Diamond afunika Dar Live…!!

April 30, 2012

image

Akisali kabla ya kuruka kwenda Mbagala Dar Live

image

Patashika nguo chanika stejini

image

image

image

Licha ya Mvua Mashabiki hawakuondoka bila kumuona Diamond, Picha Zote na Global Publishers.


Mariage Heureux John et Betty Kinabo.

April 30, 2012

image

Mr and Mrs John Kinabo

image

image

image

Feux de l’amour John et Betty Kinabo

image

Nyumba na mali mtu hupewa na Babake bali mke mwema hupewa na Mungu, Si maneno yangu ni maneno ya vitabu vutakatifu, Pichani ni mdau na swaiba wangu John Kinabo akiserebuka na Mamaa Betty in “Crazy Wedding Entrance” ambayo kila mmoja alivutiwa nayo. John hatimaye amemuoa mpenzi wake wa siku nyingi Betty Simba katika harusi ambayo lihudhuriwa na vijana wote wa mjini.

photo 4

 

photo 1

photo 1w

Mr and Mrs John Kinabo wakifurahi katika sherehe ya Harusi yao hapo Ijumaa 27th April 2012.

photo 2

Flower Girls ukipenda waite Maids wakiwa wamekula pozi na Bi Harusi Betty John.

photo 3

John Kinabo (L) akiwa na Best Man wake ®

image

Kiramo Hall kulikofanyika mambo yote

Swaiba John nakuacha na Feux de L’amour toka kwa JB Mpiana akiongelea mapenzi fatilia hapo chini maana yake utaona, Wimbo huu kwa muda mrefu umekuwa ukipigwa kwenye maharusi huko Congo kutokana na ujumbe wake. Hongera sana John.

L’amour est-ce aimer ou etre aimer? Bien que L’amour soit Le symbole d’un sentiment partage, etre aimer n’est jamais le signe d’un bonheur parfait = Je mapenzi ni kupenda au kupendwa? ingawa mapenzi ni ishara ya kubadilishana hisia, kupendwa kamwe si maana ya faraja iliyokamilika.

Bolingo eza maladie mabe dokotolo nango motema symptoma nango souci, kasi kisi nayango se presence ya motooyo ozali kolula, Lokola nalula masiya ye nde kisi nangai= Mapenzi ni ugonjwa mbaya, Dalili yake ni mawazo lakini dawa yake ni kuwepo kwa umpendaye,kama navyompenda Masiya(Yesu) ndio dawa yangu.

Bolingo lokola maladie contagieux tuna na bamoureux decus tuna na B’aveugles d’amour surtout na badivorces, Bakopesa yo temoignage na bango okoyoka mawa, okoyoka ngolo, okotikala stupefart, se kokamwa kamwa mama, se koimbaimba mama, se kotuna tina nzambe akela L’amour = Mapenzi kama ugonjwa wa kuambukiza lazima uwaulize waliokosa kupendwa, waulize vipofu wa mapenzi, waulize walioachika watakupa ushuhuda wao, utawaonea huruma,utakarahishwa, utastaajabika, Utakuwa unashangaashangaa mama, na kuimbaimba na kujiuliza kwa nini Mungu aliumba mapenzi.

Yango na po na nga Amida, hata na pasi tokovanda, hata bikebi tokoliya hata thomson tokotonda. Yesu kutu mwana ya nzambe babota ye na nandako ya mpata, Kasi mokili oyo ya tata naye, Likolo nase ya bango, kamweve o makamwisi mama = Kwa hiyo nimemchagua Amida katika mashaka tutaishi, hata samaki(thomson) tutakula tutashiba, Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alizaliwa katika zizi la wanyama. Lakini dunia hii ni ya Babaye, mbingu na ardhi ni vya kwao Usishangae maajabu.

Na Kin Liboso ya kolinga moto bakoma kotuna ofandaka wapi, A biso tovandina mwalekwa nani akolinga biso mingi baboya bango na bango, Mosika eleki, bangungi baleki Taxi kutu eboya bango = Kinshasa kabla ya kumpenda mtu wamekuwa akiuliza unakoishi, Ah sisi tunaoshi Malekwa (Manzese,Uswahilini) nani atakaetupenda. Wengi wamekataliwa eti ni mbali mno mbu wamezidi huko hata Taxi haziendi huko.

Basusu liboso ya koloba Oui” bakoma kotuna otangaka wapi, Ah biso tubuka Bic mwa kala nani akolinga biso, Tika tokosa hata kokosa, Nga nazali graduet, Nga nazali licencie, Nga nazali enginieur, mpo balinga nga mama = Wengine kabla ya kusema ndio” huuliza ulikosoma wapi Ha sisi tuliovunja kalamu (Bic)yaani (kuacha shule) toka siku nyingi nani atatupenda, Wacha tudanganye mimi nina degree, mimi nina shahada ya juu, mimi mkandarasi ili tupendwe.

Basusu liboso ya kolinga moto bakoma kotuna de quele famille es-tu? Ah biso famille ezanga riche nani akolinga biso nzambe ya mpungu bandela mokili oyo otunaka mokomoko soki nani akolinga kobotama lisusu na famille ya pauvre. = Wengine kabla ya kumpenda mtu huuliza umetokea katika familia ya namna gani? Ha sisi familia fukara nani atakayetupenda,Baba Mungu rdia maumbile halafu muulize kila mtu kama yupo atayekubali kuzaliwa tena katika familia ya kimaskini.

Passe na nga eleki mabe yango naeffacer basouvernir nyoso ya mabe na bango nanga, memoir nanga eyebi kaka kombo ya Amida Chaty naye nde pelerinage edainayo petola nga mama sukolangamama, salisa nga nabika. = Maisha yangu yaliyopita ni mabaya ndio maana napenda kufufa zote mbaya kwenye ubongo wangu. Kumbukumbu yangu yajua tu jina la Amida Chaty Nimekuja kwako kama mpitaji,nitakase,nisugue nisaidie nipone.

Nalinga mindele,Bayindo,mikuse, milayi nalinga mike mpe minene, kasi chancelier wapi alatisanga palata ata bronzo hatanatolo, soit disant nga se amoureux,ancien de saio asala kala, roi de guere O mosala mpunda mama = nimependa weupe na weusi warefu na wafupi wembamba na wanene yupo wapi afisa zawadi hata medali ya chuma kifuani ieleweke kuwa mimi ni mpenzi mkongwe wa Saio( aliyepigana vita vya Saio mfalme wa vita Kazi isiyo na Mshahara……

Mtohoo huo ni mchango wa msomaji wangu maarufu Shaibu Thabit Mwambungu ambaye alikuwa nao kwenye maktaba yake.

Respect kwa wasomaji wangu wote, Mamaa Sophia Kessy, Pendejee Maghambo Philipo popote ulipo tuko pamoja, Julie ellyston Suvereign na Mamaa Emmy, Batty My Brother pamoja na Mamam Joy, Mukubwa Edgar Kiiza muzee ya Malaysia, Ally Tandika diwani muzee ya Azam na Bimkubwa wako, Mukubwa Six Mzee wa Matombo na Mamaa Kemmy, Tom Baba Maya aka Chiluba, Mukubwa Gerald Kitima Baba Kara, Dulla Asumani muzee ya Tigo, Hadj le Jbnique, Patrol de Patrol Shaibu Thabit, Farid, bila kumsahau Swahiba Alhaj Tameem Mngoya Juma Ahmed Lukuta wa Kibanda Kicheba kwa Semkopi pamoja na Werasonique wooote, . Pamoja sana.


Twanga Moto Ule ule, Yakinukisha Rock City !!

April 30, 2012

image

image

image

Dogo Rama Lela Mwana Lelaaaaaaaaaaaaa!!!!

image

image

image

image

image

Gody Kanuti namkubali sana kijana huyu kunako mpini…

image


Watoto wa Congo na utata wa uraia wa Koffi Olomide

April 30, 2012

Watoto wa Congo na utata wa uraia wa Koffi Olomide

Ni Kitambo sasa tangua suala la uraia wa Mwanamuziki Koffi Olomide lianze, mengi yamesemwa kwenye mitandao ya kijamii huku watu wengine wakisema Koffi ni Mcongoman ambaye mmoja wa wazazi wake ndiye Mcongo na Wengine wakisema kuwa yeye Afrika ya Magharibi na wengine wakisema Koffi ni Mcongo kabisa.

Wasikie wenyewe wanavyomchambua Koffi ikiwa ni pamoja na kumtaka aonyeshe birth certificate za mamake na babake kama kweli yeye ni mcongo, sio kuonyesha ana uraia wa nchi mbili tu pamoja na mengine, japo hii ilikua zamani kidogo 2001 lakini mpaka leo kumekua na mtazamo tofauti na hasi dhidi ya ukongoman wa koffi olomide, wazawa wa congo wenyewe wamekua wakidai koffi sio mkongo mwenzao bali ni mtoto wa mhamiaji kutoka west africa Benin ikitajwa ndio nchi ya asili ya koffi olomide, mfano kuanzia dk 7:20 utamuona na kumsikia Jb mpiana akiwataja wacongo waliowahi kupiga kwenye kumbi kubwa za ufaransa kama Zenith, Olympia na Bercy akiwataja kina Abeti masikini, Tabu ley, Papa wemba na wengine lakini akiliruka jina la koffi makusudi na mwandishi anapomuuliza mbona humtaji koffi Jb nae anamuuliza mwandishi “kwani koffi nae ni mcongo? mimi nataja wacongoman waliowahi kupiga kwenye hizo kumbi kubwa, lakini wapo wengi africa waliowahi kupiga kwenye hizo kumbi, kuna wa Benin, kuna kina  Yousson N’dour na wengine wengi lakini wacongo ni hao niliokutajia…”

Na pia anasema ZENITH eza ya Mutu Te akiwa na maana zenith sio ya aina mtu, yeyote anaweza kupiga hapo.


Messi vs Ronaldo … …..

April 27, 2012

image


Mopao akiwa ofisini kwake

April 25, 2012

image

Anaitwa Mopao Mokonzy Baba Didie Stone Koffi Charles Olomide ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mwingine na Bia ya SKOL wa kumdhamini kwa miaka miwili ambapo kampuni hiyo itagharaia show zake na kuwalipa mishahara wanamuziki wake.

Koffi kwa sasa amezidisa show zake za barani afrika na kuimarisha zile za Kongo Kinshasa ikiwa ni matokeo ya wanaharakati wa Congo wanaojulikana kama Banakongo au Lecombatant ambao wameongoza kufanya fujo kwenye show za wanamuziki wote ambao walikuwa wakimsupport Rais Kabila kwenye kampeni ambapo Koffi alitunga wimbo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wa Congo kumchagua Kabila ambaye alishinda uchaguzi huo.

Koffi ambaye amesemwa anataka kugombea uchaguzi ujao kwa nafasi ya Ubunge ingawa mwenyewe aliwahi kukanusha hilo lakini watu waliokaribu naye wanasema anampango huo. Hata hivyo wachunguzi wengine wanasema haitakuwa rahisi kwa Koffi kugombea kwa vile si raia wa Kongo akisemwa kuwa anatokea Gabone na wakati mwingine inasemwa anatokea Congo Brazaville na mmoja wa wazazi wake ndio Mkinshasa.

Nakuacha na kibao hicho alichompigia kampeni Rais Kabila.


Wenge ya zamani on stage…

April 24, 2012

Hawa walikua watu wa kazi mwanzo mwisho,kila mtu aliijua kazi yake,waimbaji waliimba,wapigaji walipiga na kucheza pia,yani jukwaa zima ni full shangwe mwanzo mwisho,nani kama hawa???bila shaka hakuna na wala haitotokea kama hawa,tutaendelea kuzikumbuka kazi zao tu kama hivi sawa na mtu mliekuwa nae duniani then akawatoka na hawezi kurudi tena…..!

We miss u guyz…please do us a favour walau ka album kamoja tu ka pamoja basi!

Wadau wasomaji ombi maalum kwenu naomba mumtizame ALAIN PRINCE MAKABA kuanzia dakika 05:35 na mpaka mwisho then mumpe heshima yake kidogo, mi naanza kwa kusema Alain Makaba “SHIKAMOO”


Sauti zilizotukuka za J.B. MPIANA ET PAPA WEMBA " LE CAVALIER SOLITAIRE "

April 24, 2012

Unapoongelea hawa manguli wawili Papa Wemba na JB Mpiana kwangu mimi kikubwa kinachokuja akilini ni sauti zao mahiri.

Kiukweli hii kolabo ni moja kati ya kolabo ambazo nilizifurahia sana na huu wimbo huwa nausikiliza kila mara na ulinogeshwa zaidi na ghani za Tutuu Kaludji mwishoni na ikumbukwe kuwa kipindi hiki Kaluji alikuwa yuko juu sana na Primus ndio walikuwa wameanza kuidhamini BCBG.

Je wewe unakumbuka nini?


Usiku wa Mayenu

April 24, 2012

image

Tar 27 Mwisho wa mwezi huu.
2 in One
1:- BEST DJz in TOWN dj MACKAY & dj TOO SHORT
&
2:- THT LIVE PERFORMANCE & DANCING SHOW.
SHOW maalum kwa WATANASHATI WOOOOTE dar-eS-saLaam


MCD na Atalaku Ferguson wajiunga na Mashujaa Musica

April 23, 2012

image

Anaitwa Saulo John ‘Ferguson’ RAPPER na MUIMBAJI mahiri nchini; LEO AMESAINI MKATABA WA MIAKA MINNE na MASHUJAA BAND:

Show ya utambulisho yeye na MCD itafanyika ijumaa tarehe 27 april pale pale BUSINESS PARK-victoria kijitonyama

image

Naye Mpiga tumba maarufu kwa jina la MCD ametwangazwa kuhamia kundi la Mashujaa Musica leo kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atatambulishwa tarehe 27 April ndani ya ukumbi wa Business PARK-VICTORIA KIJITONYAMA

Mashujaa Musica wamekuwa wakijiimarisha safu yao ya uimbaji na sasa wameanza kuimarisha safu ya vyombo, ama kwa hakika kwa sasa upinzani wa Muziki wa dansi umerejea baada ya muda mrefu bendi kama Twanga na FM Academia kushika jahazi jambo lililosabababisha ufinyu wa mageuzi ya burudani.

Tunatumai huu hautakuwa upinzani wa nje ya jukwaa la muziki na  burudani na kuwa chachu ya mageuzi katika sekta nzima ya muziki wa Dansi.


Kuna nini kati ya fally na wadada???

April 21, 2012

Koffi apata ruhusa kuimba nyimbo za Franco

April 19, 2012

image

Baada ya Concert yake iliyofana ya Koffi chante Tabu Ley na Koffi chante Lutumba mwanamuziki nguli Koffi Olomide ameomba ruhusa kwa watoto na familia ya marehemu Franko Luambo Luanzo Makiadi ili aweze kupiga Concert na huku akiimba nyimbo za mwanamuziki huyo mahiri aliyetamba na bendi ya T.P Ok Jazz

Koffi amesema kuwa kutokana na Matukio yaliyojiri kwa wanamuziki wa Congo waliokuwa wakim support Rais Kabila huko Europe ameamua kuongeza show zake nchini Congo na anataka awaridhishe mashabiki wake kwa kuwapa ladha na kile kitu roho inapenda.

Akiongea na Digital Congo Koffi amesema kuwa anajiimarisha kwenye ziara za Africa zaidi kwa mwaka huu ambapo amepanga kufanya maonyesho kadhaa.

Kwa mujibu wa habari ambazo zimetolewa na Koffi mwenyewe anasema kuwa amepanga onyesho hilo la kumuenzi Luambo limepangwa kufanyika July 7, 2012, kwenye bwawa la kuogelea la Hoteli maarufu ya The Grand huko Kinshasa.

Koffi amesema kuwa mazungumzo yameshafanywa ya awali na tayari familia ya marehemu iliwakilishwa na Emongo ambaye anasema kuwa alimuandikia yeye binafsi na kumuomba aziimbe hizo nyimbo za marehemu baba yao na mazungumzo yakaanzia hapo.

Haikuwa jitihada zangu bali ni wanafamilia ya Mareemu hasa baada ya kuona picha na video za show ya Simaro Lutumba na Tabu Ley.

“Nisingeweza kukataa nafasi hiyo adhimu ya kuiimba sauti ya yule mzee kwakweli hata ungekuwa wewe ndio mwenye kipaji kama changu usingekataa aliongeza Koffi”.

Nakuwekea kibao Mamou chake kilichoimbwa na TP Ok Jazz.

 


He is Harsh, but he refines the Stars. Get ready for Tusker Project Fame 5

April 19, 2012

image


Chelsea Salutiiiiiiiii !!!!!!!

April 19, 2012

image

Mtasema sana lakini ndio tayari keshazama kwani Barelona kitu gani bwanaaaaaaaaaa Kimoja tu chwaaaaaaaaaaaaaaaaaaa !!!!

Chelsea 1 – 0 Barcelona mfungaji Drogba, Uwanja Darajani, Mashabiki 38,039, Referee- Brych

Chelsea starting lineup v Barcelona Champions League 2012:- Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Mikel, Lampard, Meireles, Ramires, Mata, Drogba

Barcelona starting lineup vs Chelsea Champions League 2012:- Valdes, Dani Alves, Puyol, Mascherano, Adriano, Busquets, Iniesta, Xavi, Messi, Sanchez, Fabregas


Nzembo Mabele, Simaro Lutumba na TP Ok Jazz wakituasa kuhusu Kifo

April 18, 2012

 

Kunapotokea misiba watu huwa wanasikitika sana na kwa vile Mungu ametuumba na kusahau huwa tunasahau mara moja, Basi leo nakuletea hiyo ikiwa Poete Lutumba akiwaasa walimwengu Juu ya Maisha ya bindamu na Kifo na udongo unavyomeza watu ni maneno mazito ya Mafundisho kwetu sote wlimwengu wape wadau katika hizi aroba za Kanumba.

Nsoso eleli, nsoso ekolela ngoya nsoso ekolela bandoki bazongi ndako, Sima ya mwa ngonga tongo ekotana ndeko ya makambo, Basusu na bisengo Basusu na mawa wapi yoo Mboleo.

Jogoo anawika, Jogoo anawika, Jogoo anawika wachawi wanarudi nyumbani baada ya muda asubuhi kutakucha ndugu wana mambo wengine wana furaha wengine wana huzuni/matatizo uko wapi Mboleo.

Kadi opesi nkanda esika na motema bougie ekotangisaka pinzoli mpo na mpasi eleli mpasi ya moto ngai naleli ya lolango okotiaka kobanza soki moto akobela oo mpo nayo bolingo eleki metele mama a mabele o dis Zwani mabele.

Kadi umeipa hasira nafasi moyoni Mshumaa unadondosha machozi kwa maumivu unalia maumivu ya moto mimi nalia ya mapenzi utafikiri kama mtu anaumwa oo kwa ajili yako mpenzi yamezidi mita mama rafiki Zwani udongo.

Mokolo nakokoma mobange ma Asimie nayeba nakotambola na nzete na balabala mpo nasengaka likuta ngai nabikela Basusu batunako soki ngai nabotaki te ba oyo nakabelaka bakomi nde koseka ngai nakipa teo nzambe nasakala la vie ya sans soucis mabele, mabele mabele

Siku nitakapokuwa mzee ma Asimie najua nitatembea kwa fimbo/mkongojo barabarani ili niombe pesa niponee wengine watauliza kama sikuoa wengine watauliza kama sikuzaa hawa niliwagawia watanza kunicheka sitojali Mungu naishi maisha bila kusononeka udongo, udongo, udongo

Mokolo nakokufa nkake ekobeta dis Tati olobelaka batu maloba na ngai ya nsuka moto na ngai bakamata basala monument soki mopaya aye balobela ye nsango bambanda bakosepela basi ngai natiki ba familles bakoepela biloko ngai natiki baenemi bakoloba apusaka lofundu ebembe ya nsoso matangate alanga nzémbo nalanga makambo mabele

Siku nitakufa radi itapiga rafiki Tati uwambie watu maneno yangu ya mwisho, kichwa changu watengeneze sanamu kama mgeni akija wamwambie Habari wanaume wenza watafurahi wake nilioacha wanafamilia watafurahi vitu nilivyoacha maadui watasema alizidi maringo maiti ya kuku haina matanga nimenzisha Wimbo nimeanzisha mambo, udongo

La vie na ngai oyo ya sans soucis e mwasi na ngai nzinzi famille na ngai mabele nautaka na mabele, na kozonga na mabele mokolo nakokufa nayeba nakopola e baliaka na ngai bakokanga nzolo na nsolo bamelaka na ngai bakokima nde kosokola ngai ebembe ya Masia e atabokimie ba nzinzi bakolela ngai nazali na confiance mabele.

Maisha yangu haya yasiyo ya huzuni mke wangu nzi familia yangu udongo nimetoka kwenye udongo nitarudi kwenye udongo Siku nitakufa najua nitaoza waliokula na mimi wataziba pua kwa harufu waliokunywa na mimi watakimbia kuniosha maiti ya Masia hata mkiikimbia nzi watanililia nina imani udongo.

La vie na ngai oyo ya bayanke falanga nasalaka ya mboto na lituma mwasi aboya ngai kasi nkopo ya masanga ve etoko na ngai nasombo mpo ngiliba tokoluka tozipa miso tongo etanela namesana kolata kaki na lipapa, oo mpo nayebi mokolo tokokufaka tokendeke na drap ya pembe ata ozali riche Joe mabele ngai nalela ye.

Maisha yangu ya ujana pesa ninayopata ya kambale na ndizi Mwanamke anikatae lakini Kilauri/Kopo la pombe hapana mkeka wangu nimenunua kwa kujisitiri tunatafuta tufunge macho asubuhi kuche nimezoea kuvaa kaki na kandambili oo sababu najua siku tunakufa tunakwenda na sanda hata kama uku tajiri Joe udongo nakulilia.

Ye yeyeye mama pokwa ekomi moi mokokota e butu ekoinda mokolo mwa bandoki banganga libala oyo ya mwana na kati Masua ekokufaka Libongo ekotikalaka mama na Lola tangelaka mwana nkombo ya tata Masia, Mokili ekokufa masumu maleki kasi nkombo ya Nzambe ekotikala seko Mundele asala manduki ya koboma batu kasi ya koboma verite Mundele akoki te Mabele, mabele, mabele.

Ye yeyeye mama jioni imefika jua linazama usiku unaingia giza siku ya wachawi waganga ndoa ya mtoto katikati Mashua inakufa (haribika) Bandari itabaki mama yake Lola mtajie mtoto jina la baba, Masia dunia itakufa dhambi zimezidi lakini jina la Mungu litabaki milele Mzungu ametengeneza silaha za kuua watu lakini ya kuua ukweli hakuweza udongo, udongo, udongo

Melesi mingi Shaibu Mwambungu Mbinga


Unaikumbuka Loketo Group?

April 18, 2012

 Wakati huo Loketo Group ikiwa na mkali wa kupiga solo barani Afrika Diblo Dibala na wakongwe wengine kama Aurlus Mabere, Jean Baron, Lucien Bokilo, Mack Mackaire ambaye alikuwa anapiga Drums huyu jamaa alikuwa balaa na wengineo waling’ara sana na kufanikiwa kuziteka nyoyo za wapenda midundo ya Afrika si tu kwa Congo bali kwa Bara zima la Afrika.

Namkumbuka Ronald Rubinel ambaye alikuwa anapiga kinanda enzi hizo wapiga vinanda mashuhuri walikuwa yeye na Jamaa wa Pepe Kalle kama sikosei anaitwa Butamu. Huku wakiwa na wacheza show wao wawili “Wana Wandere” wazungu ambao walikuwa wakicheza vilivyo.

Kwa kilingala Loketo inamaana chezeza hips zako “move your hips” na ndivyo Aurlus Mabere ilikuwa style yake ya kuchezesha.

Mwaka 1987 wakiwa wametiamia Loketo waliwasha moto kwenye klabu moja ijulikanayo kama Kennel Club huko San Francisco Amerika na inasemekana ile ilikuwa ni Concert kubwa na iliyobamba sana. Baadaye walianza kutoa kila mmoja na solo albam yake. Jamaa walitisha sana.

Kaka yangu Mungu Marehemu Nhangale Nkandi Mungu amlaze peponi alikuwa analipenda sana hili kundi enzi hizo tunakunywa Texco Club pale Sea View Upanga kabla ya kuingia Pink Coconut nilikuwa mdogo lakini burudani nilikuwa naipenda sana.

Wimbo nimeweka Malou kwa heshima ya mdau Le Grand Paa Sentuke, Sikiliza huu wimbo pale Lucien Bokilo alipompa nafasi Diblo Dibala ambaye kwa kiasi kikubwa aliutendea haki.

Nimefarijika kupata simu kutoka kwa mdau na shabiki mwenzetu Neema Jua akiwa Dodoma Mwangaza Fm anasema anapenda sana tunavyowachambua na kuuchambua huu muziki wa Africa Congo. Na kwa leo alitaka kujua kuhusu Aurlus Mabere na loketo Group yake.


KITABU CHA HISTORIA(BIOGRAPHY) YA WERRASON CHATOKA!

April 18, 2012

Na Hadji Le JBeeneque

Nadhani Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa kama sio duniani kiujumla. Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu. Lakini safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo kupitia kitabu maalau ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki, kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye mafanikio makubwa pia.

Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa. Katika hilo Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra, Aime Buanga, Jean Belix Luvutula, Didier Masela na Christian Zitu, ambapo Aime Buanga alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha bendi lilitoka kwake.Lakini wakati fulani kwenye siku hizo hizo za mwanzo mwanzo za kundi lao Aime Buanga alitaka kuachana na kundi hilo changa ili aendeleze kipaji chake kwenye sanaa za mapigano (martial arts) huku akimpa masharti rafiki yake werrason kwamba kama unataka nirudi kundini na wewe jiunge na mimi kwenye sanaa za mapigano (martial arts) sharti ambalo kwenye kitabu hiki werra anadai alilitekeleza kwa kujumuika na swahiba wake kwenye martial arts.

Wakati ya Werrason na Aime Buanga yakiendelea hivyo kwa upande mwingine Didier Masela alikua shule nje ya Kinshasa katika mji mdogo uitwao Mbanza Boma pamoja na Alain Makaba.Baadae huku nyuma Jb Mpiana akafika kuja kujiunga na bendi ambapo werra anasema katika kitabu hiki akamueleza “rafiki yangu nimesikia wewe ni muimbaji mzuri sana kama hitajali naomba uniimbie wimbo kidogo nikusikie na mimi” baada ya kauli hiyo ya werra jb inaelezwa akaimba wimbo uitwao “Abidjan” wa Viva la Musica uliotungwa na Debaba,ambapo Werrason mwenyewe na kila aliekuwepo pale wakavutiwa nae sana kiasi cha kumpigia makofi kwa wingi na watu wote, baada ya hapo werra akapendekeza Jb ajiunge na bendi ambapo Jb alikubali bila kusita.

Siku hiyo miongoni mwa waliomshuhudia Jb akiimba pamoja na werrason ni Didier Masela na Jean Belix.Na aliyemleta na kumtambulisha Jb hapo kundini alikua ni Jean Belix Luvutula ambae walikua wakiishi jirani na alikua akimuona Jb akiimba mtaani.

Baadae Blaize Bula akaletwa na Makaba kujiunga na bendi kama mpiga drums kutokana na kwamba alikua mpiga drum wa bendi ya shule waliyokuwa wakisoma lengo likiwa aje achukue nafasi ya binamu yake werrason  aliyekwenda kwa jina la Ladins Montana ambae ndio alikua mpiga drums, lakini Sele Bula akaonekana hana muonekano wa bcbg lakini Makaba kwa kujua kipaji cha Sele kwenye uimbaji pia akasisitiza aingizwe kundini. Hivyo wakawa wamempata Blaize(sele)Bula kama muimbaji,na kwa upande mwingine Jb ambae alikua tayari kundini alikutana na Tata Mobitch Adolphe Dominguez ambae alikua ni mtoto wa tajiri mkubwa sana Congo lakini pia akiwa na dancer mzuri akicheza sana nyimbo za DEFAO.

Jb na Adolphe baada ya kujuana kutokana na Jb kuvutiwa na uvaaji wa Adolphe wakatokea kuwa marafiki wakubwa huku Adolphe akimpigisha Jb pamba za ukweli kiasi cha kung’aa mbaya miongoni mwa wanabendi,ndipo baadae Jb akamtambulisha Adolphe kwa Werrason na wengine kundini ambapo wakaanza kumfundisha muziki Adolphe hapo hapo kundini huku yeye akilipa fadhila kwa kuwafadhili upande wa mavazi kupitia utajiri wa babake!

Kitabu kimeongelea mambo mengi hatuwei maliza ngoja nitoe dondoo za alichozungumzia werra kuhu su maisha yake binafsi.Katika maisha yake binafsi werra anasema alikutana na mkewe kipenzi Mama Pastor Silvie Mampata akiwa shule kupitia rafiki yake kipenzi wakati huo aitwae Wasenga Kipuni.Sylvie alikua ni binti wa mfanyabiashara tajiri na aliutumia utajiri wa babake kuisadia sana wenge huyu mama kupitia kwa werrason.

Kuhusu mgawanyiko kitabu kinaeleza kwamba ni uamuzi wa Jb kurekodi “Feux de l’amour” kwa kuwashirikisha wanamuziki wengine toka nje ya wenge kama alivyofanya Alain Makaba kwanza kwenye album yake solo iitwayo “Pile ou face” hapo ndipo mgogoro wa kiuongozi ulipoanza kuibuka,ambapo baada ya mafanikio ya Feux de l’amour Jb kwa kushirikiana na SIMON SIPE ambae ndie alikua meneja wao akisimamia kila kitu mpaka production zao wakanogewa na kutaka kutoa album nyingine solo ya pili ya Jb,hapo ndipo werra alipokasirika na kuitangaza album yake Kibuisa mpipa huku akiwa hana hata nyimbo moja wakati huo akiitangaza ila tu alitaka kumuonyesha Jb kwamba hawezi kutoa album solo ya pili wakimtazama tu.

Baada ya hapo bendi ikagawanyika na werra  ili kushindana na Jb akawa na mawazo ya kuanzisha tu bendi haraka haraka na kuanza kuperfom matokeo yake akachemsha sana mwanzoni kwenye concerts zake za awali zikawa “flop” mpaka ndugu zake wanaotoka kijiji kimoja kina Marie Paul wakamuonea huruma na kuamua kumsaidia ambapo Marie alimpa bure mwanamuziki wake JDT na yeye mwenyewe akawapata watu kama Didier Lacoste,Adjan n.k. ndipo mambo yakaanza kwenda vizuri sasa na kutoa FORCE INTERVENTION RAPIDE.

Ambapo badae mwandishi wa kitabu hiki nae alimpa wazo werra la kutarget zaidi concerts za watu wa kawaida kuliko za VIP kama wafanyavyo Bcbg,pia werra akapata msaada mkubwa toka kwa mamaa Tshala muana,baadae wakapata kazi ya kwanza ulaya kwa kualikwa kwenda kupiga London ambapo muandishi wa kitabu hiki alifanya kazi ya ziada kwa ku organize umati wa watu kwenda kumpokea werra na bendi yake airport katika safari ambayo masela aliachwa kin na ikawa mwisho wako kundini.


Rais Kikwete uso kwa uso na Maximo

April 17, 2012

image

Aliyekuwa Kocha wa Timu ya Taifa Marcio Maximo akisalimiania na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walipokutana huko Brazir ambako Rais yupo kikazi. Kiukweli Maximo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipandisha hadhi soka letu ambalo kwa kiasi kikubwa watanzania walishakata tamaa.

Kuna haja ya kufanya mikakati endelevu kwa ajili ya kuokoa soka la Tanzania na moja ya mikakati ambayo Maximo aliikazania ni kuwa na timu za watoto ambapo mashindano kama Copa Coca Cola yalizaliwa.


lola Mwana Digital na kitu Tendrement

April 17, 2012

Papaa Julie Illunga Elystone ananiambia Koffi huwa anasauti Saba za kuimbia na anasema kama angekuwa Kocha wa Mpira basi Koffi ndio angekuwa Kocha aghali kuliko wote duniani, kwani huwa anauwezo wa kutengeneza kikosi kikatisha kama njaa.

Msikilize humu alivyokuwa akichombeza na kuwahamasisha vijana, Sina ugomvi na Koffi na namkubali na kumheshimu sana.

Wimbo huu unaitwa Tendrement umetungwa na kuimbwa na Lola Mwana Digital mtoto wa marehemu Dingo Yogo.

Kijana anasauti nzuri sana na alijaribu kutoka Solo hakufanya vizuri sana na kwa sasa nilipata taarifa kuwa amejiunga na Zaiko Langa Langa ya Nyoka Longo. Lola ni kati ya vijana ambao wanamkubali koffi na kukubali Quartier Latin imeshindiklia maujuzi kwenye kipaji chake cha kuzaliwa.

Nawatakia ijumaa Njema, Hadji Le JBnique, Papaa Julie Ilunga Mukulu wa Bakulu, Richard Malewa, Farid wa Muscat, Papaa Dulla wa Airport JB Die Hard Fun, Mukulu Bin Adam Aaron Mengyason respect babu, PDG Maghambo popote ulipo tuko pamoja, Mzee wa Dallas Inn “Koffi die Hard Fun” heshima kwako kaka.

Weekend njema


LINA LIVE IN NEW YORK

April 17, 2012

image


%d bloggers like this: