Obama!! Obama!! Obama!!….

January 22, 2009

Jennifer Lopez glowed in her white goddess gown while performing at the Western Inaugural Ball at the Washington Convention Center.

Jennifer Lopez glowed in her white goddess gown while performing at the Western Inaugural Ball at the Washington Convention Center.

Ili mradi kila chombo cha habari kwa wiki nzima hii hakikosi habari walao moja yenye kutaja jina la Obama, Bonyeza hapa upate uchambuzi wa ma Celebrity na vivazi vyao siku ya Kuapishwa Obama, watu wamechambua mpaka Festi ledi kudadaadeki!!


Obama akasirishwa na kikaragosi kumhusisha na Ughaidi

July 16, 2008
Kikaragosi

Jalada la juu la jarida la New Yorker

Kikaragosi kilichotumika kwenye jalada la jarida la New Yorker, kimewakasirisha sio tu Obama na Mkewe bali pia jumuiya za kidini nchini humo. Katika kikaragosi hicho ambacho kinaonekana hapo juu amechorwa Obama katika nguo za kiasili zenye maudhui ya kidini zaidi na mkewe akiwa amevaa bunduki mgongoni huku picha ya Osama Bin Laden ikiwa imetundikwa ukutani na kwa mbali inaonekana bendera ya Marekani ikiwa kwenye tanuri la kuotea moto ikiteketea, Picha hii imetafsiriwa kwa aina mbali mbali na wadau wa habari huku wengi wakisema imedhalilisha dini moja na wengine wakilaumu kitendo cha jarida hilo kumhusisha Obama na ughaidi.

Wakitolea maelezo kuhusu kikaragosi hicho Mhariri wa Jarida la New Yorker alisema nia yao wao ilikuwa ni kusafisha Mind za watu juu ya Uislamu na ughaidi, Je imekaa njema hii?


%d bloggers like this: