Queen Suzy

February 7, 2009

IMG_1771Anaitwa Queen Suzy “mamaa Tenterente” Mcheza show wa wana Mkorogo.


Wamkumbuka Maneno Uvuruge?

February 7, 2009

Maneno Uvuruge akishikilia mpini wa Solo

Jina la Maneno Uvuruge wengi tumelisikia siku nyingi kwenye bendi tofauti hasa enzi za Vijana Jazz ila kwa sasa Maneno Uvuruge yuko na wana Kilimanjaro Cionnection Band wazee wa Mkorogo waliko ziarani Kula Lumpur Malaysia. Uvuruge ameshapiga na wanamuziki na Banana Zoro, Machozi Band na pia ameshuiriki kwenye kurekodi nyimbo nyingi ambazo amekuwa kama mwanamuziki mwalikwa.

Uvuruge amevutia mamia ya mashabiki kwa umahiri wake wa upigaji gitaa na si hivyo tu bali Maneno Uvuruge ni muimbaji mzuri sana, Binafsi namkubali sana jamaa ametulia ile mbaya, rafiki yangu MJ anasema ukimuona uvuruge barabarani huwezi mtambua kama ni mwanamuziki na sura yake ya upole, any way ni mtazamo tuu.

Pata kipande cha wimbo wa Dunia tunapita toka kwa Wana Kilimanjaro Connection waliko ziarani Malaysia na hii ilikuwa kwenye ukimbi wa Rum Jungle ambapo wanapiga jumatatu hadi jumamosi, habari njema jamaa wataendelea kuwepo hadi mwezi wa tano inshallah.

Kilimanjaro Connection ambayo kwa kiasi kikubwa inaongozwa na wanamuziki hodari kama Kanku Kelly mwenyewe anayeimba na kupiga Konga, Trampet na ala nyingine, pia yumo Faijala Mbutu huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta, hali kadhalika kuna Maneno Uvuruge  “Diblo Dibala” anayepiga gitaa la solo, huyu bwana hupagawisha watu kwa umahiri wake wa upigani solo na jinsi anavyomchezesha mwanadada Queen Suzy, Wengine ni Geofrey Kumburu anayecheza Keyboard, Sijali Moris ambaye anapiga Drums kama Papito Mbala bila kuwasahau wataalamu wa sauti Delphine Mununga na Modester Nyoni.

Bonyeza player upate mambo.

Delphine Mununga  mtaalamu wa sauti

Mashabiki wakiserebuka ndani ya ukumbi wa Rum Jungle ambapo Kilimanjaro Connection wanapiga.

Queen Suzy mamaa tenterente akipagawisha na mauno jukwaani, Binti huyu aliwahi kujumuika na bendi tofauti tofauti ikiwemo Wazee wa Ngwasuma kwa sasa anampa tafu Mzee mzima Kanku Kelly.

Mashabiki wakibanana kucheza Mkorogo wa Kilimanjaro Conecction Band usiku wa jana.

Baadhi ya vijana wa kitanzania wanaoishi Malaysia Jimmy(L) na Xslim(R)  wakiwa ndani ya ukumbi wa Rum Jungle kuwapa Shavu Kilimanjaro Connection.

DSC00182

Mamaa Suzy akiwajibika jukwaani.

Mashabiki wakiserebuka ndani na kupekecha we acha tuu kaa nyumbani yaani!!

Mj akiwa na Jimmy wakiwapa support wana mkorogo ndani ya Rum Jungle Kuala Lumpur-Malaysia.


Kilimanjaro Connection waendelea kutesa

January 26, 2009

.

.

Mwanadada Queen Suzy (kwa wale wapenzi wa Ngwasuma watakuwa wanamtambua uzuri) akiwapagawisha wamalay kwa mauno na jinsi alivyo mlaini. Queen Suzy kwa sasa yuko na Kilimanjaro Connection kwenye ziara yao hapa Malaysia ambapo wanapiga ukumbi wa Rum Jungle.

.

.

Maneno Uvuruge mzee wa Gita la Solo akikung’uka solo kumpagawisha Queen Suzy ambaye kwa kiasi kikubwa amezikonga nyoyo za mashabiki na kufanya Klabu ya Rum Jungle kufurika kila siku  ambapo Kilimanjaro Connection wanapiga kila siku isipokuwa siku ya Alhamisi tu.

.

.

Bango la wana Mkorogo The Kilimanjaro Connection kama linavyoonekana kwa barabarani.

.

.

Kilimanjaro Connection wakiwa kazini, uhodari wao wa kuimba nyimbo za mataifa mbali mbali ikiwamo Kiswahili, Kihindi, Kiingereza, Kiispaniola na hata Kimalay umewafanya kuwa maarufu jijini Kuala Lumpur na kufanya maonyesho yao kuongezwa na kuwa kila siku isipokuwa siku ya Alhamisi tuu, hii itakwenda sambamba na kuongezewa mkataba na Meneja wao ambako kwa sasa wataendelea kuwepo Malaysia kwa miezi mitatu zaidi.

Kilimanjaro Connection ambayo kwa kiasi kikubwa inaongozwa na wanamuziki hodari kama Kanku Kelly mwenyewe anayeimba na kupiga Konga, Trampet na ala nyingine, pia yumo Faijala Mbutu huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta, hali kadhalika kuna Maneno Uvuruge  “Diblo Dibala” anayepiga gitaa la solo, huyu bwana hupagawisha watu kwa umahiri wake wa upigani solo na jinsi anavyomchezesha mwanadada Queen Suzy, Wengine ni Geofrey Kumburu anayecheza Keyboard, Sijali Moris ambaye anapiga Drums kama Papito Mbala bila kuwasahau wataalamu wa sauti Delphine Mununga na Modester Nyoni.


%d bloggers like this: