Tathmini ya Hassan Mhelela wa BBC: Chelsea walizidiwa au walijiamini kupita kiasi?

September 29, 2010

Unapozungumzia uwezo wa wachezaji wa Chelsea, unaangalia idadi ya magoli waliyofunga msimu huu unaridhika kuwa huenda soka yao si ya kuburudisha, lakini huwezi kuhoji dhamira yao kutikisa nyavu nafasi zinapojitokeza.

Lakini sogeza muda mbele kidogo, mpaka Jumanne tarehe 22 Septemba usiku, ni mechi ya kombe la Carling, ikichezwa Stamford Bridge dhidi ya Newcastle United  (waliorejea upya Premier League), wengi walidhani Chelsea watakuwa kama wanasukuma mlevi kuelekea ushindi mnono.

Hapana. Matokeo ya mwisho ni  Chelsea 3 – Newcastle United 4! Inakuwaje tena? Ah! Ndiyo soka ilivyo.

Je Chelsea walijiamini kupita kiasi? Au walizidiwa na soka kabambe la vijana wa Newcastle United?

Kwa meneja Carlo Ancelotti, ambaye ameshaeleza wasi wasi wa wachezaji wake wengi kujeruhiwa, ni  wazi atakuwa akijiuliza, matokeo hayo yataathiri ufanisi katika Ligi Kuu ya Soka ya England?


Mashabiki Liverpool wakasirishwa na timu

September 28, 2010

Meneja wa Liverpool Roy Hodgson amesema “hawezi kuwalaumu” mashabiki walioendesha upinzani dhidi ya wamiliki wa klabu baada ya timu hiyo kwenda sare ya mabao 2-2 na Sunderland.

Amesema: “Sitazamii mtu yeyote ndani ya klabu anahitaji kitu kingine zaidi ya usuluhishi kutokana na matatizo ya umiliki.”

Mashabiki wanataka kuona klabu yao inasonga mbele na kumaliza matatizo ya wamiliki wanaotaka kuuza klabu.

Mashabiki takriban ya 10,000 walibakia uwanja wa Anfield baada ya mchezo kumalizika wakihoji mipango ya wamiliki wawili wa klabu hiyo George Gillett na Tom Hicks ya kuuza klabu hiyo.

Benki ya RBS, inayoidai klabu hiyo paundi milioni 237 katika deni la Liverpool la paundi milioni 282, wanasubiriwa kusema chochote juu ya deni lao mwezi wa Oktoba.

Benki hiyo inayomilikiwa kwa asilimia 84 na serikali, huenda ikaamua kumiliki kampuni ya Kop Holdings, iliyotumiwa na Hicks pamoja na Gillett mwezi wa Februari mwaka 2007 kuinunua Liverpool.

Wamiliki hao inasemekana wanataka paundi milioni 600 kuiuza klabu hiyo, huku paundi milioni 420 wakizipata watakuwa wameiuza klabu kwa hasara.

Hata hivyo iwapo klabu ya Liverpool itaangukia mikononi mwa umiliki wa benki, inaweza kuuzwa kwa paundi milioni 280, ikiwa ni pamoja na adhabu ya paundi milioni 40.

Meneja wa Liverpool Hodgson yupo katika heka heka kubwa za kuhakikisha klabu hiyo inafanya vizuri tofauti na msimu uliopita ilipomaliza nafasi ya saba katika ligi.

Hadi sasa Liverpool imeshinda mchezo mmoja tu kati ya sita ya ligi msimu huu na walitolewa katika mbio za kuwania kombe la Carling nyumbani kwao walipofungwa na Northampton ya daraja la pili hivi karibuni.


Keegan amshambulia Rooney

September 28, 2010

Kevin Keegan

Meneja wa zamani wa England Kevin Keegan, amesema Wayne Rooney asivilaumu sana vyombo vya habari kutokana na kushuka kiwango chake cha usakataji soka kwa klabu yake ya Manchester United.

Rooney mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akibebeshwa lawama nyingi kuhusiana na maisha yake binafsi, amefunga bao moja tu katika michezo sita Manchester United iliyocheza msimu huu.

Na Keegan anaamini aina ya maisha aliyochagua kuishi Rooney hayakumsaidia.

Keegan ameongeza kusema: “Huwezi kuanza kusema kumekuwa na mapaparazi wengi au vyombe vya habari vimemuandika sana.”

“Huwezi kuwa na mawasiliano ya watu wote, ukauza haki ya harusi yako kwa magazeti na mambo mengine kama hayo na ghafla unageuka na kusema, hilo ndio bomba ninalotaka kulifungua lakini jingine tulifunge.”

Ameongeza kusema Keegan:”Ni bomba moja tu na kadri ninavyofahamu enzi zangu za uchezaji soka, iwapo unatangaza viatu vya mpira na vitu vinavyofanana na hivyo, unatakiwa kujitokeza. Ni lazima uonekane magazetini.

Lakini Keegan akamuasa Rooney ni vyema kuiepusha nyumba na familia yake na mambo hayo na atafute ushauri iwapo anataka kuendelea na maisha kama hayo.

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Rooney amekuwa akikabiliwa na maudhi yanayoandikwa na vyombo vya habari kumhusu yeye na kwa mara nyingine hakucheza vizuri siku ya Jumapili walipotoka sare ya mabao 2-2 na Bolton katika uwanja wa Reebok.

Rooney alitolewa na nafasi yake ikachukuliwa na Federico Macheda katika dakika ya 61, ingawa mshambuliaji huyo wa zamani wa Everton baadae alionekana kufunga mguuni mfuko uliojaa barafu.

Lakini meneja msaidiza wa Manchester United Mike Phelan, amesema mshambuliaji huyo atakuwa tayari kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya siku ya Jumatano dhidi ya Valencia.


Tukipata kocha wa hivi lazima tucheze World Cup 2014 tu!!

September 27, 2010

Hebu angalia huyu kocha huyu jisi anavyowaadhibu wachezaji wake na ufikirie kama ndio Tanzania inapata Kocha kama huyu!! Kiukweli akina Nsajigwa, Mgosi, Tegete, Kaseja kama nawaona jinsi watakavyojituma. hehehehehehe.


September 27, 2010

Arsenal’s midfielder Alex Song attends a press conference at Partizan Stadium in Belgrade on September 27, 2010, on the eve of their Champions League Group H football match against Partizan Belgrade.


Meryl and Mwisho are Officially Engaged

September 26, 2010

A shaky Mwisho went on bended knee and asked Meryl if she would marry him and she undoubtedly said “I’d love to baby” and Mwisho slipped her tanzanite ring on her ring finger.

In his speech, Mwisho had made it clear that he doesn’t come from a romantic family. “Whatever mistakes I make now, I hope I have a lifetime to do better things,” Mwisho assured all present as he laughed.

The two then shared their first kiss as an engaged couple.
Meryl’s aunt, Jamela was curious whether this was serious or a joke and Meryl assured her that it was very serious and nothing can judge them but love and God.
Meryl said she was aware that people may have their own thoughts around their decision to get Engaged.

“The only people we have to answer to is us. We have decided that we want to spend the rest of our lives together,” Meryl said.

Meryl added that fate had it that they should be together on Big Brother All Stars because they had both seen and loved the other on TV. Meryl’s aunt helped her as she was talking saying “It was love at first sight”

Down on bended knee


Frank Lampard kukosa mechi muhimu

September 26, 2010

Frank Lampard atakosa michezo muhimu kwa timu yake ya Chelsea na timu ya taifa ya England kutokana na kuendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa ngiri.

Lampard mwenye umri wa miaka 32 hajaichezea klabu yake kwa mwezi mmoja na meneja wake Carlo Ancelotti amethibitisha kiungo huyo hataweza kucheza kwa takriban wiki mbili zijazo.

Kipindi hicho atakosa mechi dhidi ya Marseille, Arsenal na mchezo wa kufuzu mashindano ya Euro 2012 wakati England itakapopambana na Montenegro.

Ancelotti ameendelea kusema, Lampard hawezi kucheza kwa sasa, wanahitaji muda zaidi tofauti na walivyotazamia.

Kwa vile hajaichezea Chelesea, Ancelotti amesema vile vile hatakuwa tayari kuichezea timu ya taifa.

Lampard alirejea mazoezini baada ya kufanyiwa upasuaji tarehe 31 mwezi wa Agosti, lakini amekuwa akisumbuliwa na maumivu kwenye kovu.

Tayari amekosa mechi za England walizoshinda za kufuzu michezo ya Euro 2012 dhidi ya Bulgaria na Switzerland mapema mwezi wa Septemba na pia atakosa mechi dhidi ya Montenegro katika uwanja wa Wembley tarehe 12 mwezi wa Oktoba.

Mara ya mwisho kuichezea Chelsea ilikuwa tarehe 28 mwezi wa Agosti timu hiyo ilipoifunga Stoke mabao 2-0.


%d bloggers like this: