Mashabiki bwana..!!

January 31, 2010

image

Angolan soccer fan wearing a snake skin head-dress, sings during the final of their African Cup of Nations soccer match between Egypt and Ghana at the November 11 stadium in Luanda, Angola, Sunday Jan. 31, 2010.


Fally Ipupa na Olivia full kujiachia

January 30, 2010

cheki jinsi fally ipupa anavyotesha na olivia wa g unit, nlipopata chance ya kukaa nae alipokuja tanzania kizungu hakipandi na kiswahili ni mgogoro mwingine, hapo ni french na lingala, sasa sijui mawasiliano hapo yakoje mie mgeni wadau.

Kwa hizi na nyinginezo ungana na Agape Msumari kwenye viva Afrika Blog ambao anakuletea habari za burudani hasa muziki wa kiafrika toka Afrika nzima.


Kutana na Austin Steven Bingwa wa kucheza na Nyoka!

January 29, 2010

Anaitwa Austine Steven, alizaliwa miaka 60 iliyopita huko Afrika ya Kusini, Steven ni maarufu kwa Makala zihusuzo nyoka kwa wale wanaoangalia Animal Planet ya DSTV na pia ni muandishi akiwa na vitabu vitatu sokoni.

Mapenzi yake kwa nyoka yamemtembeza dunia nzima ikiwemo kumtafuta aina ya Cobra aliyemuua Cleopatra, Anaconda wa Misitu ya Amazon, Giant Cobra wa Malaysia, Cobra wa India, Vifutu wakali wa Jangwa la Sahara, na alipoamua kuwatafuta aina 10 za nyoka hatari duniani.

Nakupa kionjo cha manjonjo yake na nyoka, gonga playa kuona zaidi, kwa habari zaidi gonga hapo chini.

Read the rest of this entry »

Kuimbwa kuna gharama zake!

January 28, 2010

m53

Pichani ni Zadio Congole ambaye ni rafiki binafsi na shabiki mkubwa sana wa JB Mpiana akiwa katika moja ya shoo za Wenge BCBG huko Shengeni mwaka jana.

Ni jambo la kawaida kusikia majina ya watu fulani yakitajwa kwenye nyimbo, kuna watu wengi waliwahi kuniuliza majina hayo ni akina nani hasa na kwa nini yanatajwa?, Kimsingi ni mbwembwe na kujenga jina ambako kunatokana na umaarufu kwenye jamii ama kisiasa ama kibiashara.

Mara nyingi watu hawa wanakuwa ni watu maarufu ama kwenye sekta ya burudani ama mtu fulani ambao ni wafanyabiashara lakini wengi wao unakuwa wanamguso katika sekta nzima ya burudani, Mfano majina kama Sadam Hussein ilikuwa likiitajwa sana kwenye nyimbo za lingala, huyu ni mtoto wa Marehemu Mabutu Seseseko Rais wa zamani wa Zaire ambaye yeye alipendelea sana maisha ya anasana kama mtoto wa Rais wa Zamani wa Iraq Uday na Kusay, na alisaidia sana wanamuziki katika kutengneza Albamu zao. Pia kuna watu kama Zadio Congole, huyu pia ni ‘mpigaji” ambaye alifaikiwa kupata pesa anaishi huko Ubelgiji (shengheni kwa ujumla) na ni mshabiki mkubwa wa JB Mpiana ambaye kwa kiasi kikubwa amejitolea pesa na muda katika bendi hii,

Pia kuna watu kama Tabou Fatou Top Model ambaye ni “mfanyabiashara” na mdau mkubwa wa sekta nzima ya burudani naye yuko huko huko Paris na Ubegiji.

Boris Bondo, Bebee Ramadhani, Papito Mbala, Zamalenga, Cedric Okitundu ni baadhi ya majina ambayo unaweza kuyasikia sana kwenye nyimbo nyingi za Congo, wengi wao kama nilivyosema ni watu wenye nafasi zao kwenye jamii na hasa ulimwengu wa burudani.

Marehemu Mama Mere Malou “madame ya poto“ kwa faida ya wasomaji wangu, Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa, Pia Mere Malou ndiye alikuwa mke wa kwanza wa mwanamuziki

Sio watu tuu bali nyingine ni kampuni zinazojishughulisha na masuala ya burudani kama Kin Service Express ambayo kwa wakati fulani ilikuwa ikifanya kazi na mwanamuziki Koffi Olomide, Manuru Vaka Productions ambao kwa sasa wamejizolea umaarufu kwa Video za Live za Wenge BCBG kwa ubora wa hali ya juu.

Kwa hapa nyumbani utasikia majina kama PDG Ndama aka mutoto ya Ngombe, Papaa Musofe na wengineo ambao wote hao wanawajibika ipasavyo na ni wadau wakubwa kwenye sekta nzima ya burudani.

Wengi wa waimbwaji hawa wamekuwa wakijitoa sana kwenye shughuli nzima ya burudani na kuzigharamia bendi husika au mwanamuziki husika kwa mavazi au huduma nyingine ikiwa ni pamoja na usafiri nakadhalika.

Angalia kipande hiki uone jamaa wanavyotunza, ikiwa ni gharama ya kuimbwa.

Kwa nchini Kongo jina lako likitajwa kwenye wimbo na bahati nzuri wimbo huo ukawa maarufu basi jina la mtu huyo hutokea kuwa maarufu na wengi walitumia nafasi hizo kisiasa na kupata ushawishi wa kisiasa, jambo lililopelekee Serikali kuingilia kati.

Hivi karibuni Serikali ya Kongo imepiga marufuku kutajwa kwa majina ya wanasiasa na viongozi wa makampuni ya umma kwenye nyimbo za wanamuziki.
Vilevile kurushwa kwa miziki ya aina hiyo katika vituo vya redio na televisheni nchini humo.Kulingana na serikali ya Kongo hatua hiyo ina azma ya kuimarisha utendaji kazi .

Ni jambo la kawaida kusikia majina ya watu maarufu yakitajwa na wakati mwingine kutumika kama Kampeni kwenye uchaguzi na kuwafanya kujizolea mashabiki na wapiga kura kirahisi kwani kwa serikali za Congo wanamuziki wanachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mtazamo wa kisiasa.

Inagharimu sana kwa mtu kuimbwa kwani wengi wamekuwa wadhamini wakubwa wa wanamuziki hawa kimavazi, kugharamia kutoa albamu au mengineyo.


Kolabo inanogesha Mziki bwana!!

January 28, 2010

Sikiliza Huu wimbo wa Mzee wa Busara toka kwa Nature na Inspekta enzi hizo (Si video Rasmi)

Kuna vitu ambavyo huwa kila siku naombea kitokee tena kwenye burudani ya muziki wa Bongo Flava:-

1. Kuwaona Hard Blasters wanafanya kazi pamoja tena.

2. Kuwaona Nature na Inspector wakifanya kazi pamoja tena

3. Kuendelea kumsikia Mr. Paul akizirudia nyimbo za zamani

4. Niwasikie Mandojo na Domokaya

5. Kuwasikia GWM wakiimba tena

Oamoja na wengineo lakini ningependa kuwatolea mfano Nature na Inspekta au Hard Blasterz (Terry, Jay na Willy).

Kwa kiasi kikubwa collabo ya hawa watu wawili ilileta muamko kwenye sekta nzima ya burudani ya Bongo Flava kwani ilikuwa inatoa hadhi hasa ya Flava za Bongo, Namkumbuka mmoja wa watangazaji wa wakati huo Mike Mhagama akiwa Radio One aliitaja hii Collable kama hazina ambayo wangeendelea basi wangeleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta nzima ya Muziki wa kizazi kipya.

Wakati huo haikuwa rahisi kupenya kwenye uzio wa nyimbo kama Bongo Dance ambapo Bendi za Dance nazo zilikuwa zimeleta mageuzi kwa kutumia Mirindimo ya Ki Congo na Muziki wa Dance ndipo zikazaliwa Bendi kama African Revolution, Twanga Pepepta, TOT, Diamond sound na muendelezo wa bendi jizo.

Hivyo basi vijana wakawa wameachwa nyumba na kujiliwaza kwa muziki toka Magharibi na ndipo huu muziki wa kizazi kipya ulipoaanza na kupitia mageuzi na vikwazo kadha wa kadha kwani wakati huo ulikuwa ukijulikana kama mziki wa kihuni.

Picha ya Maktaba ikiwaonyesha The Hard Blasters, Terry kushoto,   Prof Jay (kati) na Biggie Willy (Kulia)

Nakubaliana na kila  mmoja wao kwenda solo kwani inampa uwanja mpana zaidi lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa kwenye makundi siku zote kila mmoja ana nafasi yake, kuna wengine wanajua sana kupanga sauti wengine kupanga vina na wengine kupanga mpokezano. Mfano kwenye bendi ya Wenge Muzika wakati huo kulikuwa na mtu anaitwa Blaise Bulla kwenye wimbo utamsikia Verse moja tuu ila kazi yake kubwa alikuwa kupanga sauti na wakati mwingine hata kushauri kuwa beti hii haifai kuimbwa na wewe ikiimbwa na fulani italeta mguso zaidi.

Muziki wa Bongo Flava unatofautiana na Genge (wa KEnya) kwani wao ni Commercial zaidi wakilenga kuchezesha watu na wakati mwingine hupati maana kwenye wimbo mzima hata wakihojiwa wanashindwa kusema mziki ulilenga nini. Tofauti na muziki wetu ambao unalenga kutoa ujumbe na kuburudisha na ndio maana utaona kila mtu anajitahidi kumshirikisha mtu mwingine kwa ajili ya kuleta ladha tofauti ambayo pia inapatikana kwenye makundi, na utao nyimbo nyingi ambazo mtu ameshirikisha mwingine zimewatoa sana.

Hivyo basi ni muhimu kwa makundi ya muziki kuthamini mchango wa kila mmoja tumeshuhudia makundi kama HArd Blasters baada ya kupanguka mmoja tuu amefanikiwa kutoka na wengine wamebaki waki piga kwata kwenye sekta ya burudani. Kuna ladha ambayo tunaikosa kama wapenzi napenda kumsikia Pro. Jay lakini naikosa ladha ya Loon T (Terry), naikosa ladha ya Biggie Willy (Baba Walter).  Hivyo usia wangu ni kwamba mnatutia kilema mashabiki wenu ambacho mkipanguka mnatupa kazi kuikubali hali halisi.


Wanamuziki wengi wa Bongo Flava wako “Facebook”

January 28, 2010

ay

Ukurasa wa AY kwenye Face Book

Wasanii kadhaa wa Bongo Flava kwa sasa wanapatikana kwenye mtandao wa Facebook na kuweza kuwasiliana moja kwa moja na wapenzi wao ambao wengine hawapati nafasi ya kukutana nao ama hata kuweza kubadilishana mawazo mawili matatu.

Ambwene Yessaya aka AY, Prof Jay, Chid Benz, Fid Q, Mr Paul, Mr II ni baadhi ya wasaniia ambao kwa kiasi kikubwa haipiti siku lazima utakutana nao kwenye mtandao huu maarufu kuliko zote katika ulimwengu wa Social Networking.

fid

Ukurasa wa Fid Q Facebook

Wengine ni Mwana FA, Albino Fulani, Judith Wambura, na wengineo kibao. Mamia kwa maelfu ya vijana ni wanachama wa mtandao huu ambao hata Rais wa Marekani Barak Obama alikiri kutumia muda wake kwa wakati fulani kwenye mtandao huu.

Hii ni njia nzuri ya kuweza kuwasiliana moja kwa moja na funs wao ambapo kama mtu ana swali, hoja, ushauri anaweza kuuliza moja kwa moja pasi na kutegemea radio na magazeti pekee ambapo washabiki wa wanamuziki hawa walioko nje hawapati nafasi ya kukutana nao.

mrpaul

Paul Mbena akiupamba ukurasa wake na Picha yake na Mwanaye mpya!!! Hongera kaka.

Facebook ni mtandao ambao unajipatia umaarufu na kuwa na watumiaji wapya zaidi ya 10,000 kila siku huku ikikisiwa kuwa asilimia zaidi ya 30% ya vijana wa mijini kwenye nchi zinazoendelea na 85% kwa nchi zilizoendelea wamejiunga na mtandao huu.

Facebook kwa sasa inatumika kama sehemu ya kufanyia kampeni, kutangaza biashara, na hata kujuika na marafiki toka pande mbalimbali za dunia.

Mwaka jana Waziri wa Elimu ya Juu wa Malaysia DATOO TAN SRI MUHYIDDIN MOHD YASSIN alitangaza kuwa kila alhamisi hutumia masaa manne kujibu maswali ya wanafunzi kupitia mtandao huu.


Sporah wa The Sporah Show

January 27, 2010

image

Katika mfulilizo wetu wa kuongea na vijana ama waliokatika sekta ya burudani au michezo ambao ama waliwika lakini jamii haijui kwa sasa wako wapi na wanafanya nini au wale ambao wako nje wanafanya mambo makubwa ambapo wengi wetu hatuyajui.

Hivyo basi napenda kutambulisha kwenu Irene Sporah Njau. akiwa ni mtangazaji wa kipindi cha Sporah Show ambacho kinarushwa na Television ya BET huko Uingereza na kuonekana baadhi ya sehemu kadhaa za Nchi za Ulaya.  Yeye ni nani, yuko wapi ana anafanya nini, ni moja ya mambo ambayo atatujulisha mwenyewe katika maswali na majibu yetu leo hii.

Naamini kwamba watu wakijua kuna kazi nzuri nyumbani watakua wanataka kusoma nakumaliza ili warudi nyumbani. Jamani nani anaetaka kuishi nchi za watu? Kazi ngumu, maisha magumu, tamaduni tofauti.”

Swali: Hallo Sporah habari yako?

Salama kabisa.

Swali: Labda kwa kifupi tupe Historia yako.

Jinalangu ni Irene Sporah Njau… Ni mototo wamwisho katika familia yangu, nilimaliza kidato cha sita Kampala–Uganda, nabaada yahapo nilikuja Uingereza kujiendeleza na masomo. Katika purukushani zakutafuta maisha nilijikuta nasomea vitu tofauti..

I hold IT Certificate in Desktop publishing

I hold a BET on Business and Finance

I hold a National Diploma in TV presenting

I have a National Diploma in Accounting and Businesss Management na sasaivi niko mwaka wangu wa mwisho at London Metropolitan University nasomea degree ya International Business Management.

Swali: Wakati unaondoka Nyumbani wazo lako lilikuwa nini, kuja kusoma ama kuja kutafuta maisha nini lilikuwa focus yako?

Kwakweli naweza kusema nilikuwa na mawazo yote pamoja, ila cha muhimu zaidi nilichohitaji ni Elimu. Hata hivi sasa bado naona elimu ni muhimu sana kwangu, na ndio maana bado naenda shule pamoja na kutumia muda wangu kuendesha kipindi cha The Sporah Show.

image Sporah katika pozi tofauti.

Swali: Tumeona vijana wengi wanaokwenda nje wanabadili mwelekeo kutoka kwenye elimu na kutafuta maisha zaidi unaliongeleaje hili?

Ni kweli kwamba vijana wengi wakifika Ulaya hubadili mwelekeo. Lakini mimi naweza kusema yote hii ni kwasababu ya ugumu wa maisha. Maisha ya Ulaya ni magumu sana ukichanganya na shule ndio yanakuwa magumu zaidi nahasa kwa wale ambao hawapati msaada wowote kutoka nyumbani.

Kwa kweli inataka moyo sana maana shule ni ghali, na maisha ni ghali, Ankara za mailipo ya huduma mbalimbali ni nyingi na bado nyumbani hawajakutumia mahitaji mbalimbali, kusaidia ndugu hapa na pale! kwakweli ni ngumu.

Kwa hali hivyo wengi wetu wanaishia kusimamisha masomo kwa muda fulani ili wafanye kazi kidogo wakusanye fedha za kutosha kabla ya kurudi shule.

Hapo ndio wengi wao wanajikuta hawarudi tena shule. Ukishaanza kufanya kazi na kupokea mshahara, kurudi tena shule inakuwa vigumu

Sio hilo tu pia wengi wetu tukiwa ulaya tunaona kama shule sio muhimu wengi usema sasa hata nikisoma ntaishia hapa hapa ulaya kufanya kazi hii hii, kurudi nyumbani siwezi kupata kazi hivyo wanapoteza ramani ya maisha kabisa.

Kwa hili nadhani serikali yetu pia inatakiwa kujaribu kutengeneza mfumo mzuri ambao utasaidia vijana kutapa motisha ya kurudi nyumbani na kuendeleza taifa letu .

Naamini kwamba watu wakijua kuna kazi nzuri nyumbani watakua wanataka kusoma nakumaliza ili warudi nyumbni. Jamani nani anaetaka kuishi nchi za watu? Kazi ngumu, maisha magumu, tamaduni tofauti.

Serikali yetu iliangalie hili kwaundani zaidi.

Swali: Tukirudi kwenye kipindi chako uliwaza nini kuwa na kipindi hiki na wapi hasa ni walengwa wako na kwanini umewalenga wao?

Kwakweli ilikuwa ni ndoto yangu, Ila nilipofika Uingereza nakuona jinsi ambavyo nchi zawenzetu zinamifumo tofauti ya kuelimisha jamii.. hii ilinipa motisha zaidi ya kutaka kutimiza ndoto yangu ndipo nilipoanzisha kipindi cha The sporah Show.

Ukizingatia kwamba hakukuwa na kipindi kingine cha Television kilichokuwa na dhamira kama yangu ya Kuelimisha, Kuburudisha na Kujulisha, haswa katika jamii yetu ya kiafrica huku Ulaya.

Tukiwa kama waanzilishi wa African Talk show hapa Uingereza, na Europe kwa ujumpla. Namshukuru Mungu muitikio ulikuwa mzuri hivyo kunipa morali zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi.

image

Sporah akiwa kazini akiongea na Miss Ugandan Uk.

Swali: Unawezaje kupima mafanikio ya dhamira yako kwa kupiatia Sporah Show, I mean unafikiri ulilotaka limetimia?

Oooh Nooo!!!

Bado kabisa sijafikia lengo langu.

Lakini namshukuru Mungu kwa sasa nimeweza angalua kutimiza ndoto yangu japo bado sijafikia malengo yangu lakini naamini nitafika kwani mwanzo ndio unakuwaga mgumu. Pia namshukuru sana Mungu kwani kwasasa nawenza kusimama nakuongea nakusikilizwa na watu kupitia kipindi changu (The Sporah Show) hapa UK na Europe kwakweli majibu ni mazuri, nafarijika sana kuona hivi.

Safari bado ni ndefu kwani ndoto yangu ni kipindi cha Sporah Show kuonekana Mataifa yote duniani. Dhamira yangu ni kuelimisha, Kuburudisha na kujulisha dunia kwaujumla haswa vijana wa ulimwangu huu wasasa.

Swali: Muitikio wa Vijana ukoje kwa ujumla kuhusu kipindi chako, unapata feedback zozote kama ni negative au positive feedback?

Kwaweli muitikio ni mzuri sana tu.

Namshukuru Mungu tunapata support nzuri kutoka kwa vijana hivyo kuturahisishia kazi kidogo.

The Sporah Show inawapa vijana nafasi yakuja kuonyesha vipaji vyao na pia inatoa nafasi kwa wafanya biashara kuzitangaza biashara zao kupitia kipindi chetu.

Swali: Kumekuwa na malalamiko ya maporomoko ya maadili kwa vijana, hili unalizungumziaje ukiwa kama muelimisha rika katika jamii, nani hasa wa kulaumiwa?

Wow!! Swali zuri

Kwakweli tatizo la maadili kwa vijana ni kilio cha dunia nzima, hata kwenye zile nchi ambazo zilikua zinafuata tamaduni zao.

Vijana wamekuwa wakipata pear pressure kutoka kwenye TV na Magazine, hivyo wanajikuta wanaingia kwenye makundi mabaya

Watoto wengi wanakua wakiiga vitu kutoka kwenye magazeti na television na nakuanza starehe wakiwa na umri mdogo. Kwahiyo nadhani pia wazazi wanatakiwa wawe makini kidogo na wasitupe tamaduni zetu. Ni vizuri sana kuwalea watoto namaadili mazuri mpaka watakapokua wakubwa ndipo wachague maisha yao wenyewe.

Tukirudi kwenye upande wanani wakulaumiwa!

Binafsi nadhani wazazi wana jukumu kubwa katika jambo hili. Wazazi wanatakiwa wawafundishe watoto wao maadili mazuri wakati wakiwa wadogo kama tamaduni zetu, hivyo watoto pia watakuwa wakijua wanatakiwa kufuata maadili mazuri na hivyo wataendeleza turidhisha kizazi hadi kazazi. Kwani wazazi wasipo fanya hivyo watoto hawatakuwa na kitu cha kufundisha watoto wao na hivyo kizazi chote kitateketea na mmomovyoko wa maadili

Pia upendo nikitu cha muhumu sana kwa watoto, wazazi wajaribu kuwaonyesha watoto wao upondo ili wasiende kutafuta upendo nje. Na pia wazazi wanatakiwa kujua kwamba kumuonyesha mtoto upendo haina maana kumpa mtoto uhuru wakufanya chochote anachotaka.

image

Sporah akiwa na mdau

Serikali pia inajukumu kumbwa katika jambo hili ili kushirikiana na wazazi.

Serikali ingejitahidi kuhakikisha kila shule inakua na angalau masaa mawili ya vipindi vya tamaduni na michezo kwa watoto ili kudumisha tamaduni zetu. Bila kusahau serikali inatakiwa kusaidia mashuleni vifaa vya michezo na mambo mengine mbalimbali ili kuwapa watoto vitu ambavyo watakumbuka wakiwa wakumbwa na kuwa nakitu chakujivunia kwa mataifa mengine.

Swali: Katika vipindi vyako ni kipindi gani ambacho ulitengeneza hadi mwenyewe ukakikubali na kwa nini?

Nivingi kwakweli ila naweza nikasema KNIFE & GUN CRIME IN THE UK (Uhalifu wa kutumia visu na silaha)

Hii ni kwasababu, tuliungana na vijana ambao walikua wanabeba silaha na waadhirika wa jambo hilo na wazazi waliopoteza watoto wao kupitia GUN &KNIFE CRIME (Uhalifu wa kutumia visu na silaha)

Kwakusaidiana na Wazazi tulijaribu kuelimishana adhari za jambo hili, watu wengi sana walielimika kuhusu jambo hili na vijana wengi walijitokeza kuelezea jinsi gani walivyo adhika na kwamba wameacha nawameanza maisha mapya. Kwakweli nilijisikia vizuri sana kuona hivyo kumbe na weza kubadisha maisha ya watu kwa kupitia kipindi changu.

Unaweza kuangalia video hiyo na nyingine nyingi kupitia YOUTUBE kwawanaotaka kuangalia video hizo ziko kwenye YOUTUBE.. www.youtube.com/sporahshow (Gonga Player kupata mambo)

10. Kwangu mi nakuona kama umefanikiwa hasa kwa ambacho unakifanya ukizingatia uko nje ya nchi kazi ambazo mara nyingi tumeona vijana wa mataifa mengine wakizifanya, je unaweza kusema ni nini siri ya mafanikio yako kwenye hilo?

Asante sana.

Kwakweli hakuna kingine zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi zangu zote na pia kuwa na watu wazuri na wenye upendo wakweli.

Kama unavyojua vitu kama hivi ulaya vinafanywa na watu wamataifa makubwa hivyo mimi Sporah kufanya kitu kikakubalika na watu natakiwa kufanya mara 10 ili kuweza kukubalika na mataifa mbalimbali hapa UK na Europe kwa ujumla.

Nimepoteza marafiki wengi sana, kwasababu nimekuwa busy nafanya kazi wakati wote na kuendesha kipindi sio kazi ndogo. Wakati mwingine najisikia vibaya kupoteza marafiki lakini nakua sina jinsi kwani hii ni ndoto yangu hivyo ni faraja kwangu kuitimiza.

Swali: Uliwahi kuwaza kuwa na kipindi kama hiki kwa Television za nyumbani?

Absolutely yes … Nimeshakuwa approched na TV station tofauti za nchi za Africa.lakini bado sijaamua nianzie wapi, kwasababu bado niko shule hivyo najaribu kuipa shule kipaumbele mpaka hapo ntakapomaliza. Lakini nyumbani muhimu… Hahaaa SPORAH SHOW lazima ije nyumbani.

image

Sporah akiwa na baadhi ya wadau katika jitihada zake za kuongea na watu mbali mbali.

 

Swali: Unalizungumziaje suala la uhuru wa habari kwa sehemu unayoifanyia kazi na nini mipaka yako? Ukilinganisha na hali ilivyo nyumbani unadhani tuko sawa?

Kwakweli sina uhakika sana maana sijawahi kuwa kwenye media nilivyokua nyumbani

Ila nadhani kutakuwa na tofauti kwani huwezi fananisha nchi za ulaya na nyumbani tofauti ni kubwa sana kwenye mambo mengi .

Swali: Katika Production zako kuna mahali uliwahi kukwazwa au kupata matatizo yeyote kutokana na kipindi ulichotengeneza au wakati wa kutengeneza kipindi?

Hapana

Swali: Unaizungumziaje nafasi ya mwanamke wa Kiafrika kwenye Ulimwengu wa habari?

Mimi binafsi naona wanawake wanauhuru katika katika ulimwengu wa habari kama alivyo mtu mwingine. Kama mwanamke anaweza kulea mototo akaja kuwa Raisi, Mbunge, Daktari, mwalimu na Mwanasheria!!! Then kwanini wasipewe uhuru kwenye ulimwengu wa habari?

Swali: Kwa mfano ukapewa nafasi ya kumshauri Raisi kuhusu vijana kwa Tanzania ya leo, yapi utayapa umuhimu?

· The fact are on an annual basic, Tanzania is loosing thousands of young Intelligent, Talented and hard Working into Western world for studying reasons…..

The question is how many of these do come back home? And why don’t they want to come back to home….?

Hinyo ushauri wangu kwa Mheshimiwa Rais ungekua ni kuangalia jambo hili kwa undani zaidi.

image

Sporah akiwa mmoja wa majaji kwenye mashindano ya Miss Central Afrika.

Swali: Who is your role model na kwanini?

Must be… Mama yangu na Dada yangu.

Kwasababu wamenilea viziri nakunipa maadili mazuri ambayo yananiwezesha kuishi nawatu vizuri na hasa kufika hapa nilipo leo hii. Nawapenda sana.

Swali: Vijana wengi wamekuwa wakikimbilia nje ya nchi kwenda kutafuta maisha huko na wengi wamekuwa wakiondoka kwa gia ya kutafuta shule zaidi lakini kiukweli wengi wao wanaishia kutafuta maisha kwa kufanya kazi za vibarua na si elimu, kwa uzoefu wako wa maisha ya nje hili unalizungumziaje?

Kwakweli, nitarudi tena kwenye serikali nadhani serikali inatakiwa kuliangalia jambo la ajira vizuri.

Watu kungangania ulaya na kufanya kazi zakubeba mabox na elimu zao (Degree, Masters, PHD’s) ni kwasababu ya ukosefu wa ajira nyumbani na hali ngumu ya maisha

“People feel like they cant achieve anything back home other wise you have good connection and people you can trust in the high sector. Otherwise there is no light after the tuner”

Hivyo serikali inatakiwa kutafuta nyenzo rahisi kuwaraisishia vijana kupata kazi bila kuwa na hofu yakwamba natakiwa nimjue fulani ili kupata kazi.

image

Ni vizuri kuzungumza na vijana na hasa wakiongea na kijana mwenzao kwani huondoa uoga na kuwafanya wawe huru zaidi kuongea.

Swali: Nini matarajio yako ya baadaye

Sporah Show kuonekana dunia nzima.

Swali: Mwisho kabisa napenda tu kujua interest zako.

Mimi ni muumini mzuri hivyo na penda kwanda kanisani na pia I like to learn new things.

Swali: Kama una lolote la kuongeza please do,

Ningependa kukushukuru sana kwakunipa nafasi hii.. na pia natanguliza shukurani zangu kwa watanzania wote kwaujumla kwakunipa support katika kazi yangu. Bila kusahau washabiki wangu wa FACEBOOK, TWITTER. Asanteni sana, naningependa kuwakaribisha wengine wote ambao hawajajiunga katika my FACEBOOK ambayo ni THE SPORAH SHOW au SPORAH NJAU.

Namwisho ningependa kuitambulisha The Sporah Show kwa wote na hasa kwa wafanya biashara na Makapuni yanayohitaji kujitangaza Uingereza, Europe Asia, Middle East and Africa, .

The Sporah Show, which is an African Talk show that airs on SKY 184 Every Monday at 10:30pm on BEN Television.

BEN TV is the Europe’s first and biggest black satellite TV channel on Sky 184 which also received in Asia, Middle East and Africa

We are respectfully inviting your Company to use this great opportunity to showcase its services by way of Sponsorship or Advertisements during the programme.

Read the rest of this entry »


Swali toka kwa Lady Jay Dee

January 27, 2010

Hivi hizi suruali za vijana wa siku hizi zinavaliwa robo mwili??? Unaweza kudhani inakaribia kuanguka na sijui kwa ndani huwa wanashikiza na nini hadi inaweza kuning’inia bila kuanguka..Au wanashikiza na pini??

Mtembelee Binti Machozi kwa kubofya hapa


Mambo ya Sweet Eazy jumamosi hii

January 27, 2010

Saturday Night Live & Sweet Eazy Oysterbay present:

Lady Jay Dee & Machozi Band

This Saturday, 30 January, 9pm-2am.
Reservations: 0755 75 40 74.

See below flyer for details.

Sweet Eazy Oysterbay, for the Best Live Music – Every Thursday & Saturday.

image


Wallah Mombasa laha bwana..!!!

January 26, 2010

Ilikuwa ni fainali ya kucheza Chakacha iliyofanyika Novemba 2009 huko Mombasa ambapo washiriki walionyeshana jinsi ya kulisakata Chakacha. angalia pichani kisha gonga player upayte mambo.


Misri nusu fainali, yaipiga Cameroon 3-1

January 26, 2010

image

Mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Misri jana walifanikiwa kuwatoa Cameroon katika mchezo mkali na wa kasi.

Misri wameitandika Cameroon 3-1 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika na kujiweka vizuri kuwania ubingwa wa saba wa Afrika.

Katika mechi iliyochezwa dakika 120, Cameroon ndiyo walianza kupata goli, wakati Cameroon walipojenga mashambulizi yaliyosababisha kona ambayo Achille Emana aliimalizia.

Baada ya hapo, Misri walicharuka na kusawazisha kupitia kwa Mohamed Gedo na Ahmed Hassan aliyefunga mawili.

Mechi hiyo ilichezwa dakika za nyongeza baada ya kumalizika 1-1 wakati wa muda wa kawaida.


Staring into the jaws of death

January 25, 2010

This young wildebeest found itself staring straight into the jaws of death as it crossed a river in search of food.

The animal had become separated from its family when this giant croc took a fancy to it.

But luckily for the ‘beest the toothy reptile mistimed its deadly attack by a fraction of a second – and was left with a mouthful of water.

Amazingly the juvenile wildebeest then managed to wriggle away from the croc and scramble to safety up the bank of the Mara River in Kenya.

The stunning snap was taken by British holidaymaker Austin Thomas, 43.

Mr Thomas said: "You could say they are holiday snaps with a bit of bite!"

the Sun


Kings and Queens AY….

January 25, 2010

Gonga Player upate uhondo

…………………………………………………………….

King and Queen, kama unakumbuka The King of zamunda basi ngoja uone Video hii ya Mwanamuziki AY ndio utakubali kuwa kijana kajipanga.

Hatimaye ile Video ya Wimbo wa KINGS AND QUEENS aliyomshirikisha JOKATE & AMANI kutoka KENYA.Wimbo umetayarishwa na na Super Producer HERMY B ndani ya Studio ya B.Hitz Music Group na kufanyiwa video na OGOPA DEE JAYS toka Kenya.Video imefanyika Jijini Nairobi Kenya.

“Wimbo huu nimejaribu kufikisha fikra zangu kuwa MWANAMKE WA KIAFRIKA NDIE BORA KABISA NA NAJISIKIA FAHARI SANA KUZALIWA NAO NDANI YA BARA MOJA” alisema AY kwenye taarifa yake kwenda kwa wanahabari na Ma blogger mbali mbali ikiwemo Spoti Starehe.

Binafsi namkubali sana kijana AY kwa ubishi anaoonyesha kwenye game, wapo walioanza na waliishia njia na wapo walioanza na wapo kwenye safari, Muziki ni Jihadi, unatakiwa kujitolea na endapo utaheshimu kazi yako basi unayonafasi ya kufika mbali.

Big up kaka unaonyesha ubunifu na ukomavu kwenye fani na kuwa mfano wa kuigwa.


TID, Chid Benzi waua katika track inayokwenda kwa jina la “Huyu”

January 25, 2010

tidchid

Kuna Collabo wallah ukitajiwa unakuwa unapenda kuzisikia hasa hii ya TID na Chid Benzi.

TID akiwa na kipaji kikubwa cha kuimba na Chidi akiwa na kipaji kikubwa cha kunata na Vina kwenye Rap. Wimbo huo ambao Spoti na Starehe imepata bahati ya kuupata ikiwa ni wasikilizai wakwanza kusikilizishwa toka jikoni kwa CEO wa Tetemesha RecordsSandu George Mpanda aka Kid Bwoy.

Tetemesha Records ndio waliowatoa Hussein Machozi na Sajna. Kwa mwana 2010, Tetemesha Records wamefungua mwaka kwa truck hiyo na nyingine toka kwa Syntax akimshirikisha Rama D inaitwa Usiniuze.


Stoke yaipiga kumbo Arsenal katika FA

January 25, 2010

Wachezaji wa Stoke

Stoke itaendelea katika raundi ya 5 ya FA

Ricardo Fuller aliweza kutumbiza mabao mawili wavuni, na kuisaidia timu yake ya Stoke kujitengea nafasi katika mechi za raundi ya tano ya Kombe la FA, raundi ya tano, kwa kuishinda Arsenal 3-1.

Ricardo alimharibia kabisa mchezo Sol Campbell katika mechi ya Jumapili.

Mlinzi Campbell alikuwa ndio tu amerudi tena katika timu yake ya zamani ya Arsenal, akiichezea tena timu hiyo mechi yake ya kwanza.

Bao la tatu la ushindi la Stoke lilikuwa ni jitihada za Dean Whitehead.

Katika mechi nyingine ya FA siku ya Jumapili, licha ya ushindani mkali, Scunthorpe haikuweza kuvumilia vishindo vya Manchester City, na hatimaye ilishindwa kwa magoli 4-2.


Drogba kurejea nyumbani baada ya kutolewa na Algeria

January 25, 2010

image

Algeria iliitandika Ivory Coast mabao 3-2 katika mechi ya kufana zaidi kiasi cha kulazimu muda wa ziada.

Timu zote zilionekana kujibizana vilivyo pale kipindi cha kwanza kilipomalizika 1-1.

Baada ya mapumziko Ndovu wa Ivory Coast walirudi na kishindo na mnamo dakika ya 89 mshambulizi Kader Keita alitimua zinga ambalo wengi walidhani limeamua nani ataingia nusu fainali.

Lakini Madjid Bougherra hakusita kuiadhibu Ivory Coast na hivyo kulazimu mechi kuingia muda wa ziada.

Hameur Buoazza alifunga bao la ushindi.


Wawili watemwa Maisha Plus

January 24, 2010

IMG_0283

Washiriki waliopigiwa kura ya kutoka wakiwa kizimbani huku wakisubiri hukumu yao kijijini leo usiku.

Washiriki wawili leo wametemwa katika kijiji cha Maisha Plus na kufanya jumla ya washiriki wanne mpaka sasa kuwa wameshatoka kijijini.

Mshiriki toka Iringa Shauri ndiye alikuwa wa kwanza kutajwa na Babu kisha na kufuatiwa na Abdul mshiriki toka mwanza huku mshiriki mwenza toka Dar Es Salaam Kaushiri akiponea tundu la sindano kwa mara ya pili.

IMG_0274

Hata hivyo Kaushiri ndiye aliyepata kura nyingi huku akifuatiwa na Abdul na Shauri aka Mama Afrika. Awali kabla ya babu kutaja majina, washiriki walitoa burudani ambapo Abdul alionyesha uwezo mkubwa wa kuigiza kwa hisia, lakini Abdul alionyesha kuwachosha zaidi washiriki wenzake kwa kupigiwa kura nyingi zaidi za kutoka toka kwa washiriki wenzake.

Leo hii washiriki waliobaki watakaa na kuchagua viongozi wapya.


Asamoah Gyan awafungisha virago wenyeji Angola

January 24, 2010

image

Asamoah Gyan, Muuaji wa Angola

Wenyeji Angola leo wamefungashwa virago kwa kufungwa bao moja na Ghana katika mchezo mzuri na wa kasi uliohudhuriwa na Rais wa Angola.

Hata hivyo wenyeji walipata nafasi nyingi ambazo watazijutia kwani walishindwa kuzitumia.

Soma hapa zaidi


Goli la mwaka

January 24, 2010

A beautiful goal from Jamie Milligan, captain of non-league side Fleetwood Town against Farsley Celtic to help them go top of the table in the Blue Square North. Milligan took advantage of a clearly lost goalkeeper who was just asking for trouble, blasting a shot from inside the center circle that dropped in the back of the net over the out of place keeper’s backward-diving reach like a grenade in a foxhole (topical WWI reference for you there).


Mwanadada Caroline Nderitu

January 23, 2010

image

Anaitwa Caroline Nderitu, huyu mdada ni raia wa Kenya ambaye amejizolea umaarufu kwa uwezo wake mkubwa wa Maishairi na kwa sasa anakitabu chake cha Poetry kinachoitwa Love Only. Utayajua mengi kuhusu mwanadada huyu hapa hapa Spoti na Starehe.

image


%d bloggers like this: