Twanga Pepeta Chalii!!

February 8, 2011

.

Ally Choki (wa pili kushoto mbele) akiwa na wanamuziki wake wapya leo baada ya kuwatambulisha mbele ya waandishi wa habari. Mbele kulia; ni God Kanuti, Super Nyamwela, Super Danger, Rogert Hegga, Saulo John ‘Ferguson’ na Hoseah Mgohachi.

Mashabiki wameonyesha wasiwasi wao kutokana na wimbi la wanamuziki wa Twanga Pepeta kutimka kwenda bendi nyingine.

Wakizungumza majuzi baada ya tetesi na hatimaye habari kuthibitishwa kuwa wanamuziki watatu wameondoka kwa pamoja ambao walikuwa moja ya nguzo ya bendi hiyo.

Wanamuziki waliiondoka ni pamoja na God Kanuti, Super Nyamwela, Super Danger, Rogert Hegga, Saulo John ‘Ferguson’ ambao kwa kiasi fulani walikuwa wanaibeba bendi hiyo na sasa wamejiunga na Bendi ya Extra Bongo.

Wanamuziki hao wemeenda bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Kamarade Ally Choki “Mzee wa Farasi” ambaye aliwahi kung’ara sana akiwa na Twanga Pepeta. Kadhalika huu utakuwa ni muhimili muhimu kwa bendi ya Extra Bongo ambayo imekuwa ikizidi kujizolea umaarufu siku hadi siku kutokana na kuwakuna mashabiki wengi, alipoongea na kituo cha redio moja ijumaa iliyopita pamoja na mambo mengine Ally Choki alinukuliwa akisema kuwa mahusiano yake na mmiliki wa Twanga Pepeta Asha Baraka si mazuri sana kwa siku za karibu ingawa hakufafanua zaidi.

Akizungumza jana kabla ya kuwatambulisha wanamuziki hao, Choki amesema sasa ni zamu ya bendi yake kulikamata jiji, hivyo aliwaomba mashabiki wake wakae tayari kuipokea Extra Bongo mpya.

Wanamuziki hao ni:  Issack Buriani  ‘Super Danger’, Saulo John ‘Ferguson’, Rogert Hegga ‘Caterpilar’, Otilia Boniface ‘Kandoro’ na Hassan Musa ‘Nyamwela’.

Ikumbukwe kuwa Asha Baraka awali alichukua wanamuziki toka bendi hii ya Extra Bongo jambo lililopelekea kufa kwa bendi hii ambayo kwa wakati ule ilileta upinzani mkubwa sana kwa Twanga Pepeta. Aidha mashabiki hao walionyesha kufurahishwa na Ally Choki kugangamala kuiongoza Bendi na kumsifu alivyoiimarisha kwa sasa.

“Tunahitaji kuwepo na bendi nyingi pinzani sio kila siku Twanga Twanga, Asha hawezi kukubali kuona wengine wanachanua atawanunua na kuhakikisha haifiki mbali we utaona…” ling’aka shabiki mwingine alipokuwa akichangia mada.

“Hili ni pigo kwa Asha Baraka kwani bado ana uguza kidonda cha kuondokewa na kiongozi na mpiga drum mkongwe wa Twanga Baba Diana ambaye alifariki hivi karibuni kwa ajali ya pikipiki” alisema mshabiki wa Asha Baraka ambaye alikataa jina lake lisiandikwe.

Habari pia zinasema Asha Baraka amemrejesha mpiga solo mahili ambaye aliwahi kuwemo kwenye bendi hiyo Adolph Mbinga baada ya mpiga solo wake naye kuihama bendi hiyo, Mbinga ambaye pia alitamba na bendi ya Mchinga Sound anatazamiwa kuleta chachu kwendye bendi hiyo ambayo pia imemrejesha Khadija Mnoga “kimobitel” ambaye awali alikuwa Extra Bongo kabla ya kujiunga na Twanga tena.


Aisha madinda: Sijastaafu unenguaji Twanga…

September 19, 2008
Picha ya zamani ya Maktaba ambayo inamuonyesha Michuzi akiteta na Aisha madinda

Picha ya zamani ya Maktaba ambayo inamuonyesha Michuzi akiteta na Aisha madinda.

Mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta Aisha Mbegu aka Aisha Madina, jana ameongea na Bloga Muhidin Michuzi kwa kile Michuzi alichotaka kupata uhakika wa habari za uamuzi wa kuacha unenguaji na kujishughulisha na biashara, habari ambazo zilipamba vyombo vya habari siku mbili hizi.

Katika majibu ya tuhuma hizo Aisha alimwambia Michuzi kuwa hafikirii kuacha unenguaji kwa sasa na ni bado mnenguaji wa Twanga, hata alipoulizwa iwaje Twanga wako Nairobi kwa sasa na yeye yuko Dar? Aisha alijibu kuwa aliomba ruhusa kupumzika kwani pamoja na mambo mengine yuko kwenye mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Awali ilidaiwa kuwa Aisha alitangaza kujiuzuru rasmi unenguaji na kujihusisha na biashara (gonga hapa uisome) jambo ambalo yeye anasema liliripotiwa na kituo  kimoja cha Television ambacho yeye hakuwahi kufanya nao mahojiano yeyote na baadaye kuripotiwa a gazeti moja la kila wiki ambalo lilinukuliwa na vyombo vingine yakiwamo magazeti tando.


Twanga kupagawisha Kenya tena!

September 17, 2008
Aisha Madinda wa Twanga Pepeta

Aisha Madinda wa Twanga Pepeta

BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars International, maarufu Twanga Pepeta imealikwa kwa ziara ya onyesho maalum jijini Nairobi, Kenya.

Ziara hiyo imetolewa na taasisi ya kimataifa ya African Economic Research Consortium yenye makazi yake Nairobi.

Onyesho hilo ni kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo nchini humo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (Aset) inayomiliki bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa wakiwa Kenya, Twanga watafanya maonyesho mawili kwenye ukumbi wa Intercontinental na katika ukumbi wa hoteli ya Carnivore.

Alisema kuwa mbali na maonyesho hayo mawili yatakayofanywa na bendi yake, pia watatumia fursa hiyo kutambulisha nyimbo mpya zinazotamba hivi sasa katika vituo mbalimbali vya redionchini.

Alizitaja baadhi ya nyimbo mpya zinazotarajia kupigwa na bendi hiyo kuwa ni Sumu ya Mapenzi, Nazi haivunji Jiwe.


%d bloggers like this: