Rachereau Tabu Ley afariki Dunia

November 30, 2013

image

Marehemu Tabu Ley enzi za Uhau Wake
image

Pichani Marehemu Tabuley akiwa kitandani Hospital huko Bruxelles.

Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Racereau au Tabu Ley amefariki Dunia leo asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa toka chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Tabu Ley amefariki Dunia leo asububi huko Bruxelles Ubelgiji.

Tabu Ley aliwahi kutamba sana na hasa kipindi alichofunga ndoa na Mbilia Bell ndoa ambayo ilivunjika baada ya muda.

Katika uhai wake Tabu Ley aliwahi kupiga Zingzong na wanamuziki kadhaa na kufanya maonyesho ya pamoja na wakongwe kama Koffi Olomide ambaye aliwahi kufanya onyesho la wazi (Live Concert) akiimba nyimbo za Tabu Ley (Koffi Chante Tabu Ley).
Kibao maarufu kilichotamba mpaka sasa ni Muzina ambao unatamba mpk wa leo.

Pia kuna wimbo kama Twende Nairobi ambao aliimba na Mbilia Bell. Mpaka kifo chake Tabuley alikuwa ametunga zaidi ya 200 na anasemwa ndio mwanamuziki wa kwanza wa Afrika kuuza nakala milioni moja kwa Single Albamu.

Tabuley aliwahi ingia matatani na Aliyekuwa Rais wa Zaire enzi hizo, ugomvi uliosababisha gwiji huyo kuishi uhamishoni.

Tutawaletea taarifa kadri tunavyozipata. Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.

Tafsiri ya Nobless Oblige ya Koffi Olomide

November 29, 2013

Kuna wanamuziki ambao kwa ukweli wameweza kukaa kwenye chati katika kipindi chote tangu wameanza muziki, Koffi Olomide ni mmoja wao ambaye tangu ameanza amezidi kuwa juu na anazidi kupanda, ameapa kujiweka kando na muziki ifikapo mwezi huu baada ya kuzindua albamu yake mpya ijayo.

Naomba nikukumbushe wimbo huu wa Nobless Oblige katika albamu ya Papa Plus kama sikosei (naomba kukumbushwa) ila huu umetoka maktaba ya Papa Mwambungu Presidaa nakati ya Tunduma. kama unachocha kuongezea unakaribishwa.

NOBLESSE OBLIGE

(Kaizari mpe yake)

Koffi Olomide

Kofi ana nong’ona Kwanza.

Biso tozelaka oyo ya Nzambe…. Nayembelakaaa

Tuna bango nano, George Lukundi Meriko, mais bakeyi na ngai wapi ko?

Basukisa ngai wana

Basalaka koni na nzete ya bitabi te….Papa plus plus 5/5

Sisi huwa tunasubiri riziki ya mungu…. Nilishaimba

Hebu waulize kwanza, George Lukunduki Meriko, wamenipeleka wapi?

Wakome waniache hapo.

Huwezi kujipima urefu na mgomba…… Baba ya mababa tano juu ya tano

CHANTEL AWA: Imba Hapa

Kumisa ngai ngambo te, mabe eza yango

Ndeko kopesa ngai faute te oo yo moko olukaki esakanaka na lavie

Lelo omessa pe E suffit moto x 2

Usinivike lawama, ubaya ni wako.

Ndugu usinipake kosa mwenyewe ulitaka kucheza na maisha.

Leo umeharibu, basi mwenzangu

1. Na bolingo ya biso kaka yanga bapasi ekoka ee

Lukela ngai mindondo te yo moko opanzaki ngai

Okeyi otuli Nzambe aza na importance moko te

Mbongo moke na pongi ee nani yango okokosa

Osombi ngai partout ee okomi na suka

Liwa etikali mosika

Ebale nyoso eza na ngandu na yango

Katika upendo, shida zangu zimetosha.

Usinitafutie kasheshe mwenyewe ndiye umenitangaza

Umewayawaya umechoka ukifikiri Mungu hafai hata kidogo.

Hizo hela za usingizini nani utamuongopea.

Unaninunia sehemu zote, sasa umefika mwisho

Kifo kipo mbali

Kila mto una mamba wake

2. Ngai, boina ngai, nayebi tout wana eyebani nanu

Esumu nini ngai nanu nasala po bomema

Po makila epola e nasuki zombie mawa ya tout

Mingi vraiment nasala bakondima ngai ata un jour ayee

Nyoso nzambe asala

Kopesa ngai faute te, chance elukaka na Nzambe tata na Yesu

Nafahamu vema kwamba huwa mnanichukia, na kila mtu anafahamu hivyo

Nimefanya dhambi gani mpaka mnibebe putaputa

Damu yangu imeoza nakauka natia huruma

Mengi niliyoyafanya yatakubaliwa hata siku moja baadae.

Kila kitu kilifanywa na mola

Usinilaumu, bahati huwa inatoka kwa mola baba wa Yesu.

Ye moko apesaka moto oyo ekoki naye

Oyo bokomi kosala nayebi ekosuka na mayi

Oyo bosali ngai lelo ngai napesi se merci

Kidingi dingi zero ekati loboko te Nzambe

Mwenyewe ndie humpa mtu yanayomtosha

Vitimbi vyenu najua vitaishia kwenye maji

Mnachonifafanyia leo nawashukuruni

Potelea mbali na upuuzi huo haunikati mkono, Mungu

3. Boye bo okosa Kinshasa nayebi ekosuka at na mayi

Oyo bofingi ngai lelo, ngai nalali se pamba

Kidingi dingi zero, echanger ngai nzoto te vraiment

Jinsi Mnavyodanganya mjini Kinshasa najua uzushi utaishia kwenye maji

Jinsi mnavyonitusi leo mimi naona si bure

Potelea mbali uzushi huo hautabadilisha mwili wangu

Boni bokomi kobunda ngai tongo nanu etana te

Boni bokomi koluka kobomba ngai na kati ya moto

Boni bokomi kofunda ngai bolingi te moi azala te

Bolingi pasi soki esika ngai epai na bino esengo

Ngai nalela papa ngai nalela mama aaah

Mbona mnanipiga vita wakati hata hapajakucha

Mbona unataka kunipiga Bomu kichwani

Mbona mnanisakama kwa kunisema bila kuwepo shahidi

Mnataka shida inielemee na nyie muwe na raha

Nalia baba nalia mama aaah

Scola:

Yahwe ee, Talaa bango, bango banguna, bato oyo okela

Bazala aa, po baleyi, batondi, balobi yo ozala teee

Mola aa waone hao, hao wapumbavu, watu uliowaumba

Ili wawe, wamekula, wameshiba, wanasema ati wewe haupo.

Sangu

Amuvila muyaya Eeh eeeh

Amuvila muyaya mawee iieeh KOFI OLOMIDE

Padri

Sikieni huu USIA

Sikieni huu USIA

1. Elengi munange mwiyebirika /Sangu X 2

Botuna kawala biso towelaka Te

Nasali eloko Te

Ni furaha/vizuri mkija tuungane/ Padri

Muulizeni Kawala sisi hatuna ugomvi

Sijawafanya kitu

2. Aa bodingi tongi lobi mingi na kombo na ngai ko x 2

Oh ngai natali pamba pa namesana na ngai kofingama

Oh ngai natali pamba mamani nanu azali pene

Ngai nazali tonga moke jamais soso akoki komela ngai

                Aa mnatapika matusi na kashfa dhidi ya jina langu

                 Yote bure nimezoea kutukanwa

                Nona yote bure maanani yuko karibu yangu

                Mimi ni sindano ndogo kuku hawezi kamwe kunimeza

3. Elengi munange mwiyebirika /Sangu X 2

Botuna kawala mukwetere mulimanga wowowowo mami nga nabuna

Jalousie nde a basi

Ni furaha mkija tuungane/ Padri

Muulizeni Kawala mzozo haufaidi wowowowo mama nakufa

Acheni wivu

4. Muli twana twa Zaire bampangi kwati bulangombe yaya

Biso tozalaka oyo ya Nzambe kwiyungui mukeleke yaya

Luki pe na mosala te Nzambe katange wa mungwe baza bazili

Sisi sote watoto wa Zaire, ndugu mbona tunakulana nyama jamani

Tumemkabidhi mungu maisha yetu mtindo huo hatuuwezi jamani

Hatushughuliki na kazi zetu ipasavyo, mola ametukataa kama wehu

Rap:

Moto, moto, abayangula abatika

Kinshasa moto, na Poto malili, Kinshasa maloba

Talaka mambe, Ee mundu talabake, Ekubina cent, Ekubina deux cents

Moto, moto, unaunguza, haunusuru

Kinshasa moto, Ulaya baridi, Kinshasa ngebe zimezidi

Ona mambo, yanavutia kila mtu, tukicheza mia, tukicheza miambili

Fally Afanya kweli Abidjani

November 21, 2013

Katika muendelezo wa Fally Word Tour 2013, Mwanamuziki Fally Ipupa weekend hii alikuwa na onyesho huko Abdijan Cote Devoir. Ikumbukwe kuwa Abidjani ni moja ya ngome za wanamuziki wa Congo ambao wanapendwa sana huko.

Fally ndiye mwanamuziki wa Congo anayeongoza kwa kuwa na show nyingi kwa mwaka huu akiwa booked mwaka mzima kwa show za nje ya Congo. Maanamuziki huyu ambaye ni kipenzi cha wadada “Sukari ya Warembo” kwa sasa anatamba na albamu yake ya Power 101 yenye nyimbo kama Sweet Life ndani yake ambazo zinatamba vilivyo.

Ziara hii ya Fally ambayo itahitimishwa huko Dubai mwisho mwa mwaka huu imepewa jina la Power Tour 2013 ambapo atatembelea nchi sio chini ya saba, jambo linalomfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi za nje kuliko wote wa Congo kwa mwaka huu.

Fally Ipupa akiwasili kwenye ukumbi/Uwanja kufanya Sound Check kabla ya onyesho jioni yake.

MAshabiki wakishangilia huku wengine wakichukua kumbukumbu na simu zao za mkononi onyesho likiendelea.

Safu ya Wanamuziki wa Kiume wa Fally wakionyesha umahiri wao wa kucheza Power 101.

Baba Yuko kazini

Ukisikia Muziki si lelemama angalia hii ndio utajua.

Ni kawaida wanamuziki kubadili mavazi kila baada ya kuda fulani kwenye onyesho moja kunaongeza utamu, uhai na vionjo kwenye onyesho husika, Pichani Fally akiimbisha mashabiki moja ya nyimbo wazipendazo.

Allain Mpella kupiga na Wenge BCBG Zenith Dec 21?

November 19, 2013

Allain Mpella Afande

Kuna tetesi kuwa Allain Mpela akawemo kwenye jopo la wanamuziki ambao watatumbuiza Zenith Jumamosi ya Dec 21 huko Zenith.

Katika interview na kituo kimoja cha Television wiki iliyopita Afande Mpela ambaye aliwahi kutamba vilivyo na kundi la Wenge BCBG alisema kuwa akipata mualiko wa kushiriki toka kwa aliyemuita kaka yake JB Mpiana angependa kushiriki, “…nitashiriki bila tatizo kama Rais kaka yangu JB Mpiana ataniomba nifanye hivyo….” alisema Mpella.

Afande atakumbukwa daima kwenye onyesho la Zenith miaka takribani 15 iliyopita jinsi alivyokonga nyoyo zamashabiki akishirikiana na kina Titina Al Capone , Tutu Caluji , Aimelia Demingongo , Chai Ngenge , Seguin Mignon ambao kutoa Seguin hao wengine kwa sasa hawapo kundini.

Licha ya kuwepo na mikwara ya hapa na pale ya kutokuwepo kwa onyesho hilo bado mashabiki mamia kwa maelfu wanalizungumzia onyesho hilo hasa baada ya kukosa utamu huo kwa takribani miaka minne na ushehe.

wakizungumza juu ya ushiriki wa Mpella mashabiki mbalimbali walimtaka JB Mpiana kumhusisha nguli huyo hasa baada ya bendi hiyo kuondokewa na vinara wake ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa na na mchango mkubwa kwenye bendi hiyo. “akitaka awashike amchukue Mpella maana yule ana mashabiki wake na hasa akina dada wanampendaga sana” alisema Julie Westone Mcongoman anayeishi Tanzania alipozungumza nami mbali tu kuwa ni shabiki wa Mpiana anaimbwa sana na nguli.

Kwa upande mwingine inasemekana kuwa Allain Mpella anataka kutumia nafasi hiyo kujisafisha mbele ya mashabiki hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa bendi yake iko mazoezini huko Makanza Ngiri Ngiri kwa ajili ya uzinduzi wa albamu yake mpya.

Nakuonyesha Zenith iliyopita umuone mpella akifanya vitu.

Mwanamuziki wa FM Academia Afariki China kwa Unga, Wa Akudo akamatwa nao.

November 18, 2013

Marehemu Aristote Shungu Papa Tee enzi za uhai wake

Rapa wa Bendi ya Akudo Impact ‘Wazee wa Masauti’, Kanal Top Ambaye amekamatwa na Unga (pichani).

Habari zilizotufikia zinasema kuwa Mwanamuziki mahiri wa bendi ya FM Academia Alistoti Shungu amefariki dunia nchini china. Kwa mujibu wa mpashaji habari wetu anasema kuwa Marehemu Shungu ambaye wimbo wake ulitazamiwa kupigwa kuanzia leo kwa ajili ya kuitambulisha albamu mpya alifariki wiki iliyopita huko China alipokuwa amekwenda kibiashara.

250509

Marehemu Shungu enzi za Uhai wake akiwa na Presidaa Nyoshi.

Kwa mujibu wa habari inasemekana Aristoti Shungu ambaye alikuwa muimbaji na mtungaji amefariki baada ya Madawa aliyokuwa amebeba kupasuka tumboni. Shungu ambaye ni mzaliwa wa Congo alitokea hapa nchini na hivyo kuendeleza wimbi la watanzania na wapitio Tanzania kukamatwa na madawa ya Kulevya nchini China. Spoti Starehe imetumiwa picha za unaosemekana ni Mwili wa Shungu ukiwa Mochuary baada ya kufariki, kwa sababu ya maadili hatuwezi kuzitumia hapa.

Wakati huo huo habari zilizotufikia zinasema mwanamuziki mwingine raper wa kundi la Akudo Sound Kanal Top amekamatwa na unga hukohuko china.

Meneja wa Bendi ya Akudo Impact, Ramadhan Pesambili, Novemba 14, mwaka huu alisema kwamba wamepata taarifa za kushikiliwa kwa Kanal Top nchini China kwa tuhuma hizo.
“Taarifa hizo tumezisikia, tunazifuatialia kwa umakini mkubwa na kuweza kujua kama ni kweli ama la, maana zinachanganya sana,” alisema Pesambili. Aidha,  meneja huyo ameonesha kusikitishwa na habari hizo na kudai kwamba zinaichafua bendi yao kutokana na watu mbalimbali kumpigia simu kumuulizia juu ya taarifa hizo na wengine  kumfafanulia zaidi jinsi Kanal Top alivyonaswa.
“Kama meneja wa Akudo nasikitishwa na taarifa hizo, kwa kuwa Kanal Top hatuko naye zaidi ya miezi minne sasa, mwanzo aliaga anakwenda Kongo kuoa na  aliporudi aliomba ruhusa ya kwenda Dubai kufanya shoo ya wimbo wake wa Mama Vanesa nasi tukamruhusu kwa moyo wote.
“Wiki tatu zilizopita tulisikia habari za uvumi huo na tulipofuatilia tukagundua si kweli,” alisema meneja huyo.
Pesambili alisema kuwa hata Mzee  Kapuya (Juma, mmiliki wa Akudo) alisikia uvumi huo na akasema kama kweli Kanal Top anajihusisha na biashara hiyo basi asirudi kwenye bendi yake na ikiwezekana akamatwe kabla hajachafua hali ya hewa.
“Lakini  kabla hatujachukua hatua zozote ndiyo juzi tukasikia tena kuwa amekamatwa nchini China.
“Viongozi wa Akudo tumesikitishwa sana na taarifa hizo ingawa bado tunaendelea kuzifuatilia ili tuweze kujua zaidi, maana tunasikia amekamatwa akiwa na wanamuziki wa FM Academia, wengine wanasema alikuwa na mkewe,” alisema Pesambili huku akikiri simu ya China ya Kanal Top haipatikani.

Kwa sheria za nchini China mtu akikamatwa na madawa ya Kulevya anaweza Kunyongwa, kwani bado China haina mpango wa kubadilishana wafungwa na nchi ya Kongo DRC.

JB Mpiana; “Hakuna lolote kati yangu na Werasson”

November 15, 2013

1471748

Na Lubonji wa Lubonji – Ufaransa

JB MPIANA akihojiwa na mwandishi wa habari maarufu Omar Abdel Kader huko Côte D’Ivoire, JB MPIANA kasema hakuna tatizo lolote katiyake na Werrason.

Hapa chini nayakariri mahojiano kwa kifupi :
« Je ne vais pas dire comme ça qu’il y a des liens d’amitié entre nous pour rien :siwezi nikasema kuna urafiki kati yetu bila kua nauhakika

Si je le dis, c’est que je suis sérieux et conscient de ce que je suis en train de dire:Nakama nasema yakwamba kuna urafiki kati yetu wala siutani ninauhakika na maneno yangu

On a gardé de bons rapports. Ça va. Nos enfants se fréquentent et sont des potes»:Tulibaki na uhusiano Mzuri kati yetu,kweli kabisa,kadhalika watoto wetu wantembeleana na nimarafiki kabisa.

, a-t-il expliqué, précisant que les attaques par pesse interposée entre lui et le leader de Wenge Maison Mère n’était que « juste pour les besoins du show-biz»:Kuchimbiana kupitia vyombo vya habari tofauti kati ya yeye JB MPIANA NA WERRASON ilikua ikitokana na mahitaji ya Show-Biz.

WEKA MAONI YAKO KUHUSIANA NA HAYO MACHACHE

Fally Ipupa Kiboko, Yuko Booked Mpaka mwakani

November 8, 2013

Pichani Fally Alipokuwa akiongea na wanahabari juu ya Tamasha la MTV All Star Kwa Zulu Natal huko Durban Afrika ya Kusini alipotumbuiza jukwaa moja na akina Dbanji, Snoopy Dogy na wengineo Gonga hapa.

Baada ya kutoa albamu yake ambayo inatamba kwa sasa ya Power 101 Mwanamuziki Fally Ipupa ameendelea kutamba na kupanda chati kila kunapokucha huku akiwa na sho nyingi kuliko mwanamuziki yeyote wa Congo kwa Sasa. Muziki una nguvu ya kuunganisha maadui, Tarehe 25 na 26 Mwanamuziki Fally Ipupa alikuwa Mashariki mwa Kongo huko Kivu ya Kaskazini ambako alikuwa na shoo kubwa ya kufa mtu, Baadaye atapiga shoo moja huko Kinshasa mwanzoni mwa mwezi huu kabla ya kwenda Abidjan, Côte d’Ivoire tarehe 15 mwezi huu na inatazamiwa kutakuwa na maonyesho kama mawili na baadaye mwezi ujao Fally atakuwa Guinea huko Malabo hii ni December 14 na 15.

Baada ya hapo mwanamuziki huyo kipenzi cha wadada anatazamiwa kwenda nchini Cameroun katika jiji la Younde ambapo anatazamiwa kuwa na maonyesho kadhaa na baadaye atakwenda jiji la maraha Dubai ambapo atakuwa na maonyesho matatu kati ya tarehe 20, 21 na 22. Fally atapumziki na kufanya shopping zake mpaka usiku wa tarehe 28 December ambapo atasafiri kwenda Libreville, Gabon ambako atakuwa na onyesho tarehe 29 onyesho ambalo limepangwa kuhudhuriwa na watu wengi ikiwa ni mwisho mwa mwaka na hii itakuwa zawadi ya mwaka mpya kwao.

Fally ndiye mwanamuziki wa Congo aliye na mikataba mingi ya Show nje ya Congo kuliko mwanamuziki yeyete kwa sasa.

Wacongoman wa Tshengen wagawanyika onyesho la JB Mpiana Zenith

November 8, 2013

Swali la kuwepo kwa show ya Jb Mpiana ama kutokuwepo ndilo lililotawala midomo ya jumuiya ya Wacongoman wanaoishi Shengen. hii inafuatia kuwepo kwa taarifa kuwa kundi la Bana Congo ambao walishiriki kupiga marufuku maonyesho uya baadhi ya wanamuziki wa Congo huko Ufaransa, Belgium na Ujeruman kuripotiwa kugawanyika kufuatia taarifa za hivi karibuni kuwa wapo ambao bado hawataki kuwepo kwa onyesho hilo.

Duru za kimuziki kutoka Ufaransa ambako ndio nyesho hilo la Zenith la Desemba 21 litafanyika wanasema kuwa katika Mkutano na wanahabari huko Ufaransa majuzi Waandazi walitanabaisha kuwa sehemu kubwa ya mapato ya show hiyo itatumika kuchangia kwa waathirika wa vita huko Mashariki mwa Congo ambapo waathirika wakubwa walikuwa kina mama na watoto. Kwa mujibu wa taarifa upande wa Bana Congo (de Combattants) wanaopinga wanasema kuwa hakuna faida ya kuwa na show kama hiyo kwa kumuona kuwa JB Mpiana ni mmoja wa wasaliti.

“Baadhi ya de Combattants wanakubaliana na maelezo ya dhumuni la onyesho lililoelezwa na Producer wa onyesho hilo na muandaaji hasa ikizingatiwa kuna zaidi ya takribani miaka minne tangu mwanamuziki huyo mwenye wapenzi wengi toka afanye onyesho huko” kilisema chanzo cha habari alipozungumza nami. “…. kwa upande mwingine wengine wanakataa wakibaki na msimamo wao ule ule.

Mamlaka ya Zenith imeshatangaza kuwepo kwa show ya JB Mpiana na Ticket za Show kuanza kunadiwa huku mashabiki toka Ufaransa, Ubelgiji, Norway, Sweden, Ujerumani na kwingineko wakitazamiwa kushiriki.

Waifahamu Familia ya Koffi Olomide?

November 4, 2013

Na Hadj Le Jbnique,Boston,Ma,USA.

Mamaa Aliana …huyu ndio mke halali wa ndoa wa Mopao Koffi Olomide

Koffi,Alia na Kitinda mimba wao Saint James

Huyu anaitwa Rocky,ndio mtoto wa kwanza official wa koffi kabla hajakutana na mkewe wa sasa Aliana,mkisikiliza nyimbo za koffi za miaka ya mwanzoni mwa tisini mtalisikia sana jina la huyo kipindi kile kina Suzuki walimtajataja sana na koffi alikua akijulikana kama Papa Rocky,sasa kama ulikua hujui Rocky mwenyewe ndio huyu kawa mkaka now.

Huyu ni binti pekee wa Koffi Olomide,wengi mtakua mmeshalisikia jina lake kwenye nyimbo nyingi za koffi,anaitwa Didi Stone,nyuma ni picha za wadogo zake,Del Pirlo na Saint James,hii ilikua ni tarehe 17 mwezi mwaka huu July 2013,ambayo ndio siku yake ya kuzaliwa.

Del Pirlo Mourinho “De Boss” mtoto wa pili wa kiume wa Mopao ambae mopao kwa mapenzi yake kwake humwita The boss na pia ameipa hotel yake ya kisasa jina la huyu mtoto,inaitwa VILLA DEL PIRLO

DelPirlo Mourinho Le Boss, Ambaye Hotel ya Koffi yenye hadhi ya nyota Tano imepewa jina lake.

Hapa kutoka kushoto ni kitinda mimba Saint James,dada mkubwa Didi Stone na Le Boss mwenyewe Del Pirlo.

Hapa ni mzee mzima mwenyewe Le Rambo du Zaire Mopao Mokonzi na wanae Didi Stone,Del Pirlo de Boss na Saint James.

Didi Stone a.k.a. Nike Olomide

Na hii ndio VILLA DEL PIRLO yenyewe,a four star hotel ya Koffi Olomide ambayo inapatikana : 47, Allée de Mont-Fleury, Quartier Mont-Fleury katika eneo tulivu na salama la Ngaliema jijini Kinshasa, kwa mtakaotembelea Kinshasa  basi malazi bora yanapatikana hapo kwa koffi, tumpe support kwenye kitu chake hiki kizuri,na pia hii ni changamoto kwa wasanii wetu wote kuanzia bongo movie,music na hata footballers wakumbuke kuwekeza tutawaunga mkono kwenye investment zao kwa kuwa tunawapenda.

%d bloggers like this: