapendelei kuonekana akiwa judge vijana ambao wanataka kutimiza ndoto zao wakati huo huo akiwaumiza hisia zao.

Ellen ameongeza kuwa binafsi yake hupendelea zaidi kuvumbua na kuviendeleza vipaji vya vijana na sio kuumiza hizia zao.

Gonga hapa kwa habari zaidi.


BONGO FACEBOOK BEACH PARTY 2010

July 29, 2010

ONE LOVE, ONE NATION,
PEOPLE GET READY
BONGO FACEBOOK BEACH PARTY

WEEKEND DAR ES SALAAM CALLING!!!!!
SATURDAY AUGUST 7th from 1:00 pm Till Late
AT MBALAMWEZI BEACH CLUB (Ex-Malaika House),
MIKOCHENI KWA WARIOBA ASIDE CINE CLUB
MIKOCHENI,
DJ TONNY FROM TZA feat DJ CHOKA IN THE ONE AND TWO
Saturday august 7th time 1:00pm

Nyama Choma by Special Chefs at Mbalamwezi Beach Club

plus get together party from different friends from
Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi, China, India, Malaysia, Rwanda and others
KARIBUNI
KWA MAELEZO ZAIDI
extramilestz@gmail.com
SIMU
077 302 2011
071 355 0699
PROUDLY SPONORED BY:
Sprite (Coke Cola Kwanza),

Zantel, Bunif, Mbalamwezi Beach Club, BASE MAGAZINE
KINDLY SUPPORTED BY:
ISSAMICHUZI.BLOGSPOT,

JIACHIE, G5CLICK.COM,

BONGO CELEBRITY,

BONGO STAR LINK, BAB KUBWA, BONGO5.COM,


Koffi Olomide aendelea kuwasha Moto Rwanda.

July 29, 2010

Koffi Olomide akishambulia jukwaa na Band yake

Mashabiki wakilipuka kwenye Tamasha la Fes Pad ambalo linafanyika kila mwaka nchini Rwanda. Picha hizi kwa hisani ya Manka Lady Jay Dee Ambaye alikuwepo kwenye tamasha hilo.


Sol Campbell aitema Arsenal

July 29, 2010

Sol Campbell akiichezea Portsmouth zamani

Sol Campbell sasa anaelekea Newcastle

Klabu ya Newcastle imekamilisha kutia saini ya kumchukua mlinzi wa zamani wa timu ya taifa ya England Sol Campbell kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Campbell alikuwa huru kuondoka baada ya mkataba wake na Arsenal kumalizika mwishoni mwa msimu wa ligi uliopita.

Lakini pia kulikuwa na taarifa kwamba Arsenal walikuwa na nia ya kuongeza muda wa mkataba na Campbell msimu unaokuja.

Taarifa za mlinzi huyo kuelekea Newcastle zinaondosha taarifa zingine zilizokuwepo kwamba huduma zake pia zilihitajika katika klabu ya Sunderland, na pia klabu ya ligi kuu ya Scotland- Celtic.

”Kujiunga na Newcastle, klabu yenye utamaduni wa kujivunia, na wafuasi wengi , bila shaka kwangu ni fahari kubwa.” Alisema Campbell.

Anakuwa mchezaji wa tatu kuchukuliwa na meneja wa Newcastle Chris Hughton, kwa maandalizi ya klabu hiyo ya kurejea kwenye ligi ya Premier ya England, baada ya kucheza daraja la chini msimu uliopita.

Tayari Hughton alikuwa amekwishawachukua Dan Gosling kutoka Everton na James Perch kutoka Nottingham Forest.

Campbell alifunga ndoa karibuni Fiona Barrat, na punde tu baada ya kurejea kutoka fungate alikwenda kufanya majaribio ya kiafya tayari kuanza shughuli na Newcastle.

Katika msimu uliopita aliichezea klabu ya Arsenal mechi 11 baada ya kupata mkataba mfupi nao mwezi Januari.

Ilikuwa ni mara ya pili kwa Campbell kuichezea Arsenal, aliyokuwa ameiacha mwaka 2006 kujiunga na Portsmouth.

Akiwa Arsenal waliwahi kushindi taji la premier mara mbili, Kombe la FA mara tatu, na alipojiunga na Portmouth akawaongoza kutwaa taji hilo la FA mwaka 2008.

Msimu uliopita Campell alianzia kwenye ligi ndogo ya daraja la pili katika klabu ya Notts County kabla ya kuondoka kwa hiari kurejea Arsenal Septemba mwaka uliopita.

Ameshaichezea timu ya taifa ya England mara 73.


Profesa Jay alonga Bongo Celebrity, aongelea Ziara yake ya US!!

July 29, 2010

 

image

Unapoongelea wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao miziki yao na mashairi yao yametoa mchango mkubwa katika kuufanya muziki huo ukubalike na kupewa heshima na nafasi yake katika jamii,bila shaka huwezi kuthubutu kumweka pembeni Joseph Haule au kama anavyojulikana miongoni mwa washabiki na wadau wa muziki; Proffessor Jay,MC Shupavu,The Heavy Weight MC,Jay wa Mtulinga,Mti Mkavu,Jiizeh nk.

Hivi sasa Prof.Jay yupo nchini Marekani akiendelea na tour yake ndani ya taifa hilo ambalo hivi sasa linaongozwa na Barack Obama,Rais wa kwanza mweusi. BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na ziara hiyo. Je unataka kujua atatua na kufanya shows katika miji na majimbo gani? Anasemaje kuhusu ambacho ameweza kukiona na kujifunza nchini humo mpaka hivi sasa? Kwa majibu ya maswali hayo na mengine,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

Kwa maswali na majibu basi ungana na Sir Geofrey Msangi ndani ya Bongo Celebrity kujua mengi zaidi.


%d bloggers like this: