Luiz Felipe Scolari
Klabu ya Chelsea ya Uingereza hatimaye imesitisha kibarua na kumfukuza kazi kocha wake Luiz Felipe Scolari hapo jana. Kocha huyo m-Brazili mwenye umri wa miaka 60 ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kupata mafanikio na Timu za Taifa mbalimbali ikiwemo Portugal ambayo alitokea ameshindwa kuwafurahisha matarajiri wa Chelsea na kufanya aendelee na kibarua.
Scolari ndiye aliyewapandisha Brazir huko Japan mwaka 2002 na kuwasimamisha Uingereza kwenye robo fainali kwa kiasi kikubwa alipewa matumaini makubwa ya kuiendeleza klabu ya Chelsea na moja ya mikataba aliyopewa ni kuiwezesha Chelsea kuchukua vikombe viwili vikubwa cha MAbingwa na kombe la Premier League.
Sio Scolari pekee kwani hata kocha wa klabu ya Portsmouth Tony Adams, ambaye aliwahi kuwa Kepteni wa timu ya Taifa ya Uingereza naye pia ametimuliwa. Scolari anaungana na Kevin Keegan, Roy Keane, Juande Ramos, Alan Curbishly na Paul Ince ambao kwa pamoja wamekubwa na kimbunga cha utashi wa ushindi toka kwa waajiri wao.
Katika mkataba wa awali Scolari alitakiwa kutumikia Klabu hiyo kwa miaka mitatu kwa mshahara wa paund £6.25m kwa mwaka ambapo mshahara huo ulikuwa unamfanya kuwa Kocha anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote katika dunia hii ya soka. Scolari ambaye mashabiki wanalinganisha mafanikio yake na Mportugees José Mourinho ambaye aliiwezesha klabu ya Chelsea kuchukua vikombe mara mbili kwenye ligi na kusema kuwa hana lolote jipya.
Scolari anafanya idadi ya makocha tangu tajiri Abramovich achukue Klabu hiyo ndani ya miaka 5½ kuwa wanne ambao wengine ni Claudio Ranieri na Avram Grant ambaye aliiwezesha Chelsea kufikia European Cup final ambapo walipokwa tonge mdomoni na Manchester.
JE NANI UNAFIKIRI ANAFAA KUMRITH SCOLARI?