Kila Mmoja; When Genge meet Bongo Flava

June 30, 2011

 

Nonini ni mmoja wa wanamuziki wa Kenya wanaonibamba sana, Sikiliza hii Kolabo ya Nonini akimshirikisha Lady Bee na Chege Chigunda. Wimbo unaitwa Kila mmoja. Nadani kila mmoja atakubaliana na mimi mchanganyiko wa hawa jamaa ni moto wa kuotea mbali. haya kamata kitu hiyo!!

Kwa mashabiki wa Muziki wa Genge au wa Nonini kwa ujumla, jamaa ame launch iPhone Application yake kwa ajili ya funs wake ambao wana iPhone, Binafsi ninayo inanipa nyimbo zote za Nonini, Video zake, Habari za show zake na any update, haya ni mapinduzi makubwa kuwafikia mashabiki na liwe fundisho kwa Mabongo Flava hapa muangalie ni jinsi gani ya kuwafikia mashabiki wenu soko ni hilihili lakunyang’anyana changamke mazee. Hii ina Majotroooooo!!!!

image

Picha ya App ya Nonini kwenye iPhone


Mrs Col. Maganga alipokamata Nondo yake

June 30, 2011

Mama akitayarishwa tayari kwenda kwenye Graduation iliyofanyika Verizion Center,Washington,DC Jumamosi June 25,2011

Mama Maganga akiwa na wahitimu wenzake

Mama Maganga akitabasamu, Spoti Starehe inakupongeza Mama kwa hatua uliyofikia. Kila la heri Mama.

Mama akipongezwa na Baba,Mwambata wa Jeshi Ubalozi wetu Washington,DC,Colonel Maganga

Familia ndugu na marafiki waliofika Verizion Center kumongeza

Mama Balozi Mwanaidi Maajar akimpongeza Mama Maganga nyumbani kwao Baadae jioni kwenye ghafla ndogo aliyoandaliwa Mama Maganga maaulumu kwa kukamata Nondo ya Master Of Public Administration

Wageni mbali mbali ndani na nje ya Washington,DC,walifika kumpongeza Mama Maganga,pichani anayesalimiana na Mama Maganga ni Mh Balozi wa Maziwa makuu,Liberata Mulamula,kushoto ni Colonel Maganga,mwambata wa jeshi Ubalozi wetu,Washington,DC na wapili kutoka shoto ni Mh.Balozi wetu Marekani na Mexico,Mwanaidi Maajar

.

 

Gonga hapa kwa Picha zaidi


Profesa Jay; Nimeanza Gym kukata “Kitambi”

June 30, 2011

257014_10150299347541495_762011494_9205085_5686846_o

256636_10150300189356495_762011494_9215086_3734220_o Mwanamuziki Joseph Haule aka Heavy Weight Mc, Prof Jay amekata shauri na kuamua kuingia Gym kwa ajili ya kupunguza uzito.

Jay aliyasema hayo kupitia ukurasa wake wafacebook mapema leo, “Najua mwanzo mgumu ila naahidi kupigana mpaka nifikie malengo yangu” ilisema moja ya mistari ya status ya profesa.

Wazo hilo limeonyesha kuwakuna mashabiki wake wengi ambao wamempa moyo na hata mwanamuziki mwezie AY alimpa moyo akomaye kukata utuntufye. Naona Prof kaamua na anasema anahamu sana ya mazoezi “Yaani naiwaza GYM muda wote ni kama mtoto akinunuliwa Viatu vya sikukuu kila saa anavijaribisha, hata akilala anaviweka UVUNGUNI akilala kidogo Anavichungulia kama vipo!! hahah Kidumu cha cha wafanya Mazoezi..” aliendelea kusema.

life style inafanya watu wengi kuongezeka uzito na hii kwa maisha ya mjini inachangiwa na vitu vingi ikiwemo kutumia magari binafsi, Taxi, Usafiri wa Umma na hata tabia ya kula kula (junk food) ikiwamo Chipsi, Burger na unywaji wa Bia vinachangia kwa kiasi kikubwa unenepaji usiokuwa na mpango.

Inawezekana kitendo cha profesa kuweka wazi hili kukahamasisha na watu wengine nikiwamo mimi kuanza mazoezi ili kuepukana na hali hii. Hongera profesa mwanzo mgumu komaa utashinda.


Kimwana wa Twanga Fainali tarehe 8 July Ubungo Plaza

June 26, 2011

image

Hawa ni Baadhi ya washiriki walioingia 10 Bora ya Kimwana wa Twanga Pepeta 2011. Toka shoto  ni Johari Juma, Amanda Cyprian, Rehema Said, Mariam Mwakyoma na Amina Juma.

Fainali za Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 zinatazamiwa kufanyika July 8 2011 katika ukumbi wa Ubungo Plaza.


Bongo Vipaji kibao basi tuu!!.

June 26, 2011

Tuliwahi kuandika kuhusu dada huyu kuna mdau aliwahi kumuulizia kumuunganisha na kampuni ya Matangazo, walipewa mawasiliano ingawa sijui walifikia wapi.

Hiki ni kipaji tosha.


FFU wa Ngoma Africa band jukwaan Jumapili 26.06.2011 Freudenstadt City, nchini Ujerumani

June 26, 2011

DSC_0312

Bendi ya maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya “Ngoma Africa band” aka FFU yenye makao

yake nchini ujerumani,inatarajiwa kupanda jukwaani siku ya jumamosi 26.06.2011 katika onyesho kambambe mjini

Heidelberg,ujerumani.Pia siku ya jumapili 26.06.2011 Kikosi kazi hiko cha FFU wa Ngoma Africa band,kitaelekeza

mashambulizi yake ya mziki katika oynesho lingine “Afrika Tage” mjini Freudenstadt,kusini mwa Ujerumani ambako

mshike mshike wa pata shika ya nguo kuchanika ya washabiki na gwaride la mziki “bongo dansi” utakuwapo,

Pia karandinga la FFU wa ngoma africa limeegesha hapa unaweza kuchungulia virungu na vya machozi ya mziki at:
http://ngoma-africa.com/index.php?option=com_content&view=article&id=58&Itemid=58
Jipendelee kwa kujipa raha mwenyewe kwa kukongoli au bofya at

www.ngoma-africa.com


Femme de Didier Drogba.

June 26, 2011

 

Kwa waliotaka kumuona Mke wa Didie Drogba huyo hapo!!


%d bloggers like this: