Mpira hauna Uzalendo

April 2, 2011

Shabiki akiwa amevalia Bango lenye Maandishi TP Mazembe 6-0 Simba eneo la Ferry Kigamboni Dsm, Homa ya mpambano wa marudiano baina ya TP Mazembe na Simba umepamba moto huku Ikiwa imebaki siku moja tu timu hizo kurudiana kwenye uwanja wa Taifa Jijini D’Salaam.

Posted with WordPress for BlackBerry.


Yanga yatia fora kwa mapato mechi ya Ufunguzi

July 17, 2008
Picha hii ilopigwa na Majig Mjegwa ikiwaonyesha Mashabiki wa Yanga kwenye mechi ya Ufunguzi

Picha hii ilopigwa na Majig Mjegwa ikiwaonyesha Mashabiki wa Yanga kwenye mechi ya Ufunguzi

TFF jana ilitangaza mapato ambayo yalipatikana kwenye ufunguzi wa michuano ya Tasker kati ya mechi za timu za Simba na Tusker ya Kenya na ile ya mahasimu wao Yanga na APR ya Rwanda.

Akitangaza mapato ya mechi ya ufunguzi, Dar es Salaam, jana ambayo ilizikutanisha Simba na Tusker ya Kenya, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema zilipatikana sh. milioni 79.6, ambapo watu 18,420 walilipa kiingilio.

Alisema mechi kati ya Yanga na APR ya Rwanda iliyochezwa Jumapili katika uwanja huo zilipatikana sh. milioni 95 kutokana na watu 23, 719 kulipa viingilio, ambavyo vilikuwa sh. 25,000, sh.20,000, sh. 15,000, sh.10,000, sh.7,000, sh.5,000 na sh.3,000.

Wachunguzi wa mambo ya kispoti wanasema kuwa hii inaonyesha umaarufu wa timu ya Yanga umeongezeka kulinganisha na Simba, na huenda ikatokana na usajili wa Timu ya Yanga ambapo Kusajiliwa kwa kipa Juma Kaseja kumefanya mashabiki wa Mpira kutaka kumuona awapo uwanjani.

Katika mtanange huo wa Yanga na APR mashabiki walilipuka pale KAseja alipokuwa akiingia n wachezaji wenzie uwanjani na kuwa akishangiliwa kila awapo na mpira na mashabiki wa Simba walisikika wakimzomea na kumtupia maneno ya kejeli ingawa hayakufua dafu kutokana na mashabiki wa Yanga kuwa wengi na wenye nguvu zaidi.

Aidha Mwakalebela alisema kuwa kutokana na mwamko uliooneshwa na mashabiki wa mpira wa miguu, mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza ambazo zilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa zamani sasa zitachezwa Uwanja Mkuu wa Taifa.


%d bloggers like this: