Mr Paul: Finaly I am back to Music

May 25, 2009

Mr Paul1 Mwanamuziki mtanzania Paul Mbena aka Mr Paul amerudi kwenye uringo wa muziki kama alivyoahidi nilipofanya mahojiano naye mara ya mwisho.

Paul ambaye kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake za kimuziki nchini Australia kwenye jiji la Melbourne anasema kuwa ameshakamilisha nyimbo mbili ((Nakutamani na Malaika wa Moyo wangu) ambazo ziko kwenye mtindo wa Afro Funk style, nyimbo hizi ndizo zitakuwepo kwenye mradi wa Multicultural Art Victoria Visible CD, mradi ambao unajumuisha wanamuziki wa mataifa na mitindo mbalimbali (Gonga hapa kusoma zaidi.) angalia page ya mwisho utaona nafasi ya Paul Mbena ambaye kwenye mradi huu ametambulishwa kama Project Officer.

Awali aliongelea zaidi kuhusu mradi huu Mr Paul alisema “Nitarecord nyimbo mbili  nyimbo zitapatikana World wide through eMusic, Amazon MP3 amd Nokia Music store worldwide, Si unajua music wa Zouk ni wa mapenzi, nyimbo hizo nazo zinamguso wa kimapenzi zaidi,

Pia Mr Paul aliongeza “Hii CD itatoka katikati ya mwaka huu. nadhani utakuwa ndio mwanzo wa safari yangu ya kimuziki hapa ughaibuni kwani tayari wanamuziki wengine wameanza kuonyesha interest ya kujiunga nami kuanzisha band. nitaendele kukupa info as things are proceeding.

Mr PAul ni mmoja wa wanamuziki ambao wamefanikiwa kimaisha kupitia Muziki ambapo alijisomesha na kwa sasa ameajiriwa na kufanya kazi nchini Australia akiwa anasimamia mradi wa kuelimisha rika wa Snake Condom. Tuliwahi kufanya naye mahojiano gonga hapa usome.


Mr Paul: Mambo mazuri yaja

August 4, 2008
Mr Paul

Mr Paul

Pichani Mr Paul yuko kwenye matayarisho kabambe ya Albam yake ambayo atashirikisha mwanamuziki nyota wa kimataifa toka nchini Australia na wakali wengine. Bofya hapa kujua zaidi


Mr Paul: Muziki umeniwezesha kuwa ofisa nchi za watu

July 18, 2008
Paul Mbenna A.K.A Mr Paull

Paul Mbenna A.K.A Mr Paull

Kwa mtu yeyote ukimuuliza mafanikio hasa kwa vijana atakwambia nimejenga, nina gari au kitu chochote cha thamani, lakini mtazamo wa Paul Mbenna A.K.A Mr Paul (kama alivyozoeleka na wapenziwa muziki na burudani ) kuhusu mafanikio yake kimuziki anazungumzia elimu, ungana nami kwenye mahojiano na Mwanamuziki huyu kujua ni jinsi gani muziki umemsaidia kimaisha na mtazamo wake kuhusiana na sekta ya muziki hasa wa kizazi kipya nchini mwetu.

Mr Paul kwa sasa anaishi nchini Australia akiwa anafanya kazi jijini Melbourne kwenye taasisi ya Aboriginal an Torres staight Islander Health kama Program Coordinator. Nilipata wasaa wakuhojiana machache na Mr Paul has baada ya kuwa kimya kwenye nyanja nzima ya muziki na kutaka kujua mawili matatu toka kwake, Yuko wapi anafanya nini katika shughuli za kimuziki na kimaisha kwa ujumla, ungana nami kwa maswali na majibu na Mr Paul.

SS: Vipi shughuli za muziki bado unafanya? je una mipango yeyote ya kutoa albamu?

Mr Paul: Kwa sasa nimepumzika kidogo ili kupata muda wa kutosha kuestablish maisha yangu hapa Australia. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa sijishughulishi na shughuli za mziki kabisa, kwani mwezi wa nne nilikuwa na onesho katika ukumbi wa Coolabar katika mtaa wa Pitt jijini Sydney.
Pia bado nina mipango ya kurecord album na nimepata offer ya kurecord na mwanamuziki wa Australia ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki, kwa jina anaitwa Craig. Huyu jamaa yeye ni mweupe lakini anapenda sana muziki wa Africa na hivyo anataka tushirikiane kutengeneza album ya mchanganyiko wa miondoko ya Zouk na wolrd music. However, siwezi kusema kwa sasa muda na siku sahihi ambapo kazi hii itaanza. Hii ni kutokana na kuwa sisi wote ni watu ambao tunafanya kazi maofisini na hatuna muda wa kutosha kukaa studio na kuanza kazi hii. Pia mimi kama nilivyokueleza nimeanza kazi Melbourne hivyo kutakuwa na safari nyingi kiasi kati ya miji hii miwili (Melbourne na Sydney). Hivyo basi muda wa kuanza kazi hiimkwa kweli utajulikana karibu na mwezi wa December ambapo watu wanakuwa katika mapumziko.

SS: e kina nani na nani umewashirikisha kwenye nyimbo zako mpya?
JIBU: Ni kweli kuwa nina album mpya ambayo sikuitoa nikiwa nyumbani Tanzania. Na katika album hii nimmshirikisha Stara Thomas katika wimbo unaoitwa Nakupenda. Sikuweza kufanya kazi na wasanii wengi zaidi kwa kuwa sikupata musa wa kutosha kukaa Dar-es-salaam Kwa kuwa nilikuwa masomoni mjini Arusha nikifanya BA in Development Studies and at the same time working in Iringa Municipality kama Counrty program coordinator wa mradi uitwao Secondary Education to Encourage Development (S.E.E.D). Vile vile, album hii ilimalizika siku chache kable sijaondoka kuja Australia.

SS: Ndio umehamia huko kimoja? i mean maskani yako yatakuwa huko?

Jibu: Kwakeli kwa sasa maskani yangu ni huku, labda niweke bayana kuwa nimeamia huku kimoja na tayari nimepata Parmanent residence Visa. However, nyumbani ni nyumbani tu na nitakuwa narudi mara kwa mara kutegemana na sababu za kufanya hivyo.

Mr Paul akiwa na Mkewe
Mr Paul akiwa na Mkewe Natascha Klocker

SS: Pia ningependa kujua kaka maoni yako kuhusiana na soko la muziki wetu ambao kwa sasa umeshakubalika nyumbani na kuanza kutoka nje ya nchi kwa wanamuziki mbali mbali kufanya ‘kolabo’ na wenzao nje, je wasemaje kuhusiana na hilo?

Jibu: Kuhusu soko la muziki Tanzania, mimi maoni yangu nimkwamba kwa sasa wasanii wameonesha uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa zenye kiwango kinachokubalika na wanunuzi. Hii inaonekana hata katika mabadiliko ya maisha ya baadhi ya wasanii ambao wamefanikiwa kuwika, for instance, Lady Jay Dee, AY, Prof, J, Ali Kiba na wengineo wengi. However, juhudi hizi zinaonekana kuwanufaisha wajanja wachache zaidi na sio mwasanii wenyewe kwa kiwango kikubwa. Na haya ni matokeo ya kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa Managers wa wasanii, Madj’s wa voymbo mbalimbali vya habari, na hata wahusika wa nyanya za sanaa kutoka serikalini. Mara kwa mara watu hawa Managers na Madjs) wamekuwa wakiwadhurumu haki wasanii, kwa kuuza kazi zao bila makubaliano ya kueleweka. Kwa mfano, Managers wamekuwa wakitafuta masoko na kuandaa matamasha bila ushiriki kamili wa wasanii wenyewe. Hali hii imetoa mwanya kwa Managers hawa kuingia mikataba ya siri ambayo often inatoa faida maradufu kwa
Managers kuliko ile ineyopatikana kwa wasanii. Nitatoa mfano hapa. Nakumbuka wakati fulani nilikuwa chini ya uangalizi wa Manager fulani, na huyu jamaa kutokana na kuwa karibu sana makampuni makubwa ambaoyo ndi wadhamini wa mara kwa mara wa kazi za wasanii, yeye aliweza kutengeneza proposal za matamasha zilizoomba pesa nyingi kama gharama za wasanii. Cha kusikitisha ni kwamba katika utengenezwaji wa proposal hizi si mimi wala wasanii wenzangu waliowahi kuhusishwa na hii litoa mwanya kurhusuat least robo tatu ya pesa hizo kuingia mfukoni kwake. Hapa silalamiki sana kuhusu pesa ila nataka kueleza kuwa kitu kikubwa kinachoharibu utaratibu wa soko Tanzania ni ukosefu wa uwazi katika swala zima. Mifano ipo mingi sana, hata ukiangalia swala zima la makubaliano ya usambazwaji wa kazi za msanii utakuta kuwa shughuli hii inaendeshwa kwa kuaminiana zaidi ambapo msanii anasurrender master copy yake na distribution company inarudufu na kumwambia msanii
kuweka kielelezo chake (signature or stamp) katika copy then distributor anmjulisha msanii ni copy ngapi zimeingia sokoni na ngapi zimeuzwa tayari. Pius, hapa ndipo wengi wa wasanii huumia, kwani cha kwanza mihuri inatengenezwa kila corner dar-es-salaam na ni rehisi kuforge, cha pili hapo nyumbani kuna watu amabo kazi yao ni kuiga sahii za watu na kulipwa ujira wao. Ni msanii yupi anayejua kwa uhakika kuwa mabo hatya hayamtokei katika biashara yake? na pia hakuna msanii mwenye uwezo wa kufuatilia urudufishwaji wa kazi zake kikamilifu. Hebu niambie nani ana uwezo wa kufuatilia uuzwaji wa kazi zake nchi nzima na kujua hesabu kamili ya kazi zake zilizouzwa kihalali? Mwanya huu umewapa nguvu na nafasi kubwa wasambazaji wa muziki kurudufu kazi na kuuza ndani na nje ya nchi ta Tanzania bila ya wasiwasi wowote wa kuhojiwa idadi ya kazi zilizoingia mtaani bila ya idhini ya msanii mwenyewe.
Kwa kifupi ni kwamba soko la muzilki Tanzania limekuwa sana kwa wasanii ukilinganisha na miaka ya nyuma, lakini kwa kiasi kikubwa soko hili limekuwa maradufu kwa upande wa wasambazaji na na wajanja wengine mitaani na maredioni.
Recommendation. Nadhani serikali ianza kuangalia Bongo Flava kama njia mbadala ya tatizo la ajira kwa vijana na sio kama shughuli zisizo rasmi za kuganga njaa kama ilivyo sasa. Kwa hakika kama serikali itaangalia swala hili katika jicho hili (alternative employment) , basi sheria na interventions nyingine ( kama vile serikali kufungua mtambo na mradi wa kurudufu na kusambaza kazi za wasanii) zitawekwa kuilinda ajira hii inayotoa faida kwa vijana wengi nchini na sheria hizi being policies za nchi, kwa kiasi kikubwa zitawapa wasanii haki na nguvu juu ya kazi zao kwani kwa hakika wasanii wengi watapenda kuingia mikataba na vyombo vya serikali kuliko hivi vya binafsi visivyo na uhakika.

Mr Paul akijivinjari jijini Sydney
Mr Paul akijivinjari jijini Sydney

SS: Albamu yako mpya iko kwa mahadhi gani? Maana tulikuzoea kwa muziki wa taratibu na Zouk Pia je kwa sasa unakujaje?

Jibu: Mimi bado moyo wangu upo kwenye Zouk, ila kuhusu hatma ya muziki na mtindo nitakaotumia baadae, hilo litatikana na upeop wa soko unakwendaje.

SS: Vipi mafanikio yako ya kimaisha muziki umechangiaje?
Nini unaweza kujivunia mpaka ulipofikia sasa ukasema bila muziki hili lisingefanyika au kisingekuwepo?

Jibu: Kwa hakika muziki umechangia kwa kiasi kikubwa sana katika mafanikio ya maisha yangu. Mfano, muziki umenipa umaarufu ambao nimeutumia kupata pesa ambazo baadae nilizitumia kulipia masomo yangu ya elimu ya juu. Pius unakumbuka wakati fulani ilkuwa ni kama homa vile yaani kila msanii alikuwa ananunu gari za kifahari na vitu vingine (material things. i.e, golden chains, sophiscated mobile phones, expensive outfits and so forth). Namshukuru Mungu kwamba ingawa hata mimi nilizama katika mambo hayo, niliweza kuamka na kutambua kuwa muziki unaweza kunipa mengi makubwa kuliko metrial items. Na hapo ndipo nilpoanza kuuza material items na kuinvest into education. Currently, niangalia faida za muziki siongelei magari wala chains bali elimu ambayo kwa kiasi kikubwa nisingeipata bila ya muziki sasa ninacheka na nina kazi nzuri ya ofisini (Program Coordinator-Aboriginal an Torres staight Islander Health) katika nchi iliyoendelea.

SS: Kumekuwa na wanamuziki wapya kila leo watoto wanabana wakongwe na ni wakongwe wachache wamelimudu game na mchakamchaka wa vijana wapya unasemaje kuhusiana na hili?
Jibu: Ni kweli unalolisema, kwani mwenye macho haambiwi tazama. Ninaona na kuhisi pia kubanwa na vijana. Lakini siku zote ieleweke kuwa mtot halai na pesa ila nepi na mikojo. Kadri vijana wanavyotawala Bongo Flava ndivyo wakongwe wanapopata wasaa wa kukua na kuishi maisha ya kweli ya duniani Angalia mfano kutoka kwa Stara, Dola Soul, Mr Paul, Mr 2, na wengineo wengi ambao wamelichukulia jambo hili kwa mtazamo positive na kutumia nafasi hii kama changamoto ya kufanya vizuru zaidi maishani. Kwa wale wakongwe wanaomudu mchakamchaka wa vijana (Prof J, Lady Jay Dee na wengineo) mimi nawapa hongera sana kwani mchango wao katika kuendeleza muziki Tanzania ni muhimu sana. Pia lazima kuwe na viongozi wanaotoa muelekeo wa muziki au sio? Ingawa labda watu hawaoni kama wakongwe hawa ndio wanao control game na vijan wanfuata nyayo, ukweli ni kuwa vijana siku zote husikiliza nyimbo na kazi za wakongwe then wanaangalia jinsi ya kufanya refurbisment na kuleta ladha mpya.
Based on that, wakongwe bado wapo juu.

SS: Tumeshuhudia kumeguka kwa makundi na uhamasama kati ya makundi na makundi, Je unafikiri ni vigumu sana kwa wanamuziki wa kizazi hiki kuwa na umoja katika kupigania haki yao? je wafikiri hili lawezekana?
Jibu: Pius kwenye rizki hapakosi unafiki, Vijana wanaweza kuwa na lengo zuri sana la kuungana mwanzoni lakini kadri siku zinavyokwenda na maslahi yanavyopungua kutokana na baadhi ya sababu nilizozitaja katika jibu la swali la nne, vijana wanashindwa kujikimu na ugumu wa maisha na hivyo kuingia tamaa ya kufanya kazi kama solo artist huku wakitegemea kuwa labda neema itashuka kwa mtindo huu. Na mara kwa mara baada ya mgawanyiko huu na kutotimia kwa ndoto za baadhi ya wasaliti wa kundi, basi chuki dhidi ya wale waliotimiza ndoto zao utokea.
Mimi nadhani wanamuziki wa kizazi kipya wanaweza kufanya kazi katika mfumo wa makundi. Mbona bendi za muziki wa dansi zinaweza ingawa wanamuziki huama mara kwa mara? kinachohitajika ni usimamizi wa kuaminika na maslahi kwa wale waliobaki. Kama muziki utaendelea kendeshwa kwa ustaarabu uliopo sasa wa kuwalaghai na kuwapunja wasanii basi mfumo wa makundi usahauliwe. Mifano mingi imetolewa juu ya sababu za kuvunjika kwa makundi ya muziki wa kizazi kipya, na mara kwa mara imeonekana kuwa ni mameneja. Je hii sio sababu tosha ya kuanza kuangalia nia na sababu halisi za mtu kutaka kusimamia kazi zenu?

SS:Mwanamuziki gani anakuvutia kwa ndani ya Tanzania na Mwanamuziki gani wa nje unaweza sema nikipewa nafasi nitamshirikisha?

Ans. Kusema ukweli kwa wasani wa nyumbani mimi nina machaguo mawili makuu na nitatoa sababu za msingi za uchaguzi huu. First ni Stara Thomas, na Pili ni Lady Jay Dee. Nikianza na Stara, Huyu ni msanii ambaye kwa kiasi kikubwa ame influence maisha yangu kimuziki katika nyanya mbalimbali. Mfano, Stara anafanya muziki katika maadili ya Kitanzania. Hapa ninamaanisha kuwa dada huyu ameweza kubalance sanaa na maisha ya kawaida ya kila siku. Katika miaka yote aliyofanya muziki hajawahi kufanya jambo lolote lisilo la kawaida kwa maadali ya Kitanzania eti tu kwa nia ya kujipatia umaarufu. Na hili limempatia umaarufu mkubwa zaidi ambapo currently amekuwa akihusishwa sana katika maswala ya kijamii ambayo mtu hawezi kushirikishwa kirahisi kama hana record ya kujiheshimu.
Kuusu Jay Dee, Dada huyu yeye ananivutia katika swala la uvumilivu na utafutaji wa maisha. Jay Dee ni mwanamke shupavu and qiute arrogant, which is a good thing katika kuhakikisha kuwa unapata kile unachostahili. Nakumbuka dada huyu katika miaka ya nyumba alipitia katika misukosuko mingi (negative publicity) ambayo kama sio ushupavu wake basi angeliweza kuteteka na kupotea katika game, lakini mpaka leo ameendelea kuwepo na nadhani kama Mungu atamjalia maisha basi ataendelea kuwepo kwa kipindi kirefu. Pia Jay Dee amtoa mfano wa jinsi ambavyo wasanii wa bongo wanaweza kutoka katika anga za kimataifa. Jay Dee amekwenda Kora Mara kadhaa, amerecord muziki na wasanii wa nje wa kimataifa mbalimbali. Kusema ukweli anastahili kupewa mtaa katikati ya jiji la Dar kutokan na mchango wake.
kwa wanamuziki wa nje, kutokana na kuvutiwa kwangu na juhudi binafsi za mwanamuziki katika maswala ya kujiletea maendelea ya kudumu, kama ningepata nafasi kuchagua msanii wa nje kufanya kazi naye basi ningemchagua Nameless wa Kenya ambaye just like lady Jay Dee, msanii huyu anajaribu sana kuelekeza nguvu zake katika kupanua wigo wa kazi zake. mara kwa mara nimekuwa nikifuatilia habari zake na kuona kuwa anajitokeza sana katika anga za kimataifa in comparison na wasanii wengine wanaotumia lugha ya kiswahili ndani na nje ya East Africa.

Akiwa kwenye vakeshen zake baada ya mapumziko mafupi ya kazi.
Akiwa kwenye vakeshen zake baada ya mapumziko mafupi ya kazi.

SS: Ujio wa Taasisi kama COSOTA kwa ajili ya kusimamia vitu kama Hatimiliki na Hakishiriki, je umesaidia wanamuziki kiaje katika nyanja nzima ya kimaslahi? Je unafikiri wanamuziki ambao ni mmoja ya wadau wakubwa wa chombo hiki wana elimu ya kutosha kuhusiana na suala zima la HATI MILIKI na vipengele vyake?

Jibu: .Kuhusiana na COSOTA ndugu yangu Pius, mimi sitaki kuwa bias na kutetea wasanii muda wote. COSOTA ni Taasisi ambayo malengo yake ni mazuri na yanaweza kuwa na manufaa kama wasanii watacha tabia ya kuchukulia mambo juu juu tu. Mara nyingi COSOTA wamejaribu kuandaa makongamano yanayolenga kutoa elimu na kusensitize wasanii kuelewa haki zao na kuamka kutoka katika usingizi mzito wa kutojali maslahi yao, lakini response toka kwa wasanii imekuwa ni ya kudiscourage kwa kiwango cha juu. Muda mwingine huwa najiuliza hivi wasaniiwa bongo mganga aliyewaroga amekufa na dawa za kuwasaidia hazitafanya kazi mpaka afufuke au? Kuna shida gani kwenda katika ofisi za COSOTA na kupata kijarida chenye taarifa muhimu kwa wasanii? watu wanaweza kwenda BIllicanas na clubs nyingine isipokuwa kupita COSOTA.

However, labda ni muda muafaka kwa COSOTA kubadilisha approach wanayotumia sasa kuwasaidia wasanii. Labda wakiacha kutumia top-down approach whereby COSOTA identifies isseus and remedies on behalf of the artists, na kuemploy Bottom-up approach ambapo wasanii watahusishwa katika aspect zote za uchambuzi wa matatizo yao na dawa zake, basi wasanii wataanza kujitokeza kwa kiasi kikubwa wakijua kuwa kwa kiasi kikubwa wanaown hiyo intervention.
Asante kwa kunipa nafasi kutoa maoni yangu kuhusiana na muziki wa Kizazi kipya na maswala yanayofungamana nao.
Kind regards
Paul Mbenna.

Nakuacha na kibao Zuwena toka kwake Mr Paul


%d bloggers like this: