Kidiamfuka; Utunzi wa El dorado uliombeba Fally Ipupa

April 9, 2014

Kwa wapenzi wa Fally Ipupa wimbo huu Kidiamfuka ni mmoja wa nyimbo zilizompa nafasi na chat mwanamuziki huyo. Kiukweli Wimbo huu wengi wetu tulidhani ni utunzi wake Fally Ipupa ilihali wimbo huu mtunzi halisi ni El Dorado ambaye pia ametunga wimbo 100 kilos wake FERRE GOLA na Detresse ambao awali ulidhaniwa ni wa Mimiche Bass, sikiliza wimbo huu kisha nipe maoni yako.


Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema wa Wenge

April 9, 2014

Ingawa wimbo huu maarufu toka kwa Wenge ya JB Mpiana unajulikana kama utunzi wake JB Mpiana kiukweli kabisa Wimbo huu ni utunzi wake kijana machachari Zulema ambaye ni bonge la kipaji ambacho kiukweli kwangu naona kinapotea.

Zulema ni muimbaji mzuri ambaye kwa kipidi kirefu amekuwa akisumbuliwa na uteja kwa utumiaji wa madawa ya kulevya. JB Mpiana aliamua kumsaidia Zulema kama mdogo wake na kuna kipindi alipelekwa kwa wataalamu na kupatiwa ushauri nasaha ana alitangazwa kuacha matumizi ya madawa hayo.

Mwanamuziki Zulema wa wenge bcbg ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu ambacho kilivumbuliwa JPS PRODUCTIONS ambao walimpeleka wmmm ya werrason ambako alifanyiwa interview na mtaalam wa vocal wa WMMM wakati huo FERRE GOLA na kufuzu vizuri interview hiyo ila tatizo likawa alikuja kugundulika kwamba licha ya kipaji cha sauti alichonacho anakabiliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyowafanya wmmm wasite kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuamua kumpeleka kwenye bendi yao ya pili iitwayo OPERATION DRAGON, Ndipo Jules kibens wa bcbg ambae waliwahi kupiga pamoja zamani Folk Stars alipokwenda kumshawishi JB Mpiana wamnyakue ZULEMA kwa kuwa ana kipaji.

Nakutakieni siku njema, Post hii imerudiwa kwa heshima ya Ndekwa Mwana Bebg nakati ya Dare salaam hesmima mingi kwako Mukulu wa Bakulu, Gilbert wa Mikumi Pamoja sana, Mamaa Gladys, Papaa James Maselle, heshima kwako, Mwambungu nakati ya Tunduma, Steve BCBG pamoja mzazi, Frank Le Jeebeenique, Mukulu Hadji Le Jeebeenique miss u brother.


President de Taut le Chegee; Jukwaa moja na Shaggy

April 9, 2014

Kuna mahali panafika mashabiki wanapenda ladha tofauti na ndio maana wanamuziki wengi wa Congo kwa sasa wamekuwa wakichanganya na kushirikisha vionjo tofauti ili kuleta ladha tofauti na kutanua wigo wa mashabiki wao.

Werrason ambaye anapendwa sana hasa na vijana amekuwa akijaza sana kwenye show zake huko Congo, huku ngome yake kuu ikiwa kitongoji cha Bandal (hii ni mahala kama Kinondoni) huko watoto wote wa mujini wanapatikana mwenyewe anajiita President de Taut le Chegee – Rais wa Machokoraa na wenyewe wanampenda sana, kiufupi ni mtu wa watu wote matajiri mpaka masikini. Angalia hapa Tamasha lililoandaliwa na Vodacom huko DRC akiwa jukwaa moja na Shaggy.


Koffi vs Youssou Ndour: Mabingwa wa sauti jukwaa moja.

April 9, 2014

Koffi ametangaza kuachana na muziki baada ya kutoka kwa Albamu yake ya 20 ambayo itatoka siku yoyote. Amefanya kazi hii kwa mafanikio akifanikiwa kuinua bendi hata pale ambapo wanamuziki wote karibia waliondoka na kutangaza kikosi kipya, akiwa amefanya Kolable na wanamuziki wengi wa ndani na nje ya Congo DRC.

Hebu sikiliza hiki kipande tu alipopanda jukwaani huko Grand Hotel na mwanamuziki Youssoun Ndour wa Afrika ya Magharibi.


“Mayi ya Pembe” Beach maarufu yenye historia kwa wanamuziki wa Congo

April 9, 2014

Huwa nawatania marafiki zangu wa Congo laiti kama wangekuwa na Beach kama tu za kwetu sijui ingekuwaje maana hiyo Planet Sono Beach (Mayi ya Pembe) ni sehemu tu maji yametuama pembezoni mwa mto, ni eneo liko nje kidogo ya mji wa Kinshasa kama unaelekea Airport kwa wanaoijua Kinshasa, Ukiangalia haina chochote cha kuvutia ila vurugu zake ni balaa kila mwanamuziki mkubwa ameshapiga huko na sio mara moja. mara nyingi show zao huanza mchana watu wakila na kunywa na kuendelea mpaka lyamba.

Hii ni show ya JB Mpiana akiwa na Wenge BCBG huko Planet Sono Beach Mayi ya Pembe. matamasha mengi ya wanamuziki wa Congo hufanywa hapa yakiandaliwa na kudhaminiwa na makampuni makubwa ya vinywaji kama Primus ambao ni wadhamini wa JB Mpiana, Skol ambao ni wadhamini wa muda mrefu wa Koffi, Tigo na wengineo.

Ni show ambazo zinatia raha kuangalia kwani kuna kuwa na kila aina ya shamrashamra na watu wanajiachia sana kwani hakuna kiatu kirefu (mchuchumio) wala kuogopa kutoka jasho, wengi wa washabiki huwa wamevaa beach wear au smart casual tuu kwani wako beach.


%d bloggers like this: