Ticket za kuona mashindano ya Kombe la Dunia mwakani huko Afrika ya Kusini zinaanza kuuzwa leo huko nchini Afrika ya Kusini kwa mbwembwe za aina yake ambapo tiketi ya bei ya chini ni Tsh 27,000/=
Leo hii waganga wa jadi na wananchi wapenda michezo walikutana huko Port Elizabeth kwa ajili ya kutambika kwenye moja ya kiwanja ambacho kitatumika kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa ya soka.
Maafisa wanasema wananchi walioko nje ya Africa ya Kusini watatumia mtandao kukata Ticket hizo na wale walioko ndani watanunua tiketi kwa kutumia fomu maalum ambazo zinapatikana kwenye Benki ya FNB National Bank ambayo imezagaa nchini kote.
Maofisa wanasema kuwa mipango yote imekamilika na sasa hii itawapa mtazamo wa mapokeo toka kwa mashabiki.
Michuano ya Kombe la Dunia inatazamiwa kuanza mwakani huko nchini Africa ya Kusini.
Bei ya Ticket iko kama ifuatavyo:-
Siku ya Fungua dimba: $200-$450.
Mechi ya raundi ya kwanza: $80-$160.
Round of 16: $100-$200.
Robo fainali: $150-$300.
Nusu fainali: $250-$600.
Fainali: $400-$900.