Weekend njema na Blandine ya Le Roi De La Forret Ngiama Makanda.

September 27, 2013

Kwangu Kibuisa Mpimpa na Solola Bien zinabaki  kuwa ni moja ya albamu bora kabisa Werasson na WMMM kutengeneza tangu aachane na Wenge Musica.

Anaitwa LE ROI DE LA FORRET” NOEL NGIAMA WA MAKANDA a.k.a.WERRASON hii ilikuwa kipindi chake cha mwanzo cha kujitawala alipotoka na album yake ya Kibuisa Mpipa kama sijakosea maana hii ilikuwa ni Bonus Truck. Wakati huo bado akiwa na wataalamu wake kama akina Ferre na bado hajakimbiwa na wanamuziki wengi ambao kwa sasa wanatamba sana.

Wimbo huu aliuimba kwa mahadhi ya Congo Rhumba, Ikumbukwe kuwa albamu hii ni mapishi ya Producer hatari mtaalamu  L. NZIMBI huyu ndiye mpishi wa albamu ambayo mpaka leo inauza ya FEUX DE L’AMOUR” yakwake Jemedari SOUVERAIN LEADEUR YA BA WENGEE JB Mpiana ambayo aliitoa kama solo enzi kundi la Wenge Musica BCBG halijaparanganyika.

Huu ni moja ya nyimbo ambazo mimi binafsi Werasson amenifurahisha na kama ningepata nafasi ya kukutana naye na kumshauri ningemshauri a stick kwenye nyimbo hizi za taratibu.

Kitu inaitwa Blandine wakati huo wa Kibuisa Mpipa, Ni wimbo ambao huku kwetu hauku heat lakini ni moja ya nyimbo ambazo nazipenda sana kwa Werrason, Kwa ufupi angalia nyimbo zinazombeba zaidi Werasson ni nyimbo hizi za taratibu zenye mahadhi ya Congo Rhumba ambayo Mkongwe JB Mpiana ni champion kwenye hizo najua ma werasonique mtabisha kwa hili lakini ni wazi na halipingiki.

Truck hii nilimsikilizisha Papaa Mabamba Abiud Maregesi weekend hii na akaniomba niiweke tena, Nimefanikiwa kumbadilisha huyu jamaa imani na mapenzi ya muziki pia ni maalum kwa Mukubwa Stephen Masere, Lubonji wa Lubonji heshima kwako sana, pamoja na Ma-Werasonique wooote Sadiq Tiger, Papaa Maendeka, Boss Chizenga, Moto Mkubwa Halid Mmanzi, Mdau wangu Steven na wapenzi wote wa Blog hii, Mukubwa Hadji Heshima kwako kiongozi na mnazi wa Wenge bila kukusahau Richard Malewa na mamaa Gladys Titanike nakati ya Kibo Poutry Moshi One Love Mameree.

Ijumaa Karim


Ferre Gola Kichaa akimshirikisha Heritier Watanabe katika Nostalgie

September 27, 2013

Haina ubishi kwa sasa anaweza kutangazwa kama mfalme wa Rhumba kwa Congo, Ferre Gola ameweza kwa kiwango kikubwa sana kukonga nyoyo za mashabiki wa Rhumba ambao tangu kufariki kwa mtu akama MAdilu System walijiona wapweke, wapo wanamuziki wengi ambao kwa kiasi kikubwa wanajitahidi kupiga Rhumba lakini kwa kiasi kikubwa Ferre ameweza. Swaiba wangu Ally Juto aka Ally Tandika, Ally Magari anamkubali sana Ferre Gola nadhani hapa nimefikisha.

KWenye wimbo huu anashirikiana na kijana mwingine ambaye binafsi namkubali sana anaitwa Heritier Watanabe toka Wenge Musica Maison Merre ya Werasson, kijana huyu kwa wafatiliaji wa muziki wa Congo na mashabiki wa Congo watakubaliana na mimi kwamba huyu ni moja ya animation ya WMMM.

Sikiliza kolabo yao hapa na unipe maoni yako,


“Ngulu” Biashara iliyowatajirisha wanamuziki Congo

September 27, 2013

Kwa wacongomana neno Ngulu si geni masikioni mwao ila kwa mashabiki wangu wa Spoti na Starehe inawezekana neno hili likawa geni masikioni mwenu. Bila kuuma maneno neno ngulu linamaanisha Nguruwe ila ni msamiati ulnaotumiwa kwa Wahamiaji haramu ambao wanabebwa kupelekwa Ulaya kwa kivuli cha wanamuziki.

Kwa miongo kadhaa wanamuziki wa Congo wanaongoza kwa wanamuziki wanaotoka barani Afrika kufanya maonyesho mengi Barani Ulaya na America. KWa Vijana wa Congo ndoto zao ni kufika ama Ubelgiji au UFaransa, hii ni kutokana na historia ya nchi hii kutawaliwa na Wabelgiji na lugha wanayotumia kuwa ni Kifaransa.

Masharti ya kungia nchi za TShengeni sio rahisi lakini ni nchi ambazo zinapenda sana burdani na hasa utamaduni jambo lililofanya kwa wanamuziki na vikundi vya dini kwenda kutoa burudani huko mara nyingi, mwanya huo ndioo ulikuwa unatumiwa kuwabeba hawa Ngulu na kuwabwaga huko wakiingia kwa hati za kusafiria na vibali vya kuingia (VISA) kama wanamuziki.

inasadikiwa kuwa kwa wastani kila Ngulu mmoja alikuwa akilipa kati ya dola 3500 USD na 5000 USD kufanikisha safri yake ya kufikishwa ulaya na inasemekana kuwa Bendi moja alikuwa ikiondoka na Ngulu 10 mpaka 15. “ulichotakiwa kufanya ni kufanya mazoezi ya awali ya muziki ama kupiga vyombo, kwani utasajiliwa kama mwanamuziki mpya utafanya mazoezi ambayo utayatumia kutumbuiza jukwaani ukifika Ulaya na baada ya shoo unaondoka kivyako” kilisema chanzo cha habari hii nilipokuwa nikiongea naye kubadilishana mawili matatu ya muziki huu wa Congo karibuni.

Si lazima uimbe tuu kwani wakati mwingine waliwachukua vijana na kuachana nao wakifika Airport nchi husika na hapo unaanza kutafuta maisha, kuna wengine unakuta walikuwa na ndugu au jamaa huko na hao huwapokea na kukuonyesha jinsi ya kuishi huko baada ya muda huachiwa na kuanza kutafuta kivyao.

wengi wa Vijana ambao wako Ufaransa ama Ubelgiji ambao wanaitwa Le Combatant (Bana Congo) ni matokea ya wazamiaji ambao wengine bado hawaishi kihalali na wengine wameshakamilisha makartasi na sasa wanaishi kihalali lakini walikuja Europe kwa njia za panya aliongeza mpashaji habari wangu. kwa wasiojua tu hawa Bana Congo ndio vijana wanaoishi huko nje (Diaspora) na wanapinga siasa za Congo za Joseph Kabange Kabila, vijana wanaotaka mageuzi kwa siasa za Congo na kupingana na yeyote anayemuunga mkono Kabila na utawala wake.

Wanamuziki wakubwa kama Papa Wemba na Felix Wazekwa wao kwa nyakati tofauti waliwahi kuhukumiwa na kufungiwa Visa za Kuingia Tshengeni kwa shutuma za biashara ya Binadamu (Ngulu), pia kashfa hiyo haiwaachi Bozi Boziana, Nyoka Longo, JB Mpiana, Werasson na hata Koffi Olomide wao pia wanasemwa kujihusisha na biashara hii ambayo kwa kiasi kikubwa imechangia utajiriri wao. February 6 2012 Mwanamuziki Papa Wemba alihukumiwa kifungo cha miaka 15 ama kulipa faini ya Euro 20,000 kwa makosa yanahusiana na hayo.

Kwa sasa wengi wa wanamuziki hawa wanasema kuwa kwenye hali ngumu kifedha kwani hawana show za Ulaya ambazo zilikuwa zikiwalipa pesa nyingi, wengine kwa kunyimwa Visa na wengine kutokana na mahusiano yao na Bana Congo kwa kuwa walimuunga mkono Rais Kabila. Takribani wanamuziki wote wenye majina makubwa walishiriki kwa namna moja ama nyingine kumpigia kampeniRais Kabila ambaye alishinda na kurejea madarakani jambo lililopingwa vikali na Bana Congo na leo hii wanalipa gharama za usaidizi wao.


Werason na JB Kukutana Zenith?

September 25, 2013

Baada ya takribani nusu muongo toka watumbuize Zenith JB Mpiana na kundi lake la Wenge BCBG na Werason na kundi lake la WMMM inawezekana kwa mara ya kwanza wakapanda jukwaa moja.

kwa mujibu wa habari ambazo Spoti na Starehe imezipata kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa waandalizi wapo kwenye mazungumzo ya awali kutaka kuzikutanisha bendi hizi mbili mahasimu kwenye onyesho la Zenith. Werasson na WMMM tayari wamepata VISA za Tshengen huku JB Mpiana na Vijana wake onyesho lao likiwa tayari limekubalika kufanyika na tarehe ya onyesho la BCBG ni tarehe 21 December.

“wanakubaliana kuhusu kupanda jukwaa moja kwani WMMM nao wamekubali onyesho lao liwe la kuchangia waathirika wa vita mashariki mwa Congo kama JB Mpiana” kilisema chanzo hicho. Kama hili litafanikiwa itakuwa ni ndoto ambayo mashabiki wengi walikuwa wakiisubiria. Zaidi ya mara mbili mipango ya onyesho hili linashindikana. JB Mpiana na Werasson wote kwa pamoja wana Single ziko sokoni kwa sasa na zote zinafanya uzuri, hivyo tunategemea watatupatia burudani ya kipekee.


JB Mpiana kutumbuiza ZENITH Dec 21

September 25, 2013

baada ya kimya kirefu mwanamuziki JB Mpiana na kundi la Wenge BCBG watatumbuiza kwenye onyesho kubwa la Zenith Dec 21, kwa mujibu wa Rodger Ngandu mipango ya awali ya onyesho hilo imeshafanywa na kwa sasa walikuwa wameshapata VISA za wanamuziki kadhaa na nyingine zinashughulikiwa.

JB Mpiana na Wenge watatumbuiza katika onyesho la kujitolea ambalo nia yake ni kuchangia waathirika wa vita vinavyopiganwa Mashariki mwa Kongo, “….ni onyesho la kuchangia waathirika wa vita mashariki mwa Congo kwani ndugu zetu wanapata taabu, watoto wameachwa yatima, akinamama wamebakwa na wote wanahitaji msaada wetu” alisema Ngandu. Onyesho hilo ambalo limeitwa Tamasha la Amani nia yake kubwa ni kusambaza ujumbe wa amani.

Kwa muda mrefu JB Mpiana na kundi la Wenge BCBG walikuwa hawajafanya onyesho lolote Tshengen iwe Ufaransa au Ubelgiji wakihofia vitisho toka kwa kundi linalojulikana kama Bana Congo (Lecombatent) ambalo linapingana na siasa za Rais Laurent Kabila likitaka mageuzi nchini Congo. Kwa mujibu wa habari za ndani inasemwa hii ni baada ya kufanyika makubaliano kati ya waandaaji, Uongozi wa BCBG na Bana Congo na kukubaliana kimsingi kuwa JB Mpiana anaweza kufanya Show hiyo.

inatazamiwa onyesho hili litakuwa kubwa na mashabiki toka jumuiya ya Ulaya.  kwa sasa Wenge BCBG wanafanya mazoezi ya onyesho hilo huku wakimalizia albamu yao mpya ya Balle de match.

Naomba nikukumbushe kidogo onyesho la Zenith 2009 lilivyokuwa.


Education ISIPA; Single mpya ya Werason inayoasa kuthamini elimu.

September 25, 2013
Video hii Werasson akishirikiana na Mohombi wimbo unaitwa Ifound a Way

Video hii Werasson akishirikiana na Mohombi wimbo unaitwa Ifound a Way

Mwanamuziki Werasson Ngiama Makanda ameachia Single mpya ijulikanayo kama Education ISIPA, Werason ambaye anatamba na albamu yake sokoni amesema kuwa bado anajiona anajukumu la kufanya kwa vijana wa Congo na ndio maana ameachia kibao hicho akiwahusia vijana kuthamini elimu ambayo kwa kiasi kikubwa vijana wamepuuzia hasa ukizingatia Congo imekuwa na machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe jambo linalopelekea vijana wengi kujiingiza kwenye vikundi vya vita.

Werasson ambaye ni balozi wa amani wa UNICEF amekuwa akishiriki kutunga nyimbo kwa ajili ya kuwabadili vijana wa Congo na kuwafanya wathamini nchi yao badala ya kugeukia mavita.

majuzi Werason aliitambulisha Single yake hiyo kwenye mji wa Bandundu na kuwachanganya kabisa mshabiki wake. Werason alifanya show mbili tarehe 21 na 22 katika mji huu muhimu ambao kwa sasa kila mwanamuziki Congo anakimbilia kufanya show. watu walikuwa nai wengi na walifurahi sana kumuona mtu wao alisema le Big Manager Monib production ambaye ni mkurugenzi mauzo na masoko wa WMMM.


Anaconda na Fally Ipupa

September 25, 2013

1235327

Ukitaka kujua ugumu ama urahisi wa kumiliki bendi muulize Muumin Mwinyijuma atakwambia na Tamtam yake, Muulize Asha Baraka na Twanga yake, Muulize Engineer Martin Kasyanju na Ngwasuma yake ama Muulize Ally Choki na Extra Bongo yake.

Lady Jaydee aka Binti Machozi ni mwanamuziki ambaye kama ni kuchora chati ya mafanikio utaona inaanzia chini kabisa na ikienda ikiongezeka kila uchao, tangu amemiliki bendi kuna mara kadhaa amejaribu kuhujumiwa bila mafanikio na anazidi kusonga tuu. Pichani akiwa jijini Nairobi na Mwanamuziki Mahiri Fally Ipupa De Caprio ambaye naye anapasua anga si tu la Africa bali duniani, hii ilikuwa jijini Nairobi, ilikuwa kitu gani? Je wana program pamoja? tega sikio hapa hapa utapata jibu lako. 


CAR FOR SALE: SUZUKI SWIFT 2005 MODEL

September 22, 2013

IMG-20130912-WA0006

IMG-20130912-WA0007

IMG-20130912-WA0008

IMG-20130912-WA0009

60,000 KM

2005 Model

Imetunzwa vizuri sanaaa

Ilinunuliwa 11 Million inauzwa 8.5 Million mwenyewe anasafiri.

Piga simu No. 0713 666616 au 0785 666616 (Haina Udalali)


Kutoka Albamu ya Soyons Serieux, Sikiliza masauti

September 22, 2013

Swaiba wangu Maz aka Mabamba anasema ukitaka kupata ladha ya Kwaya basi usikilize nyimbo za JB Mpiana na Wenge yake, nakubaliana naye kwa asilimia 100 kuna mahali huwa natamani kama hizi nyimbo zisichanganye.


Fally avunja rekodi!!

September 6, 2013

Mwanamuziki wa kizazi cha tano cha muziki wa Congo Fally Ipupa kwa sasa ndiye Mwanamuziki anayeongoza kwa kuwa na Show nyingi kuliko wote.

Habari zinasema toka aanze shughuli za muziki akiwa kama solo artist, Fally Ipupa kwa mwaka huu hajawahi kukaa Congo zaidi ya Wiki bila kupata mualiko ama ndani ya nchi ama nje ya nchi, Majuzi Fally Ipupa ametoka nchini Amerika ambako alikwenda kwa ajili ya kufanya shooting ya Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake mya ya Power ambapo amemshirikisha mwanamuziki R.Kelly humo ndani.

Wiki hii tarehe 6 September mwanamuziki Fally Ipupa atakuwa na show ya kufa mtu itakayofanyika katika ukumbi wa bwawa la hoteli ya Grand Hotel huko Kinshasa onyesho lililopewa jina la Power.

Fally amecukua Tuzo za uandishi na tungo zake mara tatu za Droit chemin ,Arsenal de belles mélodies et Power, kosa, leka, hii imemfanya aweze kuwa na maonyesho mengi ndani na nje ya nchi, sababu ya pili ni kuwa Fally hafungamani na upande wowote kwenye siasa za Congo jambo linalompa nafasi ya kupata mialiko ndani na nje ya Congo hasa Ufaransa na Ubelgiji ambako kuna Wacongoman wengi na mashabiki wengi wa muziki huu wa DRC.


The Dream Team

September 6, 2013

969841_10200506351209442_509519880_n

Kama ni kikosi hapa kilikuwa kimetimia kabisa Binafsi siwakumbuki wote najua wadai Le Beceebeegeeque nipe majina mdau…!!!


%d bloggers like this: