Serikali kuwasomesha mashujaa wa Brazil

July 19, 2008

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akijadili jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. George Mkuchikaijamsikia tena, katika hafla aliyoawaandalia vijana wa Under 17 kuwapongeza.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali itasaidia kuwasomesha wachezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 17, iliyotwaa ubingwa wa Kombe la Copa Coca-Cola nchini Brazil wiki iliyopita. Read the rest of this entry »


Nionavyo mimi

July 18, 2008

Waziri Mkuu Mizengo K. Pinda akifurahia kikombe alicho kabidhiwa na nahodha wa timu ya Under 17 Hamid Mao, Timu hii iliwakilisha taifa kwenye michezo ya Kimataifa ya Copa Coca Cola jijini Rio De Janeiro Brasil, anayetazama kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. George Mkuchika, (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kitendo cha vijana wa timu ya Under 17 ya Copa Coca cola kuchukua Kombe la mashindano ya Kimataifa ya Copa Coca Cola tena nchini Braziri na sio tuu kuchukua kombe bali kuzifunga timu nguli kwenye mchezo wa soka ni cha kishujaa na cha kupongezwa na kila mpenda soka.

Vijana hao ambao si tu wamechukua kombe kwa ujumla bali wamechukua na vikombe vingine ikiwa ni kile cha kombe la mashindano hayo, kombe la golikipa bora, mchezaji bora na kombe la mfungaji bora ambayo kwa kiasi kikubwa ni mafanikio kwa timu kama timu na Taifa kwa ujumla.

Tumekuwa tukilalamika kwa siku nyingi kuhusu mafanikio mabovu ya Timu yetu ya Taifa na wadaiu wengi wa soka walikuwa wakipendekeza kuundwa kwa timu za watoto wadogo ambao baadaye watalisha timu ya wakubwa ambayo ni Taifa Stars kwa ajili ya kuiwakilisha nchi, kwa mujibu wa habari toka kambini mwa klabu hiyo zinasema Vijana hao walionyesha uwezo mkubwa na kumchanganya kocha Mbrazili Carlos Perreira aliyekuwa akisimamia kambi hiyo na kusema ana imani vijana hao wanaweza kufikia kushiriki michuano ya Kombe la Dunia lamwaka 2014 endapo wataendelezwa. Hili sio ombi watoto wameonyesha wanaweza serikali isimamishe timu yetu ya Taifa kwa michezo kwa muda fulani na kujikita zaidi kwa vikosi kama hiki kuipa msaada na kuindeleza, Leo hii wadhamini tunao wengi hatuna sababu ya kufanya vibaya, ni kubadilika tuwe na msimamo wa kusema tunatengeneza timu kwa ajili ya CAN 2010 na baadaye tucheze kombe la dunia. Nimesoma mkakati wa India wa kucheza kombe la Dunia 2018 ambapo wanatengeneza kikosi kwa sasa, nani anaijua India kwa mpira kama si Kriketi? iweje sisi walao tuko kwenye ramani ya soka ingawa “chenga twawala lakini watufunga?”

Haitoshi kuwapeleka hawa vijana Bungeni na wakapigiwa makofi tutaishia hapo tunampango gani nao? Kocha wa timu ile aongezewe nguvu watoto waingizwe kwenye mpango maalumu na tuwajenge wawe ndio timu ya Taifa ya kesho tukiwa na lengo maridhawa la eidha kucheza kombe la mataifa kwa kuwatumia vijana hawa.

Tanzania ilizishinda nchi za Argentina (2-0) na Peru (5-1) na kutoka sare na Chile (0-0) na kuingia nusu fainali ambako iliishinda Paraguay (3-1).

Katika fainali ilikutana tena na Chile na kuibwaga kwa bao 1-0. Timu hiyo ilikabidhi kombe kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Wachezaji waliokuwemo katika msafara huo ni Kabari Faraji Swaleh, Mohamed Aziz Hussein, Ahmed Mohamed Chimpele, Sadik Gwaza Twabu, Adili Adam Sambiro, Kenny Ally Mwambungu, Himid Mao Mkami na Faraji Hamad Hussein.

Wengine ni Lambele Jerome Ruben, Karim Sule Suleiman, Zahoro Jailani Ismail, Jukumu Kibanda Joackim, Dotto John Greyson, Joseph Petro Mahundi, Hemed Suleiman Mohamed


%d bloggers like this: