Kilimanjaro Connection waiaga Malaysia kwa show ya kufa mtu!!

June 28, 2009

DSC01185

Faijala Mbutu mpiga gitaa mahiri wa The Kilimanjaro Connection Band akiwajibika jukwaani wakati wa shoo yao ya mwisho jijini Kuala Lumpur jana, huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta.

Kundi la Muziki wa Dansi la The Kilimanjaro Conections Band jana walifanya shoo yao ya mwisho kuwaaga mashabiki wao wa Malaysia kabla ya kuondoka kurejea nyumbani kwa mapumziko mafupi. Shoo ya jana ilikuwa ya kufa mtu na kuhudhuriwa na mamia kwa mamia ya mashabiki na kufanya ukumbi wa Rum Jungle kuwa mdogo.

Kundi hili ambalo lilikuwa nchini Malaysia kwa takribani miezi sita limejizolea umaarufu na kuitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa baada ya kuwa gumzo na story na picha zao kutawala kurasa za burudani kwenye magazeti yote ya Malaysia.

Siku ya jumatatu wana morogo walitumbuiza kwenye ukumbi wao wa Rum Jungle na mara baada ya kumaliza kiongozi wa bendi Kanku Kelly alitangaza kuwa wiki hii ni ya mwisho kwao na kuibua kelele za simanzi toka kwa mashabiki na akina dada walishindwa kuvumilia na kububujikwa na machozi kwani Rum Jungle palikuwa kiota mwanana kwa wale wapenzi wa Live Band.

The Kilimanjaro Connections Band wako pia kwenye mazungumzo ya awali kwa ajili ya mikataba zaidi ya maonyesho huku Mashariki ya Mbali.

Bendi hii inaongozwa na wanamuziki hodari Kanku Kelly mwenyewe anayeimba na kupiga Konga, Trampet na ala nyingine, pia yumo Faijala Mbutu huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta, hali kadhalika kuna Maneno Uvuruge anayepiga gitaa la solo, huyu bwana hupagawisha watu kwa umahiri wake wa upigani solo na jinsi anavyomchezesha mwanadada Queen Suzy, Wengine ni Geofrey Kumburu anayecheza Keyboard, Sijali Moris ambaye anapiga Drums kama Papito Mbala bila kuwasahau wataalamu wa sauti Delphine Mununga na Modester Nyoni mdogo wake Luiza Ntoni au Luiza Mbutu wa Twanga.

DSC01189

Mcharaza gitaa la solo Maneno Uvuruge kulia huku Queen Suzy akiwajibika kwenye kipaza sauti, Queen Suzy amebadili style na kwa sasa anaimba na kucheza awali alikuja kama mcheza show wa kundi hili, Hongera mama.

DSC01188

wakipanda wanamkorogo panakuwa hapatoshi.

DSC01186

Mbutu kushoto, Kanku Kelly katikati na Queen Suzy wakiwa kazini.

DSC01181

Kutoka kulia ni Delphinus Mununga, Modesta Nyoni (mdogo wake Luiza Nyoni au Luiza Mbutu), Kanku Kelly and Farijala Mbutu.

image

We acha tuu

image

Bango la wanamkorogo kwenye klabu ya Rum Jungle.


Wamkumbuka Maneno Uvuruge?

February 7, 2009

Maneno Uvuruge akishikilia mpini wa Solo

Jina la Maneno Uvuruge wengi tumelisikia siku nyingi kwenye bendi tofauti hasa enzi za Vijana Jazz ila kwa sasa Maneno Uvuruge yuko na wana Kilimanjaro Cionnection Band wazee wa Mkorogo waliko ziarani Kula Lumpur Malaysia. Uvuruge ameshapiga na wanamuziki na Banana Zoro, Machozi Band na pia ameshuiriki kwenye kurekodi nyimbo nyingi ambazo amekuwa kama mwanamuziki mwalikwa.

Uvuruge amevutia mamia ya mashabiki kwa umahiri wake wa upigaji gitaa na si hivyo tu bali Maneno Uvuruge ni muimbaji mzuri sana, Binafsi namkubali sana jamaa ametulia ile mbaya, rafiki yangu MJ anasema ukimuona uvuruge barabarani huwezi mtambua kama ni mwanamuziki na sura yake ya upole, any way ni mtazamo tuu.

Pata kipande cha wimbo wa Dunia tunapita toka kwa Wana Kilimanjaro Connection waliko ziarani Malaysia na hii ilikuwa kwenye ukimbi wa Rum Jungle ambapo wanapiga jumatatu hadi jumamosi, habari njema jamaa wataendelea kuwepo hadi mwezi wa tano inshallah.

Kilimanjaro Connection ambayo kwa kiasi kikubwa inaongozwa na wanamuziki hodari kama Kanku Kelly mwenyewe anayeimba na kupiga Konga, Trampet na ala nyingine, pia yumo Faijala Mbutu huyu ni mume wa Luiza Mbutu wa Twanga Pepeta, hali kadhalika kuna Maneno Uvuruge  “Diblo Dibala” anayepiga gitaa la solo, huyu bwana hupagawisha watu kwa umahiri wake wa upigani solo na jinsi anavyomchezesha mwanadada Queen Suzy, Wengine ni Geofrey Kumburu anayecheza Keyboard, Sijali Moris ambaye anapiga Drums kama Papito Mbala bila kuwasahau wataalamu wa sauti Delphine Mununga na Modester Nyoni.

Bonyeza player upate mambo.

Delphine Mununga  mtaalamu wa sauti

Mashabiki wakiserebuka ndani ya ukumbi wa Rum Jungle ambapo Kilimanjaro Connection wanapiga.

Queen Suzy mamaa tenterente akipagawisha na mauno jukwaani, Binti huyu aliwahi kujumuika na bendi tofauti tofauti ikiwemo Wazee wa Ngwasuma kwa sasa anampa tafu Mzee mzima Kanku Kelly.

Mashabiki wakibanana kucheza Mkorogo wa Kilimanjaro Conecction Band usiku wa jana.

Baadhi ya vijana wa kitanzania wanaoishi Malaysia Jimmy(L) na Xslim(R)  wakiwa ndani ya ukumbi wa Rum Jungle kuwapa Shavu Kilimanjaro Connection.

DSC00182

Mamaa Suzy akiwajibika jukwaani.

Mashabiki wakiserebuka ndani na kupekecha we acha tuu kaa nyumbani yaani!!

Mj akiwa na Jimmy wakiwapa support wana mkorogo ndani ya Rum Jungle Kuala Lumpur-Malaysia.


%d bloggers like this: