Blatter na Penati

May 26, 2012

Kwa wale watu wa soka au KANDANDA Rais wa FIFA Sepp Blatter anasema hataki mechi iamuliwe kwa mikwaju ya penati (MATUTA) baada ya dk 120…unaonaje? yupo sahihi au amekengeuka kidogo….


Account ya Mh. Kikwete yathibitishwa rasmi Twitter

May 26, 2012

verification note

Twitter hatimaye wamemthibitisha Rais Kikwete na kumtambua rasmi kama mtumiaji wa mtandao huu. Alama ya Tick nyeupe yenye duara la kijani ni alama maalumu ambayo Twittwer wanaitumia kuwa mwenye account ambaye ni mtu maarufu amekuwa verified na ndiye mhusika halisi.

Twitter huwa wana wathibitisha watu maarufu baada ya kujiridhisha kuwa ni wao kweli wamiliki wa account tajwa kwani kumekuwa na watu wanafungua account kwenye mitandao jamii kwa jina la tu maarufu kwa madhumuni yao binafsi.

Mheshimiwa Rais Kikwete amekuwa mtumiaji mzuri wa mitandao jamii na anamarafiki wengi. Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa alikuwa Kiongozi wa Kwanza kutumia mitandao jamii kwenye kampeni zake ambapo alifungua account maalum ya Twitter, Facebook na Blog ambapo alikuwa akiwasiliana moja kwa moja na mashabiki wake wa ndani na nje ya nchi.

Niliwahi kuandika kuhusu mchango wa Teknohama/Mitandao ya Kijamii kwenye uchaguzi mkuu uliopita 2010 ambapo viongozi mbali mbali walitumia mitandao hii kwenye uchaguzi huo, KAtika uchambuzi wangu pia niligusia jinsi ambavyo mitandao hii inaweza kuwa chachu ya ushindi. Ukitaka kujua zaidi soma hapa Mchango wa Teknohama/Mitandao Jamii kwenye Uchaguzi Mkuu 2010


Yanga inawenyewe bwana…!!!

May 25, 2012

Sisi ndo wenye Yanga bwana alaaaaaah…daaah huyu mzee ukimkata hapo damu inatoka ya njano… Hii ilikuwa wakati wa mkutano ulioshinikiza uongozi wa Yanga kuachia ngazi. Inawezekana Timiza wajibu wako!!


Usiku wa Mayenu

May 24, 2012

https://spotistarehe.files.wordpress.com/2012/05/thtshow.jpg?w=300


Koffi na KORA

May 23, 2012

Tuzo za KORA ni moja kati ya tuzo zilizokuwa kubwa sana kwa Afrika, na ndio zinazowapa hata muhimili Ma Werasonike humu ndani kila mara linapokuja suala na ubishi kati ya JB Mpiana na Werasson kwani Werasson aliwahi kupanda na kuchukua Tuzo kadhaa za Kora. Binaafsi sijui kama bado tuzo hii iliyokuwa na heshima yake bado ipo maana nina muda sijaisikia.

Basi naomba tujikumbushe jinsi Koffi na kundi lake la Quartier Latin walivyofunika kwenye moja ya tuzo hizi huko Afrika ya Kusini.


Unamkumbuka mamaa Mokonzi Scola Miel wa Bozi Boziana wewe?

May 23, 2012

Unamkumbuka mamaa  Mokonzi Scola Miel wa Bozi Boziana wewe???msome hapa basi umkumbuke zaidi pamoja mzee mzima Bozi Boziana live on stage na kitu BEYONIE, enzi hizo style ya nzawisa iko juu sana, ulikuwa wapi,mimi nilikua form 2 nakumbuka vizuri sana,wewe je??Mzee Bozi alikua na wacheza show ambao walikua pia waimbaji bora kabisa, huyu Scola na mwenzie Betty.


Sababu za kuchelewa Anti Tero Sehemu ya II

May 22, 2012

 

Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kabla ya kwenda South AFRICA bcbg walipitia Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya show iliyoandaliwa na PRIME TIME PROMOTION chini ya Jose Kusaga

 

Wimbo Vicky Nsongi wa PPU ulioleta kizaazaa huu hapa.

Baada ya mabadiliko hayo bcbg kukawa na kambi mbili,kambi ya kwanza ikawa ya Seguin, Pathy Moleso, Jules Kibens, JDL na Boguis Bompema na upande wa pili kukawa na kambi ya Tutu Kaludji, Burkina Faso, Ficare Mwamba, Accompa Alba, ambapo kundi la kina Tutu Kaludji ambalo pia Alain Mpela alikua miongoni mwao likitaka PPU(Gino, Nono Fuji, Abraham Mignon na wengine) wapewe nafasi ya angalau kuweka wimbo mmoja katika album ya ANTI TERRO ambapo vijana wa PPU wakakubaliana miongoni mwa nyimbo zao nyingi wautumie wimbo VICKY NSONGI, wakaanza kuufanyia maandalizi wimbo huo wakiwa Kinshasa chini ya mpiga solo Burkinafaso Mbokalia ambae wakati huo alikua anakisaka cheo cha artistic director wa bcbg kwa hali na mali, katika kazi hiyo ya kuwaongoza vijana wa PPU kuiandaa VICKY NSONGI ili iwemo kwenye ANTI-TERRO, Mbokali alishirikiana na Accompa Alba (mpiga solo na rhythm guitar) kabla kundi zima la BCBG wakiwamo wao halijasafiri kwenda South Africa kwa ajili ya kuzifanyia mixing na kurekodi baadhi ya nyimbo kukamilisha album.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kabla ya kwenda South AFRICA bcbg walipitia Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya show iliyoandaliwa na PRIME TIME PROMOTION chini y Jose Kusaga ambapo walifanya show hiyo katika ukumbi wa Diamond Jubilee na ilikua siku ya sikukuu ya Idd ambapo baada ya show hiyo kesho yake kukaandaliwa event ya kuosha magari kuchangia yatima pale victoria petrol station ambapo Jb Mpiana, Tutu Caludji pamoja na wadada wacheza show wa bcbg wakiongozwa na Monica Seles walihudhuria,na katika kuchangia kwenye event hiyo Jb aliosha gari ya Kusaga kwa gharama ya shilingi za Tanzania milioni moja toka kwa kusaga mwenyewe.

https://spotistarehe.files.wordpress.com/2009/12/bbbbb.jpg

JB Mpiana akiwajibika kwenye Show ya Ubungo Plaza Dar Es Salaam

…………………………………………………………………………………………………………………….

Baada ya shughuli hiyo ya kuchangia yatima iliyoandaliwa na CLOUDS FM na PRIME TIME,BCBG wakiongozwa na JB wakaondoka zao kuelekea South Africa kwa ajili ya kazi niliyoitaja hapo juu,lakini walipofika huko tofauti na makubaliano ya awali kwamba PPU wapewe nafasi ya kuweka wimbo mmoja kwenye ANTI – TERRO,Jules Kibens na Boguis Bompema wakataka kufuta vocals za PPU na badala yake kuweka zao kwenye wimbo VICKY NSONGI lakini wakongwe Ficarre Mwamba na Burkina Faso wakapinga vikali hilo jambo ambapo inaelezwa Ficarre aliwafokea vikali kina Kibens kwa kutaka kufanya hujuma hiyo dhidi ya vijana wa PPU ambao wote walibaki Kinshasa lakini kwa mshangao mkubwa JB hakusema lolote dhidi ya hujuma ya kina Kibens licha ya kuwa Ficarre ni mtu wa siku nyingi na anaeheshimika kwenye bendi ukilinganisha na kina Kibens.

Lakini Seguin Mignon alipowasili eneo la tukio na kukuta sintofahamu hiyo yeye moja kwa moja alichukua side ya kina Kibens na kuwatetea kwa walichokua wakitaka kuwafanyia vijana wa PPU ambapo Burkina Faso kuona hivyo akasimama na kumwambia “nyamaza wewe usiejua kupiga drum” , kufuatia kauli hiyo toka siku hiyo Seguin akaapa lazima ahakikishe anamuondoa Burkina Faso na kundi lake haraka iwezekanavyo, akaanza kumpelekea maneno ya uchochezi JB dhidi ya kina Burkina Faso, Accompa Alba na Tutu Caludji, baadae JB maneno yakamuingia akaanza kumu ignore Burkina Faso kwanza na baadae Accompa na Tutu Kaludji mpaka jamaa wakaamua kujiondoa wenyewe kundini walipomaliza tu kurekodi ANTI TERRO kwa mbinde huku kukiwa na uhasama mkubwa kundini wakati wa kurekodi,waliamua kuiondoa baada ya kuona hawana thamani tena kwa Jb(ikumbukwe Jb akiwa hakutaki anayo tabia kukudharau nje ya jukwaa tu bila kuonyesha dharau jukwaani-mbele ya washabiki).

Lakini wakiwa hapo South Africa VICKY NSONGI hatimae ilirekodiwa ambapo wakongwe “mikuli” kina Kibens,Jdl na wengine ambao Jb alikua akiwasikiliza sana kutokana na wao kuwa nae karibu wakati akiwa na wakati mgumu kufuatia suala lake la kukimbiwa na mkewe Amida Shatur na pia issue ya visa ya kwenda ulaya wakaweka vocals zao na waimbaji kutoka kambi zote mbili hasimu kundini wakalazimishwa kuimba pamoja ili kurudisha amani kundini.Kiufupi Seguin Mignon akawa ni mtu mwenye sauti sana ndani ya BCBG,ndio maana hata vijana kina Gino, Nono Fuji, Abraham,Sakoko n.k. hawaishi kumtaja taja wanapoimba ili kujiweka karibu nae,hakuna anaetaka kugombana nae kwa kuhofia usalama wake kundini kama ilivyokuwa kwa kina Tutu Caluggi na Burkina Faso.

Hicho ndicho kilichotokea lakini hatimae album ya ANTI TERRO ikatoka baada ya vuta ni kuvute ya muda mrefu na ikawa mara ya kwanza Jb kurekodi/kufanyia mixing album South Africa tofauti na Europe(Paris) walikokuzoea.


CHAI NGENGE Wenge BCBG Featuring EBOA LOTIN wa Wenge Maison Merre

May 22, 2012

Natamani JB MPIANA na WERRASON wawaruhusu vijana wao hawa Chai Ngenge na Eboa Lotin waurekodi huu wimbo wao mkali, sijui kama itawezekana but naamini hakuna litakaloshindikana kama busara zikiwekwa mbele, kiukweli wimbo mimi nimeupenda licha ya kuwa wameimba hapa studio na magitaa mawili kama wakiurekodi utatoka bomba, ni wimbo flani wa kunung’unika hivi, wasikilize hapa wakihojiwa na mtangazaji Tonny Nkoko.

Chai Ngenge ni mwanamuziki wa wenge bcbg ya De La Patria Jb Mpiana wakati Eboa ni mwanamuziki wa Wenge Maison Mere ya De La Forret Werrason.

Vitu Exclusive kama hivi utavipata Spoti na Starehe Blog pekee.


Fally alipowapagawisha Drogba, Yaya Toure, Kolo Toure & Adebayor na wengineo

May 22, 2012

Fally licha ya kupiga show kwa style ya play back wiki iliyopita katika jiji la Manchester Uingereza alizikonga vilivyo nyoyo za wapenzi wakiwamo ma super star wa premier league ya uingereza wanaotoka africa wakiongozwa na Didier Drogba, Emanuel Adebayor, Kolo Toure, Yaya Toure, Alex Song na mastar wengine wa soka akiwemo mcongoman Nonda Shaban,tizama video hasa kuanzia dakika 07:06 mpaka dakika 10:10 na kuendelea uone Yaya,Kolo na Drogba walivyolivamia na kulishambulia jukwaa…


Je wajua ni nini Kilichelewesha Albamu ya Anti Tero ya JB Mpiana Sokoni?

May 21, 2012

Na Hadj Le Jbnique, Boston, Massachusetts, Usa.

Wimbo Anti Terro

Mwaka jana tulichapisha makala za kuhusu kuparanganyika kwa kundi zima la Wenge BCBG na hatimaye kujitenga kwa Werasson na wengineo, Baada ya kuangalia kuanzishwa kwa kundi la Maison Merre la Werrason na matatizo yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapayaniliahidi kuwaletea ni kwa sababu gani Albamu ya Anti Terro ya Wenge BCBG alichelewa sokoni… Endelea sasa.

Kulikua na mambo mengi ya nje ya bendi na ya ndani ya bendi yaliyochangia album ANTI-TERRO ya BCBG kuchukua muda mrefu kutoka sokoni.Miongoni mwa mambo ya nje ya bendi lilikua ni suala la ugumu wa kupata visa za kuingia ufaransa na  ubelgiji kwa wanamuziki toka Congo, na kama inavyofahamika wanamuziki wa Congo walikua wakizitegemea studio zilizoko kwenye nchi hizo kwa ajili ya kazi ya kurekodi nyimbo zao.

Na tukija kwenye mambo ya ndani ya bendi,awali Jb alipanga album hiyo iwe na nyimbo nyingi za Alain Mpela ambae alikua ni kiongozi wa bendi (Chef De Orchestre) pamoja na nyimbo bendi ya vijana wadogo ya BCBG inayofahamika kama PPU (Presidential Protection Unit) ambayo Alain mpela aliipromote sana na mbili tatu za Jb Mpiana mwenyewe huku member wengine wakitakiwa kuweka tu vocals zao kwenye nyimbo za album hiyo bila wao kuwa na nyimbo hata moja,Alain Mpela alipewa chance ya kuweka nyimbo zake sita (6).

Lakini wakiwa kwenye maandalizi ya album hiyo huku wakisikilizia suala la visa na kuumizwa kichwa ni wapi watakwenda kuirekodi ama kuifanyia mixing album hiyo kama visa itaendelea kusumbua kukatokea sintofahamu kati ya Jb na Alain Mpela, rafiki yake mtiifu ambae alimchukulia kama mdogo wake (ikumbukwe Alain Mpela na mdogo wake Bouro Mpela kuna wakati walikua wanaishi nyumbani kwa Jb kama Herritier watanabe alivyowahi kuishi nyumbani kwa Werrason baada ya Jb kumwambia akasome kwanza shule apate degree ndio arudi BCBG).

Kilichosababisha sintofahamu hiyo ya Jb na Afande Mpela ni simu ambayo ilipigwa na Koffi kwa lengo la kumshawishi Alain Mpela ajiunge na Quartier Latin yake na badala yake simu hiyo ikapokelewa na Jb huku koffi akidhani ni Alain mwenyewe ndie aliepokea simu hiyo hivyo kuendeleza mazungumzo yao yalipokuwa yameishia.

Baada ya simu hiyo Jb alikasirika sana na kumuona Alain Mpela kama bonge la msaliti kwa kuwa licha ya ukaribu wao na yeye kumchukulia kama mdogo wake aki share nae mambo mengi hakuwahi kumtonya chochote juu ya mazungumzo yake na Koffi ambae alikua adui mkubwa wa Jb wakati huo, na Jb ana kitu kimoja mpaka leo, hakuna kitu asichokipenda kama usaliti. Hivyo basi kuanzia siku hiyo Jb na Mpela hawakua brothers tena, na ule mpango wa kumpa nafasi Mpela aweke nyimbo zake 6 kwenye ANTI-TERRO Jb akaufutilia mbali na badala yake akamuachia nafasi ya kuweka nyimbo zisizozidi tatu huku kukiwa na mipango ya kumvua u chef d’orchestre.

Kuona hivyo Alain Mpela akasusia kushiriki shows na mazoezi ya BCBG kwa wiki mbili na hatimae akatangaza kujiondoa kundini huku akitoka na single maalum kwa ajili ya kumuimbia na kumsifia adui namba moja wa Jb bilionea Didi Kinuani. Mpaka hapo Jb na kundi wakawa na kazi ya kuziaondoa nyimbo za Mpela ambazo walikua tayari wameshazifanyia sana mazoezi na walikua wakizipiga kwenye shows zao za kila weekend ndani ya Kinshasa na kuanza upya kuandaa nyimbo nyingine na kujipanga upya huku wakiwa hawana mfadhili wala mdhamini kama ilivyo sasa kwa makampuni ya bia ya Congo kutoa sponsorship,wakati huo walikua wakiwategemea matajiri wakubwa wapenzi wa muziki kama huyo Didi Kinuani ambae Jb alikua tayari ameshagombana nae baada ya Dikin kumuiba mke wa Jb mamaa Amida Shatur na kumfanya mkewe.

Alain Mpela “afande” alipoondoka kundini BCBG nafasi yake kama Chef D’Orchestre kwenye bendi ilizibwa na Tutu Caludji ambae awali alikua mkuu wa mambo ya nidhamu kundini ambapo nafasi hiyo na yeye alimuachia mpiga drums Seguin Mignon ambae De La Patria JB amekua akimpenda na kumsikiliza sana akimchukulia kama mdogo wake pia,vilevile Seguin ni mtu wa karibu sana na De La Forret WERRASON na ndio amekua kiungo kati ya JB na WERRA. Hali hiyo ya kuwa na ukaribu na JB ikamfanya Seguin awe na sauti kubwa kiasi cha kwamba ukigombana nae au kama hakutaki lazima uondoke BCBG.

Je unataka kujua nini kiliendelea? Soma hapa kesho…..

[cryptex]piusmicky@yahoo.co.uk [/cryptex]


MTUNZI WA REMISE ET RAPRISE

May 21, 2012
Original ya Mukulu wa Bakulu

Na Hadji

KUMBE MTUNZI HALISI WA WIMBO REMISE ET RAPRISE “TRESSOR MPUTU” WA MAISON MERE SIO WATA NI HUYU HAPA!!

Kumbe Mukulu wa Bakulu ndio mtunzi asilia wa wimbo mpya unaotesa wa Heritier Watanabe na maison mere???!

Msikilize Mukulu hapa then uwasikilize Werra na Wata kwenye copy ya wimbo huo huo mmoja then utoe maoni yako.Wimbo huu ambao Werrason na Heritier wameubadilisha jina na kuuita Remise et Raprise a.k.a. Tressor Mputu Mukulu wa Bakulu ambae ni shabiki mkubwa wa Jb mpiana aliuimba kwa mara ya kwanza kwenye tamasha la Fikin 2010

Copy ya wana

Nani kama Koffi?

May 21, 2012

Hadj Le Jbnique

Enter video caption here
Mwaka 2009 Koffi alifanya show ya ukweli yenye mafanikio makubwa sana upande wa mahudhurio ndani ya Paris katika ukumbi mkubwa na maarufu wa “Zenith”.

Haikua kazi rahisi kupata mafanikio bali kazi kubwa ilifanyika ya kuitangaza show hiyo kwa maana ya kwamba waandaji wa show hiyo hiyo waliijua kazi yao na kutimiza wajibu wao wa kufanyia promo ya kutosho hiyo show ambayo matunda yake yalikuja kuonekana ukumbini, siku zote biashara ni matangazo, kabla ya kuangalia video ya ‘balaa” alilolifanya Koffi ukumbini na kukonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria siku hiyo, hebe tuone video hii inayoonyesha moja ya promo zilizokuwa zikirushwa hewani Tv stations za ufaransa, ubelgiji na nchi nyingine jirani na ufaransa ili kuwahamasisha watu wafike kwa wingi kwenye show hiyo kutoka nchi mbalimbali za ulaya zilizo jirani na ufaransa.

Hapa utamuona Koffi mwenyewe akiimba na gita lake, pia “mkewe” Cindy akiinadi show hiyo ya kufa mtu….

Siku ya siku ikafika,matunda ya kuwekeza kwenye pesa ya kutosha kwenye promo ndiyo haya yanaonekana hapa hatimaye, hili ni fundisho kwa promoters wengine kuacha ubahiri wanapoamua kuandaa show ya mwanamuziki yeyote yule hata vijana wetu wakitanzia, mfano mzuri ni hii show ya diamond mlimani mwisho wa mwezi,sijui kina nani wameandaa ile show but wanaonekana wamejipanga vizuri…big up kwao,matokeo mtayaona siku ya show hiyo na mtakubaliana na mimi show ni matangazo kama biashara nyingine….Pata show murua ya bana Quartier Latin, mamaa Cindy Le Coeur


May 21, 2012


seguin mignon wa Wenge BCBG

May 21, 2012

Alain Prince Makaba 188 Memoir et Mignon Garcon Seguin

Seguin Mignon(kulia) mpiga drums wa bcbg wa sasa enzi hizo akiwa na Alain Prince Makaba”internet”, Ukisikiliza Omba Remix ile Live kuna mahala JB Mpiana alilalamika sana na kuanza kuwaita wanamuziki wake akiwataja sana Afande, Caludji na kisha kuwataja wengine alianza na Seguen kwa wanaosikiliza vizuri Seguen aliliza sana Drumz JB alipomuita huyu ndiye aliyechukua mikoba ya Titina Alcapolne na kwa kweli kazi yake inasikika.

Msikilize JB hapo chini


Flaviana aweka shada makaburi ya wahanga wa MV Bukoba

May 21, 2012

https://fbcdn-sphotos-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/536339_271136349651437_100002652237808_539133_692911028_n.jpg

Flaviana Matata akiweka shada kwenye kaburi isiyo na jina Igoma jijini Mwanza kama sehemu ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya MV Bukoba. Flaviana alimpoteza mama yake mzazi.

Pamoja na mambo mengine Flaviana Matata alikabidhi msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba – ambapo ni miaka 16 tokea meli hiyo ilizama na kuua watu takriban 1,000 akiwa pamoja na mama yake Flaviana

Picha kwa hisani ya Maria Sarungi.


Kutana na Blogger mtoto aliyeshinda tuzo kibao ni muandishi wa Vitabu pia Mtunsi wa Mashairi.

May 18, 2012

image

niliwahi kuandika kuhusu huyu mtoto Gloson, Blogger mdogo toka Malaysia ambaye kwa kiasi kikubwa amejizolea umaarufu duniani kote kwani pamoja na umri mdogo ameshatunga vitabu viwili vya mashairi akiwa amenyakua zawadi kadhaa kwenye category yake upande ya poetry.

hivi karibuni mtoto huyu alijishindia zawadi kemkem baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano la ku Blog kuhusu  Territory ya Malaysia (Blog4FT (Federal Territories) contest!).

Yeye aliandika kuhusu likizo yake kwenye jiji la Kuala Lumpur ikiwa ni hadithi kwa njia ya Picha zaidi(Gonga hapa).

Mimi binafsi navutiwa sana na huyu mtoto Mara ya kwanza nilipomuona kwa macho yangu ilikuwa wakati wa maadhimisho ya kampeni ya kitalii ya Visit Malaysia katika jengo la KLCC nchini Malaysia, na kipindi hicho alikuwa na miaka 10 tu. nilivutiwa sana naye kwani aliandika poetry nzuri sana kuhusu theme hiyo. Tangu hapo nikawa mfuasi wa Blog yake.

Dogo ana mengi sana ya kujifunza kutoka kwake kama Blogger kwani mwenyewe anasema anatumia muda mwingi sana kufanya tafiti mbali mbali na anapenda sana ku Blog na pia likuwa na kiu ya kujifunza English kiu ambayo imemfanya awe mtaalamu wa Lugha na kuzawadiwa zawadi kadhaa kutokana na vitabu vyake alivyoweza kutunga mpaka sasa.

Gloson ameandikwa kwenye vyombo vingi sana vya habari ndani na nje ya Malaysia, Hii yote ni kutambua mchango wake na kipaji chake.

Huu ulikuwa utambulisho wangu miaka miwili iliyopita niliandika kuhusu mtoto huyo kipindi hicho akiwa na miaka 10 tu.

Gloson, 10 Years Old

Gloson, 10 Years Old

Jina Gloson kwa Malaysia limekuwa si geni kwenye vyombo vya habari hasa baada ya kuandikwa sana kw mwaka jana namaanisha nusu ya mwisho ya mwaka jana.

Gloson ni mtoto wa miak 10 lakini ni Blogger anayekuja kwa kasi akiwa na miezi si zaidi ya saba kwenye ulimwengu huu wa magazeti tando, Kipaji chake si tu kwa kublog bali ni uwezo mkubwa alionao wa kujieleza, mara ya kwanza nilisoma kwenye gazeti la The Star haikuniingia hadi nilipoona akihojiwa kwenye Chanel kubwa ya Tv3 na kumuona kwa macho yangu.

Dogo anakipaji kweli kweli na ye anasema ana blog kila kitu anachoona kina manufaa kwa jamii na katika blog yake pia amefundisha jinsi ya kuandika Post yenye mvuto na jinsi ya kuchangia topic bila kwenda nje ya mada, akiwa ni wanafunzi wa shule ya msingi Gloson anasema alipata wazo la Ku blog toka kwa mama yake ambaye alimshauri ablog naye akaanza.

Mbali na kipaji hicho pia Gloson anakipaji cha kuandika mashairi akiwa meshaandika zaidi ya mashairi 100 ambayo yamechapishwa http://www.poetrytalents.com

Ikiwa na miezi 6 tu tangu ianzishwe blog ya Gloson ambayo inakwenda kwa anuani ya http://www.glosonblog.com/

Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu

“Nafurahi ninapo share nilichojifunza na wenzangu”

“naamini nina mchango kwa jamii mengi waweza kujifunza toka kwangu na kuelimika, kuna mengi yakujifunza kwenye mtandao, napenda Internet naweza kufanya kila kitu kuanzia Homework, games, kununua vitu na kuwasiliana na vitu, alisema Gloson alipohojiwa kwenye Tv3. “kuna vitu siwezi kuwaeleza wazazi wangu moja kwa moja lakini huwa natuma email na naenda kulala nikiamka baba atanijibu ama kwa email au hata akikaa kimya najua anatafakari na amepata ujumbe wangu” aliongeza mtoto huyu anayejua kujieleza kwa lugha ya ufasaha na kufanya wtangazaji wote kucheka.

Pamoja na vipaji hivyo pia Gloson anakipaji cha kutumia Photoshop kwa ajili ya kucheza na picha, na ni mtundu wa mambo ya mtandao pia.

Si mbaya mtembelee hapa utakuta mengi sana ya kujifunza toka kwake. Wana Blog wenzangu mpooo!!!!?


RIP Mafisango

May 18, 2012

Juma Nyosso kushoto na John Bocco ‘Adebayor’ kulia wakiwa wamebeba jeneza, Picha Zote na Shafi Dauda

Wachezaji wa Timu ya Taifa wakiwa wmebeba Jeneza lenye mwili wa Patrick Mafisango aliyefariki jana asubuhi kwa ajali ya Gari. atasafirishwa leo kupelekwa kwao DRC Congo kwa mazishi. Mafisango alizaliwa Congo lakini alikuwa na uraia wa Rwanda ndio maana aliweza kuchezea timu ya Taifa ya Rwanda.

Nahodha wa Simba Juma Kaseja akisaidiwa baada ya kushindwa kujizuia na kuangua kilio kiasi cha kuishiwa nguvu

Kaseja ni huzuni na kilio

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dk Fennella Mukangara (wa pili kutoka kushoto)akiingia Uwanja wa TCC, Picha Zote na Sgafi Dauda

Mungu akupumzishe mahala pema peponi – Amen


Eve Sukari Live

May 18, 2012

Kiukweli kuna watu huwa nawamiss sana tangu Allain Mpella aondoke Wenge BCBG kiukweli kwa sisi tunaosikiliza sauti ya kila amtu kiukweli namiss sana hasa walivyokuwa wakipokezana ama na Aimelia au JB Mpiana ilikuwa balaa, Sikiliza Eve Sukari hii kisha nambie unakumbuka nini?

Ijumaa njema.


Ferre Gora na Fally Ipupa kuongoza wanamuziki wa Congo kurekodi Albamu ya Kuijenga Congo

May 18, 2012

Wanamuziki Fally Ipupa na Ferre Gora kwa pamoja wamekubaliana kuweka kando tofauti zai za kimuziki na kurekodi wimbo watakao kuwa wameshirikiana wote.

Kwa mujibu wa muandaaji wa mpango huo Ferre na Fally watatoa wimbo huo kwa ajili ya kuitakia amani nchi yao. Wimbo huo utajulikana kwa jina la Congo mon pays (Congo ni nchi yangu). Fally na Ferre ambao wanatajwa kama ni kizazi cha tano cha muziki wa Congo. Albamu hiyo ambayo haijasemwa bado itakuwa na nyimbo ngapi lakini itaachiwa mwezi ujao ambapo DRC Congo itakuwa inaadhimisha miaka 52 ya Uhuru..

Pichani ni wanamuziki wakiwa kwenye mazoezi ya Wimbo huo. Picha kwa hisani ya Villageafro.com
Awali muandaaji wa project hiyo Brother Patrick Mboyo, alisema kuwa mpango ulikuwa kuwashirikisha wanamuziki kadhaa wa Congo kama  Lokua Kanza, Longomba, Olivier Tshimanga Aimelia, Soleil Wanga, Papa Wemba, Felix Wazekwa, Serge Mabiala Celao Scram, etc..  Mpaka sasa Project imeshawakutanisha wanamuziki kadhaa wanaoishi Ufaransa na kwa sasa ndio wanakutanishwa wale wanaoishi Kinshasa.

Aidha Mboyo amesema kuwa wadhamini wakuu wa Project hii ni Shirika la Msalaba Mwekundu Red Cross na Unicef. Mboyo amesema haikuwa kazi ndogo kuwakusanya na kuwafanya wote wakubaliane na wazo na wakubali kufanya kazi pamoja lakini nashukuru tumefanikiwa. “Dhamira kuu ya Project hii ni kuwakusanya wanamuziki wote wa DRC ili tuijenge Congo yetu kupitia Music” alisema Mboyo.

“Tunataka kupitia music tuweze kujenga Hospitali, tuzikarabati nyingine na kujenga mashule, huu ni mpango mpya wa kuijenga Congo yetu.” aliongeza Mboyo.

Albamu hii itauzwa ulimwenguni kote ambako kuna mashabiki wa muziki wa Congo na mapato yatapelekwa moja kwa moja Red Cross na UNICEF. Hii ni kama “We Are The World” ya DR-Congo alimalizia Mboyo.


JB Mpiana na Mule mule in Dubai

May 18, 2012

Niliahidi kuweka Video hii ya JB Mpiana na Mule Mule FBI wa FM Academia walipoimba jukwaa moja huko Dubai.

Wimbo ni 48 Hrs Gecoco ambao ulikuwa kwenye Albamu ya JB Mpiana ya Toujou Humble (TH).

Utasikia JB anatambulishwa na alipopewa Mic aliomba radhi kuwa ye haongei kiingereza ila cha muhimu alisema kuwa alikuwa mapumzikoni na alikwenda kibiashara, ila anafurahi kuwaona ndugu zake vijana wakifanya muziki pale, hii ni changamoto kwa wanamuziki wanachipukia kama hawa. Post hii imewekwa tena kwa heshma kubwa na taadhima ya Shabiki wangu Papaa Fororo Jema Salim Mandari Le Fimitive Didi Stone na i yaDallas Texas USA  Kitokoooo.

Snapshot 1 (31-07-2011 08-00)

Sulutani, Salvatore de la Patria. Papa Chéri, Bin Adam,  l’homme qui a mis l’eau dans coco

Snapshot 3 (31-07-2011 10-36)

pichani ni Mule Mule FBI (R) akiwa na JB Mpiana (L ) wakiimba jukwaa moja.

Snapshot 4 (31-07-2011 10-38)

Meneja wa Klabu akimpa JB Mpiana Zawadi.

Mara nyingi tumekuwa tukisikia majigambo ya wanamuziki wa Congo walioko nchini wakitamba kuwa waliwahi kufanya kazi na wanamuziki wakubwa wa huko Congo, lakini ni wachache wenye ushahidi wa hilo binafsi naweza sema sijaona Video ya mwanamuziki aliyeko nchini anayesema alishawahi kufanya kazi na wanamuziki wakubwa kama JB Mpiana, Werrason, Koffi Olomide au mwingine yeyote kwangu mimi isipokuwa Mule Mule FBI Liberko La Loi.

Anaitwa mule Mule FBI Libeko la Loi, binafsi namkubali sana mwanamuziki huyu wa bendi ya FM Academia, namkubali kwa kipaji cha uimbaji alicho nacho na uwezo pia na awapo jukwaani aisee jamaa ahana muchezo na kazi yake. Hii inaweza kuwa ndio chachu ya mafanikio ambayo anayafikia kimuziki kwa sasa.

Mulemule alikuwa na Bendi ya FM wana Ngwasuma kabla ya kuelekea Falme za Kiarabu akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzie walipopata mkataba wa kutumbuiza huko.

Wanamuziki aliokwenda nao pamoja naye ni Queen Suzy ambaye kwa sasa yuko na bendi ya Twanga Pepeta, na Mpiga gitaa wa FM pia, Pia yumo yule atalaku maarufu wa Defao anaitwa Theo Mbala kama unakumbuka albamu ya Familie Kikuta ya Defao ndio yeye alighani humo.

Wakiwa huko katika kazi ghafla siku moja aliibuka JB Mpiana kwenye ukumbi ambao walikuwa wakifanyia kazi na kwa sababu JB Mpiana ni mtu wa watu basi alitambulishwa na kuamua kupanda jukwaani kutoa burudani kidogo kwa mashabiki wake ambao walimshangilia sana. JB Mpiana alipiga wimbo wa 48 Hrs Gecoco ambao unapatikana kwenye albamu yake ya Toujou Humble (TH), Mashabiki walifurahi sana na yeye alipopewa mic pamoja na shukrani zake kwa mashabiki aliwsema kuwa alikuwa pale kwa shughuli zake za kibiashara na mapumziko na alifurahishwa kuona ndugu zake wako pale wanaganga njaa.

Mashabiki wa mpira wanaamini Mbrazili yeyote kama hata hajui kucheza mpira basi hata danadana 20 atakupigia ndivyo ilivyo kwa Congo unapoongelea muziki wapo wengi mnooo.

Katika wengi hao wapo ambao ni zaidi ya wenzao na ukimuona mwanamuziki amekubalika Congo ujue huyo anauwezo kweli kweli na si bla bla. JB Mpiana ni mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Congo ambao wanatamba na muziki wao.

Mulemule anasema ile kuimba pembeni ya JB Mpiana alijiona kama amepata nguvu na ujasiri wa ziada ambao anao mpaka sasa, alijifunza mambo mawili matatu toka kwa mkongwe huyo.

Kwa sasa Mule mule yuko na FM wana Ngwasuma hapa jijini Dar Es Salaam baada ya kuondoka bendi aliyojiunga nayo aliporejea ya Akudo. Mulemule anatamba sana na kibao chake kipya ambacho kinapendwa sana majukwaani cha Ndoa.


%d bloggers like this: