WERRASON NA JB MPIANA

July 31, 2014

10487492_786610188058443_8770898316309966766_n

JB MPIANA KENDA KUMJULIA HALI RAFIKI YAKE WERRASON, KUTOKANA NA MSIBA WA KATIBU MKUU WA FOUNDATION WERRASON, HUGUES KITAMBALA. KIFO KILIO TOKEA TAREHE 26 – 06 – 2014. KWENYE UKUMBI WA ZAMBA PLAYA JIJINI KINSHASA.

PICHANI HAPO NI NYUMBANI KWAKE WERRASON.

WEKENI  USHABIKI MBALI, JAMAA HAWA NI MARAFIKI. MASWALA MENGINE NIYA KIBISHARA.

LUBONJI WA LUBONJI


FALLY IPUPA KAALIKWA NA BARACK OBAMA

July 28, 2014

1401914_10151762706852844_442011655_o

 

KUTOKANA NA MUALIKO WA RAIS BARACK OBAMA, MA RAIS 47 WA INCHI ZA AFRICA WATASHIRIKI  KWENYE KIKAO CHA MKUTANO UTAKAO FANYIKA KWENYE IKULU YA MAREKANI ” WHITE HOUSE “, TAREHE 6 NA 7 MWEZI WA NANE MWAKA HUU.

UKIWAONDOA MA RAIS, MUALIKO UMETOLEWA PIA KWA WASANII WANAMUZIKI 10 KUTOKA BARANI AFRICA, AKIWEMO KIJANA FALLY IPUPA DICAP LA MERVEILLE EL MARABIOCHO. AMBAE  NDIE ATAKAE IWAKILISHA AFRICA YA KATI.

MADHUMUNI YA MKUTANO HUO, NIKUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA INCHI ZA AFRICA NA MAREKANI.

KWELI FALLY IPUPA NDIE ATAKAEKUA MWANAMUZIKI WA KWANZA KULISAKATA RUMBA KWENYE IKULU YA  ” WHITE HOUSE “? WAIT AND SEE

 

LUBONJI WA LUBONJI

 


JB MPIANA KAMGEA BINTIE DAIDA GARI AINA ( RANGE ROVER )

July 27, 2014

KUTOKANA NA DAIDA KUFAULU SHULENI NA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 18.

JB MPIANA PAPA CHERI AMBAE HUA HAPENDELEI SANA KUIWEKA FAMILIA YAKE MBELE YA VYOMBO VYA HABARI, NAONA MWAKA HUU KASHINDWA KABISA KUJIZUIA.

KWANZA KAMRUHUSU MWANAE WA KWANZA ABRAHAM MPIANA AMBAE WENGI WALIKUA HAWAMFAHAMU, AWEZE KUSHIRIKI KWENYE MIKUTANO MBALIMBALI NA KUJITAMBULISHA KAMA MTOTO WA JB MPIANA.

PILI,NI KWA MARA YA KWANZA ” MUKULUMPA PUISSANCE ” KUWAALIKA WATU NYUMBANI KWAKE JIJINI KINSHASA SEHEMU IJULIKANAYO KWA JINA LA MONT-FLEURY,AMBAKO KAJENGA JUMBA KUBWA LA KIFAHARI,ILIKUA SIKU YA KUSHEHEREKEA B’DAY YA BINTI YAKE DAIDA ALIPO TIMIZA UMRI WA  MIAKA 18.

KATIKA HALI YA KUZIDI KUMHIMIZA DAIDA ILI  AENDELEE KUFANYA VIZURI CHUONI, KAMGEA ZAWADI LA GARI ” RANGE ROVER ” MBELE YA WAANDISHI WA HABARI.

DAIDA AKIWA MWENYE FURAHA SANA, KAMRUKIA BABA YAKE NA KUMSHUKURU  KWA KUSEMA ” YEYE NI BINTI MWENYE FURAHA KUWAZIDI WENGINE WOTE DUNIANI”.KAIFURAHIA  SURPRISE NZURI YA GARI ALIYOPEWA NA BABA YAKE, PIA KATOA SHUKRANI ZAKE ZADHATI KWA BABA ZAKE WA WENGE MUSICA AMBAO KAWATAJA KWA MAJINA ( PAPA WERRASON, PAPA ADOLPH DOMINGUEZ ), KWA UJIO WAO KWENYE SHEREHE YAKE YA KUZALIWA ,PIA KUHUSU ZAWADI KEMKEM ALIZO ZIPOKEA KUTOKA MIKONONI MWA WAZEE WAKE HAO.

MWISHONI, DAIDA KAMUIMBIA BABA YAKE WIMBO WA RIHANA ” DIAMONDS “,JB MPIANA KAONEKANA MWENYE KUGUSWA SANA NA MANENO YA BINTI YAKE .

 

LUBONJI WA LUBONJI


VIDEO CLIP MPYA YA FERRE GOLA ” VIVE LES MARIES “

July 24, 2014

 

 • HERVE  BATARINGE, Maarufu kwa Jina la FERRE GOLA, kazaliwa jijini KINSHASA Tarehe 03-03-1976.
  Wazazi wake ni wenyeji wa Mkoa wa BAS CONGO.
  FERRE GOLA kaanza Muziki  kama baadhi ya Vijana wengi Inchini Congo kwenye Band za mtaani,
  WERRASON Ndie kagundua Kipaji chake, na ilikua  kwenye Tamasha Jijini Kinshasa.
  Ndipo kaja kumpendekeza  kwenye Group WENGE MUSICA ASILIA KABLA YA MGAWANYIKO.
  Siku yake ya kwanza Kwenye Group WENGE MUSICA BCBG 4×4, Aina yake ya Uimbaji na Sauti yake ilivyo Nyororo, Ikamfanya ADOLPH DOMINGUEZ AMPACHIKE JINA LA ” CHAIR DE POULE ” Ikimaanisha UIMBAJI ULIO SISIMUA NYOYO HADI MWILI UKAINGIWA NA BARIDI.
  KWENYE GROUP WENGE MUSICA MAISON MERE katunga nyimbo 3. wimbo wa kwanza ni VITA IMANA unapatikana kwenye Album ” SOLOLA BIEN ” iliyotolewa mwaka 1999, Wimbo wa pili Upo kwenye Album ” À LA QUEUE LEU LEU ” iliyo tolewa mwaka 2002 ambayo ina CD 2. kwenye CD ya kwanza kaweka wimbo CHETANI ( WIMBO ULIOMPA JINA LA SHETANI ) na kwenye CD ya pili kaweka wimbo ” VICTIME D’AMOUR ” .
  Baada ya kujiondoa  NA WENZIE KWENYE GROUP WENGÉ MAISON MÈRE MWAKA 2004 NA KUUNDA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE, wakatoa ALBUM ” MIRACLES “. kwenye ALBUM hiyo ambayo pia ilikua na CD 2. kwenye CD ya kwanza kaweka wimbo ” AMOUR INTÉRÊT ” NA KWENYE CD YA PILI kaweka wimbo ” 100 KILOS “.
  Mwishoni mwa mwaka 2005, kajiunga na KOFFI OLOMIDE (QUARTIER LATIN) Mwaka 2006 ilipo tolewa Album ” DANGER DE MORT “, kaweka wimbo ” INSECTICIDE “.
  Mwaka 2006 Kaanza career Solo, na katoa album yake ya kwanza ” SENS INTERDIT ” ALBUM STUDIO 2007 INANYIMBO 12,
  Mwaka 2009 KATOA ALBUM STUDIO ” QUI EST DERRIÈRE TOI ” INAYO CD 2 NA KILA CD INANYIMBO 9 .
  Mwaka 2013 KATOA ALBUM STUDIO ” BOITE NOIRE ” INAYO PIA CD 2. CD ya kwanza inanyimbo 12, na CD ya pili nyimbo 10.
  FERRA GOLA Katoa Single 2 . yakwanza LUMBUKUKU iliotolewa mwaka 2008, na ” AVANT GOUT ” ILIOTOLEWA MWAKA 2011
  KAFANYA FEATURING NA WASANII KADHAA!!! WAKIWEMO   :
  La vie à zéro Feat Didier Milla (2005)
  Terre sacrée Feat Doudou Copa (2007)
  Déception feat Alpatchino (2008)
  Kayembe Temba Feat Simaro Lutumba (2009)
  Dj laisse-moi la place Feat Djungle (2009)
  Love moi Feat Bill Clinton Kalondji (2010)
  Mademoiselle Feat Bolinga (2011)
  Tshekele Pete Feat Phill Darwin (2011)
  Unhappy ft Zik Berry
  Caresse Feat Singuila (2013)
  J’ai tout donné Feat Dry du groupe Sexion D’Assaut (2013)
  Ko Ko Ko Feat Lino Versace (2014)
  Songa Flesh Feat Black Bazar (2014)
  *** MWAKA HUU YUKO KWENYE MATAYARISHO YA MAXI SINGLE ” BLACK BOX ” MTAKUWEPO NA NYIMBO 5.
  TUZO ALIZO ZIPATA FERRE GOLA KATIKA CAREER YAKE.
  • 2005: Kapewa Tuzo la Group Bora la Africa ya Kati Kwenye KORA AWARDS, Wakati bado akiwa  na Orchestra  LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.
  • 2011 : FERRE GOLA kachukua Tuzo la Gold Disc Kutokana na Mauzo ya ALBUM Qui Est Derrière Toi . ZAIDI YA CD 11000 ILINUNULIWA.
  • 2011 : Kapewa Tuzo 3 Kwenye TROPHY AFRO-CARIBEEAN. ZIKIWEMO TUZO LA MWANAMUZIKI BORA, WIMBO ” ZAZOU ” UKATEULIWA WIMBO BORA. NA UKAPEWA TUZO LA BEST CLIP
  • 2011 : Kapewa Tuzo LA MWANAMUZIKI WA KIUME MWENYE SAUTI BORA AFRICA YA KATI.Kwenye  Ndule Awards
  • 2013 : L’album BOITE NOIRE Ikachukua nafasi ya kwanza Kwenye   iTunes  ‘World Music’
  • 2013 : Kapewa Tuzo 2 kwenye Ndule Awards ( MWANAMUZIKI BORA na TUZO la WIMBO BORA ” KITI YA LIBAYA “
  • 2014 : Kapewa Gol Disc kutokana na Mauzo ya ALBUM Boite Noire , ZAIDI YA CD 80.000 IMENUNULIWA .
  • FERRE GOLA NI MWANAMUZIKI PEKEE AMBAE KAHAMIA KWENYE ORCHESTRA NYINGINE KWA MALIPO. KWA MUJIBU WAKE MWENYEWE, KASEMA HADI UHAMISHO WAKE UWE KAMILI NA YEYE KUJIUNGA  NA GROUP QUARTIER LATIN,PALIKUA NA MAKUBALIANO KATI YAKE NA KOFFI OLOMIDE YALIYO MLAZIMU MKONGWE HUYO ATOE KITITA CHA DOLA ELFU 17 ( 17000 USD )KAMA MALIPO YA UHAMISHO.

  LUBONJI WA LUBONJI


TUONGELEE WENGE MUSICA BCBG 4×4 KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA ( SEHEMU YA SITA )

July 23, 2014

TUNAENDELEA NA SIMULIZI YA KUSAMBARATIKA KWA ORCHESTRA WENGE MUSICA  4×4  TOUT TERRAIN NA MPIGA GITA BURKINA FASO MBOKA LIYA.( SEHEMU YA SITA )

KWENYE SEHEMU HII TIZAMA KUANZIA DAKIKA YA 58 ” HADI 01H08.

 

BURKINA FASO : Ukorofi ukaja kujitokeza kutokana na Tamaa, natoa mfano wangu mwenyewe, ( KWENYE WIMBO WANGU WA SERGE PALMI, SERGE PALMI NI KIJANA AMBAE MAKAZI YAKE NI JIJINI BRUSSELS, KWAKUTAKA WIMBO WANGU HUO UPEWE JINA LAKE, KALAZIMIKA KUTOA KITITA CHA HELA TAKRIBAN DOLA ELFU TANO ( 5000 USD ). CHA AJABU KWA PESA HIZO, JB MPIANA KACHUKUA DOLA ELFU MBILI ( 2000 USD ) NA KAJA KUNIGEA MIMI PESA ZILIO SALIA, YAANI DOLA ELFU TATU ( 3000 USD ) HUONI KAMA HIYO NIDHULUMA  ?

MTANGAZAJI : Umejuaje kama Kutokana na Wimbo wako huo wa SERGE PALMI ,JB MPIANA kapewa Dola Elfu Tano Pahali pa Dola Elfu Tatu alizo kugea?

BURKINA FASO : Kwani wewe wafikiri kuna siri ? wala usijidanganye, katika mambo yetu haya, hakunaga na Siri!!!

MTANGAZAJI : Ukaelewaje kitendo hicho alicho kifanya JB MPIANA kwa kuchukulia kiasi cha hela zako Dola 2000

BURKINA FASO : Kwangu mimi nilichukulia kua Jambo la kawaida tuu,Binafsi sina tabia ya Tamaa,Unapo nilinganisha na wao,utagundua kwamba wao ni Watu wenye Tamaa na hupenda kuishi maisha ya Juu na ya kifahari, wakati uwezo hawana.Kuna methali isemayo : Roho ya Tamaa mwishowe humpeleka Mtu kwenye hali ya kufilisika.

Mimi nayafurahia Maisha yangu ya leo,Pia namshukuru Mungu kunijaalia kwa kunipa kipaji kinacho niwezesha kuhudumia Familia yangu. Kama Wewe hujaridhika na kile ulichonacho na hupendelea vyote vinavyo patikana Duniani viwe vyakwako, basi Rukhsa kwako!!! Unacho takiwa kukumbuka ni kwamba, Walikuwepo hapa Duniani Matajiri wakubwa zaidi yako, Waliondoka na kuviacha vyote hapahapa. Akina MOBUTU ambao walikua na Utajiri wakupindukia, wako wapi leo?

MTANGAZAJI : Kweli kabisa kwa yale uyanenayo, Watu Tunaondoka na kuviacha Vyote Hapa Duniani.Tulikuja bila Kitu na Ndivyo tutakavyo rudi. Sasa lipo Swali, Watu wanataka kujua : MENGI KUTOKANA NA MAFAANIKIO YAKO,KUANZIA WAKATI BADO MPO KWENYE GROUP WENGE BCBG 4×4 TOUT TERRAIN, HADI BAADA YA KUSAMBARATIKA KWA GROUP HILO, NA WEWE KUHAMIA WENGE BCBG, YASEMEKANA ULIKUA UKITUMIA SANA MAMBO YA KIUSHIRIKINA, WASEMAJE HAPO!!!

BURKINA FASO : Ntakacho kisema kwa hapo, ni kwangu Mimi kukubali Ndio, hua natumia Dawa, ILA SASA NILAZIMA UFAHAMU KWAMBA DAWA NIITUMIAYO MIMI SI YA KAFARA, BALI NI UWEZO KUTOKA KWA BABA MUNGU.

Ufundi wangu Kwenye GITA, wala sijaenda Shule, ni kipaji nilichopewa na MUNGU. Ntakacho ongezea hapo ni kwamba nilibahatika kufanya kazi na wapiga Gita WAKONGWE NA  MASHUHURI INCHINI CONGO, HIVYO IKANIPELEKEA NIJIIMARISHE VIZURI KABISA KWENYE KAZI HIYO.

MTANGAZAJI : Kwahiyo unatuambia kama kweli hujawahi kugusa Dawa ?

BURKINA FASO : Wala sijui kitu kinachoitwa Dawa maishani mwangu

MTANGAZAJI : Umewahi alakini kufanya kazi na Watu wanaohusudu Dawa, Wale ambao uliwataja kuwa Wafwasi wa Shetani.

BURKINA FASO : Wala sijawaita wao Mashetani kwakisa eti nimewakuta na Dawa, Hapana kabisa,Ninacho jitahidi kukuelewesha ni kwamba, Unapo wauliza wale Watu ambao ni wacha Mungu ni zipi Dalili za watu wa Shetani ? Watakujibu kua : WAFWASI WASHETANI UTAWAJUA KUTOKANA NA MANENO YAO,MWENENDO WAO,KADHALIKA NA VITENDO VYAO. Hayo yaweza kukusaidia kumjua Mtu upande gani anako elemea. Ama Kushoto au Kulia. KWAKIFUPI SIWEZI NIKAKATAA KATU KAMA MAMBO HAYO YAKISHIRIKINA HAYAPO!!! ILA BINAFSI SIJAWAHI KUMKUTA MTU YEYOTE AKITUMIA KAFARA. BALI NAONA KAMA NYOYO ZAO NA VITENDO VYAO HUENDANA KABISA NA VYA WAFWASI WA SHETANI.

Itakuaje wewe wajua fika kama Mimi kama Mfanyakazi wako, Mpiga GITA SOLO Namba Moja,niko kwenye mahitaji, Pindi ninapo kupigia simu hutaki kupokea,Nikueleweje?

MTANGAZAJI : Ni Mtu gani uliekua ukimpigia Simu na akakataa kupokea?

BURKINA FASO : Ntakupa mfano wa MUKULU ( JB MPIANA ), Yeye hujua hali yangu halisi kipesa ilivyokua Mbaya,Nikampigia Simu ili nipate Msaada kutoka kwake, huku yeye kakataa katu kupokea Simu!!!

MTANGAZAJI : Kwa wakati ule Wewe ni Mmoja wa Wanamuziki wake

BURKINA FASO : Ndio nikitembelea Gari Bovu kabisa JIJINI KINSHASA, Vijana wa JIJI hilo ndio waweza kukuhadithia vilivyo. Gari lenyewe nikalipachika Jina la ” POURQUOI OZONGELI SOUVERAIN OSALELI YUDA ” ikimaanisha ” KWANINI WARUDILIA KUMFANYIA KAZI SOUVERAIN ( JB MPIANA ) WAMTUMIKIA YUDA ESKARIOTE ” ( kacheka sana Kalipiga Gita likiendana na Maneno niliyo yataja hapo juu ) tizama Vidéo anzia kwenye Dakika 1:03:27.

TUMEACHANA VIBAYA SANA MIMI NA JB MPIANA, KANIFUKUZA KAMA MBWA!!!

MTANGAZAJI : Wewe uliamua kwa hiari yako mwenyewe kwenda kwa JB MPIANA baada ya Mgawanyiko wa Group WENGE MUSICA 4×4. JB MPIANA kakusaidia kwa kiasi kikubwa, Pesa unazo, Umaarufu unao, Magari unayo, Umesafiri kwenye Inchi Mbalimbali kutokana na JB MPIANA, Huwezi ukamsaliti. NIKIPI KILICHO TOKEA HADI UKAJIONDOA ?

BURKINA FASO : Sidhani kama nimemtukana na wala sijaongelea Ubaya wowote unao husiana naye.

MTANGAZAJI : Waonekana mwenye Hasira ulivyo ongelea swala la JB MPIANA kukataa kupokea Simu yako

BURKINA FASO : Wala sivyo,kuna kitu kimoja ambacho watakiwa kuelewa, MWANAMUZIKI ANAYO HAKI YA KUJIELEZA POPOTE PALE TENA KWA WAKATI WOWOTE ULE. Chukulia Mfano wa hapa Ulaya,utawaona WANAMUZIKI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI (MANCHESTER, LONDON, LIVERPOOL, wakipanda Jukwaani kwa pamoja wala hilo si tatizo kabisa!!!

MTANGAZAJI : Cha maana ilikua ni kwako wewe kumtaarifu Bosi wako kama wahitaji kwenda kufanya Kibarua sehemu fulani tena kwa kipindi kadhaa, sidhani kama anaweza kukataa!!!

BURKINA FASO : Mambo gani hayo ya kijinga waniletea wewe!!! Rukhsa yanini nimuombe? kwani nilikua na Mkataba naye?KWANI NI YEYE ALIENIFUNZA UTUMIAJI WA GITA ?

MTANGAZAJI : Ulikua mmoja wa Wanamuziki wa Group Lake

BURKINA FASO : Sawa,Sijakataa !!! Niwajibu wa Bosi mwenyewe ili Watu wazidi kumheshimu,ni vyema awe mwenyewe wakwanza Mtu mwenye kutekeleza kanuni na Utaratibu wa Kampuni. Nikama leo hii anavyo dharaulika Rais wa Congo, kwakua kashindwa kwanza kujiheshimu mwenyewe.

Wengi hawamtakie Mema,Maombi yao kwanza ni janga la Njaa litatuliwe, Watoto waende Shule, hivyo, iondolewe picha mbaya sana inayo zagaa kuhusu Vijana wa mtaani wa JIJI LA KINSHASA, maarufu kwa jina la ” SHEGE “. Wala sidhani kama Mwenyezi Mungu kawaleta Duniani Vijana hao kwa madhumuni ya kuteseka, Watu husahau kabisa kwamba Taifa la kesho litajengwa na Vijana hao. Kwa leo hii wanachukuliwa kama Vibaka, Walalahoi, na Watu Wengine wanawachezesha kama Mpira kwa Maslahi yao binafsi. hapa ntawataja JB MPIANA NA WERRASON. ILA IPO SIKU VIJANA HAO WATAAMKA NA UMMA UTAWAELEWA.  NA HUO NDIO UTABIRI WANGU.

MTANGAZAJI : Baada ya Mgawanyiko Wa Group WENGE MUSICA 4×4, kikosi chenu kilikua na WANAMUZIKI BORA ZAIDI,akina PRINCE ALAIN MAKABA, BLAISE BULA… IKAWAJE NAO WAKAJA KUJIONDOA ?

BURKINA FASO : Kweli kabisa, Tulikua na Kikosi kizuri na kamili kabisa, Kwenye GITA walikuwepo PRINCE ALAIN MAKABA,MIMI MWENYEWE MBOKA LIYA, PATIENT KUSANGILA, JIJINI KINSHASA WALIONGEZWA PIA VIJANA KADHAA AMBAO  WALIKUA WAPIGA GITA WAZURI. ILA kuhusiana na hawa vijana, Ntasema kilikua kikosi cha pili, kwakua Mazoezi tulikua tukifanya nao Nyumbani kwake JB MPIANA. Alikuwepo pia TITINA AL CAPONE.

MTANGAZAJI : Kweli Group lenu lilikua na Mchanganyiko wa Vichwa.

BURKINA FASO : Kwa upande wa Waimbaji,walikuwepo JB MPIANA, BLAISE BULA, AIMELIA, ALAIN MPELA.

MA REPPA WALIKUA TUTU GALLUGI NA ROBERTO WUNDA. GROUP LETU LILIKUA NA KIKOSI KIZURI SANA.

TATIZO LIKAJA KUTOKANA NA TAMAA, SISI WENGINE TUKIWA NA MIPANGILIO YA MAENDELEO KATIKA MAISHA, KUMBE MWENZETU YUKO NA NJAMA ZAKE YAKUTAKA KUWATIMUA MASTAFU WOTE WALIO TOKANAYE KWENYE GROUP WENGE BCBG 4×4.ORIGINAL.

MTANGAZAJI : Hapo ninani unaye muongelea ?

BURKINA FASO : Si Mwengine bali ni JB MPIANA, YEYE KESHATUONA KAMA PINGAMIZI KUBWA,HASA KUHUSIANA NA MASWALA YA PESA,NDO USIPIME KUMUULIZA!!! KWA HIYO NI BORA KWAKE YEYE KUWAONDOA WALE WOTE AMBAO WANAO UWEZO WAKUMUULIZA BILA WOGA WOWOTE MASWALA YOTE YANAYO ENDANA NA GROUP, YAKIWEMO YALE YANAYO HUSIANA NA “PESA”. KADHALIKA HATA HUKO KWENGINE KWA JAMAA YAKE NA RAFIKI YAKE MAMBO YAKAWA VILEVILE.

MTANGAZAJI : Rafiki yake Gani huyo?

BURKINA FASO : WERRASON, JB MPIANA NA WERRASON NI MARAFIKI WAKUBWA, NA MAMBO YAO WANAYAFANYA KWA MPANGILIO MMOJA… ITAENDELEA …

LUBONJI WA LUBONJI

 

 

 

 

 


TAFSIRI YA WIMBO ” TRAHISON ” UTUNZI WA LUTUMBA MWIMBAJI AKIWA PEPE KALLE

July 20, 2014

 

Mokili nga na ya ba ndeko na kuti makambo lelo nga na ko yemba ngo /MAMBO NILIYO YAKUTA DUNIANI NI MAKUBWA JAMANI,NA LEO HII NAAMUA KUYAONGELEA KUPITIA WIMBO

Mobembo nga na ya na mokili na moni makambo yango nga na ko yemba ngo /SAFARI YANGU YA  HAPA DUNIANI,NIMEYAONA MENGI,NI KWAMAANA HIYO  NAAMUA KUYATUNGIA WIMBO

Na nzela ya mokili to yaka mboka mboka moto na libongo na ye a ko kiteee / TUNAPO KUJA DUNIANI,HUA TUNATOKEA MAHALA TOFAUTI,NA KILA MMOJA WETU HUFIKIA KWENYE BANDARI YAKE!!!

To botama na mokili moto na ngonga na yé / UJIO WETU KWA HAPA DUNIANI KILA MMOJA HUZALIWA KWA SIKU YAKE NA WAKATI WAKE KAMILI

Moto na chance na yé na elongui na yée  / KILA MTU HUJA NA UMBO LAKE, PIA NA BAHATI YAKE

To yaka na mokili to zali nde ba paya mabélé yango nde eko yambaka biso / KWA HAPA DUNIANI SISI NIWAGENI TUU, UDONGO NDO HUA UNATUKARIBISHA

Mabélé ooh ooh mabélé to ko buakelaka soyi e / UDONGO OOH NDO HUO UDONGO AMBAO HUA TUNAUTEMEA MATE

Mabélé ooh yeh mabélé eko bombaka bosoto na biso / UDONGO OOH,UDONGO NDO HUO AMBAO HUA TUNAUTUMIA KAMA DAMPO

Mabélé ooh ooh yeh mabélé eko boyaka ebembe tè / UDONGO OOH , KAMWE UDONGO HAUMKATAI MAITI

Mabélé ooh patrick mangassa ba ko kounda yo na banda se esika moko /UDONGO OOH,PATRICK MANGASA, WEWE NA MPINZANI WAKO NYOTE MTAZIKWA SEHEMU MOJA

Mabélé ooh ooh na cimetière to ko salaka zua tè  / UDONGO OOH , WALA HUKO MAKABURINI HAKUNAGA NA MASWALA YA WIVU

Mabélé ooh ooh yeh soki ba koundi molongani pembeni ya mbanda / UDONGO OOH YEH, YAWEZA IKATOKEA  MPENZI WAKO KAZIKWA KANDOKANDO NA MKEMWENZA WAKO.

Mabélé ooh ooh mabélé to ko niataka ya ngo nde eko koundaka biso pepe hein / UNDONGO OOH, HUO UDONGO TUNAO UKANYAGA BASI NDIO HUO UTAKAO TUPOKEA PEPE HEIN

Mokolo to ko balanaka na ndako ya nzambe liboso ya ko benisa biso sango a lobaka boyé / TULIPO FUNGA NDOA KANISANI,KABLA YA KUBARIKIWA ,PADRE KATAMKA MANENO HAYA

Bo balani pour le meilleur et pour le pire bo sangisi nzoto bokomi moto moko / MNAPO FUNGA NDOA, PANAKUA NA UPATANISHO KATI YENU NA MNAKUA MWILI MMOJA, BASI KUBALINI YATAKAYO JITOKEZA YA KHERI AU YA SHIDA

Kasi mokolo ya liwa nini to ko monoka menuisier a ko sala sanduku se ya moto moko / SASA LINI UKAMUONA FUNDI SEREMALA KATENGENEZA SANDUKU MOJA KWA AJILI YA KUWAZIKA WATU WAWILI!!!

Ba ko kunda moko, moko a ko tikala / YULE ALIEFARIKI ATAZIKWA, NA ALIE BADO HAI HATOINGIA KABURINI

Ata a leli lekola a kufa kasi a ko linga te ba kunda se sanduku moko na molongani nayé / ANAWEZA KULIA KAMA MTU ATAKAE FARIKI LEO, ILA HAWEZI AKAKUBALI KUWEKWA KWENYE SANDUKU MMOJA NA MAREHEMU

Trahison ooh abbé jacque  / USALITI OOH PADRE JACQUES

Wapi libala sango o lobaka / WAPI ILIPO NDOA ULIO ZUNGUMZIA!!!

Trahison ooh yeh bo balani pour le meilleur et pour le pire / USALITI OOH,MLIFUNGA NDOA,MKAKUBALIANA KUKUMBANA NA YALE YATAKAYO JITOKEZA,YAWE MEMA AU MABAYA

Trahison ooh abbé mulumba pour le meilleur pour le pire / USALITI OOH,PADRE MULUMBA, KWA MEMA KAMA VILE KWA MABAYA

Trahison oh tite tchima / USALITI OH TITE TCHIMA ( JINA LA MTU )

Trahison oh sebene / USALITI OH SEBENE

Kasi na ndako ya nzambé ba ko tunaka mi tuna té sima ya losambo messe esili To ko bimaka se na liloba moko biso nioso ameeen /TUWEPO KWENYE SALA KANISANI,HUA HATURUHUSIWI KUULIZA MASWALI,NA PINDI TUNAPO MALIZA SALA,SOTE HUA NA NENO MMOJA MDOMONI : AMINAAA

Guy mayalase oh yeh / GUY MAYOLASE OH YEH

Liwa lekola tango to ko botamaka / MFANO WA KIFO WALINGANA NA ULE WA KUZALIWA

Mimie illumbé eh yeh / MIMIE ILUMBE EH YEH

Moto na mokolo na yé na ngonga na yé / KILA MMOJA NA SIKU YAKE, NA WAKATI WAKE KAMILI

Koko ngoma eeh yeh libala se tango to zali na bomoyi / KOKO NGOMA EEH YEH, NDOA NI NZURI WAKATI WAWILI WAPENDANAO WAKATI BADO WAPO HAI

Vamos eh yeh ba veuve pe bazali na droit ya la vie / VAMOS EH YEH, WANAWAKE WAJANE NAO PIA WANAYO HAKI YA KUISHI

Eloko oyo bolingo eloko mabé E ko komisaka moko nde zoba / PENZI NI KITU MBAYA SANA, HUMFANYA MTU AWE KAMA MJINGA

E ko tika bi teni nioso ya nzoto / HUZIACHA SEHEMU NYINGINE ZOTE ZA MWILI

E ko pona motema e ko niokolo yango / NA KWENDA KUUCHAGUA MOYO KWA MADHUMUNI YA KUUTESA

E ko mema yo ba nzela yo o yebi té / UTAPELEKWA MAENEO USIO YAJUA

E ko mema yo ti na frontière ya mboka oyo o yebi kombo té oh /UTABEBWA NA KUPELEKWA KWENYE MIPAKA YA INCHI USIO IJUA

E ko pepa yo loboko ekati ngambo / NA HAPO NDIPO UTAACHWA SOLEMBA

Moleki nzela ye wana a ké / MPITA NJIA HUYO KAENDA ZAKE

Ko linga pasii eh / NI SHIDA SANA KUPENDA

Na lingaka ba ninga ba trahir nga / NILITOKEA KUPENDA, ILA NIKAJA KUSALITIWA

Bolingo pasi eh / MAPENZI YANAMATATIZO

Na libala ba futi nga na infidelité / MALIPO YA NDOA YANGU NIKUSALITIWA

Mbongo ye ye yeh eh mbongo / PESA JAMANI PESA

Na lingaka mbongo na vie nga / MAISHANI MWANGU NILITOKEA KUZIPENDA PESA

Mbongo ye ye yeh eh mbongo / PESA JAMANI PESA

Na lukaka mbongo na vie nga / KATIKA MAISHA YANGU NILIKUA MTAFUTAJI MZURI WA PESA

Mbongo elakisi ngayi infidélité / PESA YANIFUNZA NJIA YA UZINZI

Lelo na poche na nga lobi ya beverly / LEO HII PESA ZA JAA MFUKONI MWANGU

Lobi na poche ya Tedy Kinsala / KESHO ZITAKUA MFUKONI MWA TEDDY KINSALA

Lobi kuna na poche ya franck mupezo / KESHO KUTWA MFUKONI MWA FRANCK MUPEZO

Lobi kuna na poche ya Guy Mayolase / SIKU ITAKAYO FWATIA MFUKONI MWA GUY MAYOLASE

E ko suka na poche ya Pepe Kalé / ZIKAJA KUISHIA MFUKONI MWA PEPE KALLE

Na mema yé na bar a komi kuna a tikali / NAENDA NAZO KWENYE BAR NA ZIKABAKILIA HUKO

A pesi nga masanga abo kozonga ndako / WANANIPA POMBE NA BAADAE NARUDI NYUMBANI PASIPOKUA NA CHOCHOTE MFUKONI

To kendé na zando to koma kuna a tikali / TUENDAPO PIA SOKONI,HUZIACHIA HUKO

A luli ba commerçant abo kozongo ndako / PESA HAZICHOKI KUWATONGOZA WAFANYABIASHARA

Mbongo ye ye yeh eh mbongo eh mbongo eh infidel / PESA YEH PESA EH!!! PESA NDO MSALITI MKUBWA!!!

Dokotolo a pekisi nga lelo masanga likolo ya maladie oh oh …cousin ya commerçant / DOKTA KANIKATAZA NIACHANE NA POMBE KUTOKANA NA MARADHI

Dokotolo a pekisi nga lelo cigarette ba ndeko oyo mibale na tikala na bango / DOKTA KANIKATAZA PIA NISIVUTE TENA SIGARA, NDIZO TATIZO MBILI NINAYO KABILIANA NAYO

Bayé na liaka na bango to salaka sekelé kaka bango lisusu ba trahir nga /WALE AMBAO TULIKUA TUKICHANGIA CHAKULA KWA PAMOJA,WALE AMBAO NI WATU WANGU WA KARIBU,NI WAO WAKWANZA KUNISALITI

Ba famille na ba ninga oyo na salisaka soki na zangi ba ko ndima ngai té oh / FAMILIA YANGU, PAMOJA NA MARAFIKI AMBAO NILIKUA NIKIWASAIDIA,WANANIDHARAU KWAKUA LEO HII MIMI MASKINI

Bakanisi ko yebana ezali nde mbongo / KWA WAO HUFIKIRIA UNDUGU NI PESA

Koyebana eeeh eh / UNDUGU EEEH

Koyebana ezali ndé ngambo / KUMBE KUFAHAMIKA KUNA TAABU YAKE

Ba ninga basangisi eh / MARAFIKI ZANGU UUNGANA

Basangisi lokumu na nga na mbongo / NA HUSHINDWA KABISA KUTOFAUTISHA HESHIMA YANGU NA PESA

Dokotolo eh Ingila eh / NAMUOMBA DOKTA AJE

Na lingaka masanga e boteli nga maladie / MWANZONI NILIKUA MTUMIAJI MKUBWA WA POMBE, LEO HII YANILETEA MARADHI

Cigarette ndenge moko na lingaka ciagarette e bebisi nga santé / NILIKUA PIA MVUTAJI MZURI WA SIGARA,LEO HII YANILETEA MATATIZO YA AFYA

Na tikala eh ngamoko na mokili / NABAKI MPWEKE,PEKE YANGU ULIMWENGUNI

Lokola moyi e botama na ndeko te / NIPO KAMA JUA LILIVYO,HUZALIWA PASIPOKUA NA NDUGU

Maladie eh yo ko tungisa nga / UGONJWA HUU AMBAO WAENDELEA KUNISUMBUA

Ba ko kundu nga na yo libulu moko / TUTAZIKWA WOTE KWENYE KABURI MOJA

Maladie oko niokolo nga / MAGONJWA HAYA YANAYO NITATIZA

To ko kendé nga na yo sanduku moko maladie / TUTAWEKWA WOTE KWENYE SANDUKU MMOJA, MARADHI !!!

 

LUBONJI WA LUBONJI


DIGITAL WA FM ACADEMIA HATUNAYE TENA

July 19, 2014

POLENI SANA WANA FM ACADEMIA KWA KUONDOKEWA NA DIGITAL

SALAMU ZETU ZA RAMBI RAMBI ZEWAENDEE NDUGU MARAFIKI NA FAMILIA


%d bloggers like this: