Ray C aja na Touch Me!! Imesimama…!!

March 2, 2009

Katika wanamuziki wa Kike wa Zamani waliobaki kwenye GAme basi Ray C ni mmoja wapo na kwa kweli kwa siku za karibuni naona chat yake kimuziki inazidi kupanda juu kama alivyokuwa hapo awali ambapo alikuwa akijulikana kama Kiuno Bila Mfupa.

Inasemekana wimbo huu Ray C aliutunga kwa ajili ya Mpenzi wake mpya mwanamuziki mwenzie toka Arusha ambaye alitangazwa kuwa wanataka kufunga ndoa (sijapata habari kama ilifungwa) ambapo mipango ya awali ilikuwa ni Dec mwaka jana au Mwanzoni mwa mwaka huu.

Ray C ambaye hapo kati alikumbwa na kashfa kibao ikiwamo za mahusiano na maisha yake binafsi amekuja na Wimbo mpya unaoitwa Touch Me wimbo ambao kwa kiasi kikubwa naweza kusema Video yake ni tofauti na zile tulizozoea, MEngi zaidi kuhusu Wimbo huu yanakuja, Hongera mama na mdau wangu pata burudani.


Muungano wa Africa Mashariki na Magharibi Kimuziki

February 28, 2009

NI RAY C NA RF CHORD

Original ya wimbo huu uliimbwa na Ray C Peke yake ikiwa ni Remix ya wimbo wa Sikuhitaji wenye mahadhi ya Taarabu enzi hizo alipopachikwa jina la Kiuno bila mfupa, Wanamuziki wa Bongo Flava wameamua kwenda kimataifa kwani Ray C aliamua kuukarabati huu wimbo na kuuimba tena akishirikiana na mwanamuziki RF Chord toka Siera Leone ambaye makazi yao ni MAshariki ya MBali, Wimbo huu kwa RF Chord unaitwa YAWO, RF Chord ni wanachama wa UMPA [Union Movement of Performing Artists of Sierra Leone] ,

Wakiwa ni moja ya vikundi vya muziki vyenye chart ya juu kabisa nchini mwake Siera Leone.
RF Chord ambaye anatumia zaidi mtindo wa “Dance Hall” huku akichanganya na midundo ya asili kwa nyimbo zake nyingi amejipatia umaarufu sana na Wimbo huu aliopiga na Ray C.

Hii inasaidia kuufanya muziki wa Kizazi kipya kutambulika zaidi ingawaje kwenye wimbo huu Ray C aliuimba kwenye mahadhi ya Kipwani zaidi, ukiwa ni Remix ya wimbo wake wa Sikuhitaji ambayo ilipigwa kitambo kidogo,

Hivi karibuni tumesikia Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi Uingereza Blanchard Deplaizir akifanya kolabo na baadhi ya wanamuziki wa TAnzania akiwemo Lady Jay Dee, BAnana na wengineo, Pia Kolabo ya AY na P Square.

Shime kumekucha muziki huu umekubalika nchini ni wakati wa kuuza kimataifa na kwa jinsi hii mtatoka tuu.
Pata burudani kwa kubofya Player…


Ray C aja na “Nihurumie wangu”

July 26, 2008
Rehema Chalamila AKA Ray C

Rehema Chalamila AKA Ray C

Baada ya kimya kirefu toto la kihehe mahiri ktk miondoko ya muziki wa kizazi kipya Rehema Chalamila (Ray C) ameachia track mpya iitwayo ‘Nihurumie Wangu’.

Ray C anasema aliamua kukaa nje ya ‘gemu’ kwa muda akiwa anausoma muziki na soko linavyokwenda,huku akiwapa nafasi wasanii chipukizi kuonyesha uwezo wao. ”Sio siku zote unapenda kuonekana wewe tu, ni vizuri kupisha wengine kuonyesha uwezo wao,nimekuja tena upya ndani ya ‘gemu’ sasa ni moto mkubwa unawaka na hakuna kurudi nyuma tena,mambo ni mbele kwa mbele,”amesema Ray C.

Msanii huyo amesema ujio wake huo,ni moja ya maandalizi ya kuachia albamu yake mpya itakayotoka hivi karibuni ikiwa imesheheni nyimbo kibao zilizosimama sambamba na kkuwashirikisha wasanii maarufu wa ndani na nje ya nje ya Bongo.

Aidha, amesema amejifunza mengi kuhusu muziki, baada ya kufanikiwa kufanya maonyesho kadhaa nchi za Uingereza,Marekani,Sweden,na kuweza kumpa mwanga zaidi kimuziki.

Na Dar Hot Wire


%d bloggers like this: