Power 001 – Wimbo mpya zawadi ya Christmass toka kwa Fally Ipupa.

December 26, 2012

Meery X mass Werrason and Bonne anniversair.

December 26, 2012

Werasson kwa Sebene hatariiiii

December 22, 2012

WASANII WAKONGWE WAMTEMBELEA JK IKULU.

December 21, 2012

 

Picha juu Rais jakaya kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo.

Rais jakaya kikwete akimshukuru Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi nchini King Kiki

Mr Waziri Ally kutoka bendi ya kilimanjaro Band wana Njenje akitoa salaam za shukrani na pongezi kwa niamba ya ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo — in Dar es Salaam.

 

Rais Jakaya kikwete akijadiliana jambo na Mwanamuziki Mkongwe kutoka Bendi ya Kilimanjaro Band Wana Njenje Bw Waziri Ally Muda mfupi baada ya ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu kumtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo — in Dar es Salaam.

Picha zote na Ikulu


Habari njema kwa Mashabiki wa Werasson

December 18, 2012

Habari njema kwa mashabiki wa Werason, Igwee anatarajia kuja nchini karibuni, bado mipango ya awali ndio iko mbioni,, usia wangu tu kwa wanaotaka kumleta msituwekee na Local Bands kwani hawa wanamuziki wanajitosheleza wenyewe acheni tule burudani ya kutosha hata ikiwa ni masaa mawili tu, kwani sisi tunakwenda kumuona yeye na si Local Bands, hizi tunaziona kila siku.

Tutaendelea kufahamishana hapa hapa kuhusu ujio huu mambo yakiwa tayari.

“@


Koffi awasha moto Dar

December 16, 2012
image

Cindy akianza kuimba kabla ya Koffi kupanda Jukwaani

image

Mamaa Cindy akiwajibika jukwaani kibao kilikuwa Aspirine

image

Koffi akimtambulisha Boss Kusaga na kutoa shukrani zake kwa kumleta tena nchini

image

Quadra Kora Man Le Grand Fororo Koffi akiwa jukwaani katika tamasha la Tusker Carnival usiku wa kiamkia leo.

image

Koffi akienda Sambamba na Cindy na warembo wake

image

Stage show wa Koffi wakiwajibika jukwaani na kutoa burudani ya uhakika

image

Mashabiki wamekaa wakifatilia show. Ferre Gola aliwahi kukataa na kuomba viti vitolewe akisema anataka watu wacheze sio wakae ye hafanyi maigizo.

image

Stage shows

image

Koffi na vijana wake

Stage

image

Stage

Picha zote kwa hisani kubwa kabisa ya Mzee wa Jiachie.


Fally Ipupa asherehekea Birthday yake leo kwa kuzindua Wimbo Mpya “Sweet Life”

December 14, 2012

image

Ni Mmoja wa vijana wa Koffi Olomide ambaye amefanikiwa sana kwa sasa na ana portion yake kwa mashabiki na kwenye soko la muziki wa Dansi ulimwenguni.

Leo tarehe 14 December ndio siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki Fally Ipupa huku akiizindua Single yake inayokwenda kwa jina la Sweet Life. Fally ni mmoja ya wanamuziki ambao wametoka mbali sana kwenye soko la Muziki huku nyota yake ikianza kung’ara kwenye kundi la Quartier Latin lakwake Koffi Olomide akisikika vizuri kwenye wimbo kama Sylivie na nyinginezo.

Mahadhi ya wimbo huu hayako kwenye Bolingo kama tulivyozoea ila uko kwenye mahadhi fulani kama R n B, Fally alisema nia yake ni kuupeleka muziki wa Congo kwenye level nyingine kabisa, na sasa tunaona hata aina ya muziki anayopiga, haya yanaweza kuwa mageuzi kwenye hiki kinachojulikana kama kizazi cha tano kwani hata Ferre Gola naye anatoa nyimbo akiwashirikisha magwiji kama Celine Deon na Rick Rossy.

Ikumbukwe pia Fally alishawahi kufanya interview Kwa JB Mpiana wakati bendi ikiundwa upya lakini bado alikuwa na ndoto ya kutoka kivyake kwani alikataa mpango wa kusaini mkataba wa muda mrefu. Leo hii tunashuhudia Fally akiwa na mashabiki lukuki huku akizindua albamu na zote zikiwa na nyimbo nzuri.


Yusuf Monde Arabe; Toka FM Academia hadi kwa Quartier Latin Kwa Koffi

December 14, 2012

Enter video caption here

koffi olomide

Kuna story ukizikisia za wanamuziki zinasisimua, lakini kikubwa kila mwanamuziki ukimuuliza atakwambia ama anataka aje kuwa mtu mkubwa anayekubalika au aje kufanya kazi kwenye bendi kubwa.

Kipindi FM Academia imesimama inao kundini wanamuziki wake mahiri akina Mule Mule FBI Liberko la Loi, akina Jose Mara ambaye sasa ni mmoja wa wamiliki wa Mapacha watatu, na wengineo wengi pia alikuwepo mtu anayejulikana kama Yusuf Monde Arabe, huyu bwana kama ukisikiliza kibao cha Acha Tamaaa kilichotungwa na Karbeza kuanzia 5:28 hadi 5:53 kabla ya Verse ya Jose Mara ni yeye ameimba hapo ingawa kwenye video hii sio picha yake inaonekani kwani aliondoka kabla shooting ya Video hii.

Hii albamu yenye nyimbo kama Anna, Balaa, Acha Tamaa na nyinginezo kwangu inabaki kuwa ni moja ya Albamu Bora kabisa za FM Academia na itabidi wafanye kazi sana kurudi kwenye level hii.

Yusuf alitimkia Uarabuni Dubai huko ambako hata Mule Mule anafanya kazi huko, na ndipo alipotimiza ndoto yake na kukutana na Koffi Olomide ambaye alikuwa mapumzikoni, kwa vile Koffi alikuwa amepungukiwa na wanamuziki na alikuwa anatafuta vipaji kipaji cha kijana huyu kikamvutia na kumchukua kwa majaribio hatimaye akafaulu na kusajiliwa kwenye The Dream Team ya Quarter Latin. Leo tunashuhudia Yusuf akirejea na nguli nambari moja kwenye muziki wa Dansi Afrika. kwangu mimi hapa lipo la  kujifunza kwa wanamuziki wetu kiasi kwamba nao wanaweza kujituma wakafika huko juu, majuzi niliambiwa kuna mwanadada liwahi kucheza Akudo Sound na sasa yuko kwa JB Mpiana.

Kazi kwenu wanamuziki wa Bongo umizeni vichwa na sisi tuupeleke muziki wetu nje ya mipaka yetu.


Desormais’; Wimbo Koffi aloigiza ndoa yake na Cindy

December 14, 2012

koffi olomide

Ikiwa imebakia siku moja tuu kabla ya Koffi Olomide nguli kupanda jukwaani, Koffi ni mwanamuziki ambaye anapendwa sana Africa kwa muziki wake na mandhari ya video zake, pia ni mwanamuziki ambaye amefanikiwa sana akiwa na bendi yake ingawa anaongoza kwa kukimbiwa na wanamuziki wake ambapo bendi yake imesha meguka zaidi ya mara tatu pigo kubwa likiwa ni kipindi ambacho waliondoka akina Suzuki, Geco Mpela ambaye ni mdogo wake na Allain Mpella aliyekuwa Wenge BCBG, Lola Mwana Digital mtoto wa Marehemu Dindo Yogo, Fally Ipupa na wengine.

Koffi aliwashangaza watu alipoibuka na timu mpya na kuipanga na alipotoka akatoka na nyimbo kali, mara kadhaa alipohojiwa alisema bendi yake ni kama The Dream Team akiifananisha na timu ya Taifa ya Kikapu ya Marekani akisema kila kukicha kuna vipaji tupu.

Wimbo huu ambao umo kwenye Albamu yake mpya ya Abracadabra Koffi ameigiza anamuoa mwanamuziki na mpenzi wake Cindy jambo linalopelekea kuwa Koffi ameamua kuhalalisha wale wanao hoji mahusiano haya. Ni wimbo wa Mapenzi Mzuri sana, Binafsi napenda sana nyimbo za taratibu za Koffi na huu naupenda sana.

Kama unapenda kujua yoote tuliyoandika kuhusu Koffi Gonga hapa.

Sponsored by:


Cindy Olomide alipomwaga chozi jukwaani kukumbuka alipotoka.

December 7, 2012

koffi olomide

cindy1

Bado tupo kwenye wiki ya Koffi Olomide ambapo tunaangalia zile Post zilizowekwa hapa mwaka huu zinazomhusu Koffi kwa ajili ya kuwakumbusha mashabiki wa Koffi mambo muhimu yanayomhusu mwanamuziki huyu.

Baada ya kuangalia jinsi Koffi alivyompatia “Mahali” baba mkwe kwa kumzawadia Jaguar Mpya, leo tunamuangalia Cindy Olomide tayari akiwa na Koffi ndani ya bendi ya Quartier Latin.

Wimbo unaitwa  Lily Kanik uliimbwa na Koffi Olomide. Wimbo huu ndio uliompa Cindy maks alipoitwa kwenye interview ili awe mmoja wa waimbaji wa Koffi, Lily Kaniki ni mama yake na Claudia Sasou Ngueso mke wa Denis Sassou Ngueso. ambaye amekuwa karibu sana na wanamuziki wa Congo na kila mara wamekuwa wakimuimba na Koffi mwenyewe aliwahi kufunga safari alipofariki huyu mama na kwenda kumpa pole Mheshimiwa Rais Sassou Ngueso.

 


Turejee kwenye wimbo wenyewe, Cindy amejizolea umaarufu kwa kuziimba tena nyimbo za Koffi na kuwafanya mashabiki kupata ladha tofauti kabisa. Kila mara akiimba na akifikia kuuimba Wimbo huu ambao mashabiki wanaupenda Cindy anasema huwa unamkumbusha mbali sana.

Kwenye show hii Cindy alipokuwa akiimba wimbo huu alitoa machozi utaona anashindwa kuimba kabisa na Koffi anamwambia aendelee kuimba, kisa cha kutokwa na machozi ni fikra akikumbuka alikotoka na anasema wimbo huu kila akiuimba anakumbuka safari ya ndoto yake ya kuja kuwa mwanamuziki, kwa Sasa Cindy si tu mwanamuziki ndani ya Quartier Latini bali ni mpenzi wa Koffi Olomide ambaye wameshibana kwelikweli.

Ndani ya video hii utamuona kwa mbali Zakarie Bababaswe ambaye alikuwa mshereheshaji kwenye Concert hii iliyofanyika Inter Continental Hotel huko Kinshasa. Kiukweli hii ni Concert ya kuitazama jumapili ukiwa umepumzika na Glass ya wine pembeni.

Merci mingi Papaa Julie We Ston kwa kuniletee DVD hii direct from Congo Merci Papaa Cisco ndani ya Kwetu Saloon weeeee!! kitokoooo.

BAada ya hapa tutamuangalia Koffi alipofungua jumba lake la kifahari na Hotel yake, pia tutanmuangalia Koffi na Familia yake.

Koffi Special Sponsored by:


Koffi alipomzawadia Baba Mkwe Jaguar Mpya!!

December 7, 2012

koffi olomide

Kama nilivyoahidi wiki hii na ijayo tutaangalia zile Posts ambazo zilimhusu Koffi Olomide kwa mwaka huu kuwakumbusha mambo muhimu yanayomhusu mwanamuziki huyu ambayo mashabiki wa burudani wanependa kuyajua.

Baada ya kuwa na minong’ono kwa muda mrefu  kuhusu mahusiono ya binti mrembo Cindy Le Coeur na Bosi wake Koffi Olomide a.k.a. Papaa na Didi Stone Quadra Kora Man, kuwa na uhusiano wa wawili hao umeonekana kuwa ni wa zaidi ya mtu na bosi wake, hatimaye mzee mzima koffy aliamua kufunguka na kuweka mambo yake na Cindy hadharani.

Baba Mkwe akiwa ndani ya mchuma

Kuonyesha kwamba yuko serious this time koffi aliamua kumpa zawadi baba mkwe, Baba mzazi wa Cindy….unaweza ku guess ni zawadi gani? Wala usipate taabu kwa kuwa tunakupenda sana hatutaki uumize kichwa gonga hapo kwenye video juu ujionee mwenyewe video nzima ya hafla hiyo “ndogo” lakini iliyopendeza sana, uone jeuri ya pesa ya Le Rambow Du Zaire Koffi Mopao Olomide, mzee mzima anatoa kitu cha Jaguar kwa mzee hivi hivi kwa mzee ikiwa ni zawadi ya kumzalia mtoto mzuri.

Koffi alifanya haya akiwa ndani ya Concert na ghafla ikatangazwa, sina hakika sana lakini nadhani anayetangaza ni Zakarie Bababaswe.

Jamani kuzaa kuzuri tena hasa mtoto wa kike,nashangaa watu wanaogombana na wake zao kwa kuwazalia watoto wa kike,check hapo mzee alivyofurahi.

Mamaa Cindy Olomide

Kumbuka kuwa chini ya kila Post kuna burton imeandikwa SHARE ukiweka mouse inakupa njia mbali mbali za ku share na marafiki wa facebook na kwingineko nao wapate uhondo, pia ili usipitwe kulia kuna mahala pakuweka email yako ambapo utakuwa ukitumiwa kila post mpya ikiwekwa hapa!!

Koffi Special Sponsored by:


Koffi na Cle Bora, Diamond muzika na Mapenzi

December 6, 2012

Mwenyewe anadai anapiga anaina tofauti kabisa ya Muziki ukilinganisha na wanamuziki wengine. Ikumbukwe kuwa Koffi hana asili ya Kongo ni mmoja wa wazazi wake ndio wenyeji wa Kongo hivyo basi anasema wakati mwingine huwa anachanganya midundo ya asili na muziki wa Afri Pop na kupata ladha ambayo inapatikana kwenye nyimbo zake.

Tofauti na JB Mpiana, Werrasson na wengine ambao utaona solorist anaongoza mziki kwa Koffi utazisikia zaidi Drums na Tumba zikiongoza. Jaribu kusikiliza kibao hiki kisha nipe maoni yako.

Ukisikiliza huu wimbo wa Mapenzi ni kitu gani wa Diamond Muzika utaguandua kuwa waliiga wimbo huu hapo juu kwa kiasi kikubwa mpangilio wa sauri, ndio maana kila siku huwa nasema kwa wanaojua muziki hawa wa congo wanaoimba hapa nyimbo nyingi huwa wanaiga za kwenye albamu za wacongo wenzao ambazo zili heat lakini hazikuwa na air time za kutosha ama kutopigwa kabisa hapa kwetu.

Kwangu mimi siwezi kusifia unapo irejea kazi ya mtu kwani usanii na heshima ni pale unapotunga maneno yawe wimbo yaimbike na yawe kwenye rhythm gani na si hapo tu chombo gani kianze na kipi kifatie mpaka ukatoka muziki mzima.

Jipangeni na mtoke kivyenu kama mnataka kufika mbali kama nia ni kutuurudisha siku ziende mgange njaa kibongo bongo mtaishia hapo hapo tuu.

Ni mtazamo tuu. Wiki hii tutajaribu kumuangalia Koffi na Post ambazo tuliwahi kuziandika hapa hapa kwa heshima ya ujio wake.


JB Mpiana alivyochengusha Mwanza

December 5, 2012

Jb Mpiana ‘Mukulu’ aka Binadamu usiku huu ndani ya himaya ya Villa Park Mwanza anamwaga mvua ya burudani kwa wapenzi wa ngoma za bendi waliojitokeza hapa.

Simple and clean…kwa wadada wa safu ya unenguaji ya bendi ya Wenge BCBG chini yake Jb Mpiana.

Wadada wa mwanza hawajasita kumtunza mkali huyu wa ngoma za dance toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Danico ndiyo wimbo jukwaani sasa..


Mashabiki na mtu wao kiunganishi muziki…


Jb Mpiana ‘Mukulu’ aka Binadamu na safu yake ya masauti..


Wadau walioamua kuwekeza ndani ya usiku huu. 

Huku akipewa tafu na JB Mpiana ‘Mukulu’ aka Binadamu pamoja na rapa wa bendi hiyo, mwanamuziki H. Baba alifanya ile inayotakiwa kwenye jukwaa  kubwa sambamba na kundi la Wenge BCBG. 

Utamu unapokolea ‘tafu’ muhimu.


Ngoma ikiendelea stejini naye H. Baba akiendelea kumwaga sumu.

 

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania H. Baba mwishoni mwa wiki alifanya show ya live akiwa na bendi ya Wenge Muzika BCBG na kuwastaajabisha wengi akiwemo kiongozi wa bendi hiyo JB. Mpiana, kwa umahiri wa uchezaji wake, umiliki wa sauti, jukwaa na upangaji safu yake. 

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania H. Baba alitumia vipande vya rap zake kunyanyua hisia za mashabiki huku sebene la nguvu likiendelea kushushwa na wana Wenge BCBG nao marapa wa bendi hiyo wakifanya kolabo nae kupendezesha show ya ujio wa Wenge Musica jijini Mwanza ulioandaliwa na QS Mhonda J, na kudhaminiwa na kampuni ya kutengeneza vinywaji vikali ya K Vant Gin na TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager..

H. Baba akiimbisha wakati mmoja kati ya wacheza show wake ‘Dogo Poteza’ akikisanukisha.


Hapo jeh..!

Picha zote na GSengo Blog


Onja utamu wa show ya JB na Wenge BCBG Leaders

December 5, 2012

Kama ulimiss show ya JB Pale Leaders Club basi pata kionjo hapo kwa picha na habari gonga hapa.


Joe Kusaga amualika JB Mpiana kwenye Dinner Escape 2 Kunduchi

December 5, 2012

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake,akiwemo mwanamuziki nyota wa dansi ndani ya kundi la Wenge BCBG,kutoka nchini DRC-Congo, JB Mpiana (pichani kati) akiwa na Mamaa Jasmine Demukalinga mke Debs Demukalinga Le Grand Yakuza, mmoja wa ma PDG wakikongo anaishi huko Belgium na Paris, hapa wakiingia kwenye hafla fupi ya chakula cha usiku iliyofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini Dar, hafla hiyo pia ni sehemu ya muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 13 ya Clouds FM tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake na kuzungumza nao machache na kuhakikisha wanapatiwa chochote kitu.

 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimtambulisha mke wake Johayna Kusaga  (ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd) kwa Mwanamuzik JB Mpiana na kwa wageni wengine waliofika kwenye hafla hiyo ya chakula cha pamoja.

 Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake JB Mpiana kwenye chakula

 Pichani ni baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss East Afrika  2012 ambao pia waliakwa kwenye chakula cha pamoja ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini dar.

Washiriki wa shindano la Miss East Afrika wakiwa katika picha ya pamoja

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Cassim akitumbuiza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali 

 Boniventure Kilosa a.k.a Dj Venture alikamata mashine na kuangusha ngoma kali zikiwemo za Kinaija,abazo wageni wengi walionekana kuburudishwa nazo vilivyo.

Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 wakijiachia vilivyo kwa mikato ya ngoma iliokuwa ikiangushwa na Dj Venture.

 Joseph Kusaga a.k.a Boss JOe akizungumza na baadhi ya wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ay na Mwana FA ndani ya hafla fupi ya chakula cha usiku kulichoandaliwa kwa ajili ya wageni.

 

Wafanyakazi mbalimbali kutoka Clouds Media Group walikuwepo pia

Kuserebuka kama hivi pia kulikuwepo
.

Mtangazaji wa Clouds TV,Ben Kinyaiya akifanya mahojiano mafupi na mwanamuziki mkongwe wa dansi,Ndandaa Kossovo.

Dj Venture na mshkaji wake wakivuta pumzi.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time promotios,pichani kulia Godfrey Kusaga akibadilishana mawazo na Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM,Ephrahim Kibonde huku wakiangusha moja moja.

 Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo.Kwa Hisani ya JOHN BUKUKU Mzee wa Kushangweka


Umeninyima; Kolabo ya Papa Wemba na Mashujaa Band iliyokosa Promo

December 4, 2012

image

Pamoja na kuwa hawakufanikiwa kuzindua albamu yao lakini kwangu mimi bado MAshujaa Band ni moja ya bendi ambazo zimeleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya burudani nchini Tanzania.

Ni ukweli usiopingika kukosekana kwa kipindi cha Afrika Bambataa Clouds FM kumefanya muziki wa dansi ambao pia ulikuwa na mashabiki wengi sana nani asiyejua kuwa unapoongelea burudani unawaongelea Prime Time Promotion unawaongelea Clouds, tumeshuhudia jinsi matamasha yao yalivyo fana iwe kwa wanamuziki wa ndani au wanamuziki wa nje ya nchi, utake usitake kama unataka kitu chako kifanikiwe kwenye burudani hawa jamaa ushirikiane nao hata kama ni kwa shingo upande huna budi hiyo ndio hali halisi.

Kama kipindi kile kingeendelea kuwepo ni wazi mapenzi ya muziki huu yangeendelea kuwa juu. Mimi binafsi nilibadilishwa “dini” na kuangukia mapenzi yangu kwenye bolingo na Mr C Charls Mhamiji ambaye kiukweli kolabo yake na Njaidi naweza sema hakuna kama wao kwenye kipindi, kwa maana ya habari na muziki.

Tuyaache hayo tuangalie wimbo huu wa leo, Hii ilikuwa ni kolabo ya Mashujaa muzika na nguli mwingine mkubwa wa muziki wa dansi si tu kwa Congo bali kwa Africa kwa ujumla na ukiusikiliza wimbo huu  utakubaliana na mimi ukongwe unachangia sana, ila binafsi nakosa ladha ya vyombo hakuna kick kabisa kwa maana ya kuwa sauti imeizidi nguvu Vyombo.

All in all Mashujaa wameweza na nadhani wakifany marekebisho kwa yale matatizo madogomadogo watafanikiwa sana. Hongereni na binafsi nawakubali sana.


Pardon ya Jean Barlon wa Loketo Group

December 3, 2012

Kwa wale wenzangu na mimi tulioanza kuupenda muziki huu siku nyingi utakuwa unawakumbuka Loketo Group ambao walikuwa wakiongozwa na mtu mzima Aurlus Mabere, ndani yake kulikuwa na watu kama Jean Barlon, Lucien Bokilo, Mac Macaire, Diblo Dibala, Mimi Kazidona na wengineo wengi.

kiukweli wakati ule muziki huu kwa hapa kwetu ndio ulikuwa uko juu sana na hawa jamaa walikuwa wako juu vile vile ingawa wengi wao waliondoka na kutoka kivyao. Wimbo huu unaitwa Pardon unamuonyesha mwanamuziki ambaye nilikuwa nampenda sana kwenye kundi lile, Jean Barlow. kwa yeyote anayejua walipo hawa jamaa atupie hapa.


Gangnam Style vs Mpunda Style ya Wenge BCBG we Mbaya weweeee!!!!

December 3, 2012

Angekuwa ni Joti sijui ni nani angemwambia We Mbaya wewe kwani Gangnam Style, ndio habari ya duniani kwa sasa, hii ni Video ya Wimbo ambao ni wa Korea, ni Style ambayo asili yake ni huko Korea huyu mwanamuziki huyu akiwa ni wa pili kwa video yake kutazamwa mara nyingi zaidi ambapo mpaka leo imetazamwa mara Milioni 861,218,607 kwenye mtandao wa You Tube.

Bado wataalamu wa mambo ya mtandao wanasema Video hii ni ya kwanza na si yapili kwani baada ya kutoka ziliwekwa nyingine ambazo nazo zina wa mamilioni ya watu kwa hiyo kama ingekuwa peke yake hesabu zote zingekuwa za hiyo moja.

Style ya wimbo huu inafanana kiasi fulani na style ya Mpunda Style ambayo inachezwa na Wenge BCBG. Ukiangalia utaona jamaa wanacheza mikono iko juu kama wanaendesha pikipiki na miguu wanainua na Mpunda style ni hivyo hivyo sasa angekuwa joti sijui nani angemwambia ame copy hapa, hebu angalia Video hiyo juu na hii hapa chini ya JB Mpiana kisha unipe jibu.


Gangnam Style vs Mpunda Style ya Wenge BCBG we Mbaya weweeee!!!!

December 3, 2012

Angekuwa ni Joti sijui ni nani angemwambia We Mbaya wewe kwani Gangnam Style, ndio habari ya duniani kwa sasa, hii ni Video ya Wimbo ambao ni wa Korea, ni Style ambayo asili yake ni huko Korea huyu mwanamuziki huyu akiwa ni wa pili kwa video yake kutazamwa mara nyingi zaidi ambapo mpaka leo imetazamwa mara Milioni 861,218,607 kwenye mtandao wa You Tube.

Bado wataalamu wa mambo ya mtandao wanasema Video hii ni ya kwanza na si yapili kwani baada ya kutoka ziliwekwa nyingine ambazo nazo zina wa mamilioni ya watu kwa hiyo kama ingekuwa peke yake hesabu zote zingekuwa za hiyo moja.

Style ya wimbo huu inafanana kiasi fulani na style ya Mpunda Style ambayo inachezwa na Wenge BCBG. Ukiangalia utaona jamaa wanacheza mikono iko juu kama wanaendesha pikipiki na miguu wanainua na Mpunda style ni hivyo hivyo sasa angekuwa joti sijui nani angemwambia ame copy hapa, hebu angalia Video hiyo juu na hii hapa chini ya JB Mpiana kisha unipe jibu.


Licha Ya umeme kusumbua, show kuchelewa, Jb Mpiana apagawisha mashabiki Dar

December 2, 2012

[http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=OgzuCQkuNAE]

 

image

Akiwaimbisha mashabiki

image

Wacheza show wakiwajibika vilivyo.

image
Mashabiki wakiwehuka na wenge BCBG julwaani.

image
Jb akiongoza wanamuziki Wa Wenge jukwaani.

image
Mmoja Wa wanamuziki akitoa burudani jukwaani.

image

image
Maboko likoloo kila mtu mikono yulu.

image
Suveree Mukulu Bin Adam Le Charismatique Papa Cherie Salvatory Le Patria Papa Matikakana Baba Ya Bana akiwa jukwaani. Picha na GPL

Mwana muziki Jb Mpiana akiwa na bendi yake Ya Wenge BCBG kutoka Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo, jana usiku iliwapagawisha mashabiki wa muziki huo nchini waliofurika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Katika onyesho hilo ambalo lilikuwa la aina yake, mashabiki walichelewa kupata burudani kutoka kwa mwanamuziki huyo kutokana na matatizo ya umeme, kitu ambacho kilisababisha bendi ya Mashujaa kushindwa kuwakonga mashabiki.

Pamoja na kuchelewa kuanza kwa shoo hiyo, kutokana na matatizo ya kukatika kwa umeme kila muda, JB Mpiana alianza kuwatanguliza wanamuziki wake wakiongozwa na mmoja wa waanzilishi wa bendi hiyo, Shai Ngenge, na kupiga sebene kabambe kabla ya kufuatiwa na wimbo wa zamani wa Kinie Bouger, ambao enzi zake alishirikiana na akina, Ngiana Makanda, miaka ya katikati ya 1990.

Wimbo huo uliweza kuondoa kero kwa mashabiki hao na kuwasahaulisha yale yaliyokuwa yakiwatokea wanamuziki wa Mashujaa, ambao kila walipokuwa wakipanda jukwaani na wanapofika kuanza sebene umeme unakatika, jambo lililowafanya kupanda jukwaani mara nne, lakini wakishindwa kumaliza wimbo mmoja tu wa Risasi Kidole. baada ya kukuru kakara hizo ambazo ziliwashtua viongozi wa Mashujaa na kufanya mmiliki wake Mama Sakina kuanguka kwa mshtuko na Presha kukimbizwa hospitali kupatiwa huduma ya ziada, bado haifahamiki hali yake ila kwa mujibu wa wadau wanasema anaendelea vyema na wanapanga show nyingine ya uzinduzi.

JB Mpiana alionekana kuwa ni mkombozi kwa mashabiki waliokuwa wamebaki huku wakipiga moyo konde kuwa hawataondoka viwanjani hapo bila ya kumuona JB, katika uzinduzi huo kutokana na burudani safi.

Kitu ambacho kiliwashangaza mashabiki wengi ni kutokatika kwa mara kwa mara kwa umeme kama ilivyotokea kwa bendi ya Mashujaa ilipokuwa jukwaani. Mpiana aliweza kufanya kweli katika shoo hiyo kwani umeme haukukatika mpaka aliposhuka jukwaani majira ya saa 10 alfajiri, “Kiukweli JB Mpiana ametutendea haki, nimeridhika na mi nilikuja kumuona JB ambaye nimemuona na nimeridhika sana” Alisema shabiki mmoja Mabamba ambaye anaupenda muziki huu.

Katika shoo hiyo, Mpiana aliweza kupiga nyimbo mbali mbali za zamani ikiwa pamoja na Barakuda, Djodjo Ngonda, Walay Danico, Dizoizo na zile mpya katika mtindo wa non-stop.

Mashujaa ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na mara walipoanza kucheza shoo ya ufunguzi ambao imewajumuisha wanenguaji wa kike na wa kiume na waimbaji, umeme ulikatika na kazi ya kuanza kurejesha ikaanza na kuchukua muda wa dakika zisizopungua 30.

Pamoja na hizo kasoro chache JB Mpiana ametutendea Haki mashabiki wake na kuikata kiu ambayo wengi walikuwa nayo.


%d bloggers like this: