Mpya toka kwake Celeo Scram akimshirikisha Deprick

December 17, 2015

Anaitwa Celeo Scram moja ya vijana waliotoka WMMM ambaye tangu atoke amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuweka muziki wake kwenye ramani ya wanamuziki wa kizazi cha Tano cha Congo DRC. Ikumbukwe kuwa wengi wana wanamuziki ambao awali walitamba na majina yao kipindi Wenge Musica iko pamoja na hata baada ya kuparanganyika wengi wa waliokwenda Solo hawakufanikiwa isipokuwa wachache kama Ferre Gola na Huyu Celeo Scram. Wengine kama kina Tutu Caludji ambaye ametoka miaka ya karibuni, Japonaise Maladi ambaye awali alitoka kwa WMMM pia hakufanikiwa na kurejea nyumbani,  Adolph Dominguez ambaye alitimka na Werasson na baadaye kujitenga pia hajafanya vizuri, wengine ni Allain Mpella ambaye alitamba sana kwenye album ya Titanic ya Jb Mpiana pia hajafanya vizuri kama solo artist na wengine wengi kama Rio wa Wenge BCBG nk.
Celeo Scram kama alivyo Fally Ipupa anasemwa kuhusudiwa sawa na wadasa na kwa vijana wanamuona kama mwanamuziki wa kizazi kipya cha Rhumba.


Christian Bella kutoa Kolabo na Koffi Olomide

November 22, 2015

image

Mwanamuziki nguli Koffi Olomide anatarajia kutoa wimbo mpya ambao amemshirikisha Koffi Olomide. Kwa mujibu wa habari ambazo Spoti Starehe imezipata inasemekana kuwa kwenye wimbo huo Koffi anaingia na kibwagizo chake cha Selfie ambacho kaimba kwa Kiswahili.
Mtoaji habari wetu anasema kuwa Kwa sasa Bella yuko yuko nchini ambako amerejea karibuni toka DRC ambako aliongozana na King Dodoo katika kufanikisha urekodiji wa Wimbo huo.

Kwa sasa Bella anatamba na wimbo ambao ametoa akiahirikiana na Ally Kiba. Spoti starehe inamtakia kila la heri katika kazi yake hiyo na kuosubiria kwa hamu sana single hiyo maana imejumuisha vichwa vya kazi.


Tafsiri ya Wimbo Selfie – Ekotite wa Nguli Koffi Olomide.

November 20, 2015

 

Unaweza kumuita La star congolaise de la rumba, Koffi Olomidé, Antoine Agbepa Mumba à l`état- civil, est née le 13 … le Grand Mopao, Mopao Mokonzi, QuadraKoraman, Mopao Sarkozy, le Jeune Pato kibao Selfie Ekotite, Wimbo huu ni mmoja wa vibao matata ambavyo vinapatikana kwenye Album yake mpya  ya Ishirini (20) ambayo inasemekana ndio albamu yake ya mwisho kabla haya staafu muziki rasmi.

Huu mwimbo umejizolea maarufu sana kama ambavyo Diamond alivyokuwa anafanya anawaambia mashabiki wake waigize na kijipande cha style ya uchezaji na iliitikiwa karibu Afrika nzima na nje ya Africa kwani tumeona hata Wachezajibwa Timu kubwa kama Chelsea nao wakiigiza kibwagizo cha wimbo huu. Hebu pata kwa kifupi kipande cha wimbo huu kwa tafsiri ujue wanaongelea nini!!

Dj Mopao frontiere ya liwa, kanga foto
(Dj Mopao ni mpaka wa kifo, jipige picha!!)

Tutu Roba

Veut dire oyo ako bina te aza muana ya nzambe te
(Ambaye hachezi (dance) sio mtoto wa Mungu)

Oyo ako bina te, aza mokristu te
(Yule asiyecheza sio Mkristo/mtoto wa Kristo)

Ah Jesus seigneur, seke bien
(Oh Yesu Masiha, safi sana)

Ataku

Hamed Bakayoko, l’homme du peuple
(Hamed Bakayoko, mtu wa watu)

Mbila alobi stope, allez temprorize
(Ofisa anasema (amrisha) simama, Punguza Mwendo)

Oge alobi stope, keba, allez temporize, 

(Ndenge anasema simama, kwa uangalifu, punguza mwendo)

Mbila alobi stope eh, allez temporize
(Ofisa anasema simama, punguza)

Mbila alobi stope eh, allez temporize
(The officer says stop, slow down)Mbila

alobi stope eh, allez temporize
(Ofisa anasema simama, punguza)

Le boss Paul Obambi
(The boss Paul Obambi)

Zua nga foto
(Jipige picha..!!)

To seka moke, ha ha ha ha
(Tufurahi kidogo, ha ha ha ha )

Buka kingo, ekoti te, ekoti te, ekotite…
(Geuza shingo, haujapiga,haujapiga, haujapiga (picha))….. Endelea kuimba…..

 


Ahmed Jan AKA Med Olomide

May 25, 2015

Namleta kwenu kijana Ahmed Olomide, Kiukweli jamaa unaomsikia kwa mara ya kwanza unaweza dhani kama Koffi Olomide anatumbuiza kwa maana ya kuwa wamerandana kwa sauti mnoo.

Ahmed Olomide ni Mcongoman anayeishi Kinshasa kwa Takribani miezi kama sita hivi alikuwa hapa nchini na alifanikiwa kufanya maonyesho mwili tuu hapo Nyumbani Lounge na Lady Jay Dee ila kwa taarifa nilizonazo kwa sasa toka kwa mtu wa Karibu Julie Weston Illunga anasema jamaa amekwenda Kampala ambako anamalizia Video zake. inatazamiwa albamu yake itakayomtambulisha yeye kama yeye sokoni na kwenye ulimwengu wa muziki pia.

Kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa kijana huyo hapa nchini Ahmed Olomide ameshaunda bendi yake akiwa ameleta wanamuziki toka Lubumbashi Kinshasa na sehemu zingine. Wachunguzi wa mambo wanasema jamaa huyu ataleta uinzani kwa mtu kama Christian Bella ambaye anazidi kung’aa kadri siku zinavyokwenda.


Un Prince au Congo; “Mabanga” ya Werason kwa Marehemu Ali Sibaba

April 21, 2015

Wakati inatoka Kibuisa Mpimpa binafsi nilikuwa bado sijaamua niwe upande gani baada ya Wera na Jb Mpiana kutengana.
Wimbo huu unaitwa Un Prince au Congo ni wimbo maalum kwa mtu maalum, aliutunga kwa ajili ya Alici Baba nfanyabiashara mwenyebpesa zake ambaye alijulikana kwa kupenda maisha fulani na alijipenda sana na kupachikwa jina la Prince wa Congo.

Ukisikiliza muziki huu unapata ule u “beeceebeegeeque” kabisa bado walikuwa na composition ya Wenge 4×4.
Pata rubudani hahahha


Tazama Werrason na Jb Mpiana Live kwenye uzinduzi wa Flech Ingeta ya Werrason

April 20, 2015

Ni wazi kuwa mashabiki walikuwa na hamu ya kuwaona hawa jamaa wakipanda jukwaa moja.
Baada ya kimya kirefu hatimaye juzi muujiza ulifanyika na ikawa kweli.

Tathmini nzima inakuja.


MPYA HIYO !!! VIDEO YA WERRASON WIMBO ” BLOCK CADENAS “

October 15, 2014

http://www.youtube.com/watch?v=m0ZEx1dTeQ4

 

BONYEZA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO

KAMA KAWAIDA TUNAWALETEA VITU VIPYA,

BAADA YAKUSIKILIZA AUDIO YA BLOCK CADENAS, SASA TIZAMENI VIDEO YAKE ILIO SAFI KABISA.

BURUDIKENI.

 

L.W.L

 


USIKU MWEMA NA VIDEO YA LINO VERSACE FEAT FERRE GOLA

October 14, 2014

 

TUCHEZE KWA MIONDOKO YA COUPER DECALER!!!! WIMBO ” KO KO KO ”

LINO VERSACE  AMBAE SIKU HIZI HUPENDWA KUITWA ” Soundjata Soumangourou ” Ni Mwimbaji kutoka Inchi ya COTE D’IVOIRE .

NI MMOJA KATI YA WAASISI WA MIONDOKO YA ” COUPER DECALER ”  WAKIWA PAMOJA NA MAREHEMU  ” DOUK SAGA ”

 

L.W.L

 

 


TUMKUMBUKE GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI / NYIMBO ZAKE ZILIZO PIGWA MARUFUKU

October 14, 2014

 

Miaka 25 Sasa tokea Afariki Dunia Guiji wa Muziki wa Rumba FRANCO LUAMBO MAKIADI.

Ingawa Mengi yamesha andikwa kwa kumhenzi GRAND MAITRE FRANCO, Leo hii nachukua fursa ya kuchambua Baadhi ya Nyimbo zake zilizo pigwa Marufuku.

Wala sio Siri tunapo tamka ya kwamba ” GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI FRANCO ” katokea kua Tajiri sana katika kipindi cha Utawala wa Rais MOBUTU SESESEKO.

Mbali na Urafiki ambao FRANCO LUAMBO alikuanao na RAIS MOBUTU, ilifikia wakati fulani Serekali ikazipiga marufuku Baadhi ya Nyimbo zake zilizo kua na Ujumbe uliokeuka Maadili ya Umma.

Kutokana pia na Sababu mbali mbali, SEREKALI YA RAIS MOBUTU, ilikua makini sana na Wanamuziki, hasa palikua na Watu hodari ambao kazi yao kuu ilikua kufanya uchunguzi wakina kwa Ujumbe unao patikana kwenye NYIMBO. Ikiwa kwa Namna moja au Nyingine kwenye Wimbo wewe Msanii ukithubutu Kutamka Jina la Mpinzani, Basi Wimbo huo kamwe hauta ruhusiwa na Wewe mwenyewe utajikuta ukiwa matatani.

1. Mkasa kama huo umemkuta  TABU LEY ROCHEREAU, wakati katunga Wimbo ” KASHAMA NKOYI ” kwenye Wimbo huo, ROCHEREAU kayatamka Maneno haya : ” Boni Oweleli, Okende liboso ya Baninga, Soki okutani na LUMUMBA okoloba nini PAPA ?  Tokengelaki yoo te  KASHAMA  NKOYI / INAKUAJE UKASAFIRI, WATUTANGULIA SISI WENZIO, HUKO UENDAKO, UTAKAPO KUTANA NA LUMUMBA UTAMWAMBIAJE BABA ? WALA HATUJAWAHI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KWA YALE YALIYO KUKUTA ” KASHAMA NKOYI “.

Wimbo umepigwa Marufuku, sio kwasababu  Katajwa LUMUMBA hapana, Bali Jina ” KASHAMA NKOYI “, Serekali ya MOBUTU yamushutumu ROCHEREAU TABU LEY kutumia Jina hilo Bandia kwakumhenzi ” PIERRE MULELE ” ambae alikua Mmoja kati ya MAWAZIRI wa EMERY PATRICE LUMUMBA,SHUJAA WA UHURU WA CONGO. Baada ya kuuwawa LUMUMBA, PIERRE MULELE kasimama kidete kupambana na SEREKALI ya MOBUTU. Vikosi vya Waasi vilio tawala mashariki mwa Congo hasa kwenye Mikoa ya KIVU. VIlikua vikimchukulia yeye kama Kiongozi wao Mkuu. Ndiko katokea LAURENT DESIRE KABILA. PIERRE MULELE kauwawa Mwaka 1968.

2. FRANCO LUAMBO NA WIMBO WAKE ” LUVUMBU NDOKI “, Kwenye Wimbo huo, FRANCO kaimba kwa KIKONGO, Lugha yake ya Asili. Ujumbe kwenye Wimbo huo ni kwamba ” WEWE LUVUMBU MTU AMBAE KIJIJI KIZIMA KINAKUTEGEMEA, WANAKIJIJI WOTE WAKO CHINI YA USIMAMIZI WAKO, KUTOKANA NA UCHAWI WAKO, UMEWAMALIZA NDUGU ZAKO WOTE WAKIKE KAMAVILE WAKIUME, SASA WAKATI UTAKAPO FARIKI, NANI YULE ATAKAE KUZIKA ? MIMI FRANÇOIS NASHINDWA KABISA KULIA, KWAKWELI HUA NAJIULIZA, KWANI UCHAWI WAKO UPO MGONGONI AU TUMBONI MWAKO.

Wimbo huo Ulipigwa marufuku paletuu ulipo tolewa, SEREKALI ya RAIS MOBUTU, yasema kwamba, Kupitia Wimbo huo, FRANCO LUAMBO MAKIADI kawatukuza Wanasiasa Wanne Walio Uwawa kwa Kunyongwa kwa Madai kwamba walikua na nia ya kuipindua Serekali Mwaka 1966.  Wanasiasa hao walio nyongwa ni hawa :

1. JÉRÔME ANANY ( WAZIRI WA ZAMANI WA ULINZI WA TAIFA )

2. EMMANUEL BAMBA ( SENETA )

3. ÉVARISTE KIMBA ( WAZIRI MKUU WA ZAMANI )

4. ALEXANDRE MAHAMBA ( WAZIRI WA ARDHI )

Baada ya Wimbo huo kutolewa, FRANCO LUAMBO  Tetesi zilimjia kana kwamba SEREKALI ipo kwenye harakati ya kumfungulia Mashitaka na Kumuweka Jela. LUAMBO kavuka yeye pamoja na Group lake nakwenda kujihifadhi kwa Mda JIJINI BRAZZAVILLE.

Akiwa JIJINI BRAZZAVILLE, RAIS MOBUTU kamtumia Wajumbe na kumshawishi arudi KINSHASA, maisha yake haitakua hatarini. FRANCO LUAMBO kaupokea wito huo ila kawa katika hali ya Mtu mwenye Kusita. Mwishowe kaamua kurudi KINSHASA.

Akiwa JIJINI KINSHASA, FRANCO LUAMBO kajikuta yuko matatani, Kakaribishwa na kikosi cha Wanajeshi. Wakamuamuru yeye na Group lake wapande ndani ya Gari lao, nakupelekwa moja kwa moja  Jela ya NDOLO. Huko walikaa kwa Mda wa Siku Mbili, yasemekana Walicharazwa bakora sawasawa,

Baada yakutolewa kwenye Jela ya NDOLO,  FRANCO LUAMBO na Group lake, wakahamishwa kwenye Kambi ya Jeshi ” TSHATSHI “. Huko pia wakashikiliwa kwa siku kadhaa wakiwa kambini humo.

Ndipo Ikatokea Siku amabayo RAIS MOBUTU akaja mwenyewe kujadiliana na LUAMBO MAKIADI. kamtamkia Maneno haya : ( KUANZIA LEO HII HADI ITAKAPO FIKIA WAKATI WA MIMI KUONDOKA MADARAKANI, UTAKUA UKINIIMBIA MIMI, WATAKIWA KUNIFANYIA KAZI ZANGU ZOTE, NA TENA KWA WAKATI WOWOTE NTAKAO KUHITAJI ) .

Nakwakeli Tokea siku hiyo, FRANCO LUAMBO kawa kiungo kikuu sana kwa Kampeni ya RAIS MOBUTU. na kutokana na ushirikiano huo, kanufaika sana kuwazidi Wanamuziki wengine wote wa Inchi hiyo katika kipindi hicho cha utawala wa Serekali ya MOBUTU SESESEKO KUKU NGBWENDU WAZABANGA JOSEPH DESIRE.

Mwaka 1978,  FRANCO LUAMBO MAKIADI kawekwa tena JELA kutokana na Utunzi wa Nyimbo ( HELEINI na JACKIE ),

Nyimbo mbili hizo zilikua na Maneno machafu sana tena yaku yaharibu maadili ya Umma. Sheria ikachukuliwa kuzipiga Marufuku zisipitishwe kwenye Radio na TV ya taifa. FRANCO mwenyewe kajitetea, kasema wala NYIMBO hizo hajizauzwa Sokoni zilikua bado hazijawekwa kwenye CD. bali Watu walikua wakizisikiliza Wakati wa SHOO kwenye Ukumbi wake wa 1.2.3 KINSHASA.

Aliekua MWANASHERIA MKUU WA SEREKALI kipindi hicho  ” Mr  LEON KENGO WA DONDO “,kalisimamia swala hilo, nakuamuru FRANCO LUAMBO awekwe Jela, kapelekwa kwenye JELA ya ” LUZUBU ” inayo patikana kwenye MKOA WA BAS CONGO aliko zaliwa FRANCO.

Huko JELA, FRANCO kawa mwenye masikitiko, Kwanini RAIS MOBUTU kashindwa kumsaidia ? yeye ambae alikua akimchukulia kama Rafiki. FRANCO kapigwa na Ugonjwa wa HEMORRHOID. katabaanika kabisa. Kabaki na chuki na kinyongo dhidi ya MWANASHERIA ” LEON KENGO WA DONDO ” aliempeleka JELA. Haelewi kwanini kawekwa kizuizini wakati Hajawahi kuzidumbwiza Nyimbo hizo hadharani.

Miaka michache baadae, palitokea na mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, LEON KENGO WA DONDO  Kanenguliwa Cheo cha MWANA SHERIA MKUU WA SEREKALI na kutomwa JIJINI BRUSSELS kama BALOZI WA CONGO.

Furaha ilikuaje kwa FRANCO LUAMBO MAKIADI ?, bila kukawia kamtungia Wimbo ” TAILLEUR ” kwenye Wimbo huo FRANCO kanena haya : ( LIKAMBO NALOBAKI LOBI, MONOKO NA NGAI NGANGA / UTABIRI WANGU WATOKEA KUA KWELI, MDOMO WANGU KAMA WA MGANGA WA JADI ).

MOKOLO TONGA ABOTOLI TONGA OKOTONGA NANI ? / MWENYE SINDANO YAKE KESHA ICHUKUA, SASA UTATUMIA NINI ILIUENDELEE KUWACHOMA WENGINE?

OLOBAKI TROP NA ESIKA YANGOO BATIE YO PEMBENI LOBA LISUSU MAMA / ULIKUA UKIKIJIVUNIA SANA CHEO HICHO, SIUMEONA WAMEKUONDOA, UNANINI CHAKUONGEA? Wimbo huo pia ukapigwa Marufuku kwa Mda.

Mwaka 1982, RAIS MOBUTU Kamwitisha LEON KENGO WA DONDO , na kamteua kama WAZIRI MKUU WA INCHI.

FRANCO LUAMBO hajaridhishwa ni kitendo cha RAIS MOBUTU kumpa KENGO WA DONDO cheo cha WAZIRI MKUU, bila kusita Katunga Wimbo ” TRES FACHE “. Mtamsikia akiiimba : ( OKOSI NGAI MAMA YONAYE BOBOYANA, LOBI LISUSU BAKUTI YO NA VOITURE NA YEE, ELOKO NASALA NAYEBI TEEOO MOKILI / WANIDANGANYA KAMA NYIE WAWILI SIO TENA MARAFIKI, KESHO YAKE WATU WAMEWAONA MKIWA PAMOJA NDANI YA GARI, JAMANI KOSA GANI NILILOLIFANYA MIE!!! ). Kadhalika Wimbo huo Ulipigwa pia Marufuku.

GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI KAFARIKI DUNIA  INCHINI BELGIUM TAREHE  12-10-1989.

SIKU YA MAZISHI YAKE, LEON KENGO WA DONDO AMBAE NDIE ALIEKUA WAZIRI MKUU, KAJA KUTOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA NIABA YA SEREKALI.

WAKATI WA MISA  YA MAZISHI YAKE, PADRE KASEMA : ” LUAMBO ALIKUA MTUME WA MUZIKI, HAKUNA ALICHOKISAHAU KATIKA UTUNZI WAKE, KAVICHAMBUA VITU KADHALIKA NA WATU WAKILA RIKA, HATA RAIS MOBUTU HAJAACHWA NYUMA.

NYIMBO ZAKE KADHAA ZILIPIGWA MARUFUKU, HATA HIVYO ZILIENDELEA KUPENDWA SANA NA UMMA. HUKU NYIMBO ZAKE  NYINGINE HADI LEO HUCHUKULIWA KAMA NEMBO YA TAIFA.

L.W.L

 

 

 

 

 

 

 


MA DANCERS WA WERRASON WAFURAHIA TUZO ZA BOSI WAO KWAKUNENGUA!!!

October 13, 2014

 

HAYA TIZAMENI WENYEWE, KWA NAMNA GANI WANENGUAJI WA WERRASON WANAVYO SHEHEREKEA KURUDI KWA BOSI WAO NA TUZO MBILI KUTOKA AMERICA!!!

 

L.W.L


WERRASON KALITEKA JIJI LA KINSHASA, WATU WENGI WAMEJITOKEZA KUMPOKEA KWA SHANGWE UWANJA WA NDJILI

October 13, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO YA MAPOKEZI MAKUBWA YA WERRASON.

PALIKUA NA PATASHIKA JANA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA NDJILI JIJINI KINSHASA,

WENGI WALIJITOKEZA KUMPOKEA WERRASON LE ROI DE LA FORET .

WERRASON KARUDI NYUMBANI AKITOKEA AMERICA AMBAKO KAPEWA TUZO MBILI KWENYE SHINDANO LA NAFCA, LIKIWEMO TUZO LA MSANII BORA WA AFRICA.

 

L.W.L


MKE WA MAREHEMU BABIA NDONGA CHOKORO KAJIELEZA KUHUSU KIFO CHA MWANAMUZIKI HUYO ( SIO MIMI NILIE MUUWA BABIA )C

October 12, 2014

 

Katika mahojiano yake na Waandishi wa Habari, Mama ” HALIMA “, ambae ndie Mke Halali wa BABIA NDONGA kajieleza kwa kirefu kutokana na Kifo cha Mmewe.

HALIMA : Ilitokea Siku Moja BABIA kaniambia, ” Sikiliza HALIMA, Sikutaki tena, Tokea leo hii jisikie kuwa huru, jitegemee mwenyewe. Nimeshampata Kimwana mwengine ” ( yasemekana Kimwana huyo ni  Binti wa Waziri Mmoja kwenye Serekali ya Congo ).

Nikamwambia, hebu Mme wangu, kweli waweza kuniacha Baada ya takriban miaka Minane ya Ndoa, nakwenda kuishi na Mwanamke mwengine? Maneno hayo yaliniuzi sana, Nikafungasha vitu vyangu na kuondoka Nyumbani pale ambapo tulikua tukiishi pamoja. nikahamia sehemu nyingine. Ila tukawa tunaendelea kuwasiliana kupitia njia ya Simu.

Mimi HALIMA ndie Mama mlezi wa Watoto wa BABIA alio wazaa Inje na Wanawake wengine. Hadi leo Wako Nyumbani kwetu KINSHASA kwenye Barabara ya FUNA. Watoto wake PRINCE na ANNA wanaishi kwetu.

SIKU ALIO FARIKI BABIA, KWAKWELI ALIKUA NYUMBANI KWANGU, Mimi ndo nimemuitisha aje tuzungumze. Ila kabla yakuja Nyumbani kwangu, katokea Uwanja wa Ndege akimsubiria Kimada wake aliekua akitokea Ulaya, kwa Bahati mbaya, Mwanamke huyo hajatokea, yaani kahairisha Safari yake bila kumpa BABIA taarifa yeyote.

BABIA kaja Nyumbani kwangu, Kabisha hodi mlangoni, Nilikua niko kwenye Msala nikipiga Rakaa, Mkononi mwangu nilikua nikishikilia Tasbihi, kwakua Mimi ni Muislamu.

Nikaenda kumfungulia BABIA Mlango, pindi tuu alipo ingia ndani nakukaa kwenye Kiti, BABIA akesema HALIMA nahitaji Mazungumzo yakina na!!! kabla hata hajamalizia maneno, Akawa anashindwa kabisa kuendelea kuongea, huku nikamuona Mtu akiwa mwenye kupooza Mikono hadi kwenye Miguu.

Nikashtushwa na hali hiyo, Mwenyewe nikaanza kupiga kelele,  BABIA NIKITU GANI, UNAUMWA NINI, NIKAOMBA MSAADA KWA MAJIRANI, WAKAJA, TUKAMUWAHISHA KWA HARAKA KWENYE HOSPITALI NDOGO KWA DOKTA JUDE.

MTANGAZAJI : Kwani ilichukua Mda gani tokea pale mlivyo achana? yeye akiwa anaishi Nyumbani kwake na wewe Ukawa unapanga Sehemu yako ?

HALIMA : Ilichukua kama Wiki Moja na Siku Tano vile tokea tuachane. Mwenyewe ndo kaniacha, Kaniambia fungasha vitu vyako, anza Maisha yako jinsi uonavyo. Bado ninayo MSG yake nyingi tuu aliokua akinitumia kupitia mtandao wa VIBER. kasema HALIMA JITEGEMEE MWENYEWE, ACHANA NAMIMI, NINAYO MIPANGO MINGI SANA AKILINI MWANGU. MWAKA HUU NILAZIMA NIENDE ZANGU ULAYA, NIMESHA KAA SIKU ZA KUTOSHA JIJINI ” LUANDA “, WAKATI WAWADIA SASA KWAMIMI KUMALIZIA ALBUM YANGU.

Haya narudilia ongezi la hapo awali, TULIPO MFIKISHA BABIA KWENYE HOSPITALI YA DOKTA JUDE, YEYE KAMPOKEA, kamchunguza na kumchoma sindano, Ndipo katushauri tumpeleke kwenye Hospitali kubwa, hali yake yahitaji Tiba nzito zaidi. Ilibidi tumkimbizie kwenye Hospitali KUU, Wakampokea na kumpeleka Moja kwa Moja kwenye Chumba cha dharura, wakamuweka Chupa za maji kwa haraka sana. Ila hali ya BABIA ilikua si nzuri kabisa, alikua hana tena Kauli, kawa Mtu mwenye kutizama tuu.

Nikachukua Simu yake, Nikaanza kuwapigia Marafiki zake nakuwajulisha hali halisi alionayo BABIA, Hakuna yeyote alie jitokeza na kuja kumjulia hali mwenzao. Kutokana na hali yangu ya uchovu, Ma Dokta wakanishauri niende Inje maramoja wao wanaendelea na kazi ya kumuhudumia.

BAADA YA MDA, NIKAAMUA KURUDI CHUMBANI KUCHUNGUZA HALI YA BABIA INAENDELEAJE ?, NDIPO MA DOKTA WAKANIAMBIA KWAMBA BABIA KAFARIKI DUNIA. (ANALIA …)

MTANGAZAJI : Kwani Wewe na huyo Mwanamke mwengine Mmshawahi kuonana ? Mmegombana kiukewenza? au kubadirishana maneno kwenye Simu?

HALIMA : Kuna Siku kanitumia Ujumbe kupitia MSG ya Facebook, kanitukana, kasema BABIA ni wakwake, anajiandaa kuja kumchukua na kuondoka naye, Mimi simuwezi , Baba yake ni KIGOGO kwenye Serekali ya CONGO. Hakuna kitakacho mzuia asifunge Ndoa na BABIA. kasema Mimi ni mjinga. Wala sijawahi kumuona , hata BABIA mwenyewe alikua bado hajamuona. Leo hii ndo nimepata taarifa kwamba kawasili JIJINI LUANDA.

MTANGAZAJI : HEBU TUAMBIE UKWELI Kuhusu Safari yako ya kwenda kwenye MJI WA WAMBO, Ulienda huko kufanya nini  ?

HALIMA : Kwenye MJI WA WAMBO nilienda kufanya BIASHARA ZANGU, hua nauza CD, BABIA alivyosikia niko WAMBO, kanifwata kwa haraka sana, kajakunitishia Nirudi haraka LUANDA, vinginevyo atanifanyia mpango nipelekwe moja kwa moja CONGO KINSHASA.

Nikamuambia kamwe haitowezekana kwangu mimi nirudi CONGO, Mwanaume gani wewe usie nijali? sipati hata Dola 10 kutoka kwako. Ukwali ni kwamba BABIA kaambiwa na Watu kanakwamba Mimi nimeolewa WANDO ndo kwamaana hiyo kaja akiwa mwenye hasira sana. kanigombeza hadi tukaishia Polisi.

Bado tukiwa kwenye MJI WA WAMBO, BABIA kamleta nakunionyesha Mwanamke mwengine Mbele ya macho yangu,  Dada huyo anajulikana kwa Jina la ” LOTTY “, BABIA kanifahamisha ya kwamba huyo ndo Mkewe tokea sasa. Nikamwambia BABIA naomba unipe talaka, nimesha choshwa na vituko vyako. Kwani amenisikia ?

Nikaamua kumuacha pale kwenye MJI WA WAMBO nikarudi zangu LUANDA, Bado akiwa WAMBO, BABIA kapata tenda ya kufanya SHOO mbili. Alipopewa taarifa kwamba nimeshakimbilia LUANDA, Huyo kafunga Safari nakunifwata hadi LUANDA, kaja kuniomba Msamaha, kanitaka radhi, kasema Mimi ndie MAMA WATOTO WAKE, kapagawishwa na Mambo ya Ulimwengu. Kanigea Zawadi ya Dola Elfu Tatu, na Mkufu wa Dhahabu. BABIA kaangua kilio … Moyo wa Umama,Moyo wa Huruma ukanijia, nikamsamehe… Tukaendelea kuishi tena pamoja.

MTANGAZAJI : Tumesikia kwamba Zawadi hiyo ya Mkufu wa DHAHABU ilileta kasheshe iliompelekea BABIA kuwekwa Mbaroni Polisi, ilikuaje?

HALIMA : Kumbe Mkufu huo wa Dhahabu, BABIA kapewa na Kimada wake LOTTY, walipo pezana zawadi zao kutokana na Mapenzi yao mimi wala sikuwepo. Yasemekana  BABIA alikua kampa LOTTY ahadi za uongo kama ndie Mchumba wake, wataishia kufunga Ndoa. Hali hiyo ya Wachumba, ikamfanya LOTTY aanze kumgharamia BABIA kwakumnunulia vitu kadha, ikiwemo Mkufu huo.

Ikatokea Siku moja, BABIA kapokea simu, alie mpigia ni LOTTY, wakaanza kujibishana kwa ukali, nikamsikia LOTTY akisema UMENISALITI, UMEMRUDILIA HALIMA, HAKUNA SHIDA, MWENYEWE UTAONA YATAKAYO KUKUTA.

Wala haijapita Siku, LOTTY huyo katua kwenye MJI WA LUANDA, akiongozana na MABAUNSA wawili waliojaa sawasawa. Jamaa hao walimshikilia BABIA, WAKMTWANGA MBAYA SANA, hadi kaumia Usoni, Mdomo ukamjaa kwelikweli.

Polisi wakaja kuingili kati, wakawachukua wote nakuwapeleka Kituoni kuwasikiliza. Wamewekwa huko kwa siku mbili mfululizo. Mimi nikaambiwa nirudi zangu Nyumbani wala sina hatia yeyote. Kesi yawahusu Wapenzi, Huko waliko kabidhiana Zawadi zao wala mimi sikuwepo.

Huko Kituoni cha Polisi, Muafaka ulipatikana, BABIA KAKUBALI DENI, KASAINI KARATASI NA KATOA AHADI YA KUMRUDISHIA LOTTY VITU VYAKE.

JAMANI ACHENI KUNIPAKAZIA, WALA SIO MIMI NILIE MUUWA BABIA, ALIKUA TAYARI KESHA NIKATAA, KASEMA HALIMA BASI SIKUTAKI TENA, KWENYE MAISHA YANGU, NIMESHA MPATA ” HELENA MWANZA “. YEYE KANIPA AHADI YAKUNISAIDIA NA KUNIPELEKA ULAYA NIKAMALIZIE ALBUM YANGU. JAMANI ,NTAMUUAJE BABA WATOTO WANGU? SIWEZI KUMTAKIA BABIA UBAYA WOWOTE. ACHENI KUNICHAFUA!!!

NDIO BABIA ALIKUA MME WANGU, NDIE PIA KANILEA KWAHIYO KWA UPANDE MWENGINE NILIKUA NIKIMCHUKULIA KAMA BABA YANGU. WALA SIJAMUUWA BABIA, KAFA KIFO CHA KAWAIDA KUTOKANA NA MAPENZI YAKE MUNGU. NILIVYO HAPA MWENYEWE NASHINDWA KABISA KUAMINI …

 

L.W.L


PICHA YA JB MPIANA AKIWA INCHINI AMERICA

October 11, 2014

10348390_673161909447886_2761523108126892526_npia3

 

PAPA CHERI MOTO PAMBA TOKEA MAJUZI YUKO INCHINI AMERICA,

KAENDA KUUNGANA NA FAMILIA YAKE WALIO MTANGULIA HUKO, KWA AJILI YAKUFWATILIA MIPANGILIO YA CHUO KIKUU ALICHO UNGANA NACHO BINTIE DAIDA MPIANA.

JB MPIANA KIMUONEKANO KWENYE PICHA ANAPUNGUA, YASEMEKANA ANAJIWEKA SAFI KWA MAZOEZI ILI AWE FITI KABISA WAKATI WAKUTOLEWA KWA ALBUM “BALLE DE MATCH” MWISHONI MWA MWAKA HUU.

L.W.L


SIKILIZENI UMAHIRI WA UIMBAJI WA VIJANA WA WENGE BCBG ( JB MPIANA ) SAFI SANA

October 11, 2014

 

VIDEO SAFI, SAUTI NZURI  ISIOKUA NASHAKA, KWA KWELI ALBUM ” BALLE DE MATCH ” NATABIRI ITAKUA JUU NA ITAPENDWA NA WENGI

VIJANA WA WENGE BCBG WAKIONGOZWA NA YAYA ZULEMA,  ATSHUDA  (DIEGO MILITO), HUGO BOSS, KWENYE GITA  YUKO FRENCHIE KEMBE.

SIKILIZENI WENYEWE UIMBAJI WA ” YAYA ZULEMA STRANGALEY “, ANZIA KWENYE DAKIKA 2:37 : MTAMSIKIA AKIPAA ( YE YE YE YEEEE, MA BOUCHE NE CESSE DE RÉPÉTER CE MOT JE T’AIME SOUVE / KAMWE MDOMO WANGU HAUTOCHOKA KUNENA NENO NAKUPENDA SOUVE ( JB MPIANA ).

MES YEUX RÉCLAMENT TA BEAUTÉ JAMAIS IRRESISTIBLE / MACHO YANGU YAHITAJI KUONA UZURI WAKO USINAKIFANI

SOLO NAYO YA NZOTO EKOMA ATA PARFUM PRÉFÉRÉ NANGAI : HARUFU YAKO YA MWILINI ITOKEE KUA MARASHI YANGU NIIPENDAYO …

JAMANI KAZI KWENU

 

L.W.L

 

 


KOFFI OLOMIDE KAMPOKEA KISI NDJORA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUTOLEWA JELA LEO

October 10, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO YA KISI NDJORA AKIWA NYUMBANI KWA KOFFI OLOMIDE.

HATIMAE KISI NDJORA YUU HURU BAADA YAKUPEWA MSAADA KUTOKA KWA MAWAKILI WA KOFFI OLOMIDE.

JB MPIANA NDIE ALIEKUA WAKWANZA KUMFUNGULIA MASHITAKA KISI NDJORA KWAKOSA LA KUMPAKAZIA MAMBO YASIOKUA NA UKWELI WOWOTE, BAADA YA KUTAFAKARI, JB MPIANA KUPITIA MAWAKILI WAKE, KAIOMBA MAHAKAMA JIJINI KINSHASA IMFUTIE KISI NDJORA KESI.

WAKATI AKIACHIWA HURU KUTOKANA NA KESI YA JB MPIANA, FALLY IPUPA KWAUPANDE WAKE, KAJA PIA KUMFUNGULIA MASHITAKA KISI NDJORA,KASHUTUMIWA KOSA LA KUMTUKANA , KUMTISHIA MAISHA FALLY IPUPA…

IZINGATIWE YAKWAMBA KATIKA MZOZO ULIOKO KATI YA JB MPIANA NA KOFFI OLOMIDE, KISI NDJORA YEYE NI MPAMBE NAMBA MOJA WA KOFFI OLOMIDE, KWAKUTAKA KUMUUMIZA ZAIDI JB MPIANA, KAMTUPIA KHASHFA MBAYA KWAKUSEMA, ALIMUHARIBU MMOJA KATI YA WANENGUAJI WAKE NA KUMPA MIMBA , BINTI ANAEJULIKANA KWA JINA LA ” MWANATSUKA ” AMBAE KIUMRI BADO MDOGO CHINI YA MIAKA 16.

INGAWA KISI NDJORA ANAO MUONEKANO WAKIUME, BALI NI MWANAMKE NA ANAISHI NA MWANAUME, ANA WATOTO HADI WAJUKUU!!!

KISI NDJORA ( CHRISTINE ) NI DADA WA MAREHEMU BABIA NDONGA CHOKORO ALIE FARIKI JUZI JIJINI LUANDA ( ANGOLA ).

 

L.W.L

 


KOFFI OLOMIDE ( MUTSHIRIBARA ) / CLAUDIA BAKISA NA AWILO LONGOMBA ( MUTSHIRIBARA )

October 10, 2014

HAPO JUU VIDEO YA WIMBO MUTIRIBARA ( UTUNZI WA CLAUDIA BAKISA AKISAIDIWA NA AWILO LONGOMBA )

 

  MUTSHIRIBARA KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO

 

Takriban Wiki Mbili zilizopita KOFFI OLOMIDE QUADRA-KORAMAN katoa Wimbo ” MUTSHIRIBARA ” ambao unatamba vibaya sana Kwenye Hit Parade Mbalimbali, hata kwenye YOUTUBE Umetizamwa na zaidi ya Watu Laki Mbili.

Jana Mwana Dada ” CLAUDIA BAKISA ” akisaidiwa na Mkongwe ” AWILO LONGOMBA ” Wanatoa kibao ” MUTSHIRIBARA “.

Huku Kwenye Nyimbo zote hizo Mbili, wanarudilia Refrain ( Mutshiribara laisse moi danser mutshiribara ) Mutshiribara yes yes Mutshiribara .

Nategea Mtaburudika na NYimbo zote Mbili, Ila Mimi kaupendeleo kangu kwa MOPAO, kanirudisha Nyuma kidogo na RAPA za zamani zilizo pendwa ( PUSA MAMA PUSA, OYO BABELELAKA SAMBELA, SITUTALA SITUTALA MAMA…) .

 

L.W.L


MPYA HIYO YA WERRASON NGIAMA MAKANDA WIMBO ” BLOCK CADENAS ” AUDIO

October 9, 2014

 

BOFYA KICHWA CHA HABARI UPATE KUSIKILIZA  GENERIC MPYA YA WERRASON

 

KAMA KAWAIDA YETU TUNAWALETEA GENERIC MPYA HIYO YA WERRASON, ” BLOCK CADENA ”

UNAWEZA UKAUNUNUA KWENYE ITUNE KWA BEI ISIOZIDI DOLA 1

KACHANGANYA VYOMBO KIAINA !!!

BURUDIKENI.

 

L.W.L

 

 


TUMKUMBUKE ” BABIA NDONGA CHOKORO ” TAFSIRI YA WIMBO ” AMEN “

October 9, 2014

 

MSANII MWANAMUZIKI BABIA NDONGA KAFARIKI JANA TAREHE 08-10-2014 JIJINI LUANDA ( ANGOLA )

TUNAWALETEA TAFSIRI YA WIMBO WAKE ” AMEN ” UNAO PATIKANA KWENYE ALBUM ” MAGIE ”

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA !!! AMINA


Ameeeeeeeeeeeen
Notre Père qui est aux cieux, yo moko oza mona, mapamboli tozwa / BABA YETU ALIE MBINGUNI,MWENYEWE WAONA BARAKA ZAKO ZIMETUFIKIA
Quartier Latin anti dopage / QUARTIER LATIN NI KIKOSI KINACHO PAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA!!!

Nzambe ozomona, Le Chokoro babia Ndonga azwa mapamboli!! MUNGU MWENYEWE KAYAONA, BABIA NDONGA KABARIKIWA

Papa na ngai motu ya pasi, mama aboti ngai nde mobola,/ BABA YANGU NI KABWELA ASIE NAKITU, MAMA YANGU MZAZI PIA NI MASKINI

Motema etonda posa ya kokabela mozangi, okokaba nini eee,/ MOYO WANGU WAJAWA NA NIA YAKUWASAIDIA MASKINI, SASA NTAWASAIDIAJE ILHALI MWENYEWE SINA UWEZO!!!

Nzambe na sengi se na yo ooo, bomengo oo bwanya mayele eeee, ooo bwanya aaaa. / NTAKACHO KUOMBA MUNGU WANGU UNIJAALIE  KIPATO, BUSARA NA HEKIMA

Ngai papa na ngai motu ya pasi, mama aboti ngai nde mobola,/ BABA YANGU NI KABWELA ASIE NAKITU, MAMA YANGU MZAZI KADHALIKA NI MASKINI

Motema etonda posa ya kokabela mozangi, okokaba nini eee,/ MOYO WANGU WAJAWA NA NIA YAKUWASAIDIA MASKINI,NTAWASAIDIAJE ILHALI MWENYEWE SINA UWEZO!!!

Nzambe na sengi se na yo ooo, bomengo oo bwanya mayele eeee, bwanya aaaa. / NTAKACHO KUOMBA MUNGU WANGU JAALIA NIPATE KIPATO, BUSARA NA HEKIMA

Bomengo po nini eee nalelaka na Nzambe ee/ UTAJIRI KWANI KITU GANIII, HUA NAMLILIA BABA MUNGU WANGU

Eli Eli lama saba tani, lokola Yesu na ngomba ya golgota eee Nzambe po nini yo otiki nga eee / ELIA ELIA LAMA SABACHTHAMI, KAMA KILIO CHA YESU AKIWA KWENYE MLIMA WA GOLGOTHA!!!

Bomengo po nini eee nalelaka na Nzambe ee /UTAJIRI KWANI KITU GANI, HUA NAPELEKA KILIO CHANGU KWA BABA MUNGU.

Eli Eli lama saba tani, lokola Yesu na ngomba ya golgota eee Nzambe po nini yo otiki nga eee /ELIA ELIA LAMA SABACHTHAMI, KAMA KILIO CHA YESU AKIWA KWENYE MLIMA WA GOLGOTHA!!! MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA!!!

Bomengo po nini ee na tunaka aa na maman, / UTAJIRI KITU GANI !!! LIPO SWALI HUA NAPENDELEA MAMA YANGU ANIJIBU.

Est ce que babota nga po na niokamaka, aaa ngai nalembi bo pauvreté eee / KWANI MMENILETA HAPA DUNIANI ILINIJE KUTESEKA ? NACHOSHWA  SANA NAUMASKINI

Bomengo po nini ee na tunaka aa na maman,/ UTAJIRI KITU GANI !!! LIPO SWALI HUA NAPENDELEA MAMA YANGU ANIJIBU.

Est ce que babota nga po na niokamaka, aaa ngai nalembi bo pauvreté eee / KWANI MMENILETA HAPA DUNIANI ILINIJE KUTESEKA ? NACHOSHWA  SANA NAUMASKINI

Bomego po nini ee okoma koleka ngai na mosika,/ UTAJIRI KWANI KUNANINI, PESA NAZIONA KWAUMBALI

Na sala yo na nini ee nzoka nayebi que mobola pe azwaka, po nini ngai te eeee / MBONA SIJUI KIPI KIBAYA NILICHO KUTENDEA, INGAWA BADO NAKAA NIKIWA NA IMANI KWAMBA, IPO SIKU YULE AMBAE NI MASKINI HUTOKEA KUA TAJIRI, MBONA KWANGU MIMI BADO !!!
Bomego po nini ee okoma koleka ngai na mosika, / UTAJIRI KWANI KUNANINI, PESA NAZIONA KWAUMBALI

Na sala yo nini ee nzoka nayebi que mobola pe azwaka, po na nini ngai te eeeaaaaah / MBONA SIJUI KIPI KIBAYA NILICHO KUTENDEA, INGAWA BADO NINAYO IMANI KWAMBA, IPO SIKU YULE AMBAE NI MASKINI HUTOKEA KUA TAJIRI, MBONA KWANGU MIMI BADO !!!
Bomengo na sala yo nini aaa , naluka yo na ba boulot, na mo mbongo pe na losambo,/ UTAJIRI KWANI KOSA LANGU NINI ?,KAZI NAIFANYA KWA BIDII,  KAMA NI MAOMBI KILA SIKU NATOA MAHITAJI YANGU.

Yeba ba kati ngai maboko te eee mongongo pe ezali ya Nzambe eeee / JUA YAKWAMBA BADO NINAYO MIKONO YANGU ,NA SAUTI YANGU NI ZAWADI KUTOKA KWA BABA MUNGU!!!

Bomengo ozala ata benja, na yemba yo na loyembo,/ UTAJIRI UNGELUKUA BASI WEWE NI BENJA ILI NIPATE FURSA YAKUKUTUNGIA WIMBO

Lokola Wendo ayembaka Marie Louisa, Kiabukuta ayembaka Babi ii, mbambula ya Koffi Acraaaaame eee. / KAMA VILE WENDO KAMTUNGIA WIMBO MARIE LOUISA, KIAMBUKUTA KAIMBA WIMBO BABII, MBAMBULA IKAIMBWA NA KOFFI OLOMIDE ACRAMEEE

Bomengo ozala ata benja, na yemba yo na loyembo,/ UTAJIRI UNGEKUA BASI WEWE NI BENJA NIPATE FURSA YAKUKUTUNGIA WIMBO

lokola Wendo ayemba Marie Louisa, Kiabukuta ayemba Babi ii, mbambula ya Koffi papa toooop eee. / KAMA VILE WENDO KAMTUNGIA WIMBO MARIE LOUISA, KIAMBUKUTA KAIMBA WIMBO BABII, MBAMBULA IKAIMBWA NA KOFFI PAPA TOOOPE

Nsango ya babia bakobelela na monde entier ahaha / HABARI ZA BABIA ITAZAGAA ULIMWENGUNI KOTE!!!
Nzambe yoka kolela oyo ya bana na yo ooo aaah mama aaa / BABA MUNGU SIKIA KILIO CHA WANAO
kotika te Alise baba amona se pasi iii aaah mama aaa / WALA USIMUACHE ALISI BABA KATIKA SHIDA
Yo moko osala biso Nzambe yaka kotala biso aa ah aa / ALIETUUMBA NI WEWE, BASI BABA MUNGU TUTIZAME
Oooo kotika te le vieux Manzekou amona ba pasiii aah mama aa / USIMUACHE MZEE MANZEKOU KWENYE MATATIZO
Ehh Nzambe yoka kolela oyo ya François Baniota aah mama ee / MUNGU BABA SIKILIZA KILIO CHA FRANCOIS BANIOTA
Nzambe yoka ata kolela oyo ya Lebou Kabuya aa mama eee / BABA MUNGU SIKIA BASI KILIO CHA LEBOU KABUYA
Losambo na ngai bakobele na monde entier aa mama aaeee / MAOMBI YANGU YASIKIKE POPOTE PALE DUNIANI
Bomengo atandele, aa maman aaeee (2x) / UTAJIRI IPO SIKU
Tutu Roba mwana londre papa na … Tokotika Izé bola amona se pasi / TUTO ROBA WEWE AMBAE NI MTOTO WA LONDON, BABA YAKE YA …USIMTUPILIE IZE BOLA NAKUMUACHA ATESEKE
Yo moko osala biso Nzambe yaka kotala biso aa ah aa / ALIETUUMBA NI WEWE, BASI BABA MUNGU TUTIZAME
Kotika te quartier latin bazanga.. / USIIACHE QUARTIER LATIN WAWE KATIKA HALI YA UKOSEFU
Eeee Nzambe yoka kolela oyo ya papa na Rocky iii /  EH MOLA SIKILIZA KILIO CHA  BABA ROCKY !!!
Nzambe yoka kolela oyo ya bana babola eeeehh / BABA MUNGU SIKIA KILIO CHA WANAO WALIO MASKINI
Losambo na ngai nakobelela na monde entier eee /  MAOMBI YANGU YASIKIKE POPOTE PALE DUNIANI
Bomengo atandele, aa maman aaeee (2x) / UTAJIRI IPO SIKU !!! MAMA AAEE !!!

 

L.W.L


HABARI YA MASIKITIKO KWA WAPENZI WA MUZIKI WA RUMBA, MSANII ” BABIA NDONGA CHOKORO ” KAFARIKI DUNIA

October 8, 2014

 

 

Nimeambatanisha na Post hii WIMBO WAKE ” AMEN ” ambao ndio utunzi wake wa Kwanza akiwa na KOFFI OLOMIDE kwenye ALBUM MAGIE.

Taarifa tulizo zipokea tokea Usiku wa kuamkia leo Tarehe 08-10-2014, Bado tulikua tukiifanyia kazi kabla yakuiweka kiwanjani, zaashiria kwamba Msanii Mwanamuziki wa Zamani wa Group Quartier Latin International BABIA NDONGA CHOKORO  kafariki Dunia JIJINI LUANDA ( ANGOLA ),kutokana na MUSHTUKO WA MOYO.

Wengi Wanaambatanisha Kifo chake na kitendo cha JB MPIANA , FALLY IPUPA, FELIX WAZEKWA, kumfungulia mashitaka DADA YAKE CHRISTINE maarufu kwa jina la ” VIEUX KISI NDJORA ” ambae tokea Jana yuko kizimbani kwenye Jela kuu JIJINI KINSHASA ya MAKALA.

Kwa utafiti wetu, yaonyeshakua, BABIA NDONGA, Tayari kawa na Matatizo ya Kifamilia, maelewano yalikua simazuri katiyake na Mkewe.

Usiku wa Kifo chake, Walitokea kua namabishano makali sana yakindoa, yalio sababisha BABIA NDONGA kudondoka  chini na kupoteza ufahamu,.

Wakampeleka kwa Haraka kwenye Hospitali Kuu ya PREDA JIJINI LUANDA ambako umauti ukamkuta.

BABIA NDONGA CHOKORO kajiunga na Group Quartier Latin ya KOFFI OLOMIDE tokea Mwaka 1993, Album yake ya kwanza aliochangia ni ” MAGIE ” Iliotolewa Mwaka 1994.

BABIA NDONGA Kajiondoa kwenye Group hilo Mwaka 2001, Kisha baadae akaja tena kujiunga kwa Mara Nyingine tena na Quartier Latin Mwaka 2003 .

Mwaka 2011, kaamua kujiondoa  Moja kwa Moja kwenye Orchestra Quartier Latin ya KOFFI OLOMIDE na kaanza kujitegemea Mwenyewe Kimuziki.

Baada yakujiengua kwenye Group Quartier Latin, BABIA NDONGA CHOKORO kahamia INCHINI ANGOLA JIJINI LUANDA ambako kaweka Maskani yake.

BABIA NDONGA alikua kwenye Matayarisho ya Album yake ” VRAI MOMENT ” Kutokana na Ukosefu wa Producer wa Uhakika, Ilimjia vigumu kabisa kwa  Album hiyo kutolewa.

Salamu zetu za Rambi rambi ziwaendee Familia yake, Tulimpenda sana ila Mwenyezi Mungu kampenda zaidi.

 

 

L.W.L


VIDEO YA WERRASON KAWASILI JIJINI PARIS LEO

October 7, 2014

 

TIZAMA VIDEO YA WERRASON AKIPOKELEWA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA CHARLES DE GAULE JIJINI PARIS,AKITOKEA MAREKANI.

KAMA TULIVYO WATAARIFU SIKU ZILIZO PITA, WERRASON ANATARAJIA KUONDOKA JIJINI PARIS JUMAMOSI IJAYO AKIELEKEA KINSHASA AMBAKO ANASUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA WAPENZI WAKE.

KWAUKUMBUSHO, WERRASON LE ROI DE LA FORET KAPEWA TUZO MBILI KWENYE SHINDANO LA NAFCA Mjini ((Beverly Hills California). Tarehe 13-09-2014. ( MSANII BORA WA AFRICA,  GENERIC MALEWA IKAPEWA TUZO LA GENERIC  BORA ).

 

L.W.L


%d bloggers like this: