Soleil Wanga alia na Binti wa Denis Sassou Ngueso

Purukushani ni kubwa sana kwa wanamuziki wa Congo hasa kizazi cha tano  ambacho kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakali sana kwenye nyimbo za taratibu. Soleil Wanga sio jina maarufu ni lazima uwe mfatiliaji wa muziki wa Congo ndio unaweza kumjua jamaa huyu, Binafsi yangu namkubali sana na huwezi amini huyu jamaa kwa East Africa huyu bwana Agenti wake ni Mamaa Sophia Kessy, binti mdogo Mtanzania anayefanya kazi na Clouds Media.

Wimbo huu Soleil Wanga kama walivyo akina JB Mpiana, Werrason, Koffi na hata FAlly Ipupa amemuimbia Binti wa Rais Denis Sassou Ngueso anayejulikana kama Cloudia Sassou (Pichani juu) ambaye kiwadhifa ni Waziri wa Elimu, Binti huyu mwanadada mrembo ni shabiki mkubwa wa Muziki wa Congo na mara kwa mara amekuwa akialika na kudhamini show kadhaa za wanamuziki hawa nchini wake.

Ni rahisi kuwa wa kwanza ila ni kazi sana kuendelea kuwa wa kwanza, Muziki wa Congo unategemea na nyota, inaategemea na nyota yako imeng’aa vipi kwani kama kuimba mi naimani kabisa Ferre Gola anaimba zaidi ya Fally Ipupa lakini Fally Ipupa ni maarufu na anapendwa zaidi kuliko Ferre, huo ni mtazamo tuu.

Msikilize Soleil Wanga kwenye kipande hiki Bougie en ambacho amekiimba kwa umaridadi mkubwa sana, shukrani za Kipekee kwa Swaiba wangu Husna Hamis Renee De Afrique Pride Fm Mtwara na Suveree big up kwenu, Bahati wa Moshi FM Radio. tuko pamoja.

 

ugie en

Advertisements

One Response to Soleil Wanga alia na Binti wa Denis Sassou Ngueso

 1. Papa Richard Malewa says:

  Kwa bongo hapa mtu aliyetembelea nyota ya Soleil Wanga alikuwa ni Mzee wa Kimara Jose Mara alimranda kwa kila kitu.

  Utasikiliza wimbo Fulani anaigiza kama sauti ya gari inowasha taaaah Nye nyee nyeee heeee! Jamaa alikuwa choka mbaya kweli kweli.

  Fere Gola tatizo lake alivyotoka kwa Werrason na kwenda kuanzisha Marquise Wenge na akina Bill Clinton na baada ya bendi yao kudumu kwa muda mfupi ingawa walishinda zawadi ya kora ingawa huku Tanzania Enzi hinzo Twanga na TOT na Academia walikuwa wanapewa shavu na vyombo vya habari hakutakiwa kwenda kwa Koffi.

  Mbaya zaidi baada ya kutoka kwa Koffi alitaka kupambana na Master wake Werrason kwa Masebene sehemu ambayo kwa Werrason ni ngumu sana kum-beat.

  Ila sasa nachofurahi amejijua yeye ni wapi na sehemu yake. Nafurahi sana ataweza kuliziba pengo la Madilu system (R.I.P) kwa Rhumba za ukweli halafu anamalizia kwa sebene Fulani ambazo inaendena na Rhumba zake.

  Muda si mrefua atajulikana kama King of Rhumba in DRC.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: