Messi aiua Real Madrid

April 28, 2011

image

Magoli mawili ya kipindi cha pili yaliyopachikwa na Lionel Messi, yametosha kuwanyamazisha mashabiki wa Real Madrid ambao awali walitamba kwa kuifunga Barca na kuchukua kikombe cha Ufalme wiki iliyopita.

Kutolewa kwa Pepe na Morinho kutolewa eneo la uwanjani ni moja ya matukio yaliyojiri kwenye mchezo wa kwana wa nusu fainali kati ya mahasimu hao wawili wa soka Real Madrid na Barcelona. Timu hizi zilionyesha kukamiana jambo ambalo kidogo lilipunguza ladha ya mchezo huku kukiwa na faulo za hapa na pale za kimabavu.

Hata hivyo Barcelona walionyesha kuumiliki mchezo na confidence ya Real Madrid ilikufa baada ya mchezaji wao Pepe kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi mchezaji wa Barca Daniel Alves.

Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 0-0. Ilipotimu dakika ya 76 Messi kama kawaida yake alichomoka na kuusindikiza mpira uliopigwa na Ibrahim Afellay na kumuacha Iker Casillas akidaka hewa.

Zikiwa zimebakia dakika tatu kumalizika kwa mpira Messi tena alichomoka na mpira huku akiwapita mabeki watatu wa Real Madrid na kumpiga tobo Iker Casillas na kuandika bao lake la 52 kwa msimu huu huku likiwa ni bao 11 kwenye michuano hii ya Champions League. Gonga hapa kusoma zaidi


Joto la Soka Olympic lapanda…

August 7, 2008

Argentina's player Lionel Messi runs  during a training session at the Beijing 2008 Olympics in Shanghai, Wednesday, August 6, 2008. Argentina will face Ivory Coast Thursday in a Group A soccer match.
Mchezaji wa Argentina Lionel Messi akifanya mazoezi huko Beijing jana, Agentina iko China kwa ajili ya Michezo ya Olympics 2008 Shanghai China, Timu hi itapambana na Ivory Coast alhamisi kwenye mechi za kundi A kwenye Olympic.


%d bloggers like this: