Mambo ya fiesta usiku wa leo.

July 31, 2011

image

image

image

image

image

 

Picha za matukio mbalimbali ya Fiesta toka Leaders Club, Matukio haya kwa hisani kubwa ya Camera ya Michuzi Jr.


Mambo yashaiva Leaders

July 30, 2011

281231_10150399098398902_504653901_10411190_5357842_n

Hatimaye Jukwaa limekamilika

285226_10150399213538902_504653901_10413108_244685_n

Stage kama inavyoonekana usiku huu, Shukrani Mamaa Sophia Kessy kwa Picha hizi.

223620_10150399226503902_504653901_10413337_8195691_n

Watu washaanza kujaa tayari

225999_10150399235918902_504653901_10413532_5905938_n

DJ PQ akiwa mbele ya mashine zake jioni hii katika viwanja vya Leaders…


LUDACRISS Mjengoni

July 29, 2011

277625_10150724669945004_640275003_19502380_5440613_o

Reuben Ndege (R) wa Clouds Fm akiwa na Ludacriss (L) mara baada ya Interview katika kituo cha Clouds Fm, Luda Criss atatumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta Kesho. Hongera kaak Interview ilikuwa nzuri sana.


Promo ya luda Criss na Serengeti Fiesta 2011

July 29, 2011

TIC na Bodi ya Utalii watumieni Ma Celebrities wanaokuja nchini

July 29, 2011

image

Ni Miaka 10 Sasa tangu Tamasha la Fiesta limeanza likiwa na majina tofauti tangu enzi za Dar Carnival mpaka sasa Fiesta. Ni Tamasha ambalo linakutanisha wanamuziki na mashabiki wao huku likiwa na kauli mbiu ila kikubwa ni kufikisha burudani na kuwakutanisha watanzania bila kujali umri kwani wengi wa washiriki ni vijanalakini pia wapo watu wa makamu na hata watu wazima pia. Lazima tukubali Prime Time na Clouds ni baba wa Burudani si tu kwa Tanzania bali Afrika ya Mashariki kwa ujumla.

Shukrani na hongera kwa timu nzima ya waandaaji wa Tamasha hili kubwa kwani kupitia wao tumeweza kuwaona wanamuziki wengi wakubwa wakiletwa hapa nchini katika kuchangiza na kunogesha Tamasha hilo.

Wengi wa wanamuziki hawa ni Macebrity wakubwa si tu kwa nchi wanazotoka yaani USA au Jamaica peke yake la hasha ni Dunia nzima kama si Africa Nzima.

Habari za safari zao huwa ziko kwenye mitandao yote ya burudani na picha za matukio yao huwa zinatupwa kwenye mitandao kila kona. Ikumbukwe pia hawa wanamuziki wa kipato kikubwa sana ama kwa mauzo ya kazi zao, matamasha wanayoyafanya, mikataba ya matangazo na mengineyo hii inawafanya wawe katika rank za juu kwenye orodha ya matajiri duniani. Kwa mujibu wa taarifa za mitandao Ludacris alikuwa anaongoza kwa mauzo kwa wanamuziki wanaotoka pande za kusini akiwa na zaidi za copy 19.5 millioni ambazo zimeshauzwa. (Gomba hapa upate takwimu zake)

Dhumuni la makala yangu hii ni kutaka kuwakumbusha Bodi ya Utalii na Kituo cha Uwekezaji hapa Tanzania TIC, nahisi hii ilikuwa ni nafasi kubwa kwa wao kila mmoja wao kutupa shilingi yake wani si rahisi kuwapata hawa watu na mpaka mwanamuziki wa Marekani anakubali  na kusaini mkataba wa kuja kufanya Show hapa Tanzania atakuwa ameshatafuta habari za kujua hiyo Tanzania iko wapi na vitu kama hivyo.

Kwa TIC wanatakiwa waonyeshe ushirikiano na kubaini maeneo ambayo wanaweza kuwavutia hawa wanamuziki wanaokuja kuona ni katika upande upi wanaweza kuwekeza na sisi tukafaidika. Hata kwa upande huo huo wa Burudani kwa utajiri walionao wao hata wakiamua kuwekeza asilimia 10 tu ya pato lake hii itakuwa ni neema kubwa sana Taifa letu na watu watapata ajira. Kwani hawa watu hawaji peke yao mara nyingi wanakuja na menejiment nzima ikiwemo ma Meneja wao je hawaoni haja ya kufanya vitu kama hivyo?.

image

Umati wa mashabiki wakifurahia Serengeti Fiesta huko Moshi, Picha na Michuzi Jr.

Kwa Bodi ya Utalii, hii ni nafasi kwenye ya kuwafanya hawa watu wawe mabalozi wa hizi rasilimali zetu tulizonazo, kwa mtu kama Ludacris kwa nini asipewe ofa ya kutembelea mbuga za wanyama, tukamuonyeshe Simba kisha tumpige picha si kwa matangazo ila zisambazwe kama habari tu huyu ana mashabiki wangapi ambao hawajamuona Simba?  inawezekana kamuona lakini si kwenye mazingira asili, Kama tunajivunia Ngorongoro Crater ni moja ya maajabu ya dunia kwa nini tusimpeleke aende akayaone hayo maajabu? . Gharama ya kumpeleka Ludacris au mwanamuziki kama huyo Ngorongoro sio issue ya kuumiza kichwa kwa serikali kwani kwa gharama hizo hizo wapo maofisa ambao wanakwendaga huko ama na familia zao au na nyumba ndogo zao kupumzika kwa kutumia gharama za serikali … unabisha?….

Tunahitaji kuongeza idadi ya watalii na watalii tunaotaka waje sio hawa watalii uchwara ambao wanakula elfu kumi kwa siku, tunataka watalii ambao watakuja na umati wa watu na pesa zao kuja kupumzika na kutumia pesa zao. Sio kila siku viongozi wa Bodi ya utalii au TIC wanasafiri wao tu kuzunguza huku na kule ipo siku tutaomba kuona mafanikio ya ziara hizi we ngoja tuu.

Wanamuziki wanaongoza kwa “starehe” maana burudani ndio biashara yao, ni tofauti na wafanyabiashara au wafanyakazi ambao wao wanapata mapumziko mara chache, mfano kwa mfanya kazi mapumziko ni mara moja kwa mwaka ndio anapata likizo, lakini kwa wanamuziki au wacheza sinema anajipinda kwa kazi moja kisha anatulia kula matunda, hawa tungewalenga hawa wangeongeza pato la taifa na hata la watanzania baadhi yetu tiungefaidika pia.

Wakati kwa nchi kama Malaysia kwa mwaka 2009 iliingiza watalii 24 Millioni kwetu sisi tuliingiza watalii milioni 2 na kwetu tulijisifu kuwa tumeingiza watalii wengi zaidi, Malaysia kuna nini cha kutushinda sisi kwenye utalii?

Wizara na idara husika kaeni na hawa waandaaji muangalie mnawezaje kufanikisha hili.

Shime kwa bodi ya Utaliii watumieni hawa waandalizi angalieni jinsi gani mnaweza kushirikiana nao kwenye hili, nawasifu sana Clouds (Prime Times Promotion) ni wabunifu sana naimani mkikaa nao lazima watatoka na kitu hapo.

Mi nimesema tuu na nimtazamo wangu, na wengine walonge!!

Happy Birthday to Me!!


Happy Birthday to Me

July 29, 2011

IMG_1593

 

IMG_1590

 

IMG_1590

IMG_1585

IMG_1607

 

IMG_1539

…Dont Give Up, ndio ujumbe wangu kwa Bday hii

Ni Jambo la kumshukuru Mungu kuweza kuishi kwa umri mpaka niliyofikia leo hii makumi matatu na ushehe si haba, kwani wapo waliotamani kuiona siku hata ya leo na hawakufanikiwa.

Kwa namna ya pekee kabisa namshukuru Mama yangu Mzazi Binti Kwarewere kwa salamu na wish zako saa kumi na mbili asubuhi bila kujali kuumwa kwako lakini bado unaikumbuka siku hii muhimu, Mke wangu Mamaa Ghaty Je taime, wanangu Glory thanx mamaa kwa wish uko kwa exams lakini umenikumbuka Dady wako, My Lovely Son King of Zamunda Geebril papa loves you sana, Dada Zangu Edwina, Baldwina na Esther Mungu awazidishie moyo wa Upendo nafarijika na kujidai kuwa nanyi, Kaka zangu Edwin Mikongoti, Eugen “Micky” Mikongoti , Benedict “Mfaume” Mikongoti na Deus “Uncle D” Mikongoti heshima kwenu na asante kwa kila kitu mpaka wa leo.

Marafiki zangu Tamim Mngoya Lukuta wa Kibanda Kicheba kwa Semkope salute Mpwaa!!, Mukubwa Batty Pamoko sana Kaka, Six wa SixDezo Traders heshima kwako, Papaa Aaron Mengyason Pamoko Kaka,  Rahma Bashary my loving Jirani i miss u alot thanks for the warm salaam nakumiss sana i wish ungekuwepo leo, Papaa Jully Weston maboko likolooo, Jeff Msangi heshima kwako kaka, Gerald na Mzee nakati ya UK ndenge nini Papaa, Asumani Mlalamishi Dulla wa Tigo mwanangu kaabisa tuko pamoja mwana,  Tatiana Mkumbwa Pius Mikongoti mwanangu wa kurithi thanx for everything mamito, Rose salute Mama Perovee “Saya Cinta Kamu” mamaa, Winnie na Jane mamito, Bambucha thanx for the warm greetings xie xie, Mukubwa Edgar Benson Kiiza Le Presidaa Bana Darisalama nakati ya Kuala Lumpeeee!!!! Salute Mukulu, Mamaa Simwana thanx a millions, Teri Makasih to all my Malays Friends for the Best wishes Insyallah Allah will guide me.

Kwa namna ya pekee nawashukuru wote mlioniwish si rahisi kumtaja kila mmoja hapa ila jua tuko pamoja.

Nawaburudisha na wimbo Inchallah toka kwa Koffi Charles Olomide


Haina Majotroooo!!

July 27, 2011

image


%d bloggers like this: